Inaendelea
Baada ya Mwenyekiti kuja pale niliambiwa nieleze nguo nilinunua wapi na duka gani, zingekuwa za mtumba ningedanganya kuwa nilinunua mitumbani lakini bila kufikiria vzr nilimtaja jamaa mmoja hivi kuwa ndo aliniuzia kama vipi tumpigie simu.
Nilikosea kusema hvyo huyo afande alitoa simu yake akanambia nitaje no ya huyo mtu ili wampigie aje kwenye tukio, kwa vile simu yangu nilkua nayo mfukoni ( ingawa ilipasuka kidogo kwenye zile vurugu ) niliitoa nikachagua linamba ambalo najua kabisa halipatikani nikampa afande kuipiga ikawa haipatikan kweli,nikasema afadhari.Huyo mzee na mwenyekiti walikua wananishaur kuwa niwe mkweli tu kama nataka kuwa huru.
Nilipelea maneno huyo afande akaamua kuita difenda ije inichukue nikatoe maelezo vizur kituoni, nilijilaumu sana kwa nini nimefanya kile kitendo lakini ndo ilibidi tu nikatae hivo hivo mpk mwisho wakat kichwani nilikua na hesabu zangu za kukimbia.
Jirani nao walikua wamejaa madirishani wanachungulia kuniona navyodhalilika, haikuchukua muda sana fenda ilikuja wakaingia mule chumban nikapigwa pingu ( ndo mara ya kwanza kuvaa pingu )....nilinyanyuliwa na kutolewa nje nikapandishwa ndan ya fenda na yule jamaa nae akapanda kwenda kutoa maelezo.
Tulifika Central ilikua ni kwenye saa moja usiku, nikaandika maelezo jamaa nae akatoa maelezo,ckua na viatu nilikabidh simu nikavua mkanda moja kwa moja kwenye sero.
Nilikuta raia weng weng mule sero, kesho yake niliamka na maumivu kichwani, pua lilkua linauma hatar,niliitwa tena kwenda kutoa maelezo vizur nilimkuta yule jamaa yupo na zile nguo nazodai ni zangu.Mzee alipewa taarifa lkn hakuja yani mpaka namaliza wiki niko Central ndo alikuja kuniona.kuhusu msosi nilikua naletewa na mama mmoja ni jirani yetu.
Police walimtaka mzee amalize ile kesi mapema kabla cjapelekwa mahakamani maana ninge shtakiwa kwa makosa mengi tu la kutishia kuua likiwemo ( kuna afande mmoja alikua ni jirani yetu ndo alikua ana nambia wakati ananiletea msosi mule sero, afande ana roho nzr sana ).
Mzee alichokifanya alitafuta suluhu kwanza ile familia ya yule jamaa akataka yaishe walikubaliana na siku natoka Central yule jamaa nae alikua pamoja na yule bonge, walinitaka nikili mbele ya maafande kuwa kama nikionekana pale home kwao basi nikamatwe.nilikubali masharti yao ila moyoni Mungu tu ndo alijua hasira zangu.
Ckujua mzee alitoa shngp pale central niliondoka na mzee na yule jamaa nae akasepa na bonge wake njia yao.Nilifika home niliiambiwa na mzee eti nisiingie ndani na zile nguo nilizokuwa nimevaa Central akidai nitaingia na mikosi ko kulikua na bafu la nje niliingia nikaletewa maji nikaoga na nguo nikabadili ndo nikaingia ndani.
Niliwaambia madogo mbn hawakuja kuniona Central ( kiutani lakin..maana nilifurah kuwaona tena ) hawakua na majibu life liliendelea lakin akilini tena nilikua namuwaza yule jamaa ( mtoto wa mwenye nyumba )....niliona kama kachukua points sana kwangu nili plan nirud tena kwao pale ni muibie za mwisho mwisho ili roho yangu itulie, lakin shida ilikua inakuja kama wakini shika tena na huku Central nilikir kwa ulimi wangu kuwa sitokuja kukanyaga pale kwao.
Nilikua na mawazo mawili niende kuiba or niache wazo la kuiba likapita bila kupingwa ko nilianza harakat tena za kumuibia jamaa.
Kesho yake nilirud pale tulipo hama kusoma mazingira, nilifika nikakuta grill mlangoni ( kumbe waliweka geti mlangoni baada ya sisi kuhama )...nilibisha hodi akaja yule demu akanambia nimefata nini pale nikamwambia nilisahau pisa yangu ( pisa ni kile kifaa kiko kama plaisi ni cha kusukia nondo )
Bonge nae alikuja alivyoniona uso wake ulibadilika ghafla nae akaniuliza nikasema nimekuja kwania nzur kutafuta pisa yangu, waliniruhusu kuingia kuitafuta wao wakiwa nyuma yngu nilienda kuitafuta chumbani kwa mzee wangu maana ndo kulikua na kabat la ukutani.
Niliikosa pisa nikawaambia wanipe ruhusa nioge maana kule tunapokaa maji ni shida, bonge aliniangalia kwa hasira japokua aliniruhusu kuoga lkn walikua hawana imani na mimi kabisa.Nilimaliza nikasepa zangu home, Niliona hyo plan yangu imefeli maana ckutegemea kukuta lile geti niliudhika kinoma.
Narud kuendelea.