HADITHI: Mtoto wa Pastor

HADITHI: Mtoto wa Pastor

SEHEMU YA 10



Lakini kipindi wakiwa wanatembea kuelekea stendi tangia pale mlango wa geto la Dullah, kulikuwa na kijana mmoja aliyeshika digital kamera ndogo akiwa kajibana kwenye kona moja ya uchochoro na akawa anawapiga picha kinyemela pasi na wao kujua hadi pale Asunta anapanda kwenye gari yake na kuondoka.

Dullah akiwa mwenye furaha wakati anarudi kuelekea getto kwake mara alishikwa bega kwa nyuma na alipogeuka alikutana na sura ya mtu asiyemfahamu.
"samahani kaka mi mgeni maeneo haya naitwa Sam naomba nikuulize samahani lakini eti njia inayotojea Tandale hospitali ni ipi hapa?"
aliuliza yule kijana.
"Nyoosha hii moja kwa moja hadi ukipita soko mbelembele kidogo ndo utakuta hospitali."
"haya poa, nashukuru ndugu yangu samahani kwa kukusumbua hivi unaitwa nani?"
"D"
alijibu kifupi Dullah huku akiondoka pasi na kujua mtu aliyekuwa anaongea nae ni nani na laiti angejua huenda angeangusha hata kasheshe (ugomvi/timbwili).
Dullah aliendelea na zake huku yule kijana nae akaendelea na safari yake ya uongoa na baada ya hatua chache alimtazama Dullah na kutikisa kichwa kumsikitikia baada ya hapo aliingia kwenye duka moja ambapo kumbe alipaki pikipiki yake kubwa aina ya Honda na kuiwaha nae kutimka zake maeneo yale.
Hakuwa mwengine yule kijana bali ni yule yule aliyekuwa anawapiga picha za mnato yeye na Asu pasi na wao wenyewe kujua.

* * * * *
((WIKI MOJA KABLA))-MASAKI
................................

Baada ya kurudi kutoka katika kuhubiri neno la Mungu tena safari hii alirejea akiwa na mgeni mkubwa ambae ni Askofu mkuu wa Kenya aliyeamua kuongozana na Pastor George kuja kutazama anapoishi na maendeleo yote ya shughuli za ibada na uchamungu ili kuzidi kudumisha urafiki wao wa kimwili na kiroho na akiwa nyumbani Pastor alibaini ukosefu wa furaha aliokuwa nao binti ake kipenzi Asunta.
Alijaribu kutafuta chanzo cha Asu kukosa furaha na haikuwa kawaida na safari zote kumkuta katika hali ile ndipo Pastor George alimpeleleza sana mkewe kwa maswali ya hapa na pale juu ya mtoto wao kukosa furaha.
"mh! baba Asu labda kutokana na kumzuia kwangu kuwa asiende mazoezini wala asitoke nyumbani mpaka urudi."
"He! kwanini sasa uliamua hivyo na sio kawaida yako, kuna tukio lolote baya alifanya?"
"Hapana mme wangu ila nilikuwa na hofu nae tangia siku ile alipoacha kwenda mazoezini na kwenda sehemu anazozijua yeye, sasa afadhali babaake ukiwepo utajua jinsi ya kumtafuta kuliko mimi mama tu."
majibu ya mama Asu Pastor aliyaelewa lakini kidogo upande mmoja alibaini lazima itakuwa Asunta alirudia abia yake ya kuchelewa nyumbani tu, na ndipo safari hii aliamua kutengeneza plani ambayo hakumshilikisha mtu yeyote kati yao zaidi ya kijana mmoja aliyekuwa anaitwa Samson ambae alikuwa mmoja wa waumini wake pale Kanisani.

Siku hiyo alimwita Sam pembeni baada ya ibada ya jumapili kuisha.
"Ewe kondoo wa bwana ulie mbele yangu."
"Ndio baba mchungaji nakusikiliza."
"Bwana amenionesha katika maono kuwa nikuteue wewe katika shughuli maalum unayopaswa kuifanya kwa siri kubwa pasi na mtu mwengine kujua zaidi yetu na bwana. je uko tayari.?"
"Niko tayari baba ila ningependa kujua shughuli gani hiyo."
"Sam, roho mtakatifu amesema nami katika maono kuwa wewe ni kijana hodari sana nami nakutuma kazi moja ya kumpeleleza binti angu kwa siri hususani kwenye safari zake nje ya nyumbani nataka uwe unamfatilia hasa nyakati za asubuhi kuanzia kesho anapokwenda mazoezini na ataporudi hakikisha uwe unampiga picha kila tukio ama sehemu anayopitia ambayo iko tofauti. je utaweza?"
"sawa baba niko tayari.. Nitaweza."
"Basi vizuri sana Sam, chukua hii namba zungumza na huyu mtu mwambie wewe ndie kijana uliyeelekezwa na Pastor uende ukaichukue hiyo pikipiki aina ya Honda. Nakuahidi Sam endapo utafanikisha vizuri zoezi hili basi hiyo pikipiki itakuwa ya kwako moja kwa moja. Neema ya bwana iwe juu yako."
"Asante sana babaa eeemen."
"basi sawa nataka ujue kuanzia kesho utapoiona ile benzi yangu mpya basi ujue huyo ni Asuna na unapaswa kuifatilia."
baada ya kumaliza maongezi na Sam Pastor alifanya ibada fupi palepale na kuachana na Sam na ndipo jioni ya siku hiyo alipoongea na mwanae na kumruhusu kuanzia kesho aanze kwenda mazoezini.
"Najua mwanangu jinsi gani umekosa furaha toka mamaako akuzuie kwenda mazoezini, nami nabatilisha kauli hiyo kuanzia leo nahitaji furaha ya mwanangu irejee mahali pake na kuanzia kesho mama utaanza kwenda kwenye mazoezi na ratiba zako zote zitakuwa wazi pia chukua funguo hizi za ile Benzi yangu kwani gari yako sasa itatumika kwenye shughuli ndogo ndogo tu za kumpeleka house girl sokoni sipendi mwanangu utembelee gari yenye matatizo."
aliongea Pastor na Asunta alifurahi mno moyoni mwake na kujua sasa atapata nafasi ya kukutana tena na Dullah bila kujua nini kinachoendelea nyuma ya Pazia.

* * * * *

Baada ya kurudi nyumbani Asunta huku akiwa mwenye mawazo kidogo lakini alijilazimisha kuonekana mtu mwenye furaha aliingia ndani na kulala huku fikra zake zote zikiwa juu ya Dullah vipi atakubali kubadili dini ili iwe njia rahisi ya kuwa nae.
Ilipotimu majira ya jioni Pastor alirejea akiwa na baba Askofu na walipokuwa sebureni wakiendelea na maongezi yao ndipo Pastor alipoiita familia yake kwa maongezi maalum.
Asunta alistuka baada ya kusikia kuna kikao tena mbele ya babaaskofu lakini alipata amani baada ya kumuona babaake akiwa ni mtu mwenye tabasamu muda wote na ndipo moyoni Asu alijua kuwa si kikao kilichomuhusu yeye kwenye makosa yake zidi ya Dullah kwani awali alihisi huenda babaake kagundua kitu.
"Mama Asunta hii ni habari njema kutoka kwa baba Askofu juu ya maendeleo ya binti yetu Asunta na katika msingi wake wa hapo baadae. Natumani hii habari ninayoisema hivi sasa itapokelewa kwa furaha na kila mmoja wetu kama jinsi ilivyotufurahisha sisi wenyewe, Habari yenyewe ni hivi, tunajua kuwa zimebaki siku mbili tu baba Askofu itapaswa arejee Nairobi sasa katika safari yake imetokea bahati naweza kusema ni bwana mwenyewe ndie amaemua kuwa baba Askofu aondoke na mwanetu Asunta kwenda kuanza masomo maalum ya kisayansi na kiroho katika chuo maalum jijini Nairobi...."
"BABAA!!"
Almanusura Asunta azimie kwa taarifa hizi na kujikuta anamkatisha babaake kwa kumwita ghafra huku akiwa ametahayuri hadi baba Askofu alishangaa.

"Vipi tena Asunta mwanangu mbona unatustua mama."
aliongea Pastor George na kumgutusha Asunta ambae alidhani alipayuka moyoni mwake tu kumbe alitoa sauti iliyomstua kila mtu.
"Babaa.. Baba Askofu Siamini kwa kweli nashukuru sana kwa nafasi hii nzuri ya kipekee lakini.."
"Lakini nini tena Asunta mwananguu!"
alimkatisha tena Pastor George na Asunta kubaki kimya akishindwa kuelezea sababu yake iliyomfanya atie 'lakini' katika maneno yake.
"Baba Askofu kama unavyoona mwenyewe na jinsi nilivyokwambia kuwa habari hizi tutapomwambia Asunta mwanangu kwa jinsi ninavyomjua anavyopenda elimu ya kisayansi na mazingira ya kiroho aliyokulia lazima furaha yake itapitiliza na hatoamini hahahahaaaa Ubarikiwe sana mwanangu Asunta"
aliongezea Pastor George maneno yaliyozidi kumchoma na kumkata maini Asunta na ilibidi atabasamu tu japo moyoni mwake alikuwa anaumia na alihisi huenda ile ni mbinu mbadala aliyoamua kuitumia babaake ili kuzidi kumtenganisha na kipenzi chake Dullah ambae alishamwambia kuwa hataki kulisikia jina kama hilo tena.
"ha ha ha Neema ya bwana izidi kuing'arisha nyumba hii Pastor George."
"Ameeen baba Askofu."
"Lakini binti ako niliona kama bado alitaka kuzungumza.! Eti Asunta umefurahishwa na habari hii mpaka katika moyo wako?"
aliuliza baba Askofu swali ambalo lilimfanya Asunta achelewe sekunde kadhaa kulijibu baada ya kutokea vita vikali baina ya moyo wake na akili zake. Akili zilimtuma akubali kuwa amefurahi ili atunze heshima ya babaake na maneno yake yazidi kuaminiwa na Askofu lakini moyo ulimkatalia na kumwambia aongee ukweli tu kuwa hajafurahishwa ili aeke abaki na uaminifu wake mbele ya Dullah.
"Asunta mwanangu baba Askofu si anakuuliza wewe?"
alidakia mamaake na kumstua tena Asunta
"Eeeh.. eeh ndio baba Askofu nimefurahishwa, nimefurahishwa sana baba Askofu Nimefurahi kwa kweli Mungu akubariki sana baba."
aliamua kuzilidhisha akili zake Asunta huku akiuchoma sindano ya maumivu moyo wake lakini hakuwa na jinsi yote yale aliyafanya kwa lengo la kulinda heshima ya wazazi wake mbele ya baba Askofu.
"hahahaa Umeona baba Askofu yaani hapo ninavyomjua Asunta mwanangu ndio ushampeleka kwenye mawazo ya huko chuo hahaha"
alifurahi Pastor George huku akimuangalia Asunta na walipokutana macho kwa macho jicho la Pastor George lilionesha alama ya hasira tofauti na sauti na uso wake na hii aliigundua Asunta na kuamini kuwa ile ni palni tu ya babaake.
"Vizuri sana mwanangu Asunta"
"Asante baba Askofu"
alijibu na kuonesha tabasamu bandia Asunta lililomuaminisha baba Askofu japo kwa upande wa moyo wa Pastor George na mkewe walijua wazi kuwa mtoto wao hajapendezewa hata kidogo na safari ile lakini hawakuwa na jinsi ilibidi tu wamsafirishe ili izidi kuwa heri na salama baina yake na kijana huyo wa kiisilaamu.

* * * *

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 11

Akiwa ni mwenye furaha sana jioni hiyo ikiwa imepita siku moja baada ya kutembelewa na kipenzi cha moyo wake Asunta mtoto wa Pastor ambae hadi dakika hiyo Dullah bado hakujua kama baba wa Asunta ni mchungaji mkubwa tu wa Kanisa nchini.
Aliendelea kufanya mazoezi kwa moyo mmoja na siku hiyo ilikuwa maalum pia kwake na timu ya Tandale fc ilipoamua sasa kumsainisha mkataba na kuwa mchezaji rasmi wa Tandale.
Furaha kubwa aliyoionesha Dullah kutokana na kusaini mkataba na Tandale haikulenga kwamba amefurahia kupata hela za kila mwezi kwani kutokana na hali ya kipato na uchumi wa Tandale fc aliahidiwa kulipwa laki moja na nusu kama mshahara katika mkataba wake wa miaka miwili waliomsainisha sambamba na laki tano kama pesa yake ya usajili lakini bado ukweli ni kwamba furaha ya Dullah ilitokana na kubaki maeneo yale yale ya jiji sehemu pekee anayoijua Asunta wake ambapo aliamini anaweza kuja muda wowote hata kama amekosa simu na mawasiliano na kama kweli Dullah isingekuwa Asunta na ingekuwa ni pesa tu, basi angekubali kwenda mtibwa waliomtumia milioni moja kama nauli lakini alizirudisha ili asipishane na Asu wake.
Siku hiyo alikuwepo Mbwiga wa Mbwiguke mtangazaji machachali wa michezo katika kituo maarufu cha radio Clouds fm na pia waandishi baadhi wa magazeti walihudhulia siku hiyo na si kwa sababu ya umaarufu wa timu ya Tandale bali ni kwa sababu ya kiwango cha ajabu alichokionesha Dullah katika mechi mbili za kirafiki moja dhidi ya timu kongwe ya Simba na nyengine zidi ya ile timu hatari iliyopanda ligi kuu msimu huo ya Becker fc na ndicho kilimpaisha na kusababisha watu wengi wa jiji la Dar kutaka kumjua.
Dullah alijisikia furaha sana siku hiyo na kichwani kwake alijitengenezea picha na kuwaona mamaake sambamba na Asunta wakiwa wamesimama pamoja mbele wakimpigia makofi lakini hiyo ilikuwa kwenye akili zake tu ila hali harisi haikuwa hivyo.

* * * * * *

Usiku huo ambao ndio ulikuwa usiku wa mwisho kwake kulala ndani mule na usiku wa mwisho pia kuwepo Tanzania kwa mujibu wa ratiba yao ya safari kesho yake asubuhi ambapo hadi muda huo taratibu zote zilishakuwa tayari zikiwemo tiketi za ndege watayoitumia kwa safari zilishakatwa mapema jioni ya siku hiyo na kilichobakia ni asubuhi tu ifike waanze afari ya uwanja wa ndege na kuelekea Nairobi nchini Kenya.
Asunta alipandisha ngazi na kujifungia mlango baada ya kula na kujitupa kitandani mapema majira ya saa tatu za usiku huku machozi yakimtoka na moyo wake ukimlaumu kwa kile alichokubali kukifanya na kumuacha katika wakati mgumu mtu anayempenda kweli tena bila ya taarifa yoyote.
Aliwaza jinsi gani Dullah atavyoumia mara baada ya kuja kugundua kwa namna yoyote kuwa hayupo kabisa Tanzania? hii ilimuumiza sana kwani alijua ni wanaume wachache wanaoweza kuwa na mapenzi ya dhati kama Dullah hasa akikumbuka alivyokuwa shule alishawahi kutendwa vibaya na mtu aliyemuamini na tokea hapo hakutaka tena habari za kupenda lakini alivyokutanakutana na Dullah kwa style ya kipekee sana moyo wake ulitokea kumpenda kweli kabisa lakini bado anapata vikwazo toka kwa wazazi hususani kikwazo kikubwa cha dini.

Akiwa bado anagugumia kwa kulia chumbani kwake Asunta alisikia sauti ya radio ikitangaza michezo chumba cha pili cha mdogo wake wa kiume aliyekuwa kidato cha kwanza na alivutiwa na habari moja ambayo ilimstua moyo wake na kuhisi huenda anayezungumziwa ni Dullah wake na hapo ndipo alipoacha kwanza kulia na kuchukua simu yake aina ya Galaxy l7 na kuingiza pin ya headphones na kutumbukiza visikizio kwenye masikio yake kisha nae akafungua masafa ya fm radio na kuieka chanel ileile ambayo ilikuwa ni clouds fm na mtangazaji aliyekuwa anasoma habari ile alikuwa ni Mwiga.

[[["Enheeeeeee Mbwiga wa mbwiguke hapa mkole wa nyani kibwaya mkia kiungo kisheti mwenye uchu ukinipa natoa nikikupa nauomba tena kama napiiigaa vileee aagh..chini ya udhamini mkubwa wa Binslum... Unaambiwaje, raha ya mchezaji uwe na umatemate kidogo sio miguvu tuu uwanjani umekunja sura na kutunisha misuli kama upo kwenye mchezo wa Ng'ombe au kama umetwishwa fuko la zege lililokuzidi kilo hE..!! Mpira sio mieleka babu mda wote mnarukiana rukiana kama vitoto vya sokwe wapiii bwanaaaaa.
Baasi leo nataka nikupe story moja matata sana la chini ya kapeti eenheeee unaambiwa vizuri utakula na wengi ila vya uchungu utakula kwenu na familia yako.. Na hii unajua wapi? aaagh! Tandale bwanaaa kwa wazee wa ndole unaambiwa ukisikia mwiziii mwiziiiiiii tegea tegea kufukuza sasa usijifanye una uchungu sana na mbio kuliko wenzio utajikuta umetangulia wewe mwizi kala chocho watu wanakuunganishia hadi useme sio mimi sio mimi tayari huna meno domo jaba eeeh tatizo vichochoro vingiii... kama mgeni Tandale utaishia kuzunguka na kutokea pale pale unaiacha njia ya kweli ukijua umepotea baada kuona choo mbele kumbe ndio njiaa hiyoo zunguka tuendelee na safari babaa huku ndio kwetuuu lazima tujivunie bwanaaa. Unaambiwaje Nyumbani ni Nyumbani hata kama unga robo mboga ya manati usipachukie ukapazalau na kwenda ukamsujudie jirani kisa kakukaribisha Pilau la kuku Ooooohooo utapoteaa!!
Naam unaambiwa tega sikio hapa usikie sasa siri imevuja leo ndani ya Tandaleee Unajua nani? Mribelia bwanaaaa sasa usihamaki ulivyosikia Mliberia ukadhani George Weah, sioo.. huyu ni mtoto wa kitanga Rasta mmoja muongo muongo akiwa na mpira ujiandae na uwe makini jinsi ya kumfata ukienda ovyo ovyo atakupima tu waaa mara gauni, shumizi, ohoooo hadi nguo za ndani kha! Kawaulize tandale watu waliopanua miguu uwanjani walivyozalishwa mipilaa oooh Matobo hayoo yaaani huyuuuu jamaaaa ukitaka kujua habari zake vizuri kamuulize John Kisiki kilichomkuta.
Eeeh John Kisiki huyo huyo unayemjua wewe Kigingi cha Mnyama msimbazi lakini siku hiyo mbele ya huyo Rastaa ohoooo mtu mzima akaaibika tena unaambiwa mbele ya Kidani cha moyo wake jukwaani hadi akawa anasikia aibu badala ya kusema usiniumiziieeee matokeo yake bwanaake ndio anataka kumuumiza mtu makusudi kwa hasira oooohooo lazima upanikii Rasta hafaaaiiii... kwani Tandale wanavyomwita mliberia wakimfananisha na George Weah unadhani machizi!! Kamuulize hata Kocha wa Becker fc jinsi alivyopata homa ya degedege uwanjani hahahaaa sasa Mtu mzima midevu hadi sehemu za haja kubwa na degedege wapi na wapi!!? ooh!! sasaaaa nikupe Exclusive Unaambiwa kumbe Mtibwa walishapeleka mikeka lakini Rasta kachomoaaa bwanaaaeeeh Daah! hii ilishangaza wengi sana baada ya kuvuja na Rasta kukubali kusota ligi ya mchangani akiiacha mikeka ya Mmasai inarejea Manunguuu... sasaaa Enhee sikia kumbe kilichokuwa nyuma ya pazia, jamaa leo kaamua kudondosha wino kabisa na kujifunga minyororo palepalee Tandaleee kisaaaaaaa MAPENZI.
Ninaposema mapenzi sio mapenzi ya Tandale tu, usidanganyike wachezaji wakakutoa roho hawa waone kama basi za usiku zinazoua paka... hazina ruti maalum babu kwenye abiria nazo ndio huko huko ooh! sasa bali kumbe kilichomzuia Rasta kwenda Manungu ni kwamba kuna mtoto mmoja mwenyewe anamwita Asu anaishi kwenye kifua chake na kuuendeesha moyo wake kama gari bovu lisilokuwa na kona wala breki ngoma mbele kwa mbele hiyoo hasikii wala haoni... ohoooo hadi anachomoa mitonyo ya mawe mareeefu unadhani mchezo!.. Ndio Dullah huyooo yule Rasta fundi wa Tandale mwenyewe anasema alipo Asu wake hawezi kwenda mbali na hapo.
Duh! mshkaji wangu sikia vituuu hivyooooo sio unatumbua mimacho kama fundi saa kapoteza nati ... Msikie mwenyewe Dullaaah alivyokuwa anatililika ndani ya Sport xtra na mbwiga baada ya kudondosha wino Tandale fc......."]]]

Naam hatimae sauti ya Dullah ilisikika masikioni mwa Asunta na kumfanya azidi kutoa machozi na kutabasam ukichangia na maneno ya vituko vya mbwiga na kauli za Dullah hasa aliposikia kakataa kwenda kucheza club kubwa maarufu nchini kwa sababu yake?... sasa inakuwaje leo hii yeye anakubali kuondoka tena nje kabisa ya nchi?
Alishindwa kujizuia Asunta na mwishoe alianza kutoa kilio cha sauti.

Kilio cha Asunta kilizidi kadri Dullah alivyokuwa anaongea na kujikuta tumbo linamkata ghafra na kichefuchefu kumjaa na kujikuta anashindwa kujizuia na kuanza kutapika mule ndani.
Sauti ya kutapika kwa Asunta ilimstua dada wa kazi aliekuwa anatoka kueka chumba sawa ambacho alikuwa anakitumia Askofu toka awe pale na alikimbilia chini walipokuwa kina Pastor wanaangalia marudio ya kipindi cha mchakato wa Katiba bungeni.
"Vipi wewe mbona hivyo."
"Hapana baba Asunta nimemsikia anatapika sana chumbani kwake twendeni tukamtazame nahisi anaumwa."
Kauli ile iliwastua wote sambamba na baba Askofu walikimbilia juu na kuanza kumgongea Asunta ambae bado walikuwa wanamsikia anatapika.
"Asunta mama vipi? hebu tufungulie basi mwanangu.."
aliita mama Asu na hapo Asunta alijivuta taratibu hadi mlangoni na kufungua mlango huku akijishangaa kuona mwili wake umechoka ghfra na kukosa nguvu kiasi kile.
Mara baada ya kuingia wote walimshangaa Asunta hali aliyoionesha mithili ya mgonjwa wa mwezi mzima wakati muda sio mrefu walikuwa nae chini wakila pamoja.
"Asunta vipi mwanangu?"
aliuliza Pastor kwa woga
"Tumbo baba"
"tumbo?. kwani umekula nini zaidi,,ee"
"Sijala kii......"
alijikuta moyo unamchefuka tena na safari hii kukimbilia kwenye choo kilichokuwa chumbani mwake na kutapika tena.

Yule mfanyakazi ilibidi aanze kufanya usafi haraka pale alipotapika awali Asunta na aliporudi alikuta Asu akiwa kazidiwa kabisa na sala ya maombi iliyoongozwa na Askofu mwenyewe ilifanyika kwa takribani nusu saa na hapo wakaamua kumpeleka hospitali usiku huo huo baada ya kuona sala imechelewa kufanya kazi.
hasa pale Asunta alipopoteza fahamu kabisa na kumfanya hata Pastor George aachane na baba Askofu ambae bado alikuwa kwenye maombi mazito na kuamua kumpepea mwanae na alipopata kustuka tu ndipo akatoa wazo kuwa wampeleke hospitali kwani maombi yamechelewa kujibu na huenda tatizo lenyewe limekaa kisayansi zaidi.
Wote walishangaa na kuona kama ndoto inakuwaje binti yao azidiwe ghafra usiku ule wakati hakuonesha dalili yoyote awali kama alikuwa yu mgonjwa.
"Mh! huyu mtoto isije kuwa kanasa!!?"
alijiuliza moyoni mama Asu hasa alipokuwa anaangalia alama za mapigo ya moyo ya mwanae akiwa kampakata ndani ya ile gari.

* * * * * *

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 12


-TANDALE SAA 3 USIKU-

Akiwa amekaa na rafiki zake kadhaa wakiwemo baadhi ya wachezaji wenzake wa Tandale wakimsikiliza Mbwiga kupitia Clouds fm, Dullah alikuwa ni mwenye furaha muda mwingi sana.
"Daah! mwanangu ujue maisha ndio haya babu muda wowote unatusua, si unamsikia Mbwiga anavyokuchocheaa"
aliongea jamaa mmoja mwenye upala
"Kwani rasta demu mwenyewe yupi babuuu aaaaaaaah! au yule aliyekufanya usirudi na sisi baada ya ile mechi na simbaaa?"
"hswaaa ndie yule washkaji."
"Dah! mwanangu kama kweli ndie yule basi kaza maana mtoto Mh! kifaa si mchezo afu anaonekana wa mboga saba yule."
waliongea na kufurahi na muda uleule simu ya Dullah iliita na alipoitazama ni namba ya mamaake waliyeongea jioni ile na kumuhadithia kila kitu pia aliwasisitiza kuwa wafungulie radio clouds siku hiyo watamsikia.

Dullah alifurahi zaidi na kujiona wa pekee sana siku hiyo kisha kusogea pembeni na kuipokea ambapo alisikia sauti ya mdogoake akifurahi sambamba na mamaake na kumpongeza sana huku wakimwambia kuwa ampeleke wamuone huyo mwanamke anayesema Mbwiga na kumfanya Dullah azidi kucheka na kuwambia kuwa wasijali kwani atapokwenda huko aliahidi kwenda nae Asunta.
habari ile ilimfurahisha sana pia mamaake aliyekuwa hachoki kumuombea dua mwanae kila jua lichomokapo na lizamapo na alimuombea tena kupitia simu na kumpa baraka huku akimwambia kuwa mungu atamzidishia zaidi na zaidi kwa kile alichoanza kukipata muda ule.
Na siku hiyo katika pesa ile aliyoipata D ya usajili wake, robo tatu yote ya pesa aliituma kwa mamaake ili ipate kuwasaidia zaidi na kuendeleza msingi wa nyumba ya tofari ulioanza kujengwa baada ya pesa kidogo kidogo za nyuma alizokuwa anatuma kwani moja ya ndoto aliyokuwa nayo Dullah kipindi anatoka kijijini kwao ni kujenga nyumba ya bati angalau nao waonekane watu wa heshima furani pale kijijini kwao kwani awali walizaraulika sana.
Alikata simu na kurudi kujumuika na wenzake mara baada ya kumaliza kuongea na mamaake.

* * * * * *
- SINZA (MUDA HUO HUO) _
.......................................

Alionekana John akinyanyuka na kwenda kuzima radio iliyokuwa inaendelea kutangaza habari za michezo chini ya Mwiga wa Mbwiguke hasa kipindi ilipoanza kusikika sauti ya Dullah na kumfanya Vero nusu avunjike mbavu kwa kicheko pale kwenye sofa walipokaa.
" ha hahaha ahahahaaaaaa Daaaaaah.....Jooooooohniiii hahahahaaa Mbwiga kajua kukunanga Duh!! sasa unazimia nini? hahahahaaa"
"Hebu toka hapa, mfate huyo Mbwiga kama bwanaako akakufurahishe vizuri."
"Haaaah! Kichuna changuuu Johniii mbona unaenda mbaali nawewee!!"
aliongea Vero huku akimchezea chezea kidevu John ambae alikuwa hajapendezwa na habari zile za Dullah.
"Enheee afu nimekumbuka kitu beby wangu"
alinena Vero huku akikaa vizuri.
"Kitu gani?"
aliuliza John
"Kuhusu huyo Rasta."
"Rasta? rasta yupi!"
"Si huyo wa Mbwiga..!"
"Si nishakwambia sitaki kusikia habari zake lakini, mbona unataka kunikera zaidi?"
"Sio hivyo John, ni kuhusu Asuntaa."
"Asunta!! Kivipi?"
"sasa ndio unisikilize, huyo rasta anaesema mbwiga kadata na Asu.. Asu kafupisha lakini ni Asunta."
"aagh! mbona sikuelewi sasa kama Asunta we anakuhusu nini?"
"Jamani Asunta si shogaangu nusu ndugu?"
"Ina maana una maanisha Asunta mtoto wa Pastor George?"
"Ndio"
"ndio huyo yupo na huyo Rasta mchafu wa Tandale?"
"Ndio"
"He!! we umejuaje?"
alitahariki na kuuliza John
"si unakumbuka siku ile tulivyoenda kumsaidia Asunta na kukuta kashasaidiwa na mtu ambae alituonesha kwa mbali na kushuhudi kuona rasta zake pindi alipokuwa anaingia kwenye daladala.."
"Enhee!"
"Basi ndie yule mliocheza wote siku ile ya mechi na baada ya pale Asunta aling'ang'ana kuondoka mwenyewe na kunizuga wakati mi nilishamsoma vizuri na ndio walipoanzia kudumisha mahusiano yao pale.. Na kama hiyo haitoshi siku zilivyozidi kwenda sijui yule rasta mchawi kwani Asunta alibadilika hadi ikafikia kipindi alivyosafiri Pastor George akawa anarudishwa usiku wa manane hadi kwao na yule rasta na siku hiyo ndipo walipofumwa na mama Asunta kuwaamuru maafande wamshushie kichapo lakini bado inaonekana rasta hajakoma tu."
"Duuh!! aisee kwanini sasa Unajua mi SIMPENDI yule Rastaaa.."
"Hunishindi mimi mme wangu yaani jinsi anavyonichefuaa Agh.. twende tukalale beby tuachane naye asituharibie usiku wetu tukaja kumuota bureee afu tuamke na mikosi."

Walijizoazoa kimahaba na kuzama chumbani kwao na baada ya muda mfupi mbele ilianza kusikika Miguno ya kikubwa.

* * * * * *
- HELTH KING HOSPITAL -
............

Walimfikisha katika hospitali ile binafsi ya King Helth iliyosifika kwa matibabu mazuri na ya gharama nchini ambayo pia ilikuwa na madaktari mchanganyiko wazungu, waswahili na wahindi na baada ya Asunta kupokelewa aliingizwa emergence na kuanza kufanyiwa vipimo vya harakaharaka ndipo baadae alitolewa na kuingizwa kwa daktari bingwa ambae alikuwa ni mswahili na huko alifanyiwa utafiti zaidi wa kitaalamu wakati huo Pastor George mkewe na Askofu walikuwa kwa nje sehemu maalum ya kusubiri wakisikilizia majibu ya Daktari.
Na baada ya lisaa limoja na nusu alitoka dokta na kuwaita wazazi wa Asunta na kuingia nao ofisini kwake na kuanza kuwapa majibu ya utafiti walioufanya juu ya nini walichogundua kinachomsumbua Asunta.
"Ndio dokta tunakusikiliza."
"sawa, baada ya utafiti wetu wa kina kabisa tulioufanya juu ya ugonjwa wa binti yenu, kwanza ningependa kuwatoa hofu kubwa mliyokuja nayo na kuwahakikishia kuwa binti enu atakuwa sawa hivi punde tu."
"Kweli Doktaaa aah! Asante Yesu... asante sana baba kwa muujiza uliotuonesha aaah Haleluyaaaa.."
"AMEEEEN"
walijikuta wanageuza hospitali sehemu ya ibada muda mfupi baada ya maneno ya utangulizi wa Daktari kabla hajaendelea.
"sasa Dokta mmegundua nini zaidi kilichomfanya binti angu augue ghafra namna hii hadi kupoteza fahamu?"
aliuliza Pastor
"sawa majibu yetu yalikuja sehem mbili yenye vifungu vinavyoshabihiana sana, Kwanza tatizo lililomsababisha hadi apoteze fahamu ni kutokana na mawazo ya muda mrefu aliyokuwa nayo mwanenu na kusababisha kuubadilisha mfumo mzima wa uendeshwaji damu mwilini uliochochewa na mabadiliko za homoni kutokana pia na mimba changa ya miezi miwili aliyokuwa nayo........"
"KHAAA! Ina maana Dokta unataka kutwambia mwanetu ni MJAMZITO?"
"Ndivyo vipimo vinavyosema hata tuliporudia mara ya pili na sababu ya pili inayothibisha hilo ni kwamba mwanamke yeyote anapokuwa katika mabadiliko ya homoni yaliyosababishwa na mimba ambayo bado ni ndogo kisha akawa na matatizo ya mara kwa mara kichwani mwake asiyoyapatia ufumbuzi na kumsababishia msongo wa mawazo ana uwezekano mkubwa wa kupata tatizo la kupoteza fahamu mara kwa mara kama ilivyoanza kwa mwanenu ama likizidi basi mimba pia kuharibika."
aliongezea Daktari wakati huo Pastor George alibaki katumbua macho akiwa hamini hata kidogo anachokisikia wala haelewi kabisaaaa na kugeuka kumuangalia mkewe kwa hasira.
"Mama Asu mama Asuuu utanieleza mtoto kapataje Mimbaaaa haaa.. Mwanangu mbona unataka kutuvua Nguoo"
alilalama Pastor baada ya kujisahau kama yupo hospitalini na kukumbuka kuwa nje yupo Askofu anawasubiri nae akiwa na shauku ya kujua nini kilichomsibu Asunta.

Alimuangalia mkewe na kumuomba radhi daktari huku wakiahidi watakuja asubuhi na mapema kujua zaidi alivyolala mtoto wao na baada ya kusimama na kuusogelea mlango wa kutokea Pastor George alimwambia mkewe kwa sauti ya chini kuwa aache kusema chochote yeye mwenyewe ndie atayeongea na Askofu na atachosikia ndicho atachotakiwa kuwambia na wengine wa nyumbani na kusapoti. Baada ya mkewe kumuitikia kwa kichwa ndipo alipofungua mlango na kutoka ambapo walimkuta Askofu akiwa kasimama tena akiwa ndani kabisa ya maombi mazito huku akiongea kwa sauti ya chini sana na kufumba macho yake pindi alipokuwa anazunguka hatua fupi fupi eneo lile la korido akinena neno la Mungu na kuzishinda nguvu zote za giza na kumuombea uzima Asunta.
Hata walipofika Pastor na mkewe nao waliungana katika maombi yale na baada ya kumaliza na Askofu alipofumbua macho alishukuru na kuwatazama wazazi wa Asu ambao alibaini bado nyuso zao hazijawa sawa.
"Vipi Pastor George, Daktari anasema nini?"
"Daah! baba Askofu kwanza nasema inabidi tumshukuru Mungu baba etu mpenzi mwenye neema kwa jinsi hali ilivyokuwa na ilipofikia, ila tabibu anasema kuwa tusiwe na wasi wasi sana japo inahitajika Asunta apate utulivu wa masaa 48 zaidi ili wamfanyie utafiti wa kina lakini utafiti na vipimo vya sasa vinaonesha kuwa alipata mstuko wa Moyo kidogo uliomsababishia apoteze fahamu baada ya kutapika sana kwa hiyo vipimo vya kesho ambapo majibu yake yanachukua masaa 24 zaidi ndivyo vitavyotoa jibu rasmi kwanini hali hii ilimpata."
aliongea Pastor George huku moyo wake ukimsuta kwa kuficha ukweli harisi alioambiwa na daktari lakini ilimuwia ugumu sana kunukuu kile alichosema Dokta na kumwambia baba Askofu.
"Ooooh! Yesu kristo mwenye wokovu hebu kaguse mkono wako kwenye kifua cha huyu binti Asunta na umrejeshee hali yake ya siku zote... Dah! kwa hiyo itabidi sasa niahilishe safari nisubiri nione itavyokuwa."
"Hapana baba Askofu, mi nakusihi na kukuomba wewe nenda tu kwani si vyema ukapata hasara mara mbili zaidi pia kumbuka kuwa kikao cha Jumuiya ya Maaskofu Afrika kitafanyika huko na wewe ni moja ya wenyeji hivyo uwepo wako ni lazima sana na itabidi uwahi tu baba usihofie sisi tutalishughulikia na atapokuwa amerudi katika hali yake basi nitasafiri nae mimi mwenyewe mpaka huko Nakuahidi baba Askofu na kukuomba ukubali tu mawazo yangu tafadhali."
aliongea Pastor George na kumfanya baba Askofu ainame na kusikitika kidogo kisha alikubaliana na maneno ya Pastor George baada ya mama Mchungaji nae kukazia na kumsihi Askofu asijali kuhusu hilo yeye aende tu wao watashughulika na hali yote itayojili na watampatia taarifa.

Basi baada ya kukubaliana walimuamuru dereva kuwarudisha nyumbani na tayari ilikuwa saa 7 usiku.

* * * * *


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 13



Alionekana Dullah akiwa kwenye usingizi mzito uliobeba ndoto zilizofanya awe anaweweseka huku pembeni yake akiwa kalala na rafiki ake mmoja waliokuwa wanacheza wote Tandale ambae siku hiyo aliamua alale pale kwa Dullah ili kesho yake wawahi wote mazoezini.
Alistuka Rajabu au Roja kama walivyopenda kumwita mtaani na uwanjani ambae alikuwa rafiki wa kwanza wa Dullah aliyemshauli kujiunga na timu yao wafanye wote mazoezi mara baada ya kuwa anafanya mazoezi kivyakevyake na hata mara ya kwanza kocha alipotaka kumkatalia Dullah kujiunga nao Roja alimtetea kuwa wampe nafasi kwanza na kwa kuwa Roja aliaminika Tandale na ndie alikuwa Kapteni ilibidi wakubali na kweli Dullah alipojichanganya siku chache tu kufanya mazoezi pamoja kila mtu alianza kuuona utofauti wake.
Alikaa kitako pale kitandani Roja na kumuangalia Dullah ambae alizidi kuweweseka na kuongea maneno yasiyoeleweka huku akirusha rusha mikono hali iliyoanza kumtisha Roja na kuinuka kwenda kuwasha taa kisha alimtingisha na kumuamsha D ambae muda huo alizidi kuweweseka na kuanza kulia kwa kwikwi huku machozi yakimtoka kweli.
"Oyaaaa..Oiii babuu vipi mwana."
aliongea Roja mara baada ya Dullah kukurupuka na kumtumbulia macho huku akiwa haelewa na kujifikicha uso na kuinamia chini kidogo kutokana na macho yake kuzidiwa nguvu na mwanga wa taa.
"Oyaa Dullah mwanangu vipi? uko poa?"
"Aaagh! poa Roja mbona sikuelewi?"
"Sasa hunielewi mimi au mimi ndo sikuelewi wewe? Daaah!! inaonesha mtaa wenu una wanga kweli."
"Kwanini Roja"
"Daah! yaani laiti ungejiona ulichokuwa unafanya au ungekuwa umelala na mchumba sasa hivi angeshakurupuka na kuomba umpeleke stendi asepe."
"Daaah! Ebwana hapana Roja kwani nilifanyaje?"
"Nihadithie kwanza wewe umeona nini mwana."
"Mh!! kuna ndoto nimeota mwana lakini nasikia kuhadithia ndoto usiku vibaya."
"Aaagh! vibaya nini sasa D acha mila potofu mbona unataka kuuchezesha moyo wangu kindumbwendumbwe.. we kama umeona mazombi sema tu."
"Daaah.."
Alijifikilia Dullah na kumfanya Roja anyanyuke muda ule na kuifata suruali yake aliyoitundika juu ya msumali na kutoa kete moja na rizla kisha akanyonga kitu na kutengeneza sigala kubwa na kuiwasha kisha kukaa tena huku anaivuta taratiibu.
"Haya sasa D nishaichoma hii ndio mwisho wa matatizo vinyamkera na wanga wote washakula chocho we shusha mkanda man kama vipi piga pafu mbili unihadithie vizuri"
alikazia tena Roja na ndipo Dullah aliamua kusimulia alichoota baada ya kuona rafikiake kawa king'ang'anizi.
"Unajua nini Roja mshkaji wangu, Nimemuota Asu babu tena nimeota nishamuoa sasa niko hospitali nimempeleka akiwa na mimba kubwa tu akilia uchungu lakini kila dokta niliekuwa namfata amsaidie mke wangu alikuwa ananitazama tu huku ananicheka sasa nikawa nachanganyikiwa zaidi na mke wangu akawa analalamika maumivu nami sikuwa na uwezo wowote wa kumsaidia ndipo nilipoingia hadi kwa daktari mkuu na kumuomba lakini nilipoenda nae pale alipo mke wangu Asu tulimkuta hali mbaya sana na damu zilianza kumvuja kwenye mapaja huku madaktari wengine wakiwa wamekaa kwenye viti wakimuangalia kama tv na hata yule daktari mkuu nilishangaa nae anaenda kujumuika na wenzake na kuanza kucheka huku nikimshuhudia mke wangu akitapatapa na ndipo nikaanza kulia kwa uchungu na kumkimbilia mke wangu pale chini ili nimpeleke hospitali nyengine lakini nilipomfikia tu kabla sijamgusa kuna mtu akawa ananigusa bega huku akiniita na nilipogeuka ndipo nilijikuta nimeamka nipo kitandani nakuona wewe Daaah! yaani hata sielewi."
alimalizia D kusimulia ndoto yake ambayo ilimfanya Roja acheke sana na kuanza kumtafsiria alivyojua yeye.
"hahahahahaaaa Duh! mwanangu kweli vibwengo leo wamejua kukuchezea daah! itakuwa wamekusikia redioni ulivyomsifia Asu ndio maana wameikopi sura yake na kukuonesha kama akiwa katika hali mbaya utakuwaje? je, utaonesha mapenzi ya dhati kiasi gani ili kuupima moyo wako na maneno uliyosema kwa Mbwiga hahahahaaa Daaah!! kama nawaona wanavyokucheka vileee Duuuuh! Rastaaaa hadi wanga na vibwengo wanakutoa mchozi kwa ajili ya Asu?!! jee ingekuwa kweli ..? aaagh! tulale bwana kwanza saivi wanga wote washasepa wanakuchekea hukooo hahahaaa"
"Aaaaagh! Roja taratibu bwanaaa usicheke kwa sauti hivyo basii"
aliongea Dullah na kujifunika huku Roja nae akizima kipisi kilichobaki akifanya bajeti ya asubuhi na kuzima taa kisha wakalala.

* * * * * *
- MUDA HUO HUO (MASAKI -
............................

"Hapana bwana mme wangu mi siwezi kushiliki jambo kama hilo, wala haliwezi kupendeza mbele ya bwana."
"Sasa wewe mama Asu ulitakaje, tupate aibu jamii yote itatuonaje unadhani kama watabaini jambo hili? au Kanisa litanichukuliaje na heshima hii waliyonipa eeeh... mi nisha kwambia fanya unavyojua wewe milioni tano hawezi kuzikataa hata kidogo yule Dokta tena ufanye mapema kesho na hii hata Asunta mwenyewe afanyiwe bila kujua."
"Lakini mume wangu tumuogope Mungu.."
"Sasa we unataka malumbano yasiyo na msingi mwisho niongee kwa sauti hadi baba Askofu atusikie huko chumba cha tatu"
"Hapana mume wangu"
"Hapana nini sasa?? mbona unataka kunipanda kichwani? Hata huyo Mungu unaesema simuogopi huenda yuko pamoja na mimi katika hili. wee unamjua huyo Kijana? ngoja kwanza nikuoneshe kitu.... hebu ona kwanza
unaona kabisa hili livuta Bangi pili Liisilamu halijampokea kristo tatu lihuni nne limasikini la kutupwa tano lichafu namna hii minywele ovyoovyo bado tu lituchafulie nyumba yetu kwa kuruhusu kuufuga uchafu aliouweka kwa mwanetu aaah! IT WILL NEVER HAPPEN na ndio maana hata Asu kapoteza fahamu na katapika kupita kiasi kutokana na roho mtakatifu anaezunguka nyumba hii kutoridhishwa na uchafu ulio tumboni mwake kwani mbona wewe ulivyobeba mimba ya Asunta na hawa wengine hujawahi kuzimia?.. Na ndio maana nakwambia fanya hivyo kwa gharama yoyote mshawishi yule Daktari na hata akikataa kiasi hiko muongeze milioni tano nyengine potelea mbali"
"Mhh! mume wangu!!!? hivi ni wewe kweli leo unafikia hatua yaa.."
"KELELEE MAMAA ASU... wee nambie moja utafanya au Hufanyi..?"

Ilisikika sauti ya ukali na ya juu kutoka kwa Pastor George huku uso wake ukiwa umekunjika mno kwa hasira iliyochochewa zaidi na mabishano baina yake na mkewe kuhusu nini cha kufanya juu ya hali ya Asunta iliyogundulika kule hospitali huku ukweli ukiwa bado uko kwao wenyewe juu ya tatizo hasa la Asunta.

Alitafakari mama Asunta huku akiziangalia picha za Dullah akiwa na Asunta alizooneshwa na mumewe pale kitandani ambazo alizitoa kwenye bluefkesi yake ili amuaminishe alivyo huyo kijana ambae waliamini ndie aliyempa mimba mtoto wao huku akijiuliza na kufikiri moyoni mumewe kazipatapata vipi zile picha au aligundua siri kuwa yule kijana aliwahi kuja pale? alibaki akiziangaliaangalia tu zile picha.
"Samahani mke wangu kwa kukufokea lakini we muangalie vizuri mpuuzi mwenyewe alivyo najua utajiuliza nimejuaje kama ndie huyo lakini hii yote ni kazi niliyoifanya kwa muda mfupi ili nijue huyo Abdallah kamzuzua nini mwanangu lakini lool, nilipoziona picha zake akiwa na mwanangu nilitamani nitapike au nipasuke kabisa kwa hasira."
alibembeleza Pastor kwa sauti ya utaratibu ila yenye hasira ndani yake huku akimshika mkewe nywele na kum bembeleza zaidi.
"Najua mama Asu unanipenda sana mke wangu nami najivunia kupata mwanamke mwerevu kama wewe. Najua pia unawapenda wanetu wote na unahofia kama huenda Asu akapata matatizo pindi atapokuwa anatolewa hiyo mimba lakini nataka nikuhakikishie mke wangu kuwa sisi ni watukufu tuliobarikiwa na bwana na kwa hili Mungu mwenyewe atatusamehe kabisa kwani tunachofanya ni kuliekeza heshima kanisa lake takatifu lisije kunyooshewa vidole na watu kwa ubaya... eeh Mke wangu hebu fikiria hilo kwanza, najua kwako wewe ni rahisi sana kufanya hivyo atakuelewa tu yule daktari tena ikibidi umpatie hata na lile gari alilokuwa anaendeesha Asunta zamani. Naomba kubali tu mke wangu"
"sawa mume wangu nimekuelewa nitajaribu.."
"Sio utajaribu tafadhali mke wangu tetea heshima na hadhi yetu inayotaka kuvunjika kwa moyo mmoja sema Nitafanya"
alibembeleza zaidi Pastor George huku akimtazama mkewe kwa jicho la huruma hadi machozi yalianza kumrenga juu ya swala lile la kukubali akamshawishi Daktari mapema kesho kumtoa mimba binti yao pasi hata yeye mwenyewe kujua.
Baada ya kutafakari sana hasa alipomuangalia mumewe ambae alionesha kuwa anaweza kulia muda wowote kwa kukataa kwake ndipo mama Asunta alijikuta anakubaliana na mumewe kwa huruma zake japo kishingo upande.
"Sawa mume wangu nitafanya na nitailinda siri hii"
"Safi sana mke wangu Eee roho mtakatifu Asante sana kwa kumuongoza mke wangu katika njia salama ya kuendelea kulisimamisha jina lako baba yesu Kristo katika usafi pasi na kupakwa nukta ya tope lolote aaah!! Nakupenda sana mke wangu Mmmwwaaaaaaaa"
alifurahi Pastor George na kumkumbatia mkewe huku akimpiga mabusu mfululizo na tayari muda huo ilikuwa saa kumi alfajiri huku wakiwa wamekesha pasi na kulala hata kidogo kwani saa kumi na moja ndio muda uliotakiwa wa kumpeleka baba Askofu uwanja wa ndege ambapo saa kumi na mbili ndio muda ambao ndege itaondoka.

* * * * * *

Alfajiri na mapema sana ndani ya daraja la manzese walionekana Dullah na Roja wakiwa wanafanya mazoezi ya kukimbia kwenye vingazi vya daraja na kuruka kichurachura huku pia watu wengine walionekana wakifanya mazoezi ya karate, boxer na wale wenye miili mikubwa wakifanya mazoezi kwa mashalti ya daktari wakikimbia taratibu kupunguza mafuta yaliyoelemea mwili.

Baada ya kupasha kwa lisaa lizima na kutimu saa kumi na mbili taratibu Dullah na Roja walianza kukimbia kuelekea uwanja wa Tandale kwa mazoezi ya timu pamoja na wenzao.
Siku hiyo Roja alimgundua Dullah kuwa hayuko sawa kutokana na jinsi alivyokuwa anafanya mazoezi tofauti sana na desturi yake siku zote na walipokuwa njiani wakitroti kuelekea uwanjani ndipo Roja aliamua kumuuliza mwenzake kulikoni.
"Oyaaa D mbona leo upo kimama mama sana vipi uko poa?"
"Ah! mbona mi niko sawa tu Roja"
"Mh hamna bwana mi sio mgeni na wewe, au walikuchezea tena nini?"
"Kina nani..?"
"Si vibwengo vya usiku wazee wa nyungo."
"aah! Roja taratibu bwana achana na hayo mambo kaka usije kuyafikisha uwanjani ooohoo"
"hamna D usiogope man, ila changamka kidogo basi best."
"Poa man, "
alijibu Dullah na kuendelea kutroti na walishangaa siku hiyo walipofika uwanjani kukuta watu wamekuwa wengi tofauti na inavyokuwaga hasa nyakati za asubuhi kama ile.
Wingi wa watu ulikuwa si kwa sababu wamekuja kufanya mazoezi bali wengi walikuja kuitazama timu ya Tandale wanavyofanya mazoezi ya asubuhi ambayo yalikuwa yanahudhuliwa na watu wachache tu awali ambao walikuwa watazamaji na wengi walikuwa wahuni wa vijiweni na sokoni lakini safari hii ilikuwa tofauti na kivutio zaidi alikuwa ni Dullah.
"Rasta mwenyewe aliyekuwa anamzungumzia Mbwiga ndio yulee nini?"
"Yuleyule man, si umeona hata anavyotorit..! yaani msimu ujao kwa usajili huu lazima tucheze ligi kuu daah."
yalisikika baadhi ya maneno ya watu waliohudhulia kutazama mazoezi asubuhi ile hali iliyomfanya hata Dullah kujisikia vizuri kidogo baada ya kuwa kwenye mawazo mazito muda mwingi hata walipokuwa kule darajani alifikiria sana juu ya Ndoto aliyoota siku hiyo ambayo iliuumiza sana moyo wake mbali ya kuwa alishatafasiriwa na Roja.

* * * * * *

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 14




Baada ya kumfikisha Askofu uwanja wa ndege na kuagana huku wakimuahidi kumtaarifu kila kitu kitachoendelea kuhusu Asunta na kumuhakikishia kuwa hali yake itapokuwa vizuri bila shaka atawasili nchini Kenya kwaajili ya kujiunga na hiko chuo kauli zilizomridhisha Askofu na kuondoka huku akiwa haelewi nyuma ya pazia nini walichodhamiria wazazi wa Asunta juu ya mtoto wao kule hospitali.

"sasa kazi hapa imebaki moja mke wangu na wewe ndie shujaa wa kufanikisha hili lililo mbele yetu na ndio maana nimeamua kumuacha dereva leo na kuendeesha mwenyewe ili iwe rahisi kufanikisha maongezi na mipango yetu."
aliongea Pastor huku akiwa anaendeesha gari huku upande wa kushoto alikaa mkewe aliyekuwa anamsikiliza kwa umakini pindi walipokuwa wanatoka uwanja wa ndege baada ya kumsindikiza Askofu.
"Sasa hapa unatakiwa uongee point kwa siri kubwa na umkabidhi hiki kitita na kumsihi na kumkumbusha atunze siri pia afanye hayo pasi na Asunta kujua kuwa alikuwa na mimba sawa mke wangu"
"sawa"
"Basi mungu akutangulie na roho mtakatifu akusimamie ili zoezi lifanikiwe kiurahisi na asije kujua mtu yeyote zaidi yetu na daktari tu. tena umwambie hata manesi wake wasijue na kama kuna daktari mwengine anajua nambie nae tumpe za kwake."
"sawa nimekuelewa"
alijibu mama Asunta na muda huo walikuwa washafika kwenye ile hospitali na Pastor George aliipaki gari sehemu husika na yeye kubaki ndani ya gari akimsubiri mkewe bila kushuka.
[[("Nikifanikisha zoezi hili tu.... kazi iliyobaki ni kumtafuta huyu mpuuzi anaetaka kuniaibisha katika jamii")]]
Aliwaza Pastor George pindi mkewe alipokuwa anashuka na kuondoka kuingia mule hospitali kwenda kutekeleza agizo la mumewe.

\Baada ya lisaa limoja na nusu akiwa amekaa ndani ya gari huku ameegamia usukani Pastor George aliwaza nini cha kumfanya Dullah ili asiwe jirani kabisa na mwanae kwani aliamini asipomdhibiti na Dullah itakuwa bado mwanae atavunja kizuwizi chochote hadi ataenda kuonana nae kama kawaida hasa baada ya kubaini walishakutana kimwili hivyo washarambishana asali ambayo sasa kila mmoja atataka kuchonga mzinga kabisa.
"Sijui nimtumie tena yule Kijanaaa...!!! Aghg, lakini yule kijana wangu wa kanisani kazi hii haitampendeza afu kama ataipokea vibaya inaweza kuwa aibu tena kwangu.. sasaaaaaa...Dah! huyu mshenzi manywele ndie ananiumiza kichwa hivi?!!...."
akiwa bado anawaza kwa sauti ya chini Pastor alistuliwa kwenye dimbwi la mawazo na mtu aliyekuwa anagonga kioo cha dirisha kutokana na kulockiwa milango na alipoinua uso kumtazama moyo wake ulipiga baada ya kuona ni mkewe ambae uso wake ulionesha ni mwenye wasiwasi mwingi moyoni mwake hali iliyomstua na kumtisha Pastor ambae alitoa lock na kumfungulia mlango mkewe aliyepanda harakaharaka huku akiwa anahema kama katoka kukimbia mbio ndefu.
"Vipi mama Asu mbona hivyo sasa!!...Umefanikiwa??"

Aliuliza katika hali ya mshtuko Pastor George kwa jinsi alivyomuona mkewe.
"Mh! mme wangu kazi ilikuwa ya hatari sana japo tumefanikisha lakini tumuombee mtoto awe salama kwani hajapata fahamu bado"
"Saaafi. si alimchoma sindano ya usingizi ili asijue kinachoendelea?"
"Nahisi ndio maana amenambia nisiwe na hofu."
"Basi usiwe na hofu we baki usikilizie nampigia simu dereva awafate sasaivi mi naondoka."
aliongea Pastor huku moyoni mwake akiwa na furaha sana baada ya kufanikisha lile zoezi la kumshawishi daktari na kuitoa mimba ya mtoto wao na wazo pekee lililobaki kichwani mwa Pastor ni juu ya Dullah marasta.
"sawa mume wangu ila msisitize awahi"
alijibu mama mchungaji wakati anashuka ndani ya gari na kuagana na mumewe ambae ni Pastor George.

* * * * *

Akiwa njiani tena mwendo kasi Pastor George baada ya kuwasiliana na dereva wake afike hospitali akawachukue kina Asu, alinyoosha usukani moja kwa moja kuelekea ubungo kule kwenye shule ya mazoezi aliyokuwa amempeleka Asunta.
"Huyu mpuuzi Manywele !!?? Dawa yake ipo tu."
aliwaza moyoni Pastor pindi alipokuwa anaingiza gari sehemu ya kupaki pale mbele ya lile jengo kubwa lililotumiwa na watu mbalimbali kufanya mazoezi kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa na walimu bora hasa wale wa karate, boxer na king boxer.
Baada ya kufika pale wazo lake lilimpeleka kukutana na kijana mmoja mbavu kidogo ambae alikuwa mwalimu wa King boxer aliyemkabidhi Asunta amfundishe mazoezi ya viungo.
"Ooh! baba Mchungaji bwana asifiwe"
"Milele amina mwalimu Jack habari ya mazoezi"
"salama tu baba vipi Asunta? naona muda kidogo alikuja siku moja akawa hajisikii vizuri tukamruhusu. Anaendeleaje sasa"
"Aaaah! Asunta bwana anasaidia anaendelea vizuri na siku si nyingi ataenda kuanza masomo yake ya elimu ya juu Nairobi"
"Ooooh umefanya vizuri sana baba. Karibu naona umekuja kututembelea"
alikaribishwa Pastor na yule mwalimu wa Asunta mara tu alipoingia na kumkuta nae akiwa pale mapokezi.
Pastor alimuomba mwalim Jack watoke wakazungumze zaidi kwa nje na walionekana wakizungumza kwa kirefu sana hadi walipokubaliana na ndipo Pastor alipoingia ndani ya gari yake huku na mwal Jack nae akiingia kwenye gari yake pia na kutoka kwa pamoja amapo ile gari ya Pastor George ilikuwa imetangulia ikifuatiwa na ya mwal Jack.

"Ndio kijana wangu basi si ulisema Tandale uwanja wa mpira shule?"
[['Hee, baba ndio mazoezi yanaelekea mwishoni nipo hapa']]
"Na huyo chizi yupo"
[['yupo baba']]
"Basi baada ya dakika kumi tutakuwa hapo"

Alikuwa ni Pastor George akizungumza kwa simu pindi alipokuwa njiani na alizidi kukanyaga mafuta akiongoza barabara ya Sinza na kukunja Uzuri nia na madhumuni awahi viwanja vya Tandale shule.

Muda mfupi baadae waliwasili karibu kabisa na viwanja vile na kupaki gari huku lile gari alilokuwa anaendeesha yule mwl, Jack likipaki nyuma kidogo na alipopaki Pastor George na baada ya dakika kadhaa ilionekana pikipiki moja kubwa aina ya Honda ikitokea maeneo ya viwanja na kusimama ilipopaki gari ya Pastor na kushuka kijana mpanda pikipiki ambae alikuwa ni yule yule kijana aliyewahi kuwapiga picha kwa siri kina D na Asunta na mara ya mwisho alisemezana na D akijifanya kuulizia njia.

"Vizuri kijana wangu vipi umempiga picha na leo?"
"Yaah nilimpiga pindi walipokuwa wanaingia uwanjani asubuhi hii lakini muda huu mazoezi yashaisha nahisi wanaweza kutoka muda wowote na njia yake kuu anayopitaga kuelekea anapoishi ni ile pale"
"Oooh hahaha vizuri sana sasa wewe chukua hii laki moja kanywee chai kisha baadae utanipigia nikuelekeze uende shelli ipi ukajaziwe mafuta sawa.?"
"sawa Baba Mchungaji,"
"Ok mwanangu bwana akutangulie tutaonana kwenye maombezi jioni"
"amen baba"
aliaga yule kijana na kumkabidhi Pastor kamera ndogo ya digital aina ya Sonny ambayo aliitumia kumpiga picha Dullah asubuhi ile pasi na Dullah wala mtu yeyote kutambua kisha akaondoka na kumuacha Pastor akiendelea kumuangalia D kupitia ile kamera huku uso wake ukionesha kughadhibika mno.

Akiwa bado anaangalia angalia picha za Dullah mara alisikia kelelekelele za watu waliokuwa wanatoka uwanjani na ndipo alipotuliza macho yake kwa umakini kuwatazama huku akilini mwake akimlenga Dullah tu, na ndipo mara kwa mbali aliwaona vijana wawili mmoja akiwa na rasta kichwani wakitembea kuelekea kule walikopaki gari zao na kabla hawajafikia kile kinjia walichotaka kukunja Pastor George aliamua kuwawashia taa ya ishara ya kuwaita na alipoona hawaelewi aliwapigia kabisa na honi huku akijifungua beti ay mkanda aliyojifunga kitini na kujiandaa kushuka kabisa.

* * * * * *

Mazoezi yalikuwa mazuri japo kwa upande wa Dullah hakupaform vizuri kama kawaida yake na ni Roja pekee ndie aliyekuwa na siri juu ya kitu kilichokuwa kinamsumbua Dullah kichwani mwake na hata mazoezi yalipomalizika huku watu wengi wa Tandale wakionesha dhahili kiasi gani walivyyokuwa na imani na Dullah hasa walivyokuwa wanamshangilia licha ya kuwa alikuwa anapoteza mipira mara kwa mara na hakuweza kufunga gori lolote katika mazoezi siku hiyo.
"Vipi Dullah uko sawa"
aliuliza kocha mara baada a mazoezi kuisha
"Niko sawa tu kocha ila sijui kwanini leo mwili wangu umekuwa mzito sana"
"au jana ulilala na shemeji nini kakunyongh'onyesha!"
"hahahaaa Hamna kiongozi nililala na mshkaji wangu Roja hapa na leo tuliamsha manzese kama kawaida kabla ya hapa"
"Ha!! basi vizuri ila unatakiwe uende ukapime leo Maralia inawezekana ikawa imejificha na kuuchosha mwili taratibu."
"sawa Kocha"

Nusu saa mara baada ya kuongea na Kocha na kumalizika kwa mazungumzo na nasaha zilizotolewa pale uwanjani ndipo taratibu Dullah akiwa sambamba na Roja walianza kuondoka maeneo ya kiwanja mdogo mdogo ndipo kwa mbele kabla hawajakata uchochoro waliziona gari mbili zikiwa zimepaki huku ile ya mbele ambayo ilikuwa ya kifahari ikiwawashia taa ya ishara ya kuwaita na walipokuwa wanapuuza ndipo wakapigiwa hozi na na kusimama kisha walipotazama vizuri kuhakikisha kama ni wao waliokuwa wanaitwa ndipo walipohakikishiwa kwa sauti kutoka kwa mzee mmoja wa makamo aliyevaa suti nyeupe aliyeamua kutoka ndani ya gari na kusimama mlangoni na kuwaita kwa mkono na kuwahakikishia kwa kichwa kuwa wao ndio aliokuwa anawahitaji.

"Ee bwana ee twenzetu inawezekana ikawa mshua anataka kutupa shavu asubuhi subuhi"
aliongea Roja na kumshika mkono Dullah ambae awali alipuuza na alitaka kuondoka moja kwa moja getto akapumzika kwani bado kichwa chake kilibaki kwenye fikira juu ya ile ndoto na Asunta.
"Acha stress twenzetu D tukamsikilize mshua"
"Poa babu"
walianza kuelekea pale walipoitwa na macho ya Dullah yaligongana na macho ya yule mzee ambae hawakuwahi kumuona lakini moyoni Dullah alianza kuhisi tofauti baina yake na Roja kwa jinsi yule mzee alivyokuwa anawatazama hadi walipomkaribia kabisa.


ITAENDELEA
 
Mrsfulani ushauri mzuriii...! Lkn hatufanani kwenye muda ndugu yangu..! Kwasasa niko busy sana na mitahani...! 0652691819 unaweza ipata kwa urahisi
 
SEHEMU YA 15


"Hamjambo vijana?"
alianza kuwasalimia Pastor George
"Hatujambo shikamoo mzee"
"Marhaba poleni sana na uchovu wa mazoezi pia hongereni sana"
"Asante mzee"
alijibu Roja huku Dullah akiwa kimya kidogo akitafakari jicho alilokuwa anaangaliwa na yule mzee.
"Eeh nadhani wewe ndie Dullah ee."
aliuliza kiuhakika Pastor huku akimtazama Dullah.
"Ndio mzee mimi ndie Dullah"
alijibu kwa kujiamini kidogo D japo moyoni alianza kuwa na hofu na kuhisi huenda yule mzee akawa babaake Asunta.
"Basi vizuri, nimesikia habari zako na zimenivuta asubuhi hii kuja kukutazama lakini kwa bahati mbaya kuna sehemu nimepigiwa simu inabidi niwahi huko ila chukua hizi ni contact zangu naomba unipigie majira ya jioni nikuelekeze wapi tukutane nina habari njema kidogo zinazokuhusu"
aliongea Pastor George huku akitoa kikadi kilichokuwa na namba za simu na kumkabidhi D.
"Lakini samahani mzee ningependa kukufahamu kwanza"
alitamka Dullah huku akikitazama kile kikadi
"Jina langu lipo hapo juu zaidi tutazungumza kwenye simu ila usiwe na hofu kijana wangu"
alijibu Pastor huku akijitoma tena ndani ya gari.
"sawa mzee Jack"
aliaga Dullah na kunukuu jina lililoandikwa kwenye kile kikadi cha mawasiliano na kuanza kuondoka wakati huo Pastor nae aliwasha gari taratibu na kuanza kutoka eneo lile huku ile gari nyengine ikiwa imepaki palepale.
"Daah!! mwanangu zari hiloo zariii uuuuhuuuuuwwwww Najua huo mtonyo babuu"
aliongea kwa furaha Roja huku akimpiga piga mabega Dullah wakati wanachepuka kwenye uchochoro uliokuwa unaelekea mabondeni kule alipokuwa anaishi D.

* * * * * *

[['Ndie yule yule kijana mwenyewe mwenye Rasta na nishampa kadi yako ya mawasiliano nimemwambia jioni apige nimuelekeze sehemu ya kukutana, kazi kwako kijana wangu Jack nataka mumfunze adabu vizuri sana hadi aelewe then utamrekodi na utanijulisha kesho']]
"sawa baba Mchungaji haina shida, we nenda tu mimi nitakuwa hapa na nitawafatilia hadi nijue anapoishi ndipo nitaondoka."
Yalikuwa ni mazungumzo ya simu kati ya mwl, Jack na Pastor George aliyekuwa anageuza gari na kuondoka eneo lile huku Jack akiwa makini kuwatazama Dullah na Roja kule walipokuwa wanaelekea na alipohakikisha wameingia kwenye uchochoro ndipo nae alishuka haraka na kulock milango ya gari yake na kuanza kuwafatilia taratibu.

Aliwafatalia pasi na kina Dullah kutambua mpaka pale walipoingia kwenye nyumba aliyopanga D na ndipo Jack alipopitiliza na kuzuga zuga sehemu za juu kisha kurudi na kupita tena eneo lile mpaka kule alipopaki gari yake.
(''Mh!! kweli mchungaji hana masikhara na mwanae yaani kwa kazi hii ya siku amekuwa tayari kunipa milioni mbili? hahahaaa pole sana Rasta kwa yatayokukuta leo'')
aliwaza mwl, Jack pindi alipokuwa anawasha gari na kuondoka maeneo yale taratibu.

* MUDA HUO HUO *

Upande wa pili alionekana Dullah bado akiwa ana mawazo pale kitandani alipojiegesha na wakati huo Roja alikuwa kavaa taulo kwa niaba ya kwenda kuoga na alipoiona hali ya Dullah kutingwa na mawazo kidogo ilimshangaza.
"Vipi man unafikiria mtonyooo nini au bado unawawazia waliokutembelea usiku?"
"Haa! Roja we acha tu saivi namfikiria sana yule mzee ujue sipati picha"
"Kivipi sasa!!"
"Sijui lakini moyo wangu umekuwa mzito sana. Kwani we hukuona jinsi alivyokuwa ananiangalia?"
"Aaah, D acha uswahili man sasa kukuangali ndio imekuwa sababu ya kuwa na wasiwasi!!?"
"Kwanini isiwe sababu wakati awali aliniangalia kwa jicho baya."
"Mh! mi nahisi mwenyewe unajistukia tu, mbona mzee anaonekana mtu safi sana tena anamshiko si umecheki ule mkoko."
"Haya bwana Roja kwa hiyo unanishauri nimpigie hiyo jioni?"
"Kha!! we unataka uchomoe kabla hujajua anachokuitia? acha hizo D mpigie na ikiwezekana tunawachukua wana wawili watatu tunakupa kampani ukamsikilize ama vipi"
"Poa but mi nahisi isije kuwa babaake Asunta?"
"Babaake Asunta?? yupi?.. ahaaa unamaanisha demu wako Asu.."
"eeeeh"
"Mh! sidhani ila tutajua tu jioni"
aliongea Roja huku akinyanyua plastiki alilojaza maji ya kuoga na kuchukua kopo lililokuwa na sabuni ya kipande ndani yake na kutoka kwenda kuoga huku Dullah nae akikata shauri na kukubaliana na maelezo ya rafiki ake kisha kunyanyuka nae na kuanza kupiga push up mbili tatu akimsubiri Roja atoke kuoga nae aelekee huko.

* * * * * *

Majira ya saa sita za mchana anaonekana Asunta akiwa sambamba na mamaake wakitoka kwenye hospitali ya Helth King mara baada ya kuruhusiwa na daktari huku Asu akiwa amejishika tumboni kutokana na maumivu aliyokuwa anayasikia hasa sehemu za chini ya kitovu lakini mamaake hakuchoka kumfariji na kumsaidia kufungua mlango wa gari iliyokuwa inawasubiri pale nje kisha dereva aliwasha injini mara baada ya kuhakikisha wote wameingia na kufunga milango ya gari na taratibu walianza kuondoka eneo la hospitali ili kurejea nyumbani.
"Mh! mama ukweli mbona tumbo linaniuma sana sehemu hizi sijui linaumajeumaje!!?"
aliuliza Asu pindi walipokuwa njiani ndani ya gari huku akimuonesha mamaake sehemu aliyohisi hayo maumivu
"Usijali Asunta mwanangu kama alivyosema Dokta imechochewa na kutapika kwako mfululizo ila usihofu hizi dawa zitakusaidia tu utakuwa sawa."
alinena maneno ya kufariji mama Asu huku moyo wake ukimsuta kwa uongo aliokuwa ameutengeneza mbele ya mwanae.

Hata walipofika nyumbani Asunta alielekea moja kwa moja chumbani kwake na kujitupa kitandani huku akishukuru upande mwengine kwa kutosafiri na baba Askofu kwenda huko Kenya na kumuacha kipenzi wake Dullah akihaha ndani ya jiji la Dar.
Akiwa kalala kifudifudi huku pembeni yake akiwa house girl sambamba na Vero aliyedamka kuja kumuona mara baada ya kupata taarifa ya kuzidiwa kwake usiku.
"Pole sana shoga"
"Asante Vero vipi John wako hajambo"
"Yuko poa tu, Vipi sasa unavyojisikia na ilikuwaje kuwaje kwani."
aliongea Vero na kusogea jirani kabisa alipolala Asu pindi alipokuwa anamjibu.
"Mh! kiukweli Vero mawazo tu nilijukta natumbukia kwenye dimbwi zito la mawazo ndipo ghafra nikahisi kichefuchefu cha ajabu rohoni mwangu na kuanza kutapika mfurulizo hadi nikakata network."
"Mh! makubwa... sasa nini tatizo"
"aaagh! si unajua hospitali hawakosi sababu. lakini mi najiona niko sawa japo tumbo kidogo linaumauma sehemu za chini ya kitovu lakini nimepewa dawa hizi nitazotumia kwa tatizo hili ambalo wanasema limesababishwa na kutapika kwangu sana."
aliongea Asunta huku akijipindua pindua na kumfanya Vero amuangalie kwa umakini mkubwa pale alipolala hadi usingizi ulipompitia tena Asu na hapo Vero nae aliaga na kuondoka.

* * * * * *

[{'''Samahani Mzee wangu kumetokea dharula huku kwenye timu ninayoichezea kuwa kuna ugeni jioni utakuja kututembelea na kucheza mechi ya kirafiki palepale Tandale kwa hiyo naomba tuonane hata kesho asubuhi au mchana. mimi ni yule kijana Dulla}]

Yalikuwa ni maneno ya ujumbe mfupi ulioingia kwenye simu ya mkononi ya mwl Jack pindi alipokuwa amebarizi maeneo ya Sinza ambako ndiko alipokuwa anaishi.
("Khaa! mbona kaanza kuruka viunzi huyu")
alijisemea peke ake mwl Jack na kuireply ile msg ambapo alimuuliza Dullah kama ataweza waonane saa 2 usiku huku akimsisitiza ni muhimu sana na ndipo Dullah aliporeply kwa kukubali kuonana muda huo.

Na kweli majira ya jioni ndani ya uwanja wa shule Tandale sokoni lilionekana basi la timu moja ya Nairobi iliyokuwa na ziara ya wiki moja nchini ambapo ilituma maombi ya dhalula ya kucheza na Tandale mara baada ya kusikia kuwa ni moja ya timu changa inayoonekana kuimalika.
na hiyo ni baada ya timu hiyo kuchapwa bao Nne kwa moja dhidi ya Simba na kufungwa tena tatu bila dhidi ya Yanga na hapo ndipo ilipoomba kuona changamoto ya timu ile ya tandale iliyopanda daraja la kwanza msimu huo hasa mara baada ya kusikia kuwa walitoka sare na simba.

Uwanja ulijaa japo sio kivile kutokana na mechi yenyewe kuwa ya ghafra na katika mzunguko alikuwepo pia mwl, Jack aliyekwenda kwa dhumuni la kumuangalia huyo Rasta huku akimsubiria baada ya mechi akutane nae na kumfunza adabu sehemu za maficho.
Kwa upande mwengine mbali na kuwa mpenzi mkubwa wa ngumi pia mwl Jack alikuwa anapenda sana soka na alikuwa na shauku ya kuuona uwezo wa mtuhumiwa wake wa siri kabla hajaenda kumuadhibu na kipindi akiwa amekaa kwenye vijukwaa vile vya uzushi alishangaa kusikia watu wanamzungumzia Rasta wa tandale ambae walimuita pia kuwa kiboko ya Simba na wachezaji walipoingia uwanjani hakuamini kuona watu wengi wakimuonesha vidole Dullah na kumpigia makofi hali iliyozidi kumpa shauku ya kumtazama kwa makini.

Kama kawaida mpira ulipoanza Dullah alianza kuonesha vitu vyake hadimu vilivyozidi kuwaacha watu midomo wazi hata mw Jack nae alijikuta ananogewa zaidi na burudani iliyokuwa inaoneshwa na Dullah kuliko fikra alizokuwa nazo awali.
Hakuna aliyewaza wala kuamini kama Tandale nayo ingeweza kuifunga ile timu kutoka Kenya hasa kutokana na mechi yenyewe kuwa ya ghafra na hakukuwa na maandalizi yoyote lakini kwa dakika arobaini na tano za kwanza tu zilitosha kuwashangaza watanzania na kuwanyima raha wakenya mara baada ya Tandale kuwa mbele kwa mabao matatu kwa bila na yote yakitupiwa wavuni kiufundi na Mliberia wa Tandale a.k.a Rasta.
Na huyo si mwengine bali ni Dullah aliyewapagawisha wakenya na kuwachachafya anavyotaka hadi Kocha wa Tandale alipoona raha zimezidi harafu mabeki pinzani washapaniki ndipo alipoamua kumtoa Dullah dakika ya sitini akihofia wasije kumuumiza bure na kipindi anatoka pande zote za uwanja zilisikika kelele na wahuni wakiita
RAAASTA... RAAAAASTA... RAAAASTAA
Na hii yote kumpongeza na kumuonesha jinsi gani walivyokuwa wanamtamani Dullah.
"Kesho Sudy ufanye mpango wa kupata chumba kizuri chenye hadhi maeneo ya Sinza kwa niaba ya Rasta, sawa?"
"sawa bosi"
ilikuwa ni sauti ya mdhamini mkuu wa Tandale fc ambae pia alikuwa ni Diwani akimuagiza kijana wake mmoja waliokuwa wamekaa upande wa staff ule wa Tandale kipindi wakimtazama Dullah akitoka huku akipongezwa na wachezaji wenzake sambamba na Roja ambae alionesha furaha zaidi na kubaki anamuangalia Dullah anavyotoka huku akiwa na tabasam kubwa usoni mwake.

('''Hapa mzee kanipa mtihani mkubwa, aaagh! yaani niiharibu hazina ya taifa kwa manufaa ya mtu mmoja?''')
yalikuwa ni mawazo ya mwl Jack pindi alipokuwa anamtazama Dullah akitoka uwanjani na jinsi alivyokuwa anashangiliwa alijikuta hata yeye mwenyewe akimpigia makofi huku kichwani mwake akiwa anamtafakari na kupiga hesabu nini afanye ili aende sawa na maamuzi ya Pastor George.

Mechi iliisha mishale ya saa moja kasoro jioni na baada ya kikao kifupi cha timu ya Tandale kama ilivyokuwa kawaida watu walitawanyika huku wengi wakimfata Dullah nyuma nyuma hususani watoto waliotaka kujua nyumba gani anakaa rasta yule na hata ilipotimu saa mbili usiku baada ya kufika getto na kuoga wakati alipokuwa anatoka kuelekea maeneo ya barabarani kupata chakula cha usiku kwa mama lishe kama kawaida yake ndipo alipokutana na Roja njiani ambae nae alikuwa anakuja getto kwa D.
"Ha! bora nimekuwahi ndio unaelekea nini?"
aliuliza Roja baada ya kugongeana tano (salamu za mikono za kileo)
"wapi tena.."
"Aaag! D acha hizo we si ulinionesha meseji kuwa yule kibopa kasema saa mbili muonane?"
"Daah! mshikaji wangu nimesahau kabisaaa"
"Duh!! kweli mwanangu wewe mvivu kutumia gorden chance za kitaa daah! fanya vitu babu kama unavyofanya ndani ya dimbaaa"
aliongea Roja huku akimpigapiga mabegani Dullah wakati wakitembea wote taratibu kuelekea barabarani kule alipokuwa anaelekea D.
"poa ngoja nimcheki basi"
alitoa simu Dullah na kabla hajapiga yeye mara simu iliita na alipoangalia namba ilikuwa ileile ya Jack.
"Daah! cheki Roja mzee kaamua kubanjuka mwenyewe, mh! Hatajwi!!"
"Ndio uongee nae sasa usilembe"
alishinikiza Roja na ndipo haraka D aliipokea simu lakini kidogo alishangaa kuona sauti ya yule mzee aliyempa namba kuwa tofauti sana na vile alivyokuwa anamsikia hewani na hakuongea sana Dullah zaidi ya kuitikia tu kile alichokuwa anaambiwa na kukata simu huku Roja akiwa na shauku ya kujua alichokuwa anaambiwa best ake.
"Vipi kasemaje mshua?"
"Aagh! ajabu kweli kasema eti yuko hapo kwa tumbo amepaki gari pale wanapouza matunda ananisubiri"
"Waaoo! kumbe hapo tu, twenzetu man"
aliongea kwa furaha Roja na kumshika mkono Dullah ambae alianza kuchezwa na machale juu ya utofauti mkubwa wa sauti aliousikia pindi alipoongea asubuhi ana kwa ana na yule mzee na vile alivyomsikia kupitia simu.

* * * * * *
ITAENDELEA.....
 
SEHEMU YA 16



"'' "Baaba nakuomba Umlinde huyu binti angu na upitishe nguvu zako kupitia mkono wangu huu wa kuume niliomuwekea kichwani mwake katika jina la Yesu... Nakuomba baba uende ukatende maajabu na kuvunja vunja mawazo ya Kishetani yoote yanayoitesa akili ya binti angu na uweke utawala wako roho mtakatifuuuu... Nakuamuru wewe Shetani uliyelaaniwa utoke kwenye kifua cha Asunta mwanangu na uondoke na maradhi yote uliyomsababishia.... aaaat-shaaabalaalaaa Naiweka sasa nguvu yako Yesu Kristo iingie na izunguke mwili wa Asunta..!! Babaa nasema Eeemen kwani shetani ameshindwa sasa... Nauingiza uzima utawale ndani ya kifua cha huyu binti... Nakatakata mizizi yote ya Shetani iliyosaliaaa.. Baba nasema Asante.. Asante sana Yehovaaaaaa... Nautoa huu mkono na kuziacha nguvu za uzima ndani ya mwili wa binti angu Asuntaaa .. Aaaaah asante sana Babaa. ..." ''"
"EEEEEIMEEEEN"

Yalikuwa ni maombi mazito yaliyokuwa yanaendelea ndani ya nyumba ya Pastor George yakiongozwa nae mwenyewe akiwa na familia yake sambamba na watumishi wenzake waliomtembelea kwa dhumuni la kujua hali ya binti ake Asunta mara baada ya kusikia habari za kuugua kwake ghafra.

Maombi yalichukua zaidi zaidi ya lisaa limoja huku Pastor George akiwa kamuekea Asu mkono kichwani mwake na watumishi wengine walizidi kukemea na kuitikia maombi kwa imani kubwa bila kujua siri kubwa iliyo ndani ya nafsi ya Pastor wao waliomuamini na kumtegemea katika shughuli za kutangaza neno la mungu na Maombezi.

Baada ya maombi kumalizika majira ya saa moja za usiku ambapo yalianza saa kumi na mbili kasoro jioni, kila mtu aliamini sasa Asunta atakuwa mzima kabisa hasa baada ya kudondoka kwenye maombi na kupoteza fahamu na kuwazidisha imani kuwa ni kweli alikuwa na Mapepo na yameshatoka yote.
Pastor George aliwasindikiza wenzake nje huku akimuamuru dereva awapeleke wageni wake.
"Baba Mchungaji hongera sana daah! kweli bwana amekupa upako Mkubwa sana na unajidhihilisha siku baada ya siku"
"ha ha Moses hapa kwangu Shetani akigusa tu anamung'unyuka kama saruji hahahaaa Bwana awe nanyi"
"Ameen baba"
Waliagana kisha Pastor George akarejea tena ndani pale sebureni ambapo alikuta Asunta akirejewa na fahamu huku akiwa kapakatwa na mamaake ambae ni mkewe, na pembeni yake alikaa yule mfanya kazi wa ndani na wanae wengine wawili wa kiume ambao ni wadogo zake Asunta.

Hakuongea neno lolote zaidi Pastor alipandisha ghorofani na kuingia chumbani kwake na kuelekea moja kwa moja bafuni kisha kufungua kikabati furani cha kioo kilichojengewa juu ya ukuta wa choo mkabala na mlango wa kuingilia jirani na screen ya TV iliyokuwa chooni mule, kisha akachukua mafuta frani na kuyabusu kabla ya kuyarudisha tena na kufunga vilango vya kile kikabati kwa kikufuri ambacho funguo zake alikuwa anazihifadhi kwenye pochi yake muda wote.
("Aaaagh! Asante sana Chinedu kwa zawadi ya haya mafuta Mh! maana nilishaanza kuchanganyikiwa kama angechelewa kuamka. Inabidi nikienda tena Nigeria nimpelekee zawadi kubwa sana kama shukurani")
Aliwaza kimya kimya Pastor muda huo alikuwa amefungua koki ya maji na kuanza kujisafisha mikono pale kwenye kisink maalum cha kunawia kilichokuwa mulemule chooni.

Baada ya kumaliza na kutoka chooni ndipo Pastor George alikumbuka kitu na kunyata kwa nje ya chumba hadi kwenye ngazi na kuchungulia kule chini sebureni na kuona bado hakukuwa na dalili ya mtu yeyote kunyanyuka na kupandisha juu kwani wote walikuwa bussy na kuangalia tv iliyokuwa inatangaza taarifa ya Habari.
Alirudi tena chumbani Pastor na kuchukua simu yake kisha kumpigia mwl Jack huku moyo wake ukiwa na shauku ya kujua kilichojiri.

* * * * * *

Baada ya kufika kwa Tumbo pale walipokuwa wanauza matunda kama walivyoelekezwa, Dullah na Roja waliweza kuiona gari ndogo aina ya Toyota Mark2 ikiwa imepaki huku mlango mmoja ukiwa wazi na walimuona mtu mmoja aliyejengeka vizuri sehemu za kifua huku mikono yake ikiwa imejichora misuli ikionesha dhahili alikuwa ni mwanamazoezi na mnyanyua vitu vizito aliyekomaa.
"Ohoo karibuni kina Dullah ni hapa"
aliongea yule mtu ambae alikuwa ni mwl Jack na kuwastua kina Dullah waliokuwa wanapepesa macho huku na huko wakiitafuta gari kama ile waliyoiona asubuhi.
"Ahaa asante za saa hizi kaka"
alilianzisha Roja huku Dullah akijiweka nyuma nyuma kutokana na Machale yake yaliyokuwa yanamcheza cheza na hii ilikuwa tabia yake ya muda mrefu sana toka angali mtoto, Dullah alikuwa na machale sana na hata ndoto zake mara nyingi zilikuwa na mafumbo yaliyozunguka ukweli wa kitu japo tatizo hakuwa mfatiliaji sana.
"Karibu Dullah mbona una wasi wasi"
aliongea tena bashasha na tabasam mwl Jack na kuzidi kumshangaza Dullah kwa kumtambua lakini hakujali nae alijichekesha na kusogea jirani.
"Najua unashangaa sana kutomkuta mzee but mi ni kijana wake na amenipa maagizo yote naomba ingieni kwenye gari tuzungumze kidogo"

Roja alimuangalia Dullah ambae alionesha kusita kidogo akiwa kama mtu anaetaka kuuliza kitu ndipo Roja alipom binya mguu kwa kumkanyaga kisha kumpa ishara waingie tu wasikilize kwani hakuna ubaya wataoweza kufanyiwa na mtu yule maeneo yale ya kwao na ya kujidai tena hata muda walivyokuwa wanakuja wahuni wote waliopisha nao njiani waliwapa saloot na hata wale wauza matunda walikuwa wanawatazama.

Waliingia ndani ya gari sambamba na mwl Jack ambae alikuwa bado hajajitambulisha zaidi ya kusema ni kijana wa mzee waliyeongea nae asubuhi, na katika hali ya kuwathibitishia kuwa alikuwa mtu mzuri tu kwao na kwa kumuondoa wasi wasi aliohisi kuwa nao Dullah aliamua kuacha mlango wake wa mbele wazi na kukaa huku miguu akiwa kaielekezea nje na kuwageukia kina Dullah waliokaa nyuma.
Lakini kabla hajaongea chochote simu ya mwl Jack iliita na alipoitazama alisita kwanza kuipokea baada ya kuona ni Pastor George ndie aliyekuwa anapiga.
Hali ile ilimfanya Dullah amfinye kimya kimya Roja na kumpa ishara kuwa lazima kuna kitu kinaendelea tu na hata Roja mwenyewe alianza kuhisi hivyo baada ya uso wa yule mtu kubadilika kidogo na kubaki akiitazama ile simu inavyoita mithili ya mtu aliyekuwa anafikilia cha kusema pindi atapoipokea ama hakutaka wamsikie atachoongea.

Simu iliita hadi ikakatika na ndipo mwl Jack aliamua kuizima kabisa na kuwageukia kina Roja ambao walikuwa wanamshangaa.
"Ah, samahani kidogo jamani tuachane na kelele za simu tuanze mazungumzo yetu"
alikata ukimya mwl Jack huku akiwatazama kina Dullah walioonesha tabasam bandia ingawa mioyoni tayari walishaanza kutia shaka.
"Sasa ni hivi, mimi naitwa Jack naishi sinza ni kijana wa hiyari wa mzee mlioonana asubuhi, wewe nakutambua ni Dullah ila wewe bado sijakujua."
alianzisha mazungumzo mwl Jack.
"Mi acha nijitambulishe mwenyewe, naitwa Roja rafiki mkubwa wa Dullah hapa uwanjani hadi mtaani"
"Okey bwana Roja pamoja na Dullah naomba mnisikilize kwa umakini sana. Kwa kuongezea ningependa zaidi kuwatoa hofu hususan Dullah"
"Hamnaaa kaka, mbona mi niko sawa tu.. Endelea"
alinena kiunagaubaga Dullah na kujieka sawa huku akijilazimisha kuonesha hana hofu yoyote na ndipo Jack akaendelea kuzungumza.
"Ok sawa basi kwanza napenda nikupongeze Dullah kwa kipaji kikubwa ulichojaaliwa na Mungu na ni ukweli ambao sikupaswa nikujuze lakini nahitaji uelewe kuwa kipaji chako kimesaidia sana kunishawishi nigeuze azma yangu niliokuwa nayo awali, ninaposema mimi ndie Jack namaanisha kuwa hata hiyo namba aliyokupa yule mzee mimi ndie mmiliki."
"Hee!!! bro mbona unatutisha sasa"
alidakia Roja
"Hapana, silengi kuwatisha ila namaanisha kilichokuwa kinaendelea na mlengwa mkuu ni wewe rasta Dullah na kilichotaka kukuponza zaidi ni mahusiano yako na mtoto wa Pastor."
"Mtoto wa Pastor?!!"
alitaharuki Dullah na kutazamana na Roja
"Ndio hivyo nadhani unamfahamu vizuri bint mmoja mrembo na mzuri sana mwenye rangi ya chocorate anaitwa Asunta."
"Asuntaa? Ooooo Asu. ndio namfahamu."
"Sasa yule mzee ni babaake Asu"
aliposema hivi mwl, Jack aliwafanya Dullah na Roja kubaki wanatazamana na kumgeukia tena Jack huku moyo wa D ukiongeza kasi ya mapigo mara mbili zaidi.
"Kikubwa kilichofanya hadi nikutafute ndio hiko ni agizo kutoka kwa yule mzee kwa usalama wako nakusihi achana tu na huyo bint utapata tu wengine mbona mabint wakali wengi tu, tena watakutafuta mwenyewe"
"Mh! hahahahaaa kaka labda nikwambie ukweli tu, naomba usiirudie hiyo kauli ya kuwa niachane na Asu tafadhali na hata yule mzee laiti angeuona moyo wangu ulivyo juu ya mwanae basi asingetuma maagizo haya. Mimi silengi kumtumia tu bali lengo langu kumuoa kabisa."
aliongea sasa kwa kujiamini Dullah na kumfanya mwl, Jack afikiri kidogo na kumtazama tena.
Wakati huo Roja alibaki tuli utadhani alikuwa hasikii kinachoendelea.
"sasa kama unataka kumuoa ulishafanya taratibu zipi?"
aliuliza Jack
"Mh! ukweli taratibu ni mipango na mipango ni pesa lakini tatizo muda wa kukutana na Asu ila pia niko mbioni kuwatafuta wazee wa hekima wanisaidie kufika kwao wakiwa na barua ya kuposa ili niwaaminishe kuwa sina nia ya kumchezea bint yao."
"hahahaaa Dullah unajua kwanini yule mzee hakupendi?"
"hapana sijui."
"Kwasababu hivyo ulivyo una rasta harafu unavyoishi Tandale basi anakutafsiri moja kwa moja wewe ni muhuni, mvuta bangi, pia una maisha magumu sana na utampoteza mwanae na kumuingiza katika maisha tofauti na aliyokulia"
"Lakini kaka penzi la dhati halibebwi wala kuangushwa na hivo vitu.."
"D, M i naona achana na huyo binti twenzetu,"
alikatisha Roja huku akionesha kuchukizwa na habari za yule mzee
"hapana Roja naongea kile kilicho moyoni mwangu, kaka Jack mwambie tu mzee kuwa yule rasta anampenda sana binti ake na hata binti ananipenda kweli ndio maana upendo wetu umetuunganisha licha ya kuwa renk za maisha yetu hazifanani."
aliongea Dullah wakati huo Roja alishafungua mlango ili waondoke ndipo Jack alipotabasam baada ya kugundua msimamo wa Dullah.
"Usiogope Dullah, niko upande wako naomba uzitunze namba zangu tuendelee kuwasiliana pia mi ni mwalimu wa mazoezi wa Asu."
"oooooh! kumbe we ni mwalimu wa mazoezi wa Asu wangu... hapo sasa ndio nimekufahamu vizuri na nimepata picha. Nadhani ulitumwa uje unipige kabisa ama unipasue macho lakini Mungu hakuandika hivyo na umegeuka rafiki, nashukuru sana kukufahamu kaka naomba unikaribishe siku moja nami nianze mazoezi huko."
"hahahaaa Karibu sana usijali ila kuwa muangalifu sana na kwa usalama wako zaidi kwanza hama pale ulipo sasa."
alimalizia Jack wakati huo kina Dulla walikuwa wameshashuka wamesimama nje ya gari na baada ya kuagana taratibu walianza kuondoka huku moyo wa Dullah ukiwa na amani kubwa kuliko ilivyokuwa toka asubuhi nae Jack moyo wake ulibaki na amani na kufurahi tu maamuzi aliyoyachukua huku akiwa hana hofu yoyote licha ya kuwa ameshadaka pesa kwa Pastor ili amuadabishe Dullah.
("Kwa msimamo wa huyu dogo,! Pastor imekula kwake hahaha wazuie tu watalea watoto wa kirastafarie hahahaa")
aliwaza na kucheka moyoni Jack na kuwasha gari kisha kutimka eneo lile.

* * * * * *

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 17



Pastor hakuwa na raha mara baada ya kuona simu inaita hadi inakatika bila kupokelewa na alipojaribu kupiga zaidi ikawa haipatikani lakini hakuchoka aliamua kutupa message mbili kuulizia lakini zote hazikuleta majibu.
"Kha, sasa huyu Jack vipi tena!! tuliagana vyengine kashindwa hata kunitumia ujumbe?"
alijikuta anaongea pekeake Pastor kabla hajastuliwa na sauti za viatu toka kwa mtu aliyekuwa anapandisha kule juu na alipochungulia alikuwa ni Asunta sambamba na mamaake. Hapo hapo Pastor alibadilika na kuanza kuomba kwa sauti ya wastan na kumalizia kwa kurudia rudia neno 'Emeen'
"Vipi mme wangu mbona kama ulikuwa unaonea peke yako?"
aliuliza mamaAsu
"Haa hapanaa nilikuwaaaa nilikuwaa nafanya maombi ya binafsi upande huu wa juu, vipi Asu mwanangu unajisikiaje."
"Sijambo baba nashukuru kwa kuniombea."
"Usiwe na wasi mwanangu roho mtakatifu yuko mwilini mwako anaifanya kazi yake ipasavyo. Lala kwa amani mama."
"sawa baba ila naomba mnipe simu yangu nilale nayo kama nitajisikia vibaya tena usiku niwaarifu"
aliongea kwa sauti ya upole sana Asunta na kumfanya Pastor George akose cha kumzuia zaidi ya kukubali ili kuzidi kumpa amani bint ake kwani aliamini wazi kuwa hadi muda huo huyo kijana mwenye Rasta tayari kashaadabishwa na hata simu kashanyang'anywa kama alivyoagiza.
"Hakuna shida kabisaa tena kesho nitapitia Mlimani sity nitakuletea Galaxy nyengine toleo jipya kabisa nikitoka kwenye maombezi mwanangu, mama Asu mpatie mtoto simu yake"
aliagiza Pastor George maneno yaliyoupendeza sana moyo wa Asunta huku mawazo yake yakihama kabisa na kuhamia Tandale kwa Rastaman Dullah.

Baada ya Asunta kuingia chumbani kwake ndipo Pastor na mkewe nao wakaingia chumbani kwao wakati yule house gari akifunga milango vizuri baada ya kuwakabidhi chakula walinzi kule getini kisha nae kuingia chumbani kwake akiwaacha watoto wawili wa kiume wa Pastor George ambao wao walibaki sebureni wakicheza Ps4 game.

"Mme wangu lakini ujue tulichokifanya ni dhambi kubwa?"
"Ushaanza mama Asu ushaanza."
"Sio nishaanza mme wangu ona mtoto alivyokuwa analalamika tumbo mpaka mchana...!"
"Mamam Asu sitaki unilaumu wala sitojilaumu kwa kilichofanyika kwani mbona huelewi, ile ilikuwa si mimba ya kawaida tu bali kulikuwa na pepo ndani yake.. huoni hata nilivyozama ndani ya maombi akadondoka? pale ni vita kati ya pepo lililosalia na roho mtakatifu baada ya kuingia ndani yake.. na huoni alivyoamka amekuwa tofauti eeh!! mama Asu isije kuwa na wewe pepo anakunyemelea..!?"
"Pepo!! Eeeh! lishindwe kwa jina la Yesu"
"Na lishindwe kabisaa Ameen"
aliongezea Pastor na kumfanya mkewe atulie na kuacha kuhoji tena huku upande mmoja wa akili zake akikubaliana na mumewe na kumuamini lakini upande wa pili wa moyo wake akipingana nae na kuona walichokifanya hakikustahili wala kumpendeza Mungu.

Upande wa Asunta mara baada ya mamaake kutoka na kumtakia usiku mwema alizuga kusinzia kwa dakika kadhaa na kuamka kisha kuusogelea mlango wa kuingilia chumbani kwake na kuufunga kabisa na funguo licha ya kuwa awali aliambiwa asiufunge ili iwe rahisi kama atazidiwa usiku ama atapiga simu wapate kuingia moja kwa moja.
Lakini aliamua kuufunga kwanza nia na madhumuni asije kuingia mtu kipindi yeye anazungumza na kipenzi cha nafsi yake Dullah.
Alitabasam baada ya kufunga mlango na kurudi kitandani kwake huku mapigo ya moyo wake yakibadilika pindi alipokuwa anaiandika namba ya Dullah ambayo aliihifadhi kichwani na mara simu ikaanza kuita upande wa pili na shauku ya kusikia sauti ya Dullah ikizidi kustimulate mwili wa Asu.

* * * * * *

"Mwanangu wee achana nae tuu kwanini uingie kwenye matatizo wazee wengine mamafia tuu, sasa ona mshkaji angekuwa na bomba si angeshatubong'onyoa vichwa? Sema bahati nzuri mchizi Mwana fresh tu na amefurahishwa na ulichokionesha ground sasa mi mwanangu sikushauli kabisa kuhusu huyo mtoto.."
"Roja mi huwa sibadilishi msimamo hasa ninapokuwa katika msimamo wa haki, harafu jua mapenzi hayako hivyo man, hata uniletee warembo wote wa dunia wawe mbele yangu zaidi watayaburudisha macho yangu tu kwa kuwatazama walivyo lakini moyo wangu bado utaendelea kupiga mapigo ya Asu tu kwani ndie chaguo la moyo wangu, siwezi kumuacha kaka na laiti ungekaa nae walau japo dakika tatu nadhani ungeelewa kwa jinsi nae anavyonipenda naamini yatakwisha tu ngoja nitume wazee wakaongee na mzee mwenzao turekebishe mambo."
"Daah! Mwanangu kweli we king'ang'anizi ila kwa style hiyo unaanza kunitisha kuongozana nawewe sehemu za mbali hasa nyakati za usiku kwani tayari unatengeneza balaa."
"Balaa?? balaa lipi Roja! hakuna balaa mbele ya Mapenzi ya dhati kama utaamua kunitenga mtaani kwa kigezo hiko poa tu ila naamini Mungu wangu nitakuwa nae sehemu zote yeye ni rafiki wa kweli na hamtengi mja wake hata siku moja hasa yule anayemuamini"
"Sawa D lakini usifikie huko man, kwanini umpende na kumuamini mtu kiasi hiko? tena mwanamke?? harafu ye matajiri wewe bado unaungaunga? Mi nakushauli kwanza piga soka achana nae rafiki yangu zee mafia lile litakupoteza."
"Nimesema SITAKI Rojaaaa mbona unaniudhi Man!!?"

Aliwaka Dullah na kutazamana kwa hasira na Roja huku Roja nae akiamini kuwa anachokipigania Dullah ni ujinga na kuibua mzozo baina yao pindi walipokuwa chumbani baada ya kutoka kule kwa tumbo na kupitia kwa mama lishe walipokula kabla ya kurudi mule chumbani (getto la dullah)

Mabishano yao yalikatishwa na muito wa simu ya Dullah na ambayo ilikuwa imechomekwa kwenye charge na Dullah alipoichomoa na kuangalia aliyekuwa anampigia alijikuta anaruka na kupiga ukelele wa furaha uliomstua Roja hata watu wa vyumba vyengine.
"WEWEEEEEEE YEEEEEEEAAH.."
"Nini tena Man..!!?"
"Mtoto huyu hapa sasa tena Mungu kaamua kukuthibitishia kuwa yeye ndie anayetuunganisha na kutuepushia mitihani... hahaha Mmmwaaaaa"
"Unamaanisha huyo Asu Mtoto wa mdingi mafia?"
"Huyo huyo ngoja naeka loud speaker daaah! siamini.."
('Mh! kweli D kachizika na kapatikana Duh!!!?')
aliongeaa kimoyomoyo Roja wakati akimtazama Dullah aliyepagawa kwa furaha ghafra huku akiwa amesimama na kuanza kuhesabu moja mpaka tatu na kuipokea simu kwa mbwembwe baada ya kujua kuwa ilikuwa namba ya kidani cha moyo wake Asunta a.k.a Mtoto wa Pastor

["Halloooow baby wangu Asu maamboo']
alianza kuongea kwa mbwembwe D punde tu alipoipokea ile simu kabla upande wa pili haujajibu chochote na ndipo kwa mbaali aliposikia kicheko kilichochanganyika na kwikwi mithili ya mtu aliyekuwa analia.
["Halloow Asu mbona huongei baby vipi kwema?"]
alitilia mkazo Dullah huku akitulia mara alipokuwa anatembea tembea mule ndani pindi alipokuwa anaongea huku Roja akiwa kakaa kitandani akimuangalia kwa umakini.
[["Hamna baby ni furaha tuu"]]
ilisikika sauti ya Asunta upande wa pili
["Furaha? furaha ipi tena inayokufanya hadi uliee? oooh au mzee kakubali tuoaaaneee??"]
aliuliza kwa kujipa matumaini Dullah
[["hapana baby wangu ila nitajitahidi kesho jioni nidanganye chochote ili nitoke na nitakuja kukwambia kila kitu kilichotokea huku usihofu"]]
aliongeza tena Asunta na kumfanya Dullah awe na shauku na kuona kama vile hiyo kesho ni miaka mingi sana hali iliyomfanya ajalibu kumbembeleza Asu walau amdokeze lakini Asu alimsihi na kumhakikishia kuwa kesho atafanya kila jitihada ili jioni afike.

Basi baada ya maongezi yale na mengineyo waliagana na kukata simu huku Dullah akijitupa kitandani akiwa na furaha ya kuongea na Asunta na mawazo ya ujio wa kesho yake hususani kusikia hiko kitu kilichomfanya mpaka Asu alie kwa furaha.

* * * * * *

Kulipokucha asubuhi na mapema Pastor George alikuwa mtu wa pili kugonga chumba cha Asunta na kuingia kumjulia hali akitanguliwa na mkewe ambae yeye aliingia alfajiri sana.
"Vipi mwanangu Asunta ulivyolala"
"salama tu baba Bwana Yesu asifiwe"
"Milele amina mwanangu, damu ya bwana izidi kusambaa na kukusafisha zaidi."
aliongea Pastor George huku akisogea na kukaa karibu na besela la kitanda cha Asunta jirani na alipokaa mkewe.
Aliinama Pastor mithili ya mtu aliyekuwa anafunga kamba za viatu ama anajifuta vumbi miguuni na kuchukua kitu kilichokuwa ndani kidogo ya uvungu wa kitanda cha Asunta na kukitia moja kwa moja katika mfuko wake wa suruali pasi na mtu mwengine kujua.
"Basi mama Asu mi nawahi kule nilipokwambia nitarudi muda si mrefu sana, mwanangu Asunta nawe ubaki salama usihofu kabisa kwani unae roho mtakatifu anayekutibu zaidi mwilini mwako"
aliaga na kuinuka Pastor George

Alitoka nje na kuingia kwenye gari huku akikataa kuongozana na dereva wake baada ya kuomba funguo na kumwambia kuwa angependa kunyoosha miguu kwa kuendeesha mwenyewe siku hiyo hivo hakupenda pia kuongozana na yeyote.
Baada ya hapo aliwasha gari na mlinzi akafungua geti haraka kipindi Pastor George akigeuza na kuondoka taratibu eneo la nyumba yake na kuongeza kasi zaidi pindi alipoingia barabara kuu.
Akiwa njiani alitoa kile kitu alichookota chini ya besela la kitanda mwanzoni kidogo mwa uvungu chumbani mwa mtoto wake ambae ni Asunta, kilikuwa ni kitu mfano wa simu ama radio ndogo na alibonyeza sehemu ya play na kukitupia pembezoni mwa kiti huku kwenye display yake namba zikianza kusoma hadi ikatimia dakika arobaini kipindi hiko akiwa kjwenye mataa ya Shekilango akisubiri taa za kijani ziwake zile zinazowaruhusu wale waendao Ubungo na kabla taa kuwakak ndipo aliposikia sauti ya Asunta akiongea kwa simu.
(''Daaah!! huyu mtoto hasikii haambiliki, sasaaa Jack nae ina maana kazi hajaifanya jana?!! Njoja nimuwahi anijuze kulikoni daaaah!'')
aliongea peke yake kimachungu Pastor na kukanyaga mafuta baada ya taa kuruhusu na kuelekea Ubungo.

Kumbe jana yake usiku kabla Asunta kupandisha kulala, Pastor aliwahi kuingia chumbani kwake na kutegesha i pode maalum ya kurecord na kuiweka on ili kujua kila kitachoongelewa mule ndani hususani mipango ya Asunta kama atadiliki kuwasiliana na Dullaha jambo ambalo alifauru na kuisikia sauti ya mwanae akiahidi kuwa jioni lazima akakutane na Dullah kijana marasta aliyetokea kuichefua nafsi ya Pastor.
(''Hapana nitafanya kadri ya uwezo wangu na kwa gharama yoyote kuhakikisha Asu hatutii aibu'')
aliwaza Pastor kipindi hiko alikuwa akiiweka sawa gari kwenye maegesho ya sehemu ile ambao kulikuwa na jim kubwa ya mazoezi na alifika pale akiwa na azma moja tu nayo ni kuonana na mwl Jack.

haikumchukua dakika nyingiu kukutana na mwl Jack mara baada ya kushuka kwenye gari na kuingia mule ndani kwenye Jim.
"Bwana asifiwe mwalimu"
"Milele amina baba mchungaji karibu"
"haya asante sana"
alijibu Pastor huku akimuonesha ishara ya kusogea nae pembeni mwl Jack na ndipo walipoingia chemba kidogo na kuendelea kuzungumza.
"vipi Jack naona kimya mwanangu, ulifanikisha?"
"yaaah, baba mchungaji ukweli nilifanikisha but kwa utofauti kidogo na ulivyoniagiza"
alijibu kwa kujiamini mwl Jack na kumfanya Pastor kubadilisha uso ghafra kabla hajajizuia na kuzificha hasira zake.
"aaahg! sasa umefanikishaje."
"Nimefanikisha vizuri tu Mchungaji tena kwa usalama zaidi pasi na kuvujisha damu yoyote."
"Lakini....acha utani Jack nambie ukweli "
"sijawahi kukudanganya Pastor, ila samahani naomba nikuulize baba"
"haya uliza,"
alijibu Pastor huku moyoni akiwa kafunda hasira hasa kutokana na kitendo cha Jack na majibu yake na zaidi ni swali alilouliza Jack lilizidi kumchefua kabisaa.
"Mbona yule kijana hana tabia ulizoniambia!! mi nakusihi usimkatae coz nimebaini ana mapenzi ya dhati na Asunta"
kwa mara ya kwanza Jack alimshuhudia Pastor akiwa kafunda hasira na chuki kisha akaamua kutoka moja kwa moja pasi na kumuaga.
(''Hee!! kumbe huyu mzee ndo alivyo?!!')
alijiwazia kichwani mwl Jack pindi alipokuwa anamtazama pastor George akiondoka ghafra pasi na kuaga.

* * * * * *


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 18



Akiwa ni mwenye furaha sana asubuhi ile tofauti a asubuhi kadhaa katika siku chache zilizopita Dullah alimaliza mazoezi kama ilivyoada sambambana wenzake akiwemo best ake mkubwa Roja.
Moyoni Dullah alitamani jioni ifike haraka ili aonane na Asunta apate kusikia habari hiyo mpya aliyoahidiwa na Asunta.
hata Roja alimgundua Dullah kuwa furaha yake ilichochewa sana na simu aliyopigiwa usiku wake toka kwa Asunta.
"hayahaya D naona leo mtotoo kiulainiiiii full kujinema magetoni."
"Acha zakooo weweee we unadhani wanaume wote tuna akili kama zako? tulia nikufundisheee heheheh"
waliongea na kucheka Dullah na Roja wakati huo tayari walikuwa njiani kuelekea magetoni kwa Dullah.
Lakini walipofika walishangaa kukutana na kijana wa makamo akiwa kasimama karibu na mlango wa getto la Dullah huku akiwa na bahasha mkononi na kumkabidhi Dullaha punde tu wwalipomfikia.
Hakuna aliyeelewa ni bahasha ya nini hadi pale walipoifungua na kuisoma kwa pamoja ambapo walikutana na karatasi ya barua iliyomuhusu Dullah kwa kumwambia kuwa anatakiwa ajiandae jioni yake baada ya mazoezi ya mwisho ya mchujo wa kikosi atatakiwa kuhamia maeneo ya Sinza baada ya kutafutiwa nyumba ya kuishi huko na Mdhamini mkuu wa Tandale fc.
Tofauti na Roja barua ile haikumfurahisha sana Dullah.
"Hivi hawa nimewaagiza wanitafutie sehemu ya kuishi ghaah! hizi sifa nyengine za kijinga sana Roja"
"Kwa hiyo unataka kunambia Dullah kuwa unakataa hii ofa kwa ajili ya ujio wa huyo demu?"
"kwani we unaonaje?"
"Acha ujinga Dullah usiwe boya kihivyo wewe tengeneza maisha kwanza ndipo heshima itakuja wee vipi?! kumbuka hata yule jamaa alisema ni vyema pia kuhama maeneo haya, sasa unakuwaje man? acha ujinga kupenda gani huko??"
"Sikia Roja kama unaona hili limekukera sana fanya hivi, naijibu hii barua kuwa hiyo nyumba wakupe wewe kama unaona ni mali sana."
"sio hivyo rafiki angu unapoteaa wewe huyo demu gani akuchanganye namna hiyo? pengine wenzako wanapiga kila siku na hawachanganyikiwi?"
"Roja toka unaniudhi sasa"
"Wee uchukie unune but huo ndio ukweli hayo mapenzi yako yashakuwa mafua sasa ipo siku yatakuumbua hata ukweni, oooh Asu Asu Asu Asuu watu tumeona Asusa!! mapenzi gani hayo kichefuchefu unakataa vitu vya maana, haya wee cheza na maisha tuu mi nawajua wananwake hao sio watu wa kuwaamini namna hiyo nakushauli katafute kitabu cha Wanawake ni Wauaji labda kitatanua akili zako"
"Bwanaaa eee ! Nikaushie Roja, kwanza wewe na huyo muandishi wa hiko kitabu wote akili zenu mbovu na hamjui nini maana ya Penzi la dhati hebu timua bwana kama umeamua kuniwangiaaa"

Asikwambie mtu mabishano kati ya Dullah na Roja almanusura yazue ugomvi mkubwa na laiti isingekuwa Roja kuamua kuondoka na kumuacha Dullah pekeake, basi hata ngumi zingezuka chumbani mule.

* * * * * *

["Haloo, eeh baba Askofu amani ya bwana iwe juu yako..... amina amina babaaaa saasa... Asunta amepona kabisa na habari njema ni kwamba leo hii tutaingia huko Nairobi na ndege ya jioni..... sawasawa babaaa.... ameeen ameeen......... Basi vizuri tutakutana hapo Airpot Nairobi']
Alikuwa ni Pastor George akizungumza kwa njia ya simu na Askofu yule wa Kenya aliyetakiwa kuondoka na Asunta siku chache zilizopita.

Huku akiwa anaendeesha gari kwa speed na kichwani akibeba mawazo kadhaa wa kadhaa, Pastor George alinyoosha tairi na moja kwa moja mpaka uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere na kuingia ndani yake na kukata tiketi mbili za ndege ya jioni ya Nairobi kisha alirudi tena garini.
{''Mpuuzi mmoja hawezi kuniumiza kichwa na kunivunjia heshima leo hata atapike hadi ulimi udondoke safari ya Nairobi ni lazima''}
Alijisemea Pastor George na kuwasha gari kuondoka akielekea maeneo alipokuwa anaishi huku akilini akijiona yeye ndie mshindi na atamaliza shindano muda si mrefu.

Upande wa Asunta alionekana ni mtu mwenye furaha mno siku hiyo huku akiwa anapiga story na mamaake na kuweka utani wa hapa na pale kabla hajachomekea swala la kuomba ruksa jioni yake akamtembelee rafikiake mmoja waliepoteana muda mwingi lakini mamaake aliichomoa ruhusa hiyo na kumtaka amsubiri babaake ndie amuage lakini tofauti aliporudi Pastor George kabla ya kusema nae chochote aliwaita na kuwaambia juu ya safari ya Nairobi siku hiyo hiyo na masaa machache yalikuwa yamebaki hali iliyomshangaza si Asunta tu bali hata mamaake.
"babaa, yaani unasema tunaondoka leo??"
"Ndio mwanangu Asu.."
"Aaaagh! lakini kwanini tusifanye kesho ili leo nipate nafasi nikamuone rafiki yangu wa muhimu daddy please."
alibembeleza Asunta
"Niemshasema jiandae na hii utake usitake Utaenda."
Aliongea kwa maneno makali Pastor yaliyomfanya hadi House girl aanze kutetemeka kule jikoni kwa jinsi alivyokuwa anaisikia sautiu ya Pastor ambayo siku hiyo ilikuwa tofauti mno.
"Utaenda utake Usitake uende ukasome na ukamtumikie bwana."

Aliumia sana Asunta na kubaki analia kwa kwikwi huku mamaake akimuacha kwanza na kupandisha juu kuzungumza na mumewe kujua kulikoni mbona aliondoka kwa furaha na amerudi akiwa ameghadhibika mno?
Aliingia chumbani mama Asunta na kumkuta mumewe akiwa anaoga bafuni na alipomsubiri mara baada ya kutoka alimshuhudia akitungua suti zake za bei mbaya sana na kuanza kuzivaa pasi na kusema chochote.
"Mume wangu kwani kumetokea nini? mbona umebadilika na kuchukia ghafra namna ile!!"
aliuliza mama Asunta lakini Pastor George hakujibu kitu zaidi ya kuendelea kuvaa huku akipuliza mluzi kufatisha wimbo mmoja wa kwaya uliokuwa unapigwa kwa sauti ya chini kupitia kwenye screen kubwa iliyokuwa mule ndani.
"Mume wangu jamani kwani nini kimetokea?!!"
Aliuliza tena mama Asu na ndipo safari hii Pastor alichomoa ile ipod yake iliyokuwa na rekodi ya sauti ya Asunta kisha kuipeleka mbele baada ya kubonyeza play mpaka ilipoanza kusikika sauti ya Asunta alipokuwa anazungumza kwa simu usiku na kumpa mkewe amsikie vizuri mtoto wao.
Alibaki kataharuki mama Asunta huku akimshangaa mumewe na kushindwa kugundua alitumia ujanja gani
"Sasa huyo ndie rafiki ake maalum wa umuhimu anayetudanganya."
aliongea Pastor baada ya ile sauti kumaliza maongezi na kukata.
"Mh! sasa mume wangu unadhani kumpeleka Nairobi ndo kutasaidia kumzuia wakati tayari wana mawasiliano?!"
alihoji mama Asu na kumuuliza mumewe swali ambalo halikumstua kabisa Pastor George
"Kumpeleka Nairobi ni hatua ya kwanza, hiyo ya kuzuia mawasiliano ni hatua ya pili na ni nyepesi mno."
alijibu kwa kujiamini Pastor wakati huo tayari alikuwa kashamaliza kuvaa na kufunga kamba za foengo (viatu) zake kisha kumuamuru mkewe akaandae nguo za muhimu za Asunta na amuandae kwa safari.

Alishuka chini mama Asunta na kumkuta mwanae kipenzi akiendelea kulia huku akibembelezwa na yule msichana wa kazi.
"Mwanangu Asunta usilie wala usichukie kwani babaako anakupenda sana na amefanya hivi kwa faida yako mama eeh"
aliongea maneno ya kufariji mama Asu lakini hayakutosha kutuliza kilio cha Asunta.
Hata hivyo kilio hakikumsaidia kitu Asu zaidi ya kukubali kuongozana na mamaake kwenda ghorofani chumbani mwake na kuanza kujiandaa kwa safari ile ya ghafra ambayo awali alijua ndio basi haipo tena.
"Lakini mama ujue kuwa hamnitendei haki kabisa"
aliongea kwa huzuni Asunta kipindi alipokuwa anavaa
"Hapana mwanagu amini kuwa hii ni bahati pia kwa faida yako ya maisha ya baadae"
"Sio hivyo mama, mi najua huu utakuwa ni mpango wa baba tu kuniweka mbali na mtu nimpendae kwa dhati"
"Mh sidhani kama ndio hivyo!!"
"Ndio hivyo mama ila kaeni mkijua kuwa nampenda sana Dullah wala sioni ubaya wa dini yake"
aliongea Asunta kwa msisitizo
"Unasemaje Asu? kwa hiyo unataka kusema uko tayari hata kubadili dini?"
"Kwani kutakuwa na ubaya sana mama, Mungu si yule yule!!"
"Hee!! huyo pepo naomba akuache kwa jina la Yesu, na usije kuthubutu kuongea ujinga huo mbele ya babaako mwanangu hata kama kupenda usije kufikia huko. kumbuka umempokea Bwana."
alisisittiza mama Asunta kuonesha jinsi gani hakuwa tayari kuona mwanae anakuja kubadili dini na kuwa Muislam kwa sababu ya mapenzi hata kwa sababu yoyote ile.

Baada ya Asunta kujiandaa kishingo upande na mamaake kumaliza kumpangia nguo zake kwenye begi kubwa na kumkabidhi kadi maalum ya Bank waliyokuwa wanamuhifadhia pesa kwaajili ya shule na maisha ya baadae ili iweze kumsaidia kwa matumizi yake madogomadogo pindi atapokuwa huko Kenya, na baada ya hapo kila kitu kilitolewa kwa msaada wa yule House girl na kupakiwa kwenye Land cruiser mayai iliyokuwa sehemu ya maegesho ambayo ndio ilitarajiwa kutumika kuwapeleka uwanja wa ndege.
Na baada ya masaa machache dereva aliweza kugeuza gari na kuwapeleka uwanja wa ndege Asunta na Pastor George huku wakisindikizwa na mama mchungaji (mke wa Pastor) na yule mfanya kazi wa Nyumbani (house girl)

* * * * * *

Alitulia ndani huku akiwa ni mwenye hasira baada ya kuondoka Roja ambae alimkera kwa maneno yake makali juu ya kupinga upendo anaoufuga kuhusu Asunta.
Alitafakari Dullah na kujitupa kitandani huku akimpumbaza rafiki ake moyoni kwa maneno aliyotoka kumwambia muda mfupi uliopita.
("Aaagh! potelea mbali inabidi nitulie hadi nitengeneze njia ya uhakika mimi na Asu ndipo nitapoweza kuhama")
aliwaza moyoni mwake Dullah na kuendelea kuyachekecha maneno ya rafiki ake wa kwanza kumkaribisha Tandale ambae ni Roja
("Aisee , kumbe mapenzi yanaweza kukugombanisha hata na rafiki mkubwa na wa karibu?? Daah! ila leo Roja amenikera sana kwa maneno yake ya upuuzi ila hamna noma kesho tutalisawazisha hili mazoezini")
aliendelea kuwaza Dullah na wakati huo huo simu yake ya mkononi iliita na alipoiangalia namba ilikuwa ni ya mamaake huko kijijini Tanga.
Aliipokea kwa tabasamu na kuanza kuongea
["Hallow mama shikamoo"]
[["Marhaba mwanangu kwema huko?"]]
["Kwema mama vipi nyinyi.."]
[["Sisi hatujambo baba ila ni kweli unaendelea vizuri kabisa?!"]]
["Ni naendelea vizuri mama"]
[["Kweli kabisa!!??]]
["Kweli mama mbona unanitisha! vipi..?"]
[["Hapana babaangu usiwe na hofu ila kuwa muangalifu tu katika kazi zako maana ndoto niliyoota Mmh!!"]]
["Ipi tena mama hebu nidokeze.."]
[["Nitakuhadithia siku nyengine mwanangu, kubwa nilitaka kujua hali zako tu babaangu"]]
alijibu mama Dullah na kumtoa wasiwasi mwanae
["sawa mama. Vipi mafundi wanaendeleza ujenzi?"]
[["wanaendelea mwanangu ila hela zimetuishia hivyo watapomaliza zile tofari zilizopo nadhani kwanza ujenzi utasimama"]]
["usijali mama nitawatumia pesa mwisho wa mwezi"]
[["Haya baba msalimie huyo mwenzio usiyetaka kumleta tumuone"]]
["hahaha mama bwana.. Mtamuona tuu tuombe mungu"]
[["haya baba siku njema"]]
["haya Asante mama msalimie mdogo angu"]]
Baada ya kukata simu alitabasamu Dullah kwa kuongea na mamaake ila alijiuliza sana mamaake alimuotea nini hadi akawa anamuuliza hali na maendeleo yake mara mbilimbili huku akionesha kuwa na wasiwasi.!!
Mawazo yake yalimfanya atulie pale kitandani mpaka usingizi ulipompitia na kulala.


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 19


Mlio wa muito wa simu ulioashilia kuingia kwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) ndio uliomstua Dullah kutoka kwenye usingizi mzito uliomchukua ghafra na kufanya astuke na kuchukua simu yake na kuifungua sms hiyo huku kimoyo cha shauku kikimuenda mbio akiamini kuwa huyo aliyetuma msg si mwengine bali lazima atakuwa Asunta wake akimuarifu kuwa kashafika stendi.
Lakini alijikuta akikunja uso baada ya kuusoma ujumbe ulioandikwa...
)('Oyaaa Mliberia rasta man Dullah kumbuka hata Ronaldo na Messsi wana mademu na wanapenda pia lakini hawapuuzi wala hawaachi kwenda mazoezini eti kwa sababu ya hao mademu.
Achana na demu D kwanza njoo mazoezini kumbuka ligi itaanza wiki ijayo na leo ndio mchujo wa mwisho wa vikosi')(
Hakuwa mwengine huyo aliyetuma sms bali ni rafiki ake kipenzi na pacha wake pindi wanapokuwa dimbani au kwa jina maarufu Roja.
Alisonya Dullah kwa kumpumbaza Roja na kuifuta kabisa ile msg lakini alipoangalia muda ilikuwa tayari saa kumi na moja kasoro za jioni.
Hakukuwa na missed call wala sms yoyote kutoka kwa Asunta na aliendelea kusubiri mpaka ilipotimu saa kumi na mbili kamili ambapo aliamua kukaa kwa nje na kutazama watu waliokuwa wanapitapita pale kwenye uchochoro kwa kujiaminisha huenda angemuona Asunta akimuulizia baada ya kukosea nyumba lakini hadi saa kumi na mbili na nusu bado hakukuwa na dalili yoyote ya Asunta si kupiga si sms wala hakukuonekana kupita mtu yeyote walau aliyefanana nae pale uchochoroni ambako ilikuwa ndio njia.

Alitamani atoke aende stendi lakini alihofia wasije kupishana na ndipo alipoamua kupiga namba ya Asu ile aliyopigiwa usiku lakini alipiga zaidi ya mara tatu majibu yalirudi yaleyale kuwa namba haiko hewani.
Alijifariji Dullah na kuamini kuwa itakuwa imezima charge na huenda Asu yuko njiani ila amecheleweshwa na foreni jioni ile.
Lakini taratiiibu kigiza kilizidi kuingia na alipotazama muda tayari ilikuwa saa moja juu ya alama usiku na hapo sasa alianza kujilaumu kwa kutoenda mazoezini na kuacha kupokea simu ya kocha, Kapten na mfadhili mkuu wa timu na yote kwa sababu ya kumsubiri Asunta ambae mpaka muda huo alishazidi kukata tamaa ya ujio wake.
Aliamua kuingia ndani Dullah huku akiwa na masikitiko makubwa ya kuipoteza siku kizembe kwa kutouona ujio wa Asu kukosa kuwepo mazoezini kwenye siku muhimu ya uteuzi wa vikosi na ndipo alipoamua kuvaa track yake akiwa na nia ya kwenda uwanjani akafanye mazoezi ya viungo usiku ule richa ya kuwa uwanja wao haukuwa na taa lakini aliamua kwenda kufanya hivyo hivyo kwa kuamini kuwa itamsaidia kuuchosha mwili ili ataporudi kulala asipate tabu ya kuutafuta usingizi kwani alijua asingeweza kuupata usingizi kiurahisi siku hiyo kwa mawazo mazito juu ya Asunta na timu yake ya Tandale ambayo wiki itayofata itaanza kutupa karata yake ya kwanza ligi daraja la kwanza kuwania kupanda ligi kuu msimu ujao.
Hakujua kama alichaguliwa kikosi cha kwanza ama jina lake limekatwa kwa utovu wa nidhamu aliouonesha siku hiyo kutofika mazoezini bila taarifa na kutopokea hata simu za viongozi wa club.
Akiwa anawaza huku anavaa mara mlango wa chumba chake uligongwa na moyo kumlipuka akiamini kuwa huyo si mwengine bali ni Asu wake, hivyo aliusogelea haraka mlango kwaajili ya kuufungua huku akiitika kwa sauti ya bashasha.

"Kariibuuuuu."
aliitika D huku akiufungua mlango kwa mbwembwe lakini alistuka na kutoamini macho yake mara baada ya kukutana na uso kwa uso na Kocha akiwa sambamba na wachezaji kadhaa pamoja na Roja ambae bado alionesha kuchukizwa na ugomvi uliotokea asubuhi baina yao japo alijitahidi kuzuga mbele ya kocha na kujifanya wako sawa tu.
"Karibu kocha, karibuni"
aliwakaribisha D huku nafsi yake ikiwa imetumbuka nyongo na moyo kumuenda mbio kidogo akijua lazima itakuwa Roja katoboa siri zote juu yake na Asunta kwa kocha na kaamua kuja nae kumsimanga tu na kumfumania.
"Asante bwana Dullah, vipi hali yako?"
"Sijambo tu Kocha namshukuru mungu."
"Daah! maana tuliingiwa na wasiwasi baada ya kupata taarifa toka kwa rafikiako Roja kuwa ulikuwa unajisikia vibaya majira ya mchana ngili ilikupinda na hasa tulipoona hupokei simu tulipanga tuje kukuona kwanza lakini uzuri Roja alitujuza kuwa kuna ndugu yako alikuja kukuchukua kwaajili ya kukupeleka kwa mtaalam wako huko mbagara na kama bahati muda huu tulilazimisha tu kufanya kubahatisha kama usharudi ama laah ila tunashukuru tumekukuta tena ukionesha hali si mbaya vipi ilikuwaje ulienda huko Mbagara?"
"daaah! kiukweli Kocha namshukuru sana Mungu maana mh! wee acha tu"
Aliongea Dullah na kumtupia jicho la pembeni Roja ambae alim binyia kimtindo jicho la kumsisitiza akazie anavyojua yeye humohumo
"Duh! aisee pole sana maana timu nzima tulisikitishwa kwa kutoonekana kwako mazoezini, vipi sasa upo sawasawa kwelii au!"
"Ha! niko sawa japo si sana kama unavyoona kuna dawa furani za kuchanja chale ndo iliyonisaidia kiukweli hata simu yenyewe niliisahau hapa nyumbani kwani muda alioondoka Roja mara baada ya kufika bro, ndio kama kasi ya maumivu ilizidi."
"Daaah! pole sana, lakini habari njema ni kwamba umo kwenye kikosi cha kwanza na utakuwa unacheza namba kumi"
aliongea Kocha na kuwafanya wachezaji wachache walioongozana kumuona Dullah wampigie makofi sambamba na Roja.
"Pia habari nyengine ni kwamba Kapten namba moja amepata bahati leo kulikuja viongozi wa Becker fc na wamekamilisha usajili wa mkopo na kama mambo yataenda vizuri basi watamsajili kabisa na ndipo tulipofanya kikao chengine cha dharula kilichotuchelewesha na kupiga kura za mikono harakaharaka kuwapata makapten wa muda na hivyo kuanzia wiki ijayo pindi kapten tulie nae atapoondoka nafasi yake itachukuliwa na kapten wake msaidizi bwana Roja na wachezaji wenzako na baadhi ya viongozi tumependekeza bwana Dullah uchukue nafasi ya Roja na kuwa Kapten msaidizi. Hongera sana"
makofi yalisikika tena huku Dullah akijihisi kama yuko kwenye njozi kwa kutoamini kile alichokuwa anakisikia toka kwa Kocha na kujikuta anaanza kuipoteza hali ya mawazo juu ya Asunta bila kutegemea
"Na cha mwisho hongera sana kwa kupangiwa nyumba yenye hadhi kidogo maeneo ya Sinza na sasa muheshimiwa anataka kusikia majibu ya barua aliyokuletea kuwa uko tayari kuhamia lini? nadhani kwa kuwa leo ulibanwa basi hata kesho tutapokutana utawasilisha hiyo barua ili taratibu zifanyike uweze kuhama Tandale lakini si kuhama Tandale fc hahaha"
aliongea na kufurahi kocha pamoja na wachezaji wake wachache waliokuwa wamefurika chumbani kwa Dullah na kupiga kelele za shangwe na kuzidi kumfariji Dullah na ndipo Roja aliposimama kwenda kumpa mkono Kapten mwenzake na kukumbatiana huku kila mmoja akiwa hana kinyongo na mwenzake japo Dullah alibanwa na maswali kibao kichwani mwake juu ya upeo na tabia ya ajabu aliyooneshwa na Roja kwani kwa jinsi walivyogombana asubuhi hakudhani kama angeweza kumtengenezea mazingira mazuri mazoezini licha ya kuwa alitumia uongo lakini alimuokoa na kumfanya ateuliwe kikosini na kuchaguliwa hadi kuwa Kapten msaidizi!! ilikuwa ni ajabu kwa kweli na hapo alianza kuyakumbuka maneno ya Roja mbayo asubuhi yalimkera mno lakini muda huo aliiona point yake hasa mara baada ya kutokuja Asunta siku hiyo kama ilivyokuwa ahadi yake.
(''Kweli wanawake si wa kuwaamini sana katika ahadi zao, daah! ila Roja ni rafiki wa kweli yaani kajitahidi hadi kuwazuia kuja na kunitengenezea muda hata wa kuenjoy na Asunta kama angekuja jioni daaah!!'')
aliwaza moyoni Dullah wakati alipokuwa amekumbatiana na Roja
(''Mungu msaidie rafiki angu anielewe ili asije kuumia na kupoteza malengo sababu ya wanawake daah! Dullah hajui thamani yake kweli ee Mungu mpe upeo ajitambue nafasi yake kwa wanawake'')
yalikuwa ni mawazo kwa upande wa Roja pia pindi alipokumbatiana na Dullah.

* * * * * *

Tairi za ndege kubwa la shirika la Kenya Airways zilianza kuambaa na kuiacha aldhi ya jiji la Dar es salaam mara baada ya ndege kuanza kukata mawingu mepesi na kuchukua ule usawa wa jiji la Nairobi kwa kasi iliyo jaa utulivu na amani kwa wasafiri waliokuwa ndani yake jioni ile wakitokea nchi ya Tanzania na kuelekea nchi jirani ya Kenya.
Akiwa haamini macho yake kama kweli ndio anaiacha aldhi ya Tanzania huku moyo wake ukimuuma kutenganishwa na mtu aliyempenda, msichana mrembo Asunta mtoto wa Pastor George alibaki kufumba macho na kuzuia machozi yaliyokuwa yamekinga taswira za mboni zake lakini haikusaidia na kujikuta akiendelea kulia kimya kimya huku babaake aliyekaa pembeni akiwa anamfariji kwa kumsihi asome Biblia ili iweze kumsaidia kumliwaza na upweke wa kuachana na ndugu zake akiwazuga abilia wengine wasijue sababu ya msingi iliyopelekea Asunta atokwe na machozi mfululizo ndani ya ndege.

Saa moja kasorobo jioni ndege ilitua jijini Nairobi na wasafiri walianza kushuka sambamba na Pastor George ambapo mara walipoingia maeneo ya jengo la uwanja wa ndege wa Nairobi waliwakuta wenyeji wao waliokwenda kuwapokea wakiongozwa na baba Askofu aliyefurahi mno baada ya kuwaona na wakati huo Asunta alishaacha kulia na kujitahidi kuonesha furaha ili asimtie aibu babaake japo moyoni alikuwa anaumia.
"Karibu sana mtumishi wa Mungu, Asunta mama karibu sana Nairobi"
walikaribishwa kwa furaha na baba Askofu na moja kwa moja waliongozwa hadi zilipopaki gari zilizokuja kwa niaba yao na safari ya kutoka uwanja wa ndege ilianza na hapo ndipo Asunta alianza kuamini sasa kweli yuko mbali na Dullah rasta wake mtoto wa Tandale hasa mara baada ya kufika katika jumba kubwa la Askofu na walipolala kesho yake asubuhi na mapema Pastor George alifanya msafara wa kurejea nchini Tanzania na kumuacha Asunta Nairobi kuanza maisha mapya ya chuo maalum alichounganishiwa na Askofu huku maisha yake kipindi akisoma yakiwa ndani ya jumba lile kubwa la kitajiri la baba Askofu.

Baada ya siku tatu huku akionesha ni mwenye furaha machoni japo moyoni alikuwa na kilio cha kila siku Asunta alipelekwa rasmi kuanza masomo yake ya mwaka wa kwanza katika kile chuo maalum cha sayansi na kiroho ambapo masomo yake yalihusu maswala ya kitafiti ya sayansi na ukweli katika maisha ya kiroho ili kuwasaidia wataalam mbalimbali kufanya kazi za kisayansi lakini pia kuwajengea imani ya uwepo wa Mungu ambae ndie muweza wa kila kitu.
vilevile chuo kilihusisha masomo ya tafiti mbalimbali ya uumbwaji wa dunia na vilivyomo bila kusahau tafiti za magonjwa na tiba na vitengo vya masomo mengine kedekede yanayohusu sayansi bila kusahau mafundisho ya kiimani na kumcha Mungu.

* * * * * *

ITAENDELEA
 
Ni muda gani sahihi wa kumpeleka kumtambulisha mpenzi wako nyumbani kwa wazazi na ndugu zako. Kuwa ndo mwandani wako wa masha.......!?
 
SEHEMU YA 20


Siku zilikwenda na hatimae wiki ilikatika pasi na Asunta kuonekana machoni mwa Dullah wala kupata ripoti yoyote kuhusu ujio wake na ndipo Dullah alipokubali kishingo upande kuhamia Sinza katika nyumba aliyotafutiwa na kulipiwa na Mdhamini mkuu wa Tandale fc na yote hayo yaliwezekana kutokana na ushauli wa Roja.
Ikiwa zimesalia siku mbili ligi kuanza ndipo Dullah alipoamua kumpigia simu mwl Jack na kuomba wakutane kwaajili ya mazungumzo ya dharula baina yao na ndipo Jack alipomuelekeza wakutane nyumbani kwake Sinza, na kweli majira ya saa moja usiku Dullah alielekea huko pasi na kumtaarifu yeyote hata rafiki ake Roja hakutaka ajue juu ya yeye kukutana na mwl Jack.
Baada ya kufika na kupokelewa vizuri na mwl Jack maongezi yao yalianza.
"Enhee nambie mtaalam"
alianzisha maongezi mwl Jack
"Daah kaka safi kidogo lakini hali si shwali"
"Kivipi Dullah"
"Kuhusu Asunta ukweli kaka ananiumiza sana kichwa toka mara ya mwisho aliposema angekuja tena akidai alikuwa na kitu muhimu cha kunambia lakini ndio hadi leo sijamtia machoni wala namba yake ahaiko hewani.. sijui una taarifa yoyote kaka coz mi nataka kumuoa kweli kabisa"
"Hahah, vizuri kama unawazia heri, lakini mdogo angu mi sina taarifa rasmi za Asunta toka mara ya mwisho nilipokwazana na mzee wake nae hakuonekana tena mazoezini ila kuna tetesi nilizisikia kutoka kwa John yule mchezaji wa Simba siku moja moja huwa anakujaga kupasha na sisi asubuhi kuwa amemsikia demu wake ambae ni rafiki mkubwa wa Asunta kuwa yuko Kenya kimasomo."
"KENYA!!?"
alitaharuki Dullah
"Yaah! ndo nlivyosikia hivyo, unajua nini yule Pastor ana msimamo sana na watoto wake hususani huyu wa kike."
"Daah!!"
alishusha pumzi Dullah na kushindwa kuelewa aseme nini zaidi ya kuaga japo mwl Jack alimuahidi pindi atapopata habari za uhakika angemjuza lakini kwa tetesi ile tu ilitosha kuunyong'onyesha moyo wa Dullah na kuusababishia maumivu makubwa kwa kuhisi sasa penzi lake na Asunta linaanza kuyeyuka kama barafu juani.
"Lakini usifuge mawazo Rasta, mtoto kama wako wako tu we kwa sasa komaa uwanjani utengeneze maisha, kumbuka silaha yako kubwa iliyonishinda hata mimi ni kipaji chako"
alimsisitiza mwl Jack baada ya kumsindikiza na Dullah kuitikia kwa kichwa.
Hata baada ya tafiti ya siku moja juu ya habari zile kuhakikiwa na mwl Jack na kumuhakikishia Dullah kuwa Asunta yuko Kenya zilikuwa zinagongelea zaidi na kuuzamisha msumari wa maumivu ya Penzi kwa Dullah.

Ilifika siku ya siku ambapo ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa Tandale fc kwenye mzunguko wa kwanza kuwania kufuzu ligi kuu ambapo walikuwa wanamenyana na timu kutoka Mwanza na katika mechi hiyo Dullah alionesha kiwango cha chini mno kuliko kawaida na kupoteza mipira mara nyingi zaidi pengine kuliko wachezaji wote wa Tandale hali iliyomstaajabisha kocha na kila mtu aliyemfahamu hadi mwisho wa mchezo Tandale walifungwa mbili bila.
"D mwanangu acha stress mbona huelewi best?"
"Yaani Roja wee acha tu kila nikijitahidi kupotezea najikuta nashindwa man."
"kivipi sasa"
"Kuhusu Asu Roja nimesikia yupo Kenya daah! ndio basi tenaa"
aliongea Dullah kipindi wakiwa kwenye daladala kurejea nyumbani sambamba na Roja ambae aliamua waishi wote lakini kauli ya Dullah ilimkera sana moyoni Roja na kumfanya abaki kimya hadi Dullah mwenyewe alielewa kuwa amemuuzi rafikiake lakini alishindwa kubadilisha ukweli wa moyo wake na kuucontrol.

Wiki zilisonga na mechi ziliendelea huku kiwango cha Dullah kikizidi kuporomoka na kuwavunja moyo wapenzi wa Tandale hata timu ilipokuuwa inashinda na hadi baada ya mechi sita kuchezwa Tandale iliambulia point mbili huku Dullah akiwa hajapiga shuti lolote lililolenga walau gori zaidi ya mchezo m bovu hadi siku hiyo walipokuwa wanamenyana na watani wao wa Temeke alicheza kwa dakika kumi tu kabla ya kucheza rafu mbaya na kumpasua mtu kichwa katika harakati za kuokoa mpira langoni mwao na kurusha teke mpira wa juu badala ya kichwa na kujisababishia kupewa kadi nyekundu kwa mara ya kwanza na kuighalimu timu yake kwani alifanya madhambi eneo la hatari na kusababisha penart na hapo alipokuwa anatoka tofauti na alivyozoea alijikuta anachanganyikiwa zaidi baada ya uwanja mzima kuanza kumzomea na kumuona mpuuzi huku wengine wakisema labda dawa alizokuwa anatumia ili asajiliwe zimeisha nguvu kutokana na jinsi alivyokuwa anacheza awali kabla ligi kuanza.
Roja alimuangalia rafiki ake kipindi anatoka uwanjani na kwa jinsi alivyokuwa anazomewa roho ilimuuma na kujikuta nae chozi linamdondoka kwani ni yeye pekee aliyeujua ukweli halisi wa saikology ya Dullah lakini hakujua atamsawazisha vipi mpaka arudi kwenye usawa kabisa?
(''Daah! Mapenzi gani haya mwananguu!!'')
alijisemea moyoni Roja na kugeukia uwanjani kwa uchungu huku akiangalia penart iliyokuwa inaenda kupigwa pia alipowatazama wachezaji wenzake karibu wote walionesha nyuso za kukata tamaa hali iliyomuumiza sana Kapten Roja na kujiapiza moyoni lazima akaipige msasa saikology ya Dullah atake asitake.

Penart ilipigwa na kutinga wavuni na kuwanyong'onyesha zaidi wachezaji wa Tandale hata kipute kilipoendelea walijikuta wanajichanganya licha ya Roja kujituma kwa hali na mali lakini hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa tayari Tandale walibamizwa goli saba kwa bila au kama vijana wa siku hizi wanavyoita kipigo cha wiki.
Wachezaji walitoka mikono nyuma vichwa chini huku mashabiki wachache wenye mioyo migumu wa Tandale ambao walisubiri mwanzo mwisho uwanjani wakiwa na huzuni kubwa mbali ya kuwa mashabiki wengine wengi waliondoka tangia timu yao ilipokuwa nyuma kwa mabao matatu wakiwa hawaamini kilichotokea.
Kwa upande wa Dullah yeye ndie alichanganyikiwa zaidi mara baada ya kila mtu kumuangalia kwa jicho baya na hata aliporudi nyumbani alishindwa kula na usingizi ulipaa usiku kucha aliishia kupata maluweluwe tu mpaka alfajiri alipoamshwa na Roja
"Twenzetu mazoezini D"
"Roja mi naona mpira basi."
"Whaat!!? unasema?"
"Man nitaenda tu kuomba wanifute nikafanye maisha mengine kijijini heri nikawe mkulima tuu"
"Wee Dullah hebu acha fikra potofu bwana"
"Kweli Roja, we ni rafiki mzuri sana na umenipokea vizuri sana nakuheshimu pia"
"Daaah! sasa Dulah rafiki angu ina maana na Asu wako ndio basi tena."
alimuuliza kwa kumtega huku nae akikaa pale kitandani
"Asu?? aaah! Asunta ndio basi tena sina uwezo wa kumpata"
aliongea kwa unyonge Dullah na mwili kushock baada ya kusikia jina la Asunta na kumtazama Roja kwa jicho la huzuni.
Roja alimuangalia kwa masikitiko rafiki ake kwani alijua sababu yoote ni huyo Asunta ndio imechangia akili ya Dullah kutofanya kazi moja na mwili wake na aliamua kuvunja na yeye mazoezi asubuhi hiyo ili akae aongee nae kirefu zaidi huku akifanya ujanja wa kuizunguka saikology ya Dullah kwa kusapoti uhusiano wake na Asu tofauti na awali alivyokuwa anampinga waziwazi.
"Sikia Dullah rafiki angu nahisi kumbe huna mapenzi ya dhati na Asunta."
"Nani mimi??!! Aaaah! Roja laiti ungekuwa unauona moyo wangu unavyofanya pindi tu unapolitaja hilo jina nadhani usingethubutu kunambia hivyo. Aaagh! Nampenda sana Asunta kwa kweli"
aliongea Dullah huku nae akikaa sawa pale kitandani na kumtazama Roja kwa makini akishangaa kwanini anamuambia vile.
"Hapana Dullah wewe huna penzi la dhati."
"Roja mbona huniamini? We unataka nifanyeje hadi uelewe kuwa nampenda ASU?"
"Nataka usirudi kwenu Tanga bali ufanye mpango wa kwenda Kenya ukamtafute Asunta"
"Hee! Roja? hivi ni wewe au!? khaa... nitawezajewezaje kwenda Kenya nitaanzia wapi?"
"Ni rahisi tu na kama kweli unampenda na unahitaji kuwa na Asu naomba unisikilize na uniamini kuwa utampata tu"
aliongea Roja na kumfanya Dullah azidi kumshangaa na kutoelewa anachomaanisha
"Mbona unanichanganya Roja nitaanzia wapi sasa hadi nifike huko Kenya?"
"Kumbuka siku ya kwanza Asunta alikufata yeye mwenyewe na kuomba muongee ukiwa wapi?"
"sikuuuuu aaah! ni ile siku tulipocheza na Simba, ndio nilikuwa natoka uwanjani."
"Saafi, basi amini kwamba uwanjani ndio sehemu utayoanzia kufika Kenya"
"Kivipi?"
"Namaanisha hata nikupe pesa uende kumtafuta itakuwa ngumu kumpata kwa ukubwa wa jiji la Nairobi na nchi ya Kenya lakini ukienda kwa kutangazwa yeye ndie atayekutafuta na mtakutana tena uwanjani huko huko kama alivyokutafuta na kukutana uwanjani siku ile baada ya kuachana asubuhi bila mawasiliano wala kujua chochote kuhusu Asu lakini kupitia uwanjani uliweza kukutana nae na kufahamiana."
maneno ya Roja yalikuwa ya ajabu sana katika mawazo ya Dullah na kushangaa rafiki ake ameutoa wapi upeo kama ule.
"Ila kama hujaunga urafiki na viungo vyako basi nataka usahau kuwa na udugu na uwanja ambao ndio utakusafirisha kukutana na Asunta."
"Kivipi sasa Roja"
"Namaanisha uongee na mwili wako utulie hususani miguu yako uiambie iutumie mpira na uwanja vizuri ili ikusaidie kuonekana na kukurudishia heshima yako ili upate kufika Kenya kukutana na Asunta."
"mh! unadhani nitaweza kweli?"
"Naamini utaweza tu na usiache kumuomba Mungu ila zingatia kila siku juhudi zako uwanjani ndio tiketi ya kufika alipo Asunta"
Baada ya kuongea maneno hayo Roja alisimama na kutoka kwenda kununua vitafunwa kwa niaba ya kuchemsha chai asubuhi ile huku akimuacha Dullah akifikiria yakinifu maneno ya Roja.

* * * * * *


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 21



"Bwana Yesu asifiwe...."
(..........)
"Bwana Asifiwe Asunta"
ilikuwa ni sauti ya kijana mmoja mtanashati iliyomstua Asu katika dimbwi la mawazo pindi alipokuwa amekaa darasani.
"Ameen"
alijibu kivivu Asu mara baada ya kuangalia darasani aligundua kuwa muda wa kuwepo pale umekwisha na yule alikuwa ni mtoto wa askofu ambae pia alikuwa ndie dereva aliyekuwa akimleta chuo na kumrudisha nyumbani kila siku.
"pole sana Asu kwa uchovu maana nilifika muda kidogo nimesubiri kwenye Parking hadi nikaamua kuulizia baada ya kuona wanachuo karibu wote wameshatoka ndipo lecture wako yule mrefu alinielekeza nije nikuone huku, samahani kwa usumbufu lakini"
"Bila samahani usijali kaka Fredy"
alijibu Asu na kunyanyuka pale alipoketi na kuongozana na yule kijana mtoto wa askofu aliyeitwa Fredy mpaka zilipopaki gari na ndipo safari ya kurudi nyumbani kwa baba Askofu alipokuwa anaishi ikaanza.

Fredy alikuwa kijana handsome sana mtanashati na msomi pia alikuwa meneja wa Kampuni ya utengenezaji na uuzaji wa ving'amuzi vya TV na toka siku ya kwanza alipomuona Asunta moyo wake ulitokea kumpenda mno japo alikuwa hakumwambia chochote bado lakini alijiapiza lazima siku moja atakuwa mume halali wa Asunta.
Lilikuwa si jambo la kawaida kwa meneja na mtu mwenye wadhfa na pesa zake kama Fredy kuacha shughuli zake na kwenda kumpitia mtu chuo na kumpeleka kila siku mbali ya kuwa wanapoishi wameajili madereva si chini ya sita wawili wakiwa wa dharula lakini kwake alichukulia swala la kumuendeesha Asu ni kama bahati na aliamua kumsitisha dereva aliyetarajiwa kumpelekaga Asu chuo akimzuga kuwa ingekuwa usumbufu kuamka kila siku kumfata wakati hata yeye anapoenda kazini njia ndio ilikuwa ileile na muda wa kurudi pia aliahidi angekuwa anampitia tu bila tabu hivyo yule dereva atamuendeesha katika mizunguko mengine labda.

Lakini hiyo ilikuwa ni janja tu ya Fredy nia na dhumuni lake kuu ni kujizoesha ukaribu na Asunta ili apate kumwambia yaliyo moyoni mwake jambo ambalo aliamini asilimia mia kwamba angefauru kumpata hivyo hakuwa na haraka nae.
"Vipi leo naona hauko sawa au hali ya hewa ya Kenya inakusumbua?"
aliuliza Fred wakati wakiwa ndani ya gari njiani
"hamna kaka ni usingizi tu"
"aaah oke lakini unaonekana kama mtu mwenye mawazo pia"
"hapana nipo ok tu"
alijibu Asu mbali na kuwa kweli alikuwa na mawazo lakini hakutaka mtu yeyote ajue nini kinamsumbua.

Walifika nyumbani na kama kawaida hawakuwa na mazoea zaidi wala kupiga sana story na Fredy na hili lilikuwa ni moja ya jambo lililokuwa linauumiza sana moyo wa Fredy kwani Asunta hakuwa kama wengine pale nyumbani muda mwingi yeye alikuwa n mtu wa kujisomea tu na kukaa pekeake hakupenda kujichanganya na wenzake zaidi ya kujumuika mezani wakati wa chakula ama zile siku za Kanisani kwenye maombi.
Lakini tabia ya Asu ilimfurahisha zaidi Askofu na kuona ni bint wa kipekee sana asiyependa makuu wala kuzurula ovyo na vile alivyokuwa mstari wa mbele kwenye maombi na kusoma alizidi kufurahi moyoni mwake Askofu na kuzidisha mapenzi kwa Asu na hata mama Askofu pia alifurahi sana kuwa na binti kama Asunta na kutokana na kukosa kwao mtoto wa kike walimchukulia Asu kama mtoto wao wa kumzaa kabisa.

Kwa upande wake Asunta ukweli hakuwa anasoma sana ili aelewe ama afauru bali alikuwa anatumia vitabu na madaftari yake bila kusahau laptop kwa niaba ya kumfariji na kuuliwaza moyo wake na kupoteza fikra zake ambazo muda wote aliumia juu ya Dullah.
Alitamani kutoroka kwa baba Askofu lakini aliogopa kumtia aibu babaake na kukubali tu kuwepo pale kusoma mbali ya kuwa alikuwa anaumia sana lakini kwa mapenzi aliyokuwa anaoneshwa na kila mtu pale ndani aliipata faraja kwa upande mwengine pia.
Muda mwingi alikuwa mstari wa mbele kwenye maombi hasa pale walipoomba kimoyo moyo aliomba mpaka machozi yakawa yanamtoka lakini ukweli uliokuwa moyoni mwake aliichokuwa anaomba mpaka analia ni ili Mungu amtendee muujiza aweze kupata ridhaa ya wazazi wake ya kuishi na Dullah jambo ambalo tayari aliliona limeshashindikana kwa asilimia kubwa.

* * * * * *

Saa kumi na moja kasoro manzese darajani walionekana Dullah na Roja wakifanya mazoezi ya nguvu ya kupanda ngazi na kushuka wakiwa speed ili kuzidi kuwajenga pumzi na stamina bila kusahau kichurachura push up na mazoezi mengine kibao waliyokuwa wanayafanya kwa moyo mmoja hususani Dullah ambae safari hii alikuwa kabadilika mno mazoezini tokea alipopewa maneno ya kumpa nguvu toka kwa Roja na kubadilisha mtazamo wake ambapo safari hii kila alipokumbuka kuhusu Asunta ndivyo alivyoongeza juhudi mazoezini na umakini wa kutosha.
"Daah! Dullah eeeh, taratibu bwana unataka na kesho tusiamke nini"
aliongea Roja pindi alipokuwa anaongozwa na Dullah mazoezi ya asubuhi siku hiyo mara baada ya kuona kiwango cha ugumu wa mazoezi aliyokuwa anatoa Dullah kilizidi kawaida.

Ilikuwa ni kawaida kila wanapomaliza mazoezi ya kwao ndipo wanapoelekea uwanjani kujumuika na wenzao kufanya mazoezi ya kitimu ambayo yalikuwa yanaanza saa kumi na mbili na nusu asubuhi na mara nyingi wao ndio walikuwa wanawahi mazoezini.
Lakini safari hii kila mtu alikuwa hana mapenzi na Dullah na hata Kocha na ilipofika siku ya mechi alikaa nje akiwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa ktk mechi iliyopita na nafasi yake ilichukuliwa na mchezaji mwengine ambae siku hiyo kwa mara ya kwanza Tandale iliweza kupata ushindi wa goli moja kwa bila tena mbaya zaidi kwa Dullah goli lilipachikwa na yuleyule mchezaji aliyechukua nafasi yake na kusababisha watu kumshangilia mno.
"Umeona sasa.. Kocha alikuwa anamng'ang'ania mfuga manywele buuure na kutukosesha ushindi kila siku, ona sasa vitu hivyo!? je angekuwa anaanzishwa kila siku huyu jamaa si tungekuwa mbali."
alisikika shabiki mmoja wa Tandale akiongea na mashabiki wenzake ambao walimuunga mkono kwa kauli yake ile.
mambo yalikuwa hivyo na mazoezi yalikuwa ndio chai ya Dullah kila siku alfajiri na jioni huku akiamini kuwa kiwango chake ndicho kitachoweza kumfikisha Kenya kucheza soka ambako itakuwa rahisi kukutana na Asu wake na kufufua mapenzi yao.
Wiki iliyofata nayo akiwa bado anatumikia kadi yake benchi Tandale walionesha kiwango kizuri hswa Roja ambae dakika za mwisho alichezewa madhambi eneo la box na alipotaka kupiga ile penart aliitwa na kocha na kunong'onezwa kitu ndipo alipoenda na kuongea na yule mchezaji aliyechukua tena nafasi ya Dullah na ndipo alipoenda kupiga yeye penart badala ya Roja na kwa bahati aliifungia tena gori la ushindi Tandale na kuibuka kifua mbele na huo ndio ukawa mwanzo wa kusugua benchi kwa Dullah huku mashabiki wengi wakizidi kusahau maajabu na ufundi wa hali ya juu waliowahi kuuona toka kwa Rasta wao waliowahi kumpachika hadi jina la Mliberia kutokana na ufundi wa ajabu aliokuwa nao.

"Roja rafiki angu, mi naona ndio nishapoteza tena"
"Kivipi Dullah!"
"Aaagh, si unaona mwenyewe yule jamaa ndio kashaninyang'anya namba kila mtu haoneshi kuniamini tena... We unadhani nitawezaje kujitangaza tena?"
"hahahaaa Dullah bwana. Hizo changamoto tuu zisikuumize kichwa best we tupige tizi tuu nina imani siku moja heshima yako itarudi tena maradufu"
"Mh!! sasa itarudi vipi Roja ikiwa sipati nafasi ya kucheza?"
"Utapata tuu nafasi tena siku si nyingi usijali man. Nitajitahidi kuongea na uongozi wakurudishe kwenye kikosi cha kwanza best kikubwa usiwaze, komaa mazoezini na utapopata nafasi waoneshe kivitendo"
"Daah! poa man"
Yalikuwa ni mazungumzo ya Dullah na Roja siku moja majira ya asubuhi wakiwa wanatoka mazoezini na kurejea nyumbani.

Lakini hata hivyo wiki iliyofuata bado hali ilikuwa ileile benchi lilimuhusu Dullah na hiyo ikaendelea kwa miezi miwili mbali na kuwa timu ilikuwa haipati matokeo ya uhakika sana huku sare zikiwa nyingi kuliko ushindi lakini bado haikumshawishi kocha kumrudisha Dullah kikosi cha kwanza.
Lakini bado hali hiyo haikumkatisha D tamaa ya kufanya mazoezi akipewa motisha na swahiba wake wa ukweli Roja ambae hakuacha kumsifu na kumpa moyo.

Mara kwa mara Roja alifanya jitihada za kuongea na uongozi wa timu juu ya kupewa nafasi Dullah lakini bado uongozi ulivunja kabisa matumaini nae wakiamini huenda mwanzo alikuwa anabahatisha tu.
"Kocha, jua mechi inayokuja ni muhimu sana kwetu kupata ushindi naomba umpe nafasi"
"Roja..Rojaaa nishakwambia hapa hatuangalii mapenzi au urafiki... Dullah atatucost tuu"
"Nakuomba tafadhali kocha niamini Dullah bado yuko vizuri kilichokuwa kinamsumbua ni matatizo ya kifamilia ambayo sasa kashayamaliza"
"Hapana kwa hilo tusameheane, wewe ni Kapten wetu na tunapaswa kusikiliza mawazo yako lakini kwa hili la rafiki yako kwasasa hapana"
yalikuwa ni moja ya maongezi ya Roja na kocha wa Tandale fc siku moja baada ya mazoezi ya jioni akijaribu kumuombea Dullah nafasi nyengine ya kurudishwa kikosini lakini bado kocha aliweka ngumu.
Na kweli mechi iliyofata ilikuwa ngummu sana na Tandale iliambulia kichapo cha bao tatu kwa moja na kuzidi kupoteza matumaini ya kucheza ligi kuu msimu unaofuata.
Na zikiwa zimebaki mechi sita ili mzunguko wa kwanza kumalizika Tandale ilitakiwa kushinda mechi tano ili kujieka sehemu nzuri ya top five kwenye msimamo na nafasi ya kufuzu ligi kuu msimu ujao ambapo nafasi ya kwanza mpaka wa pili wanapanda moja kwa moja huku yule watatu wakicheza mechi na nafasi ya nne na tano, na mshindi baina yao ataungana na nafasi ya kwanza na ya pili.
Lakini kwa mwendo wa Tandale uliobadilika ghafra na kuwa wakusuasua ulizidi kumfanya Roja kuwashawishi viongozi wa timu hususan kocha kuhusu swala la kumrudisha Dullah kikosini huku akijiapiza na kuwahakikishia kuwa wanafanya makosa kumueka benchi Dullah maneno ambayo safari hii kocha aliyasikia na kuyakubali kiunagaubaga na ndipo siku hiyo baada ya mazoezi ya asubuhi kocha alitangaza majina ya wachezaji ambao wataanza kesho yake katika mechi yao ambayo itawalazimu washinde ili wawafariji mashabiki wao ambao walishaanza kuvunjika mioyo kutokana na mwendo wao wa kusua sua na katika majina ya wachezaji wa akiba Dullah alisikia jina lake likiwa namba mbili na hapo alibinywa na Roja kimtindo kwa kumkanyaga mguu akimpa ishara ya kuwa kesho yake lazima atachezeshwa tu hivyo anapaswa kuwaonesha kuwa yeye si mtu wa kuekwa benchi.

"Hii ni zawadi niliyokuandalia best uivae kwa ndani siku utayorudi uwanjani nataka utapokuwa unafunga ufunue jezi na kila mtu asome huu ujumbe ahahhaaaa wacha kabisaaaaa"
aliongea Roja pindi walipokuwa nyumbani na Dullah na kumtolea singlendi nyeupe iliyochapichwa maandishi makubwa meusi yaliyosomeka 'ROAD TO KENYA'
"Agh! Roja bwana mbona suprise?! "
"Eeeh, itakuwa style ya aina yako ya ushangiliaji na itabaki siri yetu maana halisi ya ujumbe huu"
aliongezea Roja na kumkabidhi rafiki ake singlendi ile ambayo aliichapisha yale maneno siku kadhaa zilizopita kulekule Sinza.

Na kweli kesho yake majira ya jioni kenye uwanja wa Tandale shule ambao uliboreshwa kiasi chake na mfadhili wao kwa kupandwa hadi nyasi mara baada ya kupanda daraja, watu walimiminika kuangalia kipute kilichokuwa kinaendelea baina ya Tandale na club kutoka Masasi na hadi timu zinaenda mapumziko tayari Tandale ilikuwa nyuma kwa bao mbili kwa bila.
"Dullah vaa viatu, Frenk pumzika"
ilikuwa ni sauti ya kocha iliyopenya vizuri masikioni mwa Dullah na kufunga na mara kipenga cha kuwarudisha wachezaji uwanjani kilipopulizwa watu wa Tandale na wengineo waliokuja kuangali ile mechi walimshuhudia mtu mwenye rasta ambae alipotea machoni mwao kwa muda kidogo akiingia kwa mara nyengine baada ya miezi mitatu kusugua benchi.
"Eeh! kumbe yule Rasta maboko bado yupo?"
"hapa hakuna ushindi tena kocha kashachanganyikiwa"
walisikika baadhi ya mashabiki wakiteta mara baada ya kumuona Dullah.
Lakini haikumchukua muda mrefu Dullah kuanza vitu kuwaonesha hadhila vitu vyake akiyanukuu maneno ya Roja baada ya kupokea pande zuri kutoka kwa Roja katika msitu wa mabeki ambapo aliubetua mpira na kuutanguliza kwa juu baada ya kuwadanganya mabeki na alipokutana nao mbele aliachia shuti kali sana lililomshinda kipa wa Masasi na kutinga wavuni hali iliyowaamsha kidogo mashabiki wa Tandale na hata wale waliokuwa wanaondoka maeneo ya uwanjani walirudi tena baada ya kusikia shangwe na kuona wamepata gori moja.
Kipute kiliendelea huku rasta man Dullah akiwadhalilisha wachezaji wa masasi kwa kuwapiga vyenga vya maudhi na kabla hajatupia tena goli maridadi la pili na kuzifanya timu zote kuwa sawa kwa magoli mbili kwa mbili na tayari ilikuwa dakika ya themanini.
watoto wa Tandale hawakuamini kuuona muujiza uliokuwa unaendelea uwanjani na kila Dullah alivyotuliza mpira na jinsi alivyoukokota waliiona tofauti kubwa sana iliyowapa burudani na dakika ya themanini na tisaTandale walipata free kick (mpila wa huria wa adhabu) mara baada ya Dullah kufanyiwa madhambi.
"Piga wewe, usisahau kuonesha ulichovaa endapo utafunga"
ilikuwa ni sauti ya Roja akimnong'oneza Dullah na kumkabidhi mpira na jukumu la kupiga free kick wakati uwanja mzima ulibaki kimya hata kocha wa Tandale alikuwa akisali na kuomba muujiza utendeke pindi Dullah alipokuwa anarudi nyuma kujiandaa kuupiga ule mpira wa adhabu.

'Road to Kenya' ndio maneno yaliyokuwa yanasomeka kifuani mwa Dullah baada ya kuifunua jezi yake ya juu kipindi akiwa anakimbia kushangilia goli lililoibua shangwe ya hali ya juu mara baada ya mpira wa adhabu alioupiga kiufundi kutinga moja kwa moja wavuni.
"RAAAAAAASTAAAAAAAAAA AMERUUUUUUUUUUDIIIIIIII"
Alisikika yule shabiki mkereketwa wa Tandale bwana Chidy Ng'ole akipiga ukelele huku akikimbia kuelekea mitaani akiwatangazia watu kurudi kwa Rasta wao Mliberia Dullah akiwa na furaha iliyopitiliza.
Na kila mtu si wachezaji si makocha na viongozi mbalimbali walifurahi mno na kukimbilia uwanjani kumkumbatia na kumlalia Dullah baada ya kuslide pembeni mwa uwanja kwa upendo wa ajabu wakiwa hawaamini kasoro mchezaji mmoja tu wa Tandale ambae yeye alisimama katikati ya uwanja akiwa anaangalia lile tukio huku machozi ya furaha yakiwa yanamtoka.
("Welcome back to your Kingdom D")
alijisemea moyoni huku akijifuta machozi, na hakuwa mwengine bali ni Kapten Roja

* * * * * * ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 22



- NAIROBI (KENYA) -
..................................

Siku zilienda na hatimae miezi mitatu ilitimu Asu akiwa kwenye maisha mapya ndani ya jiji la Nairobi ambapo maisha yake yalionekana ni mwenye furaha kwa nje lakini moyoni akiishi na huzuni kubwa kila siku huku akiwa hajui lini faraja yake itarejea kama zamani katika moyo wake.
Mara kwa mara aliongea na wazazi wake waliokuwa wanapiga simu kila siku na alijitahidi kuwaonesha furaha ya uongo ambayo hakuwa nayo wala hakuna mtu ambae alikuwa anajua pale walipokuwa wanaishi kwa askofu kasoro mtu mmoja tu ambae yeye alikuwa anamchunguza kwa ukaribu sana mara kwa mara bila Asunta mwenyewe kujua na hakuwa mwengine bali ni Fredy mtoto wa Askofu.

Fredy nae moyoni mwake alikuwa anaumizwa na penzi la Asunta na alikuwa anatafuta njia ya kuanzia ili apate kumwambia ukweli lakini mara nyingi alikuwa anasita na kuahilisha adhma yake kila anapopata nafasi ya kuwa na Asunta na hakujua kwa nini moyo wake huingiwa na hofu ya kuwasilisha ukweli masikioni mwa Asu ama ni kutokana vile Asunta alivyomjengea heshima kama kakaake kabisa ama wazazi wake walivyomueka nafasi Asu kama mtoto wao wa kumzaa ama kwa jinsi dini alivyoishika sana ama ni nini hasa kilichouofisha moyo wake? lilikuwa ni swali lililotesa pia kichwa cha Fredy.

("Hapana kesho iwe isiwe nitavunja ukimya tuu.")
aliwaza usiku huo Fredy akiwa chumbani kwake na kesho yake kama kawaida asubuhi alimpitisha chuoni Asunta na jioni alimpitia na walipokuwa njiani kurejea ndipo alipoanza hatua ya kwanza katika adhma yake kwa kuongoza njia tofauti na ile wanayopitaga siku zote na hili lilistukiwa na Asu.
"Kaka Fredy mbona leo tunapita barabara hii"
"aahaa, usijali Asu kuna sehemu napitia kwa niaba yako"
"Kwa niaba yangu? kivipi kaka"
"Utaelewa tu Asu nataka iwe suprise kwako "
aliongea Fredy na kuendelea kukanyaga mafuta huku Asu akiwa haelewi ni suprise gani lakini kutokana na kumuamini sana Fredy hakuwa na wasi hata kidogo.
Walifika sehemu moja kulipokuwa kumepaki magari mengi kwenye jengo moja kubwa lililoandikwa New Nairobi Supermakert ambapo Fredy baada ya kusimamisha na kupaki gari alimpa ishara Asu washuke.
"Nataka ukachague chochote utachoona kitasaidia kuupa moyo wako furaha"
aliongea huku akiwa kaachia tabasamu zito Fredy na kumshangaza kweli Asunta
"Waaaoooo lakini kaka mbona mi nina furaha tu"
"Hapana Asu wewe huna furaha kamili bali una furaha nusu"
"kwanini?"
"Kwasababu hujafanya shoping ya nguo na viatu Nairobi hebu twende bwana ukawaone wanamitindo wa kikwetu haha"
aliongea Fredy na kumshika mkono Asu na kuingia nae ndani ya ile Supermakert
('Daa, aisee huyu binti mbona nakuwa zuzu jinsi ya kumuanza!! azma yangu si kuja nae huku')
alijilaumu na kujishangaa moyoni Fredy wakati akiwa anamchagulia nguo za asili zilizokuwa zinapatikana kwenye moja ya maduka yaliyokuwa ndani ya jengo lile sambamba na viatu mikufu ya thamani na mdoli mmoja mkubwa ambao ulimchekesha sana Asunta kwani hakumuagiza amnunulie lakini vyote hivyo Fredy alivifanya kwa mapenzi yake mwenyewe,
"Basi huu ndio utakuwa unakufariji pindi utapokuwa umejifungia ndani mwenyewe"
"hahahahaaa kaka Fredy bwanaa"
walitaniana pindi walipomaliza shoping na kurejea garini na safari ya kurudi nyumbani ilianza huku Asu akiwa hajui lililokuwa moyoni mwa Fredy wala Fredy hakuwa na hakika lililokuwa moyoni mwa Asunta.

Huo ukawa ndio mwanzo wa mazoea ya Fredy pindi anapompitia Asunta majira ya jioni haendi nae nyumbni moja kwa moja zaidi alimpitisha kwenye vivutio mbalimbali kama Zoo n.k ili kurefresh kichwa cha Asunta baada ya kumuhisi kuwa ana vitu anavyoviwazaga muda mrefu japo hakujua ni vitu gani na hii ilianza kumpendeza taratibu Asunta na kumzoea na kumpenda zaidi Fredy lakini hakuwahi kuwa na hisia nae zozote za kimapenzi.
Hakujua hatma ya tabia ile ya kuzurula ndani ya jiji la Nairobi majira ya jioni na siku za week end ni nini....
Hakujua kama anajirahisisha kwenye mtego wa Fredy
Na taratibu alianza kuusahau upweke wa kuwa mbali na Dullah kwa sababu ya Fredy ambae mara zote hakuwa na haraka wala papara ya kumuonesha ana nini hasa juu yake.

Siku moja ya Week End mara baada ya kutoka kanisani Fredy alimuomba Asunta kwenda kumtembeza maeneo mengine tofauti kama ilivyo kawaida ambapo waliitumia sana wiki hiyo kuzurula hasa baada ya Askofu pamoja na mkewe kupata safari ya London ambapo walikuwa wakienda mara kwa mara kwa ajili ya vikao vya Kanisa na neno la Mungu.
Fredy ndie aliyekuwa kiongozi pekee wa nyumba na wazazi wake walimuamini mno kutokana na upeo aliokuwa nao kielimu na uwezo wa kuiendeesha Kampuni yao ya ving'amuzi kwa miaka mitatu toka amalize chuo mambo yalikuwa yanaenda vizuri mno.
Vilevile walichoamini wazazi wa Fredy kuwa Asunta na Fredy walipendana kama kaka na dada wa kuzaliwa na wote walionesha tabia nzuri sana hivyo hawakuwa na wasiwasi nao kabisa waliamini maisha yataenda vizuri hata hata kama wangechelewa sana huko London.

Lakini siku hiyo Fredy alipania haswa mara baada ya kumpeleka mbali zaidi Asunta tofauti na siku nyengine alizokuwa anazunguka nae ndani ya Nairobi ileile.
"Mh! kaka Fredy mbona leo uko kasi sana harafu hatufiki tu hiyo sehemu?"
"Usijali Asu tutafika tu nataka hadi ukimaliza masomo yako uwe umeizunguka Kenya nzima"
"Mhh!!! haya bwana"

Gari ambayo waliichukua siku hiyo ilikuwa ni Hummer na mwendo waliokuwa wanatembea ulikuwa si wa kitoto na safari yao ilikomea katika jiji la Mombasa kulipokuwa na hoteli moja kubwa ya kitalii iliyojengwa pembezoni mwa bahari ya Hindi.
"Asunta hii ndio Mombasa Kenyaaaa enjoooooooy"
alinena Fredy kwa madaha kipindi anaegesha gari sehemu husika nyuma ya ile hotel.
Mazingira yale yaliupendezesha moyo wa Asu na kujisikia furaha kwa jinsi Fredy alivyokuwa anamjali na kumpeleka kwenye vivutio tofauti tofauti ambavyo viliweza kumsaidia kumuondelea huzuni aliyokuja nayo.
"Asu hatuna aja ya kukaa humo ndani twende kwa kuleeee"
aliongea tena Fredy huku akimshika mkono Asunta na kumpeleka sehemu moja kulipokuwa na miamvuli mikubwa na vitanda vile vya kamba na bembea kwa ajili ya kupumzikia wateja mbalimbali waliokuwa wanataka kupigwa upepo ama waliochoka kuogelea na kutazama mawimbi na mandhali ya bahari ya hindi.

Walibarizi eneo lile huku wakinywa maji ya dafu na matunda mbalimbali wakati wakiwaangaalia watu mbalimbali waliokuwa wanafurahia maisha kwa pamoja hususani wapendanao waliokuwa wanaenjoy kimahaba.
"Asu unamuona yule mzungu na yule jamaa black Rasta?"
Fredy alimuonesha Asu mzungu mmoja wa kike aliyekua anacheza na kukimbizana kimahaba na muafrika mmoja mwenye rasta huku wakirushiana maji na pindi Asu alipowaangalia na kumtazama yule niga mwenye rasta mawazo yake yalihama na kujikuta anaanza kumkumbuka Rasta wake Dullah na kujikuta anajenga taswila kichwani mwake na kujiona yeye ndie yule mzungu na yule black ni Dullah.
"Asu vipi mbona umeduwaa sana kuwashangaa wale tuu.. watazame wengine wale kule wengine walee haaa yaani ule ndio upendo wa kweli au unasemaje Asu"
"Kweli kaka"
"Lakini naona kama umebadilika ghafra, au umemkumbuka shemeji..?"
"hapana kaka mbona niko sawa"
"Aaaagh! masihara hayo Asuu"
"Kweli"
"Kwa hiyo unataka kunambia huko tanzania hukumuacha shemeji ambae tayari mmeeka mipango ya kuwa mke na mume baadae..?"
aliuliza Fredy swali ambalo Asu hakulitegemea kama angekuja kulisikia toka kwa kakaake yule wa hiyari na kujikuta anababaika kulijibu moja kwa moja
"Mh! shemejii....! kwakweeliiiiii mmh!! hapana "
"hapana nini sasa Asu"
"Sina huyo shemeji yako bado Mungu hajanibarikia wa kupanga nae malengo ya ndoa pia kwanza nataka nisome"
alidanganya Asu akijua kwa kujibu vile kutapunguza maswali ya Fredy kumbe ndio kwanza alikuwa anatengeneza mwanya wa maswali mapya ya vishawishi kuhusu mahusiano hadi akaanza kushangaa nini adhma ya kakaake yule ambaye alitokea kumuamini na kumuheshimu siku zote.
"Kwa hiyo hukuwa na mpenzi kabisa au wewe ndio ulikuwa unawakataa"
"Hamna basi tu"
"sasa iwapo akitokea sasa hivi mtu anayekupenda kwa dhati mwenye nia ya kukuoa utajisikiaje?"
"Mh! kwasasa sitaki kabisa kusikia maswala hayo kwakweli moyo wangu haupo radhi kabisa"
majibu ya Asu yalizidi kumpa picha Fredy hisia alizokuwa nazo awali juu ya Asu
"Lakini Asu wewe ni msichana mrembo unayeweza kumvutia mwanaume wa aina yeyote ila toka umekuja kuna kitu nilikuwa nakuhisi unaficha na najua tu lazima kitu chenyewe kitakuwa kwenye mapenzi tu kwani karibu sekta nyengine zote nilihisi upo sawa... Nahisi Asu umetendwa na mtu uliyempenda hapo awali uongo"
"Mh!"
"Usigune Asu ni hivyo tuu, ila amini kuwa kutendwa na mtu mmoja kusikufanye uchukie kabisa mapenzi"
"Kaka Fredy naomba badilisha mada bwanaa! afu muda umeenda sana tuwahi nyumbani mi nishachoka sasa"
aliongea Asu baada ya kuona Fredy anazidi kuikomalia ile mada.

Kwa mara nyengine Fredy alihisi kushindwa kuifikia adhma yake mbele ya Asu mara baada ya kujichekesha na kubadilisha mada huku akikubaliana na Asunta kuondoka maeneo yale japo moyoni ilimuuma sana tena akijilaumu kwanini anashindwa kumtamkia direct hadi anaanza kwenye mzunguko unaomtoa kabisa kwenye mood muhusika na kumpa wakati mgumu wa kulifikia lengo.
Lakini kabla hawajaondoka Fredy aliingia ndani ya hoteli na kununua maji makubwa mawili na kwa ujanja wa hali ya juu alizuga kwa kuingia chooni ambapo alifungua kabox furani alichokuwa nacho kwenye mfuko wa suruali aliyovaa na ndani yake kulikuwa na sindano ndogo sana ambayo kulikuwa na maji furani kidogo kwenye bomba lake na kuanza kuitoboa chupa moja kwa chini na kukamulia yale maji kisha baada ya kumaliza alitupia kile kibox kwenye plastic maalum la toilet paper lililokuwa mulemule chooni na kutoka kisha kuelekea kule kwenye gari alipomuacha Asunta huku ile chupa ambayo hakuiminyia ile dawa akiwa ameifungua na kuanza kuyanywa maji yake kidogo.
(''Mungu atanisamehe lakini sasa haina budi kufanya hivi'')
alijisemea moyoni Fredy baada ya kurudi na kuingia garini huku akimkabidhi Asunta chupa ile ya maji ambayo aliichoma sindano.

Aliondoa gari kurudi Nairobi na walipokuwa njiani kimya kingi kilitawala baina yao huku uisikika muziki wa injili tu uliokuwa unakita spika za ile gari njia nzima na kutokana na uchivu Asunta alijikuta anakunywa maji yale aliyonunuliwa na Fredy mara kwa mara huku Fredy akimpiga jicho la kuibia ibia na hatimae walipoanza kukaribia Nairobi ikiwa tayari majira ya saa moja za usiku Fredy alimshuhudia Asunta akiwa amelala hajitambui hali iliyomfanya atabasam zaidi na kushukuru Fredy huku mate ya uchu yakimjaa mdomoni


ITAENDELEA
 
Sasa kiongozi fanya mambo
Hadithi yetu imekaa vizuri sasa
 
SEHEMU YA 23


- TANDALE (TZ) -

Heshima ya Dullah ilirudi mithili ya umeme unaoambaa kwenye mfereji wa maji kwa jinsi alivyokuwa anawapiga short mashabiki wa kila timu iliyokuwa inakumbana na Tandale walimuona Dullah kama mzimu kwa yale aliyokuwa anayafanya akiwa sambamba na pacha wake Roja ambae mara zote hakumuangusha pindi alipokuwa anampelekea mipira Dullah alikuwa anatia kambani tu na hata Dullah alipokuwa anamtafunia Roja na kumpa pande nae Roja alikuwa anamezesha wavuni kama hataki vile na kuzidi kuleta matumaini kwa Tandale fc kupanda ligi kuu msimu ujao mara baada ya kujikuta mzunguko wa kwanza unamalizika wakiwa nafasi ya sita kutoka nafasi ya kumi na tano walipokuwa kabla Dullah hajarudi tena mchezoni.

Ni jambo lililokuwa wazi kwa kila mtu kuwa na sio sifa za upendeleo hata kidogo pindi watu walipokuwa wanasema kuwa Tandale imebebwa na watu wawili wakimaanisha Dullah na Roja.
Japokuwa timu inakuwa na wachezaji kumi na moja uwanjani na kila mchezaji ana mchango wake katika ushindi wowote ule lakini chachu kabisa ya ushindi ilichochewa na hao watu wawili ambao walipachikwa majina ya pacha kutokana na tabia yao ya kuonekana mara nyingi wakiwa pamoja mitaani na vile walivyokuwa wanacheza pamoja uwanjani.
Gumzo lengine kubwa lililozuka juu ya Dullah ni ile style yake ya kushangilia kwa kuonesha maneno yaliyoandikwa kifuani mwa vest aliyovaa yakisomeaka ROAD TO KENYA.
Hakuna mtu aliyeelewa maana halisi ya ujumbe ule moja kwa moja zaidi ya kuzuka tetesi tofauti tofauti ambazo zote hazikuwa na ukweli wowote.

"Kesho jamani nawakumbusha kuwa saa nne ndio tutaianza safari ya Tanga kwa niaba ya mechi ya mtondogoo, naomba tujitahidini kuwahi na kila mtu aweke nia kwenye moyo wake tukacheze kwa umoja tukiwa na lengo la ushindi tu.... Dullah, Roja, Costa, Iddy, Ashraf, Amos na wengine wote tunawategemea nyinyi kutuletea heshima Tandale sawa..??"
"SAWA KOCHA"
Walijibu kwa pamoja wachezaji wa Tandale siku hiyo pindi walipokuwa kwenye kikao cha mwisho baada ya mazoezi mepesi wakipewa nasaha na kocha wao juu ya safari ya kuanza kibarua cha ngwe ya pili ligi daraja la kwaza ambapo safari hii walitakiwa kwenda kucheza na timu ya Costal union ya Tanga.

Habari ya kwenda Tanga ilipokelewa kwa aina yake na Dullah na alikuwa anaisubiria mno katika ratiba na ilipowadia siku ya siku wakiwa kwenye Coaster njiani kuelekea Tanga aliwatumia nauli na pesa za matumizi mama na mdogo wake huku akiwasisitiza wasikose kufika uwanjani siku ya mechi.
Na kweli siku ya siku ilifika na kwa mara ya kwanza akiwa na jezi ya Tandale ndani ya ardhi ya kwao Dullah aliweka gumzo la mwaka mara baada ya kuwachachafya ndugu zake bila huruma tena mbele ya mamaake na mdogoake huku kila mtu akiwa haamini kilichotokea mara baada ya mechi kulazimika na ubao wa magoli kusomeka Costal union 0 Tandale fc 5 huku magoli yote ya Tandale yakitupiwa wavuni na Dullah a.k.a Mliberia ambapo mawili kati ya hayo akitengenezewa na Roja huku mengine matatu akiyafunga kwa ustadi wake mwenyewe pale alipowachambua na kuwapepeta mabeki wa Costal mithili ya pumba kwenye ungo.

Nani ambae hakuenda kumshangilia Dullah na kumpongeza kwa kile alichokionesha?
Nani ambae aliondoka uwanjani pasi na kusimulia alichokiona kuhusu Rasta yule?
Nani ambae hakustaajabu uwezo wa Dullah?
Na hakika hakukuwapo na mtu ambae alikuwamo uwanjani akitazama mechi ya Costal na Tandale harafu asizungumzie maajabu ya Dullah pamoja na style yake ya ushangiliaji kwa kufunua jezi ya juu na kuwaonesha watu maneno yaliyoandikwa kwenye vest aliyoivaa kuwa Road to Kenya.! Hakika Dullah aligeuka kuwa homa ya ligi daraja la kwanza.
"Mwanangu hongera sana baba kumbe bado unacheza vizuri namna hii?"
"Asante mamaangu nataka tukipiga bati nyumba ipangishwe yote na mje tujumuike pamoja"
"sawa baba, vipi huyo mwenzako uliyekuwa unatuhadithia kila siku umekuja nae?"
lilikuwa ni swali toka kwa mama mzazi wa D mara baada ya kumfata pindi mechi ilipoisha lililomfanya Dullah akune Rasta zake kidogo akifikiri kitu sahihi cha kumjibu mamaake.
"Usifikirie sana mwanangu, wanawake wa Daresalama nasikia wengi sio waaminifu na hawajiheshimu sasa asikuchanganye baba kama haeleweki kuna binti mzuri mi nishakuchagulia kule kijijini na nitafurahi kama utamuoa mwanangu"
"Mamaa!!! Unasema?"
alistaajabu Dullah na kustushwa na kauli ya mamaake nusura adondoke pale uwanjani

"Dullah vipi man, hongera sana.. shikamoo mama"
"Marhaba mwanangu"
"Bila shaka wewe ndie mama mzaa chema mama Dullah wa ukwe'ee"
"hahahaaa umejuaje baba"
"Aaaaah! kwa jinsi Dullah anavyowapenda na kuwasimulia kila siku nisijue tena?!! haya mama samahani kwa kuwakatiza maongezi ngoja nikajumuike kule na wengine"
"Haya mwanangu lakini hujanambia jina lako"
"Naitwa Roja, Dullah atakuelekeza vizuri mamaa"
aliongea yule kijana aliyekatisha mazungumzo ya ghafra huku akikimbia kuelekea kule ambako wachezaji wote walikuwa wamekusanyika wakisherehekea ushindi walioupata muda mfupi.
"Daaah, mwanangu Dullah huyu kijana Roja inaonekana mcheshi sana na ni rafiki mzuri sana"
"Kwanini mama unasema hivyo"
"Uso wake, tabasam lake, maneno yake, macho yake pia hayako nyuma kuonesha kiasi gani anakupenda na kukuthamini mwanangu, ni rafiki mzuri sana"
"hahahaaa Roja bwana leo kafuraaaahi, ni kweli mama ni rafiki yangu mkubwa sana, ila umejuaje kama ni rafiki mzuri.?"
"mimi ni mtu mzima mwanangu, nimemjua mara tu alipokuwa anakuja nilimuona alikuwa hajapanga kupitia hapa. Ila alisimama alipokuona vile ulivyostuka pindi nilipokwambia swala la kukutafutia mchumba na ndipo alikuja na ucheshi kwa kubadili fikra ulizoziingiza akilini ili urudi katika hali ya kawaida kwa kuhisi endapo utakuwa vile utakosana nami ilihali ni mamaako.... Nahisi alijua nilikuwa nakusema au nakulaumu kitu ndio maana maneno yake yamekuwa yakukusifu na kukutengenezea upendo wa dhati kwangu ili kama nakusema niache hilo... Nimempenda sana yule kijana hebu muone hata ameacha kukimbia anatembea huku akigeuka kututazama"
aliongea mama Dullah na kumfanya D ageuke na kumtazama rafikiake Roja ambae kweli alikuwa anageuka mara kwa mara na kutabasam.

Walijikuta mama na mwana wakitabasama na kusahau mada waliyokuwa wanaendelea muda mfupi kabla ya kuja Roja kuvuluga na baada ya hapo kutokana na Dullah kuja Tanga kitimu na si kwa nia ya kuwatembelea aliagana na mamaake sambamba na mdogoake wa kike kwa furaha na amani kisha nae kwenda kujumuika kule kwa wenzake ambao walikuwa wanamwita kwaajili ya dua maalum ya timu ili wapate kuondoka.

"Vijana hongereni sana hakika hiki tulichokivuna leo ni heshima kubwa sana kwetu na hizi ni salamu zitazowapa hofu kila timu itayokutana nasisi katika mechi zijazo haijalishi iwe nyumbani ama ugenini....."
"Raastaaa...Raastaaa..Raaastaaaa"
walipiga shangwe wachezaji wa tandale na kumkatiza meneja wa timu aliyekuwa anawapa nasaha na pongezi mara baada ya kumuona Dullah akikimbia na kuwahi walipo ili nae kupata mawili matatu yaliyokuwa yanaongelewa pale pindi alipomalizana na mamaake
"Ooohoo Ronaldo wetu huyo Mliberia mwenyewe!! vipi mama kashaondoka?"
"ndio kocha"
alijibu Dullah huku akikaa na kupeana tano na wenzake pale chini na kusikiliza nasaha zile kisha wakaomba dua ya pamoja na hapo ndipo walipojumuika na mashabiki wachache walioenda nao pamoja kuwasapoti huku mashabiki wengine wakiwa wametangulia stend kuu kuwahi mabasi ya mwisho mwisho kurudi Dar.

'^'Cheche..Cheecheeeeche.. Mchicha Umekolea Nazi^''
'^'Cheche..Cheecheeeeche.. Tandale wazee wa Dozi^''
'^'Cheche..Cheecheeeeche.. Dullah amewasha moto^''
'^'Cheche..Cheecheeeeche.. Tanga mziki wa kitoto^''

Naam yalikuwa ni makelele ya wimbo ulioandamana na mavuvuzela yaliyokuwa yanapulizwa na mashabiki wachache wa Tandale waliojumuika na wachezaji kwenye ile Coaster ambayo ilikuwa inachochewa moto na dereva wake ambae nae alikuwa mtoto wa Tandale aliyekuwa na mbwe mbwe za hatari mara baada ya kupiga lesi za kufa mtu pindi alipokuwa anatoka maeneo yale na kuingia maeneo ya barabara kuu kulipokuwa na watu wengi hususani mashabiki wa Costal waliiangalia kwa uchungu gari iliyoibeba timu ya Tandale ikiondoka kwa shangwe kwenye ardhi ya kwao baada ya kuvuna ushindi mnono wa mabao yale matano kwa sifuri.

* * * * * *
- (KENYA) -
.......................

Aliingiza gari katika guest moja iliyokuwa kilometa chache na barabara iliyoelekea sehemu walipokuwa wanaishi ndani ya jiji la Nairobi na kushuka Fredy kulipia chumba huku akirudi na kum beba Asunta aliyekuwa hoi hajitambui kwa usingizi wa ajabu uliompitia mara baada ya dawa iliyoingizwa kwenye yale maji aliyokunywa kufanya kazi yake.
"vipi kaka ?"
"Aaagh! mke wangu pombe zimemzidi kalala kabisa na yeye ndo amefanya tushindwe kuendelea na safari acha tupumzike tu hapa mpaka pombe zimtoke aagh tabu sana"
"Daah ! pole sana."
"usijali usijali "
alijibu baada ya kuutunga uongo wa palepale Fredy pindi alipokuwa amem beba Asu na kuingia nae kwenye ile guest ambayo ilikuwa ya kawaida tu huku nyuma yake ndani kwa ndani kukiwa na bar kubwa sambamba na mziki wa bendi iliyokuwa inatumbuiza.

Mara baada ya kumlaza Asu kitandani Fredy alitumia dakika tano kumuangalia na kumsikitikia huku akijipogeza upande mmoja kwa kuamini kuwa sasa anaenda kumfaidi Asunta ipasavyo bila bugudha wala usumbufu wowote na kwakuwa ile dawa alijua inafanya kazi ipasavyo kwa masaa sita na yalibaki matano na dakika kadhaa hivyo aliamini angetumia masaa mawili kuburudika nae pale na lisaa limoja kumfikisha nyumbani tena chumbani kwake na hayo masaa mawili yaliyobaki yatapotelea kwenye usingizi wake hadi pale atapoamka na kujikuta chumbani kwake tena kalala muda mrefu tu.


ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom