Inaendelea
Baada ya ujio wa huyo Jamaa ( class mate ) pale ps kiukweli hari ilianzaa kuwa mbaya kifedha kwangu.Me c nilikua nachukua hela Ijumaa na jumamosi sasa ilibid tugawane cku za kuchukua pesa, mimi nikawa na chukua ijumaa yeye jumamosi.
Nakumbuka siku ya kwanza anamekuja kuanza kazi rasmi kwa vile alikua bado learner kwenye kazi ilibidi akae kwa kutulia ili nimfundishe.Siku hyo biss alikuja akatupatia maelekezo fresh tu na alisema kuhusu swala la kula nyie hata kama mmepata buku cku hyo itumieni kwa chakula ( uzur wa boss hakua mchoyo kwenye hela )....
Boss aliondoka yani ile anaondoka tu alikuja bishoo mmoja mule ps akaulizia muhusika nikasema ni mimi, alinitoa nje kufika aliniuliza kama games za ps zina cheza kwenye Pc ( laptop )...nilimuangalia kwanza kabla cjamjibu, kisha nikamwambia kwani hujui akasema hana uhakika.
Basi nikamwambia ndio zinakubali....alitoa frash ni mkopie akaweke, nilimwambia utaweza bei za game lakin...aliniuliza tena "kwani ni shngp kwa game moja?"....nilimwambia game moja ni 15000 alistuka nikaona ananipotezea muda nilimuliza una shngap akasema alijua ni 5000 kuweka game's nilimwambia akajarbu kwingine, tena aliuliza ni game's zipi ambazo ninazo nilimtajia Fifa 19, pes 18, GTA V na Call of duty Warfare, Calls of duty black ops, call of duty WW1, Watchdog, Uncharted na mengine mengi tu.
Basi akaondoka nikarud ndani...na siku hyo wateja walikua wengi na wengi wao walikua wa loser ( loser ni Atakae poteza ndo analipa )...kwa vile nilikua master kwa wakati huo nilirud kuona ma learners wakitoana jasho.Ilipita saa moja yule bishoo alirud tena akaniita alinambia nimfanyie 10k kwa kila game na alikua anataka game's 5...nilivunga kukataa ili ananione kuwa cna shida na hela, nilivyomuona anaondoka nikamuita nikamwambia kuwa nakusaidia tu kwa vile nimemuona ni muhitaji lakin nikampa onyo kali asije kusema popote na nikishamkopia asirud tena pale ps ( nilimwambia hivyo maana nilijua kama akienda kufnya installation ya hizo game's kwenye pc zitamgomea tu, niliogopa asije kurud kudai hela yake ).
Nilimkopia game's alizotaka akanipa 50k alafu bishoo akasepa zake.Nilmuita huyo jamaa ninae piga nae kazi nilitoka nae nje nikampanga kuwa kuna game's nimemrushia mtu lakin asije kumwambia boss nilimpa 10k ya kumtuliza.Kumbe jamaa alikua snitch mzuri.
Kesho yake yule bishoo alikuja tena ps Akaniita ( alikua na rafiki ake )...alinambia mbn games hazichezi kwenye pc.Nilimwambia kwa hyo hilo ndo la kuniita tena nilimkumbusha huyo bishoo kuwa c nilikwambia usije hapo ps,bishoo alkua mpole akataka niende nae kwao nijarbu mimi kuzieka zile game.Nilimuuliza kwani pc yake ina Window ya ngap akasema ni Window 10 basi nikamwambia ndo maana zimekataa kucheza maana hyo window hua inazngua.Alinitaka nimwelekeze ni Windows gan atumie, nika mwambia aweke window 7 ( ukweli ni kuwa me habar za computer me hua cjui kabisa )....kipindi wanaondoka nilimwambia asirud pale tena kama ana shida na mimi ani text nikampa no zangu.
Huyo bishoo hela zake nilikula bure tu maana nilivyoona ananisumbua nilimpiga mkwara mzito hakunitafuta tena.
Hapo kiukweli nilifanya utapeli wa wazi wazi na tena baada ya huyo jamaa kuja kupiga kaz hapo ps ndo maisha yalianza kwenda mlama kwangu.Jamaa alikua anavunga ni mtu mwema sana kumbe mpk hyo inshu ya mimi kuuza games alimfikishia boss, Boss alicho fanya alimueka huyo jamaa awe msimamizi mkuu wa mambo yote ko mimi nikawa chini.
Hicho kitu ckukipenda kabisa yaani mtu ni mpokee na kumfundisha kazi eti ndo akawa tena boss wangu, yaan mpk hela ya kula namuomba yeye.
Japokua huyo jamaa alikua ananitegemea kwa vile me ni master ps ko kwenye loser nilikua nampa hela nyingi sana alafu nikimuomba hata ya kula ana ninyima.nilikua namuangalia na muacha tu.
Tuseme kiuchumi nilianguka kwa muda maana hata pale home Mzee alisepa kumfuata mke wake bush maana maisha ya mjini yalimshinda, mdogo wangu wa kike yeye alivyomaliza tu graduation alisepa Dodoma kwa sister kwa kifupi home nilibaki mwenyewe tu.
Sikua na namna niliona ili ni lipe bill's lazima niishi kijanja...hapo sasa nikaanza kutapeli watu ( cjui kudhurumu )...kila nikienda palee ps basi lazima nidhurumu waliokaa kiboya.
Kama kuna madogo flani hivi walikua ni wanafunzi wa Makoko seminary walikuja kucheza ps midaa ya saa mbili usiku.Na cku hyo nilikua sina hela maana nilimuomba yule jamaa hata anikopeshe ten akalialia tu.
Nilikua nimekaa kwenye bench nyuma kabisa nawaza hela napataje ndo wakaingia hao madogo wa shule.Niliona mmoja alitoa wallet kuhesabu hela,nilijisimea moyoni lazima nitoke na chochote asee...kwa vile madogo walikuta kuna watu wanacheza ilibid wasubir.
Ckutaka kuwachelewesha nilimuuliza dogo mmoja kama ana jero pale anipe nimpe buku afu jero nitachukua badae.Alidai hana nikamuuliza una shingap alisema wana elfu kumi kumi tu.Niliwaomba nika wachenjie ili wasisumbuke na chenji....wakanipa masikini [emoji26][emoji26] elfu kumi nikawaambia tena c mlete na hizo nyingine ni kawalete pia chenji wakatoa 20k ko jumla ikawa 30k niliondoka ckurudi, yule jamaa alinipigia kuniuliza niko wapi maana madogo walikua wanalia hela yao hela yao.
Nilimwambia jamaa awaambie kuwa nakuja hata wasijari,nilivyokata simu nikaizima kisha nika sepa zangu kwa hotelin kula then nikaondoka kwenda home.
Hapa nimewapeleka mbele kidogo nitarud kuendelea tena.