Hadithi: My Soulmate

equator

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
214
250
My Soulmate Episode 1

Produced by EquatorStory Specials

Stela :”Nickson uko wapi jamani ?? Mpaka sasa umechelewa sana.”. Ilikuwa ni sauti ya stela akimngojea mpenzi wake Nickson alie kuwa njiani akitokea kazini .

Nickson:”Nimekuona mpenzi hapo ulipo nakuja jamani.”. Nickson alisogea taratibu kumfikia mpenzi wake aliekuwa akimngojea na jazba taratibu ilianza kupanda kisa mpenzi wake amechelewa.

Nickson:”Mambo mpenzi?”.

Stela :”Mxxheeewww ”.

Nickson: “Jamani mpenzi nisamehe bure tu jamani ni kazi.”

Stela:”Aaah kazi gani bhana..???.” Stela aliuliza kwa hasira akianza kuhisi mpenziwe hamchukuliii serious.

Stela:”Haiwezekani tuuupange huu mtoko karibu mwezi mzima alafu uchelewe!. Baby kweli unanipenda???.” Stela alitamani kuondoka akasimama kwa hasira.

Stela:”Nenda kalale na hiyo kazi yako kama unaipenda hivyo. Maaana wewe unatumia matope ama ubongo?. Mimi si nimeondoka kazini mapema sana yani we bado hata ndo unatoka sasa. So hujapitia nyumbani kuoga ushaaanza kunukia jasho.”Nickson akamshika mkono kwa nguvu na Stela akaaanza kumpiga vikofi kwenye mkono aliemshikia Nickson ili asiondoke .

Nickson: “Baby am sorry nakupenda wewe lakini bila hiii kazi sidhani kama tungekua hapa. Baby ni dakika 20 tu jamani. Tafadhali nisamehe sitorudia mpenzi.”Stela akaaanza akakumbuka aliwahi kumwambia Nickson kipindi hicho “Mapenzi hayaliki”.

Stela:”Sawa nimekusamehe lakini usirudie tena. Lakini baby….”Stela aliamua kumsamehe na wakaaanza maongezi yao .

Nickson: “Stela sema mama!..”.

Stela:”Baby kweli wewe tunapanga mtoko unanpangia na kitu cha kula mimi si mpenzi wako natakiwa nile kitu nachotaka bhana.”Stela alisema huku akiwa na ka uchungu.

Nickson :”Baby..”.Stela akamkatisha.

Stela:”Subiri sijamaliza kuongea ”. Nickson alikaa kimya akimsikilizia mpenzi wake .

Nickson :”Sawa mama zungumza ”.Nickson aliamua kuwa mpole na kuwa msikivu kwa sababu ana amini kwamba katika mahusiano lazima kuwe na usikivu pale mmoja wapo anapotaka kuzungumza .Nickson alikaaa na kuweka mkono wake wa kuume kidevuni huku akikuna taratibu ndevu zake mbili tatu.

Stela : “Huwezi ukaniambia ety pamoja na kusubiri huu mtoko mweeeezi mzima unaniambia bajeti yako ni 10,000 tu?”.

Nickson : “Mama ..”. Stela alimsimamisha hapo kabla hajafika mbali .

Stela:”Eeeeeh nishakwambia uache kuniiita Mama unanizeeesha bhana.”

Nickson:”Am sorry baby. Unajua nataka uwe mama watoto wangu tena nataka motto wa kwanza aitwe Rose kama ni wa kiume ataitwa Samuell”.

Stela:”Nickson am serious na swali langu.”Stela alioneka akianza kunyanyua nyusi ya kulia na kupindisha shingo kidogo kama anavyofanyaga akiwa na hasira au akiwa serious na jambo.

Nickson :”Sawa Ma… I mean sawa Baby stela…. Nakujibu “.

Stela : “Enheee…..”. Stela alikaaa chonjo kusikilizia jibu huku akisogeza nywele zake za rasta zijulikanazo kama yeboyebo na kucha zake alizongezea za bandia za rangi ya nyekundu ili zisi mghasi .

Nickson:”Baby unajua mimi nina majukumu na laki na nusu nimetoka kwa ajili ya project.”.Stela akamkatisha hapo hapo .

Stela :”Tena ishia hapo hapo.” Mara wakasikia sauti ya mtu mwingine kutazama ni waiter wa pale hoteli waliopo ijulikana nayo kama “Mwambao hotel” iliopo upande wa pili kutazamana na Stand ya ma bus “Dar express”.

Waiter:”Jamani za jioni Kwema hapa!?”.Waiter aliuliza kwa sauti ya upole na kwa sauti ya ukarimu.

Nickson & Stela: ”Salama tu.” Wote waliiitikia kwa pamoja kama waliambizana kujibu hivyo.

Waiter:”Niwahudumie nini joini ya leo?”.

Nickson : “Kuku nusu kiasi gani?”. Nickson aliuliza akimwangalia waiter kwa makini asikie bei chapu apige hesabu ya fasta .

Waiter:”Ni 6000”. Waiter alijibu lakini akaongezea . “Kwa sasa kuku zimeisha ndugu labda kama hamtojali mchukue nyama choma nusu 5,000”.Nickson moyoni akajisemea kumbee bora hata bajeti itaaenda sawa sawia.

Nickson:”Sawa naomba hiyo hiyo”. Akamgeukia Stela na kumuambia. “Baby utakula na nini? “

Stela : “Na chipsi tu”. Stela alisema hivyo akizungusha macho maaana anajua ingekua mtu mwingine angeagiza nyama kilo na ndizi kama tano. Ili apate na ya kumbebea mdogo wake aliemwacha (Yunis) nyumbani.

Nickson:”Na mimi naomba na chipsi .” Alisema huku ana piga mahesabu yake “chipsi 2x2000 =4000 na nyama choma 5000 so inakuwa 9000 na soda moja 10,000 yake imeisha.”.Nickson akamgeukia mpenzi wake .

Nickson:”Baby unakunywa na soda gani?”.Alimuliza mpenzi wake kwa upendo na ujasiri kuwa bado yupo ndani ya bajet ya 10,000.

Stela : “Na grand malta.” Stela alijibu akiangalia upande mwingine wa hoteli ile ilokuwa bize kweli na ma bus yakishusha watu kutoka sehemu mbali mbali.Nickson moyoni alistuka kidogo akajisemea “Kiiiiibo na grand tena?”. Nickson akamwai waiter wakati stela akiangalia ma Bus “Mwambie haipo..” alisema kwa mdomo bila kutoa sauti.

Waiter:”Samahani Grand malta zimeisha”. Nickson akadakia fasta .

Nickson:”Leta na supa leta tu si ndio beby?. “alimuliza stela akiwa na confidence hawezi kataaa ndo soda aliokunywa walipo enda uzunguni park mara ya mwisho .

Stela :”Ndio na supa-leta ya moto tafadhali”.Stela alijibu akiwa hajui kuwa hana namna .

Waiter:”Sawa chipsi mbili na nyama choma na supa leta. Kaka utakunywa nini?”. Waiter alitaka kujua Nickson atakunywa nini.

Nickson:”Ah mi nina hii tayari”. Aliwahi kumwonesha soda ya takeaway alie kuja nayo .Sawa waiter akaondoka na kuwaacha wakiendelea mazungumzo yao.Nickson alitumia hizi sekunde kadhaaa akimwangalia mpenzi wake alivyo. Stela hyo siku alikua amevaaa suruali ya jeans inayombana nakuonesha umbo lake kiasi flani cha kuvutia . Alikua kavaa t-shirt ambayo Nickson alimpa kama zawadi imeandika na maaandishi kwa nyuma ikisema “ExonGraphics” ambalo ndo jina la kampuni ambalo Nickson anatarajia kufungua hivi punde.

Nickson:”Enhee mpenzi ulikua unasemaje?”. Stela alimgeukia taratibu akiwa anaonekana kuwa alizama kwenye kukuru-kakara za pale stand inayo tazamana na hotel waliiopo.

Stela:”Nataka ugali maharage”. Alijibu hapo wakaaanza kucheka yeye pamoja na Nickson wakikumbuka kipindi kile ambacho Stela alimjibu Nickson wakati huo bado mahusiano yao hayaja anza alikua akimtesa tu na vituko vya stela vya hapa na pale.

Stela:”Baby lakini kweli mi nakushauri uachane na hiyo project bora ufanye biashara nyingine kama kuchukua nguo kwenye soko la maimoria uje uuuze nipe hata mimi nitakuuzia. Pia ntakusaidia kuchagua.”

Nickson:”Lakini baby mimi nikipata Camera moja tu inanitosha kutoka katika maisha haya ”.Nickson alisema akiwa na matumaini.

Stela :”Kwani Camera kiasi gani?”. Aliuliza akitaka kujua yamkini ata weza kumpa ushauri.

Nickson : “Camera nzuri laki saba na lenzi laki tatu. “. Stela alianza tena kupandisha nyusi ya kulia akaweka nywele tena vizuri akanyoosha mkono kumuashiria Nickson aaache kuongea.

Stela : ”Sawa na umechanga sh ngapi mpaka sasa!? ”. Stela aliuliza huku amesogeza kichwa mbele na sikio linamtazamia Nickson asikie jibu kwa makini.

Nickson:”Ndo nimetoa laki na nusu sai….”. Stela akamkatisha.

Stela:”Baby iyo hela nyingine utapata wapi?”.

Nickson : “Ntajichanga tu Baby namwamini Mungu ”.Stela akawa ana guna mhhh mhhhh.

Stela: ”Sawa iyo hela yote uka nunue Camera uanze kutafuta wa kuwapiga picha na Studio huna na Laptop yako yenyewe ndo hyo……. ”. Stela ali kuwa kimya kidogo

Stela :” Baby kuwa mjanja umesoma mpaka umemaliza chuo umemaliza huezi kufanya vitu vya kijinga hivyo”.

Nickson : “Hayaaa sasa ushaaanza..”Nickson alijua tu wataaanza kugombana kisa mipango yake.

Stela : “Nishaanza nini? Afu nishakuambia usinikatishe nikiongea.”Stela aliendelea tu kuongea kama ana rap nyimbo anayoipenda.

Nickson: “Sasa mpenzi sikia nikuambie kitu mimi ntakupa hela uongeze na yako tuanze biashara”.

Stela : “Nickson mimi nitawezaje kutoa hela hapo na unajua dhahiri ya mimi ni secretary wa pale Matumizi Company ya Yule Mmasai Vicent Mbekure ”Stela alikua anaongea kudhibitisha hela ndogo alionayo .

Nickson:”Sawa Baby mimi nitafanya kukupa ”.Nickson sio wa maneno mengi sana na alijua mpenzi wake anataka kumwambia kitu gani.

Stela : “Sawa mimi ntaenda maimoria mwenyewe ukinipa ”. Mara waiter akaja

Waiter: ”Jamani chakula chenu kiko tayari. Munaweza kwenda kunawa pale mkihitaji waiter alisema hivyo akinyoshea mkono bomba la kunawia. “Jamani karibuni na mu enjoy.”

Nickson wakasimama wakaenda kunawa kama walivyoshauriwa wakala kwa kucheka kulishana hapa na pale. Mara wachokozane. Walipo maliza Nickson alilipa bill iliyo kuja kama alivyotegemea na kupigia mahesabu . Nickson akampa mpenzi wake nauli na pia akaanza kutembea kwa miguu kuelekea ghetto kwake.

Stela : “Baby kwaheri! Nimeshiba” . Alimwita Nickson aliokuwa ameanza kutafuta njia ya kwenda nyumbani kwake . Nickson akageuka aka mpulizia busu la hewani mpenziwe.

Itaendelea….
 

equator

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
214
250
MY SOULMATE EPISODE 2

PRODUCED BY : EQUATORSTORY SPECIAL

Ni alfajiri ya saa kumi na moja tuna muona Nickson akiwa kitandani kwake amekaa akiwa ana soma kwenye simu yake yeye sio mwanafunzi na isitoshe kamaliza chuo miaka kadhaa iliopita.Lakini kwa sababu Nickson hajaridhika na mahali alipofikia katika tadhnia yake mambo ya computer ama kwa kimombo tunaeza sema (IT).Nickson ameamua kutoa japo lisaaa la kuwa anasoma vitu kadhalika ili kuwa sambamba na ulimwengu huu ya maswala ya technology yanayo badilika kila siku. Mpaka ilipo fika saa kumi na moja na nusu akaaamka akabandika maji ilia pate ya kuoga kujiweka fresh kimwili na ki akili saa kumi na mbili kamili akaya bandua jikoni alipo kuwa ameyaweka kwa jiko la gas ili yasipate moto sana. Akaweka kwenye ndoo yake kijani na akiwa na taulo lake lililo chorwa picha ya Paris na limeandikwa welcome again. Sijui kama aliwahi fika Paris but haya ni ma taulo ya wageni kwenye ma hoteli ma kubwa makubwa yamkini alilipata mtumbani?. Nickson alipo bandua maji aka anza mchakato wa kupika tambi ambazo ndo atazokula mchana ili kuoka bajet yake. Akafungua mfuko wa tambi akijaribu kuzigawa nusu kwa kutumia kipimo cha macho. Akawacha nusu kwa ajili ya siku ifuatayo akavunja vunja zile alizo chagua kama mara 6 hivi ili kuzifanya ziwe ndogo ndogo ziweze kulika . Aka wacha maji yakiwa jikoni yapate moto ili akirudi aendeleee. Nickson akabeba ndoo na maji yake akaenda kuoga haraka akarudi akamalizia kupika tambi na kuweka kwenye container akafunga vizuri akaweka kwenye begi lake. Akachukua nguo zake na kuvaaa akabeba na simu akaondoka kwenda kuanza shughuli yake za kila siku.

Nickson : ”Chief kwema umeamkaje bhana?”.Alikua akimsalimia mlinzi aliekuwa amekaaa maeneo ya ofisini kwenye kampuni ya Matumizi App.

Mlinzi : “Fresh Chifu naona unawahi kweli siku hizi!?”.Mlinzi alijibu.

Nickson : “Chifu si unamjua boss Sambeke alivyo mkorofi.?”.Mlinzi alidakia kwa kukubaliana naye.

Mlinzi : “Aaah Yule mzee Sambeke achana naye bhana. Yani…”Mlinzi alianza maneno yake kama kawaida amabapo ukimpa nafasi haaachi kuzungumza.

Mlinzi : “Mi nakuambia huyu jamaa hana mtu anao ishi nae sio mke wala ndugu wala mtoto.”. Nickson akadakia kwa mshangao.

Nickson : “Weweee usiniambie… Man!?” Nickson alionekana kuhitaji taaarifa zingine japo kuwa haaamini amini.

Mlinzi : “Ndio Chifu mi nakumbuka nlishawahi kulinda kwake miaka kadhaa iliopita pako kimya jumba kubwa lakini ndani inawaka taaa moja tu!.” Maongezi yao yalianza kunoga wakiwa wanasubiria mlango wa ofisi ufunguliwe ili Nickson aweze kuingia.

Nickson: “Au ulishuhudia yote wakati watu wote wamelela? .”.Nickson alimuuliza mlinzi bila kua amini amini.

Mlinzi : “Hapana man nimekaaa pale mwezi nikilinda na sijaona watu wengine zaidi ya wafanyakazi tu. Boss wetu Sambeke alitumia mda mrefu sana ili kupata mafinikio mpaka mke wake Wanjiku alimuacha maaana alikua anakaaaa mwezi hapigi kitu yake .”Nickson akadakia tena.

Nickson : “Mwezi hapigi kitu anaumwa ama? “Mlinzi alimdakia na kwa kuashiria yupo serious kwamba ni kweli.

Mlinzi : “Hapana chifu alikuwa anajifanya bize sana kazi tu kumpa vitu vya thamani mke wake mambo mengine kama baba wa familia alikuwa hagusi saivi mke wake kaolewa na kadogo ambako hana hela lakini anamjali sana.”Mara wakakatishwa na sauti ya stela.

Stela : “Habari za asubuhi jamani”. Stela aliuliza huku akiwa anatafuta simu kwenye pochi yake alio kua amebeba . Nickson alichukua nafasi hiyo kumwangalia Stela vizuri ambaye ndiye mpenzi wake na secretary wa boss Sambeke. Nickson na mlinzi wakaitikia kwa pamoja.

Mlinzi & Nickson : “Kwema tu hatujui wewe.”

Stela : “Aah salama tu”. Stela alifanikiwa kutoa funguo alizokuwa akipekuwa huku Nickson hajabandua macho yake kuangalia alichokua amevaaa. Stela alikuwa amavaa Blauzi ya Blue na Sketi fupi nyekundu ambayo ilikuwa imembamba kweli na kuchora ka figure yake kidogo.

Nickson : “Mambo mengine lakini?”. Nickson aliuliza hivyo utasema sio mpenzi wa Stela maaana bado hawaja report mahusiano yao kwa Manager wao ili wajulikane ni wapenzi na sheria za kazi haziruhusu vitu kama hivyo . Kwayo wameamua kuya ficha kwa muda mpaka mapenzi yao yatakapo kolea.

Stela : “Kwema tu” Stela aligeuka na kumuangalia Nickson . Ambaye alikua amevaaa kama anaenda kanisani nguo zote alio vaaa ni za kitambaa na sio nyembamba kama za wakaka wengine lakin angalau yupo smart.

Nao wakaingia ndani Nickson akageuka kumu ashiria mlinzi kwamba maongezi yao yanaeza endelea. Nickson akatoa bahasha ya kaki aliekuwa amambea mpenzi wake vitumbua ili anywee chai hii ni kuonesha kujali tu.

Stela : “Vitumbua umenunua jana nini?”.Stela aliuliza akiwa amepindisha mdomo kidogo na ka kushangaaa kiasi .

Nickson : “Leo asubuhi jamani Mpenz…. I mean stela.” Aliogopa kutamka neno mpenzi aki hofia anaeza sikika akafukuzwa kazi mara moja.

Stela : “Akasema mbona vya baridi jamani sasa mimi nakulaje!?. Bhana mi nipe buku nikanywe supu.”.Stela alisema huku akiwa ametoa mkono nje katika namna ya kupokea .

Nickson : “Acha ushamba wewe kuna Microwave tuvipashe bhana.”Nickson alipotezea hyo bajet nyingine ya supu isiyo na mpango. Nickson akachukua akaweka kwenye microwave akaweka na mda na kiasi cha joto cha kupashia. Akaenda kukaaa na kuwasha computer aliopewa ili aanze shughuli zake na wafanyakazi wengine wakaaanza kuingia katika kampuni hiyo ya Matumizi App.

Angela : “We muinjilisti wa tabora mjini umeamkaje!?”.Hiyo ni sauti ya Angela mmoja wapo wa wafanyakazi katika kampuni hiyo . Nickson alipogundua ni Angela anamtania kama kawaida yake alianza kutabasamu na kujibu.

Nickson : “Bwana Yessssssu asifiwe…?”. Nickson aliangualia ka kicheko huku Angela akimwangalia kwa tabasamu bashasha.

Angela : “Ah we acha kunihubiria saivi umetumwa nini!?” Angela alijibu huku akiwa anaanza kucheka .

Nickson : “Kwema lakini!? Jamani!?”. Saivi Nickson alijibu huku akiwa ana angalia simu yake ilio toa mlio wa kua ashiria messeji mpya.

Angela : “Kwema vipi ile kipande cha presentation ulicho nipangia si umekipata?”.Alimuuliza Nickson aliokuwa ana soma text mpya aliokuwa ameipokea kwenye simu yake.

Nickson : “Ya niliipata kwenye email asubuhi nimeisoma nikiwa njiani nikawa najiuliza uliandika wewe au aliandika mtoto wako? Sio kwa huo mwandiko mbaya”.Wakaaanza kucheka tena.

Angela : “Acha kunichora mwandiko wa mtoto kwenye computer bhana!?. Haahahah”. Nickson akawa bize anasoma text alietumiwa kumbe ni text kutoka kwa stela aliemtumia akiwa hapo ofisini “Acha kucheka na huyo kigagulo mi nina wivu eti. Ntakuja nimlabue hapo hapo!!!!!. Mwambie aondoke kabla sijapandisha mapepo yangu.”.Nickson aliposoma hivyo akamkatisha Angela kia akili.

Nickson : “Haya bhana usiwaze nimeipata ntashughulikia wala usiwe na shaka!”. Angela alipoona maongezi kama yamefifia akanza kuondoka na kuelekea kwenye kiti chake.

Basi siku ikaendelea huku kila mmoja akiwa bize na kazi zake lakin macho ya Stela yalikua kama radar inayomfatilia Nickson kila hatua hata akienda chooni haaachi kupashangaaa hapo mpaka atoke.Ilipofika mda wa kula Stela akamwambia Nickson kwa sms “Twende tukale” lakini Nickson aligoma kwa kusema “Wewe ni vipi huoni watu watatu shtukia kwamba tupo pamoja sana!?”. Stela nayo aliona ni point.

Angela : “Hey mtumishi twende tukale ama ndo upo kwenye mfungo!?.”.Kabla ya Nickson haja jibu alimwangalia stela akagundua stela alikuwa ana waaangalia tena kwa uso uliofura.

Itaendelea…..
 

equator

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
214
250
MY SOULMATE EPISODE 3

PRODUCED BY : EQUATORSTORY SPECIAL

Tulipoishia

Angela : “Hey mtumishi twende tukale ama ndo upo kwenye mfungo!?.”.Kabla ya Nickson haja jibu alimwangalia Stela akagundua stela alikuwa ana waaangalia tena kwa uso uliofura.

Tuendelee sasa.

Ni ndani ya ofisi ya Matumizi App Company. Angela amesimama mbele ya meza ya kazi ya Nickson akiwa amevalia style ya kipekee mabuti yaliofika karibu kidogo na magotini suruali ya jeans alio chomeka kwenye viatu vyake vya brown iliopauka ikiwa na vinakshi kidogo vya urembo wa kama manyoya meupe kwa juu. Na blauzi yake ambayo haijambana saaaana ya rangi ya njano . Angela ni mdada flani mwembamba size yani sio njiti sana lakini hivo anao ka unene flani hivi. Ana ngozi ya maji kunde . Alionekana akisimama kwa shauku akingojea jibu la Nickson.

Nickson : “Ah leo roho ameniambia anataka Kunena na mimi so sili leo ntafunga mpaka nimsikie roho.”Nickson alijibu hivyo kwa sauti ya kukwaruza ikiwa ni mithili zile za wa injilisti mashuhuri unaowajua . Kwa akili sana ili aweze kumpotezea Angela. Angela alicheka na kutoka ofisini humo na wafanyakazi wengine wawili wa humo humo ofisini.

Basi ilikuwa ndo muda wa lunch kila mmoja alitoka ofisin kwenda kula kulingana na hapetait yake na mfuko wake unavyosema. Nickson akaangalia kushoto na kulia akaona wengi wamepungua hata Stela hakuwepo maeneo hayo basi aka nyanyua begi lake na kuelekea jikoni akachukua maji akaweka ndani ya heater ya kupashia maji ili aweze kutengeneza chai. Wakati anangojea maji yachemke akawa anawaza situation yake ya kimapenzi . Akajisemea ingekua naweza kubadilisha wapenzi ninge mbadilisha Stela ili nipewe Angela maana ana nivutia sana kwa tabia zake na uzuri wake anavaaaga style flani ivi inakufanya usahau hata ulichokuwa unafanya yani ni mcheshi na tunapatana sana. Lakini Nickson akajiambia moyoni kwamba ni wengi sana wamejaribu kumtongoza Angela hapo ofisini kasoro yeye tu na hao wote walio mtongoza amewakataaa hata akiwemo Mr Sambeke pamoja na hela zake. Aliwaza kwamba kuliko ampoteze Stela alafu avunje urafiki wake na Angela awe kwenye kikundi cha waliokataliwa na Angela bora abaki na Stela wake. Basi mara baada ya maji kupata moto aka toa tambi alizopika asubuhi na kutengeneza chai akala na tambi zake akatoka mapema kwenda kukaa kwenye meza yake maana hataki watu wamu ulize maswali mengi sana. Nickson akakaa mezani kwake akiwa na earphones zake kaweka mziki kwenye simu yake akawa anasikiliza nyimbo azipendazo. Mara ghafla akatikiswa bega kuhamaki ni Boss Sambeke ndo ameingia.

Nickson : “Shkamooo boss”. Nickson alisema huku akitoa headphone masikioni haraka.

Boss : “Marahaba Nickson unafanya kazi kweli!?”. Boss wake aliuliza akiwa na mashaka maana hakuwa ofisini tokea asubuhi.

Nickson : “Ndio Boss nafanya kazi hapa nipo kwa ajili ya kazi boss.”.

Boss : “Kwani sijui hapa upo kwa ajili ya nini hujui kwamba hata kukaa bure ni kazi?” Boss aliuliza hivi kwa sauti ya hasira kidogo .

Nickson : “Ndio Boss najua lakini hapa nlikuwa nafanya kazi ulioniajiri kufanya boss.” Nickson alijibu hivyo akiwa anajua tu ndo kawaida ya boss wake ndo hivyo inabidi amzoe tu.

Boss : “Sasa yerro kuna mabadiliko ile presentation nilio waambia itafanyika kesho kutwa ita fanyika kesho saa nne kwahyo naomba uache kila kitu unafanya umalizie hiyo presentation kabla hujaenda.”

Nickson : “Lakin boss mda huatato……” Boss akamkatisha.

Boss : “Acha uzembe kila mmoja ana masaa 24 na wengine wanafanikiwa sasa wewe una shindwaje kwa mfano!?”. Boss alisema hivi huku waliokuwa lunch nje ndo wanaingia ikiwemo kina Angela na Stela na wakimsalima Boss wao.

Nickson : “Sawa boss ntahakisha kabla sijaenda ntakuwa nimeshamaliza”. Nickson alijikuta akikubali kazi ambayo ingechukua siku nzima ndani ya masaa machache ya kazi na mengine ya extra ambayo halipwi overtime lakini hana budi kwa ajili ya kuilinda ajira yake ambayo angalau inamuweka mjini.

Boss akaondoka na kunyooka moja kwa moja kwenye meza ya Stela kujua kama kuna hili na lile ama kuna walio mulizia jumbe zilizopo maaana hiyo ndo kazi ya Stela. Alipofika kwa stela alikaaa kama dakika 10 wakiongea na kucheka cheka . Nickson akaligundua na akakumbuka asubuhi alivyo textiwa na Stela kuhusu Angela naye akaaamua kutumia haki yake ya kulinda penzi lake aka mtext Stela akisema “Mnacheka nini hamumalizi tu!?”. Akamalizia na kusema “Mimi nina wivu eti.”. Vile vile alivyo andikiwa na stela asubuhi kama masaa matano yaliyo pita. Wakati bado stela anaongea na Boss alionekana kusoma ile messeji kisha akaweka simu pembeni kwa kuifunika kioo chake. Boss alipo ondoka kwenye meza yake na kuingia ofisini mwake alimjibu Nickson. “Acha utani huyu ni Boss unataka niachishwe kazi??. Tumia akili wewe mwanaume!.”.Wakati Stela ana andika hiyo Sms alionekana akisunya kabisa. Nickson akaisoma hiyo message akaona hana point ya kujitetea maana ni Boss kweli lakin aliona dalili za Stela kujigonga gonga kwa Boss wao alitamani aweze kupata ushahidi athibitishe lakini anajua lazima tu jitihada zake zigonge mwamba. Aka kumbuka ana kazi ya kuwasilisha wivu wa mapenzi usije uka mkost aka kosa namna ya kuishi mjini.

Basi Nickson aliendelea kufanya kazi huku aki pambana na muda aliendelea mpaka alipo kuja kunyanyua kichwa akaona ni saa nne usiku . Aka kumbuka hata Stela hakumuaga akahisi labda alichukia pale Angela alipo kuja kumuaga mida alipo kuwa akiondoka akajisemea nimebakisha kidogo tu ngoja nipambane nika lale alisema hapa nisipo pambana nikimuwaza Stela japo nampenda Itakua sio vyema .Lakin moyoni Nickson aliwaza na kusema hiii ndo mida Stela anayo lala labda cha kufanya ni kumuwish usiku mwema akachukua simu kwa lengo la kumuaga stela.

Nickson : “Usiku mwema mpenzi wangu. Nakupenda sana”Ali mtumia messeji ikiwa na maneno hayo Stela naye akajibu mara baada ya sekunde 30.

Stela : “Thnx”.Duh Nickson aliwaza yani huyu ni mpenzi gani jamani? . Lakin aka achana naye akacheki na sms zingine akakuta aliotumiwa na Angela “Usiku mwema jamani ufanikiwe kwenye project yako.”Angalau hayo maneno kutoka kwa rafilki yake Angela yalimfariji.

Nickson akaendelea kwenye kazi mpaka ilipo timia mida ya saa saba kasoro akai print presentation na aka copy kazi alio kuwa ana andika kwenye flash ya ofisi akasogea mpaka kwenye meza ya Stela ambaye ndiye secretary wa ofisi hiyo aka weka vitu vyote pale akazima taaa akafunga milango yote.Aka toka aka kutana na mlinzi.

Mlinzi : “Za kwanzia jana Chifu?”.Mlinzi alisema kama utani wakacheka lakini ukiangalia ni jana asubuhi Nickson aliingia kwenye ofisi hii na anatoka saa saba usiku ambayo ni siku nyingine ambapo boss wake aliondoka mapema sana.

Nickson : “Weweee kumbe siku nyingine hiiii?. Alaaaah Sasa si bora nikakae tena naweza nkatoka mwezi ujao nkasamehewa kodi yangu ya mwezi.”Basi wote wakaangua kicheko japokua kwa mbali hayo yanampa machungu Nickson.

Nickson huyo na begi lake akapanda toyo waka kubaliana 8,000 baada ya ju bagein kwa mda apunguziwe japo kidogo maaana anujua kuna kesho.

Dreva toyo : “Man vaa helment nisije kamatwa na ma trafiki”.

Nickson : “Sorry bro siwezi hapa nasikia usingizi sana nkivaa naeza sinzia nika anguka.”Dreva toyo aka cheka akidhani ni janja janja za kukwepa kuvaa helment.

Wakaaanza safari wakaenda kama 20 wakafika mahali ambapo barabara ina makorongo kwa dreva toyo alipitia karibu na pembezoni mwa barabara kuyakwepa makorongo na kufanya safari isiwe ngumu sana. Wakapita mahali kuna kama kichaka pembeni ya pikipiki inapopita mara ghafla dreva alipigwa rungu la kichwa kutokea mtu aliekuwa amejificha kwenye vichaka ilio sababisha arudishe kichwa nyuma kumgonga Nickson mdomoni . Nayo piki piki ikakosa mwelekeo wote waka hangaika huku na kule waka anguka . Dreva toyo akasema “Hapa wameanza uwizi tena!”. Akanyanyuka nduki akimbilie pikipiki wakimbie kuokoa maisha yao.

Dreva toyo :”Oya mchizi shika toyo tukimbie ”. Nickson bado alikua chini akihamaki nini kimetokea akaona hi indo nafasi yake ya kukimbia aka nyanyuka akimbilie toyo hapo dreva tayari amesha anza kwenda mwendo mdogo kibishi bishi akisubiri Nickson adandie mara nickson akasikia kuna sauti za watu nyuma yake wana mkimbilia.

Itaendelea…
 

equator

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
214
250
My SoulMate Episode 4
Produced By: EquatorStory Specials
Tulipoishia Nickson alionekana kuwa katika majanga ya uvamizi wa majambazi kwenye mida ya saa nane usiku.
Dreva toyo : “Oya kamata twende wewe”. Japokuwa dreva toyo alikuwa ameumia aliona sio mda sahihi wa kujivuta ni muda wa kukimbilia maisha yake.
Nickson : “Mmmmmh”. Alishindwa kutoa hata neno moja kwa sababu ya maumivu aliokuwa akiugulia akawa ana chechemea kuifikia hiyo pikipiki ambayo ilikuwa kwenye mwendo.
Mara ghafla alisikia kuna watu kama watatu wanakimbia nyuma yake alisikia sauti ya wawili wa hao watu walipita mbele yake wakiiifata pikipiki dreva toyo alivyo ona hivyo aliongeza mwendo akakoswa tena na. Dreva akaponea chupuchupu akakimbia akiwa amemuacha Nickson chini.
Nickson akawa amezingirwa na watu wanne wawili mbele wawili nyuma mmoja alimulika tochi kali sana mmoja kwa mmoja kwenye macho ya Nickson yaliomsabibishia kutokuona mbele. Nickson akajisemea moyoni ama zangu ama zao hapa natoka kiume.
Nickson : “Niacheni!..”. Alisema kwa sauti iliokuwa ikitetemeka na hasira .
Jambazi1 : “Hahahahahah wewe jamaaa unasikitisha.”Alisema jambazi aliekuwa mbele ya Nickson.
Nickson : “Nini wewe mnakuja wan ne mna fikiri siwawezi?”. Nickson alikusanya nguvu na kutoa sauti hiyo akiwa bado katika machungu.
Jambazi1: “Una dhani unaeza jitetea? Ivi unajipenda kweli we tupe vyetu na hatutakupiga saaana!”. Jambazi wa kwanza alisema kwa sauti ya kibabe kidogo.
Nickson : “Hapana alie mwanaume aje achukue nitavunja mtu meno mimi.”. Jambazi wa pili aka mpa tochi yule wa kwanza akamwambia usisogeee.
Mara paaah nickson alirusha ngumi ya ghafla na ya kasi sana kumuelekea jambazi huyo aka fanikiwa kumpiga ya pua. Jambazi wa pili akarusha ngumi yake kumuelekea nickson usoni nickson akainama kwa mgongo kidogo kukwepa ngumi akajipinda kuelekea kushoto aka mpiga tena ngumi ya mbavuni jambazi huyo aka guna kwa maumivu “uuuuuungh”.
Majambazi wawili waliopo nyuma yake wakamshika mikono kwa nguvu nickson asiweze kufurukuta huku majambazi wa kwanza na wa pili waka mshambulia kwa pamoja lakini Nickson haku anguka alisimama wima jambazi wa kwanza akamsachi Nickson akatoa simu yake ya smartphone yake akasema.
Jambazi1 : “kwa sababu umejitetea tuna kuachia line kwa leo”. Alisema huku akitoa line zote na kumrudishia mfukoni wakati wote huo bado Nickson anamulikwa na tochi usoni. Jambazi wa tatu aliepo upande wa kulia wa Nickson alipenyeza mkono akatoa wallet yake akamrushia wa kwanza.
Jambazi1: “Aisee kidogo nisahau kuchukua nauli. Hahahahaha” alisema hivyo huku akifungua wallet iliokuwa na akiba ya Nickson takribani laki moja na elfu tisini akaibeba yote na kurudisha wallet ya nickson.
Mara wakaona kuna gari ambalo linakuja kutokea upande ambao dreva toyo alikimbilia.
Jambazi3 : “Babaaaa ako iyo ni Pt man.” Alisema hivyo akiendelea ku hamaki gari iliokuja kwa mwendo kana kwamba hamna makorongo maeneo hayo.
Wakati bado wanaitazama ile gari iligeuka nyuzi 180 inayojulikana maarufu kama u-turn ama kupiga chapati kwa lugha tuliozoea mitaaaani ikianza kutazamia kule ilipotoka mara wakaona kuna mtu ameruka na ana kuja kwa mwendo wa kasi nao wakaanza kukimbia .
Afande Maria : “Simameni nyie ma mbwa ni waoneshe”. Alisema Yule mwanamke alieruka kwenye gari kama hamnaga kufa .Nickson alibaki anashangaaa alisahau ata alikua anavamiwa na hao majambazi.
Afande Maria : “Simameni nyie ma kima niwaoneshe nani mkali hapa mbona mnakimbia!? ”.Alisema afande maria akijaribu kuwakamata lakini watu hao walikua wamesha shika kasi kukimbilia mtoni.
Afande Maria akarudi na kumfuata Nickson alie kuwa kajilaza baada ya kuchoka kusimama . Afande Maria alimshika kwa shati na kumnyanyua na mkono mmoja.
Afande Maria : “We nani na ulikuwa unafanyaje na hao watu!?”Afande aliuliza kwa ukali lakin pia alitaka Nickson ajitambulishe kwa sababu kuna mawili aiza nickson ni mmoja wapo wa ma jambazi au alikua ni muathirika wa hao majambazi.
Nickson : “Nai naitwa Nickson na hao ni majambazi waliotuvamia kwenye pikipiki”. Alijielezea kwa kukugumia.
Afande Maria : “Anhaaa tulipata taarifa zako kwa Yule dreva toyo aliekuja mpaka kituoni aliekuwa ame umia sana jamani hapa tutawadaka tu hawa watu”.Wakati akisema hivyo aliekuwa akiendesha ile gari alishuka akawa anawakaribia akamsaida Nickson kukusanya vitu vyake na wakamsaidia mpaka kwenye gari lao.
Wakampeleka Nickson mpaka kituon wakamjazia fomu ya “Pf3” ambayo itamsaidia kujielezea atakapofika hospitali. Naye Nickson aliomba kupelekwa kwenye hospitali ya Mtume Danny ambayo ipo karibu na kwake alipo panga.
Nickson alipokelewa kupelekwa na kuoshwa madonda alio kuwa nayo kwa hisani ya Afande Maria ambae muda wote alikua akimuonea Nickson huruma sana kwa kuwa yeye pia ana mtoto wa miaka miwili anajua ulimwengu ulivyo mbaya.
Nickson : “Niko wapi!?” . Alijiuliza baada ya kuamka kesho yake mida ya saa tano asubuhi akakukumbuka yote yaliyo mtukia alitoka hapo akiwa na bandeji aliofungwa kichwan baada ya kupata majeraha kadha ya kichwa kwa kuanguka . Nickson alikuwa amevimba uso kwa ngumi alizopokea bila huruma.
Docta Danny : “Unaendeleaje ndugu!?”. Aliuliza huku ajirabu kumchunguza Nickson pale alipoumia .
Nickson : “Nasikia maumivu karibu kila mahali ”. Nickson alisema hivyo akielekea chooni .
Docta Danny: “Sawa pole sana mungu ni mwema hauna majeraha makubwa Mungu ni mkubwa.”.
Nickson : “Aaah asante Docta”. Nikson aliendelea kujongelea mbele. Docta akamsimamisha.
Docta : “Eeem Nickson ngojea kidogo. Nenda chooni ukajisaidie alafu ingia ukaoge kabisa ntamwita nurse akuletee chai ndani ya dakika 30 Afande alie kuleta jana amesema atakuja akupitie uende ukatoe report ya kilicho kutokea ili waanze na upelelezi wa kilichokutokea.”. Docta alivyo sema hivyo alianza kuondoka kuwa tazama wagonjwa wengine.
Nickson : “Asante sana Docta. ”
Basi Nickson akaenda kujisaidia japo mwili mzima unampa taabu sana . Akaingia kuoga na baada yam da kidogo akawasha tv iliopo chumba hicho mara ghafa akaisikia saut ya kipole ya mdada.
Nurse : “Kaka unandeleaje!?. Nimekuletea supu karibu ”.
Nickson: “Asante sana naendelea vizuri .”Nickson akanywa supu alioletewa ikampa mwili wake nguvu kidogo.Mara ndani ya mda mchache akaingia Afande Maria.
Afande Maria : “Kaka unaendeleaje!?.”Nickson alibaki kushangaa uzuri wa huyu afande aliengia ndani . Akamtamani kiasi akatamani sana asiwe na Stela maana huyu uzuri wa mwili wake umemzidi stela wake kwanza stela mwenyewe alivyopasua kichwa.. .
Nickson : “Mhhhh Naaam”. Nickson alikuwa anaguna maana mawazo mengi yalikua yanapita mengi sana kichwani mwake .
Afande Maria : “Unaendeleaje kaka!?”. Aliuliza akipaza sauti kidogo maana ya kwanza nickson hakusikia sijuiii.
Nickson : “Salama sana dada habari za asubuhi!?”. Nickson aliuliza kwa tabasamu.
Nickson akasalimiana na Afande Maria pale akamwambia kweli haku amini kama ndo Yule ali ruka kwenye gari kama alikua anarukia mto yani kama hamna kuumiaga vile. Ali mpongeza sana Askari huyo wa kike aliekuwa na ushujaaa.
Nickson wakaongozana mpaka reception pamoja naye Afande Maria walipofika hapo Afande Maria alitoa pesa ya mauguzi na hospitali walimshukuru sana uyu mmama kwa wema anaoufanya kwa watu.
Afande Maria alichukua Statement ya Nickson kwa ajili ya uchunguzi . Nickson naye akatafuta usafiri mpaka alipo kuwa ana ishi.
Alipo fika na majereha kila mmoja alianza kumpa pole.
Watoto : “Uncle Nickson Poleeee.” Watoto walipokezana kumpa pole Kaka yao ambaye ni dhahiri alionekana ameumia.
Mama Grace ndo mwenye nyumba ya pale anapoishi Nickson na wapangaji wenzake alijitokeza pia kumpa pole kijana aliekuwa mkarimu hana makuu.
Mama Grace : “Kirrrru jamani pole mwanangu ni nini shida!?”. Mama grace alisema kwa uchungu akitaka kujua nini kimemsibu Nickson.
Nickson : “Mama majambazi jamani kidogo wanitoe roho.”
Nickson na Mama Grace aliwaelezea kinaga ubaga kila mmoja alionekana kukunja sura akisimuliwa . Wakampa pole majirani zake wengine wakawa wanamletea chakula na kumsaidia michango ya chochote alicho nacho 5,000 10,000 hata 2,000 walitoa kuonesha wapo pamoja naye.
Basi ilitimia week nzima Nickson hajaenda kazini lakini afya yake ina anza kuendelea vizuri. Ndipo alipoamua kurudi ofisin maana ni week hajaonana na stela wala hata hajui nini kitamsibu.
Nickson : ………….
Aaaaaaah wewe itaendelea!.........
 

sonnita

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
1,616
2,000
Mmmh ina maana ofisini hawana taarifa kua alivamiwa?
Au ndo Stella kaamua kua bandidu.
 

equator

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
214
250
My Soulmate EPISODE 5
Produced By : Equatorstory Specials
Ilikua ni siku nyingine ofisini kwa kina Nickson ni siku ambayo hakuonekana na ilikua ni siku ya muhimu sana kwa sababu alipaswa afanye presentation ya kuweza kuwa kamata wateja wapya ambao watakua ni sehemu ya muhimu ya kampuni yao.
Stela : “Boss Nickson hapatikani na sio kawaida yake huwa hachelewi.”.Stela alisema hivyo huku akiwa amevuta mdomo kidogo na akilini mwake akiwa na wasiwasi wa mpenzi wake wa ki siri siri.
Angela : “Mh labda alilala sana maana jana nlimwacha huku ofisini.” Angela alidakia . Stela akamwangalia kwanzia juu mpaka chini na mdomo ndo ukazidi kuvutwa. Wakati huo Angela akiongea akiwa ana mtazama Boss wao kwa hiyo hakuona akiwa ana katwa jicho na stela.
Boss : “Sawa sasa nani atafanya hiyo presentation na yeye ndio tunamtegemea yani hiii kijana hayupo serious na maisha kabisa.”. Boss alisema akamalizia na kurusha mikono aka egemea kiti chake cha blue na aka zunguka akiwaza.
Boss : “Sawa nendeni presentation inatakiwa kufanywa saa sita mchana labda atakua amekuja na atatueleza alikuwa wapi wakati wote huo.” Boss akamwita Angela wakati wanatoka.
Boss : “Angela..”
Angela : “Abee”. Angela na Stela walisimama ili kumsikiliza Boss wao.
Boss : “Si mlishirikiana na Nickson kuandaa hiyo presentation!?”.
Angela : “Ndio Boss lakini mimi nilifanya kama robo tu Boss!.”
Boss : “Enheee safi sasa nakupa chalenj Angela ..”.
Angela : “Ndio Boss nakusiliza .”Kipindi hicho stela alikua amemtangulia Stela kama hatua kadhaa alimwangalia vibaaaya Angela kwanzia chini mdomo nao upo kama amelamba aloevera bahati mbaya.
Boss : “Najua Angela bhana we mwanamke mwenye akili ndo maaaana nikakuchukua uje unifanyie kazi.”.Boss alianza kumpamba Angela kabla Hajasema haja yake iliopo akilini mwake.
Angela : “Nashukuru Boss kwa kutambua hilo.”Stela bado yupo Nyuma yake ana badilisha tu mapozi ya kumwangalia Angela vibaya.
Boss : “Nakuambia ukiweza hii we mdada nakupandisha cheo.”Angela ni mwanamke shupavu na mwenye akili ya juu sana kwayo alijua kitu ambacho Boss wake anataka kusema. Nadhani msomaji unaeza imagine stela alivyo fura.
Angela : “Sawa nakusikiliza.”
Boss : “Hiyo Presentation yote amesha iandaa Nickson so wewe ichukue uisome halafu ikitokea Nickson hajaja basi wewe utaifanya basi ukiweza kufanya vizuri utakuwa mkuu wake Nickson.”
Angela : “Sawa Boss ntafanya hivyo”.
Stela aliondoka kwa hasira mpaka kwenye meza yake ambapo Nickson aliacha Presentation yenyewe.
Angela : “Stela Dear naomba basi hiyo presentation.” Angela alikua tayari kwenda kuanza na bahati nzuri au mbaya alikuwa anafahamu so nikusoma tu.
Stela : “Mxxxxxheeewwwwwwwww….” Alimkabidhi na kusonya kwa sauti na madharau na akageuzia shingo upande mwingine. Angela hakuelewa kwa nini stela alifanya hivyo lakini ana misheni kubwa zaidi ambayo ina faida zaidi na Angela sio kama wadada wengine yeye alichukua presentation na kuelekea ofisini.
Muda ukaendelea kuyoyoma na huku akiendelea kumpigia mpenzi wake bila mafanikio bila kujua yaliyomkuta ambapo kidogo apoteze roho yake. Stela alikua na mawazo mawili kama sio nickson ame acha kazi basi alilala na Angela ili Angela apate hii nafasi ya kupandishwa cheo. Stela hakai ofisin kwake kwa kutulia mara ana shika hiki hakiendi mara apige simu hampati mpenziwe. Anatamani hata aende kwa Nickson lakini shida ni hapajui .
Muda uliendelea na Angela aliendelea kujianda kukariri point kama amepata mtihani wa ghafla alionekana akienda kushoto na kulia akiongea maneno akiwa mwenyewe. Kila Stela akiangalia ofisini mwa Stela ambayo ni ya kiooo ana sonya tu anatamani apusuke au hata akamwakie Angela kwamba atakua anayo njama na bwana wake wa siri lakini hana ushahidi inabidi anyamaze tu.
Muda uliwadia na wateja waliokuwa wakingojewa kwa ajili ya presentation walifika pale. Boss na Angela waliingia kufanya Presentation hiyo. Walienda masaa na ma dakika muda huo mbele ya Stela ilikuwa kama siku 4 labda alitamani watoke humo ndani na ajue kwamba Angela amefeli ali tamani utokee muujiza Nickson atokee paaap na aende aka ifanye presentation hiyo kuliko Angela afanye hivyo.
Stela : “Eeeh mungu ntalia na nani mie”. Stela alijisemea moyoni machozi yakimlenga mlenga machoni.
Mara ukawadia muda wateja waliokuwa kwenye presentation walianza kuongozana kutoka wakiwa na tabasamu na wakishikana mikono na Boss Sambeke.
Wateja : “Haya Dada kwa heri jamani!.”Wateja walisema hivyo wakielekea mlangoni kuondoka kwa sababu kikao kimekwisha.
Lakini Angela alionekana amebaki ameketi huku machozi yakimtoka taratibu machoni.
Boss : “Aiseee huyu mdada yupo smart sana”.Alikuwa amesema hivyo huku ame egemea meza ya stela.
Stela : “Kwa nini!?”.
Boss : “Mbona kama unataka kulia!?.” Boss aligundua macho ya stela yalikuwa sio kawaida.
Stela : “Ahh Boss nimepatwa na maumivu ya jino kwanzia asubuhi nimejikaza lakin duh nimeshindwa sasa.”Stela alidanganya kuhusu sababu ya huzuni yake.
Boss : “Aise jino ni mbaya sana mi enyewe lina nisumbuaga shyeee staki hata kukumbuka yeeuwi.”. Boss naye alionesha kujali na kuelewa maumivu ya uongo asemayo Stela. “Pole sana jamani kwa nini hukusema!?”.
Stela : “Boss mama yangu aliniambiaga mwanamke haumwagi hata akiumwa nani ataye walea watoto?”.
Boss : “Mambo ya zamani hayo!. Pole sana binti utapona.”
Stela : “Asante Boss. So ulikuwa unasema nini kuhusu Angela!?.”
Boss : “Prezenteshen amefanya very smart sijui huyu Nickson hayupo serious na maisha. Huyu binti yuko very smart..”
Stela : “Ah hongera zake.” Machozi yakazidi kujaa machoni kwa stela.
Boss : “Yani nimempandishia mshahara na nimemfanya awe Boss wa nickson kwayo huyu ni Chief wa IT katika kampuni hiiii.”
Stela : “Dah boss hapo una mfanya kazi mzuri.”
Boss : “Ndio hivyo. Wewe naomba uende nyumbani ukatibu jino bhana jino sio mchezo.”
Hivyo ndivyo ilivyopita siku hiyo wakati huo hakuna mtu anayejua Nickson yuko wapi.
Itaendelea..
 

equator

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
214
250
My SoulMate Episode 6.
Produced by: EquatorStory Special
Nickson alikaa akawaza na kutathmini maisha yake hapo alipofika alitumia muda huu kama nafasi ya kuyawaza maisha yake maswali chungu nzima yakiwa yanapita kuhusu maisha yake akiwaza aendelee ku fanya kazi pale? Aendelee na Stela ambaye kwenye matukio kama haya hayupo ana umuhimu gani?. Alikaaa chini akaanza kuwaza na kuwazua lakin yote alioamua aliya weka moyoni. Moyo wa mtu ndo una siri nzito.
Ilikuwa ni mida ya saa saba mchana ofisini kwa kina Nickson amerejea akiwa na bahasha mkononi hakuna ajuae amebeba nini humo ndani yamkini ni barua ya kuacha kazi ama!?
Mlinzi : “Mwana mpotevu ulienda mpaka wapi jamaa yangu ile usiku ulipata na dhahabu nini!?”.
Nickson : “Ah mama alinichapa akanikataza nisirudie tena kurudi huku.” Wote walicheka kama wanamuangalia Mr Bean.
Mlinzi : “Mama yako dada yake Tyson ama sio kwa hayo ma alama usoni na kuchechemea huko.”Mlinzi aliuliza huku akijichekesha kidogo . “Teh teh ".
Nickson : “Aisse pale Mianzini bhana si nilivamiwa na ma jambazi.”Nickson saivi alisema akiwa serious mlinzi akajua hapa hataniii.
Mlinzi : “Weweeee.” Mlinzi kwa mshangao akiwa na rungu lake mkononi.
Nickson : “Wachaaaa ni ugonjwa man!.”.
Nickson alipiga story mbili tatu aka mpa hadithi kwa juu kidogo lakini mlinzi alimuelewa. Nickson akasonga ndani kuingia ofisini kwao.
Angela : “Wow jamani umefufuka.”Angela aliongea hivyo akimkumbatia Nickson kwa furaha .
Nickson : “Neno linasema hatuta ishi kwa mkate tu!.”Nickson na Angela walicheka lakini nickson wakati ana angalia kushoto na kulia alimuona stela akimcheki tu .
Angela : “Naona bhana ulifanikiwa kuongea na roho wa bwana maana ile siku ulisema unataka kuongea na roho ndo maaana haukuenda lunch”.
“Mhhh Angela anakumbuka ile lunch mpaka leo!?” Nickson alijiuliza lakin akawacha kuwaza pale alipokumbuka huyu mdada ni smart anajua uwezo wake. “Au labda kuna mengine….? Mh amna nisijisumbue tu bure.”
Angela : “Enhe kilichokusibu wewe mkaka!?”. Angela alisema huku akimpiga ka kofi kwenye kifua Nickson.
Stela aliona hapa naibiwa nikiwa nimesimama. Stela huyo naye kaja kumlaki Nickson.
Stela : “Nickson Jomoni…….. Ulikuwa wap jomoni ”. Alisema kwa madoido akiwa anavuta mdomo kidogo kwa maringo yani namna flani hivi ya madeko.
Nickson : “Mambo jamani za kupotezana Stela!?”. Nickson alijikaza ajizuie asioneshe ku bugudhiwa na hiyo ‘salamu’ ya stela.
Stela : “Enhee twambie”.
Nickson : “Huezi amini ile siku nilivyo toka hapa nilivamiwa na majambazi njiani.”
Stela & Angela : “UNASEMAAAA!?.” Walijibu kwa sauti ya juu wote kama waliambizana.
Stela : “Yesuuu ndo maaana una ngeu ngeu usoni”.
Angela : “Sasa wewe inakuaje ulikuwa usiku mwenyewe.”
Nickson akaanza kuwa hadithia mkasa mzima kwanzia mwanzo hadi mwisho wote walionekana kusikitika nao walijibu kwa uchungu wakiona kama inawatokea wao vile.
Mara tu walipo maliza kusimuliwa nae Nickson kuhusu kila kitu mara ghafla Boss Sambeke akaingia Ofisini.
Stela & Angela : “Shkamooo Boss.”. Walisema huku kila mmoja akitafuta njia ya kwenda kwenye meza zao kabla boss wao haja anza kuwasha moto.
Boss : “Marahaba warembo aisee ni wazima!?.”.Boss alisema kwa tabasamu akiwaangalia wanavyo ondoka. Sijui alikuwa ana angalia nini.
Nickson : “Shkamo bos…”. Boss aka mnyoshea mkono kumkatisha.
Boss : “Hivi Nickson una miaka mingapi!?. ”Boss aliuliza akiwa na mshangao kiasi flani huku akichezea funguo alizonazo mkononi.
Nickson : “Boss nina miaka 27 nina elekea 28.”Nickson alijibu kwa heshima zote huku akijiuliza Boss ana maanisha nini.
Boss : “Sasaa… yerro unajuwa wewe ni mtu mzima lakini pia ni kijana mdogo bado.”
Nickson : “Ndio Boss najua.”
Boss : “Sasa yerroo inakuaje haupo serious na maisha!?”. Boss alianza kukunja ndita kiasi flani akiendelea kuzungusha funguo zake.
Nickson : “Boss nili ……”Nickson aliovyo anza kujieleza ali simamishwa tena akashusha pumzi kana kwamba alipoteza matumaini flani hivi.
Boss wake aka nyoosha mkono kuelekea ofisini kwake akionesha wakaendelee na maongezi hayo ofisin na Boss alitangulia Nickson kabla hajaanza kwenda kwa Boss wake alimfuata stela alipo aka fungua bahasha yake ya rangi ya kaki akatoa bahasha nyingine ndogo akampa Stela .Akamfuata boss wake kuendelea na maongezi yao.
Boss : “Sasa mbona bado umesimama!?” Aliuliza huku akimwonesha akae kwenye mmoja wapo ya viti vilivyopo.
Nickson : “Boss ile siku niltoka hapa saa saba usiku.”.
Boss : “Enheee .” Boss alisema akijitikisa kwenye kiti chake akae vizuri .
Nickson : “Wakati naelekea nikavamiwa na majambazi nikiwa kwenye pikipiki.”
Boss : “Hahahahahahaa ahahaha we dogo bhana hahahaahahaha”. Boss alicheka kwa nguvu na ghafla akionesha kutokuamini .
Nickson : “Boss mimi sitanii..”. Akafungua ile bahasha yake na akaeka nyaraka kadhaa kwenye meza ya bosi wake.
Boss : “Ndo ninI hii!?”.
Nickson : “Ni copy ya ‘pf3’ na copy ya vitu kadhaa vinavyo dhibitisha yote nlio sema.”
Boss : “Ngoja nione kijanaa. ” Boss akaanza kukagua hizo document.
Boss : “Dogo sio kwamba ulifumaniwa na mke wa mtu!?.”
Nickson : “Heheh hapana Boss”. Nickson alijichekesha kwa akijua boss wake anatania.
Boss : “Aisee dogo pole sana kwa yalio kukuta” . Boss alisema kwa mbali akijuta kwa nini alicheka mara ya kwanza lakini yaliotendeka yalisha tendeka.
Nickson : “Asante Boss.”
Boss : “Sasa cha kufanya andika email ambatanisha na hizi document ili iende kwenye record za wa fanyakazi . Na pia email yako uitume kwa Angela.”Nickson alianza kushangaa Angela tena!?
Nickson : “Boss ulisema Angela!? .” Aliuliza kuhakikisha hajasikia vibaya Boss wake aliosema.
Boss : “Ndio Angela saivi Angela ni Mkuu wa kitengo wa IT . Ile presentation aliifanya vizuri sanaa.”
Nickson : “Ahaaaa Sawa Boss.”Nickson alijuiliza akilini inakuwaje kapandishwa cheo wakati mimi nimefanya presentation kama mia hapa hapa!?. Huyu Boss hajui kujipangilia au kila mtu na ngekewa yake.
Boss : “Aya yerro pole sana kwa majeraha fanya hivyo pia uendelee na kazi.”Nickson alianza kuinuka na kuelekea mlangoni.Akasimama karibu na mlangoni akamgeukia Boss wake na kusema.. .
Nickson : “Boss lakini nina shida nyingine .”
Boss: “Niambie yerroo.”
Nickson : “Wakati navamiwa nilopeteza hela zote nlizonazo pia nlipoteza na simu yangu.”
Boss : “Kwa nini unatembea na hela ndefu hivyo!?”.
Nickson : “Nlipo pokea ile siku nilitarajia kuwahi niende nikaziweke benk lakini ndo ikawa hivyo.”
Boss : “Eeenh kweli uwizi unarudisha maendeleo nyuma.”
Nickson : “Kweli Boss.”Boss alikaa akiwazaaaaa halafu akamjibu
Boss : “Sawa andika hiyo email na uende kwa Stela atakupatia cheki ya nusu ya mshahara kama advance ya mwezi huu wako alafu uilete niisaini uende uka nunue simu kwa sababu ni muhimu sana kuwa na mawasiliano.”
Nickson : “Sawa asante sana boss.”
Nickson akatoka kuelekea meza ya stela na kumpasha alichoambiwa kuhusiana na cheki ya advance ya mshahara wake. Alipo maliza kumpa hayo maelezo akawa anaelekea kwenye meza yake.
Stela : “Psssst Nickson njoo.”
Nickson : “Niambie mwaya.”
Stela : “Ntamdanganya Boss naenda hospitali kwa ajili ya dactari wa meno ili tutoke wote.”
Nickson : “Sawa wala usiwe na wasiwasi.”
Nickson alienda kwa Angela akampa pongezi ya kupata cheo kipya.
Nickson : “Hongera Angela Jamani au niseme Mtumishi Angela Bwana amekuona Haleluyaaa.”
Angela : “Hahaha yani wewe huishiwagi na vituko vyako. Nta waambia ma jamaa waku ongezee we bado hujakoma.” Wakacheka kidogo.
Mara Stela kaingia ghafla kama kaitiwa nyama.
Stela : “Nickson umempongeza Angela kapandishwa cheo sasa.” Stela aliuliza kama sio aliomsunya Angela siku ile ya presentation.
Kipindi hiki stela ni rafiki yake sana na Angela mpaka imefikia mahali wana ambiana siri NZITO lakini kuhusu mahusiano yao stela na Nickson haja thubutu kuambizana bado hajaya taja. Hakuna ajuae kuhusiana na stela alichopanga kwenye kichwa chake yamkini ana mpango au ndio alivyo.
Nickson : “Ndio nimemwambia naona asha anza kuvaa viatu virefu wakat sio kawaida yake amevaa ki boss yani unaeza uka data.”
Stela : “Heheh yani we acha tu”. Lakini Stela hiyo imemuumiza kusikia mwananume wake ana zungumzia vizuri angela.
Nickson : “Jamani ngoja nika andike hiyo email mara moja nika fatilie simu ili kesho nije nikiwa free.”
Nickson aliondoka aka kaaa kwenye kiti chake aka andika aliyo kua akifanya kazi hapo awali. Akamaliza kua andika akamtumia boss wake pamoja na boss wake mpya wa kitengo cha IT.
Nao wakati huohuo Stela akaenda kuaga kwamba anaenda kwa boss kuwa anaenda kwa dactari wa meno Nickson aka patiwa Cheki yake.Wakaondoka wote mpaka bank kwa ajili ya kutoa hela zilizopo kwenye cheki hiyo.
Stela : “Baaby unajua nina shida ya elfu 30 ya kwenda kusuka .” Stela alisema kwa madeko na kabla Nickson hajamjibu stela akaongezea.
Stela : “Baby leo si una hela utanipeleka tukale kuku na niende nkapake rangi kucha baby wangu nipendeze.”Nickson hakuamini anacho sikia.
Nickson : “We stela acha zako una shida gani we mwanamke!?.”
Stela : “Baby please…...” Aliongeza kulegeza macho.
Nicskon : “Jamani baby hii ni hela ya mwezi ujao unataka niiishije!?.”
Stela : “Sasa wewe unapotea week nzima alafu unaniletea card mimi!?.”Stela alianza kuonesha kuchukia.
Nickson : “We niaje bhana kwani sijakwambia kwamba nili vamiwa na majambazi kwani!?”.
Stela : “Sawa lakini….”
Nickson : “Lakini nini!?”.
Stela : “Card yenyewe imeandikwa ”. Stela aka bana pua “I MISS YOU”.
Nickson ali juta kumletea mpenzi wake ile card amabayo alimpatia kule ofisini.
Nickson : “Naomba usinizoe.”Nickson alisema huku sauti yake ikionesha kukasirika.
Stela : “Sasa Baby si wewe mwenyewe ulikuwa unanisumbua na kuniambia unanipenda sasa usipo ni tunza ntajuaje unanipenda.”
Nickson : “lakiniii”. Nickson alitamani hata kulia.
Stela : “Baaaaaby jamani..”
Nicskon : “Sikia nikuambie kitu week ijayo ntakupa ya kusuka kuna hela nafuatilia. Leo twende pale New restaurant nkaku fanyie mpango wa chipsi kuku. ”
Stela : “Na mshikaki…. Baby na juice.”
Nickson : “We kuku na mshikaki acha tamaaa wewe!....”
Stela : “Mhhh haya.”
Hao wakaongozana kula na maisha yakaendelea.
Itaendelea……..
 

equator

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
214
250
My Soulmate kipande cha 7
Produced by: EquatorStory Special
Mpendwa msomaji leo nataka nikuoneshe sehemu nyingine ya hadithi hii ya Soulmate.
Ni mida ya saa kumi na mbili tuna mwona Mwanamke mzuri aitwae Betha akiwa yupo jikon anapika huku akipiga hadithi na rafiki yake kipenzi Hamida.
Hamida : “Yani nakwambia shoga…”.Hamida aliongea kwa mwendo wa kutaka kuanzisha umbea .
Bertha : “Niambie shoo ”. Bertha aliendelea na shughuli za kupika anavyo weza.
Hamida : “Si nimemkubalia Nelson bhana”. Bertha kusikia hivyi aligeuza kichwa kumsikiliza vizuri rafiki yake alekuwa amemgeuzia mgongo akiwa bize.
Bertha : “Nelsoon!? Yule aliekuwa..”Hamida hakutaka hata bertha amalizie.
Hamida : “Eeeh Yule ambae alikua akinifukuzia na nilikua simtaki hata mtu mwenyewe hana hela ananitaka anipeleke wapi!?”
Bertha : “Eeh umempenda kisa umesikia amepata ka gari ka kuendesha!?.”
Hamida : “Kuhusu gari mmmh sio saanaa.”.
Bertha : “Bali nini sasa au amekuwa handsome ghafla alipo badili nguo anazovaa kama mchungaji na kuanza kuvaa vi modo kama wengine.”
Hamida : “Heheeheh usinichekeshe shoooo” Hamida alitamani kumpa mwenzie tano sema ndo hivyo yupo bize aka nyanyua mkono akapiga kofi kwa kupishanisha mikono kama anajikung`uta vumbi.
Bertha : “Sasa bali imekuaje!?”.
Hamida : “Mwenzangu nlivio enda chuo kule sumbawanga nimerudi James wangu hanitaki tena anaongea maneno mengi anasema sijui ntamwendesha kisa ety nina ka bachela changu ambacho chenyewe nimepata kwa mkopo tu shooo. Jamani mie moyo una niuma… ”.
Bertha : “Sasa umemkubali Nelson ili umtese James ama!?”.
Hamida : “He enhee na wewe si usubiri nikupe cake yote sasa..”.
Berha : “Haya niambie sasa.”
Hamida : “Jamani nimembeleza James wangu nimemwambia tuta fanikiwa kwa pamoja mimi ni yule yule Hamida wake ambae nilienda kusoma na nimerudi.”
Bertha : “Enhee….”
Hamida : “Kumbe bhana mapenzi yameingia mchawi bhana..”.
Bertha : “Mchawi gani!?”.
Hamida : “Nelson si tulikua tunasoma nae kule Sumbawanga bhana akanitongoza sana akijua mimi nina mpenzi wangu James. Nikamkatalia lakini bado kaningania naona alienda kumjaza sumu James wangu jamani.”
Bertha : “Wewe..”
Hamida : “James kila anasema ooh Nelson aliona mimi chuo nilikuwa na watu wakati jamani kwa jina la mungu sina mwingine.”
Bertha : “Weweee.”Cake (Umbea) alio kuwa anapewa bertha ulikuwa unampa shida maaana kila saa anamwangalia bertha mara ageukie chakula.
Hamida : “Sasa uyu Nelson kwa jina la Mungu atanikoma nitakavyo mtesa na kula hivyo vi hela vyake anavyopata kwenye hako ka ofisi.”
Bertha : “Mhhh wewe kwayo ndo unalipiza.”
Hamida : “Bertha unanijua unanisikia shooo!? Yani nakuambia kama Nelson ningekuwa mchepuko wake ninge mtesa mpaka angetamani kuomba ushari kwa mke wake.”Wote wakacheka.
Bertha : “Jamani Hamida sio vizuri kumfanyia hivyo bora umwambie humtaki ubaki na mpenzi wako. ”
Hamida : “Weeeeeeh mama mtenda hutendwa alivyo ni gombanisha na James wangu alitegemea kupata nini kwa mfano. Bertha nakuhakikishia nita fanya visa huyu mkaka hajawai kuona wala kusimulia ntamfanya alale kwenye maji agaregare kama Kambale.”
Bertha : “Mama we fanya uwezalo huyo ana stahili yanayo muijia. Maaana sio vizuri lakini angalia na wewe usije ishia kwenye mapenzi na wewe ujikute umenaswa upitie machungu.”
Hamida : “Aaaah wapi Mimi nampenda James wangu milele mpaka Nife unajua huyu ndo Mpenzi wangu wa kwanza!?.”
Bertha : “Haya sawa mama.”Mara Simu ya Hamida ikaita .Ni Nelson alikua anampigia.
Hamida : “Kima mwenyewe ndo huyo ana piga ana ni fatilia fatilia kama mbuzi mxxxxxxxhewww”.
Bertha : “Heheh”.Hamida akapokea simu.
Hamida : “Hello laazizi.”Hamida alipokea kwa madeko kama sio nelson aliekuwa akimtukana.
Nelson : “Niambie uaridi la moyo wangu bado upo kwa shoga yako!?”.
Hamida : “Ndio mpenzi mekumish.” Mara Sautu ya hamida ilianza kuwa kama ya kitoto vile.
Nelson : “Toka bhas nje nimefika nimekuja kukuchukua tukale pizza si unakumbuka ratiba yetu inasema tukutane leo tupate mda wetu wawili tuka zungumze . Nipate mda na mpenzi wanguuu.”
Hamida : “Haya honey nakuja. I LOVE YOU mwaaah”.Hamida alikata simu aka muaga rafiki yake Bertha na akaenda nje kumfuata mpenzi wake aliekuwa kwenye gari la Toyota Mark II.
Wakati huo Bertha alikua ana angalia dirishani akiwa na maswali juu ya mipango ya Hamida na Nelson wake. Lakini kabla mlinzi haja funga mlango aliona gari jeusi aina ya Range-Rover imengaa kama kiatu kipya cha mtoto shuleni. Bertha alilitambua gari hilo ni la mume wake leo alitoka na Range Rover. Bertha alijifuta mikono akaenda nje kumpokea mume wake ambae ni Mr Mandoto.
Bertha : “Karibu nyumbani mume wangu Pole na kazi.”Bertha alisema huku aki piga ka goti kwa mbali.
Mr Mandoto : “Mumeshindaje humu ndani!?”. Alisema huku akiingia ndani akawa kama hajaona mke wake alivyo jaribu kumkumbatia.
Bertha : “Salama tu mume wangu. Nikuandalie chakula mume wangu!?”.Aliuliza akimwangalia mumewe akiwa anapita kuelekea mlango.
Mr Mandoto : “Hapana nina kikao kazini jioni ya leo naenda tu kuoga na naondoka mwambie Dreva aniandalie lile gari laaaaaaa.” Mr Mandoto alisema huku akiangalia magari alionayo lipi litampendeza leo.
Bertha : “Lipi mume wangu!?” Bertha aliuliza kwa udhaifu maaana kwa vitendo vya mumeo vimemkata maini kabisa chakula kapika sasa atakula na nani!?
Mr Mandoto : “Ntaenda na ile VanGaurd mpya.” Alisema huku akifungua mlango na kuzama ndani.
Bertha : “Sawa! ”. Huku akipindisha shingo kinyonge .
Betha : “Johnyyyy..” Alimwita dreva wao kwa ajili ya kumpa maaagizo aliopewa
John : “Abee mama..”.
Bertha : “Jamanii mi si nlikuwambia mimi mdogo tu jaman nina miaka 24 tu wacha kuniiita mama jamani.”
John : “Sawa mama…. samahani Dada Bertha .” Basi Bertha aka mpa maelekezo aliandae gari lilio agizwa na mumewe na bertha akaingia ndani.
Bertha alimkuta mumewe akioga. Akaenda ku badili avae taulo aka msaport anaeoga kusugua mgongo.
Mr Mandoto : “No usiingie kani nyooshee zile nguo pale jamani si nimekwambia nina kikao!?”.
Bertha alichoka alitamani kulia lakini ndo hivyo mapenzi ni kuvumiliana.
Bertha : “Sawa mume wangu.”
Bertha akaenda kuchukua nguo alizo ambiwa na mumewe azinyooshe lakini bertha alishangaa mbona mumewe hajawahi kamwe kwenda kwenye kikao na Tshirt na jeans. Bertha alishindwa kuelewa labda ni mtindo mpya wa mumewe labda anajaribu kuunganisha urafiki zake na wateja zake.Akachukua koti jekundi la mumewe alilo sema akali futa vizuri kabsa mara baada ya muda mume wake ali ingia akavaa nguo akiwa amejifunika na taulo kana kwamba hataki mke wake amuone labda mume wake alijisahau akafikiri Bertha ni mjomba wake!?.
Mr Mandoto hakupoteza muda aliondoka na kupanda gari haku diriki hata kuaga mke wake alimsimisha
Bertha : “Mume wangu unaenda wapi?.” Bertha aliuliza kwa upendo tu.
Mr Mandoto : “Ushaaa anza si ndio?.Nilipokuja si nimekwambia naenda kwenye kikao ama? Eeeh nimekwambia niandalie nguo ume andaa bado tu hujui ninapo enda !?”.
Bertha : “Ndio mume wangu ! Samahani .”Bertha alijibu kwa upole.
Mr Mandoto : “Haya basi naenda kufagia barabara si ndo unachotaka nikuambie jiongeze bhana.”
Mr mandoto aliondoka kwa haraka akapanda gari na kuondoka akapandisha kioo chake cha tinted asi diriki ku punga kwa heri.Bertha alipiga magoti na kuanza kulia pale kama kafiwa kusiwe na mtu wa kumembeleza kwenye nyumba hii kubwa kama hoteli lakini ni nyumba ya watu. Hii imekuwa ni mara nyingine bertha akilia hivi hata bila kupigwa kwa mwezi wanne sasa!
Itaendelea...
 

equator

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
214
250
My Soulmate kipande cha 8
Produced by: EquatorStory Special.
Ilikuwa mida ya saa moja asubuhi bertha ana amka kesho yake baada ya mumewe kwenda kwenye ‘kikao' na hajarudi mpaka wasaa huo.
Aliamka akiwaza mengi sana kichwani mwake akiwaza ni mambo gani ya kufanya mumewe hajamshughulikia kama mwezi wa tano sasa na majibu anayo mpa sio ya dunia hii. Ndoa ya bertha imekuwa kama jinamizi anakumbuka mara ya kwanza wakati haya matatizo yana anza wakati kulikuwa na ka tafrija kadogo ka familia mumewe alikua kama malaika akimbusu mkewe na kumuongelesha vizuri kama sio yeye mwenye majibu ya kukata maini. Bertha alitaka kuwa onesha wazazi wa mumewe machungu anayopitia lakini tatizo ni kwamba iyo siku mumewe alikua mwingine kila mmoja akamgeukia bertha kumshutumu kwamba ana matatizo mbona mumewe hajifichi kuonesha kwamba anampenda hakuna alieamini kuwa kuna matatizo.
Bertha anawaza ataongea na nani amuamini zaidi ya shoga wake hamida amsaidie. Hamida mwenyewe ana lala na mwanaume ambaye hajaolewa naye na saivi ana mtu ambae ndiye siye. Bertha ana amini kwamba kabaki na Mungu tu japo ana jitahidi kwenda kwenye maombi mumewe ana mzuia akisema anaenda kwa wanaume wake. Bertha husikiliza maombi kwa radio na mara kadhaa anaomba kwa uchungu sana mpaka anatokwa na machozi. Bertha huyu hajaenda kanisani kama ilivyo kuwa kawaida yake tokea aolewe na Mr Mandoto ni siku mbili alienda baada ya hapo aka achishwa kwenda kanisani ki mzaaa mzaa tu.
Wakati Bertha akiwaza na kuwazua mawazo yake yalikatishwa kwa sauti ya mtu aliekuwa akigonga mlangoni kwao. Akafuta uso vizuri akajiweka vizuri akitumai ni mumewe ametoka kwenye hicho “Kikao”alichoenda. Akakimbia kiasi akafungua mlango.
Bertha akafungua mlango akaona ni mdada amesimama mlangoni .Huyo mdada ni wifi yake Bertha aitwae Rose.
Bertha : “Karibu Rose.”
Rose : “Embu nipishe mie.” Alisema hivyo aki msukuma kidogo Bertha na kuingia ndani.
Rose alipaza sauti akiwa ndani ana muita kaka yake Mr Mandoto bila kujua yuko wapi.
Rose : “Kakaa kakaaa”. Alipaza sauti akigeuza kichwa huku na huko.
Bertha : “Mume wangu hayuuu……”. Rose alimnyooshea kidole chake kilichokua na kucha kama za vile vyombo wanavyotumia kuchotea unga dukani aki ashiria bertha anyamaze.
Rose : “Sijaongea na wewe kikaragosi nimemuita kaka yangu. Mbwa wewe nyamaza.”Rose aliongelea kwa nguvu huku akipandisha mi kucha yake kama shetani na akamsonya.
Bertha : “Unasema!!!??. Bertha hakuamini alicho kisikia kutoka kwa rose aliongea huku akimgeuzia shingo.’
Rose : “Kwani hujanisikia we Malaya!?? Wewe kazi yako kulala na wanaume wengine unajifanya sijui unajifanya unaendaga kanisani kumbe hamna kitu mwanaharamu wewe.”Rose aliongea huku akipeleka shingo mbele na akimnyooshea mkono Bertha.
Bertha : “Rose wewe ni wifi yangu usitake tugombane! Jamani.”. Bertha alisema kwa upole hakutaka shari.
Rose : “Utanifanya nini wewe tasa? umetoa mimba huko ututoni ndo maaana hujaweza kuzaaa na kak……”.
Betha sijui alimfikia saa ngapi Rose aka mwasha kibao cha kwanza cha kulia akaona haitoshi akampiga vingine vya haraka yani paaah paaaah.
Rose : “Niaccche!!!! Niachee!!!!.”Alisema hivyo akiwa ameshavimba mashavu na wigi limekaaa kushoto na alama nyekundu kutokana na vibao alivyo labuliwa .
Bertha : “Nimekuchoka wewe leo ndo utanijua!!!.”
Bertha bila kupoteza muda akamrushia ngumi ya nguvu zote tumboni kwa rose.
Rose : “Mamaaaa!! Niacheee!! ananiua!!.”
Bertha bado amewaka na hasira akamvuta na wigi akijua ni nywele zake wigi likamvuka rose. Rose akarusha kibao cha kuotea kika mpata betha.
Bertha : “We unampiga nani kwa jina la mungu utashika adabu.”
Bertha akamshika rose kwa vinywele zake ambazo zilikua hazija sukwa na kufichwa na wigi akamwinamisha akampiga vibao vya mgongoni akamburuza kwa nywele mpaka kwenye kochi.
Bertha : “Kaaa hapo nkupe somo umekua ukinidharau sana.”
Rose : “Nisamehe kakaaaaa nisaidiiiieee ananiua huyu.”Rose hakujua kama kaka yake hakuwepo nyumbani.
Bertha akamuweka rose kwenye kochi akaegemea kwa magoti na kumziba rose akamshika kichwa kwa nguvu akamgongeza kwenye kochi.
Rose : “Jamani kakaaaa jamani uuuuwi nisamehe ananiuwa!!! .”.Bertha hakua anamsikiliza alikuwa bize kugawa kipondo .
Bertha akamshika kwa nguvu rose akamgeuzia kwenye kochi kwa pua yake akamburuza kwenye kochi kushoto kulia mara ampigize.Bertha akatulia kidogo aka mwangalia rose aliekuwa na make up kwa upande huu upande mwiingine hana hapo uepe wake ulikua umeanza kupungua.
Bertha : “Sasa kwanzia leo utanheshimu wewe mbweha mdogo.”Akamwasha kibao cha uso paaaah kibao kizito hicho.
Bertha : “Wewe yani ntaku adabisha mbweha mwitu ngumi ya kifua.”
Rose : “Jamani utaniua .”Bertha akamkandamiza kwenye mdomo akamfukia kwenye kochi nusu uso.
Rose alipo ona hivyo akamsukuma Bertha akainuka akaanza kukimbilia nje bertha naye anamfatia kwa nyuma akimkaribia ana mwasha kibao cha mgongo.Mpaka nje rose hajui pochi yake ikowapi make up hana tena wigi hajui lakini bora uhai. Akatoka kwenye gate mbio Yule alikimbia kama kaona jini.
Wakati hayo yanatokea kwa rose kukimbia alipishana na gari la kaka yake ambae ndo Mr Mandoto hata Rose hakulitambua kama ndo lenyewe alikua kwenye harakati za kubaki na uhai.
Mr Mandoto : “Rose ana shida gani!?”. Wakati huo bertha anahemea juu.
Bertha akamwangalia mume wake kwa hasira akageuka akaenda mpaka ndani. Akapitia jikoni akachukua kisu akaweka kwenye sketi kama anaficha bunduki vile afu akafunika kwa blauzi yake aka anza hatua kubwa kubwa akielekea chumbani kwake.
Bertha akafika kabatini kwake akatoa begi aka chukua na bahasha ndogo ya kaki akafungua akatoa kama kitita cha million nne ama tano hivi . Akaweka kwenye begi la kusafiria aka anza kuchukua nguo zake zilizo ningin`ia kwenye henga na kuzisokomezea kwenye begi bila mpangilio unaeza dhani ana pora mahali vile.
Wakati huo mumewe alikua ana paki gari vizuri akapanda juu kuelekea kwenye master bedroom na akamkuta mke wake yupo bize kama yupo kwenye mashindano ya kupaki nguo haraka.
Mr Mandoto : “Enheee kwa hiyo unafanyaje!?”.
Bertha : “ “Bertha kimya . Huku mumewe ameshika kiuno kujiuliza nini kinaendelea huku hajapata jibu kujua kwa nini rose alikua anakimbia na isitoshe amekuta vitu vyake pale sebuleni . Viatu huku wigi kule.
Mr Mandoto : “Na rose imemtokea nini mpaka anakimbia!?”.
Bertha : “Nenda kamu ulize atakuwambia.”
Mr Mandoto alitembea kasi na kumfikia mke wake na kumwasha kibao kama anapigana na mwanaume mwenzake.
Bertha akatoa kisu alipokuwa amekificha.
Bertha : “Usinisogeleee we fala!.”Bertha alisema akiwa na kisu mkononi.
Mr Mandoto : “Wewe unichome kisu si utaenda kuozea jela!?”.
Bertha : “Unafikiri mimi mjinga sana!?.”. Aliuliza huku akihema kwa juu na machozi yanamlenga lenga.
Mr Mandoto : “Una kiburi wewe mwanamke baada ya kukufanyia vyote hivi.”Mr Mandoto aliongea akimsogolea bertha . Bertha akajigeuzia kisu tumboni.
Bertha : “Usinisogeleeeee usinisogeleeee. Tayari umenipiga kibao ukinisogelea najichoma kisu tuone kama hutoenda kuozea jela wewe izo hela utazisikia bombani sogea uone.”Bertha alipaza sauti.
Mr Mandoto alijua kwenda jela wakati anazo mali zote hizi kisa mwanamke na aliona ni ujinga pia aliona Bertha anayo point maana ashampiga hakuna mtu atakae mwamini akiwa mahakamani maaana kuona ushahidi wa kumpiga yeye kwanza. Mr Mandoto akarudi nyuma .
Bertha : “Nenda kule kwenye kona kulleeee.” Bertha akachukua begi lake akafunga kwa nguvu huku akimwangalia Mr Mandoto asijaribu kumsogelea.
Mr Mandoto : “Sasa ukiondoka nitabaki na nani na unajua nakupenda!?.”Aliuliza akijaribu kuleta suluhisho kwenye mkasa huu.
Bertha : “Unanipenda!? Unanipenda!? Na umekuwa ukinitesa hiivi!? Hutaki niende nje.”
Mr Mandoto : “Lakini mimi si nakupa kila kitu!? Magari yapo hela zipo!”.
Bertha : “Hata kama haitoshi wewe ni wa kwenda kwenye mikutano usiku mzima !? Ehh. Wewe ni wa kujifanya hunijui wewe mbwa wa kuoza na kutupa umeniharibia maisha yangu tu bure.”
Mr Mandoto : “Lakini nisameheee.”Mr Mandoto alisema akijaribu kupiga magoti lakini anaishia njiani.
Bertha : “Nyooooooo mwanaume gani wewe unampiga mwanamke!? Ile siku nimekuliza ulipo kuja saa tisa usiku umetoka wapi ukaniwasha kibao nika angukia meza nimevimba kichwa ukanilizamisha niseme kwamba nilianguka wakati nina deki afu ukanipa laki moja ety ya kuombea msamaha unazani mimi trainer wako wa boxing kwamba unipige alafu unilipe”. Bertha alianza kuongea hivyo akaaanza kulia machozi yanatirika akiwaza maisha alio kuwa akitaaabika afu saivi anasema anampenda!?.
Mr Mandoto alivyo ona hivyo alijaribu kumvamia Bertha amkamate asiondoke. Wakati anamkibilia bertha sijui alipata wapi nguvu zote alinyanyua lile begi akampiga mumewe la uso akamwangushia kitandani.Bertha akageuka akatoa funguo akamfungia mumewe kwa nje ya chumba akachomoa funguo akaondoka nao.
Mr Mandoto : “Bertha nikikumata wewe Malaya ntakukata ngeu za uso nifungulie we kima FUNGUAAAAAA FUNGUAA nikitoka huta kuwa hai wewe wewe wakunipiga wewe!?”.
Bertha ali simama dakika moja akaungalia mlango aliomfungia mumewe aliamini kwel huyu ni shetani kama sio shetani atakuwa shemeji yake na shetani wallahi. Akakumbuka kanisani alipotokea mchungaji na mama mchungaji walimwambia huyu sio mtu aliepangiwa aka bishana maaana kipindi hicho alikua kipofu kwa hii ngozi ya kondoo ambaye mumewe alijifunika kumbe ni mbweha shetwani kabisa.
Bertha alijifuta machozi akatoka akawakuta wafanyakazi wao Johny yule dreva na Musa ambaye ni mlinzi. Akamwita johny.
Bertha : “Joooohny naomba uje mara moja nikwambie kitu.”. Alimwita dreva.
John : “Naaaam mama.. Sorry sorry….. sister bertha.”Johny alibadili jina haraka baaada ya kuona macho ya Bertha alivyokuwa akimwita “mama”
Bertha : “Sasa huu funguo na zile funguo za haya magari ya kimbize kwa dada wa boss wako boss wako amesema ukifika huko baada ya lisaaa limoja umpigie atakuambia cha kufanya lakini amesisitiza uzime simu yako maaana kuna majambazi wanamfatila kwan hiyo zima simu usije uka uliwa huko njiani ukifika baada ya lisaa uwashe na umpigiie sijui umenielewa!?”.
John : “isssihiii!!!! hawa majambazi wa mitandao mimi sitaki kufa!.”Johny akatoa simu yake akazima akaenda moja kwa moja akachukua funguo alizo ambiwa akaenda upesi aka chukua funguo zote aka panda toyo kwenda alipo tumwa bila kujua ni trick ya bertha ili kuzuia mtu asijue aendapo lakini pia wasiende kumfungulia mume wake.
Bertha : “Mlinziiii” . Akamuita na mlinzi ampe maaagizo.
Mlinzi : “Naaaaam”.
Bertha : “Sasa wewe nenda nyumbani katulie urudi jioni simu yako ikowapi!?”.
Mlinzi : “Nimeiacha kwenye chaji nyumbani maana umeme unasumbua sana so nimeiacha ntaifata jioni.“
Bertha : “Aya baba tembea nikuone ukiondoka bhana nenda kamsalimie wifi yetu kamfanyie hata surprise leo kuwa mjanja!. Au unaogopa utamkuta mme mwenzako!?”.
Mlinzi : “Hahahahahhahah sasa ntamfanyia surprise na nini wakati sina kitu.”Bertha alichomoa elfu kumi akampa.
Bertha : “Kanunue hata cheni mpya ukamvishe si unajua mapenzi kudekezana!?”
Bertha alipo ona mlinzi ameondoka alitoka zake akapanda toyo mpaka mitaaa flani akashuka akamlipa toyo akaenda kama mitaa mi nne mbele akapanda toyo nyingine ili Yule toyo asiseme alimpeleka wapi na mmoja kwa moja stendi akapanda gari ya kwenda Arusha. Akafikia hoteli ya Florida 2000 ambapo hakuna mtu amjuae alipo wala hakubeba simu yake ili asitafutwe aliona hii ndo nafasi ya kwenda kuanza maisha mapya.
Itaendelea….
 

equator

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
214
250
My Soulmate kipande cha 9
Produced by: EquatorStory Special.
Bertha baada ya kukaaa hotelini kwa juma lizima aliamua kwenda kutafuta nyumba hata akipata chumba itamsaidia kwa sababu ataishi ndani ya nyumba hiyo mpaka lini. Basin aye akaondoka mpaka maeneo ya makazi ya watu akazunguka huku na kule kutafuta chumba aya anze maisha upya.
Bertha alipata dalali akawa anapita vyumba mpaka vyumba kutafuta chumba kitachompendeza macho yake mpaka alipofika kwa mama Grace ambapo alipata chumba kimoja ambacho kilikuwa wazi na alikuwa tayari kuhamia hata kesho yake.
Mama Grace: “Sawa binti kesho ntamwita kijana akifanyie ukarabati na usafi kidogo ili uje uhamie kabisa.” Alisema akiwa na uhakika wa kwamba atakuja kwa sababu ashatoa hela kidogo ya kuzuia mtu mwingine asimuwahi.
Bertha : “Sawa mama linah jamani nimefurahi kupata sehemu nzuri!.”
Wakati huo Bertha anakaribia kufungua mlango mara mlango ulisukumwa na kumgonga Bertha puani .Bertha alikunja sura.
Bertha : “We mpumbavu unafunguaje mlango hivyo.”
Nickson : “Samahani dada sikujua kama ulikuwepo hapo.”
Bertha : “Achana na mimi bhana! Pole yako haisaidi kitu mxxxxheww.”
Nickson : “Dada samahani.” Bertha kwa hasira alimsukuma Nickson kwa hasira na kutoka kwa kasi na hasira.
Bertha : “Haya mama grace kwaheri.”Nickson alibaki kushangaaa tu huku bertha na dalali wake wakitoka kwenye nyumba hiyo.
Basi siku hiyo ikaisha. Bertha aka nunua vitu vya nyumba yake japo ni chumba kimoja ni pamoja na kitanda, mashuka, mito na vyote ambavyo zina mruhusu mtu aanze maisha kiasi fulani.Bertha ndani ya siku mbili bertha tayari ame hamia kwenye maisha yake mapya.
Asubuhi ya skiu ya tatu akawa anafanya shughuli zake. Mara ghafla akakutana na Nickson.
Nickson : “Habari za asubuhi?”.
Bertha : “Mxxxxxheew!!!”Aka mtizama kwanzia juu mpaka chini akikumbuka Nickson ali mbiza na mlango bahati mbaya.
Nickson aliachwa ame simama kama mlingoti akijiuliza amekosea nini. Labda ni ule mlango ulivyombamiza aliwaza aka amua tu kuendelea na shughuli zake.
Nickson ali endelea na michakato za kila siku. Akamaliza kila kitu aka ondoka kuelekea ofisini kwao.
Nickson aliendelea na kazi zake pamoja na Boss wake kumkandamiza kila siku lakini akawa anajikaza kuendelea na kazi yake.
Ilipofika kazini Nickson alienda kwenye chumba cha jiko dogo la ofisi yao na kumkuta Angela akinywai chai.
Angela : "We mkaka leo mbna umependeza hivyo!?".
Nickson : "Aaah mama yangu kaninunulia nguo mpya ". Alijibu Nickson huku akafunga mlango na waka anza kucheka.
Angela : "Wewe kaka huishiwi na vituko vyako tu!?".
Nickson : "Aaah kawaida tu unajua Mungu hajaweka bandama bahati mbaya mwilini inabidi tuitumie ikiwezekana tutafute na za nyongeza tubadili hizi zikichakaa. ".
Angela : "Haya bhana umeshinda."
Nickson : "Mbona kama una kaa ki huzuni leo!? una waza nini!?".
Angela : "Wacha tu ni maisha kuna kitu kimetokea siamini amini."
Nickson : "Nini hicho embu nipe umbea.". Angela alitabasamu kidogo akisikia ety Nickson anataka umbea.
Angela : "Bhana unajua mama yangu..... Lakini usije ukamwambia Nickson. Wewe unajua mimi ni supervisor wako sasa tukianza kuchanganya na mambo ya familia haipendezi sana!".
Nickson : "Wala usiwe na shaka we pia ni bin-adamu kama nilivyo."Alijibu kumpa nguvu ya kuendelea.
Angela : "Hivi kwanza nina anzaje kuku ambia mambo yangu!?".
Nickson : "Roho yumo ndani najua huwezi kujizuia kusema ukwel we nena tu."Wakacheka tena.
Angela : "Lakini kweli wewe mkaka ni wa tofauti nimekupenda bure.. Lakin kama rafiki usije enda kanisani kutoa ushuhuda."
Nickson : "Sema ukweli.. tu unajua hilo ni agizo la Mungu hilo kasema tupendane."Nickson aliona ndo mbinu ya kujua kama Angela yupo singo ama vipeee. Lakini anakuwa na kusita sita moyoni maana tayari yupo na Stela na Nickson.
Angela : "Kwani unataka kujua kama nina mtu!??". Angela aliuliza baada ya kujua mbinu ya nickson Angela alianza kumuangalia vizuri nickson akiwa ana ng`ata kucha.
Nickson : "We sema hali ipoje wadau tujue!."Nickson hakutaka ku uliza swali hilo maaana siku hizi Angela na Stela wapo karibu na yamkini Stela alisham mwambia kila kitu.
Angela : "Mi kusema kweli saivi sina mahusiano na mtu lakini kwa sasa sipo tayari nataka kukaa hivi hivi kwa muda maana mahusiano nliopitia dah ni noma yani nyie wanaume."
Nickson : "Vipi ali kataa kukupa hela ya ku suka nini!?".Nickson aliuliza ili kumchokoza Angela amtoe paka kwenye mfuko yani siri hiyo.
Angela : "Kaaa sasa nikupashe kwanza si muda wa kula huu."
Nickson : "Sawa nena sasa nakupa masikio yangu."
Angela : "Bhana kuna huyo kijana nilikutana naye ni hendsamu lakini hakukutii wewe."
Nickson : "Unanionaje!? ". Akikaaa vizuri ili aendeleee kupewa simulizi hii.
Angela : "Nakuambia huyo mkaka alikuwa anaitwa Hemedi."
Nickson : "Enhee.."
Angela : "Nickson nakuambia huyo mkaka alikua anavaaa vizuri yani ukimwona kama wewe ni mdada lazima ubaki mdomo wazi. Na nilimpenda alivyoonekana alikua mrefu zaidi kwangu lakini sio sana. Na alikua ana cheo kizuri alikuwa ni kwenye kampuni flani ya huko Dar-es-salaamu tena alikua ana lipwa vizuri sana."
Nickson : "Enhee nini sasa kikatokea!?".
Angela : "Yule kaka alikua amejiendeleza vizuri lakin alikua na shida mbili tu."
Nickson : "Zipi hizo!?."
Angela : "Nickson yani mkaka alikuwa anapenda wanawake hujawai kuona."
Nickson : "Sasa kwani kupenda wanawake si vizuri au ulitaka apende wanaume wenzie!?".
Angela : "Hapana sio hivyo nickson!!". Alinyoosha mkono na kumgusa kidogo Nickson.
Nickson : "Vipi sasa!?".
Angela : "Yule mkaka alikua ni macho na wanawake. Hata akiwa na mimi kila saa akipita mwanamke aliejaliwa umbo zuri au hata wasio na maumbo makubwa sana alikua anageuza macho kuwa tazama."
Nickson : "Acha utani!.".
Angela : "Yani hata nikiwa nae anapepesa macho kila saaa. Na nikimwambia ana niwakia ooooh mbona una wivu sana!? Mimi si nipo na wewe jamani ama unataka nikuache nikawe nao!?. Yani kusema kweli alikua ana nikera sana lakini nitafanyaje wakati nampenda!??."
Nickson : "Maaajabu na mengine!?"
Angela : "Sasa yote tisa kumi yule mkaka alikua ana penda pombe heeeee.".
Nickson : "Ungempeleka kanisani."
Angela : "Hahahaah Wewe kaka bhana."
Nickson : "Enhee endelea"
Angela : "Yule kaka alikua anapokea kama millioni mbili kwa mwezi hela ambayo mimi siipokei. Lakini hutamwona usiku nyumbani kama wiki na akirudi hana hata sumni!."
Nickson : "Labda kawekeza!?."
Angela : "Hapana.. Yule mkaka alikua anakaaa baaa mpaka baaa akinywa na wanawake zake na marafiki zake ambao walikua wakimtafuta mwisho wa mwezi tu akisha ishiwa wanapotea wao wanafanya maendeleo yao lakini wanalewa nae mpaka mkaka wa watu anaishiwa afu wanapotea."
Nickson : "Si ungemshauri kuhusu marafiki zake sasa!?."
Angela : "Unadhani sijamwambia? Nimemwambia lakini hataki kunisikia anasema mbona hanichagulii marafiki!?"
Nickson : "Hapo mtiani."
Angela : "Unazani kidogo sasa!? Lakini yule mkaka sijui alikua ananifanyia nini nisimwache!."
Nickson : "Labda ni limbwata."Angela akacheka .
Angela : "Wacha tu sasa kilichonichefua sasa kafukuzwa kazi baada ya kuonekana ni mnywa pombe uliokidhiri. Ni kamwambia ahamie Gheto kwangu kinpindi hicho naishi mwenyewe akawa anaishi na mimi yule mkaka bhana."
Nickson : "Kweli unajua kupenda wewe dada na kuji wekeza kwenye uhusiano."
Angela : "Yani we acha tu. Namshukuru rafiki yangu ELiza kunishauri nisizae nae kabla sijamjua kwa kina maana sijui saivi ntakua wapi kama angeniachia mtoto."
Nickson : "Bora hata inaokena unajua kuchagua marafiki wema ndugu maana wengine wasinge diriki kukuonya kuhusu hilo swala. Enheee ikawaje sasa shoooo!"Wakacheka sana.
Angela : "Wakati tunaishi nae akawa hana mbele wala nyuma akauza mali zake zote nazo zoteee kwenye pombe. Mimi namuangalia tu nikasema huyu maisha yatamnyoosha na atabadilika."
Nickson : "Duh hiyo ngumu lakini."
Angela : "Sasa akawa hana kitu kabisa na nyumbani kwao alishindwa kurudi kwa sababu ya aibu. Mimi nikawa najinyima namlisha nampa nguo nalipia umeme yeye yupo tu!."
Nickson : "We ni mwanamke shupavu ngepata kama wewe ningeoa hata wanne hata kama dini haini ruhusu."
Angela : "Weee unioe na mwingine mi siezi nina wivu lakini kwani mimi sikutoshi!?. Lakin bhana siku nimeenda kazini night narudi asubuhi namkuta yupo na mdogo wangu uchi wa mnyama na ni shuka tu limewa funika."
Nickson : "Wacha wewe!."
Angela : "Nili leta fujo kama nadai tapeli hela zangu. Badae ananiambia kwamba ali jikuta akimpenda mdogo wangu kwa sababu ni mdogo kuliko yeye alafu pia mimi nilikua bize sana. Eti nikifika nafua mara nipo bize na pika mara nipo kazini lakini mdogo wangu ndo alikua na yeye. Lakini akaniambia kwamba mdogo wangu alikua anampikia wakati sipo lakini pia daaaaa."
Angela aliacha kusimulia na aka anza kutiririsha machozi. Nickson akasimama akaenda kumkombatia na akambembeleza Angela. Angela alikua analia kwa huzuni sana huku akiegemeza sura yake kwenye kifua cha Nickson . Nickson akamshika upande wa uso akitaka kumbusu mdomoni angela. Angela alipo ona hivyo aka funga macho na kumuachia Nickson afanye atakalo Nickson akaugusa mdomo wa Angela.
Mara Ghafla mlango uliguswa na mtu Nickson aka muacha Angela haraka akaenda kushika kikombe cha chai na angela akaenda kwenye sinki la kuoshea vyombo na aka anza kunawa uso.
Stela : "Nickson Computer yangu ina kataa ku chapisha makaratasi twende ukanisaidie kurekebisha."
Nickson : "Sawa ngoja nichukue kahawa nasikia ka usingizi."
Stela : "Bertha vipi mbona kama macho mekundu!?".
Bertha : "Jana nilikesha nakuambia hapa nina lala sasa nimekuja kunawa hii kupandishwa cheo ni kazi sana sio kwa hayo ma kazi."
Stela : "We sema tu ulikua una angalia movie wewe!"
Angela : "Hahahahahahah wewe na huyu jamaa ni timu moja eeeh!? maaana na yeye amesema hivyo hivyo!."
Basi Nickson na stela wakaondoka mpaka kwenye computer ya stela .
Nickson : "Mbona ina chapisha vizuri tu!?".
Stela : "Mi sikutaka ubaki na huyo ngedere asije akakuiba."Wakati huo Nickson akapokea sms kutoka kwa Angela.
Nickson : "Wewe una kichaaa syeti mimi natokaje na boss wangu!? Lakini pia huniamini!?".
Stela : "Haijalishi nitakulinda mi sitaki kufanywa mjinga!."
Nickson : "tafadhali usiniharibie siku yangu na nikikuona unaendelea hivi tuta achana we unawaza tu mimi kuchepuka kila saa!?."
Stela : "Haihusu..."
Nickson akaondoka bila kujibu aka enda kukaaa ili asome sms alio isikia kwenye simu dakika kadhaa awali.
"Asante kwa kunisikiliza nlikua nahitaji mtu wakuongea nae!."Nickson akajiuliza alisahau kuhusiana na lile busu ama!?. Lakini aliamua kuli mezea hilo kwa kiasi flani ana furahi pia Stela hakumfuma maaana wote wangekua na hatari ya kupoteza kazi kwa skendo kubwa!.
Ukafika mda wa kuondoka kila mmoja akaenda kwake. Nickson alifika kwake akaoga na akavaa nguo zingine za kushindia alipo kuwa ameketi aanze kufanya shughuli zake akasikia mtu anagonga mlango.
Bertha : "Hodiii.."
Nickson akafungua mlango akakumbuka "Huyu si ndo yule mdada mpya alie nitukana kisa mlango!?".
Itaendelea!
 

equator

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
214
250
My Soulmate Kipande cha 10
#####Tulipoishia#####
Nickson alifika mlangoni baada ya kufungua akakuta ni yule mdada aliemtukana kisa mlango.
### Tuendelee ####
Nickson : "Unasema nini!?".
Bertha : "Kaka umeshindaje!?".
Nickson : "Salama! lakin unataka nini ongea chapu!."
Bertha : "Sasa kakaaaa".
Nickson : "Samahani nina jina langu naitwa Nickson."
Bertha : "Sawa Nicky".
Nickson : "Sorry ita jina langu kamili unaniitaje kwa kifupi mi sipendagi kama huna mda wa kumalizia sema mi nifunge mlango nifanye vyangu!."
Bertha : "Nickson sikiliza basi.."
Nickson : "Haya ongea ". Nickson anakumbuka alivyo semeshwa na Bertha kisa alivyo fungua mlango na uka mgonga bahati mbaya ana jua hapa lazima alipize kisasi.
Bertha : "Nimekuja kuomba msamaha Nickson sasa saivi wewe ni jirani sasa nitakaaaaje na mtu wakati hatupatani kisa tu stress zangu!?".
Nickson : "Ah wapi we dada stress wakati ndo tabia yako. Wa dada wengi mnakuaga na madharau mimi madharau sipendagi hata kidogo."
Bertha : "Nickson sikia mpaka mimi kuja na kuomba msamaha ni kwamba nimetambua kosa langu na nataka kujirekebisha."
Nickson : "Nakusikiliza."
Bertha : "Nickson naomba tueke utaofauti wetu pembeni na tuanze upya. Nisamehe kwa yote nliokukera."
Nickson : "Saw nimekusamehe hivyo ndo mtu anavyo takiwa kuwa jitahidi msamaria na utaishi vizuri."
Bertha : "Nashukuru kwa kunisamehe. Uwe na jioni njema Nickson."
Nickson : "Sawa haina shaka karibu sana huku mtaani kwetu."Wakati huo Bertha alikua amesha anza ku ondoka kuelekea chumbani kwake. Nickson akamsimamisha.
Nickson : "Dada umesema jina lako nani!?"
Bertha : "Hahaha ndo una kumbuka saivi. Naitwa Bertha."
Nickson : "Haya sawa nafurahi kusikia hivyo".
Bertha : "Haya kwa heri."
Wakati huo jirani mwingine wa Nickson alikua ndo anaingia kwenye nyumba hizi za kupangisha.
Nickson : "Niaje Dulla".
Dulla : "Ah ni poa mwana niaje!?"
Nickson :"Poa tu tuna enda na kasi na ari mpya.".Wakati huo Dulla anamsogelea Nickson.
Dulla : "Nakuona una winda babu!. Usha anza na Jirani mpya we jamaaa hatari wewe". Dulla alisema huku aki tabasamu kidogo.
Nickson : "Aaah wewe usiwaze hivyo haya ni mambo ya kawaida."
Dulla : "Aaaah wapi wewe! Yangu macho tutaona tu una cho panga!."
Nickson : "Haya mtu wangu ngoja niingie bhana ni kachakarike na ma msosi. Si unajua sisi tuliopo kivyetu vyetu hatuna msaaada!."
Dulla : "Ngoja na mimi nika lale!."
Nickson : "Poa poa mkuu!."
DUlla aliondoka kuelekea kwenye chumba chake na ndivyo siku ilivyomalizika.

Nayo miezi ikaendelea kusonga mbele urafiki wa Nickson ukapamba moto waka ivana na kuwa karibu zaidi. Hakuna ajuae Bertha yupo Arusha na ana urafiki wa karibu sana na Mwanaume mwingine japokuwa ni marafiki tu sio rahisi kuamini.
Ni asubuhi Nickson anaelekea ofisini mara akasikia akiongeleshwa.
Bertha : "Nickson njoo unywe chai rafiki yangu kabla hujaenda!."
Nickson : "Aaah ungeniambia mapema tayari nishakunywa!."
Bertha : "We jifanye tu hulagi kwa watu!."
Nickson : "Ushaaa anza zako rafiki yangu!."
Bertha : "Haya siku njema. Uwahi basi tupige stori."
Nickson akaondoka na kuondoka kwenda kazini. Aka fika mpaka jiko la ofisi kwa ajili ya kupata maji!. Akamkuta Stela ndo anaandaa chai. Akafunga mlango kwa nyuma yake aka muwahi stela kabla ya kugeuka akamfunga macho.
Stela : "Jamani Boss acha zako."
Nickson : "Unasemaje!?"
Stela : "Hahahaah mbona umeshtuka wewe si ndo Boss wa moyo wangu au unawaza nini mwaya!?".
Nickson : "Kweli mi ndo Boss!? "
Stela : "Ndio mwaya We nipelekeshe unavyotaka."
Nickson : "Haya ni busu mdomoni."
Stela : "Sawa boss nafanya unalotaka".Wakati Stela ana mbusu Nickson Boss wao alikua ofisini na aliwatazama kwa kupitia kideo kilicho unganishwa na Camera za ulinzi.
Nickson : "Mpenzi unajua nina mpango wa kuacha kazi hapa naona kama siwezi kwenda mbele yani nakwama bure."
Stela : "Unasema!?". Aliuliza akianza kukaa mbali na Nickson huku akianza kukunja sura.
Nickson : "Mpenzi nimekaa hapa miaka miwili lakin sioni kama kuna maendeleo. Na pia sioni umuhimu wangu".
Stela : "Kwani unakaa hapa!?".
Nickson : "Nalipwa lakini mshahara nilio anzia mwaka juzi ndo ninao mpaka leo."
Stela : "Sasa kinachokuwasha!?"
Nickson : "Hamna kinacho niwasha nataka nifike mbali sana katika tasnia yangu ya mambo ya Computer. Ikiwezekana nijiajiri."
Stela : "Hehehe ushaaanza na ujinga wako wa kujiajiri una hela ya kujiajiri we una matope ubongoni si ndio!?".
Nickson : "We unataka tuoane tukae nyumba ya kupanga mpaka lini!?"
Stela : "We nani kakwambia nataka kuolewa nikae nyumba ya kupanga!?."
Nickson : "Kwa hiyo mimi nifanyaje!?."
Stela : "Jiongeze! Mi sitaki mwanaume masikini nimetaaabika sana unioe unirusdishe kwenye umasikini eti nyumba za kupanga!?."
Nickson : "Sasa mimi nafanyaje na nkiendelea kukaa kwenye kampuni hii siendi popote."
Stela : "Mxxxxhewww."Stela alifyonza aka acha hata chai yake na akaondoka kwa hasira.
Wakati wote hayo yote yanafanyika Boss alikuwa ndo amefika na akawa anaona kila kitu kitu kwenye camera alizoweka!. Lakini bahati nzuri au mbaya aliona tu picha hakusikia sauti.Boss aliketi akatafakari bila kuamini alicho kiona akapanga mipango yake na hakutaka kusema kuwa ameona.
Basi ikafika muda wa ku funga ofisi Nickson akaelekea zake nyumbani moja kwa moja akakutana na Bertha.
Bertha :"Mambo Nickson pole na kazi."
Nickson : "Poa asante. Umeshindaje!?".
Bertha : "Salama tu."
Nickson : "Haya sawa ". Nickson akawa anaanza kuondoka kuelekea chumbani kwake.
Bertha : "Nickson!.."
Nickson : "Naaam.".
Bertha : "Leo una mpango wa kula nini usiku!?"
Nickson : "Sina uhakika kwanza nimechoka kujipikia sijui hata nitafanyaje."
Bertha : "Ahhhaaaa".
Nickson : "Kwa nini umeuliza?"
Bertha : "Nataka niende nikale vitu kama mihogo ya kukaanga na miguu ya kuku!. Nikipata na ka pilipili kidogo na chips kidogo mi na ridhika!."
Nickson : "Mhhh haina shida."
Bertha : "Usiseme hivyo bhana."
Nickson : "Sasa niseme aje jamani!?"
Bertha : "Mi nataka unisindikize afu bill mimi nitalipa."
Nickson : "Saa ngapi una enda!?".
Bertha : "Saa moja au mbili hivi."
Nickson : "Sawa ngoja nkaoge ni pumzike kidogo alafu nitakusindikiza angalua leo sipiki maaana nimechoka sana."
Bertha : "Haya sawa usichelewe sasa."
Ilipo fika mida ya saa mbili kasoro bertha na Nickson walitoka kwa pamoja na kuelekea kula kama walivyopanga na wakarudi wakitembea kwa karibu sana hii ikawa ni kawaida yao mara zingine hata Nickson ana msahau Stela japo kuwa Bertha sio Mpenzi wake yeye ana ufurahia ukaribu wake na Bertha.
Nickson anajiuliza huyu mwanamke kama huyu nitampata wapi sio kwa ukaribu huu. Lakini pia ni mwanamke ambaye hapendi makuu. Yeye chochote kidogo ana ridhika yani ana tamani Stela awe kama huyu lakini ndo hivyo!.
Itaendelea......
Comment yako na Reaction kama zote itakuwa safi sana!
 

Kaijadan

Member
May 31, 2017
41
125
My Soulmate Kipande cha 10
#####Tulipoishia#####
Nickson alifika mlangoni baada ya kufungua akakuta ni yule mdada aliemtukana kisa mlango.
### Tuendelee ####
Nickson : "Unasema nini!?".
Bertha : "Kaka umeshindaje!?".
Nickson : "Salama! lakin unataka nini ongea chapu!."
Bertha : "Sasa kakaaaa".
Nickson : "Samahani nina jina langu naitwa Nickson."
Bertha : "Sawa Nicky".
Nickson : "Sorry ita jina langu kamili unaniitaje kwa kifupi mi sipendagi kama huna mda wa kumalizia sema mi nifunge mlango nifanye vyangu!."
Bertha : "Nickson sikiliza basi.."
Nickson : "Haya ongea ". Nickson anakumbuka alivyo semeshwa na Bertha kisa alivyo fungua mlango na uka mgonga bahati mbaya ana jua hapa lazima alipize kisasi.
Bertha : "Nimekuja kuomba msamaha Nickson sasa saivi wewe ni jirani sasa nitakaaaaje na mtu wakati hatupatani kisa tu stress zangu!?".
Nickson : "Ah wapi we dada stress wakati ndo tabia yako. Wa dada wengi mnakuaga na madharau mimi madharau sipendagi hata kidogo."
Bertha : "Nickson sikia mpaka mimi kuja na kuomba msamaha ni kwamba nimetambua kosa langu na nataka kujirekebisha."
Nickson : "Nakusikiliza."
Bertha : "Nickson naomba tueke utaofauti wetu pembeni na tuanze upya. Nisamehe kwa yote nliokukera."
Nickson : "Saw nimekusamehe hivyo ndo mtu anavyo takiwa kuwa jitahidi msamaria na utaishi vizuri."
Bertha : "Nashukuru kwa kunisamehe. Uwe na jioni njema Nickson."
Nickson : "Sawa haina shaka karibu sana huku mtaani kwetu."Wakati huo Bertha alikua amesha anza ku ondoka kuelekea chumbani kwake. Nickson akamsimamisha.
Nickson : "Dada umesema jina lako nani!?"
Bertha : "Hahaha ndo una kumbuka saivi. Naitwa Bertha."
Nickson : "Haya sawa nafurahi kusikia hivyo".
Bertha : "Haya kwa heri."
Wakati huo jirani mwingine wa Nickson alikua ndo anaingia kwenye nyumba hizi za kupangisha.
Nickson : "Niaje Dulla".
Dulla : "Ah ni poa mwana niaje!?"
Nickson :"Poa tu tuna enda na kasi na ari mpya.".Wakati huo Dulla anamsogelea Nickson.
Dulla : "Nakuona una winda babu!. Usha anza na Jirani mpya we jamaaa hatari wewe". Dulla alisema huku aki tabasamu kidogo.
Nickson : "Aaah wewe usiwaze hivyo haya ni mambo ya kawaida."
Dulla : "Aaaah wapi wewe! Yangu macho tutaona tu una cho panga!."
Nickson : "Haya mtu wangu ngoja niingie bhana ni kachakarike na ma msosi. Si unajua sisi tuliopo kivyetu vyetu hatuna msaaada!."
Dulla : "Ngoja na mimi nika lale!."
Nickson : "Poa poa mkuu!."
DUlla aliondoka kuelekea kwenye chumba chake na ndivyo siku ilivyomalizika.

Nayo miezi ikaendelea kusonga mbele urafiki wa Nickson ukapamba moto waka ivana na kuwa karibu zaidi. Hakuna ajuae Bertha yupo Arusha na ana urafiki wa karibu sana na Mwanaume mwingine japokuwa ni marafiki tu sio rahisi kuamini.
Ni asubuhi Nickson anaelekea ofisini mara akasikia akiongeleshwa.
Bertha : "Nickson njoo unywe chai rafiki yangu kabla hujaenda!."
Nickson : "Aaah ungeniambia mapema tayari nishakunywa!."
Bertha : "We jifanye tu hulagi kwa watu!."
Nickson : "Ushaaa anza zako rafiki yangu!."
Bertha : "Haya siku njema. Uwahi basi tupige stori."
Nickson akaondoka na kuondoka kwenda kazini. Aka fika mpaka jiko la ofisi kwa ajili ya kupata maji!. Akamkuta Stela ndo anaandaa chai. Akafunga mlango kwa nyuma yake aka muwahi stela kabla ya kugeuka akamfunga macho.
Stela : "Jamani Boss acha zako."
Nickson : "Unasemaje!?"
Stela : "Hahahaah mbona umeshtuka wewe si ndo Boss wa moyo wangu au unawaza nini mwaya!?".
Nickson : "Kweli mi ndo Boss!? "
Stela : "Ndio mwaya We nipelekeshe unavyotaka."
Nickson : "Haya ni busu mdomoni."
Stela : "Sawa boss nafanya unalotaka".Wakati Stela ana mbusu Nickson Boss wao alikua ofisini na aliwatazama kwa kupitia kideo kilicho unganishwa na Camera za ulinzi.
Nickson : "Mpenzi unajua nina mpango wa kuacha kazi hapa naona kama siwezi kwenda mbele yani nakwama bure."
Stela : "Unasema!?". Aliuliza akianza kukaa mbali na Nickson huku akianza kukunja sura.
Nickson : "Mpenzi nimekaa hapa miaka miwili lakin sioni kama kuna maendeleo. Na pia sioni umuhimu wangu".
Stela : "Kwani unakaa hapa!?".
Nickson : "Nalipwa lakini mshahara nilio anzia mwaka juzi ndo ninao mpaka leo."
Stela : "Sasa kinachokuwasha!?"
Nickson : "Hamna kinacho niwasha nataka nifike mbali sana katika tasnia yangu ya mambo ya Computer. Ikiwezekana nijiajiri."
Stela : "Hehehe ushaaanza na ujinga wako wa kujiajiri una hela ya kujiajiri we una matope ubongoni si ndio!?".
Nickson : "We unataka tuoane tukae nyumba ya kupanga mpaka lini!?"
Stela : "We nani kakwambia nataka kuolewa nikae nyumba ya kupanga!?."
Nickson : "Kwa hiyo mimi nifanyaje!?."
Stela : "Jiongeze! Mi sitaki mwanaume masikini nimetaaabika sana unioe unirusdishe kwenye umasikini eti nyumba za kupanga!?."
Nickson : "Sasa mimi nafanyaje na nkiendelea kukaa kwenye kampuni hii siendi popote."
Stela : "Mxxxxhewww."Stela alifyonza aka acha hata chai yake na akaondoka kwa hasira.
Wakati wote hayo yote yanafanyika Boss alikuwa ndo amefika na akawa anaona kila kitu kitu kwenye camera alizoweka!. Lakini bahati nzuri au mbaya aliona tu picha hakusikia sauti.Boss aliketi akatafakari bila kuamini alicho kiona akapanga mipango yake na hakutaka kusema kuwa ameona.
Basi ikafika muda wa ku funga ofisi Nickson akaelekea zake nyumbani moja kwa moja akakutana na Bertha.
Bertha :"Mambo Nickson pole na kazi."
Nickson : "Poa asante. Umeshindaje!?".
Bertha : "Salama tu."
Nickson : "Haya sawa ". Nickson akawa anaanza kuondoka kuelekea chumbani kwake.
Bertha : "Nickson!.."
Nickson : "Naaam.".
Bertha : "Leo una mpango wa kula nini usiku!?"
Nickson : "Sina uhakika kwanza nimechoka kujipikia sijui hata nitafanyaje."
Bertha : "Ahhhaaaa".
Nickson : "Kwa nini umeuliza?"
Bertha : "Nataka niende nikale vitu kama mihogo ya kukaanga na miguu ya kuku!. Nikipata na ka pilipili kidogo na chips kidogo mi na ridhika!."
Nickson : "Mhhh haina shida."
Bertha : "Usiseme hivyo bhana."
Nickson : "Sasa niseme aje jamani!?"
Bertha : "Mi nataka unisindikize afu bill mimi nitalipa."
Nickson : "Saa ngapi una enda!?".
Bertha : "Saa moja au mbili hivi."
Nickson : "Sawa ngoja nkaoge ni pumzike kidogo alafu nitakusindikiza angalua leo sipiki maaana nimechoka sana."
Bertha : "Haya sawa usichelewe sasa."
Ilipo fika mida ya saa mbili kasoro bertha na Nickson walitoka kwa pamoja na kuelekea kula kama walivyopanga na wakarudi wakitembea kwa karibu sana hii ikawa ni kawaida yao mara zingine hata Nickson ana msahau Stela japo kuwa Bertha sio Mpenzi wake yeye ana ufurahia ukaribu wake na Bertha.
Nickson anajiuliza huyu mwanamke kama huyu nitampata wapi sio kwa ukaribu huu. Lakini pia ni mwanamke ambaye hapendi makuu. Yeye chochote kidogo ana ridhika yani ana tamani Stela awe kama huyu lakini ndo hivyo!.
Itaendelea......
Comment yako na Reaction kama zote itakuwa safi sana!
Shukrani sana mkuu....japo umeipunguza alosto, usipotee sana.....fanya kutupia tupia nyingine leo kama ikiwezekana.
 
Jan 21, 2018
35
125
My Soulmate Kipande cha 10
#####Tulipoishia#####
Nickson alifika mlangoni baada ya kufungua akakuta ni yule mdada aliemtukana kisa mlango.
### Tuendelee ####
Nickson : "Unasema nini!?".
Bertha : "Kaka umeshindaje!?".
Nickson : "Salama! lakin unataka nini ongea chapu!."
Bertha : "Sasa kakaaaa".
Nickson : "Samahani nina jina langu naitwa Nickson."
Bertha : "Sawa Nicky".
Nickson : "Sorry ita jina langu kamili unaniitaje kwa kifupi mi sipendagi kama huna mda wa kumalizia sema mi nifunge mlango nifanye vyangu!."
Bertha : "Nickson sikiliza basi.."
Nickson : "Haya ongea ". Nickson anakumbuka alivyo semeshwa na Bertha kisa alivyo fungua mlango na uka mgonga bahati mbaya ana jua hapa lazima alipize kisasi.
Bertha : "Nimekuja kuomba msamaha Nickson sasa saivi wewe ni jirani sasa nitakaaaaje na mtu wakati hatupatani kisa tu stress zangu!?".
Nickson : "Ah wapi we dada stress wakati ndo tabia yako. Wa dada wengi mnakuaga na madharau mimi madharau sipendagi hata kidogo."
Bertha : "Nickson sikia mpaka mimi kuja na kuomba msamaha ni kwamba nimetambua kosa langu na nataka kujirekebisha."
Nickson : "Nakusikiliza."
Bertha : "Nickson naomba tueke utaofauti wetu pembeni na tuanze upya. Nisamehe kwa yote nliokukera."
Nickson : "Saw nimekusamehe hivyo ndo mtu anavyo takiwa kuwa jitahidi msamaria na utaishi vizuri."
Bertha : "Nashukuru kwa kunisamehe. Uwe na jioni njema Nickson."
Nickson : "Sawa haina shaka karibu sana huku mtaani kwetu."Wakati huo Bertha alikua amesha anza ku ondoka kuelekea chumbani kwake. Nickson akamsimamisha.
Nickson : "Dada umesema jina lako nani!?"
Bertha : "Hahaha ndo una kumbuka saivi. Naitwa Bertha."
Nickson : "Haya sawa nafurahi kusikia hivyo".
Bertha : "Haya kwa heri."
Wakati huo jirani mwingine wa Nickson alikua ndo anaingia kwenye nyumba hizi za kupangisha.
Nickson : "Niaje Dulla".
Dulla : "Ah ni poa mwana niaje!?"
Nickson :"Poa tu tuna enda na kasi na ari mpya.".Wakati huo Dulla anamsogelea Nickson.
Dulla : "Nakuona una winda babu!. Usha anza na Jirani mpya we jamaaa hatari wewe". Dulla alisema huku aki tabasamu kidogo.
Nickson : "Aaah wewe usiwaze hivyo haya ni mambo ya kawaida."
Dulla : "Aaaah wapi wewe! Yangu macho tutaona tu una cho panga!."
Nickson : "Haya mtu wangu ngoja niingie bhana ni kachakarike na ma msosi. Si unajua sisi tuliopo kivyetu vyetu hatuna msaaada!."
Dulla : "Ngoja na mimi nika lale!."
Nickson : "Poa poa mkuu!."
DUlla aliondoka kuelekea kwenye chumba chake na ndivyo siku ilivyomalizika.

Nayo miezi ikaendelea kusonga mbele urafiki wa Nickson ukapamba moto waka ivana na kuwa karibu zaidi. Hakuna ajuae Bertha yupo Arusha na ana urafiki wa karibu sana na Mwanaume mwingine japokuwa ni marafiki tu sio rahisi kuamini.
Ni asubuhi Nickson anaelekea ofisini mara akasikia akiongeleshwa.
Bertha : "Nickson njoo unywe chai rafiki yangu kabla hujaenda!."
Nickson : "Aaah ungeniambia mapema tayari nishakunywa!."
Bertha : "We jifanye tu hulagi kwa watu!."
Nickson : "Ushaaa anza zako rafiki yangu!."
Bertha : "Haya siku njema. Uwahi basi tupige stori."
Nickson akaondoka na kuondoka kwenda kazini. Aka fika mpaka jiko la ofisi kwa ajili ya kupata maji!. Akamkuta Stela ndo anaandaa chai. Akafunga mlango kwa nyuma yake aka muwahi stela kabla ya kugeuka akamfunga macho.
Stela : "Jamani Boss acha zako."
Nickson : "Unasemaje!?"
Stela : "Hahahaah mbona umeshtuka wewe si ndo Boss wa moyo wangu au unawaza nini mwaya!?".
Nickson : "Kweli mi ndo Boss!? "
Stela : "Ndio mwaya We nipelekeshe unavyotaka."
Nickson : "Haya ni busu mdomoni."
Stela : "Sawa boss nafanya unalotaka".Wakati Stela ana mbusu Nickson Boss wao alikua ofisini na aliwatazama kwa kupitia kideo kilicho unganishwa na Camera za ulinzi.
Nickson : "Mpenzi unajua nina mpango wa kuacha kazi hapa naona kama siwezi kwenda mbele yani nakwama bure."
Stela : "Unasema!?". Aliuliza akianza kukaa mbali na Nickson huku akianza kukunja sura.
Nickson : "Mpenzi nimekaa hapa miaka miwili lakin sioni kama kuna maendeleo. Na pia sioni umuhimu wangu".
Stela : "Kwani unakaa hapa!?".
Nickson : "Nalipwa lakini mshahara nilio anzia mwaka juzi ndo ninao mpaka leo."
Stela : "Sasa kinachokuwasha!?"
Nickson : "Hamna kinacho niwasha nataka nifike mbali sana katika tasnia yangu ya mambo ya Computer. Ikiwezekana nijiajiri."
Stela : "Hehehe ushaaanza na ujinga wako wa kujiajiri una hela ya kujiajiri we una matope ubongoni si ndio!?".
Nickson : "We unataka tuoane tukae nyumba ya kupanga mpaka lini!?"
Stela : "We nani kakwambia nataka kuolewa nikae nyumba ya kupanga!?."
Nickson : "Kwa hiyo mimi nifanyaje!?."
Stela : "Jiongeze! Mi sitaki mwanaume masikini nimetaaabika sana unioe unirusdishe kwenye umasikini eti nyumba za kupanga!?."
Nickson : "Sasa mimi nafanyaje na nkiendelea kukaa kwenye kampuni hii siendi popote."
Stela : "Mxxxxhewww."Stela alifyonza aka acha hata chai yake na akaondoka kwa hasira.
Wakati wote hayo yote yanafanyika Boss alikuwa ndo amefika na akawa anaona kila kitu kitu kwenye camera alizoweka!. Lakini bahati nzuri au mbaya aliona tu picha hakusikia sauti.Boss aliketi akatafakari bila kuamini alicho kiona akapanga mipango yake na hakutaka kusema kuwa ameona.
Basi ikafika muda wa ku funga ofisi Nickson akaelekea zake nyumbani moja kwa moja akakutana na Bertha.
Bertha :"Mambo Nickson pole na kazi."
Nickson : "Poa asante. Umeshindaje!?".
Bertha : "Salama tu."
Nickson : "Haya sawa ". Nickson akawa anaanza kuondoka kuelekea chumbani kwake.
Bertha : "Nickson!.."
Nickson : "Naaam.".
Bertha : "Leo una mpango wa kula nini usiku!?"
Nickson : "Sina uhakika kwanza nimechoka kujipikia sijui hata nitafanyaje."
Bertha : "Ahhhaaaa".
Nickson : "Kwa nini umeuliza?"
Bertha : "Nataka niende nikale vitu kama mihogo ya kukaanga na miguu ya kuku!. Nikipata na ka pilipili kidogo na chips kidogo mi na ridhika!."
Nickson : "Mhhh haina shida."
Bertha : "Usiseme hivyo bhana."
Nickson : "Sasa niseme aje jamani!?"
Bertha : "Mi nataka unisindikize afu bill mimi nitalipa."
Nickson : "Saa ngapi una enda!?".
Bertha : "Saa moja au mbili hivi."
Nickson : "Sawa ngoja nkaoge ni pumzike kidogo alafu nitakusindikiza angalua leo sipiki maaana nimechoka sana."
Bertha : "Haya sawa usichelewe sasa."
Ilipo fika mida ya saa mbili kasoro bertha na Nickson walitoka kwa pamoja na kuelekea kula kama walivyopanga na wakarudi wakitembea kwa karibu sana hii ikawa ni kawaida yao mara zingine hata Nickson ana msahau Stela japo kuwa Bertha sio Mpenzi wake yeye ana ufurahia ukaribu wake na Bertha.
Nickson anajiuliza huyu mwanamke kama huyu nitampata wapi sio kwa ukaribu huu. Lakini pia ni mwanamke ambaye hapendi makuu. Yeye chochote kidogo ana ridhika yani ana tamani Stela awe kama huyu lakini ndo hivyo!.
Itaendelea......
Comment yako na Reaction kama zote itakuwa safi sana!
Safi sana mkuu ,,tunasubiri next episode
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom