Inaendelea
Nikiwa bado nipo Arusha sema huku ckufanya matukio sana, ila ndo sehemu ambayo nilijifunza kupiga keyboard

kikweli kweli.
Nilikua nawadanganya washkaji zangu me ndo mpiga kinanda kanisan kwetu ( na walivyokua wakiniona napiga kwenye simu


) walikua wana niamini kingese, sasa cku hyo jumamosi kwa vile me nilikua off nilikuwa nipo magetoni nimelala kufidia usingizi niliokua naukosa.
Mlango uligongwa kufungua nilimkuta ni mshkaji wangu mmoja hv yupo na mkaka mmoja na wadada wawili.
Tulisalimiana kisha yule mshikaj wangu akanambia kuwa kawaleta wale watu kuwa wanashida na mimi.mmoja wa wale wageni alijitambulisha kuwani fulani wametoka kanisa la wasabato ( silitaji ) walikua wanaomba niwe mwalimu wao wa kwaya, nilivyosikia hvyo nikawauliza wamejuaje kuwa mimi ni msabato....yule mshikaji wangu ndo akanambia kuwa kawambia ( maana c me nilimdanganya kumbe alichukulia ni ukweli ). Niliwaambia hilo sio shida alafu nikawaambia kuwa niko busy na kazi za kiwanda ko nahisi itakua ngumu.
Walisema sio shida me ni kupanga tu rratiba yangu fresh. Bora hata wangesema niwe mwalimu tu walitaka niwapigie beats nyimbo zao walikua nazo kama tatu niliwaambia kinanda sina huyo jamaa akasema kitapatikana ( duh....) aisee nilikuibali tu kuwa nitawapigia bure kabisa beats na ilikua beat nianze kupiga cku ya jumanne nikiwa off (
Off yangu ilikua jumamosi na jumanne ).
Walivyosepa nilimlaumu mshkaji wangu kwanini kawaleta wale watu, niliamua kumwambia ukweli me cjui kupiga kinanda nilikua nawadanganya....sikua na namna maji niliyavulia nguo mwenyewe.
Siku hyo niliweka bundle la kutosha nikawa YouTube tu naangalia zile tutorials how to play piano for the beginner, how to create beat yani cku hyo nili such mambo mengi mpk nikaanza kujua chord za f# ( sharp ) niliona ndo rahisi kwangu alafu nikabahatisha na namna ya kutengeneza beat ko nilijifunza kwa bidii sana kwa hizo cku sana nilikua nakomalia nijue chord kwanza uzur idea nilikua nayo ko haikua shida sana kuielewa.
Kesho yake jumapili nilienda kanisa moja la walokole nia yangu tu nipate kinanda.Ila ckufanikiwa kupata maana napo cku hyo nilikua naingia shift ya usiku ko kipindi natoka kiwandani jumatatu asubui nilipita kwenye kanisa moja nikamuona jamaa mmoja anapiga kinanda ( kanisa lile ni la nje )....nilimfuata pale alipo nikamwomba samahan kuwa anielekeze jinsi wanavyo creat beat nae akasema hajui anajifunza.
Kinanda kilikua ni Yamaha psr 2100 vile ambavyo vinatumia diskette ( sio flash ) ko nilichofanya nilichukua simu nikaingia YouTube faster.
YouTube inasaidia sana tena sana kila kitu inacho yani hadi raha.Nilianza kujarbu mdogo mdogo mpk nikajikuta naanza kuweza weza, nilikomaa cku hyo mpk ikafika midaa ya saa 7 mchana ndo nikaenda magetoni kujiandaa tena na shift ya usiku ili kesho ndo niwe off.
Jumanne ilifika na nilitoka cku hyo saa mbili asubui maana tulicheleweshwa kupewa kadi ( bila kadi na barakoa huingii kiwandani ) nilivyofika tu magetoni nakutana na yule msabato ananisubir nje ya geto langu....niliona huyi jamaa vipi ni mwambie tu ukweli kuwa me cjui kitu aah...niliacha nilisema ngoja tu nikaaibike tu kihivyo hivyo.
Nilimkaribisha ndani akasema hakai me nijiandae tu ili niondoke nae akanipeleke kwenye kinanda nianze kazi.Mimi hata kama kitu cjui nitakwambia najua na ninasimamia huo ukweli kuwa najua kumbe cjui.
Tuliondoka nae mpk sehemu moja hivi Ngara ya chini ( ilikua sio mbali sana na pale napoishi ) tulifika kwenye nyumba flani hivi nzur tu tukaingia mpk ndani sebuleni nikakutana kinanda kipo mbele yangu kinanisubir



.
Nilitaman umeme ukatike lile zoez lisifanyike lakin wapi...ilibidi tu nikakae kwenye kinanda tu ckua na ujanja.Uzur ni kwamba yule jamaa alinambia niwasubir wale wadada waje ili wame wanaimba alafu me napiga beat.
Nilitumia muda huo kuingia tena YouTube kukumbushia niliyojifunza cku zilizopita.
Nilianza kukipiga kinanda kwa uwoga hapo bado wale wadada walikua hawajaja na kinanda kilikua ni Yamaha psr 650 kilikua kinatumia flash na MID cable, styles zake nilizipenda drums,jazz, rap na kadhalka.
Walipofika wadada niliwaambia kabla hatujanza kazi tuombe kwanza tena me ndo niliomba na niliomba ombi la huruma sana.Nadhan Mungu alisikia ombi langu.
Nyimbo ya kwanza ilkua haina kona kona nyingi ( Minor ) ko ilikua nyepesi kidogo nilivyojua tu hatua zake kwenye chord ya f# ( sharp ) basi nilienda kwenye function kuanza kutengeneza beat
Kazi ilkua ni kupiga intro na zile lead zake duh..mwanzo mgumu ila hyo beat niliibahatisha




mpk wao waliipenda niliweka break za kutosha ( me hua napenda sana beat zangu kuwa na break ).Wimbo uliofuata nilishindwa maana ulikua una minor za kutosha mpk nikawashaur tubadili uwe na format nyingine, walikubali ko cku hyo beat nilipiga moja.
Nilifurahi maana kalee ka beat ninako mpk leo hua nikikasikiliza hua nakumbuka mengi.
Ila cku hyo ndo nilijua sasa kinanda vizur yan mpk nimerud musoma hua napigia kwaya beat japo saiv nipo mbali na kinanda lakin kwenye simu yangu hakikosi hua napiga beats ili ujuz usiondoke.
nitarejea tena.