Inaendelea
Before sijasimulia ni jinsi nilivyo kamatwa ngoja tena ni wape kisa kimoja hivi.
Na jamaa angu alikua ni classmate wangu, huyo jamaa alikua ni wale vipanga wa darasa yaani mkiwa kwenye chumba cha mtihani utaskia tu wenyewe wanasema "
Another paper sir/madam" afu ukiangalia wewe unakuta hata hyo paper yako moja hujaandika chochote yan ilimrad tu watuumishe roho.
Huyu classmate wangu licha ya kuwa tu na akili pia alikua na heshima na ustarabu mpk walimu walimpenda sana, ilikua ikitokea ni mashindano ya debate na shule nyingine basi jna lake lilikua halikosi kwa maticha.
Sema licha ya ustarabu wake alikua ni fala yaani muoga anawai kupanic hatare....kingine nilikua c mpendi tu na ukielele wake.
Nilikua naendaga na cd za porn darasani bila uoga tena yale ma dvd yenye covers kabisa nikifika nawaonyesha masela atakae taka kuona namkodishia kwa jero tu....huyo jamaa na ustarabu wake nae kuna cku alinikodi na yeye cd.Tokea hapo alikua mdau sana wa porn yan mpk leo navyosimulia hiki kisa.
Kuna siku moja niilikua class nimesikilizia tu kiaina huku nasubir muda ufike wa break ili niondoke zangu shule.Na kweli kengele iligonga ya break basi me niliwai kutoka nje nikaenda form 4 C lengo langu niwafungie mlango ili wasitoke break ilikua nafanya kama utani tu.
Na kweli niliwai nikawakuta bado wako darsan alafu wapo kimya, me nikafunga mlango kwa nje bila wao kuniona.



kumbe humo class kulikua na ticha ubaya huyo ticha ni mfupi hata ckumuona vzr kama yumo humo class....niliondoka nikawa nasuburia kuona jinsi watakavyo sumbuka kufungua mlango, na kweli nilikua naona mlango unasukumwa kwa nguvu ili ufunguke lakin wapi mtalaamu nilikua nimesimama chin ya mti nacheka tu.
Nilishanga kumuona huyo kipanga wa darasa anaitwa na huyo ticha kupitia dirishani ( hapo ndo nilijua kumbe ukimya wote ule kumbe ticha alikuepo class nikasema ngoja nijikaushe kama sio mimi ).....mlango ulivyofunguliwa wa kwanza kutoka ni huyo ticha, alikua amevimba kwa hasira na kibao kikamuangukia huyo kipanga kuwa yeye ndo kafunga mlango.
Kipanga alivyomjinga c akanitaja kuwa aliniona nikifunga mlango, kwa vile nilikua pembeni na wao basi ticha aliniita akatupeleka staff me pmj na huyo kipanga.
Tulifika ofisini kipanga yeye ni kulia na kujitetea tu kuwa sio yeye alie funga mlango bali ni mimi ndo aliniona, me pia nilikataa kata kata kuwa sio mimi.
Ko ikabidi tule wote bakora mimi na kiranga.Kiranga alilia sana siku hadi nilimuona fala kwanzia hapo japokua ndo urafik ulikua mkubwa tu.
Mwingine nilie muona ni fala ni kiranja wa stoo, huyu alikua mjinga sana tena nilimpiga makofi sana.nakumbuka tukiwa kwenye paper ya history niliingia na nondo za kutosha na zote zilikua mule mule kwenye mtihani.
kipindi nazitumia hizo nondo kumbe huyo kiranja aliniona ( nilikua nimekaa karibu nae ) alinisemesha kwa sauti ya chini kuwa nimpe hizo nondo na yeye atumie.
Nilimpa paper yangu moja ya kujibia maswali ili akopi then anirudishe...alivyomjinga c akakopi mpaka jina langu kwenye karatasi yakee.
Kesho tukiwa kwenye paper ya civics akaingia teacher wa history akauliizia holy holm ni nani humu nikanyoosha mkono kuwa ni mimi.Basi akanambia "
yaani wewe na ujinga wako majibu uliyoandika na huyo mwenzako kaandika hivyo hivyo mpaka jina lako kaandika kwake"....wanafunz walicheka ko ticha aliendelea kusema "
nakupa zero wewe na huyo mjinga mwenzio" siku jibu kitu nilikua kimya maana ilikua c mara ya kwanza kuwekewa zero kwasababu ya ku cheat kwenye paper niliona kawaida tu.ila huyo kiranja muda wa kutoka shule nilimpiga vibao vya kutosha alafu alikua ananiogopa vbya mno.nilimwambia ahakikishe cpat zero lasivyo anipe hela kama fidia...jamaa alilia nimuhurumie nikampiga makofi nika mwambia sasa ukaseme kuwa nimekupiga...alikimbia kama kuku nilivyomuacha.
Binafsi darasani nilikua ni mpole lakin naogopeka ukinichokoza tena kipindi nipo form three ingawa ckuisoma sana ( ndo kipind nilkua nateka watu simu zao )...lakin mademu tu ndo nilikua nawaonea aibu cjui kwanini kumwangalia demu usoni dakika moja nilikua siwezi kabisa.
Nirud kwa huyo kiranga, baada ya lile tukio la kumfungia teacher mlango basi huyo kiranga alikua analazimisha urafiki na mimi sana.sema yeye hakufanya mtihani wa taifa alichanganyikiwa ( cjui akili zilimzidia )...alimaliza from four mwaka ulio fuata.
Nilipotezana nae huyo kiranga tokea hyo 2013 mpk 2017 ndo tulikutana alikua amekua baunsa kinoma alivyoniona siku hyo nakwambia alifurah kinoma kuniona.kipind hicho anasomea udokta lakin akili zake kama sio nzur hivi.Ndoto zake ni awe pornstar kumpita John Dhambi na Bryan ( kwa maelezo yake huyo jamaa alivyokua akinambia )
Me nilikua namkubalia tu hizo ndoto zake namwambia unaweza jamaa wewe pambania ndoto yako.Alikua ananichosha kitu kimoja jamaa anapenda picha kuliko kula, yani asubuhi bado watu tumelala yeye kashatoroka chuo kwao kuja home nikampige picha ( alikua anasoma chuo kile pale hospital ya mkoa )
Jamaa alisababisha cku moja hata kiboko angetuua.Kama kawaida yake alikuja asubui kuwa nikampige picha kule ziwani ( pump house ya zamani ) huko ziwani karibu na kwa mkuu wa mkoa siku wamekataa hakuna mtu kupita kwenda kule Tembo beach kwa sababu ya usalama wao maana viboko huwa wanakuja midaa ya usiku kula mlo wao alafu ile asubui wanarud ziwani.
Sasa siku hyo huyo kiranga alivyokuja ili nikampige picha huko ziwan hatukujua kama bado kuna viboko havijasepa....tulifika vizr tu nikaanza kumpiga picha ufukweni mwa ziwa, kwa pemben walikuepo wafungwa wana mwagilia bustani ya nyanya kwa mkuu wa mkoa.
Nilivyokua na mpiga picha tulisikia kitu kinatoka kichakani kuja huku tulipo, kumbe kilikua ni kiboko ndo kinarud ziwani kilikua kiko speed hatari, jamaa alivyo fala ( ndo maana namuita fala ) yeye ndo aliwai kukiona badala anambie kuwa ni kiboko yeye alikimbikia bila kunambia afu kibaya kipindi anakimbia alini push nikaanguka mimi na kisimu changu ( kisimu kililoa kikawa hakipigi picha vizur )...yani cku ni Mungu hakupenda tu nife..nilivyokiona kiboko kinakuja nilipokua kwa pembeni kulikua na fensi za seng'enge kiwanja cha Mchina mmoja ni dokta, nilikimbia nilizipanda zile fensi na zilikua zina vi ncha lakin cku jali niliona bora kuumwa na mbwa wa mchina kuliko kuuliwa na kiboko.Na kiboko ni kikubwa asiee ilikua sio mara yangu ya kwanza kukiona lakin ilikua ni mara yangu ya kwanza kunifukuza.
Nilivyoruka fence niliingia kwenye zizi la ng'ombe lilikua hapo kando maana mbwa wa mchina nao walikua wananibwekea cjui walijua me ni mwizi.
Kiboko kilivyonikosa kiliingia zake ziwani hku kinapumua maji ni kuruka juu.Nilikaa zizin mule mpk mchina na mlisha ng'ombe wakaja maana walisikia mbwa wanabweka sana.ndo nilitoka walivyowatoa wale mbwa.
Yule kipanga eti ndo akawa anarud sasa yupo na baadhi ya wafungwa na askari jela mmoja nilimwangalia vbya huyo kipanga nilimuana sio mwana ila cku mwonyesha kama nimechukia.Nilijichana kwenye paja na zile ncha za fensi kipind niliidandia kuruka.
Watu wanapitia shida lakin me nae hili tukio nitalisimulia vizaz na vizazi kama Mungu ataniruhusu kusimulia.
Zoez la kupiga picha liliishia pale mpaka leo ziwani kusipokua na watu wengi cwez kuogolea au kupita mwenyewe.Kwa mliokuwa Musoma 2017 kama mnakumbuka kuna tukio lilitokea la viboko kupindua mtumbwi wa wavuvi na wavuvi wanne walikufa maji eneo lile lile la pump house ya zamani sasa baada ya mimi kukoswa na kiboko ilipita muda kidogo ndo hilo tukio likatokea.mpaka Mkuu wa wilaya aliahid kuweka mitego ya viboko lakin hakuweka mpaka leo.
Tuliondoka na kipanga tukaelekea town huku ananipa sifa za kinafki kuwa me ni hatare sana.nilimuacha tu hata kama ningempiga isingesaidia kitu.
Nikirud nitasimulia sasa ni jinsi gani nilivyoshikwa kabla hatujaendelea mbele zaidi.