Hadithi nahadithia leo

Mapinduzi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
2,422
96
Siku za karibuni mume wangu kipenzi, al aziz, nuru ya macho yangu kwa siku tofauti amekuwa akisumbuliwa na magonjwa kama vile tumbo, homa, kichwa, malaria na siku nyingine uchovu uliopindukia. Haya yote yalisababisha dia wangu arudi nyumbani kupumzika. Pamoja na hayo ufanisi wake kiunyumba ulikuwa umelegalega. Pia amebadilika tabia na kuwa mtulivu nyumbani, hata kutoka toka weekends au nyakati za jioni anapokuwa fit, amepunguza kama sio kuacha kabisaaa. Nilimshukuru Mungu kwa kumtuliza mwenzangu huyu nyumbani, kwani kutokatoka nako kuna mengi.

Jana majira ya saa saba mchana nilipokea simu toka kwa mume wangu, barafu wa moyo wangu kuniarifu kuwa anaumwa sana, na amekwenda hospitali kapimwa na kugundulika ana malaria. Kwa jinsi anavyojisikia vibaya inambidi arudi nyumbani mida ile ile nyumbani kupumzika. Aliniambia nipitie duka la dawa nimnunulie dawa alizonitajia. Nilisikitika sana na hizi homa zinazomsumbua baba watoto wangu, ikanibidi niondoke kazini muda ule ule, nipitie duka la dawa na kuanza safari ya kurudi nyumbani kumliwaza.

Nilipofika nyumbani, niligonga sana geti, halikufunguliwa. Niliomba msaada kwa kijana wa jirani akapanda ukuta na kunisaidia kufungua geti kwa ndani. Nyumbani palikuwa kimya mno, gari ya mwenzangu ilikuwepo, na msaidizi wa kike wa kazi za nyumbani sikumuona kama nilivyotarajia na nyumba ilikuwa imefugwa. Jasho lilinitoka kuwa labda mpenzi baba wa watoto wangu kazidiwa na kupelekwa hospitali au hata ameshaaga dunia nikirejea alivyokuwa akilalamika kuumwa sana. Nilipiga simu yake ya mkononi haikupokelewa, ya msichana wa kazi haikupokelewa pia.

Nikazidi kuchanganyikiwa nianze kufanya nini na nianzie wapi. Nifungua nyumba kwa funguo zangu, nikaenda chumbani kwa binti hayupo, kwa watoto hakuna mtu. Mwisho nikaingia chumbani kwangu. Nikaingia chumbani kwangu......nilichokiona sikuamini. Nikatoka na kwenda kumwita jirani yangu alisaidie kuangalia pengine angeelewa. Jirani yangu kidogo azimie.... mume wangu na msaidizi wangu wa nyumbani walikuwa wamelala fofofo kitandani kwetu, wakiwa kama walivyozaliwa!

Naomba niishie hapa.
 
lewinski hebu malizia mpenzi ndio nini kutuacha njia panda,,,,,la pili pole hayo yapo si kwako tuu wanaume si wakuaminika wallah kumi kwa mmja kama sio wote,,pole sana allah atakupa maliwaza habibty lakini hebu malizia kidogo tuu usifanye hivi jf watakasirika,,,,,
 
anaza marriage viktim.
pole dada, muda si mrefu magreti thinka watakuja kukuliwaza. usihofu.
 
lewinski hebu malizia mpenzi ndio nini kutuacha njia panda,,,,,la pili pole hayo yapo si kwako tuu wanaume si wakuaminika wallah kumi kwa mmja kama sio wote,,pole sana allah atakupa maliwaza habibty lakini hebu malizia kidogo tuu usifanye hivi jf watakasirika,,,,,

Nililia, nikajuta, nikalalamika. Mwenzangu aliomba radhi na kusema ni shetani alimpitia. Msichana kaondoka bila kufukuzwa.

Kwa upande wangu nilipewa pipi nikatulia, leo nashare kitanda na huyu bwana, tena. Naconnet dots uhusiano huu ulianza lini, na hatua gani nichukue. Sijijui sijielewi sijutambui.
 
Hadithi yako nzuri, inatufundisha nini?

Inatufundisha ukilala na mume ama mke wa mwenzio malipo ni hapahapa duniani. Ms. Lewinski alirodoka na mume wa Hilary sasa leo yeye kaja kulia msaidizi wake wa nyumbani karodoka na mumewe!
 
Ur H'ban wasn't sick, wanted u to know how sweet the H'gal is....Trust me!!! Kutulia kwake ni kuwa karibu na kipenzi chake H'gal....Na kukuonyesha kuwa anakula tunda ndo maana akakuita uje uone...Ni unyama sana ambao mie naweza hisi kuwa ni kisasi....Hii story umeianzia kati...Anza mwanzo ili yujue wewe ulimegwa na nani hadi yeye akaamua kummega H/G??? POLE
 
Kata hiyo kitu tupia mbwa wale shameless, useless, gud 4 nthn man.. On ur matrimonial bed kha amevuka mpaka aisee! Hata cjui ingekuwa mm ningemfanyeje kama hadithi tu imenipa hasira hv..
 
Nililia, nikajuta, nikalalamika. Mwenzangu aliomba radhi na kusema ni shetani alimpitia. Msichana kaondoka bila kufukuzwa.

Kwa upande wangu nilipewa pipi nikatulia, leo nashare kitanda na huyu bwana, tena. Naconnet dots uhusiano huu ulianza lini, na hatua gani nichukue. Sijijui sijielewi sijutambui.
are u serious?kama ni true aisee pole sana bidada
 
Back
Top Bottom