HADITHI: Mtoto wa Pastor

HADITHI: Mtoto wa Pastor

SEHEMU YA 43


["Unasema Chinedu mwanangu Asu anaaa...?!"]
aliuliza tena Pastor George baada ya kukaa kwa dakika nzima akitetemeka midomo pindi alipokuwa anafikiria cha kujibu na kujikuta anauliza mithili ya kwamba alivyoambiwa awali hakusikia.
[["Mwanao Asunta kipindi tunafanya ile mudawa tulikosea kitu moja ambayo hatukukijua nacho ni Mimba. Na tatizo itakuja ule upendo aliokuwa nao Asunta sambamba na mudawa tuliyoifanyia kazi zote zimeingia tumboni kwa kiumbe ambaye ana damu ya mutu yule tumemrogea Asunta amsahau na sasa muunganiko wa yule mutoto ndio unamrudishia fahamu mwanao na kujiuliza maswali, na atavyozidi kuiona sura ya yule kijana ndivyo habari itapozidi kutumwa kwenye memory za mutoto ambae nae atamsababishia mamaake kumuonesha vile vyote vilivyojificha juu ya yule mtu aliyemfikiria, na hapo hadi ulichokifanya kitakuwa wazi kwenye maono ya mwanao."]]
maneno ya Chinedu kwa njia ya simu yalizidi kukichanganya kichwa cha Pastor George na kubaki na bumbuwazi kusikia kumbe ujauzito aliokuwa nao mwanae ni wa yule adui yake mkubwa manywele?
Na si kwamba ni ya Fredy kama alivyodhani...!
["Yaani Mimba ya yule mshenzi hasidi wa maendeleo ya mwanangu?"]
aliuliza kwa ghabhabu Pastor George mithili ya kwamba alikuwa haongei kwa simu.
[["Usifoke George ndio hivyo ilivyo, sasa unachotakiwa wewe kuamua jinsi ya kufanya ili Asu asipate muda wa kumfikiria au kumuona iwe kwenye picha au live"]]
["Huyu afe tuu, Fanya mpango Chinedu ua kabisa manywele hili"]
[["hahahahahaaa George kumuua huyu ni kumuua na mwanao pia kwani endapo akisikia habari za kufariki kwake akiwa bado hajajifungua jua nstuko ataoupata yule mtoto utamfanya aruke mfurulizo tumboni na kumkosesha hewa na nguvu mwanao na lazima afe tu"]]
jibu la Chinedu lilizidi kumchanganya George asijue sasa wamfanyeje Dullah kwani ni kweli atapofariki lazima Asu atasikia na yote imechochewa na umaarufu ule wa Dullah ulioanza kuonekana siku baada ya siku akiwa nchini Kenya.
["Chinedu, naomba nisaidie jinsi ya kufanyaaaa"]
[["sawa George, Hapa nitachofanya ni kumtengeneza VUNJESHA ambae ataenda kumshughulikia katika kazi yake onayosababisha kusikiwa na Asunta muda mwingi na ataenda kuugulia kwao hadi Asu atapojifungua sasa hapo ndipo tunamaliza muchezooo hahahaha']]
ushauri wa Chinedu uliungwa mkono moja kwa moja na Pastor George na baada ya kufika ule muafaka waliagana na kukata simu.
"Mwana izaya huyuuu, Dunga dunga... Kamdunga mwanangu Mimba ya pili??!!"
alijiongelea kwa uchungu Pastor George huku akisimama kujiandaa kutoka mule chumbani.

* * * *
NAIROBI - KENYA
________________

Furaha mara dufu ilirejea katika familia ya Dullah mara baada ya Ilham kurejewa na akili zake za kawaida mara aliporuhusiwa kule kwa mganga na kuhamia kwenye nyumba ile nzuri waliyokuwa wanaishi ambayo ilikodiwa na Tusker fc kwa niaba ya star wao Dullah.
Ilham aliona kama ndoto maisha yale ambapo kila siku walikuwa wanakula vyakula vizuri, wanavaa vizuri na mambo kwenda raha mustarehe.

Sala na maombi ya mama Dullah yalianza kujibu kwa kuonesha dariri za wazi wazi kwamba Ilham anampenda sana Roja na Roja anampenda sana Ilham ila tatizo kila mtu alikuwa anahofia kumuanza mwenzake kutokana na heshima iliyokuwepo baina yao.
Roja alimuheshimu sana mama Dullah na kutokana na urafiki wake mkubwa na Dullah ilifika wakati alijifikiria kama Ilham anamchukulia sawa na kakaake tu, kumbe hata Ilham nae alikuwa na hisia hizo na kuogopa kumtamkia Roja akichukulia kutokana na urafiki wao na kakaake Dullah basi hata na yeye Roja anamchukulia kama mdogo ake tu.
Na hata walivyokuwa wanapiga story mbalimbali na kucheka pamoja kila mtu alikuwa na hisia zake moyoni mwake lakini kwa utu uzima wa mama Dullah alibaini kuwa kuna kitu akilini mwao hasa kwa mwanae Ilham.

Baada ya mwezi mwengine kuisha wakati wakiwa mapomziko ambapo iliwabidi Dullah na Roja kusafiri hadi Tanzania mara baada ya kupigiwa upatu na Clouds fm, hatimae wote waliitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya Taifa kwenye michuano ya kukata tiketi kucheza kombe la Dunia.
Ilikuwa ni habari njema kabisa kwao na ya furaha kwa kuingia kwenye historia ya kuitwa timu ya Taifa jambo ambalo kila mchezaji alilitamani kwani anapoonesha kiwango bora na timu ya Taifa anakuwa amelitangaza taifa lake.

"Hili ni tukio kubwa sana Dullah ona mwenyewe ratiba ilivyowekwa daah! mechi ya kwanza wiki mbili zijazo harafu mzee tunapanda dege hadi Nigeria?"
aliongea Roja mara baada ya kila mchezaji aliyeitwa kupewa kijitabu kidogo cha ratiba nzima ya mechi za makundi kuingia katika mtoano wa kuzipata timu za taifa 5 ambazo zitaiwakilisha Afrika katika michuano ile mikubwa kabisa katika ngazi ya mpira wa miguu.
Timu ya Tanzania maarufu kama Taifa Starz wao walieka Kambi Bagamoyo mkoani Pwani wakijiandaa na safari ambayo ilikuwa inawakutanisha na timu ya Nigeria iliyokuwa kundi moja na wao.

Mbali ya kuwa Dullah na Roja walikuwa na umaarufu lakini bado umaarufu wao haukusambaa kwa wananchi wote wapenda michezo zaidi ya wale wachache waliobahatika kuwaona uwanjani.
Hata ile siku ya siku ilipofika na timu ya Taifa ya Tanzania ilipoondoka kwenda jijini Lagos kukutana na moja ya timu ngumu ya Nigeria na watu walijua kuwa Tanzania wanachokifata kule ni kipigo tu kutokana na kuachwa mbali katika viwango vya ubora wa kisoka kwa mujibu wa Fifa.
Lakini manaojua wanasema mpira ni dakika tisini ndio zinazoamua, na kwa mara ya kwanza Dullah pamoja na Roja waliweza kuchanganyika na watu maarufu waliowajua kabloa toka wanacheza Tandale na humo D alukutana na John beki kisiki wa Simba mbae aliijua vizuri habari ya Dullah mara baada ya kuangushwa kwa vyenga zaidi ya mara mbili.
***********
Maneno ya Mbwiga na Shafii kuhusu uwezo wa ajabu wa Dullah kupitia Clouds fm radio ndio yaliwahamasisha watu wengi kukaa kwenye mabanda ya video siku hiyo kuangalia mtanange mkali ambao walijua kuwa timu yao kushinda si rahisi kutokana na kuzidiwa kila idara tangia kipindi cha kwanza hadi kinamalizika walikuwa washafungwa goli moja kwa bila.

Kipindi cha pili kilianza huku Tanzania safari hii wakijitahidi kushambulia ili wapate goli lakini hadi dakika ya 80 mambo yalizidi kuwa magumu kutengeneza nafasi ya ushindi japo kipa wa Tanzania alifanya jitihada nyingi sana hadi wanigeria walishangaa kwa jinsi alivyokuwa anaokoa magoli ya wazi kabisa.
Kocha alikata shauri na kuamua kumuingiza Rastaman Dullah kwa mara ya kwanza ili akajaribu na yeye bahati yake baada ya mshambuliaji tegemeo wa Tanzania kuuniana hapo ndipo jicho la kila mtanzania lilipoganda kwenye tv kumuangalia kwa umakini huyo mchezaji aliyesifiwa wiki nzima kupitia clouds baada ya kuitwa na kocha wa timu ya Taifa kwa mara ya kwanza.

Na kweli Dulla baada ya kuingia ile ilipofika dakika ya 87 alifanya vitu vya ajabu sana pindi timu yao ilipokuwa inashambuliwa na mpira ulipookolewa na kuja kwake akiwa zaidi ya mita sitini na gori la timu pinzani, alianza kukimbia na mpira na kuwachambua kama karanga wachezaji sita wa Nigeria waliokuwa mbele yake huku uwanja mzima ukiwa umesimama hadi Rais wa Nigeria ambae alikuwa mgeni rasmi siku hiyo ya mechi nae alisimama na kustaajabu na si kwa uwezo ule pakee aliouonesha Dullah... Bali ni baada ya kuwachenga wachezaji sita na alipotokea goli kipa nae alimpiga chenga ya maudhi na hatimae kubaki yeye na goli lakini chaajabu na kushangaza Dullah alipotaka kuupiga ule mpira alisita na kusimama ghafra mbele ya macho ya watu zaidi ya elfu arobaini walimshuhudia Rasta wa Tanzania akishindwa kuipatia point muhimu timu yake ya Taifa na kuuganda kwa sekunde kadhaa na kuanguka mzima mzima bila kusukumwa wala kuguswa na yeyote
Kipa wa Nigeria aliwahi na kuukimbilia mpira uliokuwa unaelekea gorini taratibu na kuudaka kabla wachezaji wengine pamoja na madaktari wa timu ya Tanzania hawajakimbilia uwanjani pindi refa alipopuliza kipenga cha kuusimamisha mchezo kutokana na kudondoka ghafra kwa Dullah.
"Aaaaaagggggg... Rooojaaaaaa Nakufaaaa aaaagggg"
alipiga kelele Dullah pindi madaktari na wachezaji wenzake walipofika pale alipodondokea kutaka kujua nini kimemkumbuka lakini hawakuweza kwa kuona jeraha kwa macho wala uvimbe zaidi ya kuhisi kuwa mguu ule wa kushoto ambao ndio alikuwa anautumia sana Dullah kuuchezea mpira, ulikuwa unamletea maumivu makali ukiwa umekakamaa huku ukivibrate mithili ya simu mbovu ya kichina.
Kadri madaktari walivyomshika ule mguu kuangalia harakaharaka tatizo ili wampatie huduma ya kwanza ndivyo Dullah alivyozidi kupiga kelele huku akimwita Roja ambae alikuwa hajaingizwa kabisa kucheza siku hiyo lakini pindi alipomuona rafiki ake akidondoka ghafra yeye nae alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kufika pale alipodondoka Dullah huku akiwa na wasiwasi mkubwa.

Kutokana na sheria za michezo ilibidi Dullah abebwe kwenye machera ili akatibiwe vizuri nje ya uwanja kupisha kipute kiendelee na hapo ndipo kocha wa Tanzania alipomuamuru Roja achukue nafasi ya rafiki ake aliyekuwa anatolewa huku akipiga sana kelele za maumivu makali hadi kila mchezaji na aliyekuwepo pale uwanjani walimuonea huruma na wengine walijikuta wakitokwa machozi wakiwa hawaelewi nini kimemkumba mchezaji yule aliyeingia muda mfupi tu na kuonesha vitu hadimu sana kwa kuwachachafya wachezaji saba tegemeo wa Nigeria lakini yakamkuta mazito yasiyojulikana yalipotokea..!! hii iliwashangaza wengi sana na si kwa wale tu waliokuwa uwanjani bali hadi waliokuwa wanafatilia mtinange ule kupitia tv hususani wananchi wa Tanzania walijikuta wanaghadhibika sana na kuwalaani wanaigeria wakiami kuwa ule ulikuwa uchawi tu walioutega gorini si kweli kabisa eti nyonga imestuka kama ambavyo wachambuzi wa Spersport walivyokuwa wanasema muda mfupi baada ya kuwa wanalirudia rudia lile tukio kwa karibu na kiminyato jinsi alivyoanguka Dullah.

Jopo la madaktari wa Nigeria waliungana na wenzao wa Tanzania ili kumsaidia Dullah pale nje na kumfunga ule mguu huku wakimpulizia dawa mbalimbali za kutuliza maumivu na kulegeza nyonga ambapo ajabu hakukuonekana hata dariri kama alikuwa anapata nafuu zaidi ya kulalamika kuwa maumivu yanazidi na hapo ndipo walipoamua kumpakia kwenye gari ya wagonjwa iliyokuwa pale uwanjani kwaajili ya dharula na haraka safari ya kumpeleka hospitali ilianza ili akachunguzwe kitaalam zaidi ule mguu wake umepatwa na nini..(?)

* * * *
WIKI MBILI KABLA - NIGERIA
__________________________

Pastor George kwa mara nyengine tena alifunga safari ya kwenda kukutana na Chinedu kwa ajili ya kumaliza suala lile waliloongea juu ya Dullah na Asunta na hii ilimchochea mno kwenda kule kule Nigeria mara baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari juu ya uteuzi wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania baada ya kuongezwa majina mapya kwa mara ya kwanza na kulisikia jina la adui wa moyo wake Dullah likiwa ni miongoni mwa majina ya wachezaji walioongezwa kwa mara ya kwanza.

Aliwasiliana na Chinedu kama kawaida baada ya kufika walielekea kule kwenye makazi ya Chinedu na kuanza mambo yao kwenye chumba kile cha kichawi kama ilivyo desturi yao na Pastor kuanza kunuia anachotaka afanywe Dullah ili iwe njia rahisi ya kutoonekana machoni mwa mwanae hadi ajifungue na ndipo wammalize kabisa.
"Wakuu, nataka huyu kijana mwenye manywele pindi atapokuja na wenzake kwaajili ya kucheza huo mpira hapa kwenye ardhi hii yenu tukufu basi mumtie adabu kwa kumpa adhabu itayomfanya imlaze kitandani ashindwe kutembea hadi mwanangu Asunta atapojifungua ndipo mumpeleke kabisa kuzimu...."
aliongea Pastor George huku akiwa kashika kile kimdori cha maajabu na baada ya kumaliza nia yake ile alimkabidhi kile kimdori Chinedu ambae nae alifanya yake kimaajabu ndipo moshi ukaanza kufuka na kutengeneza tena kifungu kama cha tv pale juu ya chumba na mara ilisikika sauti iliyokuwa inaongea lugha ambayo Pastor hakuielewa zaidi ya Chinedu ambae alikuwa anamtafsiria na kisha moshi ule ukatoweka kwa kurudi moja kwa moja kwenye kile kimdori.
"Hahahahaaaa Mutume Joji wewe ni mutu ya bahati sanaaa, hahaha aa Habari iko muzuri kabisaaaaaa, misiku si mingi akifika hapa Lagosi jua hatorudi kama alivyokujaaa. Huyu ambae metoka zugumza hapa ni Jini mukubwaaaa sanaaaaaaaaaa saaaaanaaaa, naye atamfanyia muchezo mudogo sana hahahahaaaaaa"
aliongea kwa kujiamini Chinedu na kufurahi pamoja na Pastor George ambae habari zile ziliukuna sawia moyo wake na kuisubiri hiyo siku kwa hamu kubwa sana.

*******

Siku ya mechi ilifika ambapo kwa upande wa Pastor George alikuwa tayari amerejea nyumbani Tanzania akindelea kujitangaza na kujichukulia umaarufu mkubwa kuwa yeye ni nabii mpya mwenye upako mkubwa baada ya kutokewa na Yesu usiku na kum bariki ili kupitia yeye awasaidie na binaadam wengine wenye shida.
Hakuwa na aibu wala soni Pastor George pindi awapo jukwaani akijinadi kuwa yeye ni miongoni mwa wabora katika kizazi cha mwisho mwisho.
Na baada ya mizunguko siku ile ambayo alikuwa anaisubiri kwa hamu sana usiku wake majira ya saa moja ilipotimu alikaa sebuleni na watoto wake wale wawili wa kiume waliokuwa wapo likizo baada ya kuwa muda mwingi wanakuwa boarding shuleni.
Hata watoto wake wenyewe walishangaa siku hiyo kuona baba yao akiwa na 'mzuka' (shauku) sana kuangalia mpira siku hiyo baina ya Nigeria na Tanzania huku wakijua fika kuwa baba yao hakuwa mpenzi kabisa na mpira hata ukimwambia awataje wachezaji watano wa timu ya taifa alikua hawajui lakini hawakujua siku hiyo kulikoni yeye kuwa mtu wa kwanza kufatilia matangazo yale ya mpira tokea saa moja kasoro usiku wakati mechi husika ilikuwa ni saa moja na nusu?
Hata mkewe siku hiyo aliona maajabu na kubaki anacheka.
"Hee! mume wangu naona na wewe leo unaonesha uzalendo?"
"hahaaa si unajua sisi watakatifu macho yetu yanaweza kuwa neema muda mwengine kuwatazama vijana wa nyumbani wanaolitangaza taifa."
alijinasibu Pastor George lakini ukweli ulibaki moyoni mwake juu ya kile kilichomsukuma kuiangalie ile Mechi.

Na kweli baada ya Dullah n=kuingia na kufanya vitu vya ajabu vilivyowafurahisha wanae kwa jinsi alivyokuwa anawachambua wachezaji wa Nigeria lakini mara aliposhindwa kufunga na kuanguka wote walistuka kusikia ukelele wa furaha uliomtoka ghafra Pastor George pale sebuleni.
"Weeeeweeeeeeeeeeeeeeee.."




ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 44


Watoto walimshangaa baba yao kipi kilichomfurahisha wakati mchezaji wa timu yao ya Taifa ameanguka uwanjani na kushindwa hata kufunga akionesha amepatwa na tatizo kubwa na si masikhara...?
"Khaaaaa...!! Kumbe hajafunga?? Imekuaje tenaaa !!"
alizuga Pastor George kwa kujifanya kumbe alitoa ule ukelele wa shangwe akidhani Dullah amefunga baada ya kumchenga kipa ila amefanya mbwembwe (utani) ya kujiangusha kama aina ya kushangilia tuu.
kauli ya Pastor George iliwafanya wanae waangue kicheko wakijua baba yao kumbe alikuwa na 'mzuka' (shauku) wa goli bila kuangalia mpira kiumakini unavyoenda.
Lakini ukweli ulibaki moyoni mwake na furaha ya ajabu iliyokuwa ndani yake laiti ndio ingetoka kila mtu aione vile alivyojisikia pindi Dullah alipoanguka na alivyokuwa anaoneshwa akiugulia maumivu kwa sauti kabisa basi hata watoto wake wangemchukia baba yao kwa moyo wa kinyama aliokuwa nao.
Lakini tofauti hakuna binaadamu anayeweza kuutazama moyo wa mwenzake na kugundua kilichomo kwa macho tu, zaidi wengi walitumia kuutazama uso na uso wa Pastor George siku hiyo mara baada ya kujifanya ndio amejua kumbe yule mchezaji kaumia, ulikuwa unaonesha huzuni kubwa pengine kuliko hata nyuso za watoto wake.
"Eeee, bwana hebu muokoe yule kijana wetu kikombe cha umauti kisimkute angali yu bado na nguvu zakeee.."
aliomba kwa sauti palepale Pastor George kipindi ilipooneshwa Ambulance iliyom beba Dullah ikitoka pale uwanjani kumkimbiza hospitalini, lakini moyoni mwake alichoomba Dullah asije kunyanyuka tena bali ateseke mpaka mwanae huko ulaya ajifungue ndipo afariki.

* * * *
NAIROBI - KENYA
_________________

Wakiwa na furaha Ilham na mamaake walikuwa wanaiangalia ile mechi na walifurahi zaidi mara baada ya kumuona Dullah akiingia uwanjani lakini furaha yao ilidumu kwa dakika saba tu kabla ya kugeuka huzuni na kukosa kabisa hamu ya kuendelea kuangalia ile mechi wakiwa wamejaa wasiwasi mkubwa moyoni wakijiuliza, nini tena kimempata Dullah..?
"mama, ile sio hali ya kawaida kabisa iliyompata kaka Dullah"
"Yaani mwanangu, mi namkabidhi Mungu Inshaallah yeye ndie mwenye kupanga na kuamua. Kama ni mkono wa mtu basi naamini Mungu atamfichua tu na kunilipia kwa kile alichomtegea mwananguu"
aliongea kwa uchungu mama Ilham na kusimama huku nae machozi yakimtoka mara baada ya kumuona mwanae akilia kwa sauti kuonesha ni maumivu makubwa aliyokuwa anajisikia muda ule.

***********

Upande wa Askofu ambae nae alikuwa anaifatilia ile mechi ya Tanzania na Nigeriakwa njia ya tv alishangaa mno kilichompata mchezaji wa Tanzania hasa vile alivyokuwa analalamika.
("Mh! hii si kawaida kabisa... Mungu wangu..!")
alitaharuki moyoni Askofu kwa jinsi alivyokuwa anatazama kilichokuwa kinatokea na kujikuta moyo ukimuuma kama ni yeye ndie aliyeumia au ni mwanae kabisa hasa mara baada ya kuona mwanaume akishindwa kujikaza na kulia kwa sauti mbele ya umati alibaini kuwa maumivu aliyoyahisi yalikuwa makali mno.

Askofu Mbukinyo alikuwa na imani ya kweli kabisa na alimuamini Mungu.
Wakati akiwa na masikitiko makubwa pindi alipokuwa anamuangalia yule kijana Dullah akikimbizwa hospitali kwa gari ile ya wagonjwa huku akijiuliza kulikoni kikubwa kilichomfanya hadi kawa katika hali ile..? Fikra zake na maswali aliyokuwa anajiuliza huku moyo ukimuuma kwa kile akionacho alijikuta macho kama yanaingia kiza kwa usingizi ambao ulianza kumkamata ghafra na kujikuta anasinzia pale pale alipokaa kwenye sofa akifatilia mtinange ule na katikati ya usingizi ule wa ghafra mara alianza kuota na yeye yuko uwanjani ambapo alimuona yule kijana akicheza huku akikimbiza mpira lakini kulikuwa na mchezaji mwengine aliyekuwa na mapembe kichwani huku akiwa na uso wa kutisha sana alikuwa anamkimbilia pindi alipokuwa anawachenga wale wengine na ajabu mara alipomaliza kumchenga goli kipa yule mchezaji mwengine mwenye mapembe na uso wa kutisha aliruka na kwenda kumgonga mguu pindi Dullah alipotaka kupiga mpira uingie wavuni na ajabu alipomgonga tu ule mguu palepale yule mchezaji waajabu alianza kubadilika na kuingia kabisa kwenye mguu wa Dullah hadi akapotelea kabisa pindi Dullah alipoanguka.
"HEEEEEEEEEEEE.....!!!!"
Alikurupuka ghafra usingizini Askofu na kuishangaa ile ndoto aliyoota muda mfupi na alipoangali mpira ulikuwa ndo umeisha muda mfupi lakini alishangaa kuona full match matokeo ni 1-1 huku upande wa Tanzania alishangaa jina Roja 91 likionesha ndie mfungaji na dakika aliyofunga tokea Tanzania japo hakuliona hilo goli lenyewe lilivyofungwa lakini moyoni aliamini kuwa kile kilichomkuta yule mchezaji wa Tanzania pale ni nguvu za giza tu na si vyenginevyo.

* * * *
LAGOS - NIGERIA
________________

Baada ya Dullah kukimbizwa hospitali na nafsi yake kuchukuliwa na Roja ambae alitumia dakika chache sana kucheza lakini alifanya kitu kikubwa sana kwa Taifa Starz mara baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira mzuri wa klosi uliopigwa na Mrisho Ngasa na kwenda kutinga moja kwa moja wavuni na kuisawazishia Tanzania hali iliyowafanya Wanigeria wote kubaki nyuso chini mbele ya Rais wao kutokana na kushindwa kukusanya point tatu muhimu kwenye uwanja wa nyumbani tena wakicheza na timu ambayo kila mtu alijua ni 'vibonde' (siojua) ambao walistahiri kupigwa nyingi lakini mwisho wa siku mambo yakaenda Kombo kabisa.

Kuna kitu kimoja alikifanya Roja kilichowashangaza watu na kuwakera hasa mashabiki wa Nigeria kwa vile alivyoshangilia goli alilofunga kwani, mara tu Roja alipohakikisha ule mpira aliousukuma kwa kichwa kikali ukitinga wavuni.... alichokifanya yeye alikimbia mpaka eneo lile alipoangukia Dullah na na kusimama ghafra mara alianza kupiga ukelele wa maumivu huku akijidondosha na kuushika mguu wake akigaragara sekunde zilezile mara baada ya wachezaji wenzake kumfikia alinyanyuka na kuunyoosha mguu wake mithili kwamba kuna kitu kilikuwa ndani yake kisha akafanya kama amekikamata hiko kitu na kukimbilia upande wa mashabiki wa Nigeria na kuwatupia.
Watu walimzomea kwa kujua kuwa amewatukana kupitia mchezaji mwenzake aliyeumia na kuwaambia kuwa wao ni wachawi walieka kitu kibaya pale alipoanguka mwenzake.

Mechi iliisha na kila mchezaji alitamani kujua maendeleo ya Dullah na majibu yalikuja usiku wake kuwa hakuonekana tatizo lolote mwilini mwake na hata ile hali ya kupiga kelele ilikoma muda mfupi baada ya kupelekwa hospitali na ndipo Roja alipompigia simu Ilham kumuelekeza ampoze na mama kuwa Dullah anaendelea vizuri ule ulikuwa ni msuri tuu ulikaza.
Lakini hata kesho yake aliporuhusiwa si kwamba aliruhusiwa kwa kuweza kutembea mwenyewe bali alibebwa na kiti maalum alichonunuliwa kule kule kutokana na kushindwa kabisa walau kuukanyagia ule mguu wake wa kushoto na kwa bahati kocha wa Tusker alipigiwa simu na Askofu Mbukinyo na kumpa maelekezo aongee na uongozi wa timu ya Taifa Tanzania wamchukue yule mchezaji wao akafanyiwe tiba maalum Kenya.
Suala lile halikuwa gumu sana ukizingatia mechi nyengine ilikuwa itachezwa mwezi ujao na ndipo ndege iliyowabeba Taifa Starz ilipotua kwanza Kenya kwa dharula maalum ya kuwashusha wachezaji wale wawili walioonesha kitu kikubwa sana kwa Taifa mbali ya kuwa ndio ilikuwa mechi yao ya kwanza na walicheza dakika chache mno.
Askofu alitoa gari maalum kwaajili ya kwenda kumpokea Roja na Dullah ambae hali yake ilibadilika ghafra akiwa ndani ya ndege baada ya mguu kuzidi kuvimba huku kila mtu akishangaa lakini safari hii alikuwa hapigi kelele kama ilivyokuwa mwanzo na hata walivyofika ambapo Roja ndie aliyekuwa anamsukuma kwa njia ya kiti maalum cha matairi walichokinunua kulekule Nigeria.. Alihakikisha anakuwa nae makini rafiki ake mpaka walipoingia garini mara baada ya kuwakuta kina Ilham wakiwa wanawasubiri ambapo mama Dullah punde alipomuona mwanae akiwa hawezi hata kutembea anakokotwa na guu limevimba kupita maelezo alijikuta analia sana muda wote wakiwa kwenye gari iliyotolewa na Mkurugenzi wa kampuni iliyowadhamini timu ya Tusker.
Lakini Roja alishangaa mno baada ya kufika kwa Askofu ambako ndiko walisema kuna tiba m badala ya kilichomkuta Dullah ambae toka amenyamaza hakunyanyua mdomo wake kusema chochote tangia alivyoumia.
Kilichomshangaza Roja si wingi wa watu ambao walikuwa ni waumini bali ni uwepo wa mtu aliyejua wazi ni adui wa Dullah nae ni Pastor George.

***********

Kumbe Askofu mara baada ya kuota ile ndoto na kugundua kuwa lile tatizo halikuwa la kawaida aliwasiliana na Pastor George aliyeamini Mungu amempa upako na kumuomba kuwa pindi watapokuwa wanarudi kina Dullah nae awepo nyumbani kwake kwani alitaka wamsaidie yule kijana ambae alijitoa sana na kuipa mafanikio club aliyokuwa anaidhamini.
Hivyo aliwaandaa hadi waumini wa kanisa lao siku hiyo wakusanyike kwa pamoja nyumbani kwake kwa niaba ya maombezi maalum tena kutoka kwa yule mchungaji mwenye upako mkubwa aliyepewa utume na unabii.
Askofu hakujua undani wa Pastor, nae Pastor hakutaka kujikweza alijiapiza kuitumia fulsa ya kwenda Kenya akijifanya kumuombea Dullah huku akiwa na lake lengine moyoni.
("Lazima nimuongezee dozi niliyofundishwa na Chinedu... hahaha Lazima nikamtie na uchizi kabisaa")
aliwaza Pastor pindi alipoiona gari iliyoelekea uwanja wa Ndege ikurudi mule mjengoni.

"Mama mi sidhani kama panafaa hapa.... Jamani eeh baba Askofu mbona umetufanyia hivi..? sisi waislaam bwana mtu anaponywa kwa imani."
alilalama Roja mara baada ya kuona wanapokelewa na waumini wa dini tofauti na wao kwaajili ya kufanyiwa maombi rafiki ake.
Lakini alichokuwa anakikanusha Roja si kwamba aliuchukia sana Ukristo la hasha japo
bali alimchukia sana Pastor George na aliamini fika ni mchawi wala hana upako wowote bali anatumia nguvu za giza ila alishindwa jinsi gani aseme pale watu wamuelewe hivyo aliona ni heri atumie njia ile huenda ingesaidia waachwe na wampeleke hata kwenye msikiti Dullah akasomewe kuliko pale kwa Askofu kutokana na uwepo wa Pastor George aliamini kunaweza kuzuka matatizo zaidi badala ya kusuruhisha.

"Hapana mwanangu Roja sisi tuombee uzima tuu"
aliongea mama Dullah wakati huo wote ajabu bado Dullah alikuwa hawezi kuzungumza chochote zaidi ya kutazama tu na ndipo Roja alipokosa nguvu baada ya mama kuekea mkazo kuwa anachotaka mwanae apone tu haangalii hapa kanisani au msikitini.
Mama Dullah hakujua kama yule Pastor ndie baba wa Asunta japo Pastor George yeye alijua kila kitu na alianza kuisugua ile pete yake huku akinuia maneno ya kichawi moyoni mwake aliyofundishwa na Chinedu pindi atapotaka kumroga mtu akili kwa kutumia ile pete iliyojaa nguvu za kichawi toka kwa majini wabaya.
Waumini walianza kuimba nyimbo za kumsifu mungu taratibu pindi Dullah alipokuwa anashushwa kwenye gari wakiwemo wachezaji wa Tusker fc na zaidi ya yote hadi timu ya Clouds media ikiongozwa na Mbwiga nao walikuwepo pale kwa Askofu baada ya kupata taarifa mapema kuwa Dullah mchezaji aliyepata matatizo ya ajabu alipokuwa uwanjani Nigeria atashukia Kenya ilipo familia yake na club yake kwa matibabu zaidi na ndipo kina Mbwiga nao waliposafiri hadi Kenya kujua kila kinachojiri zaidi kutaka kumuhoji Dullah mwenyewe.

"''TEEEEENDAAA MUUUUJIIZAAAAA (TENDA BWANA)...
TEEEEENDAAA MUUUJIZAAA (USIACHE)...
USIACHE BWANAA... MWAKA UUUUUPITE.
BILA KUTEEEEENDA MUUUJIZAAA..."''

Waumini walizidi kuimba kipindi hiko sasa Pastor George alikuwa anajiandaa kuwaonesha watu muujiza wake kwanza amfanye Dullah aseme kumbe alichotaka kumrusha kabisa akili.
Watu walikuwa wengi sana hadi wananchi na wapenzi wa Tusker fc walienda kuuona muujiza utaondeka kwa Messi wao wa Afrika, Mliberia wa Tandale na Zidane wa Tanga bwana Dullah Kombo.
Shughuli nzima ilifanyika kwenye eneo kubwa la Garden lililokuwa ndani ya fensi ya jumba lile la Askofu.
Wakati Pastor akiwa anaanza mambo yake huku akisugua sugua pete yake akimzunguka Dullah ambae alikuwa akama mtu aliyepigwa na bumbuwazi na moyoni mwake alikuwa anasali kwani hata yeye aliona pale kuna balaa wala hakumuamini yule mzee mchungaji kwa kuwa alijua ni adui yake kamwe hawezi kuwa na maombi ya kweli juu yake.
Ila kwa bahati mbaya au nzuri mama Ilham na Ilham mwenyewe hawakujua kama yule Pastor ndie babaake Asu.

"Leo ndio muujiza wa kihistoria utafanyika mbele ya macho ya kila mmoja aliyekuwa eneo hili katika Jiiiiiinaa la Yesu."
alianza Pastor kwa mbwembwe huku akimzunguka Dullah pale kwenye kiti cha matairi alichowekwa.
"Leo hii kijana umekutana na Nguvu kutoka........."
alijikuta anasita Pastor mara baada ya kuhisi kama kitu kinamkaba kooni wakati huo Roja alikuwa pemeni amefumba macho akisoma baadhi ya aya fupi za Dur'aan alizofundishwa madrasa miaka hiyo zile za kumlaani shetani.
Wakati mama Dullah na Ilham nao wkiomba wanavyojua wao halikadhalika baba Askofu nae akiwa na Biblia mkononi alizama kabisa ndani ya imani akimuomba Mungu muujiza utendeke kwa yule kijana.
Karibu kila mtu alijijengea imani ya kweli pale kwa kile kinachoendelea kasoro mtu mmoja tu ambae alikuwa ndie wamemuamini akiendeesha yale maombi kumbe akiwa na lengo tofauti kabisa.

'''fumbuuuuaaaaaa maaaachooooo...fumbuuuuaaaaaaa'''
ilikuwa ni sauti ya ajabu ilipenya masikioni mwa Askofu na pia hadi kwa Roja ambao wote kama walivyo waumini wengine waliokuwa pale walikuwa wamefumba macho. Lakini sauti hii ya ajabu ambayo Askofu awali hakuizingatia lakini Roja aliwahi kufumbua macho yake na mara alishangaa kuona pale kwenye mkobo wa Pastor aliokuwa amemuekea kichwani Dullah kulikuwa na nyika mkubwa sana.
"HAPANAAAA"
Alipiga kelele zilizowastua na kuwafanya watu wote kufumbua macho kushangaa pindi Roja alipokimbia na kumsukuma Pastor George aliyeanguka kama gunia.
"Huyuu sio Mchungaaaajiii ni Mchawiiiii jamaaaani Msimuaminiii."
maneno ya Roja ambae alikuwa kamkumbatia rafiki ake pale kwenye kiti yaliuchoma sana moyo wa Pastor George na kunuia kumtupia kombola la kumuua kabisa kupitia jini aliyekuwamo kwenye ile pete wakati huo watu wote walistaajabu huku waumini wenye hasira kali alikuwa wanamkimbilia Roja kwa nia ya kumpiga kwa kitendo chake cha kumsukuma Pastor lakini kumbe kile alichokuwa anakiona Roja hata Askofu nae alikiona na ndipo dakika zilezile kwa hasira Pastor aliponyanyuka kutaka kumnyooshea mkono Roja ndipo Askofu Mbukinyo alipojistukia naye anapata ujasiri wa ajabu baada ya kumnyooshea mkono George.
"Nakuamuru Shetani Shindwaaaaaa"
alitoa tamko kwa imani kabisa Askofu na mara alishangaa kwenye mikono yake vimtoka vitu kama radi na kwenda kumpiga Pastor George na kumrusha mbali kabisa huku watu wote wakishangaa na kutoamini kile kilichokuwa kinatokeaa.
"ALLAAAAAAAAAAAHUUU AKBAAAAAR.."
Roja nae alitoa tamko la Kumtakasa na kumsifu Mwenyezi Mungu baada ya kushuhudia Pastor akipigwa na Radi ya ajabu kutoka kwa Askofu na papo hapo baada ya Roja kutamka maneno yenye tafsiri kuwa Mungu ni Mkubwa ndipo watu wote walishangaa kuona wingu la ajabu likitanda maeneo yale na kuleta kiza cha ghafra kilichowafanya kila mtu aogope na kuanza kulia kwa hofu na mara ilisikika sauti kubwa wasiyojua wapi imetokea ikisema.
"MUNGU NI MMOJA, HAKUZAA WALA HAKUZALIWA. OLE WAO WANAEKIUKA NA KUMSHIRIKISHA NA VITU VYENGINE VYA UPUUZI NA KULICHAFUA JINA LAKE. HAKIKA ADHABU YA MUNGU NI KALI NA INAUMIZA NA ITAWAPATA WOTE WATU WABAYA WANAOTANGAZA KAZI YA SHETANI KWA KIVULI CHA MUNGU....."
Sauti hii ilipokata tu mara ulizuka mwanga mkali sana uliowafanya watu wote kuinamisha nyuso zao chini kwa hofu kubwa mno.

* * * *
LAGOS - NIGERIA
__________________

Akiwa ndani ya chumba kile cha kichawi pamoja na mgeni wake mwengine akimpatia dawa maalum za kichawi kama ilivyo kawaida yake Chinedu, alishangaa kuona vitu vinaanza kugongana gongana mule ndani lakini alipotezea kutostuka ili asimuogopeshe mteja wake.

Lakini kadri dakika zilivyoenda mbele ndivyo mtetemo ulivyozidi na safari hii havikuwa vyombo tu bali hadiwao wenyewe walianza kutetemeshwa na kurushwa rushwa huku yele mteja akiwa amechanganyikiwa zaidi kwani mwanzoni alijikaza akidhani ni mbwembwe tu za Chinedu lakini alipoona hadi Chinedu nae akichanganywa na kuvurugwa na ule mtetemo ilibidi aanze kupiga kelele za kuhitaji msaada.
"Londeee mbondeeee wewe uko nakuja na mudaaawaaa ganiiiii???"
alilalama Chinedu vile alivyokuwa sasa anaelea juu juu samba na viru vyote vilivyokuwemo mule ndani na kwa bahati mbaya matereo ya kile chumba kilivyokuwa ilikuwa haiwezekani sauti kutoka nje hata sebuleni.
"wooooooo maaaweeeeeee"
"Wooooooooooo"
Vilio vilipishana baina ya Chinedu ambae jicho lilimtoka, hofu ilitaanda mwili mzima nakutamani apewe walau dakika moja atubie lakini muda huo haukuwepo zaidi kilizuka kivulavumbi cha mzunguko na kuzidi kuwazungusha kwa kasi huku wakipigizwa vibaya vibaya kwenye kuta za kile chumba wao na vitu vyote vilivyokuwemo kuanzia makolokolo ya kurogea watu na kadhalikavilivurugwa pamoja nao.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA MWISHO (45)

Upepo ule ulivuma kwa mzunguko mkubwa zaid na zaidi na hatimae katika hali ya kushangaza ghafra likatokea tetemeko kubwa na mara aldhi ya kile chumba ikapasuka na kuanza kutitia wakati na upepo nao ulianz kutulia na kuwafanya kina Chinedu waliokuwa hoi bin taaban, Mahututi kabisa na kudondoka kwenye ule mpasuka pindi upepo ulipotulia lakini bado haikuwa salama kwao kwani chumbakizima kiliporomoka na kupigizwa matofari ya vichwa kabla ya kufukiwa kabisa na vifusi vya zege pindi nyumba nzima ilipotitia na kubomoka kimaajabu.
Na huo ndio ukawa mwisho wa Chinedu na tambo zake zote za ujuaji na uchawi wa majini mabaya.

* * * * *
LONDON - UINGEREZA
_____________________

Wakati ule Afrika yakiendelea yale huku kwa kina Fredy mambo nayo yalikuwa si mambo mara baada ya Asunta kuzidiwa ghafra baada ya mtoto kuruka kupita kawaida tokea siku ile ya Mechi kule Nigeria mara tu alipopata taarifa kutoak kwa Fredy kuwa yule mchezaji wao aliyetokea club ya Tusker mwenye rasta ameanguka ghafra kwenye mechi.
Tokea Asu apate habari ile mtoto alikuwa hatulii tumboni na kumsababishia maumivu makali mno hali iliyompelekea kulazwa katika hospitali ya Newghton London mpaka siku ile Dullah aliyokuwa anaombewa na babaake Asu kule Kenya kwa upande wa Asu hali ilizidi kuwa mbaya kule hospitali baada ya mtoto kuzidi kupanda juu na kuwafanya madaktari waamue kumfanyia upasuaji wa haraka ili kuwez kuokoa maisha ya mama kama ikiwezekana na mtoto pia.

Fredy alichanganyikiwa kwa hali ya mke wake ambae alikuwa amebakiza miezi miwili tu kujifungua kwani mimba ya Asu ilikuwa tayari ni ya miezi saba na nusu.
Alijaribu Fredy kupiga simu nyumbani kwao Nairobi lakini bahati mbaya simu zote ziliishia kuita bila kupokelewa na hapo hakuwa na jinsi zaidi ya kukaa akiombea upasuaji wa mkewe uende salama salimini aliombea vivyo hivyo Fredy na kubaki pale kwenye eneo la kusubiri ambapo baada ya masaa kadhaa alikuja Daktari akiwa mwenye tabasam zito na kumwambia Fredy..
"Hongera, mkeo ana mtoto wa Kiume ila kwa sasa tumemuhifadhi kwenye vyumba maalum vya joto na mamaake nae anaendelea vizuri usiwaze kabisa."
Maneno haya ya Dokta yalimpa nguvu sana Fredy na kumshukuru Mungu huku akimuomba amsaidie mkewe arudi kwenye hali ya kawaida lakini mara alishangaa kusikia anakuja Daktari mwengine akimwita yule wa kwanza kutokea kule kwenye oparation huku akiwa kama amechanganyikiwa.
Alinyanyuka kwa taharuki Fredy kutaka kujua tatizo na hapo alifanikiwa kusikia kwa mbali kuwa Asu amepandwa na kifafa kile cha uzazi na hali imekuwa mbaya maradufu.

* * * *
NAIROBI - KENYA
___________________

Mwanga ule uliokuwa mkali mno ulianza kumchoma Pastor George ilihali wengine walikuwa hawachomwi na walishangaa na kustushwa na maneno ya Pastor muda ule ambao wote walikuwa wameinama kwa hofu.
"Nasemaaaa, Jamaaaaniiii mimi sijawahi aaaahh!!! Sijawahi mimi kutokewa naaaa Yesuuu sijahiiiiiiiii... Yaaalaaaaaaaa Nimmeeeemrogaaa Mwanaanguuu Asuntaa ili asimpendeee asimpendeeee huuuuuuu asimpendee huyyuuu kijaaaanaaaa... Aaaaghhhh... Nimemrogaaa kweeeeliiii Nigeriaa miiimiiii aaaaaaa.. yalaaaa..Nasemaa nasemaaa. Nimeroga kwa sababuu siiikupeeendaa diiinii yakeeee iiiingeeenikoseeeshaa pesaaaaa pesaa yaa kuaminiwaaa kaamaaa Mchungaaji wa kweliii aaauuuuuuuuuuu,. Nimerogaa akiliina aaaaa ufahamuu wa mwananguu ampendee mtoto wa Askoofuuuuu aaayaaaaaaaaaaauuuuuuuuuuu"
Basi Pastor aliendelea kubwabwaja huku akichojoa nguo alizokuwa anaona zinazidi kumchoma moto Pastor George na kuzidi kuushangaza umati na mara tu mwanga ulipopotea watu wote waliinua vichwa na kushangaa kumuona Dullah akiwa amesimama mwenyewe sambamba na Roja huku nae akijishangaa na walipoangalia mguu wa Dullah ulikuwa umenywea kabisaaa na kwa Upande wa Pastor walishangaa alipokuwa anacheza na kuruka ruka huku akiwa kama alivyozaliwa baada ya nguo zote kuzivua na kuzitupa mwenyewe kipindi alipokuwa anaunguzwa.

Watu wengine walitimua mbio baada ya utulivu kuona ni mauzauza yalikuwa yanatokea na kila mtu hakuamini wakionacho na hapo hata kina Mbwiga wenyewe nao walitafuta pa kwenda baada ya kuona hadi yule waliyemtumainia nae kumbe alikuwa na biashara zake wala hakuwa na upako wowote kama walivyodhani na alipomaliza kubwabwaja nae alitoka mbio akiwa vile vile uchi wa mnyama na kutokomea.
"Haaaaaa....."
Watu waliobaki walitaharuki na wale waliokuwa na imani kali waliongozwa na Askofu kuimba nyimbo za kumsifu Mungu na Kumshukuru kwa yote huku Roja akifurahi mno baada ya kuona rafiki yake akiwa vizuri kama zamani hana hata dariri za maumivu yoyote, mguu upo sawa kabisa tena hadi yeye mwenyewe alishangaa.
"Unajisikiaje sasa?"
"Yaaani nilikuwa najiona ndo nazaliwa upya lakini ajabu mama aliyekuwa ananizaa ni Asu..!"
"hahahahahahaaa Dullaaaaaaah yamekwisha tenaaa hayooo, Asu yuko London, mama na Ilham nataka niwajulishe kuwa Asu ni msichana mwenye mapenzi ya kweli kabisa, wala hakuwafanyia visa kwa makusudi.. bali ni uchawi aliofanyiwa na babaake ili asiweze kuishi na Dullah kivyovyote.. Iwapo Dullah atarudiana na Asu amini sasa hakuna tatizo lolote"
aliongea maneno haya Roja yaliyoitikiwa na wote kukubali asemacho.
"Roja wewe ni rafiki wa kipekee sana kwangu, sina cha kukulipa wala sijawahi kukufanyia wema kama ulionifanyia na kunionesha siku zote... Asunta wangu umesema yuko London? Nitampataje tenaaaaa...!?"
aliuliza Dullah akiwa na taharuki kubwa lakini Roja alicheka sana na kujifunua tishert aliyovaa ambayo ndani yake kulikuwa na vesti iliyoandikwa 'LOAD TO LONDON' ambayo haikujulikana lini aliyachapisha yale maneno japo kumbe safari hii alikuwa nazo nyingi sana na alikuwa anangoja amfanyie suprise rafikiake.
"Road to London..?!!"
aliuliza Dullah
"Yeeah, na ndio kifuatacho sasa, tiketi yako iko uwanjani inakusubiri nyavuni, club bingwa Afrika ndio visa yako usisahau Kombe la Dunia ndio ndege ya uhakika itayokufikisha.. hahahaha"
maneno ya Roja yaliwafanya wote wafurahi sana japo Ilham na mama Dullah walikuwa hawajaelewa vizuri.. lakini mara Ilham machozi yalianza kumtoka na kusogea alipo Roja huku wote wakimshangaa.
"Rojaa ROJA.... Jamani Mnisamehe mama na kaka Dullah....... aaah Nimeshindwa kuvumilia kabisa.. NAKUPENDA SANA ROJAA"
Ilikuwa ni sauti ya Ilham iliyomfanya Dullah abaki amestaajabu pindi akimshuhudia dadaake akikumbatiana kwa nguvu na Roja na kuanza kupeana mabusu motomoto hadhalani na alipogeuka kumuangalia mamaake alishangaa kumuona amenyoosha mikono juu akimshukuru Mungu kwa kuijibu dua yake ya muda mrefu.

* * * *
((MIAKA MITANO BAADAE))
ZURICH - USWISI
* * *
==================

Ilikuwa ni siku ya Kihistoria duniani kwa macho ya wanamichezo wote hususani Afrika na furaha zaidi iliangukia Tanzania pindi walipokuwa wanamuangalia mchezaji aliyekuja kuwa maarufu kuliko wote Afrika na kwa mwaka huo aliongoza mafanikio ya kisoka kuliko wote duniani baada ya muda mfupi uliopita kutangazwa kuwa ndie mchezaji bora wa Dunia mwaka huo.
Kwaajili yake alipewa dakika 15 ya kuongea na dunia juu ya tuzo yake ile baada ya kuibwaga miamba ya soka alioingia nao katika tatu bora nao ni Leonel Messi wa Argentina sambamba na Christiano Ronaldo wa Ureno huku tuzo kwa mara ya kwanza ikiangukia kwa Dullah Kombo wa Tanzania ikiwa ni kwa mara ya pili kwa mchezaji toka bara la Afrika kutwaa tuzo ile baada ya miaka mingi kupita tokea achukue George Whea wa Liberia.
Aliendelea na hotuba yake ile Dullah iliyokuwa inawatoa machozi karibu robo tatu ya wanamichezo waliokuwa wanafatilia zile tuzo...

....''''
"... Basi huo ndio ukweli jamani, kama alivyonishauri rafiki yangu Roja ambae sasa ni shemeji yangu aliyekuja kumuoa dadaangu Ilham baadae kuwa mambo sasa Load to London. Hali ile ilinifanya nijitume sana tena sana kila siku nikiwa na ndoto ya kusajiliwa ulaya hususani London lakini yote ili niweze kukutana na Asunta wangu ambae sikujua kuwa kipindi chote nahangaika na kujituma kumbe yeye alikuwa anateseka hospitalini baada ya kupata strock iliyosababisha na kifafa cha uzazi alichokipata siku aliyokuwa amejifungua kwa njia ya upasuaji kule London.
huenda ningebaki kucheza Kenya ningezipata hizi habari lakini Load to London illivyoanza kampeni yake msimu ule ule kwenye ligi ya mabingwa Afrika nilipata bahati ya kujiunga na Keizer Chiefs ya South Afrika ambayo mimi na shemeji ya Roja lakini nayo sikupata muda mwingi wa kuichezea mara baada ya kucheza mechi ya kirafiki na Celtic ya ulaya ambao walinisajili moja kwa moja kwa kuweka rekodi kwa Keizer kuwa mchezaji wao wa kwanza kuuzwa pesa nyingi nami kwa mara ya kwanza nikashangaa kuona nasaini mkataba utaoniwezesha kulipwa kwa wiki zaidi ya milioni tisini kwa pesa za Kitanzania na hapo nikahamia na mama yangu Ulaya tukiwaacha Ilham na Roja pale South waendelee na maisha yao mapya baada ya kuoana muda si mrefu.
Sikujua kumbe kipindi nahamia Celtic ikiwa imepita miaka miwili na nusu na ndipo Asu wangu alipofariki tena habari kutoka kwa Fredy na madaktari zilisema kuwa alizidiwa kutokana na furaha aliyokuwa nayo siku hiyo alipokuwa anaangalia tv iliyokuwa inatangaza habari zangu za kusajiliwa Celtic na kuwa mchezaji wa kwanza mtanzania mwenye thamani kubwa.
'Aaaaaagh.. Asu wangu kweli ulinipenda yaani hadi umekufa kwa furaha ya mafanikio yangu?!'

Basi kama kawaida nilijituma siku zote ujumbe niliuandika kwenye nguo ya ndani ya tisheti niliyovaa mchezo alionifundisha rafiki angu Roja.
Na katika kombe la Dunia mwaka huo kama alivyotabiri Roja na kweli 'Road to London' ilitiki nikiwa bado kwenye michuano ya Kombe la Dunia baada ya Celtic kukubaliana na Chelsea fc ya London kukamilisha uhamisho wangu ambapo wakala wangu aliponijuza nilikubali na nikafurahi mno japo timu yetu ya Taifa ilitolewa katika hatua ya kumi na sita bora lakini nilifurahi kufika London kwani nilijua kuwa sasa nitakutana na Asunta wangu uwanjani kama ilivyokuwa miaka ile Tandale lakini loool.
Sikuamini siku ya kwanza tu natua London na kupokewa kifalme na mashabiki wengi lakini nilistushwa na shabiki mmoja aliyenipa kikaratasi kilichokuwa na maneno 'ASUNTA GEORGE - MTOTO WA PASTOR' sambamba na namba za mawasiliano na hapo ndipo baada ya kusaini na kutambulishwa nilisaidiwa na rafiki angu mpya niliyemfananisha na Roja nae ni Edin Hazard kwenda kukutana na huyo mwanaume niliyeongea nae kwenye simu ambapo awali nilijua angekuwa Asunta na ndipo nilikutana na Fredy aliyenihadithia kila kitu huku mikononi mwake akiwa amemshika mtoto mdogo aliyefanana sana na mimi hata Hazard alikiri hilo.
Nililia sana baada ya kujua yote yale daaaaaaaaaah.
Na hii ndio sababu toka nimejiunga na Chelsea hadi hii leo style yangu ya ushangiliaji ni ile mnayoona kila nikifunga nawaonesha maneno
'R.I.P ASU' tokea nafunga goli la kwanza nikiwa na Chelsea hadi msimu ulioisha niliponyakua viatu viwili vya ufungaji bora wa England na Ulaya.
Mpaka sasa sijamuona mwanamke wa kuchukua nafasi ya Asu moyoni mwangu. Sina mpango huo labda kama itatokea huko mbele sijui.
'Asu ameondoka lakini bado imebaki kumbukumbu kubwa sana na historia isiyokuja kusahaulika kwao na kwetu'
Niliyajua mengi baada ya kukutana na Fredy alinijuza kuwa mama Asu amekuwa Mlokole na sasa ana imani kali kabisa juu ya Mungu.
Lakini Pastor George bado yuko hai ila amekuwa Kichaa maarufu sana Afrika hususani Nairobi na Tanzania anatembea uchi na kula vilivyooza huku akilala majalalani.
Shemeji yangu Roja na dadaangu Ilham leo wako hapa lakini makazi yao ni Paris Ufaransa anakochezea Roja sasa katika club ya PSG.
Mimi na mamaangu bado tupo London na sina mpango wa kuhama Chelsea kwani safari yangu kisoka imetokana na mapenzi yangu kwa mtoto wa Pastor Asunta. Hivyo kama safari yake kimaisha imeishia London acha nami safari yangu kisoka iishie London.
Naota siku moja nicheze tena na Shemeji yangu Roja.
Na hii Tuzo ya leo ni Ahsante kwa woooote waliofanikisha safari yangu ya kimpira lakini tuzo hii haitakuwa yao wala yangu hii tuzo ni ya.......
MTOTO WA PASTOR."
''''

Alimaliza kuongea Dullah ambae pia alikuwa mmiliki wa club ya Tandale fc ya Tanzania na alijenga kituo kikubwa cha kufundishia mpira Muheza pale kijijini kwao kulipokuwa na ghorofa moja kubwa la kisasa alilojenga karibu na nyumba ya udongo ambayo alikataza isibomolewe na hata alipowahi kurudi kule kijijini kwao kabla hajaungana na wenzake kwenda kwenye michuano ya kombe la dunia, yeye alilala kwenye kile kile kijumba cha nyasi japo sasa alikuwa anakusanya zaidi ya tsh milioni 850 kwa wiki.
Mbwiga nae maisha yalikuwa mazuri mno mara baada ya kuunganishiwa na Dullah kupata kazi katika kituo cha SKY SPORT huko Ulaya.

Alishuka jukwaani Dullah huku machozi yakimtoka na hapo watu wote walisimama na kumpigia makofi sambamba na mamaake mzazi aliyekuwa amesimama na mtoto wa kiume aliyekuwa na umri wa miaka mitano ambae nae kichwani alikuwa amesokotwa rasta ndogo alimkimbilia Dullah huku waandishi wa habari wakimpiga picha pindi Dullah alipokuwa anashuka pale jukwaani na kukumbatiana na yule mtoto ambae alivaa jezi na nyuma yake iliandikwa maneno 'DULLAH Jr'
Na huyo alikuwa ni mtoto wa Dullah aliyezaa na Asu.

* MWISHO *

CONTACTS
FB: Prince Naahjum Alsina
INSTA: Prince Naahjum Alsina
WhatsApp: 0652691819
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom