Guasa Ambonii
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 8,545
- 10,296
Tupo pamoja ndugu yetu pana kitu alikuwa ana niasa mimi.Sasa unaharibu halafu unasema "tusiharibu?"
wacha muandishi amalizie kazi yake.
Tupo pamoja ndugu yetu pana kitu alikuwa ana niasa mimi.Sasa unaharibu halafu unasema "tusiharibu?"
wacha muandishi amalizie kazi yake.
Naomba Msamaha kaka angu kahtaan ,kwanza nimefurahi kukuona tena hapa JFSasa unaharibu halafu unasema "tusiharibu?"
wacha muandishi amalizie kazi yake.
Nami natamani hivyo aweke yote,bila samahani ndugu. hii Hadith imenikumbusha mbali sana natamani jamaa yetu aweke yote hapa lkn naona anatupeleka kama Azam Tv na Sultan.
.Pamoja sana
nilichukua likizo ndefu akhy lkn nimerudi rasmi na tunaendelea na minakasha kama kawaida.Nami natamani hivyo aweke yote,
Pamoja sana,ila namiss 'Ilmu' na 'Darsa' lako ktk Mikanasha ya humu Mkuu
Naomba unitag huko ,maana nimekua mzururaji tu humu,baada a kukosa mikanasha mizito mizitonilichukua likizo ndefu akhy lkn nimerudi rasmi na tunaendelea na minakasha kama kawaida.
niko na wenzetu huko ktk majukwaa mengine tunakumbushana kuhusu Siku ile ambayo mama atakimbia mwanae.
ukinitafuta napatikana tu Insha Allah .
Barakallahu fiik.
Bila shaka maalim.Naomba unitag huko ,maana nimekua mzururaji tu humu,baada a kukosa mikanasha mizito mizito
Nadhani ni kabila, wanapenda sana vita kama wakukuana.....Hawa 'wajivuni' wananichekesha kinoma
Ni kabila??
Kikundi tu fulani cha watu??
Ama ni 'watu wanaojivuna??
Kwa description aliyoitoa ya jinsi mjivuni alivyo na anavyovaa surely hao so wamasai.kwenye version ya kiingereza wametumia masai,sijajua kwanini kwenye kutafsiri wamewaita wajivuni....lakini ndio ni kabila.
Mkuu unayo hiyo version kwa PDF unitumie?Yaah kisha pana mtu wa kuitwa Alfonso katika hiki hayupo wala khabari zake hazitajwi pana siku alimzingua yule mtu mkubwa wa kizulu basi alimkosa kwa lile shoka lake na ikawa nidhamu kwa kwenda mbele. Na huyu Alfonso ndio alio pewa maandika haya ayalete huku katika ulimwengu mwingine.
Wakuu hii kitu ni tamu, huyu Makumazahn angeweza andika script tamu sana kwa movieSURA YA NNE
Tulipokwisha kula tulitembea kuzitazama nyumba na mashamba na bustani za mission. Nadhani ni mahali pazuri kupita pote nilipopata kupaona katika nchi ya Afrika.
Kisha tulirudi tukakaa barazani, nikamwona Umslopogaas anazisafisha bunduki zetu. Alikuwa amekaa chini, na shoka lake la vita likiegemea ukutani nyuma yake, akawa anaisafisha kila bunduki kwa uangalifu sana. Kila bunduki aliipa jina.
Moja kubwa sana aliita ‘’Mngurumaji,’’ nyingine ndogo aliita ‘’Yule mdogo anayelia kama mchapo wa mjeledi,’’ nyingine zilizotoa risasi mfulizo aliziita ‘’Wanawake wanaosema upesi sana, hata huwezi kutambua neno moja linapokwisha na jingine linapoanza,’’ na bunduki sita za vivyo hivyo, aliziita ‘’watu tu,’’ na vivyo hivyo.
Alipokuwa akizisafisha, alisema nazo kama kwamba ni watu, akazisimulia habari za matendo aliyoyafanya katika vita alivyopigana.
Pia alizoea kusema na shoka lake ambalo alilifanya kama ni sahibu yake. Aliliita shoka lake ‘’Inkosikazi’’ kwa Kizulu maana yake, mke wa mfalme. Nililitwaa shoka hilo ili nilitazame vizuri.
Kipini chake kilifanywa kwa pembe kubwa sana ya faru, na urefu wake ulipata futi tatu na inchi tatu, na unene wake kadiri ya inchi moja na robo, na mwisho wa kipini ulikuwa kama rungu, yaani kisiweze kuponyoka mkononi.
Kipini hicho kiliweza kupindika kama henzarani lakini kilikuwa na nguvu sana, hata hivi kilizungushiwa nyuzi za shaba huko na huko.
Karibu na sehemu iliyoingia katika shoka lenyewe, kilichorwa alama nyingi, ndiyo hesabu ya watu waliouawa kwa shoka hilo katika vita.
Basi,ndiyo lilivyokuwa shoka la Umslopogaas aliloliita Inkosikazi, naye ni shida sana kuliacha popote wakati wowote isipokuwa anapokula, na hamu wakati huo aliliweka chini ya miguu yake.
Sikuweza kufahamu kwa siku nyingi kwa nini aliliita Inkosikazi, yaani mke wa mfalme, na siku moja nilimwomba anieleze. Akasema ya kuwa kwa hakika shoka ni mwanamke, maana ni desturi yake kupeleleza sana katika mambo, tena kwa hakika ni malkia au mke wa mfalme kwa sababu watu wote huanguka mbele yake wameshangaa kwa uzuri na nguvu zake.
Tena alieleza ya kuwa amezoea kumuuliza shauri akipatikana na shida, kwa sababu halikosi lina akili nyingi kwa sababu limechungulia katika ubongo wa watu wengi!
Basi, nilipokwisha kulitazama sana shoka, nikamrudishia Umslopogaas, akaendelea katika kazi yake ya kuzisafisha bunduki.
Hapo mtoto wa Bwana Mackenzie aitwaye Flossie akaja akanichukua nikayatazame maua yake katika bustani. Mengine yalikuwa mazuri sana nisiyopata kuyaona mpaka siku hiyo.
Nikamuuliza kama anayo maua ya namna Fulani ambayo nilisikia habari zake zamani kuwa ni mazuri mno.
Mtoto Flossie alitambua namna yake, akaniambia kuwa alijaribu kuyapanda katika bustani yake yasiote, akasema ya kuwa anadhani ataweza kunipatia ua moja la namna ile.
Baadaye wale watu waliotumwa na Bwana Mackenzie kupeleleza habari za Wajivuni walirudi, wakatuambia kuwa wametafuta kila mahali katika mwendo wa maili kumi na tano wasione hata Mjivuni mmoja, wakafikiri wamekwisha rudi walikotokea.
Tuliposikia habari hizi tulifurahi. Basi, watu wote walipoondoka tulizungumza, na halafu tukaenda kulala.
movie ipo inaitwa kings solomons minesWakuu hii kitu ni tamu, huyu Makumazahn angeweza andika script tamu sana kwa movie
mkuu hii ni kazi ya kubuni sio lazima kila kitu kiwe exactly sawa na uhalisia,pia sina hakika kama uvaaji wa masai wote afrika mashariki unafanana.Kwa description aliyoitoa ya jinsi mjivuni alivyo na anavyovaa surely hao so wamasai.
AiseeChakula kilipokuwa karibu kwisha, niliomba ruhusa niondoke mezani. Nilitaka kwenda nje, nikafikiri juu ya mambo.
Nikaenda barazani, nikakitia moto kiko changu, nikakaa katika kiti karibu na mwisho wa baraza.
Nilikuwa nimeketi muda wa dakika sita saba, nikafikiri nimesikia mlango wa ukuta wa boma unafunguliwa, Nikatazama huko nisione kitu, nikafikiri ni mawazo yangu tu, Ulikuwa usiku wa giza, na mwezi haujapanda juu bado.
Baada ya kupita dakika moja tena, kitu kama tufe kilianguka juu ya sakafu ya baraza, kikaviringika kikapita mahali nilipokuwa nimekaa.
Kwanza sikuondoka, nilikaa nikifikiri ni kitu gani. Kisha nilifikiri labda ni mnyama mdogo. Ndipo wazo jingine likanijia, nikaondoka hima.
Kile kitu kilikuwa kimelala mbali kidogo, nikaunyosha mkono wangu karibu nacho, kisijongee, basi ni dhahiri si mnyama. Nikakigusa. Kilikuwa laini chenye uvungu na kizito. Nikakitwaa kwa haraka, nikakiinua katika mwangaza wa nyota. Kilikuwa ni kichwa cha mwanadamu ndio kwanza kimekatwa!
Mimi ni mtu aliyezoea mambo mengi, wala sichafukwi na moyo upesi, lakini lazima nikiri ya kuwa nilipokitazama kichwa kile, moyo wangu ulielea, nikataka kutapika. Kilifikaje hapa? Cha nani? Nilikiweka chini nikaukimbilia ule mlango mdogo.
Sikuweza kuona kitu wala kusikia mtu. Nilianza kutoka na kwenda katika giza nene, lakini nilikumbuka ya kuwa nikifanya hivyo nitakuwa ninajiweka katika hatari ya kuchomwa mkuki.
Nikarudi, nikaufunga mlango, nikatia komeo. Kisha, nilirudi barazani, nikamwita Sir Henry kwa sauti ambayo nilijaribu kuifanya kama hakuna jambo lililotokea.
Lakini naona sikuweza, maana si Sir Henry tu aliyetoka, ila Bwana Good na Bwana Mackenzie, wote wakaondoka mezani wakaja nje mbio. Bwana Mackenzie akauliza, ‘’Kuna nini?’’ Basi, ikawa sina budi kuwaambia.
Rangi ya uso wa Bwana Mackenzie ilibadilika, ikawa kama ya mfu. Tulikuwa tumesimama nje ya mlango wa sebule, na humo ndani mlikuwamo taa.
Akakishika kile kichwa kwa nywele zake, akakiinua ili akione vizuri, akasema, ‘’Ni kichwa cha mtu mmoja katika wale waliofuatana na Flossie.
Namshukuru Mungu si chake!’’ Sote tulisimama tukatazamana, tumetunduwaa, lakini tufanyeje! Hapo mlango ukabishwa, na sauti ikalia, ‘’Fungua baba, fungua!’’
Basi, tuliufungua mlango, na mtu alijiingiza amejaa hofu. Alikuwa mmoja wapo wa watu wale tuliowatuma kupeleleza habari.
Akasema, ‘’Baba yangu Wajivuni wanatujia! Jeshi kubwa limepita kuzunguka mwinuko, na sasa linaliendea lile boma la mawe la zamani la ng’ombe lililoko karibu na mto. Baba yangu, ujikaze moyo! Katikati yao nilimwona Yule punda mweupe na juu yake amekaa bibi Flossie.
Mjivuni mmoja alikuwa anamwongoza punda, na yaya alikuwa anatembea ubavuni analia. Sikuwaona wale watu waliofuatana nao asubuhi.’’
Bwana Mackenzie aliuliza kwa sauti iliyopwaya ‘’Mtoto yu hai?’’
Yule mtu akajibu, ‘’Ni mweupe kama theluji, lakini hakudhurika, baba yangu. Walipita karibu sana nami, nikauona uso wake.’’
Bwana Mackenzie akaguna, akasema, ‘’Mungu amsaidie yeye na sisi pia.’’
Nikauliza, ‘’Wako Wajivuni wangapi?’’
Akajibu, ‘’Zaidi ya mia mbili na hamsini.’’
Tukatazamana tena, tukaulizana kimoyo moyo, ‘’Tufanyeje?’’
Ndipo tuliposikia sauti inalia kwa uthabiti nje ya mlango. Ikasema, ‘’Fungua mtu mweupe, fungua mlango! Nimetumwa kusema nawe.’’
Umslopogaass alikimbilia ukutani, akainyosha mikono yake mirefu akajiinua aweze kutazama juu ya ukuta, akasema, ‘’Namwona mtu mmoja tu. Anazo silaha, tena amechukua kapu mkononi mwake.’’
Nikasema, ‘Fungua mlango,’’ Umslopogaas, akatwae shoka lako ukasimame hapa karibu na mlango. Mwache mtu mmoja tu apite ndani, mwingine akijaribu kuingia, muue.
Basi, mlango ulifunguliwa. Katika kivuli cha ukuta Umslopogaas alisimama ameliinua shoka lake juu tayari kupiga.
Hapo mwezi ukaangaza. Kukawa kimya muda kidogo, kisha, Mjivuni mmoja akaingia amevaa mavazi ya vita kama yale niliyoeleza, tena, amechukua kapu kubwa.
Mwezi uliung’arisha mkuki wake alipokuwa akijongea. Alikuwa mtu mshupavu, mwenye umri upatao miaka thelathini na mitano.
Alipofika karibu alisimama, akaliweka lile kapu chini, akaukita mkuki wake katika ardhi. Ukasimama wima. Akasema , ‘’Tuongee, Tarishi wa kwanza tuliye mtuma hakuweza kuongea,’’ akaonyesha kile kichwa kilicholala barazani kitu cha kutisha katika mwangaza wa mwezi.
‘’Lakini ninayo maneno ya kusema kama ninyi mnayo masikio ya kuyasikia. Tena, nimeleta zawadi.’’ Akaonyesha lile kapu, akacheka kwa ufedhuli na kiburi kisichoweza kuelezeka, na hata hivi hatuna budi kumsifu, hali amezungukwa na adui.

Ok mkuukwenye version ya kiingereza wametumia masai,sijajua kwanini kwenye kutafsiri wamewaita wajivuni....lakini ndio ni kabila.
Ntaitafuta mkuumovie ipo inaitwa kings solomons mines
In most cases hadithi za kubuni is from reality au maisha ya maeneo flani. James Hadley chase novel zake zote zilitokana na miji na maisha ya eneo flani. Mfano ni kweli kwamba Kenya kuna Mto Tana kama ilivyozungumziwa hapa. Pia wamasai niliowaona Kenya tamaduni zao ni sawa kabisa na walioko Tanzanian, kuna kipindi wamasai wa Tanzania wakiiba mifugo walikuwa wanaipeleka Kenya.mkuu hii ni kazi ya kubuni sio lazima kila kitu kiwe exactly sawa na uhalisia,pia sina hakika kama uvaaji wa masai wote afrika mashariki unafanana.
Hahaah kwa nini mkuu?Mkuu blackstarline naona hili shauri la kuiweka yote lime slow process, tafadhali usipate tabu, twende tu kwa mfumo ule ule tulioenda nao tukamaliza Mashimo ya mfalme Suleiman bila tatizo, sura moja kwa siku
Kunradhi kama nimemkwaza yeyote