Simulizi: kisasi cha haki (13+)-sura 1

Simulizi: kisasi cha haki (13+)-sura 1

Niidondoshe lini?

  • Kila siku

    Votes: 1 100.0%
  • Wikiendi Tu

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    1

Babas Babas

New Member
Joined
Oct 12, 2026
Posts
2
Reaction score
1
Kisasi cha haki
Mtunzi: Mr Babas
Mawasiliano: +255 758 276 010 whatsapp

Sehemu ya Kwanza

Ilikua ni siku nzuri ya ijumaa suzi na rafiki yake getu walikua wakitoka chuo mida ya jioni kuelekea hostel walipokua njiani kuna gari aina ya harrier ya lecturer mmoja aitwae joseph tukisema tumuelezee alikua ni kijana mwenye miaka 28 mrefu wa nchi 5.9 na mweusi, gari hiyo ilikuja na kupaki kwa mbele kidogo na huyo lecturer alishusha kioo cha gari na kuwasalimia wanachuo hawa,

"jamani habari zenu" lecturer yule aliwasalimia,

"salama shikamoo:" getu aliitikia,

"marahaba vipi mnaenda wapi niwasogeze" lecturer alisema,

"asante si mbona tumefika tupo karibu tu hapo" getu aliitikia,

"aaah pandeni hamna shida" lecturer aliwaambia,

"shoga angu twende" getu alimwambia suzi,

"mmmh shoga unamuamini nini huyu" suzi alimuambia rafiki ake getu,

"aaah bhana ee we twende atatufanya nini"getu alisema huku akieleka kwenye gari,alifungua mlango na kuingia suzi nae akaona isiwe tabu akaingia siti ya nyuma na kutulia kimya,

"wewe mbona upo kimya sana vipi?" lecturer alisema,

"huyo hanaga maneno mengi" getu aliitikia, Safari ilienda mpaka katika hostel yao,

"hosteli ndiyo hii??" Lecturer aliuliza,

"ee ndio hapa hosteli kwetu" getu alijibu,

"aaaya sawa mshuke taratibu maana vidimbwi hivyo vinaweza kuwachafua" lecturer alisema,

"hamna shida tumepazoea asante" suzi alijibu huku akielekea hostel,

"samahani" lecturer alimsimamisha suzi,

"ndio" suzi alijibu,

"unaweza ukaniachia namba yako ya simu" lecturer alitoa ombi huku kijasho kikionekana kwa mbaali,

"hapana sina simu" suzi alijibu kisha kuingia hostel kwa mwendo wa haraka tofauti na mwanzo,lecturer aligeuza gari na kuendelea na safari yake.

"eeh bora tumepata lifti maana hili jua plus vumbi so powa" getu alisema,

"em niendee na mkoba wangu nataka niende chooni maana nilibanwa" suzi alimwambia getu,

"ahahhaaaha ndo mana ulikua ka bundi" getu aliitikia huku akicheka,getu akaonganisha mpaka chumba walichokua wakikaa na suzi maana hostel ilikua inavyoo vya jumla. Suzi alitoka chooni na kupitia chumba cha jirani kwa mashoga zake kuwasalimu na kuonganisha mpaka chumbani kwake,

"shoga hivi ulikua unamuona yule lecturer anavyokutazama kwenye kioo" getu alisema,

"nimemuona sana sema sikutaka mambo mengi mimi" suzi alijibu,

"kijana bado mbichi kabisa" getu alichombeza,

"unaanza sasa kwani me nnashida nae akileta shobo ahakikishe watu tunafaulu tu" suzi alisema kwa tabasamu huku akipunguza nguo kutokana na joto kali,stori ziliendelea na marafiki hawa wakazidi kufurahi chumbani mwao.

Kesho yake asubuhi getu akiwa anapiga mswaki gorofa ya pili alifatwa na kijana wa mlemle hostel mwao,

"mambo vipi mrembo" karlosy alimsalimia getu,

"yamekua hayo, poa vipi?" getu alijibu huku akiendelea kupiga mswaki,

"safi tu enhe vipi sasa ombi langu?" karlosy aliuliza,

"bado nakufikiria sana kaka angu" getu alijibu,

"kunifikiria mpaka leo jamani wiki ya tatu inakatika hii" karlosy anaongea kwa hisia,

"ahahaa kuwa mvumilivu" getu anaongea kwa tabasamu,punde si punde anakuja suzi na ndoo iliyobeba nguo za kuanikwa,

"karlosy vipi" suzi alimuuliza karlosy,

"safi tu za asubuhi" karlosy alijibu,

"nzuri!! naona asubuhi asubuhi tu" suzi anaongea huku akimtazama getu,

"nini mbona wanitazama mie" getu alimuuliza suzi,

"eeeh bibi wewe umenionaje si na wewe unanitazama au? suzi anamjibu getu kwa utani na lugha za ishara zikiendelea hapo,

"bhana usimzunguuushe kaka wa watu wakati wewe mwenyewe umekufa umeoza" suzi aliongea huku akianika nguo zake,getu kwa aibu alikimbia na kuelekea chumbani mwake,karlosy alivyoona hivyo kuwa na yeye anapendwa alifurahi na kumfuata suzi "asante shem lake",

"aaah ndo unizingatie na mimi sasa" suzi alisema,

"aaah hilo limeisha shemeji" karlosy anaondoka anadunda kama snoopdog.suzi aliendelea kuanika nguo zake bila mawazo yoyote yale lakini akiwa juu aliona gari ya lecturer joseph ikielekea chuo,

"getu! getu! getu!" Suzi alikua anamuita rafiki ake,

"abee mbona hivyo shoo" getu anaitika,

"si nimemuona yule lecturer kapita na gari nikasema tungekua na kipindi asubuhi hii tungepata lift" suzi anamwambia getu,

"sema yule anaonekana ashavutiwa na wewe" getu alisema,

"mmmh shoga malecturer hawa utakuta ana mke huko ila huku unafanywa mchepuko mwisho wa siku niangukie pabaya mie,hata sitaki" suzi alisema,

"ungempa hata namba basi uwe unamfuatilia kichinichini" getu alisema,

"hivi unawajua wanaume vizuri wewe,yani mwanaume akitaka kitu atakuficha mpaka akipate ndo utaanza kuona siri zao" suzi anamwambia getu huku akirudi huwani kuendelea kufua,

"kwahiyo na mimi karlosy atakua ananidanganya sio" getu alimuuliza suzi,

"aaah sidhani ila huyu akikuficha kitu nampiga ngumi za tumbo mpaka ajutie" suzi anamuambia getu kwa utani,

Ilipofika mida ya saa kumi jioni suzi na getu walijiandaa kwenda chuo kujisomea,walitoka mdogo mdogo kuelekea chuo

"hivi getu malengo yako wewe ya kimaisha yako je?" Suzi alimuuliza getu,

"kwanini unauliza hivyo?" Getu akarudisha swali kwa suzi

"hamna nataka nijue tu rafiki angu" suzi alisema,

"anha me malengo yangu ni kumaliza chuo salama then nipate bwana mwenye ela niolewe" getu alisema kwa kujidai,

"khaa kwahiyo huyu kaka wa watu?" suzi aliuliza kwa mshangao,

"nani karlosy?"

"eee karlosy kwani una nani mwingine ambaye hujawai niambia"

"atafute ela tu binti wa kihaya sina shida na mtu mie" getu alisema,

"yani wewe ela zitakupeleka pabaya nakuambia" suzi alimwambia getu huku wakikaribia kufika chuoni,

"pabaya wameenda wangapi na mimi niwe wangapi?" getu aliuliza,

"shauri yako me yangu macho" suzi alisema,

"usisahau na masikio pia" getu alijibu na wote wakaanza kucheka,

Walipokaribia getini getu alisikia akiitwa nyuma yake alipogeuka alikua ni karlosy akiwakimbilia ghafla gari ilikuja na kumgonga karlosy kisha kuondoka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom