Hadithi ya Ndoa yangu

Nyamwi255

JF-Expert Member
Dec 2, 2022
3,285
8,189
Ilianza Send off, hii ilifana sana mpaka nikajiuliza kimoyo moyo harusi itakuwaje!

Naam siku yenyewe ikafika haloo, sijui hata niseme vipi ila dah harusi yangu ilifana sana sana!

Picha linaanza nilifanyiwa bonge Moja la surprise (Nakazia tuishi peace sana aisee) hizi surprise nilifanyiwa na watu ambao nafahamiana nao ningefanyiwa na watu wa karibu na familia ningesema ni matunda mazuri ambayo wazee wangu na familia kwa ujumla wameyapanda kwa watu hao ila haikuwa hivyo.

Hawa ni watu wakiwemo walimu wangu WA P/s, secondary na chuo, wanafunzii wenzangu, staff mate wangu mbalimbali ambao niliwaho fanya nao kazi intern kabla sjaajiliwa hapa nilipo leo.

Hizi ni surprise babkubwa saana en very expensive mpaka wazee wangu wanashangaa jinsi mtoto mbichi wa 2000 kasoro nilivyo na circle ya watu wa maana kabisa.

Ukiwatoa wazazi wa Pande zote mbili yaani hamna mwanafamilia aliyetoa zawadi za gharama namna Ile. Yote tisa, kumi kuna watoto kama under 12 hawa walifunga safari kutoka kigamboni mpaka Tabata wakiomba waingizwe kwenye hall wanione.

Ubaya hao watoto wapatao 7 walikuwa hawanijui jina waliishia kuniita "mwanangu sana" hili ni jina ambalo huwa namuita mtoto yeyote niliyemzoea hasa Wanao Kaa karibu na nyumbani huku nikimpa tano👊

Hivyo Hawa watoto walinizoea sana, walipofika walikataliwa kuingia ndo mmoja wa wasimamuzi wa harusi alitoa amri kuwa waingie.

Haloo nilivowaona tu sikutegemea dah. Walikuja mbele yetu ... (😭😭 Hawa watoto waliniliza sana), msemaji wao alisema "ndugu wageni waalikwa mtusamehe kwa kuwaingilia kwa sababu hatukuwa kwenye ratiba ila sisi tumekuja kwa ajili ya "mwanangu sana"(watu wakacheka) huwa tunaishi nae vizuri na ni msaada mkubwa sana ila tunasikitika kuwa hatutakuwa tunamuona mara kwa mara kwa sababu wanamchukua. Sisi ni wanafunzi hatuna zawadi ghari ila tunaomba mturuhusu tutoe hiki tulichobarikiwa.. mwakilishi wao akafungua mfuko akatoa bibliia na Quran ambazo zilikuwa sio mpya, yaani zilichakaa.

Binti mmoja wa kiislamu miongoni mwa wale akaanza kutuombea Dua huku akiwa ametushika vichwani Mimi na mume wangu ambayo ilifanya watu waliehuku wakiitikia amiina. Mvulana Mmoja mwingine huyu ni mkristo ila sjui dhehebu gani naye alituombea Dua yenye maneno mazito....basi bwana hawa watoto waliniliza sana!! Sio Mimi tu ila Kila mtu aliyekuwa kwa halll ilimtachi sana!!

Hawa malaika walionesha upendo mkubwa sana ambao sikutegemea, baada ya hapo hawa watoto walimiminiwa pesa kama Tsh. 200,000 kwa upendo walionesha. Mimi pia niliwatunza pesa Tsh. 50,000 pamoja na ahadi (sitoisema hapa)

Vilio vya Furaha pale ukumbini vilikatishwa na staff mate wa mume wangu ambao walikuja kututunza packets 14 za karanga😁 hii iliwafanya watu pale ukumbini waangue vichekoo na kusahau kama walilia machozi ya Furaha yaliyosabibishwa na wale watoto muda mfupi uliopita.

Basi maharusi tulienda kupumzika. Nilimwambia mume wangu nimechoka hivyo tupumzike ...mume wangu alinielewa na tulipumzika. Ilipofika alfajiri alinambia bila shaka uchovu umeshaisha nikamwambia Naam. Kilichofatia hapo......

Itaendelea......
NB: Picha haihusiani na nilichokiandika😊
1720199762567.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom