HADITHI: Mtoto wa Pastor

Prince Naahjum_

Senior Member
Jun 13, 2016
139
125
MTOTO WA PASTOR

SEHEMU YA 1

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya nguvu na akili ya kuweza kufikiri na kubuni hadi kuandika hii hadithi ambayo unaisoma hii leo,
Nami nasema Ahsante Mungu kwa baraka na rehema zako.

Pili napenda kuwashukuru wazazi wangu hususani baba angu kipenzi japo umetangulia mbele ya haki lakini nakumbuka vizuri maneno yako na mafundisho juu ya maisha na vile ulivyonisapoti ktk kazi zangu za uandishi tangia nipo shule ya msingi na kunisisitiza nizidishe juhudi nisife moyo ktk hili.
Nitakukumbuka daima baba. Mungu akuhifadhi mahali pema peponi Amiyn.
Vilevile mamaangu kipenzi pia siwezi kukuweka nyuma kwa mengi mazuri uliyonifanyia na unayonifanyia hadi leo na sapoti yako kwa hali na mali, nakuombea mungu akuzidishie maisha marefu na yenye baraka.

Tatu nakushukuru wewe mdau wangu kwa sapoti yako hususani uliyejitolea kwa kunichangia kiasi chako cha pesa kununua hadithi hii nami nakuombea mema na baraka kwani najua bila ya wewe nami si lolote. Mungu akuzidishie ktk kipato chako pia nakuahidi kuzidi kukupa vitu vitamu zaidi.

Mwisho kabisa nisingependa kukuchosha kwa maneno mengi zaidi napenda nikukaribishe tuwe pamoja katika hadithi hii nzuri yenye burudani na mafunzo tele.

Karibu.

RIWAYA - MTOTO WA PASTOR
Sehemu Ya 01 hadi 30

BY - MTOTO WA BECKER
_______________________
_______________
_________________
* SHUKURANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZI MUNGU *
==================
KARIBU TUWE PAMOJA
--------------------

* * * *
DAR ~ TANDALE

likuwa ni siku ya jumatatu tulivu majira ya saa kumi na moja alfajiri katika jiji la Dar es salaam ambapo hali ya hewa siku hiyo ilikuwa na manyunyu mepesi ya mvua sambamba na kajiubaridi murua kinachoweza kumzuia mvivu asitoke mapema chumbani na kuendelea kuvuta shuka.
Walionekana watu tofauti maeneo ya vituo vya daradara na kwengineko wakiwa ktk pilikapilika zao alfajiri ile hususan wanafunzi walipenda kuamka muda huo kuepuka usumbufu wa usafiri na kukataliwa kwenye madaladala.

Katika uwanja wa michezo wa shule ya msingi Tandare kulionekana kijana mmoja mwenye rangi ya kahawia kichwani mwake akiwa na rasta pia mwili wake ulionekana kujengeka vizuri kimazoezi akiwa anatroti taratibu kurejea anapoishi mara baada ya kujiridhisha na mazoezi aliyofanya siku hiyo.
Aliingia chumbani kwake mara baada ya kufika kwenye nyumba aliyokuwa anaishi maeneo ya Kwa tumbo ambapo alichukua ndoo ya maji na kuelekea bafuni kujimwagia (kuoga) na alipomaliza alirejea tena chumbani na kuanza kujiandaa chap chap huku kichwani mwake akiwa na mawazo mengi akifikiri wapi ataanzia siku hiyo ktk safari yake ya kutafuta kazi iliyomchukua zaidi ya mwezi mzima toka ahamie rasmi jijini Dar akitokea kwao Tanga.
Hali ya maisha na upatikanaji wa kazi jijini Dar ilikuwa tofauti kabisa na alivyodhania pindi alipokuwa anapata story ya uzuri wa jiji na uwepo wa ofisi nyingi na makampuni binafsi hivyo awali alidhani atapofika tu hatopata tabu ya kupata kazi na baada ya kupata pesa ya mavuno waliyouza huko kijijini muheza aliamua kutumia kama nauli na pesa ya kupangia chumba pindi alipofika Dar huku akimuahidi mamaake kipenzi kuwa ameenda kutafuta maisha na atapopata kazi nzuri atahakikisha anawasaidia na siku moja watajenga nyumba ya bati na kuepuka adha ya kuloana kipindi cha mvua kubwa kwenye nyumba ile ya nyasi waliyoachiwa na marehemu baba ake ambapo alibaki na mamaake na mdogo ake wa kike.

"Mwanangu Dullah nakuombea kila la heri baba mungu akuongoze utapofanikiwa utukumbuke baba.."
"Usijali mama nitawakumbuka na nitakuja mara kwa mara kuwajulia hali pindi nitapopata kazi tu."

Alikumbuka Dullah walivyoagana na mamaake siku alipokuwa anaondoka walipokuwa stendi, alitabasamu alipoiangalia picha aliyoibandika ukutani ikimuonesha akiwa kijijini na mamaake na mdogo wake.
Alitoka na kufunga mlango wa getto lake kwa kufuri na kuangalia saa ya kwenye simu yake ya mkononi aina ya nokia ya tochi na tayari ilishatimu saa kumi na mbili kasorobo.

* * *
SINZA - 08;30 a.m

"Asssss.. asante sana baby wangu."
"Mmh!! asante na wewe sweety"
"Naomba usije kuniacha John, niahidi"
"Nakuahidi Vero, sitokuja kuthubutu hilo. niamini."
"Nakuamini baby.. Mmmmwaaa"

Zilikuwa ni sauti za chumbani juu ya kitanda kikubwa ambapo alionekana msichana mrembo Veronica akiwa kalala juu ya kifua cha kijana mcheza mpila maarufu aliyeitwa John huku wakiwa kama walivyozaliwa mara baada ya shughuli pevu alfajiri ile.

"Leo ndio umesema mtakuwa na mechi ya kirafiki hapo Tipi..!"
Aliuliza Vero huku akimchezea kifua John.
"Agh! kuna hako katimu Tandare kapo daraja la pili kalituomba mechi ndio leo. si utakuwepo baby"
"Nitakuja dear tena yule shogaangu anakusalimia sana"
Aliongea vero na mala simu yake iliyokuwa juu ya dressing table mule ndani iliita na ndipo aliponyanyuka huku akiwa vilevile mtupu na kuelekea lilipo dressing table huku John akibaki anaangalia makalio makubwa ya Vero jinsi yalivyokuwa yanapishana na kuleta vibrate za hatari zinazoweza kuamsha ashki hata za kikongwe.

"Hallow, Asunta.. Mh! shogaangu kweli una maisha marefu yani tumekuzungumzia na shemeji yako sasaivi... Eeeh!! hallooow... halooow Asunta!!?"

Uso wa Vero ulibadilika ghafra na kumshtua John.

"vipi baby..?"
Aliuliza John na kukaa vizuri pale kitandani.
"Mh! Asunta amepata tatizo gari yake imepata pancha alipokatisha njia ya Tandare kwa tumbo kwa kuhofia foreni sasa sielewi simu yake kabla haijakata nimesikia upepo na kelele. twende tuwahi labda kuna tatizo lengine limetokea.."

Aliongea Vero na John kusimama haraka wakavaa na kutoka nje ambapo waliingia kwenye gari yao ndogo na safari ya Tandare kwa tumbo ilianza.

* * * * * *

Akiwa anamalizia uchochoro wa mwisho kutokea barabara ndogo ielekeayo tandare sokoni ikitokea kwa tumbo, na ndipo ghafra Dullah alisikia ukelele wa msichana wa kuomba msaada na mbele yake aliwaona vijana wawili wakikimbia kuelekea upande ule wa uchochoro aliokuwa anatokea yeye huku mmoja wa wale vijana akiwa ameshika simu kubwa ya tachi mkononi mwake na kwa haraka Dullah alibaini kuwa wale vijana walikuwa ni wezi na kutokana na nafsi yake kuchukia sana vitendo vya uhalifu hususani wizi alijikuta anamtegea mguu kimakusudi yule kijana wa mbele na kuanguka kisha alimpiga ngumi ya shingo yule mwengine alipomruka mwenzake eneo lile na kabla hajatua chini alimdaka mkono na kumpora ile simu.

"Aaaaaghhhhh! Rasta tukaushieee bwanaa.."

Alipiga kelele mmoja wa wale vijana aliyebinywa ipasavyo na Dullah na kumfanya mwenzake asimame na kukimbia kwa woga.
Mwishoe alimuachia na yule mwengine na kumuonya waache tabia ya kutaka vitu kirahisi inabidi watafute kazi ya kufanya.

"Asante sana kaka Mungu akubariki.."
aliongea yule dada pindi Dullah alipomrudishia ile simu yake baada kuwadhibiti wale vijana na kuichukua ile simu aina ya Galaxy.
"Usijali dada pole sana, vipi una tatizo?"
"Yah, gari yangu imepata pancha na tairi la akiba na jecki vipo lakini siwezi kufunga na nilipokuwa napiga simu kumwita mtu wa kunisaidia ndio wale vijana wakanipora kwa kunishtukiza."
"Daah! pole dada but usijali nitakusaidia.."
Aliongea Dullah na kufunguliwa bonet na yule dada na mara baada ya dakika kumi na tano alikuwa kashamaliza kazi hadi yule binti akashangaa.

"Hapa kila kitu safi sasa unaweza kuendelea na safari yako"
"Asante sana kakaangu asante.. "
Alishukuru yule bint na kutoa noti tano za elfu kumi kumi na kumkabidhi Dullah
"Daah nashukuru sana dada lakini umenipa kiasi kikubwa sana tofauti na kazi yenyewe"
"Usijali kakaangu kwani wewe umefanya kazi kubwa mno huoni ningepoteza mawasiliano na watu wengi sana muhimu, hiko chenyewe nilichokupa hakifiki hata robo ya thamani ya hii simu.. bahati mbaya sina hela tu leo."
"sawa dadaangu, nakutakia safari njema ila kuwa makini siku nyengine.

Waliagana na Dullah kuendelea na safari yake kuelekea stendi kwa tumbo.

ITAENDELEA
 
MTOO WA PASTOR

SEHEMU YA 2

MIDA HIYO HIYO

Gari ndogo aina ya toyota prado ilisimama baada ya kuiovatake ile aliyokuwemo yule binti kipindi alipoanza kuondoka nae alipaki pembeni mara baada ya kuitambua ile gari.

"Aaah.. Jamani Asunta umenitisha sana.."
Aliongea Vero pindi aliposhuka kwenye ile prado nae yule binti ambae kumbe ndie Asunta alishuka na kukumbatiana huku wakimuacha John akiwa kaegamia mlango wa gari akiwaangalia.

Asunta aliwasimulia haraka haraka kwa kifupi ilivyokuwa na wote kustaajabu ukalimu wa huyo kijana kwani ni Nadra sana ukipolwa Tandale kupata msaada wa kurudishiwa kitu chako na mkazi wa tandale.

"Yaani wee acha tuu kaka mwenyewe ni yulee.."

Aliwaonesha eneo la stendi nao walipotazama hawakumuona vizuri sura zaidi walishuhudia Rasta tu za Dullah pindi alipojitoma ndani ya daradara iliyokuwa inaelekea ubungo kwa nia ya kuendelea kutafuta bahati yake ya kupata kazi.

Waliingia kwenye magari yao ambapo Veronica alijumuika na shogaake Asunta huku John akirudi pekeake kwa nia ya kwenda kuungana na wenzake mazoezini asubuhi ile na walipoongozana waliachana njia panda ya barabara kuu kina Vero wao walielekea sehemu nyengine wakiahidi kujumuika pamoja uwanja wa Tipi jioni yake.

Upande wa Dullah hakuamini kabisa kama asubuhi ile anaweza kupata kiasi cha pesa namna ile kwani tayari awali alikuwa na mawazo vipi ataishi kama siku zitazidi kupita pasi na yeye kupata kazi..!
Gari ilipofika kituo cha stendi ya mabasi yaendayo mikoani Dullah alishuka na moja kwa moja alielekea kule stendi lengo likiwa si kusafiri bali ni katika harakati zake za kutafuta kazi.
Na mara baada ya kuingia ndani aliangaza huku na huko na ndipo alipoamua kumfata kijana mmoja wa makamo yake aliyevaa t shirt iliyokuwa na maandishi makubwa yaliyosomeka SUMRY ikiwa ni moja ya majina ya kampuni ya mabasi yaendayo mikoani.

“Habari za asubuhi best”
“Poa poa mwanangu wapi Iringa, Dom, Mwanza au Bukoba?”
Aliuliza yule kijana chapchap huku akifungua kitabu cha tiketi pindi tu Dullah alipomfata na kumsalimia.
“Hamna kaka mi sisafiri ila nilikuwa na kashida kidogo naomba unisikilize”
Aliongea Dullah kwa sauti ya utulivu na busara ya hali ya juu.
“Tungamana basi nimalizane na abilia .... eeh mama mwanza au Bukoba..”
Alijibu kwa lugha ya kihuni kidogo yule kijana na kuendelea na shughuli nyengine na Dullah alitulia kumsubiri kwanza kama alivyomuelekeza.

Ilipita nusu saa Dullah akiwa amesimama pale huku yule kijana akiwa anapita pita na kazi zake nyengine hadi ile basi ikaondoka na kuendelea kukata tiketi kwenye basi nyengine na abiria walipokuwa wamepungua huku yule kijana akiwa haoneshi hata dalili kama kuna mtu alimwambia amsubiri ndipo Dullah alipoamua kumfata na kumkumbusha.

“Ndio ndugu yangu bado nilikuwa nakusubiri naona umeshasahau.”
“Hee!! Kumbe bado upo mwana.. poa ongea harakaharaka si unajua asubuhi hii..”
“Ndugu yangu mi shida yangu kubwa ni kazi, natafuta kazi na kwa kuwa we kijana mwenzangu nimekuona unaweza kunisaidia hata kunielekeza kama naweza kupata wapi kazi humu ndani..”
“we kwani ulikuwa unatafuta kazi gani..”
“Yoyote tu kaka.”
“Sasa sikia lete elfu kumi kwanza ili nimuachie mtu hiki kitabu tuongee pembeni kidogo..”
Aliongea yule kijana huku akimuangalia kwa umakini Dullah nae Dullah kwa kuwa alikuwa na uchu wa kazi alitoa bila hiyana kiasi alichoambiwa na ndipo yule kijana alipompa kitabu cha tiketi mwenzake mmoja na kusogea pembeni kabisa na eneo lile na kuendelea na maongezi yao.

“Sikia mwanangu nikutonye, huku town kazi hazitafutwi kwa njia hiyo babuu... hapa inabidi uwe na refa”
“Refaa!!”
“Eeeh, mtu wa kukushika mkonooo, na marefa humu wanapatikana kwa laki mbili kama unazo nikuunganishe sasa hivi kwa mtu”
Aliongea tena yule kijana na Dullah alichekecha akilini na kumsoma yule jamaa alikuwa ni mtu wa tamaa na alimchukulia yeye kama boya sana lakini bado Dullah alijitia upole na kumsikiliza vizuri

“Lete basi man tumalize mchezo faster faster kuna magari kampuni ya Abood yameingia juzi tuu mapyaaaa hahahahaaa una bahati weweee”
Alijichekesha tena yule kijana.
“sikia ndugu yangu mi hizo hela za refa hata sina”
“sasa kama huna unafikiri utapata kazi humu!? Man mi naona unanichelewesha hauko sereous..”
“sitanii ndugu yangu, nina shida kweli”
“Daah! Mi cha kukusaidia zaidi hata sina labda kama una toroli kubwa la mizigo ukaombe na kujiandikisha kule mwishoni na utakuwa unalipia 2000 kila siku”
Aliongea yule kijana huku safari hii akipiga hatua ndogo ndogo kuondoka na kumuacha Dullah akiwa haelewi elewi inakuaje sasa.

Kwa hasira Dullah aliamua kuachana nae yule kijana na kujiondokea kuhamia upande mwengine huku nafsi yake ikimuuma pia kwa kutoa ile elfu kumi ambayo haikumletea hata robo ya faida.

Alizunguka karibu ubungo yote lakini bado shughuli ya kupata kazi ilikuwa ngumu sana hasa baada ya kuoneshwa dhalau na watu mbalimbali huku mabosi wengine aliowafata ofisi kuu wakimuuliza maswali ya dhalau hasa pale alipoulizwa na bosi mmoja wa kihindi kuwa anataka kazi gani ya kuvuta bangi au kutengeneza kacha..!!
yote hayo kwa sababu ya rasta zake kichwani.

Kauli zile na nyenginezo zilimuumiza moyoni Dullah na alipoona imefika saa saba ilibidi aondoke eneo lile la Ubungo na alitoka mpaka kituo cha daladala kusubiri gari itayomrudisha nyumbani akatulize kichwa huenda akapata mbinu m badala juu ya cha kufanya.

Alipanda daladala na aliposhuka kwa tumbo kabla hajavuka barabara alitupa macho kwenye nguzo ya umeme ambapo kulikuwa na tangazo la kazi limebandikwa, moyo ulimripuka pindi aliposoma tangazo lile la kazi na kuchukua zile namba zilizoandikwa kwenye lile tangazo na kuzipiga muda uleule na simu ilipokelewa na baada ya Dullah kueleza shida yake ndipo alipoelekezwa kesho yake mapema saa nne afike mwananyamala makumbusho zilipo hizo ofisi.

Alishukuru sana Dullah na kurejea magetoni akiwa na furaha zaidi na matumaini kwa mbali ya kupata kazi sasa.
Mara baada ya kufika geto aliwasha jiko lake la mchina na kujisongea ugali kisha alinunua fungu la samaki wa kukaanga na barafu na alipomaliza kula alijilaza kwenye godoro lake pale chini huku akiyachanganua maisha kichwani mwake.

* * * * * *

Majira ya saa kumi kamili watu walijazana uwanja wa tipi hususani wahuni na wananchi wa tandale kuishuhudia moja ya club kubwa tanzania Simba iliyokuja kucheza mechi ya kirafiki na club ndogo iliyokuwa imepanda ligi daraja la kwanza kutoka daraja la pili na ilikuwa imepania kwamba lazima wafuzu daraja la kwanza ili mwakani wacheze ligi kuu.
Club hiyo iliyojulikana kwa jina la Tandale fc a.k.a wakukloo iliundwa na vijana wa kuokotana okotana waliokuwa wanacheza kwa moyo na kujituma sana.

“Ee bwana yule rasta hajafika..!”
Aliuliza moja ya makocha wa tandale fc.
“Agh. Yule pale anakuja ila nawe acha kumuamini mtu ambae hata miezi miwili hana bwana.”
“Hamna bwana yule dogo mzuri bwana mi nimemcheki sana afu anapenda sana mazoezi”
“haya bwana ila hatutaki umuingize kikosi cha kwanza.. eka kikosi cha ushindi kwanza..”

Yalikuwa ni majadiliano ya baadhi ya viongozi wa Tandale fc pindi walipomuona Dullah akiwasili eneo lile la uwanja.
Kiukweli Dullah alikuwa na kipaji cha kucheza mpila pia aliupenda mno na ndio sababu ya kujumuika kila siku mazoezini na ktk kucheza kwake kuna baadhi ya viongozi walimkubali sana na walianza kumfikilia kuungana nae ktk timu yao na ndio sababu hata mechi hiyo iliyokuwa gumzo maeneo ya tandale walihitaji awepo ili waone kama anaweza kuonesha kama kile anachooneshaga mazoezini.

Saa kumi na nusu mpila ulianza huku Dullah akiwa nje akiwaangalia wenzake walivyokuwa wanacheza ambapo hadi kipindi cha kwanza kinaisha walishafungwa gori mbili kwa bila.

Watu walifurika mno uwanja wa tipi huku wakifurahia burudani na magori waliyokuwa wanafunga simba japo haikuwa timu inayowakilisha mtaa ule.
Upande wa makocha wa tandale uliibuka zogo juu ya kucheza kwa Dullah ile mechi ambapo mwishoe dakika ya themanini ndipo walipokubaliana hasa baada ya kuumia mshambuliaji tegemezi wa tandale.

Dullah alivaa jezi na kuingia huku watu wengi wakimtupia macho kwani alikuwa mgeni machoni mwa watu wengi na katika timu yao ni yeye tu aliyekuwa na rasta.

“Hee mwana unaona vitu anavyofanaya Rastaa!!”
Ilikuwa ni sauti ya moja wa shabiki wa tandale mara aada ya Dullah kumtia kanzu mchezaji mmoja wa simba na dakika si nyingi akiwa na mpila alimpiga chenga ya maudhi beki hatari wa simba John na kuufanya uwanja ulipuke shangwe na miluzi kutoka kwa wahuni na upande wa jukwaa alipokaa demu wa John ambae ni Vero akiwa na Asunta walijisikia aibu na kushangaa uwezo wa ajabu wa yule rasta.

Ilimchukua dakika saba tu Dullah toka aingie ambapo aliweza kusawazisha bao moja alilofunga kwa ufundi wa hali ya juu kwani alimtisha na kumpiga tena chenga maridadi John iliyopelekea kuteleza na kuanguka na kipa alipotokea tu Dullah aliunyanyua ule mpila kwa kuuchopu na kudondokea wavuni ambapo gori hilo lilisababisha mpila kusimama kwa dakika tano nzima mara baada ya mashabiki wa Tandale kushangilia na kuingia uwanjani huku kila mmoja akitaka kumpongeza Dullah lakini kwa bahati polisi walikuwa makini kuwazuia na kuwalinda wachezaji hususani wale wa Simba.

Shangwe liliendelea huku Dullah akishangiliwa kila alipogusa mpila na kama hiyo haitoshi, ilipotimu dakika ya tisini na mbili tandale walipata kona aliyosababisha mwenyewe Dullah mara baada ya kuuluka mpila aliokuwa anaukokota pindi alipomuona John akija vibaya kwa lengo la kumchezea rafu na kujikuta akimkosa Dullah na kupiga mpila na kutoka upande wa gori lao na kusababisha kona.
Wahuni wa Tandale walimzomea huku wengine wakimtisha kwa maneno John kuwa endapo angemvunja mchezaji wao basi nae asingetoka salama uwanjani, na hadi dakika hiyo macho ya kila mtu pale uwanjani yalicheza sana kwa Dullah Rasta.

Na hapo ndipo kona ilipopigwa na mchezaji aliyeitwa Roja ktk mazingira ya ajabu na kushangaza umati uliofurika tipi ulimshuhudia Dullah akijibinua tikitaka ya hatari na kufunga bao maridadi lililomfanya hadi kocha wa tandale machozi ya furaha kumtoka.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 3

Shangwe na kelele zilizolipuka zilikuwa si za kawaida na akiwa anakimbia sambamba na wachezaji wenzake na mashabiki huku wakishangilia goli lile pembeni ya uwanja, macho ya Dullah yaligongana na macho ya mabinti wale wawili ambapo Asunta alipokutanisha macho na Dullah tu alistaajabu sana tena sana na kujikuta anatabasamu huku akiwa kasimama alianza kumpigia makofi yule Rasta.
Hali ile ilimshangaza zaidi Vero na kumuangalia shogaake kwa jicho la kumshangaa huku akimuuliza kulikoni...!?

Uwanja uliripuka shangwe na kila mtu alimshangilia sana yule rasta hata kocha wa simba mwenyewe alifurahishwa na kushangazwa na kiwango cha Dullah.

"Vipi Asunta mbona unamuangalia sana yule rasta"
"Hamna vero namfananisha na kaka aliyenisaidia leo asubuhi"
"Unamfananisha rasta au sura yake.."
Aliuliza vero kwa sauti ya kutopenda rafikiake kumshobokea yule rasta hususan kutokana na bwanaake kupigwa chenga ya maudhi na yule rasta.
"Hamna vero bwana ni yeye kabisa "
"ahaa poa basi kampe shukurani kwa mara nyengine"
"hahaha vero bwana"
Aliongea na kujichekesha Asunta huku nafsi yake ikifarijika sana baada ya kumuona Dullah kwa mara nyengine na macho ya Asunta muda wote yalikuwa kwa Dullah pale uwanjani alimshangilia kwa kila alichokifanya.

Mpila uliisha kwa sare ya bao mbili kwa mbili na mara baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa watu wengi walimzonga Dullah hususani wahuni na mashabiki wa Tandale na kumpongeza huku wengine wakimpa kete kadhaa za dawa (bange) na kumshushia sifa kedekede.
Hata yule kocha aliyekuwa hataki Dullah acheze ile mechi alijikuta akijisikia aibu na kumpongeza Dullah huku wahuni wengine pamoja na kocha aliyekuwa anamkubali Dullah wakampachika jina la utani la Mlaiberia wakimfananisha na mwafrika aliyewahi shinda uchezaji bora wa dunia George Weah ambae alikuwa raia wa Liberia hivyo walimwita Dullah jina hilo la Mliberia.

Mara baada ya timu ya Simba kuondoka huku Vero akidrive gari la bwanaake na kuagana na Asunta aliyezuga kuwa atapanda bajaji kwani safari ile walikuja kwa kutumia gari ile ya John bwanaake Vero baada ya John kufika pale kwa gari ya timu huku ile gari ya Asunta aliiacha nyumbani ikifanyiwa service pindi alipofatwa mchana wake na Vero.
Japo Vero hakupenda moja kwa moja kumuacha shogaake lakini alijua kuwa Asunta hakuwa na la ziada lolote pale uwanjani zaidi alihitaji kuonana na yule rasta na kutokana na kutompenda yule rasta vero hakuwa na budi alimuacha mwenyewe Asunta huku akimsihi awe makini na asichelewe kuondoka pale kwa kuwa wahuni walikuwa wengi pia.

"Mambo kaka.."
Ilikuwa ni sauti raini iliyopenya masikioni mwa Dullah alipokuwa anajiandaa kupanda canter iliyowaleta wachezaji wa tandale na alipogeuka alikutana na sura nzuri ambayo haikuwa ngeni machoni mwake na kujikuta anawaambia wenzake watangulie tu ye atakuja mdogomdogo.
"hahya haya bwana Rastaaa Mliberiaa ila shemeji usiende kumkamua supu nyingii akashindwa kuja mazoezini kesho bado tuna mechi shemm oyooooooo"
Walipwayuka wahuni na kumfanya Asunta atabasam na kuonesha dimpoz zake na kuudhihilishia uso wake ni kiasi gani alikuwa mzuri.
"Nambie sister.."
"poa.. kumbe na wewe Ronaldo wa bongo jamani hongera"
"hahaaha hamnaa tunajifurahisha tuu"
"kujifurahisha!! acha utani ajira hiyo"
"aah.. ingekuwa ajira nzuri si ningekuwa napokea mshahara hadi sasa.. enhee wapi sasa mbona huna gari"
"Niliipaki nyumbani baada ya kurudi asubuhi ile nimeogopa kusumbuliwa tena"
"Duuh! pole kwa hiyo huku unaenda wapi"
"nafika hapo mbele tu nachukua bajaji"
"ok,poa "
"kwani wee unaishi wapi.."
"kwa tumbo."
"samahani umeoa .!"
"hamna dadaangu mi niko mwenyewe hata dem sina na ni mgeni hapa Dar ila mungu akininyooshea mambo yangu nadhani baadae atanionesha mtu sahihi. vipi wewe"
"haha mi mwenyewe hivyo hivyo "
"hivyo hivyo vipi na we mgeni..!"
"hamna ila sijaolewa wala sina mchumba"
"ha ha ha ahaaa"
"mbona unacheka!!! ni kweli japo wengi hawaniamini nikisemaga hivi, niliwahi kuwa na mahusiano zamani nikiwa shule sekondari lakini toka nianze chuo mwaka wa pili huu sasa sijawahi.."
Dullah alimsikiliza kwa makini yule mrembo na kuyachanganua maneno yake kipindi wakitembea kuelekea zilipo bajaji na bodaboda huku akilini akiwa haelewi kwanini yule mrembo alimwita.
Walifika zilipo bajaji huku baadhi ya madereva bajaji wakimchangamkia sana Dullah hadi mwenyewe alishangaa.
"Rasta twenzetu humu free kabisa ni offer kwaajili yako na shemeji"
Aliongea kijana mmoja aliyevaa tshirt ya yanga na kusogeza bajaji yake ambapo Dullah na Asunta walipanda pamoja na kumuamuru dereva awapeleke Masaki ila apitie tandale kwa tumbo na walipofika Dullah alishuka na kuagana na mrembo.
"Ok, but hizi ni namba zangu naomba unipigie tafadhali nione zako"
Aliongea Asunta na kumpatia namba Dullah aliposhuka.
"poapoa Rasta asante sana kwa kutuletea heshima Tandalee"
Aliongea yule kijana wa bajaji na kumuaga Dullah ambapo alibaini kuwa offer ile ilitokana na kiwango chake uwanjani.

Taratibu Dullah aliongoza njia ya magetoni na kuisev ile namba ya mrembo yule ambae hadi kipindi hiko hakuna aliyetambua jina la mwenzake.

* * * * * *

Asubuhi na mapema siku iliyofatia baada ya kurudi mazoezini Dullah alijiandaa na safari ya Mwananyamala makumbusho zilipo ofisi za ile kazi aliyoona tangazo lake jana yake na kufikia saa mbili alikuwa kashafika na kuambiwa asubiri mpaka saa nne ofisi zifunguliwe na ndipo alipongoja na ilipotimu saa nne Dullah alikuwa ndio wa kwanza kiuingia na kusikilizwa.
"sawa elimu yako je?"
Aliuliza mtu wa makamo aliyekuwa anaongea na Dullah baada ya kumpa taratibu za kazi.
"darasa la saba kaka"
"poa, kwa bahati ilibaki nafasi moja ya upendeleo na kwa kuwahi kwako hongera kwa kupata nafasi hii na utaanza kazi leo utaondoka na kijana mmoja ambae atakufundisha na kukupa taratibu zaidi za kazi ila naomba ujitahidi kunyoa hizo rasta zako... sawa"
"sawa kaka nitafanya hivyo"
Aliongea Dullah na kushukuru na baada ya nusu saa aliingia kijana mmoja na kuelekezwa kutoka na Dullah siku hiyo ambapo waliingia stoo na kupakia vitu mbali mbali kwenye mifuko mikubwa ya rambo zaidi vikiwa ni vyombo kama chupa za chai mahotpoti na kadhalika.

Mara baada ya hapo walitoka na kazi yenyewe ilikuwa ni kutembeza vile vyombo sehemu mbali mbali ya jiji hususani majumbani na kuvinadi kwa bei za promosheni.
kazi ilikuwa ngumu kwani ni kutembea muda mrefu juani na mzigo na kuongea muda mwingi ktk kumchombweza mteja lakini kwa upande wake Dullah hakuwa na kinyongo zaidi alijituma na kila siku aliwahi ofisini na baada ya wiki mmoja alianza kuwa mzoefu .
Lakini pia kazi haikumfanya akosekane mazoezini kila siku asubuhi aliwahi mazoezini na mida rasmi ya kazi ilikuwa saa mbili asubuhi tofauti na siku ile ya usaili.
jioni saa kumi alipotoka kazini tu alielekea uwanjani na sasa alikuwa maarufu sana tandale na aliteuliwa kikosi cha kwanza cha timu huku taratibu za kumlipa kiusajili zikiendelea kwa kusuasua.
Ila kwa kipindi hiko chote hakuwahi kumpigia yule bint na alisahau kabisa swala hilo kwa kutomueka akilini tofauti kwa upande wa Asunta muda mwingi alimfikiria sana Dullah na alitamani kuona simu yake ikiingia lakini alijikuta wiki inakatika na hatimae zikapita wiki mbili zaidi.

"Dullah leo nataka nikupeleke kiwanja tofauti kabisa kwa washua huko utashangaa mwenyewe.."
Aliongea Fred kijana aliyekuwa anatembeza vyombo na Dullah wakiwa njiani na vyombo vyao.
"Wapi huko mzee.."
"we twende tu bingwa nimepigiwa simu jana na mama mchungaji anahitaji vyombo na ndio maana leo nimepakia mzigo mkubwa coz namjua yule mama ni mteja mzuri sana siku akikwita jua ni neema.."
Aliongea tena Fred na mwendo uliendelea maeneo hayo yote yalikuwa mageni kwa Dullah hususani uzuri wa nyumba na upepo mwanana wa bahari uliokuwa unawapuliza pindi wakiwa njiani na ndipo baada ya mwendo mrefu walifika kwenye geti la nyumba moja nzuri ya kifahari na Fred kubonyeza alarm ambapo mlinzi alipotoka hakushangaa sana kumuona Fred kwani hakuwa mgeni machoni mwake na isitoshe alishaambiwa kuwa angekuja siku hiyo hivyo aliwaruhusu moja kwa moja na kuingia ndani na baada ya kubinya alarm ya mlangoni mfanyakazi wa ndani alifungua na kuwakaribisha.

"mama yule kaka muuza vyombo amekuja.."
Aliita yule dada wa kazi na mara yule mama alishuka kutokea ngazi za juu na kuwakaribisha vizuri huku Dullah akishangaa mazingira mazuri ya mule ndani na ubaridi wa AC uliokuwa unawapuliza.

Na kama alivyosema Fredi yule mama alichukua vyombo vingi sana hadi Dullah alishangaa na malipo yake yalikuwa juu zaidi .

"Asunta hebu njoo mamy uangalie kama kuna vya kuongeza.."
Aliita yule mama na muda si mrefu vilisikika viatu vikigonga kimadaha na mara macho ya Dullah hayakuamini baada ya kugongana macho na mrembo aliyekuwa anashusha kwenye ngazi baada ya kuitwa na yule mama.

Hata Asunta nae hakuamini macho yake lakini alizuga kutomuangalia sana ili asistukiwe na mamaake na hata Dullah mwenyewe aligundua hiko kitu na kuzuga pia baada ya kusalimiana.

"Vipi mwanangu naona leo umeshangaa Fred katuletea Marasta.."
Aliongea yule mama baada ya kina Dullah kumaliza biashara na kuaga, lakini upande wa Asunta alitamani sana kuongea na Dullah na kwa kuwa walikuwa na namba ya Fred haikuwa tabu sana alikimbilia juu kilipo chumba chake na kujifungia kisha kuipiga namba ya Fred aliyoichukua kwenye simu ya mamaake bila yule mama kujua na kipindi hiko kina Fred hawakuwa mbali na eneo lile.

.........

Mkuu ndio mwisho hapo?????

Story tamu sananaaa
 
SEHEMU YA 04

"Mwanangu simu yako hii.."
Aliongea Fred na kumkabidhi simu Dullah baada ya kuongea na sauti upande wa pili kumuomba aongee na Rasta lakini Fred hakujua nani aliyepiga kwani hakuwahi kuwa na namba ya Asunta pia alishangaa inakuaje mtu anampigia na kumuomba aongee na rasta (Dullah). kichwani mwa Fred hakuwa na idea na alikuwa na shauku ya kumuuliza maswali Dullah pindi tu atapomaliza kuongea na huyo mtu.
Dullah alishangaa sauti ya mtu aliyeongea nae na alipojitambulisha kuwa ni Asunta ndipo akabaini kuwa ni yule mrembo aliyewahi kumpa namba ya simu na hakuwa na maneno mengi Asunta zaidi ya kumuomba Dullah atapofika nyumbani ampigie kwani alikuwa na maongezi muhimu sana nae.

Baada ya kukata simu Fred alianza maswali lakini Dullah aliyajibu kiujanja ujanja na kuzidi kumtia mashaka Fred na kuanza hisi huenda akawa Asunta mtoto wa yule mama, lakini kilichomshangaza zaidi Fred kama ni kweli Asunta walikutanakutana vipi na Dullah hadi iwe vile na wana ajenda gani..! maana hawakuendana kabisa.

Walimaliza mizunguko siku hiyo na kurudi ofisini ambapo wakiwa stoo wanakabidhi vitu vilivyobaki ulikuja ujumbe kwa Dullah kuhitajika na bosi ofisini.

"Bwana Dullah inaonekana sasa ushaanza kuwa na uzoefu na tabia yako imependezwa na kukubaliwa na ofisini lakini tatizo kitu kimoja tu.."
Aliongea yule bosi meneja muajiri huku akimtazama Dullah kichwani.
"lipi hilo tatizo bosi?"
"Ni hizo Rasta zako. hakikisha baada ya siku tatu uwe umeshazinyoa haziiletei picha nzuri ofisi yetu mbona huelewi?"
"Sawa nimekusikia bosi."
"Kipindi unaajiliwa nilikwambia ukajibu hivyo hivyo lakini hadi leo bado zipo, sasa mara ya tatu sitokwambia tena ila utaona kitachofata. Haya kwaheli."
Baada ya kumaliza kuongea na bosi na kutoka ofisini huku akili yake pia ikijadili juu ya kunyoa rasta zile lakini mara nyingio moyo wake haukukubaliana na akili zake za kunyoa rasta lakini aliwaza endapo ataendelea kukaidi basi ajira yake pia itakuwa hatarini zaidi.
Muda ulikuwa ushaisha na kila mtu akaenda kwake kwa makubaliano ya kukutana tena kesho yake.

* * * * * *

Usiku huo Dullah akiwa getto kwake aliamua kumpigia Asunta.
“Hallow Asunta Mambo..”
“poa nani..”
“Rasta naongea..”
“Ooooh, Rasta jamani nimefurahi kusikia sauti yako shwali..?”
“Shwali nambie”
“Aaagh. Samahani hivi na wewe unafanya ile kazi au ulimsindikiza tu Fred..”
“hamna ndio kazi yangu pia..”
“Mh! Mpira je..”
“mpira ni burudani tuu..”
“acha utani bwana nambie kweli..”
“kweli Asunta..”
"Hapana siamini hata kidogo.. unajua wewe una kipaji sana? tena unastahili kucheza moja ya club kubwa duniani kama barcelona, Madrid, Man utd au Bayern.. sasa unapouza vyombo utajulikana vipi unadhani, hata itokee kazi ya ofisini usikubali D, wewe ofisi yako ipo uwanjani acha utani."
" Daaaah! kiukweli napenda kweli mpira tena sana tuu lakini nitashinda vipi kuzurula viwanjani muda wote ilhali tumboni hakuna kitu, mifuko imetoboka na natakiwa kulipa kodi kila mwezi na malipo ya umeme?"
“Eeeh.. haya ila naomba basi kesho usiende kazini asubuhi nitakupitia huko kwako kuna sehemu naomba unisindikize..”
“Mh.. Asunta si unajua ile kazi.. utaniponza mwenzio..”
“Niamini mimi Rasta nahitaji kukusaidia pia naomba usiwazie hiyo kazi..”
“mmmmmh.. haya dada..”

Alijibu kiunagaubaga Dula na kukata simu huku akiwazia kushobokewa na mrembo ambae pia aligundua kuwa kwao mambo safi.

Na kweli kesho yake Asunta alifika kwa tumbo na kumpigia Dullah na baada ya kukutana alimuomba aingie kwenye gari na safari ilianza mpaka pande za fukwe za mikadi huko kigamboni.
Kiukweli moyoni Asunta alishampenda Dullah na alitamani awe mpenzi wake japo kwa upande wa dulah nae alitamani kuwa na mrembo mzuri kama Asunta lakini moyoni alihofia ufukara wake na uzuri wa asunta ulimtisha pia aliamini yeye si aina yake lakini aliwazia na kutafuta ufumbuzi kwanini Asunta anamfanyia yote yale.

“Rasta nimekuleta huku kuna mambo mawili muhimu nataka nikwambie ila kwanza naomba nitajie jina lako halisi..”
Aliongea Asunta kipindi wapo kwenye kamgahawa pale beach wakipata kifungua kinywa.
“ok, naitwa Abdallah Kombo au kifupi najulikana kama Dullah”
“Nashukuru kukufahamu Dullah mi naitwa Asunta George ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kati ya watoto watatu ktk familia yetu.. “
“Hongera..”
“Asante Dullah.. sasa naomba unisikilize kwa umakini D, kiukweli nilipokuona jana unauza vyombo moyo wangu ulisononeka sana na leo hii nimeamua kukuleta huku kwasababu mbili, moja nataka nikusaidie ili ujiajili mwenyewe... pili nataka nikwambie kitu kilicho moyoni mwangu kinachonisumbua kwakweli kuhusu wewe..”
Aliongea Asunta na kujing’ata ng’ata huku Dulah akiwa anamsikiliza kwa umakini mkubwa na kamoyo kalianza kumdunda dunda akiwa haamini kama zali la mentali limeangukia kwake.
Alimtazama Asunta ambae alimwambia kuwa anahitaji afungue biashara lakini Dullah ndie awe msimamizi mkuu pia kitu cha pili alichodai Asunta kinamsumbua moyoni kilikuwa kigumu kidogo kukitamka moja kwa moja kwa Asunta na ndipo Dullah mwenyewe alipoanza kuhisi hiko kitu hata pale Asunta alipotamka..

“..Ok kiufupi Dullah Nimetokea kukupenda sana na nahitaji tuwe wapenzi uje uwe mume wangu kabisaa... serious si utani, Nakupenda”

Aliongea Asunta huku macho yake maregevu yaliyobebwa kwenye sura ile nzuri ya upole yakimaanisha kile akitamkacho huku Dullah akiwa kaganda kama amechomwa sindano ya ganzi akiwa haamini kile akisikiacho.

"Asunta, siamini hiki nikisikiacho... lakini unawezaje kunipenda mtu kama mimi? acha utani bwana nitawezaje kukuoa na hali hii niliyokuwa nayo isitoshe we ni mzuri sana hustahili kuolewa na fukara kama mimi"
"Hapana Dullah, mapenzi si ufukara wala pesa, pesa ni kama pambo tu kwenye maisha kamwe haiwezi kununua penzi la kweli, niamini Nakupenda kuhusu hayo mengine ondoa shaka"
Alisisitiza Asunta na kuvishika viganja vya mikono ya Dullah pale kwenye meza na kuvibinyabinya.
Taratibu Dulah alianza kumuelewa Asunta na moyoni mwake alifurahi pengine kuliko hata Asunta mwenyewe.

Waliinjoy lakini kutokana na Asunta kutotaka achelewe kwao waliondoka mapema eneo lile na wakiwa njiani Asunta aliendelea na maongezi.
"Unajua vipi baby.."
"enhee"
"Huwa nabanwa sana nyumbani na asubuhi napataga nafasi ya kutoka kwa sababu nimejiunga na jim moja ubungo plaza ndipo napopashaga viungo"
"haha kumbe na wewe unapenda mazoezi."
"haswaa napenda sana mazoezi hata baba hufurahi sana ninapofanyaga mazoezi na hapa nataka nikishakuacha nipitie huko Jim nikaonane na mwalim wetu isije baba akapiga simu bure kuniulizia maana nipo nyuma ya muda na sim yangu nimezima"
"poa baby usijali"

Gari ilifika kwa tumbo na mara baada ya kuagana Asunta alimuachia elfu hamsini ya matumizi Dullah kisha wakaagana nae kuelekea huko Ubungo.

* * * * *

"Habari baba mchungaji"
"Nzuri tu tunamshukuru mungu neema ya bwana iwe juu yako"
"Amen baba karibu"
"Asante sana habari za siku tele na vipi maendeleo yenu na mazoezi"
"aah tunamshukuru mungu tunaendelea vizuri vijana wanaelekea kabisa"
"Ooooh, vizuri sana na bint yangu je"
"yuko vizuri baba ila hajafika leo vipi anaendeleaje au anaumwa"
"HAJAFIKA!!.."
Alistuka sana Pastor George mara baada ya kusikia mwanae kipenzi Asunta hajafika mazoezini pale ilhali alitoka nyumbani akiwa anaelekea mazoezini.
"Eee sijamuona leo na wenzake wametoka muda si mrefu sana"
"aaah.. ok basi sawa"

Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Pastor George na mwalimu wa mazoezi ubungo plaza asubuhi ile mara baada ya pastor kupitia pale kwa lengo la kuagana na bint ake baada ya kupokea simu ya dharula juu ya safari yao nchini Uganda na alipoona mwanae anachelewa sana kurudi siku hiyo na hakupatikana hewani ndipo alipomuamuru dereva ampeleke huko Jim lakini alishangazwa na taarifa kuwa mwanae kipenzi Asunta hakufika mazoezini siku hiyo ilihali nyumbani aliaga kuwa anaelekea huko.

"Vipi baba naona kama hauko sawa "
"Hapana, nilikuwa nafikiria wapi ameelekea Asunta mwanangu na imekuaje amechelewa hadi saa hizi na ikiwa hajaja huku... ee baba ulie mbinguni naomba umponye mwanangu kama kuna jinamizi lolote baya linalomnyemelea.."
Aliongea pastor George huku mawazo yake yakienda mbali na kufikilia mwanae tabia ya uongo kaanza lini au kuna kitu gani kimempata kibaya.
Alimpigia tena simu hakupatikana ndipo alipoamua kupiga nyumbani huenda wamepishana lakini mkewe alijibu kuwa bado hajafika, hali hii ilianza mtia wasiwasi Pastor George.
"Lakini vipi mahudhulio yake kiujumla"
Aligeuka na kumuuliza tena yule mwalimu.
"Aaah, kiukweli ni mazuri, tena mazuri sana na hata kutofika kwake leo kumeuliziwa na kila mtu hapa Jim kutokana na ubora wake wa mahudhulio."
"Na jana mliagana vipi"
"kama kawaida kuwa tungekutana leo mapema"
"sawa mwalim nisikuchoshe kwa maswali mengi ngoja tusikilizie huenda kapitia kwa rafiki yake Vero na kwa kuwa sina namba yao kina vero itabidi niende kwani ni muhimu kuonana nae kabla sijasafiri"
"haya baba usijali"
Waliongea na kutoka kuelekea zilikopaki gari.

Mzee George na mzee Mwai babaake na Vero walikuwa marafiki wakubwa sana hapo awali na walipanga nyumba moja miaka hiyo ya nyuma kabla mambo hayajamnyookea George na kupewa wadhifa mkubwa na kanisa kutoka nchini Marekani kuwa msimamizi wa matawi yake nchini Tanzania, Urafiki wao na kutembeleana kwao mara kwa mara ndio kuliwafanya watoto wao Vero na Asunta kupendana na kuunga urafiki tangia wangali wadogo na zaidi walisoma shule moja ya msingi hadi sekondari na ndio sababu urafiki wa Asunta na Vero ulishibana sana.

* * * * *

"Eee bwana vipi Rasta mbona hujaja leo job"
Ilikuwa ni sauti ya Fred kwenye simu pindi alipompigia Dullah asubuhi ile baada ya kuona muda umekwenda sana.
"Haa.. we acha tu Fred tumbo limenisumbua sana usiku hapa nilipo hata nguvu sina.."
Alidanganya Dullah kipindi hiko alikuwa anafungua mlango wa chumbani kwake baada ya kuachana na Asunta muda mfupi.
"Oooh, pole sana swahiba, basi nikirudi jioni nitakupigia unielekeze geto nije kukuona"
"poa ndugu yangu usijali"
Alikata simu Dullah na kujitupa kitandani huku mawazo yake yakimpeleka mbali sana zaidi alifikiria kilichotokea juu ya mahusiano yake ya ghafra na binti mrembo Asunta na zilimjia picha nyingi za furaha na starehe huko mbele na kuamini sasa ataweza kuwagomboa ndugu zake pia huko kijijini hususan mamaake na mdogoake pindi tu watapofungua hiyo biashara na Asunta.
Hakuamini Dullah na kujikuta anamshukuru mungu kwa sauti ya juu sana.

"Eee mwenyezi Mungu asante kwa kunikutanisha na huyu bint nakuahidi Nitampenda daima."

* * * * * * ITAENDELEA

PRINCE NAAHJUM ALSINA

0652691819
 
Back
Top Bottom