Inaendelea.....
NILIVYOANZA KUIBA NA KUTEKA WATU VITU
Siyo kwamba ndo nilikua naanza wizi, hapana sema nilkua nimepumzika sasa ndo nikawanimerudi tena rasmi kwenye wizi.
Twende kazi sasa.....
Mwaka 2011 Yule jamaa mtoto wa mwenye nyumba alikua kashamaliza chuo nakurudi home.Alitaka tumuachie chumba kimoja aanzie maisha na kimoja kwa ajili ya wazazi wake wakiwa wanakuja wanafikiapo.Hilo jambo lilitufedhehesha sana hasa mimi lakin tayar jamaa alishaamua nyumba c yao bna tutafanyaje sisi wapangaji....basi jamaa alichagua chumba alichokua analala sister na young sister ndo watoke kusudi yeye ahamie.Sister alimpisha akahamia chumba walichokuwa wanafikia wageni wetu ( kumbuka hiyo nyumba ilikua na vyumba vitano ) ko sisi tukabaki na vyumba vitatu.
Hicho kitendo kilifanya ni mchukie huyo jamaa ila ckuonesha kama namchukia nilijisemea moyoni ni lazima nimkomoe,ckujua na mkomoa vipi ilanilisema cku akijiset tu ataumia.
Basi bna jamaa hata hakukaa sana home akawa amepata kazi idara ya Maji ( Mzee wake ndo alimfanyia connection akawai kupata kazi )
Kabla hatujampa funguo za chumba alichokua anataka nilichomoa funguo mbili, moja ya hicho chumba chake nyingine ya chumba cha wazazi wake.Nilifanya kisiri hakuna alie jua kama nimechomoa funguo.
Wakati huo ndo kwanza nipo form 2 ila jamaa yeye alikua anaongea nasisi vizuri alikua hana noma ila sema alikua ana majivuno sana hicho ndo nilikua simpendei.Siku moja kuna pick up ilikuja hapo homee ikiwa imebeba maboksi yalikua 30.Yale maboksi yalikua yamebeba vitabu vya secondary.Vitabu vilkua vya Chemistry, Physics na Mathematics form 1,2 na 3.
Usiku wa siku aliniita chumbani kwake akanipa vitabu vitatu cha Physic, Chemistry na Mathematics vya form two.Nilimshukuru nikaondoka ila hata nilkua sivisomi.Kuna siku niko darasani kuna jamaa mmoja ( john kisomo wa darasa ) alitaka nimuuzie kitabu cha physic nilimuuliza unashingap akasema buku tano nikasema poa, akanipa nikampa kitabu ila nilimwambia ninavyo vingi anitaftie wateja akasema frsh
Kuna siku sikwenda shule nilikua home tu huyo John kisomo alikuja home ule muda wa wanafunzi kutawanyika.Alikua anataka kitabu cha mathe nikampa kwa ileile bei niliyomuuzia mara kwanza akasepa.Siku hyo nikawaza nikasema kumbe humu ndani nakaaa na mali tu burebure.
Basi nilimtafuta rafiki angu mmoja tulikua tunasoma nae nikamweleza hyo inshu yeye akasema atakua anatafuta wateja kisha hela tunagawana.Na kweli alikua anapata wateja me nampa mali anauza.
Nilikua natumia zile funguo nilizochukua kisiri kuingia chumbani mwa huyo jamaa na kuchukua vitabu kisha tunaenda kuuza.Niliafanya kwa Umakini mkubwa na usiri ckutaka home wajue kitu nachokifanya, kuingia tu nilikua nahakikisha hakuna anaye niona.Nilikua naona ni fresh tu kwa niliyokua nafanya, na tulipiga sana hela me na huyo muhuni wangu tukawa madoni shuleni 🙃🙃 .
Jamaa wala hata alikua hashituki kama namcheza vitabu vyake na ckuwai kujua leengo lake la kuleta vile vitabu ni nini.Nilifurahi maana vilikuwa vinanipa hela za buree.
Siku moja huyo muhuni wangu alipata dili kubwa tu kuna maticha fulani wa shule za private walikua wanaitaji vitabu vya kutosha walitaka vitabu 20 Chemistry na Mathematics kwa Buku 4 kwa kila kitabu.Nilifurahi sana nikaona mambo cndo hayo muhuni wangu alinambia kuwa atavifata jioni home kwetu me nikampanga muda wa kuja nilimwambia ni saa moja ndo atokee tuchukue mzigo tukauhifadhi kwao then kesho yake tukafanye biashara na hao Maticha.
Niliingia chumba cha huyo jamaa kama kawa nikachkua mzigo nikatoka sikuonwa na yoyote nilivificha chini ya godoro langu madogo wasivione nikawa subir saa moja ifike muhuni aje tuvihamishe.Na kweli Muhuni alitimba na Rafiki ake hata nilikua cmjui ila hilo halikua likinihusu kwanza nifurahi maana kazi ilikua imerahisishwa, Tuliviweka kwenye limfuko la Rambo yale Makubwa safari ikaanza kuelekea Maeneo ya buhare ( ndo muhuni alikua anaishi ) tulipitia barabara ya kuelekea Makoko.Tulifika Eneo moja linaitwa Boda 2 Boda darajani ( Mwisenge ) kwa mbele kidogo barabara ilikua ni yavumbi kuna kamto kalikua kanapita chini ya daraja kana mwaga maji kuelea ziwani.
Ghafla tulikutana Kundi la Wahuni nahisi walikua wanatokea Makoko, walikua zaidi ya kumi.Walituteka bna wakaanza kutupiga sachi bahati nzuri ckua na chochote mfukoni mee nilikua mpole ila wale wahuni wangu wawili walikua wabishi kinoma waliparanganya nao ikawa ni vita ni vita Mura 🤣🤣.Hao wahuni walikua wanadai eti tulifanyia Fujo makaburini nilikataa kuwa sio sisi nilichezea bapa za Panga mgongoni walinambia nikae chini.katika zile harakati za kupigana wale wahuni wangu walipata upenyo wakakimbia vitabu vingi viliangukia darajani na baadh vilichanika ko biashara ikawa imeishia hapo.Baada ya wale wahuni wangu kukimbia na kuniachw pale mwenyewe hasira zao zikikahamia kwangu nilipigwa bapa.Huwez amini nilikua napiga kelele za msaada lakini raia walikua wanaogopa kuja kunisaidia.Waliamua tu kunisamehe wenyewe, walinambia nikimbie nilitoka baru sendo ckujua hata zilipoangukia 🤣🤣🤣🤣.Nilikimbia mpk nikawa nasema kumbe kuna kipaji ndani yangu cha riadha ila me ndo ckitumii.
Basi bna biashara ilikufa cku hyo ckujutia sana maana vitu vilikua vya wizi nikaacha maisha yasonge Ila nilistop kuingia kwenye hicho chumba kwa muda.
Nitaendelea tena....