Inaendelea
Baada ya kuchukuliwa siku hiyo kilichofuata ni kwenda hospital kupima afya zetu ( ukimwi nao ulikua mmoja wao )....siku hyo ndo kwa mara ya kwanza nilipima h.i.v, nilikua naogopa majibu lakini yalitoka vizur yani nilifurahi siku hyo.
Baada ya hayo kupita nilianza rasmi kaz kiwandani nikiwa kama operator wa mashine za kushona mifuko ya saruji ( cement ) na mifuko mingne ( magunia/junia ).
Siku ya kwanza ndo tunapelekwa idaran sasa duh..nilivyoona zile mashine za kufuma hyo mifuko jinsi zile nyuzi ( tape ) zilivyopita nilikua nasema hii kaz kweli nitaiweza.
Tulipelekwa kwa meneja wa section yetu akatupa mawaidha ya kutosha, alafu tukakabidhiwa tena kwa waalimu wetu ambao walikua wanatufundisha mashine zinafanyaje kazi.
Siku tunaingia tulikua watu 22 wengi wao wakiwa ni wadada, sisi wanaume tulikua wachache.Na mule Idarani asilimia kubwa ya wafanyakaz ni Wanawake alafu ni waarembo hatar mpk nikawa nawafikiria mademu zangu kama zile kazi wangeweza kweli.
Kwa vile sharti la kiwandani pale lazima ufanye kazi siku kumi bure ( for free ) alafu zikiisha ndo wanakukadilia hizo cku zilizo baki mshahara.
Huwez amini hata wale waalimu walipokua wakitufundisha namna ya kutumia mashine nilikua hata siwaelewi kabisa, kwanza makelele yalikua ya kutosha.Na siku ndo tunamaliza tu zile siku kumi ilikua lazima tujue kuendesha ( ku operates ) mashine moja, cku hyo niliumbuka nilivyopewa mashine yan sikua na ninalolijua, sio mimi tu karbia na wenzangu wote.
Sema kwenye ile line niliyokua nimewekwa kulikua kuna kadada kazur sura mpk roho ndo alikua mkomboz wangu yani alikua anaacha mashine zake tatu anakuja kunisaidia mimi mwenye mashine moja.
Kwa vile kile kiwanda ni kikubwa basi mashine nazo zilikua ni nyingi, idaran kwetu tu kulikua na mashine zaid ya 300, section yetu zilikua mashine 214 lakin ni aina ya mashine zilikua 4 tu.Na kila mashine ilikua na speed yake na lengo lake ( goals )..
Uzur mimi niliwekwa kwenye mashine yenye speed kubwa ko lengo pia lilikua kubwa.
Maisha yalibadilika kabisa kwangu nilizoea kipindi niko musoma naamka muda naotaka lakin huku ilinilazimu kuamka saa 11 alfajir ili niwai kiwandani.Mwanzo ulikua mgumu kwangu maana usingiz wa asubui ni mtamu hatari [emoji16].
Ko nilivyo kwisha kupata kazi niliamua kutafuta nyumba faster ili nijitegemee kivyangu ( ckupenda kuishi na watu ).nilipata nyumba nyuma ya kiwanda ko ilikua ni rahisi kwangu kuwahi.
Kwa vile nilikua na kahela nilinunua vitu vya gheto na vingine nilipewa na Shangaz angu alikua anakaa Njiro.
Ile kazi ki ukweli ilikua ni ngumu yani masaa 12 umesimama tu kuendesha mashine.Kuna siku nilingia shift ya usiku ( night shift ) mashine ilinisumbua hatar yan kwanzia saa 1 nimepewa mashine ilinisumbua mpk niliiomba msamaha [emoji23][emoji23] kufikia saa sita ndo mashine ikakubali msamaha wangu iliunguruma mpk saa 12 asubui.
Nilipiga kaz kwa bidii yule manzi aliyekua akinisaidia kaz zangu tulizoena nae sana mpk tukawa wapenzi [emoji7][emoji7] lakin tu sikutaka kuishi nae japo yeye alitaka hvyo ( niliona tukiish nae atanibania ridhiki ).
Siku moja ilikua ni cku yangu ya Off ko nilikua mageton nimetulia tu na manzi mmoja hivi alkua ni wakala wa mpesa.Basi jioni yake niliamua kwenda getini kuonana na wale jamaa zangu walio nipokea.
.Kipindi nawasubir watoke kiwandani nilkua nimekaa kwenye vibanda vilivyokua nje ya kiwanda napiga zangu piano kwenye simu.
Kuna Chalii mmoja alikuja nae akakaa pemben yangu alivutia sana na ninavyopiga piano ko uzalendo ulimshinda akaniuliza "inaonekana wewe ni mtaalumu wa hilo dude" nilimwambia ndio licha ya kupiga tu natengeneza na beat kabisa...nikamuekea apps moja hivi ni yakutengenezea beat ni nyepesi kinoma, lakini mimi niliamua kuchukua point kwa yule chali.
Tuliongea mengi na yule chali tena yeye muda mwingi alikua ananiuliza maswali tu kuhusu utayarishaj wa muziki namjibu ivyo ivyo tu kibabe.
Mwisho wa siku alidai kuwa yeye anaimba na hajapata mtu wa kumtoa kimuziki alishukuru kukutana na mimi labda ninaweza kumsaidia.Moyoni nilijisemea hivi huyu chalii yupo serious kweli.
Chali alikua anataka nimtengeneze beat na mimi hata piano yenyewe tu nilikua bado najifunza.Nilisema sasa nitafanyaje kumkwepa huyo chalii na alkua serious kweli.
Nilimwambia tu kama yupo serious na muziki akanihakikishia kuwa yupo serious.Nilimuuliza anakaa wapi akanambia Majengo niliona majengo na Matevesi ni mbali sana.
Ko nilimwambia tufanye jumamosi nikiwa tena nko off ndo tufanye kazi akakubali alinambia nitamchaj bei geni, nikamwambia kwa vile unaonekana uko serious me nitakupigia beat kwa 50k tu alikubali tukabadilisha namba pale kila mtu akafanya yake.
Jumamosi ilifika Chalii alinipigia simu kuniuliza tukutananie wapi, niliona kumwambia aje magetoni ni uongo na mimi kwenda kwake pia ni uongo.Ila niliamua kwenda kwake huko Majengo ili likitokea la kutokea ni fresh tu.
Saa nne nilipanda dalala nikamfuata mpk magetoni kwake.Sikumkuta yeye tu bali walikuepo na machali wawili pamoja na manzi mmoja ( inaonekana alikua ni manzi yake).
Nilifika wakanikarbisha fresh tu kumbe huyo chalii aliwaambia wenzake kuhusu ujio wangu pale ko walikua wananisubir kwa hamu.
Nadhani walinishangaa kuniona sina vitendea kazi na mmoja aliniuliza nikamtolea simu yangu nikamwambia mambo tunamalizia humu.
Nilimwambia yule chali aimbe kwanza nimsikie akaanza kuimba nilitamani kucheka ila nilijikaza.
sijui ile ni style gani ya kuimba [emoji23][emoji23][emoji23] nilimuacha aimbe kwanza nilichofanya nilimrekod sauti yake afu nikafungua ile apps nikawa namsikilizisha sample ya beats akataka beats iwe reggeton.
Yaan uongo wa siku hyo aisee nilio wapiga hao machalii [emoji23][emoji23][emoji1]....niliona ili wasistuke niliwaambia kwa vile beats inahitaji utulivu basi waniache nirud mageton niitengeneze nikiwa nimetulia, nilimrekod tena afu nikaomba hela ili nisepe.Alinipa nikamwambia beats nitamtumia whatsapp.Alinipa no za whatsapp huyo nikaondoka.
Nilivyoondoka nili mblock kote kote cjui walibaki kwenye hali gani hao machalii na sio hao machalii kipindi nimerud musoma kuna wasimbiti nao waliingia kwenye anga ( sema wenyewe walinikuta najua kutengeneza beat sema kufanya Recording tu ndo nilikua cjui kumix ) niliwatapeli wakabaki hawaamini, cjui hata walikua hawanistukii aah..never mind.
Nakarbia kuhitimisha story yangu bado visa vichache sana nikamilishe kisa changu.
Nitarejea tena.