Hadithi ya umslopagaas

Hadithi ya umslopagaas

SURA YA KUMI NA TANO

Tulipokwisha okolewa katika mikono ya Agon na watu wake wa dini, tulirudi katika vyumba vyetu katika jumba la Malkia tukawa katika hali njema, Malkia wawili, watu wakuu na watu wenyewe walishindana wao kwa wao kutupa heshima na zawadi, jambo lile la kuwaua viboko lilisahauliwa, wala hatukutaka kuwakumbusha watu habari zake.

Asubuhi iliyofuata mambo yale yaliotokea hekaluni, walimu watatu wenye vitabu vya maandiko ya mkono na wino na kalamu wakaja wakatuashiria kuwa wameletwa kutufundisha.

Basi, tulijitahidi sana kujifunza kila siku muda wa saa nne. isipokuwa Umslopogaas, Umslopogaas alikataa kabisa, akasema kuwa yeye hataki kujifunza lugha ya kike.

Na mwalimu mmoja alipomwendea na kitabu na wino na kuvipunga mbele yake, ili kumvuta macho, aliondoka kwa ukali akapunga Inkosikazi mbele ya macho ya Yule mwalimu, na huu ulikuwa mwisho wa kujaribu kumshawishi kumfundisha lugha ya Kizuvendi.

Kila sehemu watu walikuja kutuamkia na kutazama bunduki na nguo zetu na vyombo vyetu, na hasa saa zetu zilizowafurahisha sana. Watu wengine, hasa vijana maridadi waliyaiga mavazi yetu.

Basi baada ya haya, tulianza kuvaa mavazi ya kienyeji kwa sababu hatukutaka, Kuendelea kuwavuta watu kututazama.

Tena na pia nguo zetu zilianza kuchakaa. Umslopogaas tu hakukubali kubadili namna ya mavazi yake. Tena tulijitahadi katika kujifunza lugha ya nchi, tukaendelea vizuri.

Basi, hivyo kila asubuhi tulitumia wakati wetu katika kujifunza na baada ya saa sita tulitumia wakati kujiburudisha.

Pengine tulikwenda kutazama mashimo ya kuchimbua dhahabu na marumaru, na pengine tulikwenda mwituni kuwinda pamoja na mbwa waliofugwa na walio fundishwa kwa ajili hiyo.

Siku nyingine tulikwenda kuwaamkia mabwana wakuu katika ngome zao, tukaiona miji ya wenyeji. Jioni tulikwenda kula pamoja na Malkia, si kila siku ila labda mara tatu nne kila jioni na, walipokuwa hawana wageni wengi, wala shughuli iliyohusu utawala.

Nadhani tabia ya kupendeza ya Nyleptha ilikuwa upole na kwa sababu alipenda kujua habari za mambo madogo madogo ya mtu mzuri kupita wote nishajua lakini hata hivi, kwa kweli nimwanamke anaependa kujifunza mambo mapya.

‘’Basi, vivyo hivyo miezi mitatu mingine ilipita sasa tulikuwa tumekwisha jua lugha ya Kizuvendi kwa kadiri, maana si lugha ngumu.

Na huku nyuma tulikuwa tunapendwa na watu wote na pia watu wa jumbani mwa Malkia walitupenda kirafiki, tukapata sifa ya kuwa watu wenye ustadi na busara.

Sir Henry aliweza kuwaonyesha namna ya kutengeneza kioo, na kwa msaada wa kitabu tulichokuwa nacho chenye habari za jua na mwezi na nyota, tuliweza kupata habari za namna nyota zitakavyo pangwa siku fulani habari hizi ziliwashinda wanajimu wao.

Tena tuliita mkutano wa watu wenye elimu tukawaonyesha namna, nguvu iliyomo katika mvuke wa maji inavyofanya kazi, na namna mashine za mvuke zinavyotengenezwa, watu hao wenye elimu walishangaa ushangao mkuu! Tukatengeneza vim vingine vya namna ile ile.

Basi, kwa sababu ya mambo hayo wenyeji walikusudia tusiruhusiwe kabisa kutoka katika nchi yao, tutakaa ya kuwa hata kama tukitaka kutoka, hatutaweza.

Tena, tulipewa heshima, tukapewa vyeo katika askari walinzi wa Malkia, tukapata vyumba maalum katika jumba la Malkia, tukapewa nafasi ya kutoa ushauri katika mambo ya utawala wa nchi.

Lakini ingawa anga ilionekana kuwa na rangi ya samawati, lakini kulikuwa na wingu kubwa kwenye upeo wa macho yetu.

Kweli, tulikuwa hatukusikia habari za viboko wale tena, lakini tulijua kuwa habari za kufuru yetu hazikusahauliwa, wala hasira na uadui ulioongozwa na kuhani mkuu Agon haujatulia bado.

Na kwa kweli ulikuwa unawaka kwa ukali zaidi kwa kuzidishwa na wivu. Maana tangu hapo makuhani walifikiriwa kuwa watu wenye elimu kubwa katika nchi.

Lakini watu walipoyaona maarifa yetu, nguvu zao zilielekea kuvunjika. Tena, hatari nyingine ilikwepo maana wakuu wengine wakiongozwa na Nasta walituonea wivu sana, na uadui wao ulielekea kububujika kabisa.

Nasta alikuwa ametumaini kwa muda wa miaka mingi kumwoa Nyleptha, lakini sasa mambo yamebadilika.

Nyleptha moyo wake haukwepo tena kwake! Na Nasta alikuwa mwepesi kutambua sababu yake ni nini.

Basi, katika hasira yake alimgeukia Sorais, akaona kuwa ni bora zaidi kuposa mlima kuliko Sorais! Kwakweli Sorais alikuwa mzuri sana napia ni jasiri lakini uliochangajika na uovu.

Basi, nasta aliwakumbuka watu wake elfu thelathini wenye panga walio tayari kufuata amri zake kutoka chini yake milimani na kuushambulia mji wa Milosis.

Lakini kwanza alikusudia kujaribu tena kumposa Nyleptha! Akafanya shauri la kumposa mbele ya baraza ya mwaka inayofanywa ili Malkia watie sahihi sheria zote zilizoamriwa nao, katika muda wa mwaka ule.

Basi, Nyleptha akapata habari, akatuambia usiku kabla ya siku ile ya kutia sahihi, na ingawa alifanya kama si kitu, nilitambua ya kuwa anaona hofu.

Sir Henry alijiuma midomo na kujaribu awezavyo lakini hakuweza kuficha fadhaa aliyoisikia. Nikamuuliza Nyleptha kama kwa udadisi, ‘’ Malkia atamjibu nini bwana Nasta?’’

Malkia akajikunia mabega. Akasema, ‘’Nitamjibuje Makumazahn? (maana tulijulikana kwa majina yetu ya kienyeji).
Sijui Mwanamke dhaifu anaweza kufanya nini na hali anajua kuwa Yule atakaye kumposa anao watu elfu thelathini wenye panga kuhimiza posa yake?’’ Akamchungulia Sir Henry katika kope zake ndefu.

Basi, hapo tuliondoka mezani kwenda katika chumba kingine, Sir Henry akanijia, akasema ‘’Njoo upesi Quatermain, nataka shauri lako. Sikiliza, Ingawa sijasema neno, hukosi umeona kuwa nampenda sana Nyleptha. Je, nifanye nini?’’

Kwa bahati nilikuwa nimekwisha yafikiri mambo hayo, nikaweza kumjibu upesi, nikasema, ‘’Lazima useme na Nyleptha usiku huu huu. Wakati wako ni sasa, ama sivyo, hutapata nafasi tena.

Sikiliza, Tuendapo katika chumba kile cha maongezi, umkaribie umnong’oneze umwambie akukute saa sita usiku karibu na sanamu ya Rademas mwisho wa sebule kuu. Mimi nitakuwapo kushika zamu, basi, wasaa ni sasa ama haupatikani tena.’’

Basi, tulikwenda katika chumba kingine. Nyleptha alikuwa amekaa ameiweka mikono yake mbele yake, na uso wake ulikuwa wa kuhuzunisha sana. Mbali kidogo Sorais alikaa anazungumza na Bwana Good kwa sauti yake ya pole pole.

Sasa wakati ulikuwa ukipita, nikajua ya kuwa baada ya dakika kumi na tano Malkia wataondoka kama ilivyo desturi yao, na Sir Henry bado hajapata nafasi ya kusema na Nyleptha kwa faragha, maana ingawa tulionana na Malkia mara nyingi, ilikuwa shida kuweza kusema na mmoja wao peke yake.

Nilifikiri sana kisha nikapata akili nikamwendea Sorais, nilijiinamisha mbele yake, nikasema, ‘’Tafadhali, Malkia, utuimbie watumishi wako.

Mioyo yetu ni mizito leo, utuimbie ewe bibi wa usiku.’’ (Ndilo jina wanalomwita wenyeji.) akajibu, ‘’Nyimbo zangu hazielekei kuuondoa uzito wa mioyo yenu Makumazahn. Lakini ukitaka nitaimba.

Akaondoka akaenda mezani akaichukua gambusi akaanza kuipiga kivivuvivu. Ndipo alipoanza kuimba, na sauti yake ilikuwa nzuri kama sauti ya ndege, lakini wimbo ulikuwa wa kuhuzunisha kabisa, na kiitikio chake pia kilikuwa cha huzuni sana.

Sauti yake ilipanda juu ikawa kama inayeyuka kwa mbali sana. Kisha, ilizidi tena, ikasafiri kama imejaa huzuni yote ya ulimwengu na taabu zote za wote waliopotea.

Ulikuwa wimbo wa ajabu mno, lakini sikupata nafasi nyingi ya kuusikiliza vizuri. Walakini baadaye niliyaandika maneno yake, nikajaribu kuyatafsiri. Kadiri nilivyoweza kuyatafsiri, ni kama haya yanayofuata:

Wimbo wa Sorais

Kama ndege mwenda pweke aliyepotea anavyoruka gizani.
Kama mkono ulioinuka buree kuikinga mauti wakati wa kufa.

Ndivyo yalivyo maisha! Maisha yanayotia upendo na pumzi wimboni.
Kama wimbo wa ndege uliojaa utamu usiotamkikana.
Kama roho inayofungulia milango mbinguni kwa ishara.

Ndivyo ulivyo upendo! Upendo utakaoanguka ukiisha vunjika..
Kama vishindo vya hatua za mashujaa wanaokwenda vitani.

Kama sauti ya ngurumo za umeme unapopasua mawinguni,
Ndivyo ulivyo uwezo! Uwezo utakaoanguka mavumbini mwishoni.
Maisha ni mafupi: hata hivyo vitu vyote vyaweza kutuacha.

Ni ndoto chungu usingizini wala hakuna awezaye kutuamsha,
Mpaka hatua za mauti! Mauti asubuhi au jioni zatupata.

Kiitikio.

Ndiyo, dunia ni nzuri asubuhi asubuhi asubuhi.
Lakini jua jekundu huzama damuni jua jekundu huzama damuni.

Basi Sorais alipoanza kuimba ubeti wa pili wa wimbo wake, niligeuka, nikamwambia Sir Henry kwa sauti ‘’Haya sasa nenda,’’ nilimwambia.

Niliweza kusikia kila neno alilolisema, maana moyo wangu ulifadhaika sana na kwa hiyo nilikuwa na mang’amung’amu. Akasema, ‘’Nyleptha! Nyleptha, naomba nisema nawe usiku huu huu, nakuomba usikatae.’’

Akajibu, ‘’Nawezaje kusema nawe? Malkia si kama watu wengine, nimezungukwa na walinzi na kuangaliwa kila ni endapo.’’

Sir Henry akasema, ‘’Sikiliza Nyleptha. Nitakuwapo mbele ya sanamu ya Rademas karibu na sebule kuu saa sita usiku. Makumahn na Umslopogaas watakuwapo ili kutulinda. Usikatae eh Malkia wangu.’’

Akajibu, ‘’Haiwezekani, ikawa kesho?’’ Sir Henry akamsii, ‘’ Tafadhali nakuomba iwe leo Malkia wangu!’’

Basi, hapo itikio la wimbo lilianza kuishia, na Sorais aligeuka pole pole.
Hapo Nyleptha akasema kwa haraka; ‘’Vyema, nitakuwapo, nawe usikose kuwapo pia.’’
 
Nzuri
 
SURA YA KUMI NA SITA

Ulikuwa usiku mkubwa. Mji wa Milosis ulikuwa kimya kabisa, Sir Henry, Umslopogaas, na mimi tulifuatana pole pole kama watenda uovu, tulipita katika vichochoro kuelekea sebule kuu.

Njiani tulikutana na askari wa zamu, lakini nilitoa neno la zamu ili tupate kupita na Yule askari aliukita chini mkuki wake akatupisha. Tena, kwa kuwa tu wakuu walinzi wa Malkia, tulikuwa na haki kupita bila kuzuiwa.

Tulifika sebuleni salama. Mahali palikuwa kimya sana, na tulipokuwa tumekwisha pita, vishindo vya hatua zetu vilirudishwa na kufanya mwangwi juu ya dari iliyonakshiwa, kama vipigo vya hatua za watu waliokwisha kufa na sasa wamerudi kupatazama mahali walipokanyaga zamani.

Mahali hapo palinitisha sana. Mwezi ulikuwa mpevu, ukatupa miali mikubwa ya mwangaza katika madirisha membamba katika kuta ikalala juu ya weusi wa sakafu kama maua meupe.

Mmojawapo wa miali hiyo ya fedha uliiangaza sanamu la Rademas na Yule mwanamke mzuri aliyemwinamia ukafanya duara ya nuru kuizunguka.

Basi hapo karibu ya sanamu tulisimama, tukangoja. Sir Henry na mimi karibu karibu na Umslopogaas hatua chache katika giza hata tuliweza kuliona umbo lake refu kwa shida, ameliegemea shoka lake.

Tulingoja sana hadi nikataka kusinzia nikiegemea ukuta wa marumaru japokuwa ulikuwa baridi sikuona shida kwa jinsi nilivyo choka, lakini mara niliamshwa kumsikia Sir Henry akivuta pumzi.

Ndipo kwa mbali sauti ndogo ilitokea kanakwamba sanamu zilizosimama ukutani zinanong’onezana habari za miaka mingi iliyopita.

Sauti ilikuwa kama sauti ya kuchakura ya mavazi ya mwanamke, Ilikaribia! Ikazidi kukaribia zaidi. Tukaona mtu anajongea taratibu toka kivuli mpaka kivuli, tukasikia vishindo vidogo vya viatu vyake.

Mara nilimwona mzee Umslopogaas akiuinua mkono wake kuamkia bila kufanya kelele, na Nyleptha akasimama mbele yetu.

Akanong’ona, ‘’Nimekuja lakini ilikuwa hatari sana. Hamjui jinsi ninavyoangaliwa! Makuhani huniangalia, Sorais huniangalia kwa macho yake makubwa. Hata walinzi wangu nao pia hunivizia ! Nasta naye hunivizia.’’

Akaupiga mguu wake chini kwa hasira. Na ajihadhari! Mimi ni mwanamke mgumu, na kwa hiyo sishawishiki ki rahisi.

Tena, ni Malkia , nami naweza kujilipiza kisasi. Na ajihadhari nisije nikamkata kichwa badala ya kumpa mkono wangu.’’

Akalia kidogo, kisha akacheka akatutazama.
‘’Uliniita Bwana wangu Inkubu. Bila shaka unalo shauri juu ya ufalme wangu unalotaka kuniambia, maana najua ya kuwa siku zote unafikiri juu ya ustawi wangu na watu wangu. Nami nimekuja ingawa naogopa giza.’’

Basi, hapo nilitaka kujijongeza kidogo nisiyasikie maneno yao. Lakini alifanya ishara nisiondoke, akasema kuwa anaogopa watu watawatokea ghafula.

Basi, nilisimama, na haya ndiyo nilivyoyasikia katika maneno yao. Sir Henry akasema, ‘’Wewe unajua Nyleptha ya kuwa sikutaka uje mahali hapa pa faragha kwa habari za ufalme wala za watu wako. Nyleptha usipoteze wakati bure, unisikilize, maana nakupenda.’’

Aliposema maneno hayo, niliuona, uso wa Nyleptha umebadilika. Ubishi ulimtoka, na badala yake uso wake ulijaa nuru ya mapenzi yaliyofanana na ule uso wa sanamu ile ya marumaru ya Yule mwanamke mzuri iliyokuwa imesimama karibu.

Akasema, ‘’Wasema kuwa wanipenda, na sauti yako inaonyesha ukweli wa maneno yako, lakini nitajuaje ya kuwa unasema kweli? Au nitajuaje kuwa unanipenda? Nitajuaje ya kuwa huta nichoka wala hutaniacha uende katika nchi ile uliyotoka na kuniacha mpweke?

Nani anayeweza kuniambia kama kuko kuna mwanamke mwingine unayempenda, mwanamke mwingine mzuri nisiyemjua mimi, ambaye anakaa mahali pengine anakusubiri, na hata sasa hivi anavuta pumzi chini ya mwezi huu unaoniangazia usiku huu? Niambie nitajuaje?’’

Akainyosha mikono yake akamtazama kama mtu anayesihi. Sir Henry akasema, ‘’Nyleptha, nimekuambia nakupenda! Nawezaje kukuambia zaidi jinsi ninavyokupenda? Je, kiko kipimo cha kupimia mapenzi!? lakini hata hivyo nitajaribu.

Sisemi ya kuwa sijatazama mwanamke mwingine kwa mapenzi, lakini nitasema kuwa nakupenda kwa dhati kabisa tena kwa maisha yangu yote na kwa nguvu zangu zote, nitakupenda!

Sauti yako ni wimbo masikioni mwangu, na mguso wako ni kama maji katika nchi iliyokauka nikuonapo dunia huwa nzuri, lakini nisipokuona ni kama kwamba nuru imekufa.

‘’Mpenzi Nyleptha sitakuacha hapa kamwe! Na sasa kwa ajili yako nitasahau watu wangu na nyumba ya baba yangu, ndiyo, nitawasahau wote. Nitakaa pamoja nawe, Nyleptha, na pamoja nawe nitakufa.’’

Nyleptha alikiinua kichwa chake polepole, akamkazia macho yake ya ajabu yanayong’aa kwa wingi wa mapenzi yake. Kama kwamba anajaribu kuisoma roho yake. Ndipo aliposema kwa sauti ndogo lakini ilikuwa kama mlio wa kengele ya fedha.
 
‘’Kweli mimi nimekuwa mwanamke dhaifu, lakini na sina budi nisikuamini. Na sasa nisikilize ee mwanaume uliyefika hapa toka mbali kuuiba moyo wangu na kunifanya niwe mateka wako.

Nauweka mkono wangu juu ya mkono wako hivi, na mimi, ambaye sijambusu mtu yeyote mpaka sasa, nakubusu pajini na sasa kwa mkono huu wangu na lile busu takatifu la kwanza, na kwa ustawi wa watu wangu, na kwa kiti changu cha kifalme, na kwa jina la ukoo wangu, na kwa mwamba mtakatifu, na kwa utukufu wa milele wa jua.

Naapa ya kuwa nitaishi kwa ajili yako na kufa kwa ajili yako.
Naapa ya kuwa nitakupenda wewe! Wewe tu pekee yako mpaka kifo, ndiyo, na baada ya kufa, yaani ikiwa upo uhai baada ya kufa na mapenzi yako yatakuwa mapenzi yangu, na njia zako ni njia zangu.

‘’Tazama bwana wangu! Hujui jinsi mwenye upendo alivyo mnyenyekevu, mimi ambaye ni Malkia, napiga magoti mbele yako, hata miguuni pako kukuheshimu,’’ basi hapo Yule mwanamke mzuri akajitupa miguuni sakafuni mbele yake.

Baada ya hayo sijui yaliyotokea, maana sikuweza kuvumilia zaidi nikajijongeza mbali kidogo pale aliposimama Umslopogaas, nikawaacha wayatengeneze mashauri yao, nao walichukua wakati mwingi.

Nilimkuta Yule mzee Umslopogaas ameegemea Inkosikazi kama ilivyokuwa desturi yake, anatazama kwa kicheko mambo yanayotokea.

Akasema, ‘’Ee Makumazahn, naona labda ni kwa sababu ninaanza kuwa mzee, lakini nadhani sitasahau kabisa mambo ya ninyi watu weupe. Tazama wale nakusihi, ni jozi la hua wazuri mno, lakini matata ya nini?

Mume anamtaka mke, na mke anamtaka mume, basi kwa nini halipi ng’ombe kama mwamume na kumaliza shauri? Ingemaliza matata mengi, na sisi tungepata usingizi wetu.

Lakini maneno, maneno, maneno na kubusiana busiana tu! Kama watu wenye wazimu. Upuuzi kabisa.’’

Basi baada ya kupita kadiri ya saa moja kasoro robo ‘’jozi la ua’’ wale walitujia, Sir Henry alikuwa kama aonaye haya, na Nyleptha ametulia kabisa, akasema kuwa mbalamwezi inaing’arisha marumaru vizuri sana.

Kisha akaushika mkono wangu akasema kuwa mimi ni rafiki mpenzi wa bwana wake na kwa hivyo ni rafiki mpenzi wake.

Kisha, akalishika shoka la Umslopogaas akalitazama sana, akasema ya kuwa labda itampasa alitumie kumlinda yeye hivi karibuni. Kisha, akakiinamisha kichwa chake, akamtazama mpenzi wake tena, akatoweka katika giza kama ndoto nzuri.

Asubuhi yake Bwana Good aliambiwa habari zilizotokea usiku, akafurahi sana. Hakufurahi kwa sababu ya mambo yalivyompita ila ni kwa sababu ya shauri lake mwenyewe.

Yeye naye anampenda Sorais kama Sir Henry anavyompenda Nyleptha, na shauri lake halijastawi vizuri bado. Kwa kweli ilionekana kwamba Sorais pia anampenda Sir Henry kuliko anavyompenda Bwana Good.

Basi, Bwana Good alifurahi kwa sababu mshindani wake amekwishapatikana na mwingine.

Lakini hakufurahi alipoambiwa kuwa mambo hayo ni ya siri na hasa Soras asizijue habari hizo, maana habari kama hizo zikitangazwa sasa pengine mambo ya ufalme yatavurugika.

Na labda Nyleptha atatolewa katika kiti chake cha kifalme katika ghasia. Asubuhi ile tulihudhuria tena katika sebule kubwa, nikataka kucheka nilipofikiri juu ya mambo yaliotokea hapo usiku.

Walikuwapo watu wengi sana, maana pamoja na shauri la kutia sahihi sheria za mwaka, watu walikuwa wamepata habari kuwa Nasta atamposa Nyleptha mbele ya watu wote, kwa hivyo sebule ilijaa kabisa.

Makuhani wengi walikuwamo na Agon aliwasimamia, alitutazama kwa macho yake ya chuki. Tena, mabwana wakuu wengi walikuwamo na kila mmoja alikuwa amefuatana na wafuasi wake waliovalia mavazi mazuri.

Nasta naye alikuwamo anazipapasa ndevu zake nyeusi, na uso wake ulikuwa umekunjamana kuliko kawaida.

Ilikuwa shani kubwa kuwaona wote. Na hapo mkuu mmoja aliposoma kila sheria na alipomaliza kuzisoma akaweka hati mbele ya Malkia wazitie sahihi na huku panda zinalia. Na askari walinzi walipiga chini mikuki yao kwa kishindo.

Kazi ya kusoma na kutia sahihi sheria zote ilichukua wakati mwingi lakini hatimaye sheria moja ya mwisho ilisomwa.

‘’Kwa kuwa wageni mashuhuri wengine na kadhalika ikatupa kila mmoja cheo cha heshima pamoja na amri katika majeshi na sehemu kubwa ya nchi.

Zawadi ya Malkia Iliposomwa, panda zililia na mikuki ilipigwa chini kwa kishindo kama desturi, lakini niliona kuwa wakuu wengine waligeuka waka nong’onezana na Nasta aliyeyasaga meno yake kwa hasira.

Hawakupendezwa na heshima tuyopewa, na kwa hakika kadiri mambo yalivyokuwa. Walikuwa na haki ya kutopendezwa.

Basi, hapa kukawa kimya kidogo, kisha Nasta alisimama mbele akajiinamisha kwa unyenyekevu, ingawa macho yake hayakuwa ya unyenyekevu, akaomba fadhili kwa mkono wa Malkia Nyleptha.

Nyleptha aligeuka rangi kidogo, lakini aliinama kwa madaha, akamwambia aeleze haja yake, ndipo aliposema maneno ya posa kwa usemi thabiti kama inavyompasa askari.

Kabla Nyleptha hajapata nafasi kujibu, kuhani mkuu Agon akaanza kutoa hotuba ya nzuri sana tena kwa ufasaha kabisa! Akaeleza jinsi ya kuoana watu wawili hawa kutakavyousaidia ufalme na kuziunganisha sehemu zote za nchi pamoja.

Alieleza ya kuwa shauri hili litamweka Malkia imara katika kiti chake cha kifalme, naya kuwa ndoa hii itapata Baraka za jua, yaani za makuhani na kadhalika.

Maneno mengi aliyosema yalikuwa ya haki naya maana kabisa, yaani kwa upande wa ufalme na serikali, lakini si rahisi kuugeuza moyo wa mwanamke aliyezama mapenzini.

Alipokwisha toa hotuba, Nyleptha alijifanya tayari kujibu, lakini kabla hajawahi, Sorais aliinama mbele akamwambia kwa sauti ndogo, lakini niliweza kuisikia, akasema, ‘’Fikiri sana dada yangu kabla hujajibu, maana naona ya kuwa utawala wetu unayategemea majibu yako.’’

Nyleptha hakumjibu neno, na Sorais alikaa anasikiliza tu. Ndipo Nyleptha alipojibu, akasema, ‘’Kweli nimefanyiwa heshima kubwa sana, ya kuwa mkono wangu dhaifu hautakiwi katika ndoa tu, ila Agon pia anafanya haraka kuipa ndoa Baraka za jua.

Nadhani angaliendelea dakika moja tu zaidi, angalinioza papo hapo kabla bibi harusi hajapata nafasi au kukubali ama kukataa.

Nasta, nakushukuru sana, nami nitayafikiri maneno yako, lakini kwa sasa hivi sina nia ya kuolewa. Nakushukuru tena Nasta.’’ Akafanya kama anayetaka kuondoka.

Uso wa Nasta uligeuka ukawa mweusi kama mtu aliye kufa kwa hasira! Maana alibaini ya kuwa maneno ya Malkia ni maneno ya kumkataa kabisa.

Akajitutumua kwa shida, kisha akasema ‘’Asante sana ee Malkia kwa maneno yako ya ufadhili, moyo wangu utayaweka kama kwamba ni hazina.

Na sasa naomba neno jingine, yaani unipe ruhusa kwenda katika miji yangu ya kaskazini nikangoje huko mpaka utakapokuwa na jibu la kunipa, na labda Malkia atapendezwa kufika huko kuja kunitazama na kuleta pamoja naye mabwana hawa wageni.

Ni nchi maskini tu, lakini watu wangu wana nguvu nyingi kwa kuzoea kupanda milima, naye akifika watakawapo watu elfu thelathini wenye panga kumshangilia.’’

Aliyasema maneno hayo kwa sauti ya dharau, ikawa kama anamwarifu Malkia kuwa amekusudia kujitenga naye na kuasi.

Lakini Nyleptha aliyasikiliza, akatoa jibu thabiti, akasema: ‘’Hakika, Nasta, nitakuja na kuwaleta wageni hawa pamoja nami, na kwa kila mmoja wa watu wa milima yako anayekuita mkuu, mimi nitaleta wawili toka uwandani wanaoniita Malkia, nasi tutaona watu gani ni wenye nguvu zaidi. Kwa heri mpaka siku hiyo.’’

Basi, panda zililia, na Malkia wale wawili wakaondoka na mkutano ukafumukana kwa ghasia na mivumo ya sauti.

Mimi, nilirudi chumbani, na moyo wangu ulikuwa mzito maana niliweza kubashiri vita vya kindanindani.

Baada ya hayo mambo yalitulia kwa muda wa majuma machache.

Sir Henry na Malkia hawakuonana mara nyingi, wakazificha sana habari za uchumba wao; lakini hata hivyo penzi la kweli huwa si rahisi kufichika. Minong’ono ilianza kusikika! Wala ilikotokea hatukujua.
 
Back
Top Bottom