Hadithi ya kweli ya maisha yangu

All the best mkuu, ndio maana siku zote kwenye mahusiano usikose plan B, plan C, Plan D...........Plan Z
 
Poleee
 
Mzee Old
 
Umetuweka sana mzee tutasahau matukio
 
Inaendelea


Wakati nikiwa bush nilikua nikikaa alone basi nilikua namkumbuka sana hyo Manzi hyo hari ilikua inanitesa moyoni.

Pindi ndugu zangu wamekuja nao bush atleast nika avoid hyo situation...bro wangu alinambia kuwa kanitafutia kazi kiwandani ko niende kupiga kazi kuliko kukaa home bila kazi maalumu.

Nilikubali na kiwanda kilikua kiko Arusha nilitakiwa mwezi wa nne niwe Arusha kuanza kazi ( sikuambiwa na sikuuliza kiwanda kinatengeneza nini ).....lakini kutokana na Korona kupamba moto sana kiwanda kilisitisha kwa muda kupokea watu.

Ilibidi nisubir mpk waanze kuchukua tena watu....bush nilikaa mwez mmoja nikapachoka kutokana kaz ya kupalilia aaah...kiukweli ckuweza niliamua kurud tu musoma kwa vile Nyumban kwao mama ni wakulima wa mpunga, Bibi kizaa Mama alinituma gunia mbili na Nusu..ko mimi nilichukua kilo 80 ili nikifika nazo msoma niuze kwa wadau.

Basi siku ya safari nilishangaa....bro ma yule mdogo wangu ( mwiz ) nao walitaka kuondoka bush basi kwa pamoja tukasepa kurud musoma.Bush walibaki Mzee, mama na ndugu zangu watatu.

Nikiwa musoma niliuza ule mchele kama kilo 50 kwa kilo 1 sh 1000 watu walikua wanaung'ang'ania hatar.

Kwenye mwez mei hivi kuna dogo mmoja alinifuata pale ps.

Nilitaka kusahau kuhusu yule classmate wangu kumwelezea
.

Wakati nikiwa bush boss siku moja alinipigia simu akaanza kunieleza madudu ya classmate kuwa ckuiz kawa mjanja na hela haioni.Mpka akawa anasema bora ungebaki kupiga na cjui kwanini nilimkimbia.
duh..nilicheka na kusikitika kwa wakati mmoja.Huyo boss alisahau kuwa hyo biashara ina wenyewe na wenyew ilikua ni sisi kiukweli alikurupuka sana kumweka classmate wangu ndo asimamie kila kitu.

Me nilimpa pole tu nikamwambie amvumilie ataziona hela.Hazikupita siku nyingi classmate nae alinipigia simu, alikua anadai kuwa kuna demu alianza nae mahusiano kumbe demu alikua ni mdangaji hatari.Hela za ps zilikua zinaishia kwa huyo demu.

Alitaka nimsaidie 240k ili ampe boss wake maana alikua hajampa boss hela kama wiki tatu karbu mwez hela ya ps.Yaani alikua hana hata aibu kuniomba hela yote ile maana nikikumbuka nilivyokua nikimuomba hata buku tu ya msosi anasema hana hela.

Nilimwambia siko vizur kipesa labda nimpe 20k akasema nimkopee kwa mtu.jamaa alikua fala
nilikataa ikabid nimpe tu hyo 20k.

Jamaa boss alimtema ko alifunga ps kwa muda akawa ananisubir nirud msoma niendelee na job.Sikutaka kurudi kupiga job pale tena nilichofanya nilivyorud msoma nilienda tu ps nikakaa kwa muda nikawa na mtafutia dogo ili ampigie kaz maana me nilijua muda wowote nasepa zangu Arusha.

Turudi tena kwa huyo dogo aliyenifuata ps.Huyo dogo alikua anasimu anauza ( samsung A20 ) lakini ilikua mbovu ( screen na touch vilikua vibovu ) ko alitaka nimpe 50k tu.Nilikubali lakin nikamwambia kwa muda huo sina kitu aje kesho yake achukue pesa.

Niliipeleka simu kwa fundi aone itani cost shngp kutengeneza kwa vile fund nilikua nafahamiana nae alinambia kioo na touch pamoja na hela ya fund jumla nimpe 160k nililia lia akakubali kunitengenezea kwa 120k cku fund nikampa 10k kwanza ikabaki 110k.

Na nilikua sina smartphone kabisa ko nilitaka hyo simu fundi atengeneze chap ili nirud mtandaoni.Kama kawaida ya mafundi sio waaminifu kila nikienda anasema njoo kesho njoo kesho yani mpk mwezi wa sita ukafika ni njoo kesho.

Wakati fundi ana nambia njoo kesho na mimi ndo nilikua namwambia yule dogo mwenyewe simu hivyo hvyo.Na mwezi wa sita ilifika kiwandani niliambiwa niende na hapo hapo Mzee alikua amepata mkwanja ( cjui alitoa wapi ) mkwanja ulikua mrefu sana, alinipa 1.2 milioni za kuanza nazo maisha, nilichofanya nilichukua 300k nikanunua smartphone Samsung A30 na vitu vingine vya kwenda navyo chuga.kwenye yale matumiz nilijikuta nimebaki na laki 8.

Kwa vile likizo ilikua imeisha basi ilibid pia wale wadogo zangu wawili ( wa kike na yule mwiz ) pamoja na sister tusafir nao pamoja kwenda wao wakiwa wanaenda kwanza Karatu kuchukua vitu fulani alafu ndo waende dodoma.

Siku ya safar me niliwaambia kwanini wasisubir twende siku inayofuata, walikataa wakasema wanawai, basi me ckwenda nao.Kesho yake ilikua ni cku mby sana kwetu kama familia tulipata habari kuwa sister na wadogo zangu wawili basi walilokua wanasafiria limeanguka na kuua na kujeruhi.


Sister angu yeye hakuumia kabisa lakin hao madogo ndo waliumia sana hasa huyo wakike
aliumia vby yani alkua mahututi.Waliwapeleka hospital iliyokua jiran na mdogo wangu huyo wa kike alihamishiwa hospital ya mkoaranga akawa anapigania maisha yake ( ICU )...huyo wa kiume yeye alivunjika mguu, wakike nae alivunjika mguu vby mpk saiz hawez kutembea bila magongo.

Nacho shukuru ajali hyo ilitokea Mzee alikia ana hela sana ko pesa ilitumika nyingi sana kwenye matibabu..yan nyie acheni tu kila muda tulikua tunapigiwa simu kuwa tumuombe mdogo wetu muda wowote ana kata kamba.

Sicheki kwa mazuri ila katika kipindi nilichomkumbuka Mungu kwa dhati ni hicho kipindi nilikua naomba kila muda tena kwa dhati.


Mungu ni mwema sana alijibu maombi na Huyo dogo kwa uwezo wa Mungu alipona ubaya tu ndo hatembei dogo.


Ngoja nikomee hapa kwanza nitarejea.


Poleni kwa kuwaweka sana.
 
Na wao wakipata wa kuwaumiza wawaumize tu akili iwakae sawa, akuna kiumbe nisicho kipenda hapa chini ya jua kama mwanamke
Ila hawa viumbe ukijua kuwa maintain basi wala hawakupi shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…