Yajayo yanafurahisha
New Member
- Jul 20, 2024
- 4
- 33
Mimi ni muajiriwa katika sekta ya umma mke wangu sio mwajiriwa yaani ni mama wa nyumbani. Tuko kwenye ndoa ya kikristo kwa miaka 14 na tumejaaliwa watoto.
Ili kupunguza ukali wa maisha na kuondoa utegemezi kwa mambo madogo madogo, niliamua kufungua kibanda cha duka na kumkabidhi mke wangu ili kisaidie kwa baadhi ya mahitaji muhimu ya nyumbani huku Mimi nikitumia sehemu ya mshahara kuwekeza kwenye maeneo mengine ya maendeleo.
Ni mwaka mmoja na miezi kadhaa imepita tangu nimfungulie mke wangu biashara lakini jambo la kusikitisha ni kuwa sioni tena faida ya kibanda kile maana mke wangu anabadilisha aina za nguo na marashi huku nikimuuliza anadai kuwa ananiheshimisha kwa watu. Pia ananitangaza kwa ndg na jamaa zake kuwa sitoi matumizi yeye ndiye anayetoa matumizi.
Tumekaa vikao kadha wa kadha tukihusisha ndg zetu lakini haonekani kubadilika na kikao cha mwisho alitamka kuwa mtaji wangu umeishahivyo uliomo ni wa kwake.
Hali hii imesababisha migogoro ya mara kwa mara na sioni tena raha ya ndoa.
Pia hali hii imenijengea tabia ya kumchukia mke wangu mara kwa mara ninashikwa na hasira hata bila sababu ya msingi japo kiukweli Sina nia ya kuvunja ndoa yangu bali ninahitaji mke abadili tabia.
Ninaomba ushauri ili kunusuru ndoa yangu.
Ahsanteni.