HADITHI: Mtoto wa Pastor

HADITHI: Mtoto wa Pastor

SEHEMU YA 24


(''Kwisha Jeuri yako Asuntaa'')
aliwaza moyoni Fredy na kuanza kumchezea taratibu asunta na kumsaula viwalo vyote alivyovaa na kumuacha (......................)
hakuamini kabisa Fredy kwa jinsi umbo la Asunta lilivyovutia tena akiwa (..................) alipiga kelele za (.............) kileleni Fredy kabla hata ya kuanza (...............) danguso lake kwenye (.......) ya Asunta mara tu alipolitoa na kujikuta anaishiwa nguvu ya kuanza (.....) tena lile tendo ambalo aliishia kumchezea(.....) Asu kwa vidole pekee na hakujua kwanini njomba nchumali wake kashindwa kuvunja biskuti ile iliyolowanishwa na kujikuta anafika kilele kabla hata hajapanda mlima wenyewe.

("Ooooooh! shit!! Nimerogwa nini!?")
alijilalamikia mwenyewe Fredy mara baada ya kutumia dakika nyingi akijiche(..) mwenyewe ili aweze kumsimamisha tena askali wake aweze kumuadhibu Asunta bila mafanikio yoyote na alipoangalia muda tayari lilishapita lisaa la pili katika masaa sita.

Wasiwasi na mawazo ndio wakawa maadui wakubwa waliokuwa wanamtafuna Fredy kumfanya ashindwe kumsimamisha tena askali wake aliyekuwa na kiherehere cha kutema risasi kabla hata ya kufika vitani na kusababisha kushindwa vita vyenyewe mapema kiasi kile mbali ya kuwa adui alisharahisishwa.

alifikiria cha kufanya harakaharaka ili aweze kutimiza azma yake kuu ndipo alipokumbuka story za chuo miaka mitatu iliyopita kuwa pombe inaleta ashki na kuamsha(.......) hususani Konyagi inafanya mtu achelewe sana ku(.....) ndani ya uwanja wa seremala.
Lilipomjia wazo hilo ndipo alisimama haraka na kuvaa nguo zake kisha alitoka kwenda upande ule wa bar nia na madhumuni akapate hiko kinywaji ambacho aliamini huenda kingekuwa na msaada wa kufanikisha zoezi lake mbali ya kuwa ukweli Fredy hakuwahi kunywa pombe hapo awali wala kuitamani kutokana na mazingira ya kiroho aliyolelewa na wazazi wake.

(''Khaa, mbona mi nina mikosi namna hii na huyu binti daah! kila ninapomuweka kwenye anga zangu nimwambie najikuta nashindwa mwenyewe. Leo tena ndio nimejitengenezea njia nyeupeeee lakini duh! nashindwa kumaliza mchezo katika dakika za mwisho kabisaa!? aaaah sikubali leo mimi na Asu lazima kieleweke tuu.'')
alizidi kujiapiza moyoni Fredy huku akiendelea kunywa ile konyagi aliyoagizia japo haikuwa na ladha nzuri mdomoni mwake lakini alijitahidi hivyo hivyo kuimeza kibishi akiamini endpo atamaliza robo lita aliyonunua sambamba na kitimoto nusu aliagiza aletewe vitasaidia kumrudishia nguvu na morali wa kutimiza lengo siku hiyo.
Nyama zilliletwa mezani kwa Fredy na kuzidi kuhondomola huku akishushia kwa kukandamiza mikono ya bingwa ili akawe bingwa kwenye chumba alichomuacha Asu.

Hakuwa mzoefu wa pombe lakini kwa nguvu na uchu wa kitimoto alijikuta anamaliza vyote japo alitumia muda mrefu ambao yeye alijiona amefanya harakaharaka tu kutokana na nguvu ya konyagi iliyoanza kuharibu milango ya fahamu zake japo haikumpelekea kufuta lengo lake kwani ndio kwanza alinyanyuka huku anayumba yumba na kuelekea mule chumbani ambapo pindi alipofungua mlango tu Hamadi!! alikumbana uso kwa uso na Asunta ambae alikuwa amevaa nguo zake huku akionesha hali ya wasiwasi na kuchanganyikiwa mno.

Walibaki wanatazamana kama majogoo huku Fredy akichukulia masihara kutokana na akili yake kuanza kupelekwa na pombe na kubaki akikenua meno na kuurudishia mlango kwa style ya kuyumba yumba wakati Asunta akiwa kasimama anamuangalia kwa hasira tena akihema kwa nguvu
"FREDY..!! Hivi ni wewe Kweli..!?"
alibwatuka Asunta kwa sauti ya juu na kumvamia Fredy ambae alikuwa anapepesuka pale mlangoni pindi alipogeuka na kumkunja kwa nguvu kola ya shati alilovaa sambamba na tai kwa hasira.
"Kwanini Fredy umekuwa mnyama kiasi hiki..? Nilikuheshimu siku zote kama kakaangu na kukupenda kwa ukalimu uliokuwa unanionesha kumbe wewe ni sawa na Chui aliyevaa ngozi ya kondoo na kujichanganya kwa wana kondoo ili aweze kuwatafuna kirahisi..? AAH! Siamini hata kidogooo Fredy kwaniniiiiii.... Kwaniniiii Fredy umenifanyia unyama huu??? KWANINI.?"
aliendelea kulalamika Asunta huku akimtikisa tikisa Fredy ambae alishindwa kabisa kumzuia Asu kutokana na konyagi aliyokunywa mikono yake ilikosa nguvu ya kuiondoa mikono ya Asu shingoni mwake wala miguu yake pia haikuwa na stamina ya kujizuia asiyumbe kwa vile alivyokuwa anatikiswa na Asunta ambae alionesha dhahili alikuwa na hasira mno baada ya kuwa anaongea huku analia.
"Aaa Asuuuntaaa...ni...Upeee...ndo tuuh uuphhh .. I lov...youuu"
kwa lugha ya kilevi alibwabwaja Fredy na kumzidisha hasira Asu ambae alizidi kumtingisha kwa nguvu na kumsukumizia pembeni ambapo kwa bahati mbaya Fredy alidondoka na kichwa chake kugonga kwenye besela la kitanda kabla hajafika chini ambapo alianza kurusha rusha miguu huku damu zikimvuja maeneo ya kichwa.
"Katiri mkubwa wewe I hate you"
aliongea Asunta bila kujali hali ya Fredy pale chini na kutoka nje ya ule mlango huku akiwa hajui wapi pa kuingilia wapi pa kutokea.
Alitazama huku na huko na kugundua lazima ile sehemu itakuwa ni guest hivyo aliamua kuelekea upande ule alipousikia mziki ukipigwa akidhani kuna njia ya nje lakini alijikuta anaingia kwenye bar na hapo akiwa bado moyo wake unamuenda mbio kwa hasira ju ya kitendo alichofanyiwa na Fredy, Asu alimfata dada mmoja aliekaa kwenye meza ya pekeake na baada ya kumsalimia alimuuliza njia ya kutokea nje ya pale sehemu zilikopaki gari.
"Atii.? Inaonekana wazi wewe ni mtizedi yani wazani bar zinakaa barabarani kama huko kwenu? fata wahusika wakupe maelekezo mi sio muonesha watu njia"
alijibu yule dada ambae alikuwa na sauti nzito kidogo na kumfanya Asu atoke na kuelekea kule kule ndani na alikutana na muhudumu mmoja kwenye ukumbi ambae yeye ndie aliyemuelekeza njia sahihi na kutoka hadi nje akiwa hajui sasa aelekee wapi na kujikuta anasimama akitazama magari yaliyokuwa yanapita ndipo taratibu hasira zilianza kupungua na moyo wa huruma ulianza kumjia pindi alipokumbuka vile alivyomsukuma Fredy na kujigonga pale kitandani na kujipasua sehemu za kichwani na hapo alianza kupata wasiwasi huenda akawa ameumia zaidi.

Mawazo yale yalimfanya aondoke pale barabarani alipokuwa anasubiri taxi na kurudi tena mule guest moja kwa moja hadi kwenye kile chumba ambapo alipoingia kumuangalia Fredy alishangaa kuona kalala vilevile akiwa katulia huku mapovu shati aliyovaa ikiwa imetapakaa matapishi sambamba na damu nyingi ikionekana pale alipoanguka.
"Fredy.. kaka Fredy..?"
aliita Asunta kwa hofu akiwa haelewi kama Fredy ni mzima ama amekufa na alipojaribu kumsogelea na kumwita kwa ukaribu aligundua kuwa anapumua kwa mbali na hapo ndipo alipojua endapo atachelewa kufanya msaada wa aina yoyote basi maisha ya Fredy yanaweza yakamalizikia mule guest.
"Baba baba babaa naomba msaada wako tafadhali.."
aliongea kwa msisitizo Asunta huku akimshika mkono baba mmoja aliyekuwa anatoka chumba kilichofatana na kile alichokuwamo Fredy pindi tu alipofungua mlango kwa ajili ya kutoka kwenda kutafuta msaada.
"Nini tena..?"
"Ndugu yangu ameanguka ghafra ameumia naomba tusaidiane kumbeba nimuwahishe hospital tafadhali baba... kakaangu atakufa tafadhali njoo unisaidie"
"sasa kaka lakooo au libwana lako? aaah mbona twapeana shida"
alijibu yule baba na kuingia chumbani pindi Asunta alipotangulia na kweli kwa shida waliweza kumnyanyua na walipotoka nje kufika mapokezi ya guest yule muhudumu alishangaa mno baada ya kusikia mteja wake aliyeingia pale masaa kadhaa yaliyopita amedondoka ghafra ndani bahati mbaya amejigonga na kujiumiza kichwani kwa hiyo hawana budi kumkimbiza hospital kwanza.
(''Khaa! lakini huyu si amepita na yule mwanamke akiwa kabebwa akinambia kuwa mkewe kazidiwa pombe! sasa mbona sasa hivi mwanamke ndie mwenye nguvu ya kum beba mwanaume ambae nae pia kazidiwa hadi kajitapikia pombe... Mh!!wateja wengine mbona mauzauza sasa'')
aliwaza yule muhudumu pindi nae alipokuwa anasaidia kumfikisha Fredy kwenye gari yao aina ya Hummer ambayo pale kwenye parking ya ile guest na bar ilikuwa pekeake.
Asunta alizifungua funguo za gari zilizokuwa zinaning'inia kwenye luksi za suruali ya Fredy na kuitekenya ambapo muhudumu yule wa guest alichukua na kitabu cha kumbukumbu za wageni hususani wa siku hiyo na kujiunga nao kwa safari ya hospital ili pia kama watahitaji na ushahidi wa kipolisi basi vielelezo vyote muhimu iwe rahisi kuwapa.

* * * * * *
- (TANZANIA) -
..................................

Tairi za gari ziliendelea kutalii barabara kwa mwendo wa usijaribu pindi Coaster ile old model ilipokuwa njiani kuwarudisha Dar Tandale fc.
Kila mtu alionekana na uso wa furaha ya kipekee ambapo dereva alikuwa makini sana na barabara na kutokana na kupungua kwa magari na uwepo wa trafki majira yale ya usiku mkubwa, deleva wa ile Coaster alizidi kuwaonesha tandale na yeye kipaji chake cha udereva kwa kutamba barabarani akiwa speed kali.
Wakiwa wamekaa siti zilizofatana baina ya Dullah na Roja au mapacha kama walivyotungwa na watu mbalimbali pindi wanapowaona pamoja.
Na kweli walikuwa mapacha haswaaa tena wazee wa kazi na waliiteka timu na mitaa kwa muda mfupi tu na ukitaka kujua shughuli yao basi ngoja uzione harakati wanazofanya uwanjani ni za kipekee sana huku siri ya mafanikio yao zaidi ikiwa mioyoni mwao na hakukuwa na mchawi wala mganga yeyote zaidi ya mazoezi ya moyo mmoja waliyokuwa wanafanya wenyewe kila siku iendayo kwa Mungu.

"vipi D anasemaje mama?"
alikuwa ni Roja ndie aliyemuanza mwenzie katika mazungumzo pindi wakiwa njiani ndani ya ile Coaster.
"aaagh hana usemi zaidi ya kuniagiza niwasalimie wote hususan wewe mamaangu ametokea kukupenda sana na kunisisitiza nilinde urafiki baina yetu"
"Ahaa ila unajua nini mzee.. mi niliona kama vile mama kuna vitu anakulaumu harafu nikaona mwana umeanza kuvimba kimtindo...!"
"hamna Roja, hakuwa ananilaumu ila kuna habari alikuwa ananambia ndio ilinistua kwani sipendi kusikia habari za namna ile"
"habari ipi tena man, naweza kuijua na mimi au kifamily zaidi."
"aagh nitakwambia tu usijali"
alikatisha mazungumzo Dullah kwa kutopenda swala lile waliongelee mule ndani ya gari kwani wengi wangesikia wakati hapendi mambo yake ajue kila mtu kasoro Roja ambae ndie mtu alietokea kumuamini siku hadi siku.


ITAENDELEA

Watsap
0652691819
 
SEHEMU YA 25



Gari iliingia kwa mbwembwe maeneo ya Dar ambapo mbali ya kwamba iliiingia karibu na alfajiri ya siku lakini haikusababishwa kutowakuta mashabiki wakereketwa ambao walitangulia kuondoka sambamba na wale ambao hawakupata nafasi wakiwa wamekusanya maboda boda wakiwangojea tokea maeneo ya Mbezi na pindi ilipotokeza tu ile basi ya Tandale fc ndipo shangwe na kelele za boda boda ziliposikika na kuizingira gari barabara nzima na kuieka kati wakiwa wanaisindikiza kwa style ya kipekee.
Daah!! asikwambie mtu bwana watoto wa uswahilini wanajua kusherehekea na ni wabunifu sana.
kwa makelele na honi za bodaboda huku wakiimba nyimbo za kuipongeza timu yao ilitosha kuwafanya watu wa jiji la Dar hususani wa maeneo ilipopita ile ulipopita msafara ule kuacha shughuli zao kwa muda alfajiri ile na kushangaa huku wengi wakiulizana kunanini kuna nini..?! na wale waliojua waliwapasha wenzao na hapo ndipo habari ya maajabu ya Rasta wa Tandale Dullah ilizidi kuvuka mipaka midomoni mwa watu wengi huku wale wasiomjua wakipania kwenda kuiangalia siku Tandale ikicheza japo ligi yao haikuwa na hamasa kubwa kama ligi kuu.

Baada ya kufika na kushangiliwa pindi waliposhuka maeneo ya kwao baada ya ile gari kuwa inampeleka kila mchezaji maeneo anapoishi ndani ya jiji tena kukiwa na msafara ule uliofanya waliolala waamke na kuchungulia madirishani.
Dullah na Roja waliingia chumbani kwao na alfajiri ile hawakuitumia kulala zaidi ya kupiga story ambapo mada kubwa ilikuwa juu ya habari ya mama Dullah kumtaka mwanae akaoe kijijini kwao na kumtahadharisha na wanawake wa Dar kuwa wengi wao si wanawake wenye maadili mema.
"Umeona sasa Roja, mama si anataka kunirushia njiwa wangu Asu"
"hahahahahahaaaaa"
"sasa unacheka nini Roja wakati unaona kabisa tayari mtihani huu!!!"
"hahah Dullah bwana.. hakuna mtihani hapo Rastaa"
"kwanini?"
"Kwa sababu mama yuko sahihi kwa kile akisikiacho na wewe uko sahihi kwa kile ukionacho lakini mmekisahu kitu kimoja kilichonifanya nicheke hahahaa"
"kipi sasa Roja"
"ni hivi Rastaaa hahaha mmesahau kuwa Mungu ndie anayejua yakinifu ukweli wa jambo tofauti na tunavyoona sisi ama kusikia.. endelea kupiga soka man na umuombe Mungu kila siku mi naamini kama yeye amepanga uwe na Asu utakuwa nae tu hupaswi kupa nick wala kumkasilikia mama ila mi nitazungumza nae kitu kimoja mama ambacho naamini atanielewa endapo tu utazidisha juhudi uwanjani na imani yako kwa Mungu"
aliongea Roja maneno yaliyozidi kuitanua akili ya Dullah na kuupa moyo nguvu ya kupambana na kuushinda udhaifu wa kukata tamaa.

Maisha yaliendelea kama kawaida jioni yake walikutana mazoezini ambapo siku hiyo hakukuwa na mazoezi yoyote zaidi ya tafrija maalum waliyoiandaa kwa ajili ya kuwapongeza wachezaji na kuwapa motisha ili wazidi kufanya vizuri mechi zijazo.
Kila jicho la mwananchi wa Tandale hususani mpenda michezo lilikuwa kwa Dullah, walimuona kama roho ya timu na walimuheshimu kupita maelezo.
Nani aliyekwambia Dullah na Roja wakikatiza sokoni Tandale watatoka patupu? yaani hata wakatize kwa siku mara kumi bado lazima watoke wakiwa na mifuko iliyojaa matunda kama maembe, machungwa, mananasi, maparachichi n.k. Na hii si kwamba walikuwa wananunua.. la hasha, bali walikuwa wanagaiwa bure na masela wauza matunda wa pale kwani hata asili ya Tandale fc ilitokana na timu ya sokoni kama utani wakifanya sehemu ya kujiburudisha lakini ilikuja kukua na kupatikana vijana wengine wa Tandale wakapanua wigo mpaka wakaanza ligi daraja la nne mpaka kufikia hatua ile, kwa hiyo mashabiki wa sokoni walijiona wao ndio waasisi ama wenye timu na waliipenda mno na kuwatukuza wachezaji wao ambao walikuwa wanafanya vizuri, wenyewe walijiita wazeee wa Kukloo na wao ndio waliompachika Dullah jina la Mliberia.

Mechi ya wiki iliyofatia ilikuwa ndani ya uwanja wa mdogo wa Taifa na hii haikuwa kawaida kwa sababu Tandale walikuwa na uwanja wao lakini kutokana na umati uliokata tiketi kuitazama mechi hiyo ndipo chama cha mpira tanzania (TFF) walipokubaliana kwamba mechi hiyo ya mahasimu wakubwa baina ya Tandale fc na Freands Langer ikachezwe uwanja mdogo wa Taifa kwaajili ya usalama zaidi na kuwakidhi mashabiki.
Naam upinzani wa Tandale na Freands Langer ulikuwa mkubwa mno mbali ya kuwa Frends Langer ilianza kujulikana lakini ule ukaribu wao na utani uwanjani iligeuka chuki kubwa huku kila upande ukitaka kujionesha wao ndio zaidi.
Yaani hiyo mechi ilifananishwa na ile ya Simba pindi wanapokutana na Yanga kutokana na uhasimu mkubwa uliokuwepo huku safari hii Tandale wakivimbisha kifua kwa kuwa na wachezaji wawili waliokuwa ktk fom ya ajabu Dullah na Roja na kuwatunishia msuli wa maneno watani zao kuwa lazima wakione cha mtema kuni lakini nao Frends kutokana na rekodi yao ya kuifunga mara nyingi Tandale waliwabeza na kuwaambia kuwa mbwa hata awe mkali vipi kwa chatu atageuka mjinga tu.
Basi ilimradi watani hawakuacha kurushiana maneno ya hapa na pale na kipindi hiko wakiwa katika vyumba vya kubadilishia nguo kabla ya mchezo kuanza ambapo tayari uwanja wa Taifa ulifurika vya kutosha huku macho ya mashabiki wengi sambamba na waandishi wa habari waliokuwepo walikuwa na shauku ya kumuona Dullah ambae nyota yake ilizidi kung'aa huku umaarufu wake ukiongezeka kasi mbali ya kwamba alikuwa anacheza ligi iliyokuwa haifatiliwi sana.
"Road to Kenya ishajibu, kawaoneshe Freands leo wewe nani kuna mascout wa club ya Tusker ile ya Kenya uliyoichachafya siku zile wamekuja kukuangalia. All the best D"
yalikuwa ni maneno ya sauti ya chini Roja akimwambia Dullah pindi walipokuwa wanakumbatiana wachezaji baada ya kuvaa wakijiandaa kutoka kukianza kipute.

* * * * * *
TUSKER FC (KENYA)
____________________

Upepo m baya wa uchumi na matokeo mabovu ligi kuu ulizidi kuvuma ktk club kongwe ya Tusker iliyokuwa na maskani yake jijini Nairobi katika nchi ya Kenya.
Hii ilipelekea kufukuza makocha zaidi ya mara mbili katika msimu mmoja na msimu mpya ulivyoanza waliamua kuwagawa mascout wake sehemu mbalimbali nchini Kenya na nchi jirani kwaajili ya kutafuta vipaji ambavyo vitaweza kuiokoa club yao ambayo almanusura ishuke daraja msimu uliopita.

"Italazimika Yoel uende Tz kwenye ile club tuliyocheza nao unakumbuka kuna rasta mmoja mzuri sana tunasikia sifa zake na alitusumbua hata sisi"
"Kweli kabisa tena nasikia sasa hivi ana kiwango cha hali ya juu sana inabidi tuwahi kutuma ofa"
"Nilitumiwa ujumbe wa whatsapp na jamaa angu wa Tz kuwa inaonesha yule Rasta ana mapenzi sana na nchi yetu kwani aina yake ya ushangiliaji hata mimi nilivyoiona nimeuona urahisi wa kumpata"
"ipi hiyo"
"Hii hapa, ona hii picha kuna maandishi kwenye nguo yake ya ndani yanasema Road to Kenya"
"Kweli kabisa ikiwezekana wiki ijayo safari ianze"
"Hilo ndio suala"

Yalikuwa ni moja ya majadiliano na mikakati ya Tusker katika kuimalisha kikosi chao msimu huo ambacho bado kilikuwa na mwendo wa kusuasua.
Na kweli walitoka mascout wawili kwenda Tanzania na lengo kuu ni kukutana na uongozi wa Tandale kwa niaba ya mazungumzo ya kunasa sahihi ya Dullah na siku ya mechi ya Tandale na mahasimu zao Freands walikuwepo uwanjani kwaajili ya kumuangalia vizuri Dullah ambae nae alishazipata tetesi hizo toka kwa Roja ambae nae aliusikia huo mnuso toka kwa Kocha wao.

* * * *
HOSPITAL KUU NAIROBI
__________________

Lilionekana jopo la madaktari wakiwa katika jitihada za kuokoa maisha ya Fredy aliyefikishwa pale nusu saa iliyopita akiwa hajitambui kabisa.
Jina la Askofu Mbukinyo lilikuwa siraha tosha ya kuwafanya madaktari wazidishe umakini kwa Fredy baada ya kugundua ni mtoto wa Askofu wao waliompenda sana japo walishangaa mno kuona alcohol nyingi mwilini mwa mtoto wa Askofu.

Akiwa amekaa sehemu aliyoambiwa asuburi Asu alikuwa analia muda wote huku akijilaumu kwanini alimsukuma ni heri angemuacha tu aondoke, sasa endapo Fredy akifa harafu ndie mtoto wa pekee kwa familia ya Askofu nani atayemuelewa katika maelezo yake.
Mbali na hayo pia Asu aliwazia wapi ataificha sura yake pindi atapoonana na wazazi wa Fredy na ataongela lugha gani rahisi watayomuelewa.
"Njoo huku we dada uliyekuja na mgonjwa"
sauti ya daktari ilimtoa kwenye wimbi la mawazo Asu na kunyanyuka kumfata yule daktari.
"Karibu hebu kaa hapo nina maswali machache na wewe sambamba na taarifa ya mgonjwa wako."
aliongea yule daktari wakati alipomkaribisha Asunta kwenye ofisi yake.
"Hivi unasema Fredy ni kakaako?"
"Ndio Dokta,"
"Kwahiyo na wewe ni mtoto wa Askofu Mbukinyo! Daah hivi baba yenu yupo?"
"Hapana amesafiri."
"Sasa bint naomba unisikilize kwa umakini, ndugu yako tumefanya jitihada na kugundua tatizo lililomkuta ni kwenye ubongo. tatizo hili kitaalam linaitwa brain shock na inaweza kumchukua muda mrefu kurecover na kurudiwa fahamu kabisa hivyo kwa sasa tumemuhamishia icu kwani tatizo lake linahitaji utulivu zaidi. vilevile usiogope wala usistuke ni muhimu sasa ufanye mawasiliano na baba Askofu umpe taarifa kwani yeye ndie tutayejadili nae yakinifu kuhusu suala hili"
maneno ya yule daktari kuhusu ripoti ya Fredy yaliustua mno moyo wa Asunta na kushindwa jua ataanzia wapi kuhusu hilo.

Alitoka na kuelekea nyumbani wanapoishi na tayari ilikuwa alfajiri lakini ukweli jina la Askofu lilisaidia sana kupokelewa na kutibiwa Fredy pasi na viambatanisho vya polisi.
Asunta aliingia ndani kila mtu alimshangaa kuanzia walinzi getini mpaka wadada wa ndani kwani haikuwa desturi yake vile alivyokuwa anatembea vile alivyo pamoja na kutokuwa na Fredy wakati walitoka wote na hawakuwahi kulala nje ya pale.
aliingia chumbani kwake na kujitupa kitandani akilia na kujilaumu huku akiwaza nini afanye.
Ilimchukua kutwa nzima akitafakari na kujiuliza ndipo lilipomjia wazo ni bora atoroke na kurudi Tanzania
('Yaah! liwalo na liwe ee Mungu nisaidie.. Sitafikia popote zaidi ya Tandale kwa Dullah wangu nimshawishi tuondoke tukaishi mbali tu potelea mbali kuliko tuhuma hii kunivaa huku.. Pesa ninayo kwenye account yangu na ile niliyopewa na mama. kwanini ning'ang'ane hapa. Nishaua mimi')
aliwaza Asu na kunyanyuka ili aweze kujiandaa haraka kwa niaba ya kutoroka.


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 26


Aliingia bafuni na kujisafisha harakaharaka na kurejea tena chumbani kujiandaa ambapo baada ya kuvaa na kukunja nguo chache alizozitia kwenye Kamkoba kidogo (hand bag) kisha baada ya kuhakikisha yuko sawa alifungua mlango kwa dhumuni sasa la kutoka rasmi,
"dada Asu vipi unaenda wapi?"
alisikika msichana wa kazi akimuuliza Asunta pindi alipokuwa anataka kufungua mlango wa sebuleni na kumfanya asimame na kumuangalia.
"Naenda kumfata Fredy, nilirudi mara moja."
"Aahaa kwa hiyyo kumbe toka jana mlikuwa wote na kaka Fredy?"
aliuliza tena yule dada wa kazi swali ambalo Asunta hakulipenda ila aliamua kulipotezea na kutoka pasi kumjibu kitu.
"Bwana asifiwe dada Asu unatoka tena?"
lilikuwa ni swali la mmoja kati ya walinzi wa getini ambalo hakulipenda kabsa Asu japo halikuwa na madhala yoyote wala haikuwa tusi,
"wee, kazi yako fungua geti acha maswali, kaka twende mara moja"
alijibu maneno ambayo si yule mlinzi tu yaliyomshangaza bali hata yeye mwenyewe pindi alipokuwa ndani ya gari ile Hummer ambayo ndio aliingia nayo na aliamua kumwita dereva wa emergence aliyekuwa anapiga story na walinzi na moja kwa moja safari ya kuelekea uwanja wa ndege ilianza huku Asu akiendeesha mwenyewe.
"Nimepata dharula naenda London Askofu amenitumia tiketi"
alidanganya Asu kumwambia yule dereva
"ooooh kumbe ni hivyo dada, vipi Fredy yupo huko Airpot nae?"
aliuliza swali yule dereva lakini maswali kuhusu Fredy hakuyapenda kabisa Asu na aliishia kunyamaza na hata yule dereva aliamua kukaa kimya kutouliza tena.

Mawazo juu ya hali ya Fredy ambae aliamini si rahisi kupona kutokana na maelezo aliyoambiwa na yule daktari yalizidi kuitesa fikra ya Asunta muda wote alipokuwa anaendeesha gari.
wakiwa bado njiani simu ya Asu iliita zaidi ya mara nne bila Asu kuipokea wala kuiangalia kujua mpigaji akiamini lazima itakuwa kule hospitali tu wanataka kumpa taarifa ya kifo cha Fredy hivyo aliipuuza na kuendelea kupiga gea na haikuchukua muda mrefu sana kufika uwanja wa ndege wa Nairobi kutokana na hali ya barabara jioni ile kuwa shwali kabisa bila msongamano wa magari.
Aliegesha gari sehemu maalum ya maegesho nje ya uwanja ule na kushuka akimuelekeza dereva arudishe gari nyumbani, lakini mara kabla dereva yule hajamjibu chochote Asunta macho yake yalishangazwa na upande alipokuwa anaangalia kulipokuwa na lango kuu la kutokea uwanja wa ndege.
"dada, dada dada Asu hebu angalia kule? si baba Askofu yule pale na mama !!"
alishangaa sana yule dereva na kumwita Asunta aliyekuwa anataka kuondoka na hata yeye mwenyewe Asunta moyo ulimlipuka mno mara baada ya kuona ni kweli kabisa baba Askofu yuleyule na mkewe wakiwa wamesimama eneo karibu na lango kuu la kutokea linalotumiwa na wasafiri tena wakiwa wanahangaika kufanya mawasiliano na haikuchukua dakika nyingi simu ya mkononi ya Asu iliita tena na ndipo safari hii alipoitoa mfukoni na kuangalia kumbe mpigaji muda wote alikuwa ni baba Askofu..
Moyo ulimlipuka na kuanza kumuenda mbio huku akili ikiwa imeganda asijue nini afanye.

* * * * *
DAR - TANZANIA
_____________________

Uwanja ulilipuka shangwe pindi timu zilipoanza kuingia kwaajili ya kuuanza mchezo ule wa kukata na shoka baina ya mahasimu wakubwa watoto wa uswazi Tandale fc na vs Friends Langer.
Hali ya hewa ya jiji la Dar siku hiyo ilikuwa moja ya kivutio kikubwa sana kutokana na kutokuwa na joto sana huku kiupepo mwanana kikipuliza na hali ya jua la wastani sana lililozidi kuwapa hamasa hadi wachezaji wenyewe.
("Hapa leo ndio nakata tiketi sasa")
aliwaza Dullah moyoni akiwa kasimama hukukaukanyaga mpira akisubiria firimbi ya muamuzi huku macho yake yakiutazama uwanja hususani upande wa wapinzani wao hasa kule golini mara baada ya shilingi kurushwa na wao ndio waliotakiwa kuanzisha kipute kile.

'PRRRRRRRIIIIIIIII'
Kipyenga kilipuliza na Dullah kulisukuma gozi kumuanzishia Roja aliyeurudisha mpila nyuma kwa kisheti ambae nae alipasi pembeni taratibu na kumkuta Joshua aliyeukokota kidogo na kuuleta tena kati kwa Roja ambae alitishia kama anapiga na kumuinulia Ismaili upande wa pembeni aliyeutuliza mpra kwa mbwembwe na kumzidi mbio beki wa Friends na kuendelea kuingia eneo la hatari na kuumimina ndani mpira kwa Roja ambae nae aliususa na kuwadanganya mabeki waliojua anautuliza na ndipo mpira moja kwa moja ulikutana na Mliberia Dullah na hapo uwanja mzima haswa upande ule wa Tandale ulilipuka shangwe za kutosha kwa jinsi vijana wao walivyolianzisha lile kabumbu na kutakata vilivyo wakiwafanya Friends kuhaha kuutafuta mpira kwa tochi na siku zote Tandale walishajiekea usemi wao pindi mpira anapokuwa nao Dullah husema kuwa 'Mpira umefika kwao'
Na kweli Dullah baada ya kupokea pasi ile aliingia kwa speed eneo la hatari na kutisha kama anaachia shuti kali na kuwafanya mabeki wawili wa Friends wote waslide na kuseleleka kwa kudanganyika na hapo ndipo alipowafinya kwa style ya aina yake huku shangwe likiongezeka pindi Dullah alipomvisha dalizi beki wa mwisho na kuingia eneo la box kiulaini na kipa alipotokea kufanya jitihada za kumzuia Dullah asifunge nae alirambwa chenga ya maudhi sana na D alipobaki ndani ya mita sita yeye na goli huku mashabiki wa Friends, viongozi na wachezaji wakiwa hawaamini kinachofanywa na rasta yule mbele yao kwa kuiandikia Tandale bao la kuongoza dakika ya pili tu tangia mpira kuanza huku wao wakiwa hawajaugusa hata kidogo.

'ROAD TO KENYA' Yalionekana maneno haya tena kifuani mwa Dullah pindi alipokuwa anashangilia bao lake sambamba na wachezaji wenzake na kupita pembeni ya uwanja ambapo mashabiki wa Tandale waliangua shangwe na kuanza kumuimbia shujaa wao na hata wale mascout wa Tusker walisimama na kumpigia makofi Dullah huku wote wakiamini ni chaguo sahihi kabisa.

Nani ambae hakuiona tofauti baina ya Dullah na wachezaji wengine 21 waliobaki uwanjani pindi mpira ulipokuwa unaendelea?
Nani ambae hakushangazwa na uwezo binafsi aliokuwa anaonesha Dullah?
Ama kwa hakika moto wa Dullah ulizidi kukolea siku hadi siku na ndio sababu siku hiyo hadi mpira unaisha Friends kwa mara ya kwanza walilala kwa mabao matatu kwa moja tena yote wakifungwa na mchezaji ambae alitolewa dakika ya sabini mara baada ya kocha kuingiwa na wasiwasi ya kuumizwa pindi alipoona Friends wameanza kumuwinda kwa kumchezea mpira mchafu Mliberia Dullah Rasta.
Yeye ndie alikuwa nyota wa mchezo siku hiyo.

* * * * * *

Baada ya siku moja ya mapumziko waliyopewa kufurahia ushindi wao walioupata siku hiyo kama kawaida majira ya jioni mazoezi kwa vijana wa Tandale yaliendelea na kutokana na kutokuwa na wakala muda mfupi baadae Dullah aliitwa na uongozi wa timu yake ya Tandale na kwenda moja kwa moja kwenye ofisi ndogo iliyokuwa pale maeneo ya shule karibu na ofisi ya kubwa ya serikali za mitaa.
"Usikubaliane na hizi Ofa Dullah kataa tu sisi tutakuongezea mshahara hawa hawana lolote wanataka wakakiue kipaji chako tu"
yalikuwa ni maneno ya kocha msaidizi pindi alipokuwa anaongozana na Dullah kuelekea kule ofisini ambapo kwa nje aliona sura ngeni za watu wawili wakiwa wamekaa kwenye benchi na alipoingia ndani ya ofisi alishangaa kukuta karibu jopo zima la uongozi wa Tandale wakiwa wanajadili huku wakibishana bishana na jina lake ndio lilichukua nafasi kwenye mjadala ule.
"Karibu Dullah, sasa ni hivi kijana wetu shujaa wetu, mwana Tandale mwenzetu... kuna ofa zimetumwa hapa kutoka club Nne, tatu za hapa hapa Tanzania zote zikiwa ligi kuu na moja kutoka kenya tena wao hawakutuma barua tu bali kuna watu wao wamekuja kabisa tumewambia wasubiri hapo nje.
Timu kutoka Tanzania ya kwanza kutuma ofa ni Mtibwa na katika barua yao wameahidi kutulipa milioni 3 za usajili wako pia mshahara wa laki tano watakuwa wanakulipa kila mwezi pamoja na bonasi ndogo ndogo endapo utakubali ofa yao... ya pili kutuma ofa ni club ya Simba ambao wao wameahidi kukulipa laki saba kwa mwezi ila kuhusu uhamisho wametuekea gepu sisi, ya tatu ndio hawa wa Kenya wanaotoka Nairobi ktk club ya Tusker wao wameahidi kukulipa elfu sitini za Kenya kwa mwezi na kuhusu uhamisho wako wapo ladhi kuzungumza na sisi... Na ofa ya Mwisho tuliyoipokea leo asubuhi hii imetoka kwa Becker fc wao wametenga mil 5 za usajili na mshahara wako wamedai watakulipa kwa wiki laki tano sawa na mil 2 kwa mwezi.
Sisi tumejadili lakini bado tumekuita mwenyewe utoe tamko kwani tunakuhitaji na tungependa ubakie ili tuwepo ligi kuu pamoja naamini huko ndipo thamani yako itapanda au unasemaje"

alimaliza kuongea yule kiongozi na wote macho na masikio waliyaelekeza kwa Dullah ambae waliamini kuwa lazima atachagua ofa ya Becker fc kutokana na kiwango kikubwa cha pesa walichoeka ama atachagua Simba kutokana na ukubwa na umaarufu wake lakini jibu la Dullah ndio liliwashangaza sana na hawakulitegemea japo kuna wachache walihisi.

"Naipenda sana Tandale na miaka yote itakuwa moyoni mwangu hata niende wapi, lakini ndoto zangu zilikuwa Kenya hususani Nairobi, napapenda sana tena sana.. Niko tayari kujiunga na Tusker kwa moyo mmoja tena sasa hivi naomba muwaite tu wanisikie. Chaguo la ndoto zangu ni Kenya."
ndivyo alivyoongea Dullah na kuwafanya viongozi wa Tandale wabaki wanatazamana.
"Una hakika Dullah unachoongea..?"
"Kabisa Kocha"
"Mi naona angesubiri msimu uishe"
aliongea Mwenyekiti wa timu ya Tandale na kumfanya Dullah amgeukie na kumuangalia kwa jicho la hasira ambalo hata yeye hakulitegemea.
"Eeeh! hebu waitwe hao watu"
aliongea tena Mwenyekiti baada ya kustushwa na jicho la Dullah hali ile iliwashangaza na wengine hususani kocha ambae hakutaka kabisa Dullah aachiwe aende.
"Kwani muheshimiwa anasemaje?"
alihiji kocha msaidizi akimuulizia mdhamini wa timu ambae nae alijitolea kumpangia Dullah makazi kule Sinza yaani mh Diwani.
"Aaah! sa unafikiri atafanyaje kama kutakuwa na mkwaruzo na mchezaji mwenyewe kumbukeni kuna kipengere cha Tff kinatubana na tukisema tumzuie hadi mwisho wa msimu lazima ataondoka bure na tutakosa kuambulia kitu, nyie waiteni tu hao jamaa si ndio mapenzi yake mwenyewe au sio Rasta."
aliongea tena yule mwenyekiti wakati huo wote Dullah alibaki kimya akiwaangalia bila kujibu kitu.
Baada ya mvutano wa hapa na pale ndipo walipomuomba Dullah atoke kwa kigezo kuwa watamwita baada ya muda mfupi, ndipo baada ya kutoka Dullah waliwaruhusu wale wakenya kuingia tena na wakajadili nao kwa zaidi ya saa zima Dullah akiwa nje akisubiri mpaka pale alipoitwa tena.


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 27



"Bwana Dullah hawa ndugu zetu tumeongea na kukubaliana kama tulivyoongea na kwa matakwa yako wamekubali kulipa gharama zote kwetu na Tff hivyo wiki ijayo mambo yakiwa tayari itakuwa safari ya huko Kenya utapoenda kusainishwa mkataba rasmi pindi utapofuzu vipimo vya afya ila hapa kuna mfano wa mkataba huo, tumia dakika tano kuusoma kwa umakini kwanza."
aliongea mwenyekiti na kumkabidhi Dullah makaratasi matatu yaliyobanwa pamoja ambayo yalichapishwa vizuri waliyokuja nao wale wakenya.

Baada ya dakika kadhaa Dullah alipomaliza kuusoma ule mkataba aliukubali kwa moyo mmoja na hapo ndipo walipopeana mikono na kupanga kuwa taarifa zile zifike Tff kesho yake ili keshokutwa zifanyike taratibu za uhamisho na usajili kwa kujumlisha pasi ya kusafiria na makazi kisha baada ya kila kitu kukamilika wiki ijayo acheze mechi moja ya kuwaaga mashabiki wa Tandale na siku mbili baadae safari ianze.

Swala lile lilimfurahisha mno Dullah na moyo wake ulifunguka na kumshukuru Mungu huku akiwa haamini kama ile kauli ya rafikiake kipenzi Roja imetiki mapema vile.
"Asanteeee Rojaaaaaaaaaa wewe ni zaidi ya Rafikiiii"
aliongea kwa furaha Dullah pindi aliporudi uwanjani na kukutana na Roja mara baada ya mazoezi kuisha alimkumbatia kwa furaha sana.
"Welldone D, nitakukumbuka sana rafiki angu"
alijibu Roja baada ya kugundua kuwa dili la Dullah kwenda kucheza Kenya limekamilika kwa asilimia kubwa.

Siku zilienda na mambo yalikuwa mepesi kabisa baada ya wale mascout kuwasiliana na matajiri zao na viongozi wakuu wa Tusker ambao walizipokea kwa furaha habari zile na kutuma kiasi cha pesa kufanikisha haraka zoezi lile kwa wale maskauti na ndipo walipomaliza kila kitu Tff na serikalini na sasa Dullah akawa ni mchezaji mtarajiwa wa Tusker kwa asilimia tisini.
Siku hiyo majira ya saa 3 usiku Kama kawaida kila kilichokuwa kinaendelea juu yake hakumficha hata siku moja mamaake, alimpigia simu na kumjuza lakini mama hakupenda hata kidogo mwanae aende mbali zaidi tena nchi nyengine ambayo hata yeye hajawahi kufika bila hata kurudi nyumbani wamfanyie matambiko na mila za kwao..!
Lakini kwa Dullah alimsihi na kumpa maneno matamu mamaake akimuahidi hakuna tatizo lakini mama bado alipinga kabisa ndipo Roja alipomuomba Dullah amruhusu aongee na mamaake ili amsaidie kumuelewesha na hapo mama Dullah pindi alipoisikia sauti ya Roja alianza kutulia na kumsikiliza kwa umakini kutokana na jinsi Roja alivyojua kuongea na kushawishi kwa hekma na ujanja wa ajabu.
["Mama, kiukweli uko sahihi kabisa nami naungana na wewe lakini nilichokuwa nakuomba kitu kimoja, hii ni nafasi ya kipekee sana aliyoipata Dullah ambayo wengi waliililia na kwa bahati mbaya miakataba yote ipo Kenya.. kwahiyo naomba mama mruhusu Dullah aende kwanza akasaini hiyo mikataba harafu baada ya nusu msimu wa ligi kuisha kwenye ile likizo ya mwezi atatumia muda huo kuja kukamilisha mambo ya mila kwani ni Muhimu sana mama, najua kabisa"]
Maneno ya Roja yalimrainisha mama Dullah na kukubali mwanae aende huko Kenya ila kwa sharti hilo kuwa lazima aje arudi kufanyiwa hizo mila baada ya huo Muda.

Siku ya mechi ya mwisho ilifika ambayo ilikuwa ndani ya uwanja wa shule wa Tandale fc.
"Man, nitakumiss sana "
"Hata mimi Roja siamini kabisa kama kweli leo ndio siku yetu ya mwisho kucheza pamoja"
"No, usiseme hivyo Dullah milima haikutane inawezekana siku moja tukacheza tena pamoja kama leo hata kama haitakuwa Tandale"
Waliongea na kupeana moyo Dullah na Roja na mra firimbi ya refa kuwaita wachezaji kati ilipulizwa ndipo wageni walitangulia uwanjani wakifuatiwa na Tandale waliokuwa wakishangiliwa kwa nguvu zote na mashabiki wao huku kioja kikiwa kwa shabiki mkereketwa au naweza kusema shabiki aliyechanganyikiwa na Tandale ambae hata umwambie Tandale na Barcelona wakicheza atabet wapi yeye lazima atakwambia Tandale tu na huwezi kubishana nae.
Huyo si mwengine ni bwana Chidy Ng'ole ambae alionekana akiwa kifua wazi huku ameshika bango lililoandikwa maneno MLIBERIA BAKI NA SISI
... Dullah alimuangalia yule shabiki na kulisoma lile bango lililomfanya moyo kumuuma kidogo kwa kujua kiasi gani alipendwa na wana Tandale, lakini aligeuka tena safari hii kwa mshtuko kutazama upande ule aliposimama yule shabiki baada ya kukiona kitu ambacho awali alikipuuza lakini moyo wake ulimlazimisha ageuke tena ahakikishe kile akionacho na hapo alijikuta anasimama kwa taharuki akiwa haelewi ni mawazo yake ndio yalikuwa yanamtengenezea kile anachokiona ama ni kweli kile anachokiona ndicho? Hii ilikuwa ni zaidi ya bango la Chidy Ng'ole

* * * * * *
- NAIROBI AIR PORT -
____________________

Alitafakari nini afanye Asu na kuona ni bora ajibane tu apokee ile simu ajue cha kudanganya hapo hapo japo ukweli hakuwa mjanja katika uongo.
"Hallow baba"
[["Eeh! Asu mwanangu mbona simu yako haipokelewi muda mrefu mama? Nimepiga na kaka yako halkadhalika ndio haipatikani kabisa vipi kwema?"]
"Kwema kiasi baba si kwema"
[["Vipi mama, kuna mtu anaumwa au nini kimetokea?"]]
"Babaangu nimepigiwa simu mgonjwa sana ndio sasa tunakaribia kuondoka uwanjani hapa Nairobi"
uongo huu wa Asunta ulimfanya yule dereva aliyekuwa anaibia kumsikiliza astuke zaidi na kuanza kumtilia shaka Asu kuwa lazima kuna kitu kibaya kinaendelea.
[["Mbona hata sisi tupo Airport hapa Nairobi tumeshuka muda si mrefu, uko kwa wapi.. Oooh! Kumbe Pastor George kazidiwa bila kutuarifu na sisi aaah, juzi tu tuliwasiliana nikiwa London dah! uko wapi Asu mwanangu"]]
Aliongea Askofu kwa mshtuko huku akiangaza huku na huko na mara alibutwaa kwa mbali kuiona gari aliyopenda kutembelea mwanae ambae ni Fredy na Asu aliposhtukia hilo ilibidi ajikwepeshe na kujifanya hajawaona huku akielekea kule upande wa kuingilia uwanjani na kukata simu kikauzu kwa makusudi na kuwahi kujichanganya na watu asionekane.
Lakini mara Askofu alimuona na kuanza kumkimbilia huku akimwita
"Asunataaa, Asuntaaa, Asuntaaa mama subiri"
aliita Askofu ndipo Asunta huku moyo ukimuenda mbio alijikuta anasimama na kugeuka nyuma na kumuona Askofu akiwa anatweta japo hakukimbia sana.
"Mwanangu , usichanganyikiwe... Mamaako ataenda tu nyumbani na dereva aliyekuleta. itabidi mimi na wewe tuongozane Tanzania kumuona baba"
Kauli ya Askofu iliuchoma moyo wa Asunta na kuusisimua mwili mzima kwa mshtuko mkubwa.

"Hapana baba, nyinyi ndio kwanza mmetoka safari, pumzikeni tu harafu isitoshe ndege niliyoikatia tiketi inaondoka muda si mwingi baba naomba niwahi"
aliongea Asu na kuondoka akiwa mtu mwenye haraka na kumshangaza Askofu aliyebaki ametumbua macho akiwa haamini jinsi bint alivyochanganyikiwa.
("Ama kweli mzazi anauma! .. Asu anawapenda sana wazazi wake, yaani kabadilika namna hii hasikii wala subira hana!!?")
aliwaza moyoni Askofu na kuanza kupiga hatua kurudi kule alipomuacha mkewe akiwa kasimama akiwashangaa baada ya yule dereva kwenda na kuanza kubeba vibegi vidogo viwili kwenda kuvipakia kwenye gari.
"Mme wangu kulikoni?! mbona imekuwa kama picha ya kihindi hapa?!"
alihoji mama Askofu baada ya kumuona mumewe amerudi kwa unyonge taratibu bila Asunta ambae alikuwa amemkimbilia.
"Aaagh, mke wangu mtoto amechanganywa sana na hali ya babaake."
"Ina maana kweli Pastor George amezidiwa kiasi hiko ghafra hivi!?"
"Yaani hata mimi nashangaa."
"Si juzi tu tulizungumza nae!!"
"Mh! mke wangu binaadam muda mwengine si kitu, muda wowote mtu anaweza kubadilika ama kufa, Mungu ameeka siri kubwa sana kwetu"
"Dah! hebu mme wangu jaribu kumpigia Pastor George kwanza tujue kinachoendelea"
"sawa mke wangu ila twende kwanza nyumbani kwanza tuonane na Fredy tueke mambo sawa ikiwezekana alfajiri kesho mimi niende Tanzania"
"sawa mme wangu"
alijibu mama Askofu na kuongozana na mumewe hadi ilipopaki gari yao na kujitoma ndani yake.

Wakiwa njiani Askofu alijaribu kumpigia Pastor George lakini kwa bahati mbaya simu haikupatikana hata alipojaribu zaidi ya mara tatu.
"Mh! mke wangu, nazidi kuwa na wasiwasi na hali ya rafiki angu Pastor George, simu zake zote hazipatikani"
"Mh! lakini kwanini hawajatutumia hata ujumbe hao ndugu waliowasiliana na Asunta?"
"Yaani hata mimi nimeshangaa sana, huenda wakawa wamechanganyikiwa."
alijibu Pastor huku akituma ujumbe wa maneno kwenye namba za Pastor George akimuombea Mungu apone mapema pia baada ya hapo kimya kingi kilitawala baina yao ndani ya gari.
Kwa upande wa dereva aliokuwa anawaendeesha muda huo yeye mawazo yake yalikuwa tofauti na wao.
("Mh! huyu binti huyu binti nina wasiwasi nae..! kwanza alitoka na Fredy jana usiku hawajarudi.. Amerudi leo pekeake akiwa katika hali ya kuchanganyikwa..!! harafu ametoka akidai anaenda London ametumiwa tiketi na baba Askofu..!! Tena anakutana na baba Askofu anasema anaenda Tanzania babaake mgonjwa!!? Mh.. hapa si bure kuna kitu tu nina mashaka na usalama wa Fredy")
Yalikuwa ni mawazo ya yule dereva baada ya kusikia mazungumzo ya Askofu na mkewe pale nyuma walipokaa.
Alitamani kuwaambia hali halisi ilivyokuwa lakini moyo ulisita na kushindwa kujua ataanzia wapi na kubaki amelimezea kifuani mwake na kunyoosha usukani mpaka nyumbani kwa Askofu Mbukinyo.

* * *

Upande wa pili alionekana Asunta akihaha uwanja wa ndege huku akienda huko na huko kulazimisha safari siku ile na kwa kutumia jina la Askofu Mbukinyo na la babaake Pastor George kidogo uongo wake ukazaa matunda na kukubaliwa kusafiri kwa ndege maalum iliyokuwa inaelekea Dar Tanzania kupeleka wanakwaya wa Kiroman kutokana na ratiba ya ndege ya abiria kuondoka usiku baada ya ile ya mchana aliyoitegemea kumuacha kwa dakika kadhaa pindi alipokuwa katika mizunguko mule ndani ya vyumba vya uwanja ule wa Nairobi.

Alikuwa haamini pindi ndege ile ilipoiacha ardhi ya Kenya baada ya kupaa na kuanza kuchana mawingu kuitafuta anga ya jiji la Dar nchini Tanzania,
Asunta alimshukuru Mungu kimoyo moyo na kuzidi kumuomba afike salama na lengo lake kuu lilikuwa moja kwa moja afikie Tandale akutane na Dullah ili wajue watorokee wapi watapoweza kuishi kwa amani kwani alijua lazima atakuwa amemuua Fredy na atatafutwa na polisi kwa kesi ya mauaji kwa kujulikana yeye ndie mtu wa mwisho kutoka na Fredy nyumbani na alirejea nyumbani mwenyewe tena kwa gari la Fredy na hakuusema ukweli jambo ambalo alihisi lazima litawaaminisha kuwa alimuua Fredy.
Moyo wake ulijilaumu kwa kubaini kuwa ameshindwa kuusuka uongo vizuri na zaidi alijiona hana bahati kwa kukutana na Askofu pale uwanjani kwani watapogundua ukweli watamshusha thamani kubwa na kumkasilikia mno, lakini hata hivyo alijiuliza angetumia uongo gani ambao usingekuwa na madhara?
hapo alikosa jibu na kuamua kuongeza sauti ya mziki uliokuwa unasikika kwenye headphones za simu yake zikiwa masikioni mwake na kujilazimisha kujipa faraja ambayo ilikuwa haiji hata kidogo moyoni mwake.

Majira ya jioni ndege ilitua DsM Tanzania na hali ya hewa ya jiji la ilionekana ni tulivu mno taratibu Asu baada ya kushuka hakuzubaa kujichanganya na kuwapotea wale wanakwaya waliokuwa wote ndani ya ndege na kuelekea moja kwa moja upande wa nje zilipo Taxi.
Naam wanasema hata Mbwa koko anapokuwa maeneo ya kwao huwa mkali kwa kujiamini, na ndivyo ilivyokuwa kwa Asunta ambae sasa alikuwa mitaa ya nyumbani aliijua kila kona ya ule uwanja ambao mara nyingi walifika pale kama sio kumpokea babaake basi hata safari za mule ndani ya nchi alizosafiri kishule ama kifamilia pamoja na wazazi wake zilitosha kumjengea uwenyeji wa pale.
Baada ya kutoa kiasi furani cha pesa kupitia ATM iliyokuwa mule uwanjani Asu aliingia kwenye ile Taxi na kumpa maelekezo dereva.
"Twende Tandale kwa Tumbo"
"Elfu thelathini na tano"
"Hakuna tatizo twende"
aliongea Asu kwa kujiamini na kumfanya dereva awashe gari na kuondoka eneo lile la uwanja wa ndege wa mwl J.K. Nyerere.
("Siamini kama leo hii naenda kuonana na D wangu daah! nitamsuprise sana")
aliwaza Asu kipindi gari ikichanja mbuga kuitafuta Tandale.

* * *


ITAENDELEA
 
SHEMU YA 28



Gari ilifika getini na kuingia ndani ya mjengo ule mkubwa wa Askofu Mbukinyo ambapo baada ya kushuka na kuingia ndani walipokelewa na wale wadada wa kazi lakini kuna kitu Askofu alikihisi hakipo sawa mara tu alipoingia mazingira ya nyumba yake.
"Vipi kwema kabisa hapa,?"
"Kwema tu baba"
"Mh! ok au ndio mna majonzi na habari zilizomstua shoga enu Asu eeh"
aliongea Askofu kauli iliyowafanya wale madada watazamane tu na kushindwa kuelewa wajibu nini
"Fredy yuko wapi ?"
aliuliza Askofu swali lengine lililowafanya tena wale madada watazamane wakati huo mama Askofu alikuwa ameshapandisha juu kuel chumbani kwao lakini Askofu Mbukinyo alizidi kuwa na wasiwasi na hali ya pale baada ya kuona wale mabinti wanajiuma uma kujibu hali iliyomfanya asimame na kuwahoji kwa umakini zaidi wamwambie nini kinaendelea pale.
"Eti, mbona siwaelewi wanangu mnaonekana mna wasiwasi harafu kama mna huzuni na mnashangaa maswali yangu kulikoni?"
alihoji Askofu lakini kabla hajajibu mlango uligongwa na aliingia yule dereva aliyewaendeesha kutoka uwanja wa ndege muda mfupi uliopita huku akihema na jicho limemtoka akionesha wazi kapata habari zilizomstua sana zinazomuhusu aidha yeye binafsi hivyo amekuja kuaga ama zinamuhusu bosi wake mweneyewe ambae ni Askofu.
"Bosi bosi baba Askofu"
aliita yule dereva huku akihema
"Vipi tena kuna nini"
"Kuna mtu hapo nje Uupphhhh kuna mtu kaleta habari mbaya sana baba"
"Zipi tena hivyo"
alistuka Askofu sambamba na wale mabinti walibaki wamepigwa butwaa nao wakati wakisikiliza taarifa ile iliyoletwa na yule dereva.
"Kuhusu Fredy baba, kuhusu Fredy."
"Fredy kafanya nini tena mwananguuu"
Ilisikika sauti ya mama Askofu akishuka ngazi harakaharaka mara baada ya kuona mumewe anachelewa kule juu ndipo alipobadili nguo kurudi kujua nini kinamchelewesha na hapo ndipo aliposikia sauti ya dereva wao akiongea huku akihema sana.
"Fredy baba amelazwa hali yake sio nzuri kabisaa uuuphh"
Kauli hii ilimfanya hadi mama Askofu apige mweleka pale kwenye ngazi kwa mshtuko mkubwa na kuwastua na wengineo ambao walistushwa na taarifa ile ya ghafra.

"Irene mke Wanguu!"
aliita Askofu tena kwa kutaja jina kabisa la mkewe ambao hata wale madada hawakulijua na kumsaidia kumuinua pale kwenye ngazi pindi alipokuwa anajizoazoa huku akiwa kajipasua sehemu za juu za mdomo na vidamu kuanza kutoka.
"Hapana baba Fredy niache, mi sijaumia bwana tuwahi huko hospital kumuona mtoto."
aliongea mke wa Askofu na kumtoa mkono mumewe aliyemshika baada ya kuhisi mkewe ameumia kutokana na ule mweleka na moja kwa moja mama Askofu alifungua mlango wa kutokea akifuatiwa na mumewe sambamba na yule dereva.
"Kijana mwenyewe yuko wapi?"
aliuliza Askofu
"yule pale baba"
"Hebu kijana twende kwenye hiyo hospitali anayosema."
"Aliongea Askofu na kupanda ndani ya gari mara baada ya dereva kutangulia sambamba na mkewe aliyekaa siti ya nyuma akiwa analia hanyamazi.
"sasa mama Fredy mbona unafanya uchuro?! pengine tunaweza kufika pale tukakuta sio Fredy aliyelazwa bali wamefananisha vibaya."
"Mh! mme wangu mi nina wasiwasi sana lazima atakuwa yeye Fredy vilevile Asunta inawezekana alikuwa na taarifa hizi hapo kabla au huenda walikuwa wote, aaaaah! Fredy mwanangu uuuuuu"
aliendelea kuongea kwa uchungu mama Fredy kipindi hiko dereva alikuwa speed ya hali ya juu na kabla hawajafika kule hospitali ndipo simu ya mkononi ya Askofu ilipoita na alipoangalia jina alikuwa ni Pastor George na kuanza kusita kwanza kuipokea akidhani sasa huenda rafikiake akawa amefariki na sasa walikuwa wakiwaarifu rafiki zake kupitia simu yake marehemu.
"Nani huyo baba Fredy, mbona unajifikiria kupokea"
aliuliza mama Fredy mara baada ya kuona mumewe akijifikiria kupokea ile simu.
"Kha!1 we acha ni namba ya Pastor George sasa sijui ndo mzima au kazidiwa ama wanataka kutujuza kuwa amefariki wazidi kunichanganya yaani daah! "
aliongea kwa masikitiko Askofu .
"sasa si upokee tu mume wangu unajuaje kama ndio hivyo, mi nahisi huenda mawazo yako ndio yanakudanganya baba Fredy, pokea bwana"
alisisitiza mama Askofu huku akili yake yote ikiwa huko hospitali wanakoenda na ndipo hapo Askofu alishusha pumzi na kupokea ile simu.

Lakini pindi Askofu alipopokea na kuanza kuongea kuisikiliza sauti upande wa pili alibaki kataharuki ndani ya gari na kushindwa kujibu chochote mwishoe aliamua kukata simu kwanza.
"Vipi baba Fredy!?"
aliuliza mama Askofu
"Huyu ni Pastor George aliyenipigia"
"Ina maana kapona?!!"
"Sio kama kapona, bali ni mzima buheri wa Afya haumwi hata chembe."
"Whaat,!? Asuntaa..!!!"
alihamaki mama Askofu wakati huo gari ilikuwa inaingia pale hospitalini.

* * * * * *
DSM - TANZANIA
_______________________

Taxi ilifika maeneo yale ya Tandale kwa tumbo majira ya saa moja kasoro jioni kutokana na usumbufu wa foleni na miundombinu mibovu ya barabara ya Tanzania.
Alishuka msichana mrembo Asunta kwenye ile Taxi baada ya kumlipa ujira wake yule dereva na taratibu alianza kuongoza njia ambayo haikuwa ngeni sana machoni mwake huku moyo wake ukiwa na shauku moja tu la kuonana na Dullah.
("Lazima sasa ivi atakuwa karudi mazoezini mwenyewe aaah D bwana")
aliwaza moyoni Asu huku akikatiza vichochoro kwa hofu na umakini mkubwa hadi alipokaribia kwenye ile nyumba aliyokuwa anaishi D wake.

Aliukaribia mlango wa chumba alichokuwa anaishi Dullah lakini kabla hajasogea kuufungua mara alijikuta uso wake ukifula hasira baada ya kusikia kicheko cha mwanamke na mara akiwa kasimama akifikiria cha kufanya ndipo alipomshuhudia binti mmoja akitoka mule chumbani akiwa kajifunga kanga na taulo huku mkononi akiwa amebeba plastiki dogo lililojaa maji na kopo la sabuni na kugongana nae mlangoni uso kwa uso.
"Aaah! We Anti Vipi..! Umetumwa?!!"
alitahamaki kwa hasira yule bint baada ya kugongana na Asu kwa bahati mbaya kutokana na kusimama kwake jilani kabisa na mlango.
Kauli ile ilizidi kumchukiza zaidi Asu ndipo ghafra alimkamata koo yule binti na kuanza kufiligisana pale chini huku akimsababisha mwenzake kumwaga lazi hivihivi.

Kelele ya ndoo na kishindo cha watu kudondoka jilani ya ule mlango ndio kilimstua yule bwana aliyekuwa ndani na kutoka haraka ambapo hakuamini kumkuta mkewe na msichana mwengine asiyemfahamu wakigalagazana chini na kuwavuta wapita njia muda mfupi na majirani waache shughuli zao na kutoka kuangalia sinema ya bure iliyokuwa inaendelea.
"Hebu achianeni nyinyi vipi?!! Wee hebu muache Mwenzako"
aling'aka mwanaume huku akiidadavua mikono ya Asu iliyokuwa shingoni mwa mkewe ambae ukweli alishazidiwa baada ya kuwahiwa na Asu.
Lakini moyo ulimlipuka Asunta na kumuachia haraka yule binti mara baada ya kuutazama uso wa mwanaume aliyetokea chumbani na kuja kuwagombeza kuwa tofauti kabisa na alivyodhania awali kuwa aliyekuwa ndani ya yule bint ni Dullah.
"Shemsa rudi ndani alaah! sitaki kelele hapa na wewe bint imekuwaje kuja kuleta ghasia na kumdhalilisha mke wangu namna hii?"
"samahani kaka bahati mbaya."
"Bahati mbaya..!? yaani wewe umepita nyumba zote huko umefika hapa, umemvizia mke wangu anaenda kuoga umemvamia na kumdhalilisha tena kwa kumkaba haswa harafu nakuuliza tatizo unasema bahati Mbaya..?!!"
aling'aka yule bwana na kumzaba kibao kimoja Asunta kwa hasira hasa alipokumbuka mkewe alivyokabwa muda mfupi.
"Nielewe hivyo kaka ni bahati mbaya kwani hapa ni kwa mchumbaangu so, nilivyomuona mkeo anatoka nilijua ni mwanamke anayeniibia mtu wangu aah! Wapi Dullah wangu miee"
aliongea Asu kwa kujikaza na kukisikilizia kile kibao ambacho kilimuuma vilivyo na kumsababishia machozi kumtoka
"Sikia we bint, hapa sisi tumehamia huu mwezi wa sita sasa sasa unanishangaza unaposema ni kwa mchumbaako,! Mchumbaako gani sasa?"
"Jamani kaka, hapa ndipo kwa mchumbaangu anaitwa Dullah!! sijakosea kabisaa nyumba ni hii hii"
aliongea Asu huku akijifuta machozi
"Wee bint yaani leo ungenikuta nishafanya vitu vyangu maskani..! basi saa hizi tungeongea mengine, sikia usitujazie kiwingu mi naitwa Mussa au baba Kidi na huyu uliyemvamia ni mke wangu anaitwa Shemsa. Naomba uondoke sasa hivi kaulizie kwengine kabla mizimu ya kwetu haijahamia hapa nikakutafuna mzimamzima"
aliwaka yule bwana na kumfanya Asunta aondoke haraka huku akiwa na hofu kubwa.

Na huo ndio ukawa mtihani mkubwa kwa Asu kujua wapi alipo Dullah na hakuwa na uzoefu na maeneo yale ya uswahilini na muda wote aliamua kuzima simu kwa kuhofia kutafutwa na wazazi wake kwani alihisi lazima issue nzima juu yake na Fredy ishabumbuluka na nyumbani kwao washapata taarifa hivyo aliona hata kama angeamua kwenda kwa kina Vero bado isingesaidia kitu, ndio kwanza angejipa wakati mgumu na kujitengenezea mazingira rahisi ya kukamatwa.
Alielekea moja kwa moja mpaka kwenye guest ya pale kwa tumbo stendi na kulala huku akili na mawazo yakiwa juu ya Dullah wapi atampata na nini hatma yake.

Zilipita siku nne Asu akihaha kumtafuta Dullah huku akiwa amevaa baibui na nikabu kwaajili ya kujificha ili asije onekana na mtu anayemjua katika harakati zake za kumtafuta Dullah na kila siku alienda mazoezini uwanja wa TP na ndio kosa alilolifanya kwa kukalili siku ile ya Mechi kati ya Simba na Tandale iliyochezwa uwanja wa TP aliamini kuwa D huwa anacheza pale bila kujua kuwa ile timu iliyokuwa inafanya pale mazoezi haikuwa Tandale fc.
Lakini kosa lengine alilokuwa anakosea ni kumuulizia kwa jina la Dullah kwani nje ya Tandale fc wengi walimtambua haraka Dullah kwa jina la Mliberia au Rasta wa Tandale lakini hata hivyo Asu aliweza kujibiwa swali lake baada ya siku moja usiku alipokuwa anakula kwenye mgahawa mmoja huku akiangalia habari ndipo alipoiona picha ya Dullah wake akitangazwa na chama cha soka Tanzania kuwa usaili wake wa kujiunga na club ya Tusker ya Kenya umefanikiwa na kuruhusiwa kucheza mechi moja ya mwisho kwa niaba ya kuwaaga wana Tandale, mechi ambayo ilitangazwa itafanyika kwenye uwanja wa Tandale sokoni kesho yake saa kumi jioni.
Moyo ulimlipuka wa furaha na kutoamini hadi akashindwa kuendelea kula kwa shauku ya kukutana na D wake hiyo kesho.
Na kweli asubuhi na mapema Asu alichukua Taxi na kwenda kufanya shopping za suprisse na kununua nguo, viatu na kadha wa kadha kwa niaba ya Dullah.
Na ilipotimu majira ya jioni aliamua siku hiyo kubadilisha muonekano wake aliojipachika baada ya kurudi TZ na kuacha uso wote nje ili iwe rahisi hata Dullah atapomuona kumtambua.. na ndivyo ilivyokuwa ndani ya uwanja wa Tandale akiwa amesimama upande wa mashabiki wa Tandale karibu kabisa ya uwanja huku hatua chache mbele yake alionekana shabiki yule mkereketwa akiwa amenyanyua bango na hapo ndipo macho yake yalipowashuhudia wachezaji wa Tandale wakiingia uwanjani na mboni zake ziliganda muda wote kwa yule rasta mwanaume wa ndoto zake japo awali macho ya yule rasta pindi alipogeuka hayakushughuliaka sana na yeye hata aliponyoosha mikono na kutabasamu lakini mara yule rasta aligeuka tena na kukutanisha macho kwa mshtuko wakabaki wanatazamana huku kila mmoja akiwa haamini anachokiona,



ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 29




("ASU!! ASUNTAA!!!")
Alijiitia Dullah katika mawazo yake kabla ya Roja kurudi na kumshika mkono waelekee katikati ya Dimba kwaajili ya kukianza kipute kwani alisimama kwa zaidi ya dakika moja akiwa kapigwa na bumbuwazi Dullah akiutazama ule upande ambapo mashabiki wa Tandale walizidi kumshangilia na kumuimbia asiondoke wakiamini kuwa maneno ya bango alilobeba Chidy Ng'ole ndio yaliyomzubaisha Dullah na kubaki anayatazama na kuwatazama mashabiki wa Tandale huku moyo ukimuuma kwa kuondoka kwake.

Lakini ukweli haikuwa hivyo kabisa. Macho ya Dullah yaligongana na macho ya kidonda cha moyo wake nae si mwengine ni Asunta mtoto wa Pastor.
"D, man nini tena?"
alihoji Roja huku akimvuta Dullah baada ya kuona kawa king'ang'anizi akienda huku amegeuka kulekule.
"Asu Roja, Asu Roja, Asu wangu yule pale Roja"
maneno yaliyosikika kwa sauti ya chini iliyojaa taharuki toka kwa Dullah yalimfanya Roja ageuke na kuangalia upande ule wa uwanja ambapo nae alimshuhudia binti mmoja mrembo sana akiwa ametabasamu anawatazama huku uso wake ukitililikwa na machozi ya furaha.
"Yaaah, inabidi umuoneshe na Asu burudani"
aliongea Roja na kumpiga piga D mgongoni mara baada na yeye kuhakikisha na kumuona Asu pale nje ya uwanja akiwa analia kwa furaha na kuamini kuwa lazima yule ndie Asunta bint anayeziendeesha akili za Dullah kama gari bovu.

Ilikuwa tofauti kabisa na matokeo ya maneno ya Roja kwa Dullah mara baada ya kipute kuanza ambapo D kila alivyogusa mpira aliukokotea upande ule alipokuwa kasimama Asu akihisi asije kuondoka pale bila kumuona na hali hiyo ilipelekea Dullah kucheza ovyo kupita maelezo na mara zote hakuwa makini kuangalia mpira bali alikuwa makini kumuangalia Asu pale nje hadi wachezaji na mashabiki wa timu zote walimshangaa.
"Rasta vipi leo?"
alishangaa hadi Chidy Ng'ole pale nje na kujikuta anashusha bango alilolishika muda mwingi baada ya kuona Dullah akizingua na kucheza ovyo kupita maelezo.
Kwa upande wa Dullah alifanya yote yale kwa makusudi wamtoe aende kukutana na Asu hata muda uleule kwa jinsi alivyompenda alijikuta anajiamini kupitiliza.
("Asu wangu, siamini kama leo uko hapa.!!")
aliwaza Dullah huku akisukuma gozi mpaka akalitoa nje pasi na kuangalia uelekeo aliokuwa anakimbia na kitu hiko kilimkera zaidi kocha wa Tandale aliyeamua kumtoa muda uleule jambo lililomfurahisha Dullah na kumsikitisha mno Roja.
("D rasta kadata na mtoto wa Pastor mpaka kapitiliza Daah!!")
alisema na moyo wake Roja kipindi akimuangalia best ake Dulla aliyekuwa anatoka nje ya uwanja baada ya kufanyiwa mabadiliko ndani ya kipindi kile kile cha kwanza.

* * * * * *
NAIROBI - KENYA
__________________

Walikatisha maongezi na maswala ya kumpigia Pastor George mara baada ya gari kufika pale hospitalini na kushuka harakaharaka kuelekea mapokezi na baada ya maelekezo machache na kutokana na umaarufu wa baba Askofu walipita moja kwa moja hadi kwa mganga mkuu wa ile hospitali.
"Karibu baba Askofu, tulisikia umesafiri."
"Ndio Dokta nimerudi muda si mrefu uuph.. vipi ni kweli yule mwanangu kalazwa katika hospitali hii?"
"Aah! ina maana kumbe bint ako hajakwambia?.. ni kweli kabisa tulimpokea tangia jana usiku mwanao yule wa kiume akiwa ameletwa hapa na bint ako wa kike aliyejitambulisha kwa jina la Asunta"
"ASUNTA??!"
Alitaharuki Askofu na kushangaa kuona kumbe ni kweli Asunta alikuwa anajua kila kitu kuhusu Fredy..! na yeye ndie aliyemfikisha hospitali..?! hapo alishindwa kuelewa Askofu hata mkewe nae alishindwa cha kuongea zaidi ya kutaka kujua maendeleo ya mtoto wao Fredy.
"Ndio hivyo baba Askofu mbona mmestuka sana au sio mwanenu huyo bint kafanya udanganyifu hapa maana mimi ndie niliyebeba dhamana ya mwanao Fredy kutibiwa hapa bila hata maelezo yakinifu toka kwa polisi kwani tumempokea akiwa ana jeraha kichwani"
maneno ya yule Dokta ndio kwanza yalizidi kuuchoma moyo wa Askofu na mkewe na kuzidi kuchanganyikiwa kwa habari zile.
"Eeh! sasa Dokta hebu njoo kwa huku mara moja"
alimsogeza pembeni baba Askofu yule Daktari na kuendelea kuongea nae kwa kina huku akitaka ajue ukweli wa hali ya mtoto wao Fredy na sababu ya hilo jeraha wanalosema amekutwa nalo.
"Ukweli mzee wangu Fredy hali yake bado haijakaa vizuri kabisa lakini hajambo.. Na tatizo lililomletea jeraha inaonesha kuwa alianguka vibaya na kupigiza kichwa chake sehemu moja iliyokuwa ngumu sana na kumsababishia mstuko wa mishipa ya fahamu iliyoenda kwenye ubongo na kumsababishia tatizo la mstuko wa Ubongo ambapo kitaalamu tunaita Brain Shock."
maneno ya yule Dokta yalimfanya Askofu azidi kukosa nguvu japo alimvutia Dokta pembeni ili mkewe asisikie maelezo ya kina kwa kuhofia angechanganyikiwa zaidi.
"Mama ingia huko nesi akusafishe vizuri inaonekana una jeraha mdomoni"
aliongea yule Dokta baada ya kutoka chemba na Askofu na kumuona vizuri mama Askofu akiwa na anavujwa damu maeneo ya mdomoni.
"Jamaani mwangu Fredy, ee baba Mungu mponye mwanangu babaa"
alianza kulia na kuomboleza pale pale kwa daktari mama Askofu baada ya kupata uthibitisho juu ya mtoto wao kuwepo pale na kilichomstua na kumuuma zaidi mama Askofu mpaka aonekane kama aliyechanganyikiwa, ni baada ya kupata ripoti kuwa Fredy hayupo kwenye wodi za kawaida bali yupo kwenye wodi maalu za wagonjwa walio serious zaidi ama kitaalamu waliziita ICU.

Waliongozana na mganga mkuu kwenda kuhakikisha kama kweli ni mtoto wao Fredy kutokana na maelezo kuzidi kuwachanganya na muda mwengine kutoamoni kabisa hasa mara baada ya kuambiwa kilichomsababishia avuje damu nyingi maeneo ya kichwani ni pombe kali aliyokunywa ambapo alikutwa mwilini na alcohol nyingi jambo ambalo si mama Askofu tu bali hata Askofu mwenyewe alilipinga katakata kuwa mtoto wao hajawahi kuwa mnyaji pombe acha ya ulevi tu bali hata hiyo harufu ya pombe hakuwa na matamanio nayo.. sasa iweje leo waseme kuwa alikutwa na alcohol nyingi mwilini mwake?
Swali hili liliwaumiza sana hasa pale walipokuwa wanamuangalia mtoto wao kipenzi na wapekee Fredy akiwa amelala kwenye mashine iliyokuwa inamsaidia kupumua huku akiwa kabandikwa vipira frani mwilini vilivyokuwa vimeelekea kwenye computer maalum iliyokuwa pembeni ya kitanda ikisoma na kwenda sawa na mapigo ya moyo ya mgonjwa.
"Asu anajua kila kitu mume wangu wapigie sasa hivi wamkamate huko alipokimbilia kwao.. si umeona uongo wa wazi wazi huu"
aliongea kwa uchungu mama Askofu lakini kwa sauti ya chini sana mara baada ya kulidhiswa kwa kumuona mtoto wao pale wodini wakiwa nje ya kioo maalumu kilichokuwa kinaonesha pande zote za wodi ile kiufasaha kabisa.

Hakuwa na jinsi Askofu akiwa nusu kuchanganyikiwa alitoka na kuzunguka nje ya jengo akimuacha mkewe ambae aliishiwa nguvu pindi walipotoka kule i.c.u na kuingizwa kwney chumba cha kupumzika.
Alichukua simu na kuamua kumpigia Pastor George na kumuelezea hali halisi ilivyokuwa hadi kuondoka kwa Asunta.
[["Haiwezekani Askofu baba.!! mbona Asu hakutupa taarifa yoyote, hata hiyo kwamba anakuja na hadi sasa hajafika huku?!!"]]
ilisikika sauti ya Pastor George kupitia simu ya Askofu pindi alipokuwa anazungumza nae.
["Nina mashaka kabisa George bint ako amehusika kiasi kikubwa kwa hili lililomkuta kijana wangu.. nami sitaki mambo haya yafike mbali kutokana na heshima kubwa iliyopo baina yetu.. Nakuomba fanya jitihada za kumdhibiti Asu nina hakika yupo huko ila tunamuhitaji kwa msaada na maelezo kwa hiki kilichotokea tu si vinginevyo najua bwana akitwaa ni mapenzi yake lakini namuombea mwanangu Fredy kikombe hiki cha umauti kimuepuke."]]
aliongea kwa simanzi Askofu na kurudi tena wodini alipoingizwa mkewe ambapo alimkuta ametengamaa na kuwa sawa japo huzuni kubwa ilitanda kwenye nyuso zao wote.

* * * *

Siku zilienda na hatimae zilikatika siku tatu huku hali ya Fredy ikiwa bado vilevile akisaidiwa kupumua kwa mashine na kula kwa mipila vilevile tetesi za kupatikana Asunta zikizidi kugonga mwamba.

Pastor George kiubinadamu na heshima kubwa alifunga safari hadi Kenya na kuishuhudia mwenyewe hali aliyokuwa nayo Fredy huku wakishindwa kuelewa wapi alipokimbia Asunta.
Jitihada zilifanywa za kumtafuta Asu ambae sasa alianza kuzitia huzuni maradufu familia zake kikeni na kiumeni ambapo walieka kikao cha pamoja na waliahidiana endapo itapita wiki hawajamuona basi itawalazimu watoe taarifa polisi kwa msaada zaidi jambo ambalo Pastor George awali alilikataa lakini alipoona sasa mwanae amepotea kweli alianza kulikubali jambo hilo.

Lakini ikiwa zimepita siku tano ndipo siku moja majira ya jioni vijana wawili waliopewa kazi ya kumtafuta Asu maeneo ya Tandale ambayo Pastor machale yalimcheza isije kuwa mwanae kakimbilia huko kwenda kumtafuta manywele kama alivyopenda kuita mwenyewe, ndipo wale vijana waliweza kumuona Asunta akielekea na yeye kwenye mechi ambayo ilikuwa inachezwa siku hiyo pale Tandale akiwa hana lile wala hili.
"Pius si Asu yule?"
"Haswaa, ni yeye sasa inatubidi tuwe makini asituone hasa wewe mliokuwa mnasali kanisa moja, fanya mpango wa kumtumia ujumbe mzee Pastor mwenyewe tudake mapesa baab"
walizungumza wale vijana na kujibanza banza migongoni mwa watu ili wasionwe na Asu mpaka muda ule ambao Asu anaonana na Dullah pale uwanjani akiduwaa na wao walikuwa wanamchukua picha za kimya kimya na kuzituma kwa Pastor George muda ule wakisubiri maelekezo hatua gani wachukue.
)("Subirini atapoondoka na huyo manywele mumvizie mumkamate na kumshikisha adabu huyo shetani Manywele na Asu mwanangu mniletee nyumbani")(
Ndivyo ujumbe mfupi wa maneno ulivyosomeka baada ya kutumwa kwenye simu ya wale vijana kutoka kwa Pator George pindi walipomjulisha uwepo wa Asunta pale uwanjani.

Na kweli mara baada ya Dullah kutolewa pale uwanjani kwa mabadiliko alielekea kwenye benchi kisha akaomba ruhusa kwa kocha kuwa kuna mtu muhimu anataka akaongee nae,
"Bwanaa eeh! we hata kama ukitaka kwenda nyumbani Nenda tu Kocha wako yupo Kenya huko"
Alijibu kwa sauti ya ukali kocha baada ya kuchukizwa na alichotoka kukifanya Dullah na kumuharibia mood nzima ya mchezo ambao waliamini wangepata ushindi mnono pia Dullah angeonesha kitu special kwa mashabiki wa Tandale kwa nia ya kuwaaga sambamba na na mashabiki wa Tusker ya Kenya kwa nia ya kuwaonesha makali yake.
"Duh!"
aliguna Dullah na kuanza kuondoka eneo lile la benchi na kila mtu pale uwanjani hususani mashabiki asilimia kubwa macho yao waliyapepesa kwa Dullah mara kwa mara hadi pale alipotoka na kuelekea eneo lile alipokuwa yule shabiki mkereketwa ambae alikuwa kachuchumaa huku bango lake amelilaza chini na kulikanyaga kwa miguu.
Dullah alipozidi kusogelea pale huku akiwa katabasam Chidy alijua anafatwa yeye na hivyo alinyanyuka nae kuachia tabasam kwa ajili ya kumkumbatia rasta wao aliyemuhusudu vilivyo akiamini huenda maneno yake ya kwenye bango yameshashawishi akili za Dullah na kubadilisha maamuzi ya kuondoka.
Lakini ilikuwa tofauti kabisa na mawazo ya Chidy Ng'ole na kubaki ametanua makwapa baada ya kuona D ameanza kunyanyua na yeye makwapa kwa nia ya kumkumbatia lakini alimpita pakavu na hata Chidy hakuamini alipogeuka pamoja na macho ya mashabiki zaidi ya mia tano pale uwanjani wote walishangaa kumuona Dullah akienda moja kwa moja na kukumbatiana na bint ambae wengi hawakumfahamu.
"OOYOOOOOOOO"
Chidy Ng'ole alianzisha ukelele ulioungwa mkono na watu kibao huku wengi wakiwa katika hali ya sintofahamu juu ya kile wakionacho.

("Oooh! camoon Dullah unaharibu, daah!!")
alijisemea moyoni Roja mara baada ya mlipuko wa kelele kuwastua hata wao waliokuwa wanapepeta kipute muda ule dimbani na alipotazama na kumshuhudia Dullah akifanya yake hadhalani moyo ulimlipuka na kuona rafiki yake anajiharibia kwa kuwaonesha watu kile kilichokuwa kinamzubaisha hadi akacheza vibaya muda mfupi.

"SIAMINI ASU NI WEWE?!!"
"Ni MiMi D AMINI"
Walikumbatiana kwa nguvu huku kila mmoja akitokwa machozi na wale waliokuwa na Smartphone zao walianza kuwapiga picha hata benchi zima la ufundi la Tandale walisimama wote wakiwa wamejishika kiuno wakishangaa kitendo ambacho walikiona ni cha aibu alichokuwa anakifanya mchezaji wao kwa kuboronga na kuzembea uwanjani kushangaa nje kumbe alikuwa anamshangaa mtoto wa kike!?


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 30





* * * * * *
NAIROBI - KENYA
__________________

Baada ya maombezi mengi kufanywa katika baadhi ya makanisa hususani Kanisa kuu la Anglikana Nairobi lililokuwa chini ya usimamizi wa Askofu Mbukinyo ilifanyika sala ya mkesha kwa siku tatu lakini haikufanya kurejesha hali ya Fredy kuwa ya kulidhisha kule hospitali na ndipo hapo Askofu Mbukinyo lilipoanza kumjia wazo jipya la kumuhamishia mwanae nje ya nchi kwa matibabu ya kina baada ya kuwasiliana na viongozi wa kule katika Jiji la London ambao walimuahidi kwa tatizo la mwanae wako tayari kutuma ndege maalum itayom beba hadi London na atatibiwa na Daktari bingwa wa maswala ya ubongo wa kule London.
[["Ondoa shaka Askofu, huko Afrika unaweza kumsababishia mtoto kupoteza maisha wakati kuna wataalam wanaweza saidia huku"]]
Ilikuwa ni sauti ya Kiongozi mkuu wa Kanisa la Anglikana London ambae alikuwa ni rafiki mkubwa wa Askofu pindi alipokuwa anazungumza nae kwa njia ya simu na kumuelezea tatizo lililomsibu mwanae kipenzi Fredy.

Na hivyo ndio ilivyokuwa siku chache baadae ndege maalum ya kukodi ya kubebea wagonjwa ilitumwa nchini Kenya kutokea London na hapo taratibu makini za kumuamisha Fredy zilifanyika zikiongozwa na Askofu mwenyewe aliyekuwa bega kwa bega na mkewe ambae muda mwingi alikuwa ni mtu wa kulialia tu akiwa haamini kile kilichokuwa kinaendelea tangia apate habari za matatizo yaliyomkumbuka mwanae siku kadhaa zilizopita.
"Baba Fredy, leo tunaenda na mwanetu akiwa hajitambui London, naomba Mungu akatende muujiza huko apone. Lakini nitaporudi nitahakikisha namfunza adabu huyo Asunta kama kwao walishindwa kumfunza adabu na wewe kukataa tuwatumie polisi kumsaka kwaajili ya urafiki wenu na George lakini kwangu, hapana... Mwanangu ananiuma sana aaa.."
aliongea kwa uchungu mama Fredy kipindi wakiwa ndani ya ndege kwaajili ya safari ya London Uingeleza.

* * * * *
- TANZANIA -
____________

Baada ya kustuka na kulisikia zogo lililoibuka muda mfupi pindi alipojikuta anamkumbatia Asu hadhalani Dullah aliamua kujichanganya kabisa kwenye kundi la watu wengi huku akiwa kamshika mkono Asu na kuwafanya watu wazidi kushangilia na wengine wakitukana.
Sijui kama ni midadi ya wivu, chuki ama ni mapenzi kwa Dullah yaliyowafanya watu washangilie na wengine wazomee pindi Dullah alipokuwa anajichanganya nao na kumzonga huku wengine wakimshika rasta hadi alipofanikiwa kuchomokea nyuma ya ukuta wa shule ambao uliwatenganisha na ule uwanja na kama bahati ilitokea bajaji aliyoisimamisha na kuingia ndani yake huku miluzi na kelele za watu zikiwasindikiza nyuma.

"Tunaomba utufukuzie ile bajaji iliyoondoka saivi aliyopanda Rasta na yule demu ila chunga usiipite wala isikuache."
"Poa lakini kwema jamani."
"Kwema tu, sisi ni waandishi wa habari"
"Haa! wazee wa kimuli muli hamna noma mmeiwahi mbona"
alijibu kijana dereva bajaji mara baada ya kufika vijana wawili na kumuamuru awafatilie kina Dullah ambao waliondoka dakika zile kwa bajaji.

Na kweli baada ya mwendo mfupi waliweza kuwa nyuma ya bajaji iliyowabeba kina Dullah na safari iliwapeleka hadi mitaa ya Sinza vatican alipokuwa anaishi Dullah na mara baada ya kushuka nao wale vijana walishuka na kumlipa dereva bajaji ndipo walisubiri pindi Dullah akifungua geti dogo na kujitoma ndani yake na papo hapo nao walisogea kwa mwendo wa haraka na kutokana na usiku kukaribia walijiamini sana wale vijana na hapo mmoja akachomoa kisu huku yule mwengine alisimama getini muda uleule na kugonga.
Hamadi!! Dullah alipofungua tu alikutana na teke lililomrudisha ndani kisha yule mwengine aliingia na kufunga geti kipindi mwenzake alipomrukia tena Dullah kwa lengo la kumchana chana visu.
"Aaaaaaaghh.......!!"
alitaka kupiga yowe Asunta lakini aliwahiwa na yule jamaa mwengine ambae alistajabu mno kuuona uso wake kwani alimjua vizuri na alimkumbuka ni mtu waliyekuwa wanasali kanisa moja.
Lakini kipindi purukushani zile zinaendelea mara kuna mtu mwengine aliingia mule ndani ya fensi ya nyumba ile kwa style ya kuruka ukuta kwa sambasoti baada ya kusikia vishindo vya purukushani vikiendelea.
"Haya tulieni hivyo hivyo acheni fujo kabla sijayavynja makoo yenu."
aliongea kwa sauti ya kujiamini mno yule mtu aliyeingia kwa sambasoti pale na kuwastua wale vijana sambamba na kina Dullah na kufanya wageuke ambapo Kwa upande wa Dullah na Asunta wote walimfahamu vizuri yule mtu na mioyo yao ilipata nguvu na amani kwa ujio wake ambao hawakuutarajia muda ule pale, na hakuwa mwengine yule mtu bali ni Mwl, Jack.

Kilichotokea pale ni Jack kuwafanya Kivan Damme (Kuwashambulia kwa mateke hatari) wale jamaa ambao mwishoe waliamua kutoka mkuku na kupalamia geti huku damu zikiwavuja.
"Wapumbavu tu wale, vipi wapendanao mpo salama?"
aliuliza mwl Jack mara baada ya wale vijana kukimbia na kuwaacha waende pasi na kuwafukuza.
Swali la mwalimu Jack liliwafanya Dullah na Asu walijibu kwa kichwa pasi na kuongeza neno lolote ndipo mwl Jack alipoendelea kuwauliza maswali hususani kwa Asunta ambae hakujua majibu yake.
"Asu, kwanini unadhani wale vijana wamewavamia na kumshambulia Dullah"
"Mh! hapana Master sijui"
"Dullah je?"
"Mi ndio kabisaaa"
"Sasa sikilizeni niwaambie jambo, nina hakika wale watu wametumwa na babaako Asunta,nawe Dullah tafuta njia m badala ya kutengeneza amani na Pastor George ikiwezekana kubali kubadili dini, nyoa rasta umuoe Asu hilo ndio suruhisho la sivyo Mh...."
aliongea maneno haya Jack ambayo yalimchoma Dullah hasa aliposikia kipengele cha kubadili dini.
"Ukweli kaka kama ni kunyoa rasta tu, haina shida niko tayari hata sasa hivi ili nimuoe Asu kwani najua nywele zitaota na nitafuga tena, lakini swala la kubadili Dini!! hapo ndio kwenye tatizo kubwa"
alijibu Dullah kwa msisitizo
"Sasa rastaaa, hebu nisikilize. Jifanye mjinga kwa mara moja tu.. Kubali matakwa ya mzee ili upate tunda hili na litapokuwa ndani mwako si mnapanga tu au unarudi kwenye dini yako ya zamani!! Mi najua fika hakuna tatizo kubwa linalokupa kikwazo wewe zaidi ya dini. sio pesa wala nywele."
maneno ya Jack safari hii yalipenya vizuri kwenye milango ya fahamu ya Asunta ambae muda wote alikuwa anashangaa mwl Jack kafahamiana vipi na Dullah hadi kuelewa kuwa ni mpenzi wake na kuwajuza mambo yote yale ambao yalijaa ukweli ndani yake hasa alipokumbuka toka siku ya kwanza analitaja jina la Dullah lilimchefua babaake kabla hata hajamuona Dullah mwenyewe na kuamini maneno ya Jack asilimia zote kuwa dini ndio kikwazo kikubwa baina yake na Dullah kwa wazazi wake.
"Lakini baby si ukubali tu anachosema Master Jack"
aliongea Asu kumuelekeza Dullah ambae sagari hii alikuwa anajifuta futa vumbi lililotokana na kuanguka kwake pindi alipovamiwa na yule kijana mwenye kisu na kumpiga teke.
"Asu naomba usinitibue kuhusu hukotafadhali"
Jibu la Dullah safari hii lilitosha kumpa tafsiri mwl Jack aliyeamua kuwaaga baada ya kugundua kuwa msimamo wa Dullah ndio ulikuwa ule hivyo ni vigumu sana kum badilisha kama imefikia anam badilikia hata kidonda cha moyo wake Asu.

Baada ya mwl Jack kuondoka muda ule ule geti lilifunguliwa na kuingia Roja akiwa na mpira mkononi.
"Vipi jamani mlidondoka na bodaboda?"
lilikuwa ni swali kabla ya salamu toka kwa Roja mara baada ya kuwashuhudia wapendanao wakiwa wamechafuka vilivyo vumbi hadi kichwani bila kujua kitu gani kimewapata.
"hamna Roja, vipi matokeo"
"Safi tu, leo nilijikuta navaa viatu vyako"
"Kivipi"
"Nimepiga hattrick kimaajabu kweli dakika za mwishoni na hadi nimechelewa hivi nilikuwa na mabishano juu ya huu mpira na kocha aliyetaka ubaki kwenye kabati la mipira yetu lakini nikaona haiwezekani swahiba wangu aondoke bila zawadi.. Na hii ndio zawadi yangu kwako siku zote utanikumbuka kupitia mpira huu na utaikumbuka mechi ya mwisho"
Aliongea Roja huku macho yake muda mwingi yakiwa kwa Asunta na ndipo Dullah alipowaunganisha kwa kuwatambulisha.
"Asu, huyu ni Roja rafiki angu mkubwa sana Roja huyu ni Asu malkia wa moyo wayo wangu"
Baada ya Roja na Asu kutambulishwa mbele ya Dullah, ndipo hapo Roja aliamua kuondoka ili awape muda wa mazungumzo wapendanao wale ambao waliacha kiroja uwanjani kwa kushindwa kuficha hisia zao mara baada ya kupotezana kwa muda mrefu.

Asu hakuwa na jipya zaidi alimuhadithia kila kitu kilichojiri nchini Kenya alipokuwa na kumstua mno Dullah.
"Ina maana tuseme ndio umerudi rasmi hutokwenda tena Kenya?"
"Ndio hivyo baby wangu, hapa nilipo nimechanganyikiwa kwani ndo nishaonekana sasa najua natafutwa sana na sikupanga nikae hapa Dar ila ni kwaajili ya kukutafuta wewe, naomba tuondoke kabisa kwenye hili jiji"
Maneno ya Asu yalizidi kumvuruga akili Dullah hasa alipokumbuka kuwa yeye tayari ni mchezaji mtarajiwa wa Tusker ya Kenya na alifanya yote yale kwa moyo na jitihada kubwa ili akawe jirani na ,tu anayempenda ambae sasa amerudi na hatokuwepo huko aliposajiliwa, yaani ni sawasawa Dullah ametwanga maji kwenye kinu.
"Daaah!! Asu ujue aah! hadi nachanganyikiwa"
"Kwanini D"
"Kenya"
"Kenya, kivipi?"
"Mi nishakuwa mchezaji wa timu ya kule na kesho sitolala hapa, natakiwa nikaungane hotelini na scouts walionifata kwaajili ya safari kesho kutwa."
"Whaaat!!?"
Alihamaki Asu.

* * * *
LONDON - UINGEREZA
______________________

Ndege maalum ya wagonjwa ya kukodi iliyom beba Fredy pamoja na wazazi wake iliwasili katika uwanja wa London na kupokewa na Ambulance maalum iliyokuwa inawasubiri na moja kwa moja safari ya kwenda katika hospital ambayo kuna Daktari bingwa wa maswala yale kama ambavyo babaake Fredy Askofu Mbukinyo alivyopashwa habari zile na rafikiake kiongozi wa Kanisa la Anglikana London.

Jitihada za kuokoa maisha ya Fredy zilianza kufanyika mara moja pindi tu alipofikishwa kwenye ile hospitali na kuingizwa kwenye wodi maalum ambayo aliweza kuhudumiwa na kuchunguzwa yakinifu na yule Daktari bingwa akisaidiana na computa mbalimbali maalum zilizokuwa wosini mule.
Uchunguzi ulifanyika wa zaidi ya masaa matano kabla yule Dokta hajatoka na kukutana na Askofu kumueleza juu ya nini wamegundua kuhusu hali ya mtoto wake hadi kushindwa kuamka kwa wiki nzima sasa.

"Inaonekana amepata brain Shock wakati akili zake hazipo sawa, yaani mfano wa mtu aliyekunywa pombe nyingi akalewa then akapigwa na kitu kizito sehemu hizi (anaonesha) za kichwa, sasa sijajua kwa mwanao ilikuaje?"
aliuliza swali yule daktari lililomfanya Askof anyamaze kwanza na kufikiria cha kumjibu kwani ukweli majibu ya tafiti alizofanya yule Daktari kwa namna moja yanafanana na ripoti ya daktari wa Dar Tanzania kuwa mtoto wake alikutwa na alcohol nyingi mwilini iliyosababishwa asichomwe hata sindano pindi walipompokea.
Ila angewezaje kukubali kuwa mawanawe alikutwa na alcohol mwilini nae kutamka hivyo mbele za watu?
Swala hilo alilipinga mdomoni Askofu japo moyoni alivuta hisia na kukubali kuwa mwanae kweli alikutwa na alcohol mwilini lakini swali ni kwamba lini alianza Fredy kunywa pombe na kwa sababu zipi za msingi wakati wamemlea katika maadili mazuri hadi anakuwa mtu mzima na ofisi yake?
("Sikutegemea kama Asunta anaweza kuja kumtia mwanangu katika ushetani, kumbe yule bint upole wako ilikuwa silaha ya kutumbaza tu! hapana siamini... Yaani Asunta ulevi kwake binafsi kaona hautoshi mpaka kamuingiza na mwanangu!!? Pastor George rafiki angu sana lakini kama mwanangu ameponzwa na bint ake basi ana wajibu wa kulipa hili .. Eeh Mungu mbona yananijia mawazo haya tena!!? Bwana kaa nami")
aliwaza moyoni Askofu pindi alipokuwa anafikiria jibu rasmi la kumwambia yule mtaalam.
"Alianguka tu Dokta, lakini kuhusu alcohol mwanangu hana kabisa mazoea na hivyo vitu, amekua katika mazingira ya kiroho"
alijibu Askofu
"Basi ondoa shaka, tutafanya kila liwezekanalo na atarudi katika uzima tu"
aliogea maneno yaliyowatia nguvu wazazi wa Fredy yule Dokta na kuelekea tena kule wodini alipo Fredy.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 31


* * * *
TANZANIA
_____________

Kauli ya Dullah kuwa inatakiwa kesho yake asubuhi kujiandaa na safari ya kutimkia Kenya ilimuuma sana Asu wala hakuipenda na kuanza kumsihi Dullah asikubali kwenda huko zaidi akubali waende wote popote lakini si Kenya.
"D baby wangu nakuomba sana, hebu nitazame nimetoroka kule na sikuja Tanzania kwa sababu ya wazazi wangu bali ni kwa sababu yako.
Fikiria jinsi gani nakupenda Dullah... Naomba usiniache katika wakati mgumu kama huu nilio nao sasa please baby naomba tutoroke tu achana na habari ya Kenya tafadhali"
Maneno ya Asu yalipenya vizuri kifuani mwa Dullah na kubeep katika mizizi ya moyo wake na kuanza kudunda kwa nguvu huku akitafakari jinsi gani atavunja agano na Tusker ili abaki Tanzania na Asu?

Alitamani kumfata Roja kumwambia suala lile lakini alipofikiria kwa kina aliona lazima majibu ya Roja yatapishana na mawazo yao na Asunta na atataka kulazimisha tofauti na matakwa yao hivyo akaona haina umuhimu wa kumwambia Roja suala lile.

"Asu, kama wewe Unanipenda tu, basi mwenzio Nimechanganyikiwa kabisa juu yako, na kwa hiyo kesi uliyonisimulia harafu ukichangia na hawa watu waliotuvamia, haina budi kuondoka hapa Asu usiku huu huu hapafai mambo yanaweza kuharibika"
aliongea Dullah maneno ambayo yaliungwa mkono na Asunta na hapo ndipo safari yao ikaanza kutokea pale Sinza huku kwa upande wa Dullah alibeba nguo chache ikiwemo jezi na ile vest ya Road to Kenya pia alichukua na mpira alioletewa na Roja kama zawadi na kisha kuondoka na Asunta kinyemera bila kumsubiri wala kumuaga Roja.

Safari yao iliwakomea kwenye guest moja iliyokuwa jilani na stendi kuu ya mabasi ubungo.
"Asu, mi nataka kesho tuelekee Nyumbani moja kwa moja Tanga kule kuna wataalam sana wa kufunga mambo haya yanayokuandama."
"Mh! D unamaanisha Waganga!?"
"Eeh! We unadhanije, kule kuna waganga wazuri ambao watatusaidia"
"Hapana D mi sikubali kabisa maswala ya waganga tena kama kwenu ndio hivyo naogopa hata kwenda"
alianza kutia shaka Asu na kumfanya D awe mpole na kumsihi aondoe hofu kwa kile anachokifikiria kuhusu kwao.
"Asu, kwetu sisi ni mafukara sana tu ila tuna upendo wa dhati wala simaanishi tunaendekeza sana waganga ila tunaamini waganga wapo na uganga upo"
"Sawa D lakini mimi sina imani hiyo"
"Kwa hiyo huamini kama kuna waganga?"
"Yah! siamini mi najua ni matapeli tu. Mganga wa kweli ni Yesu pekee"
"haha Asu bwana, kwa hiyo hata wachawi na wanga huamini kama wapo?"
"Mi ninachojua hao ni mapepo wachafu tu najilinda mbele ya bwana."
"Basi baby ila naomba nikuulize kitu"
"Kipi tena D"
"Unanipenda kwa dhati kabisa?"
"Kabisa Dullah naomba usitie shaka, hebu fikiri mwenyewe wapi nimetoka hadi nikaja kwako"
"Sawa Asu ila naomba tutavyofika kijijini upendo huu unaonionesha uwaoneshe na ndugu zangu hususan mamaangu Kipenzi"
"Usijali baby I love you so much"
Aliongea Asu na kumsogelea Dullah na kum busu,
basi waliendelea na maongezi yale yaliyowapelekea wasahau matatizo yote muda mfupi yaliyo mbele yao na kujikuta wanazama katika ulimwengu mwengine wa kimahaba ndani ya chumba cha ile guest na kwa mara ya pili Dullah aliyafaidi mautamu ya Asunta.

*****

Asubuhi na mapema yaani ile saa kumi na mbili Asu na Dullah tayari walikuwa ndani ya basi la kampuni ya Raha Leo kwaajili ya safari ya Tanga nyumbani kwa kina Dullah huku wote wakiwa katika hali ya kutoroka, kwani Dullah alitoroka kujiunga na club ya Tusker ya Kenya huku Asu nae akiwa katika mlolongo huo kwa kuhofia juu ya kile kilichomtokea Fredy ambae mpaka muda huo hakuwa anajua kama ni mzima au amekufa.
Basi iliondoka Ubungo majira ya saa 12 asubuhi huku wote wawili wakisali wafike salama huko waendako ambapo waliombea asijue mtu yeyote wapi walipo.
Na kwa kuwa safari yao hawakumuaga yeyote kidogo hiyo iliwapa matumaini mioyoni ya kutojulikana wapi wameenda na hata Asu aliona hiyo itakuwa ni njia sahihi ya amani kwake.

Majira ya jioni walifanikiwa kushuka Muheza mjini ambapo walipanda basi iliyowapeleka mpaka katika kijiji alichokuwa anatokea Dullah ambapo ndio ilikuwa kwao kabisa alipokulia
"Mh! baby kumbe ni mbali hivi? Kha!!"
aliongea Asu huku akiwa kajishika kiuno baada ya kuona safari ya kutoka stendi pale waliposhushwa na basi ya kijijini ikizidi kuwa ndefu.
"Hamna baby ni nyumba ilee"
"Ile ya Nyasi?"
"Eeeh mke wangu ila kuna nyumba nyengine tunajenga utaiona tu"
"Mh!!! Makubwa"
alitamka Asu kauli ambayo kidogo ilichoma moyo wa Dullah kwa kuhisi Asu anapaonea kinyaa kwao lakini alishindwa kumwambia chochote Asu kwa kuogopa kumuudhi.

"Idi.. Idi.. kaka Zidane yulee, Idi kaka Zidaneee"
Ilisikika sauti ya kijana mmoja akiwa kavaa sare chakavu za shule mara tu alipomuona Dullah na kuwastua wenzake waliomkimbilia na kumkumbatia pamoja na Asu ambae alijisikia kinyaa kuwashika wale watoto ambao kiukweli walikuwa wachafu na miili yao ilijaa ukurutu huku miguu ikiwa imepasuka magaga.
Lakini tofauti na Dullah ye aliwakumbatia na kufurahi nao huku wakimtukuza jina la Zidane ambalo alitungwa katika mechi za kule kijijini kipindi alipokuwepo kutokana na uwezo wake wa kumiliki mpira na kuwatesa wachezaji wenzake ndani ya Dimba, na ndio sababu na asili ya kutungwa jina la Zidane.

Baada ya mwendo mfupi tokea walipopokelewa na wale watoto ndipo walipofika nyumbani ambapo walimkuta mama akiwa anatwanga mpunga sambamba na mdogo ake wa kike Dullah aliyeitwa Ilham.
"Mama, Kaka Dullah huyoo, kaja na wifiii"
aliacha kutwanga Ilham na kumkumbatia kwa furaha kakaake pamoja na wifi ake ambae bado alikuwa hata hajatambulishwa na ndipo mamaake Dullah nae alipoacha kutwanga na kuwakumbatia watoto wake kwa furaha hasa kutokana na ujio ule wa kustukiza tena alifurahi zaidi kumuona mwanae amkuja na mwanamke ambae wote waliamini amekuja kuwatambulisha rasmi huyo mwanamke aliyekuwa anawaambia anampenda.

* * * *
DSM - TANZANIA
________

["Haiwezekani, Nimesema haiwezekani hata kidogo nyinyi ni wazembe sana tena sijapata hata kuwaota aaaaaaaaghhhhhhh!!! Yaani mna muacha bint angu anapotea hivihivi wanaume wazima.>!? tena mpo wawili!!? Hapaaanaaa Sitaki kuendelea kusikia ujinga huo..! Mbona hamkufa sasa kama aliwazidi? Aaaah mbekesu wene mwavela buruhjuvua kinzezziii Aaaagh!!"]
alionekana Pastor George akibwata kwa njia ya simu asubuhi na mapema mara baada ya kupewa taarifa na vijana aliowapa jukumu la kumfunza adabu Dullah na kumrejesha mwanae Asunta ambae alitoroka nchini Kenya kukimbia kesi juu ya Fredy na kujikuta anazidi kudata na kuongea lugha ambayo haikueleweka pindi alipokuwa anaongea kwa simu na papo hapo aliibamiza simu yenyewe ukutani kwa hasira kali sana.
"Baba Asu, baba Asu mume wangu vipii?"
alisikika mke wa Pastor George akiwa na wasiwasi mkubwa pindi alipokuwa akitokea ndani na kuelekea kwenye korido ya pale ghorofani kwao aliposimama Pastor George akiwa kavimba kwa hasira.
"Vipi mume wangu mbona hivyo?"
"Mama Asu hii sasa Too Much aah"
"Jamani kwani kimetokea nini?!"
aliendelea kuhoji mama Asunta pindi alipomkuta mumewe katika hali ya hasira hata simu aliyokuwa nayo alishaivunja baada ya kuibamiza ukutani kwa hasira zake.
"Si hawa wapuuzi niliowambia wahakikishe wanakuja na Asu hapa!!"
"He ! masikini nini kimempata tena mwanangu?"
"Wamemuacha kaondoka na yule Kichaa manywele Aaaagh!1 Yaani..."
"Basi mume wangu shusha kwanza hasira umuombe vizuri bwana usije kupata dhambi"
"Mama Asu, Sidhani kama kuna dhambi mbele ya Bwana kwa mtu anayepigania mstari mwema kwa mtoto wake, sasa mimi kuanzie leo napigania mstari mwema kwa bint angu Asu kwa udi na uvunba."
Aliongea tena Pastor Gorge na kujiapiza kabisaaaa.

Hasira alizokuwa nazo Pastor George zilivuka kiwango na alishindwa kuzizuia kabisa na kuzidi kutoa viapo vikali mbele ya mkewe ambae aliamua kunyamaza japo nae alikuwa na uchungu na wasiwasi kuhusu mwanae lakini hakufikia kuwa na hasira za namna ile.
"Lazima nimuoneshe huyu manywele popote alipoenda na mwanangu Atajuta kuzaliwa"
alijiapiza Pastor George mbele ya mkewe wakati akiokota line iliyokuwa kwenye simu yake ambayo aliipasua kwa hasira pindi alipokuwa anazungumza na wale vijana na kurudi tena chumbani.

Alifikiria mambo mengi sana Pastor George kuhusu nini cha kumfanya Dullah hadi akae mbali na mwanae pia alifikiria sana na kupata wasi wasi huenda mtoto wa askofu alishambuliwa na huyo huyo Rasta kwaajili ya Asunta, lakini pia aliwaza kawezaje yule manywele kwenda kumshambulia Fredy huko Kenya ilihali ye yupo Tandale?
Moyo ulimuuma na hasira dhidi ya Dullah zilizidi kutawala kifuani mwake.
("Sitoweza kuvumilia mambo haya wala kuyafumbia macho, lazima nimshikishe adabu huyu mbwa anaenipotezea mwanangu... Mungu atanisamehe tu kwa hiki nitachomfanya huyu kijana. Haiwezekani ampe Mimba mwanangu harafu imeshindikana kuadhibiwa na Jack, harafu leo hii anakutwa na mwanangu imeshindikana tena kuadhibiwa na wale vijana. Sasa kadiliki kutokomea kabisaaa na mwanangu asubiri kufunzwa adabu na mimi Mwenyewee... Lazimaa tena lazimaaa nimuendee Nigeria huyu Mbwa")
aliendelea kuongea moyoni mwake Pastor kipindi akitembea kuelekea ndani mwake huku akijiapiza lazima atekeleze analolikusudia juu ya Dullah.


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 32

LONDON - UINGEREZA

Ilikuwa ni siku ya tatu tangia Fredy afikishwe pale kwenye ile hospitali ya Daktari bingwa aliyesifika kwa matatizo ya ubongo lakini bado alikuwa hajapata fahamu yoyote japo jopo la madaktari lilikuwa makini kila saa kujaribu kumtibu ili arejewe na halli ya kawaida lakini bado mambo yalikuwa magumu na pale Londo lakini pia haikuwakatisha tamaa madaktari ya kuendelea kumchunnguza na kumpia Fredy kila mara huku vipimo vikirudi na majibu yale yale.

Upande wa shingo kurudi chini Fredy alikuwa mzima kabisa, kila kitu kilifanya kazi vizuri kama binaadam wengine kuanzia kwenye mapigo ya moyo na kadhalika.
Lakini tatizo linakuja ni kuanzia juu ya shingo kuja kichwani huko ndio balaa lilipo.
Wazazi wake walikesha kanisani siku zote wakitumia muda mchache sana kulala hiyo yote kumuombea yeye tu Mungu amponye katika tatizo lile lililomkumba ghafra na kumlaza bila fahamu kwa zaidi ya wiki.
Hakukuwa na mawasiliano ya karibu na Pasor George kama ilivyokuwa kawaida hapo awali japo kuna muda Pastor alikuwa anatuma msg kutaka kujua hali ya mgonjwa lakini Askofu alikuwa anazifuta tu bila kuzijibu pindi anapozisoma na wala hakumpigia.
Hali hii ndio ilisababisha Pastor nae abaki kimya pasi na kupiga wala kutuma msg tena akiwa anajua kuwa bado mambo magumu na imani imewatoka juu yake hata alipowaambia kuwa Asunta hayupo kwake wala hajui alipo.
Hali hii ya ukimya wa pande mbili marafiki wakubwa ilianza kutengeneza dosari kubwa kwenye mioyo ya waumini na viongozi hawa wawili wa kidini.

* * * * *
MUHEZA - TANZANIA
_____________

Furaha ilitawala kwa mama Dullah hasa mara baada ya kutambulishwa msichana ambae alikuwa anapata hadithi zake na sifa za mara kwa mara kutoka kwa mwanae D pasi na kuwahi kuiona sura ya huyo mkwe mwenyewe.
"Karibu sana mwanangu, karibu sana mimi ndie mamaake Abdallah au Zidane jina wanalomtambua haraka mchumbaako hapa kijijini.. Jisikie amani mama karibu sana"
aliongea kwa furaha mama Dullah na kumshika mikono miwili mkwewe mtarajiwa ambae ni Asunta.
"Karibu wifi jisikie upo nyumbani"
aliongea Ilham dada wa Dullah kwa furaha.
"Asante"
alijibu Asu kwa sauti ya chini huku akionesha kama mtu mwenye mawazo mengi sana na akili zake zilikuwa mbali sana na pale.

Story ziliendelea wakiwa wamekaa kwenye mkeka pale nje ya nyumba yao majira ya saa mbili usiku huku kwa upande wa Asu akiwa katika hali ya unyonge ambao Dullah hakuustukia kutokana na kubezi kimazungumzo na mamaake hususani maisha ya pale kijijini toka ameondoka na kuhusu ujenzi wa nyumba yao na kadhalika bila kusahau utani wa hapa na pale ilimradi kila mmoja moyo wake ulionesha dariri zote za furaha siku hiyo kasoro Asunta pekee ambae muda wote yeye alibaki kimya akiwa ni mnyonge na mwenye mawazo.
"Vipi wifi unaumwa nini!"
aliuliza Ilham lakini Asu alikanusha kwa kuitikia kwa kichwa.
"Ilham bwana, hebu acha kumuuliza uliza maswali mwanangu. Tena kapakue kabisa chakula huo wote ni uchovu wa safari wifi ako amechoka sana, si eti mamaa eeh..?"
aliongea mama Dullah akiwa mwenye furaha na tabasamu akimpamba mkwewe kutokana na vile anavyoonekana mnyonge lakini alipomuuliza kwa mara nyengine Asu aliitikia kwa kukubali kwa mtindo ule ule wa kichwa bila kuongea kitu huku mkono wake mmoja akimpapasa papasa mgongo Dullah ambae alimuangalia Asu na kumuangalia mamaake ambae alikuwa na furaha sana siku hiyo kuliko kawaida.

Chakula kiliandaliwa kwenye sinia na kuekwa mkekani huku macho ya Asu yakishangaa hali ile kupita kawaida.
"He!! Ndio chote, umejaza kwenye sinia moja?"
ilikuwa ni kauli ya Asu iliyomshangaza kila mmoja haswa Ilham kauli ile hakuipenda kabisa lakini aliamua kujichekesha tuu.
"Aaah! jamani wifii!!! nimepakua hivi kwa niaba yako nataka ule wifi angu uone mapishi ya kwetu"
aliongea Ilham na kulipeleka bakuri la maji kwa Asu ambae alichovya kidogo vidole na kumsogezea bakuli Dullah ambae alikataa kunawa kwanza akampelekea mamaake.
"Aaah! nawa tu baba."
"hapana mama nawa wewe."
"Nimekuruhusu mwanangu nawa"
"Hapana mama nawa kwanza"
"Hee! Dullah bwana,! haya nawa sasa"
"hapo sawa sasa "
alijibu Dullah baada ya mabishano ya kutangulia kunawa baina yake na mamaake mpaka aliponawa mamaake ndipo nae alinawa na kumrudishia bakuli Ilham aliyenawa mwisho.

Mtindo ule wa kunawa moja kwa moja kwenye bakuli pasi na chombo chengine cha kutilizia maji kilimtia kinyaa Asu moyoni mwake hususani na alivyokuwa anakitazama kile chakula ndio alichoka kabisa.
("He!! haya makubwa? mboga za majani kwenye wali?!")
alijisemea kimoyo moyo Asu huku akipekusia pembeni mboga ambayo ilikuwa ni majani ya maboga yaliyomenywa kama matembele pamoja na wali jambo ambalo hakulizoea kabisa Asu na aliona kama kituko.
Kila mtu alikula huku akimpiga jicho la pembeni pembeni Asunta hususani Ilham ambae tayari moyo wake ulianza ingia kinyongo na wifi ake pindi tu alipotamka maneno ya awali ambayo yalimaanisha chakula kile kingepakuliwa sahani tofautitofauti jambo ambalo kwao halikuwepo.
Alichota vtonge viwili tu Asu tena bila mboga na kuomba maji ya kunawa hali ile hata mama Dullah ilimtia unyonge moyoni japo hakutaka kuonesha mbele ya wanae.
"Ndio umeshiba wifi?"
aliuliza Ilham na kama kawaida Asu aliitika kwa kichwa na kutoa leso yake kujifuta mikono.
"Hao watu wa mjini Ilham mwanangu, we unafikiri kama wewe unakula hadi unaona uvivu kunyanyuka?"
aliongea mama Dullah na kusababisha Ilham na Dullah waangue kicheko.

Dullah hakuonekana kujali sana wala kubembeleza Asu kuhusu kula, yeye aliamini kinachomsumbua Asu ni ugeni tu lakini baada ya siku chache atakuwa sawa.
Alijua ni mwanamke pekee mpaka muda huo aliyekaa katika mtima wake ataenda nae sawa mpaka atapokaa vizuri kwani alijua mazingira yale ni mageni kwa Asu pengine toka kuzaliwa kwake.
Majira ya saa tatu na nusu usiku waliingia ndani kulala baada ya story za muda mrefu na kibatari kuanza kuisha mafuta pia ukichangia na kusinzia kwa Asu ilibidi waende kulala ambapo kwa mara ya kwanza Asu toka kuzaliwa kwake aliingia kulala kwenye nyumba ndogo ya Nyasi huku ukuta wake mwembamba uliozungukwa na fito nyingi zilizochoka ukiwa na vitundu vidogo vinavyoonesha nje hali iliyozidi mpa mashaka ya usalama wao Asunta na kuanza kujutia kwanini alikubali kwenda kule na Dullah aliwazia ni bora angemshawishi waende sehemu nyengine ambayo wangeinjoy walau kidogo kuliko pale ambapo nyumba zilikuwa mbalimbali sana hakuna umeme na alishindwa kabisa kunywa maji siku hiyo kutokana na rangi ya maji na hali ya mtungi wenyewe aliouona wa maji ulimchefua pia.

("Mungu wangu mbona balaa hili!!?")
alizidi kuumia moyoni Asunta mara baada ya kukitazama kitanda ambacho ndio ilitakiwa walale pale.
Kilikuwa ni kitanda kidogo cha kamba kilichotandikwa mkeka juu yake sambamba na vitenge viwili.
"D baby wangu ina maana ndio tunalala hapa?"
aliuliza Asunta kwa sauti ya kustaajabu pindi walipokuwa mule ndani
"Eeeh! baby wangu hiki ndio kitanda chetu kizuri eeh.. Njoo basi tulale sweety"
alimvuta mkono Asu na kukaa nae kitandani kimahaba lakini kwa upande wa Asu alitokea kupachukia ghafra nyumbani kwa kina Dullah.

Usiku huo ulikuwa ni wa furaha sana kwa Dullah mara baada ya kurudi kijijini kwao tena akiwa na mtu ampendae na alisahau kabisa sababu za kuondoka pale kijijini haikuwa kwenda kutafuta mke mjini bali ni kwenda kutafuta kazi na maisha bora ili apate kuwatunza ndugu zake na kuisaidia familia yake na yeye mwenyewe hapo baadae pindi atapooa.
Lakini penzi la ajabu lililoibuka moyoni mwake kwa mtoto yule wa Mchungaji lilitosha kubadili adhma na nia yote ya Dullah na kujikuta anapoteza muelekeo na kukataa hadi nafasi adhimu alizokuwa anazipata kutokana na kipaji chake cha kusakata kabumbu.
Hakujali vyote lakini yeye alijali kwanza kumpata mtoto wa Pastor ndipo baadae aanze kutafuta pesa hivyo hakuwa na hata chembe ya majuto kwa kile alichokifanya na usiku ule ulikuwa burudani kabisa katika kuta za moyo wake.

Tofauti na upande wa Asunta yeye hakuwa na furaha hata kidogo moyoni wala hakupafurahia mahala pale kwa kina Dullah na si kwamba hampendi Dullah, la hasha ukweli Asunta alimpenda sana Dullah tena sana lakini mazingira ya pale hayakumfurahisha kabisa na alishindwa kujizuia juu ya hilo na kujikuta anaonesha dalili zile waziwazi.
Alipenda kuishi na Dullah tu kwa kuwa ndie alikuwa anampenda, moyo wake haukuvutiwa na muonekano wa Ilham mdogo ake Dullah wala mamaake Dullah kila alivyomtazama hakumfurahisha moyoni japo alijua ndie mama mzaa Dullah wake kidonda cha mtima wake.
Alitamani Asu kuche haraka ili waondoke pindi alipokuwa analala kifuani mwa Dullah aliyelalal chali pale kwenye Kitanda kile maarufu kama 'Telemka Tukaze' ikiwa na maana ukilalia sana au imepita muda au amaelalia mgeni kibonge basi kamba huwa na mtindo wa kulegea hata usiku unaweza kujikuta upo kwenye tobo hadi utelemke kikazwe zile kamba upya na ndio sababu kikaitwa telemka tukaze.
Japo hakuwa na chaguo zaidi ya kukubali hali halisi aliyoikuta pale lakini aliwaza hata akiolewa na Dullah hatoweza kukaa kwenye mazingira yale tena kijijini kama vile ni heri waende wakaishi mbali peke yao.
Akiwa anafikiria mambo kadha wa kadha Asu huku mikono na kichwa chake kikiwa kifuani mwa Dullah mara alianza kuguswa na vitone vya maji tokea juu.
"D kuna kidudu kinatukojolea juu D hatariii"
aliogopa Asu na kukurupuka pale kitandani.
"Aaagh! baby acha uoga si matone ya mvua!"
"Mvua?!"
"Hee, mbona kuna mvua kubwa tu nje inanyesha sasa hivi"
alijibu D na kuanza kusogeza kitanda upande ule panapovuja na kulieka plastiki ili matone yote yaliyoanza kuvuja yadondokee mule.
"Njoo bhana baby usiogopee"
aliongea Dullah na mara muungulumo mkubwa wa Radi ulisikika baada ya mwanga mkali kuwaka
"Aaaaaaaaaaagh babyyyy"
aliogopa Asu na kwenda kumkumbatia Dullah.


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 33




(UPANDE WA PILI)
___________________

Wakati upande wa Asu na Dullah mawazo na vituko vikiendelea tofauti upande wa pili walipolala Mama Dullah na mwanae Ilham wao nao baada ya kuingia chumbani kwao na kutokana na wembamba wa ukuta kutozibwa dali waliweza kusikia sauti na maneno yote ya Asunta yaliyowafanya nao waanze kujadiliana kwa sauti za chini sana ili upande wa pili wasiwasikie.
"Mh! mama Mkwe umepata.."
"Yaani mwanangu Ilham hapa kazi ipo"
"Hivi unavyoona mama anamfaa kweli kaka Dullah!?"
"Mh! mwanangu ni mapema sana kulizungumzia hilo."
"heee, ila mi sikufichi nimetokea kumchukia ghafra tofauti na nilivyomuona walivyofika."
"Kwanini Ilham"
"Wee, mama huoni? kwanza anajiona sana ana dharau na majivuno ukimsemesha anajibu kama bubu yaani maneno yake yananiboaa"
aliongea Ilham kilichokuwa moyoni mwake muda ule na kumuelekeza mamaake ambae japo aliona utofauti kidogo wa tabia toka kwa Asunta lakini bado hazikumfanya asimuamini mapema kiasi kile mkwewe mtarajiwa.
"Unasikia kivumbi hiko mama..?"
aliongea tena Ilham mara baada ya kusikia ukelele wa Asu pindi alipostuliwa na matone ya mvua sambamba na Radi.
"Mwanangu Ilham hupaswi kumtafsiri mtu mambo chungunzima kwa tabia uliyoiona siku moja tu. Hebu kwanza jitengenezee upendo kwa wifi ako"
aliongea mama Dullah na kumfanya Ilham abaki kimya na kulala.

* * * *
DAR - TANZANIA
________________

"Haiwezekani kabisa kabisa wala haituingii akilini hiki mnachotwambia. Hii sasa imekuwa mpya hatujawahi kusikia mchezaji aliyesajiliwa akafichwa kwa maslahi ya timu iliyomuuza. Kha!! Hapana hapanaaa Inabidi mtwambie ukweli tu nini tatizo kuliko orojo mnazosema sasa."
"Ni kweli kabisa ndugu kwa fikra zako una haki kusema hivyo lakini pia tumia hekima kama mtu mzima kufikiri kwa kina kuwa kama kweli tulikuwa hatutaki kuwauzia huyo mchezaji na bado tunamng'ang'ania si tungekataa ofa yenu wala tusingemwita?? Hebu acha kufoka bwana Tushakwambia hadi sasa hakuna anaefahamu alipo huyo mchezaji."
"HAPANA.. Wewe muongo tu harafu kesho mnajua ndio safari ya Nairobi na kila kitu kisha tangaza kule watu wanasubiri ujio wetuuu aaahg Mbona mnakuwa waongo waongo nyinyi Watanzania..?"
"He, he !!! Ndugu sasa unatafuta ugovi mwengine, Hebu jiheshimu wewe."
"Nijiheshimu nini..? Niache kuwaambia ukweli? Sasa Hii Kesi usitegemee itaamuliwa hapa tu bali lazima ifike Caf."
"Wewee Usitutishe peleka hata Fifa kama unataka"

Yalikuwa ni majibizano ya ghadhba kati ya Scout wa Tusker fc na Mwenyekiti wa Tandale fc juu ya kutoweka ghafra kwa Dullah bila taarifa yoyote wala hakuna aliyejua wapi ameenda.
Kizungumkuti kiliendelea ndani ya vichwa vya watu huku Roja akipata wakati mgumu kutokana na urafiki baina yake na Dullah viongozi na mashabiki karibia wote waliamini lazima Roja atakuwa anajua wapi Dullah alipo.
"Twambie Roja wapi ameelekea rafiki ako na yule bint maana kesho ndio safari harafu hawa jamaa wana maneno na msimamo mkali sana hii itatusumbua hata sisi, tafadhali usifiche ujuacho Roja tunakutegemea wewe ndie Kpten Roja."
alikuwa ni kocha wa Tandale akim bembelez Roja aseme kama anajua wapi alipoelekea Dullah ili wajivue zigo zito la lawama lililokuwa linawaelemea muda huo.
"Hapana Kocha kweli kabisa mimi hajaniaga wala sijamuona anavyoondoka sijui kabisa kwa kweli"
aliongea kwa msisitizo Roja lakini bado haikumfanya yule kocha kulegeza uzi wa imani kuwa kweli hajui Dullah alipo zaidi aliamini kuwa Roja anadanganya kwa maslahi mengine anayoyajua yeye na Dulla na si kweli kama hajui wapi alipo.
"Haya Roja ila tegemea hatua zitazochukiwa dhidi yake na wewe utahisika"
aliongea Kocha na kuondoka akimuacha Roja katika taharuki zito asijue afanyanyeje kwani ni kweli kabisa hakujua wapi Dullah alipo japo alikuwa na hisia kuwa huenda wametoroka na Asunta nyumbani kwao Tanga mbapo hata yeye Roja hajawahi kufika zaidi ya kukanyaga ardhi ya Tanga siku ile ya mechi waliyovuna ushindi mnono.

Baada ya kuwa anaondoka jioni ile maeneo ya uwanjani kurejea mahala alipokuwa anaishi kulekule Sinza ndipo kabla hajafika stendi tandale kwa Tumbo alisikia honi ya gari iliyokuwa inamfata nyuma yake na alipoipisha ili ipitae ndipo ile gari ya kifahari aina ya Vorgie iliposimama kabisa na kiliposhushwa kioo ilisikika sauti ikimwita Roja na mara aliposogea kwenye ile gari kuchungulia kumtazama dereva wake moyo ulimripuka baada ya kukutana na sura ya yule mzee ambae alimkumbuka vizuri na aliyakumbuka maneno ya Jack pindi alipowafahamisha kuwa yule mzee ni Pastor na ndie baba mzazi wa Asunta.
"Shikamoo mzee."
alisalimia Roja
"Marhaba kijana, ingi garini nina mazungumzo machache kidogo na wewe"
"Mh! mzee wangu nina haraka sana kuna sehemu muhimu inapaswa nifike saa moja kwa hiyo haitawezekana mzee wangu labda nikuachie namba za simu tutaongea kwenye simu tu"
alijibu Roja na kuchomekea uongo ambao aliamini utamsaidia kuvuka katika mtego wa yule mzee ambae alihisi kabisa si mtu mzuri hasa kutokana na vile alivyotaka kumfanyia Dullah mara baada ya kumtumia mwl Jack ambae kwa bahati nzuri alikuwa anapenda soka na kiwango kizuri cha Dullah ndio ikawa silaha kubwa kumuokoa katika mikono ya Jack mara baada ya kutokea kumpenda ghafara na kuachana na matakwa ya yule mzee kufikia hadi kutoboa siri na mipango ilivyokuwa yeye mwenyewe.
Hivyo kitendo cha kumwita na kutaka waongelee ndani ya gari hakukiafiki hata kidogo moyoni mwake ukizingatia Dullah hayupo na alijua fika na Asu nae hayupo lazima itakuwa wametoroka pamoja huko sehemu ambayo hawajamwambia wala kumuaga mtu yeyote.
"Hapana kijana wangu ni mazungumzo ya muda mfupi sana, niko tayari hata kukupeleka hiyo sehemu ambayo ni muhimu unatakiwa uende pasi na kuchelewa... Tafadhali mwanangu ingia tuzungumze"
Alisisitiza tena Pastor George kwa sauti ya upole na ushawishi lakini bado Roja alitilia mkazo na kuweka msimamo wake tena zaidi ya mwanzo.
"Mzee, yaani hapa tunavyobishana ndio nazidi kabisa kuchelewa. Kama vipi njoo kesho mapema saa tisa hapa uwanjani kabla hatujaanza mazoezi saa kumi nadhani lisaa limoja litatosha kabisa kuzungumza"
alisisitiza Dullah na kuanza kuondoka hali iliyomfanya Pastor George apaki gari pembeni na kuamua kushuka kumfata kule alipokuwa anaelekea.
"Kijana...kijana..haya nisubiri basi.."
aliita Pastor George kumsimamisha Roja ambae aliamua kukatiza njia ambayo huwa hapitagi kabisa.
("Mh!! Leo,! mbona D ameniachia mitihani hivi?!")
alijisemea moyoni D na kusimama kumsikiliza yule mzee Pastor anasemaje.
"Sikia kijana uuuphhhh Nisikilize vizuri, mimi naitwa George Pascal ni babaake Asunta, najua unamfahamu vizuri usinidanganye hata kitu kimoja ndio maana hata mimi nimeamua kuwa muwazi leo. Najua sura yangu si ngeni kwako ila naomba unifikishie salamu zangu kwa rafikiako manywele kuwa sina ubaya nae wala sihitaji matatizo yoyote ila anachotakiwa kufanya ni kumrudisha bint angu nyumbani kwao.... Mwambie na umsisitize nampa siku tatu tu kama kweli anampenda na anataka kuishi na mwanangu Asu basi amrudishe kwanza salama usalimini kisha afate taratibu kama wanazofata wenzake wanapohitaji kuishi na watoto wa watu na kuwa wake zao na sio kama alivyofanya yeye kujimilikisha mtoto wa watu pasi na taratibu za msingi kufatwa...."
Aliongea Pastor George kwa sauti ya wastani yenye mtetemo wa hasira ndani yake.
"Sawa mzee nimekusikia lakini hiko unachozungumza mi sikijui kabisaaa wala sijui pa kuanzia wapi kwa kuwa kwanza sina rafiki anayeitwa Manywele wala simfahamu bint anayeitwa Asunta. Samahani sana mzee wangu utakuwa umekosea"
alijibu Roja na kutaka kuondoka lakini alidakwa mkono na Pastor na mara alipogeuka kuutazama uso wa Pastor safari hii ulimtisha mno kutokana na kukunjika kwa hasira na macho kuwa mekundu huku jicho moja likitiririka chozi.
"Nenda Kijana Ila kumbuka mimi si Chizi na Najua Umenielewa"
Kauli ile Ya Pastor George mara baada ya kumdaka mkono kwa nguvu Roja na kumuachia iliufanya moyo wa Roja kuingiwa na hofu kubwa juu ya usalama hata wake binafsi na kuondoka bila kujibu kitu akitafakari kwa kina hatua gani stahiki inapaswa achukue.


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 34


* * * *
MUHEZA - TANZANIA
_____________________

Usiku ulikuwa wa shida sana kwa Asunta usingizi ulipaa hofu ilitawala moyoni mwake kila alichokiona mbele yake kilikuwa kero kasoro mtu mmoja tu ambae ndie alimfanya wafike pale nae ni Dullah.

Asubuhi ilitimu baada ya mvua kubwa ya usiku kucha kunyesha na kusababisha chumba kigeuke kama chekecho au chujio na ulikuwa ni usiku wa adha ya aina yake kwa Asunta na aliona kama amelala pale mwaka mzima kwa jinsi alivyopachoka ghafra.
"D mpenzi wangu tufanye mpango leo tuondoke tukatafute nyumba ya kuishi hata Tanga mjini kuliko hapa baby"
aliongea Asu akiwa amekaa kwenye kile kitanda telemka tukaze huku akiwa amejishika tama.
"Unasemaje Asu?!"
aliuliza kwa mshangao Dullah
"Ndio hivyo tuondoke bwana hapa tuwaache wenyewe waliozoea adha, mi siwezi bwana khaa!!"
alijibu Asu kauli iliyomchoma na kumchefua mno Dullah lakini alihofia kumfokea kwa kuhisi asije kumpeperusha mapema ndege wake aliyeingia tunduni mwenyewe.
"Lakini Asu baby hapa ndio nyumbani kwetu, harafu nataka ujue baby hata mimi nakereka pia kwa hali hii lakini navumilia kwa kuwa najua siku moja haya yataisha tu. Vumilia baby"
alibembeleza Dullah japo moyoni aliifikiria sana kauli ya Asu ile eti 'wawaache waliozoea adha ile!'
Nani kakwambia shida ina mazoea? Moyo ulimuuma kwani watu aliowalenga Asu ni mamaake mzazi na dadaake ambae mdogo kuzaliwa harafu anaambiwa awaache?
Hii ilimuuma sana Dullah japo aliificha machoni.
"Sikia nikwambie kitu D, kama kweli unakerwa na hali hii kama mimi basi kwanza twende tukatafute nyumba ya kukaa mimi na wewe mjini, kisha tuwaache wenyewe waliozoea tutakuwa tunawatumia pesa waendelee kusimamia hiyo nyumba ya bati uliyonambia unajenga, ikishaisha imepakwa rangi vizuri kabisa tunanunua faniture za kisasa na kueka umeme wa Soral sambamba na jenerator kubwa kisha kila kitu kikiwa vizuri ndipo mimi na wewe tutafikiria walau kurudi kukaa hapa mara moja moja, au unasemaje baby..?"
Kauli ya safari hii alishindwa kabisa kuivumilia tena Dullah na kujikuta kwa mara ya kwanza anamtazama Asunta kwa hasira hadi Asu alistuka baada ya kukutanisha macho na Dullah na kuanza kuogopa huku akiwa hajui alipokosea ni wapi wala hakuona ubaya wowote aliouzungumza.

"Asu mbona una.. unakuwa na maneno machafu hivyo...?
Yaani unadiriki kupaona kwetu kama Jehanamu? Asu mimi ni masikini na nilishakwambia hivyo naomba usitudharau kiasi hiko kwa kuwa nyinyi matajiri huko kwenu Aaagh!!"
alibwata kwa hasira Dullah hadi machozi yakaanza kumtoka na kumfanya Asu abaki anamtazama kwa mshangao kwani kile alichokuwa anakisema kwa upande wake alijua kingemfurahisha Dullah.
"He basi samahani D sikujua kama ungefika huko"
aliongea kwa sauti ya upole Asunta na kuanza kum bembeleza Dullah ambae alikuwa amejiinamia kwa uchungu huku machozi yakimtoka.

* * * *
LONDON - UINGEREZA
_________________

Siku zilienda na hatimae baada ya wiki tatu Fredy alianza kupata ahueni kule London hali iliyoanza kurudisha furaha katika mioyo ya wazazi wake hususani mamaake ambae toka mwanae apate ule msuko suko hata kula kwake nako ilikuwa shida, hakuwa na hamu ya kula kabisa siku zote alikuwa mnyonge na mwenye kuombeleza, furaha iliota mbawa moyoni na usoni mwake alionesha huzuni muda wote lakini ilipofika ile siku wanaambiwa kuwa Fredy amefumbua macho na ameanza kuchezesha vidole ndipo kidogo alianza kujisikia njaa na kula chakula vizuri.
"Ni jambo la kumshukuru sana Mungu kwa hatua hii ilipofikia maendeleo si mabaya na hali itapoenda hivi baada ya siku tatu tutamuamishia kwenye wodi ya kawaia tu"
Yalikuwa ni maneno ya Daktari yaliyozidi kuwapa faraja na nguvu wazazi wa Fredy.
"Tunashukuru sana Dokta"
waliitika kwa pamoja pindi walipokuwa wanamtazama pia Fredy kupitia kioo kikubwa kule wodini alipolazwa muda huo.

Na kweli baada ya siku tatu hali ya Fredy ilizidi kutengemaa na kuruhusiwa kuhamishiwa kwenye chumba cha wodi nyengi za kawaida baada ya kuweza kumudu hata kuongea na kula mwenyewe japo muda mwengine akili zake zilionekana kama zinaruka ruka (kama mtu aliyechanganyikia) lakini Daktari yule alizidi kuwatoa hofu wazazi wake kwa kuwajuza kuwa atakuja kukaa sawa tu wala wasijali.
Ilikuwa kama sinema jinsi ambavyo mama Fredy alivyokuwa anamtazama mwanae muda mwingi pindi alipokuwa wodini na hakuamini kama kweli Fredy wake amekuwa mzima tena kwani alishahisi huenda asiamke tena.
Kilichomuumiza kichwa ni kutamani kujua ilikuwaje kuwaje mpaka mwanae akafikia kufanyiwa vile na Asunta? Na ndivyo alivyoamini mama Fredy kuwa lazima Asu alimpiga na kitu kizito mwanae kichwani kilichomsababishia mateso yale ya kukaa zaidi ya mwezi bila fahamu.
Lakini hakujua kama ndio hivyo chanzo hasa kilikuwa nini? na kama Asu alikuwa na nia mbaya kimakusudi kwanini alimuwahisha Fredy hospitali?
Haya maswali yalimchanganya sana mama Fredy na alijua mwanae pekee sasa ndio atayeweza kuwapa jibu juu ya kile kilichotokea na ukweli ilivyokuwa ambapo pia alijiapiza kama Asu alimfanyia vile mwanae makusudi kwa roho mbaya tu, basi lazima na yeye aje amlipizie kivyovyote vile ili nae ayapate walau mateso kama aliyoyapata mwanae Fredy.

Kwa upande wa Askofu yeye alikuwa muda mwingi anafanya ibada ya kutubia binafsi na kujilaumu muda wote kwa jinsi shetani alivyojaribu kuichezea imani yake na kufikiria kumfanyia kitu kibaya Asunta na kukata mawasiliano na Pastor George kwa sababu ya tukio lililomkumba mwanae.
Alitubia mwenyewe kwa siri Askofu hadi machozi yakawa yanamtoka na kweli alionesha kujutia haswaa kuwa kile alichokifikiria kukitenda ama alichokionea na kui=kionesha hakipendezewi na Mungu kwa kuwa yeye ndie mawenye kuhukumu a kujua kila kitu.
"Hee baba Mungu najua wewe ndie Mfalme na mwenye mamlaka ya kuhukumu. Naomba unisamehe kwa kile kilichotamkwa na ulimi wangu na kujiapiza kwa moyo kuwa nitalipa kisasi kwa yaliyomkuta mwanangu, najua baba nimekosea ni shetani alijaribu kucheza na imani yangu na kusahau kama wewe ndie mpangaji mkuu wa mambo, naomba baba sasa ninatubu baada ya ufahamu wangu kurudi katika hali ya kawaida. Kama ulivyomtuma mwanao aje atutoe katika ujinga na kutuonesha njia ya uzima nami nasema baba Asante kwani naamini katika Jina la Yesu Kristo nitasamehewa."
Aliendelea na maombi ya majuto kwa imani ya juu kabisa Askofu na kutubia kwake alifanya hasa nyakati za usiku pindi mkewe akiwa kalala.

* * * *
DAR - TANZANIA
____________________

Baada ya wiki kupita pasi na Kuonekana kwa Dullah ndipo club ya Tusker fc ya kenya ilipofungua kesi katika chama cha mpira wa miguu Afrika mashariki ambapo baada ya utafiti na uchunguzi yakinifu pamoja na uthibitisho wa kutoweka Dullah akiwa mikononi mwa Tandale ndipo adhabu ilitolewa kwa Tandale kuilipa Tusker gharama zote walizotoa sambamba na faini ya shilingi milioni kumi kwa uzembe.
Lilikuwa ni pigo kwa Tandale kurudisha kiasi kikubwa kama kile walichotoa Tusker ambacho tayari walishakimega mega viongozi harafu kama haitoshi na faini juu, kitu ambacho kiukweli kiliwaumiza sana vichwa na katika kuangalia jinsi ya kupata hizo pesa haraka au kupungua adhabu ndipo jopo lilipokaa tena chini kuzungumza na Tusker huku wakiwaomba wakubaliane nao ambapo katika maongezi yao Tandale walikubali kulipa hiyo faini lakini kwa upande wa pesa zilizotolewa kwaajili ya kumsajili Dullah waliomba wawape mchezaji mwengine ambae waliamini atawafaa sana kwani ndie tegemeo pia kwa Tandale wenyewe vilevile alikuwa kama pacha na Dullah pindi wawapo uwanjani, nae si mwengine bali ni Roja.

["Unadhani kweli atafaa? maana sisi tulitaka kwa Marasta."]
aliongea katibu mtendaji wa Tusker kwa njia ya simu na mascout wake pindi walipopata barua kutoka Tandale fc juu ya kile walichokuwa wameomba.
Lakini hata kwa maelezo ya mascout wenyewe na kufata historia ya uwanjani ya Dullah waligundua kuwa Roja ndie mchezaji aliyekuwa akisimama nyuma ya Dullah na kumchezesha kwa kumpelekea mipira mingi hivyo hawakuwa na jinsi ilibidi wakubali kutokana na ukweli nao walikuwa na ukame wa wachezaji wazuri baada ya kikosi chao kuzeeka kwa pamoja na kufanya vibaya kwenye ligi kuu ya Kenya.

Kazi sasa ilibaki kwa Roja kushawishiwa akubali kuondoka Tandale kupitia mkataba ule ule wa Dullah ambao utabadilishwa kidogosehemu ya jina na kuekwa lake kabla ya kwenda kusainishwa mkataba rasmi nchini Kenya.
Walifanya jitihada za kuongea nae na kumsihi asiwaangushe juu ya yeye kukubali nafasi ile adhimu na ndipo Roja alipokubaliana na ripoti ilifikishwa tena chama cha soka Afrika mashariki ambao wao baada ya kupokea faini yao na kusikia matakwa ya waliofungua kesi kukubaliana na Tandale nao hawakuwa na kesi zaidi ya kuruhusu jambo walilokubaliana walifate kisheria na ndipo taratibu husika zilianzwa kufatwa na hatimae Road to Kenya ikahamia kwa Roja ambae yeye ndie aliyatoa idia ya yale maneno kwa mdarizi ili iwe changamoto kwa rafiki yake Dullah arudi mchezoni na apate nafasi ya kuonekana na club za Kenya ili aende akacheze huko kwa nia pia ya kuwa jirani na Asunta lakini leo hii kibao kiligeuka na ikawa yeye aliyetoa idea na ushauri ndie anayeenda Kenya huku rafiki ake pamoja na mwanamke aliyetakiwa kumfata Kenya hajui wapi walipo hadi dakika hiyo.
Alipiga moyo konde na alijipa moyo kwenda kuvaa viatu alivyotakiwa kuvaa Dullah kwa juhudi zote na kujituma kwa niaba ya rafiki ake na kwa faida yake pia.

* * * *
MUHEZA - TANZANIA
__________________

Maisha yaliendelea huku Asu akiwa anaumia moyoni mwake na mazingira ya pale nyumbani lakini alibaki kulia na moyo wake kutokana na kuwa na upendo sana na mtu ampendae ambae alimgomea ushauri wake wa kutaka waondoke pale wakaishi mjini.
Nyota yake na Ilham iligeuka kuwa chui na paka siku baada ya siku kutokana naIlham kumuona wifi ake ana dharau sana na ni mtu mwenye majivuno mengi kwani muda wote Asu alikaa alipokaa Dullah, hakupenda kujichanganya na mama wala kuongozana na wifi ake kuchota maji kisimani lakini si Dullah wala mamaake aliyewahi kumsemesha Asu juu ya tabia ambazo alikuwa nazionesha pale nyumbani.
Kipindi hiko chote simu zao Dullah na Asu hazikuwa hewani kabisa na walizizima kwa sababu ya kuogopa kutafutwa au kuuliziwa kiurahisi kwa watu wa mitandao pindi simu itapopigwa na kutoa location wapi walipo.

("Masikini mwanangu, anampempenda sana huyu bint lakini sidhani kama ni mke bora kwakweli mh! huyu bint si mlezi wa familia. Hivi hata wakifunga ndoa tutaweza kweli kukanyaga na kuishi kwa amani kwa mwanangu Dullah!! Aaaah! hapana hili inabidi nilidhibiti mapema lisitokee najua mwanangu hajui wala haoni kutokana na upendo alioufuga")
aliwaza mama Dullah siku moja akiwa kakaa nje mkekani akiwaona Dullah na Asu wakirudi kwenye matembezi pale kijijini huku wakiwa wameshikana mikono.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 35


"Mama leo tuna habari nzuri sana utafurahi"
aliaongea Dullah pindi alipofika jilani na mamaake.
"Vipi tena wanangu?"
"Mama, tumetoka hapo zahanati kumpeleka huyu kupima kwa jinsi alivyokuwa anajisikia imegundulika ni mja mzito na tumeongea yuko tayari mamam kubadili dini tuoane"
aliongea kwa furaha sana Dullah hata mama ake alifurahi kusikia habari kuwa Asu ni mja mzito lakini swala la kuolewa nae ndio kidogo lilikuwa tatizo akilini kwa yule mama.
"He ! hongera sana mama, hongera eeh"
"Ahsante mama"
alijibu Asunta, wakati huo Ilham alikuwa ndani na alisikia yale maongezi ambayo kwa upande wake yalimchefua mno.
("Eti mimba lol!! kaka nae asijichafulie damu yake bure, mwanamke ana dharau sana huyu na nyodo")
alijisemea moyoni Ilham na kinyongo alichomjengea wifiake kutokana na tabia ambazo yeye aliziona si nzuri taratibu alijikuta anajenga chuki.

******

"Ash-hadu.."
"Ashaadu"
"Al laailaha"
"Alaailaha"
"ila Allah"
"ilAllah"
"wa ash hadu"
"Waashhadu"
"An na Muhammad"
"an na Muhammad"
"Rasul Allah"
"RasulaAllah"
Naam alikuwa ni Sheikh akimsilimisha Asunta mara baada ya kupelekwa na Dullah katika msikiti uliokuwa kule kijijini kwao nia na madhumuni waweze kufunga ndoa.
Ndoa ambayo hata wazazi wa Asunta hawaijui wala hawakuwahi kulidhika nayo na siku zote alisisitizwa asije kuthubutu kubadili dini.
Dullah alifurahi sana kumuona Asu akiingia katika uislam lakini kwa upande wa Asu moyoni aliumia sana vile anavyosilimu na alifanya yote yale kwa sababu ya upendo kwa Dullah na kukubali wawe kitu kimoja ili aolewe nae.
Sheikh baada ya kumuelekeza Asunta kwa lugha ya kiarabu sasa alianza kumfafanulia atamke kwa lugha ya Kiaswahili kama ambavyo atavyotamka yeye ambapo alimwambia.
"Nakubali kwa Moyo, nathibitisha kwa ulimi kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa Haki ila Mwenyezi Mungu"
Aliongea Sheikh yule na Asu kutamka maneno yale kisha sheikh akaendelea.
"Na pia nakubali thabiti na naamini kwamba Muhammad ni Mtume wa mwenyezi Mungu"
Asu nae akatamka vilevile lakini Sheikh alipofika kipande alichosema
"Nakanusha kwamba Yesu au Issa si Mungu wala si Mwana wa Mungu bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu."
hapa Asu ulimi ulikuwa mzito hadi Sheikh yule akarudia zaidi ya mara tatu ndipo kwa shingo upande Asu alitamka yale maneno lakini moyoni aliumia mno kukanusha kuwa Yesu si Mungu lakini kwa kua alimpenda Dullah ilibidi aseme tu japo moyoni mwake alijiapiza kamwe hatoacha kukiamini kile alichokiamini angali mtoto hadi anakua kutoka kwa wazazi wake.

Basi baada ya hayo yote kufanyika Asu alitakiwa kuchagua jina alipendalo katika uislam ndipo Dullah alipoomba Dullah amchagulie na Dullah bila kuchelewa alimpa jina la MARIAM.
Ilikuwa ni furaha mpaka nyumbani kwao ambapo siku hiyo alichinjwa Jogoo mkubwa kwa niaba ya Asunta aliegeuka kuwa Mariam.
Lakini muda wote Asu aliikumbuka kauli ya mamaake juu ya uislam na hasira za babaake na kujikuta analia sana akijutia alichokifanya lakini pia hakuacha kujifariji kuwa bado imani yake ipo kwa wazazi wake hata kama anatafutwa lakini sasa alifikiria kurudi kwao hivyo hivyo kwa kuhofia kupata laana ya wazazi kwa kwenda kinyume na matakwa yao.

* * * *
LONDON - UINGEREZA
________________________

Hatimae alionekana Fredy akiwa mwenye furaha sambamba na wazazi wake pindi aliporuhusiwa rasmi kutoka hospitalini.
Mioyo yao wote hawakuamini kabisa kama kweli mtoto wao amerudi katika hali ya kawaida na vichwani mwao wote wawili mama na baba Fredy walipanga kukaa na mtoto wao awahadithie nini kilitokea na Asunta hadi yakampata yaliyompata.

Walipofika pale walipokuwa wamefikia pindi Fredy alipokuwa kalazwa katika lile jiji la London ndipo kikao cha dharula kilianza baada ya maongezi mengine na msosi.
"Eti mwanangu unakumbuka nini siku ya tukio lililokupata."
alianzisha mada Askofu
"Mh! baba ukweli ni aibu hata kusema"
aliongea kwa upole Fredy na kumshangaza mamaake ambae alikaa vizuri kumsikiliza mwanae kwanini anasema vile.
"Mama na baba, kwanza kabisa naomba mnisamehe sana"
alizidi kuongea kwa huzuni Fredy na kuwafanya wazazi wake wazidi kumuonea huruma na kumzuia pale alipokaa asitoke kupiga magoti kama ambavyo alitaka kufanya.
"Pia wazazi wangu kuna mtu nimemkosea sana tena sana, aaah sitoishi kwa amani hadi nisikie kauli yake ya kunisamehe"
alizidi kuongea Fredy na safari hii machozi yalianza kumlengalenga
hali ile ilizidi kuwashangaza wazazi wake na kukaa kiutulivu kabisa kumsikiliza.
"Wazazi wangu, ukweli sikumbuki vizuri mara ya mwisho ilikuaje hadi nilipostuka na kugundua nipo hapa hospitali na mmenishangaza sana milivyonijuza kuwa hapa si Tanzania bali ni London, aaaah naona dhahili nilikuwa nusu mfu...... Lakini cha mwisho ninachokumbuka wazazi wangu nilikunywa pombe."
"ULIKUNYWA POMBE?!!"
Walistuka kwa pamoja wazazi wa Fredy hasa Askofu hakuamini kabisa.
"Ni kweli wazazi wangu sitaki kuficha, Kwa mara ya kwanza nilikunywa pombe na yote ni kwa sababu ya Asunta."
"ASUNTA, huyu mtoto lazima tumfunze adabu mume wangu. Asunta!!! aagh"
aliongea na kuwaka mama Fredy kabla hata hajajua vizuri alimsababishia vipia mwane anywe pombe.
"Hapana mama, Asunta hana makosa ahata kidogo, wala yeye hakunywa pombe ila ni mimi mama niliekosea kwa kuwa nilimpenda sana na kila nilipojaribu kumwambia moyo ulikuwa mzito kwa vile alivyokuwa ananiheshimu kama kaka, ndio sababu nilikunywa pombe ili inisaidie kukata mshipa wa aibu kama nilivyosikia watu wakiisifia ili nami inasaidie nimwambie ukweli Asunta bila soni lakini sikujua kama ingeniletea madhara kiasi hiki."
kauli hii ilizidi kuwapa taharuki wazazi wa Fredy lakini upande wa mamaake Fredy yeye ndio kwanza alizidi kuwa na hasira na Asunta kwa taswira zilizokuwa zinamjia na chuki iliyomuingia ghafra juu yake kabla mwanae hajazinduka zilimfanya aone picha ya mbele ilivyokuwa vile mwanae alivyokuwa anahadithia kumbe ilikuwa tofauti.
"Kwahiyo hiyo ndio akaona Jambo la busara kukupiga na chuma kichwani. Mi bado nina hasira na huyu bint baba Fredy."
"Hapana mama, sio hivyo kabisa Asunta hajanipiga ila mimi mwenyewe nilidondoka kwaajili ya ulevi"
"Kauli hii sasa ilimfanya mama Fredy ashushe pumzi na kukumbuka maneno ya daktari kule Tanzania kuwa aliyempeleka hospital Fredy alikuwa ni Asunta, sasa alishangaa kwanini Asunta hakuwambia ukweli na kuamua kutoroka?

"Kwa hiyo mwanetu kumbe ulikuwa unampenda Asunta kwanini hukulieka wazi tuongee na wazazi wake mbona lilikuwa swala dogo tu. Kwasasa unatwambiaje kuhusu Asunta?"
"Baba, kwanza nitaridhika nimuombe msamaha kisha nitafurahi zaidi kama mtanisaidia niweze kumuoa kabisa awe mke wangu."
Maneno haya ya Fredy yalizidi kumfanya mamaake achoke lakini kwa Askofu yeye alionesha tabasamu na moyoni mwake aliwaza kukutana na Pastor George wajadili kuhusu hilo.

* * * *
LAGOS - NIGERIA
______________________

Ndege iliwasili jijini Lagos ikitokea Tanzani na wasafiri walianza kushuka huku miongoni mwao alionekana Pastor George babaake Asunta.
("Asante Yesu kwa kutufikisha salama. sasa lazima nikamkomeshe mwana hizaya yule")
alijisemea moyoni Pastor pindi alipokuwa anashuka kwenye ile ndege na kukanyaga ardhi ya nchi ya Nigeria huku mkononi akibofya bofya simu yake kuandika ujumbe mfupi kwa mwenyeji wake aliyewasiliana nae kwa nia ya kumpokea.

Alipoingia ndani ya jengo la uwanja sehemu ya kutokea wasafiri alifurahi Pastor mara baada ya kukutana na rafikiake ambae ndie alikuwa mwenyeji wake aliyekuwa amewasiliana nae kumpokea.
"Aaaaah Chineduuu ca'vaa?"
"bien George karibu sana"

SEHEMU YA 42
_____________________

MTOTO WA PASTOR (42)
NA - MTOTO WA BECKER (The Special Thinker)
___________________________
__________________

Alikaribishwa Pastor George na mwenyeji wake yule aliyetambulika kwa jina la Chinedu na kutoka nje ya uwanja ambapo Chinedu aliegesha gari yake sehemu husika na kuingia sambamba na Pastor George ndipo safari ikaanza taratibu huku maongezi yakichukua nafasi kubwa baina yao.
"He, za siku nyingi Pastor?"
"Aaah, safi kiasi Chinedu lakinii...!"
"Lakini nini sasa! eeh, au Mudawa nakupa haiko fanya kazi muzuri?"
"Hapana, dawa ile kiboko.. Imeniongezea heshima sana."
"sasa Iko na mushida gani tena?"
"Mwanangu ndie ananisumbua kama nilivyokuelekeza ufanye dawa huko alipo apachukie na atamani kurudi nyumbani lakini naona siku zinaenda tu"
"Hahahaaaa Pastor George hapana weka mapureshaa hivyo, ile mudawa iko nafanya kazi baada ya misiku thelathini. sasa hivi iko chezesha mutima, pamba gutwi (sikio) hapana sikia kitu iko narudi Asu wako hahahaaa misiku hii hii hahahaa"
aliongea kwa kujiamini Chinedu huku akicheka wakati huo gari iliacha ile njia ya rami na kuingia barabara ya vumbi ambako ndiko huko Chinedu alipokuwa anaishi.

Chinedu yeye alikuwa ni mganga maarufu sana wa kienyeji jijini Lagos na alikuwa anadili na watu mbalimbali wenyeshida tofauti.
Kwa mtazamo wa Chinedu kwa nje utamuona kama mtumishi wa Mungu kwa jinsi anavyojiweka na kupenda kujichanganya na wanaojiita watumishi wa Mungu lakinoi kumbe pembeni wana siri zao wanazoziendeesha pamoja nae.
Yeye alikuwa anatibu na kuroga, alitumia majini ya kutengeneza kwa uchawi na mazingaombwe mbalimbali katika matibabu yake na alizijua dawa nyingi sana za kichawi na alitumiwa na watu wengi hususani wale waliokuwa watumishi wapenda fedha na umaarufu wa haraka kama ambavyo Pastor George alivyokuwa anataka hadi akapewa kichupa cha dawa ambayo atapopaka kwenye mikono na akiwa anamuombea mtu kama kuzuga tu mwishoni kuna maneno yasiyoeleweka anayopaswa kuyatamka na akifanya hivyo ndipo pepo lililokuwa ndani ya ile dawa humuingia yule aliyeshikwa kichwa akiombewa na kumuangusha huku wau wakidhani pepo ndio linatoka kumbe ndio limeingia.

Walifika pale alipokuwa anaishi Chinedu katika jumba moja la kifahari na mara baada ya mlinzi kufungua geti na kuingia ndani, Chinedu sambamba na Pastor George waliingia kwenye lile jumba ambalo mbali ya kuwa lilikuwa kubwa lakini ajabu Chinedu alikuwa anaishi mwenyewe hakuwa na mke wala mtoto.
"Karibu sana, karibu kwenye muchumba yetu tukomplete (tumalize) mambo George hahaha"
aliongea Chinedu na kufungua chumba kimoja wapo kilichokuwa na muonekano wa kutisha sana kutokana na fuvu kubwa la mtu lililokuwa kwa ndani kwenye kiti cha mifupa na maajabu ya hilo fuvu lilikuwa na uwezo wa kusema jambo ambalo si la kawaida kabisa.
Baada ya kuingia na kukaa Chinedu alibadilisha nguo na kuvaa zile za kazi na hapo akafanya dawa anazozijua yeye na kunuia jina la Asunta kisha ndipo maajabu yalipoanza baada ya kile chumba kuanza kufuka moshi ulioganda na kujikusanya sehemu moja na kutengeneza kitu kama TV wakati huo Chinedu alikuwa bussy kuongea lugha zisizoeleweka na mara ule moshi ulibadilika pale na kuanza kuonesha video ya Asunta akiwa anasilimishwa na Sheikh mmoja na pembeni yake alionekana Dullah na watu wengine ambao Pastor George hakuwatambua.
"Khaaaaaaaaaa! yaani mwanangu ndio amefika hapa?!!"
alistaajabu na kupayuka Pastor George pindi alipoona mwanae kipenzi Asu akisilimishwa tena ilionekana bila ya ridhaa yake.
"Nawaombaaa jamani nawaomba sana mnisaidiee, Mfanye mnavyojua nyinyi wakubwa mwanangu zisizidi siku tatu arudi mwenyewe nyumbaniiii... Aaaag"
aliumia Pastor na kuwaomba majini yaliyotoka kwa Chinedu na kuipoteza kabisa imani yake ju ya Mungu aliyekuwa anamtumikia.
"Kwa hiyo George natakaje Fanza ili ukuwe nasikia muzuri?"
aliuliza Chinedu na kumfanya kwanza Pastor George afikirie kidogo cha kufanya ili amkomeshe kabisa Dullah.


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 37



Kesho yake asubuhi na mapema familia ya Askofu Mbukinyo walisindikizwa uwanja wa ndege na wenyeji wao na mara baada ya kuagana na kutaniana kila la kheri ndipo muda wa abiria kuwa Ndegeni ulitimu na wakaacha wenyeji wao pale wakiwaangalia kwa furaha nao kuingia kwenye ile ndege kubwa ambayo ilikuwa inaenda moja kwa moja Nairobi Kenya.

Safari ilikuwa nzuri na yenye amani kwa masaa zaidi ya manane angani kabla ya Ndege kutua katika uwanja mkubwa wa ndege jijini Nairobi ambapo tayari taarifa zilishafika kuwa wanarudi siku hiyo huku kila mmoja hususani watu wa karibu na Askofu na wale wa Fredy wakiwemo wafanyakazi katika kampuni aliyokuwa anaisimamia na wengineo walioguswa na taarifa za kulazwa kwake hadi kusafirishwa akiwa katika hali ya kutojitambua, ziliwasikitisha wengi na siku hiyo walivyopata habari za kurejea kwao ndipo nao walienda kuwasubiria kabisa uwanja wa ndege.

Msafara wa gari tatu ikiwemo coaster moja iliyobeba wafanya baadhi ya wafanya kazi waliokuja kuwapokea kina Fredy uliondoka uwanjani pale mara baada ya kufika kwao na moja kwa moja safari ya kwa Askofu ilianza ambapo nako kulikuwa na ibada maalum ya kumuombea Fredy.
Na baada ya ibada ile Askofu aliwatangazia waumini kuhusu tafrija itayofanyika wiki moja ijayo katika ukumbi wa Nairobi Hall kwaajili ya watu kufurahi pamoja na Fredy na kumshukuru Mungu kwa wema wake.

* * * *
LAGOS - NIGERIA
________________

Walionekana sasa wanatoka nje ya jengo lile baada ya Pastor na Chinedu kumaliza mambo yao kwenye kile chumba maalum cha kichawi alichokuwa anarogea watu Chinedu na kuwapa dawa mbalimbali za kijini wateja wake wapate kufanikiwa kwenye mambo yao tofauti na hususani zile za mvuto kwa viongozi mbalimbali na wasanii.

"Chinedu wewe ni kiboko kwa kweli, Yesu na Maria dah!"
aliongea kwa furaha akiwa haamini Pastor pindi walipokuwa ndani ya gari wakitoka mahala pale.
"Nilikwambiaa nilikwambiaaa ni vikazi dogo sanaaa kwangu, hapana nakuwa naa moyo kwenda aa mbiooo. hahahaaa"
alijinadi Chinedu.
"Na ile siku naondoka nataka nikupe mudawa ya Pete. hiyo ndo tamaliza kabisaaa ile wewe nataka kwenye mambo yako hahahaaa"
"Daah! Nitafurahi sana Chinedu maana nataka nikirudi sasa kila mtu ajue kuwa mimi ndie mzee wa Upako mwenyewe"
"Ondoa mashakaa mambo yakuwa muzuriiii tu."
"Haya Chinedu kama kawaida mzigo wako wote nitakuingizia kwenye acount yako kama siku zote."
"Iko nafanya muzuri sana."
Baada ya maongezi ya hapa na pale gari ilifika kwenye hoteli moja pale Lagos karibu na uwanja wa ndege na hapo Chinedu aliagana na George kwani ndio hoteli ambayo mara zote Pastor alikuwa analala pale pindi anapokuwa Nigeria.

Akiwa ni mwenye furaha sana Pastor Grorge mara baada ya kumaliza uandikishwaji na kuingia kwenye kile chumba cha hoteli alichopenda kufikia ndipo mara ujumbe wa simu ya mkononi uliingia na alipousoma ilimbidi kwanza akae pale kitandani na kuurudia tena ambapo ujumbe ulikuwa umetoka kwa Askofu tena kwa ajabu ulikuwa ni ujumbe wa kuombwa msamaha yeye na familia yake hususani Asunta ili aweze kurejea tena Nairobi kumalizia masomo yake.
("Shaaaabbash, dah! kweli Chinedu noma. Yaani kukaa tu kwenye kile chumba Nishamlewesha hadi Mbukinyo? jee nikiipata hiyo pete..! Si watu watakuwa wanalia wakiniona? ahahahahaa")
alijinasibu Pastor George wakati akiisoma ile msg ya Askofu Mbukinyo ambae alikumbuka mara ya mwisho alikuwa hataki hata asikie sauti yake kutokana na kitendo cha mwanae kupata matatizo mikononi mwa Asunta na Asu kutoroka nchini Kenya.
Alitulia na kuanza kuijibu ile msg kwa utulivu kabisa.
)('Baba Askofu, hupaswi kabisa kuniomba msamaha katika suala lililotokea kwani naamini ni shetani ndie alitaka kuzichezea nafsi zetu na kuziharibu imani zetu ili twende kinyume na bwana. Nilikuwa na mpango pia wa kuja huko London kama nilivyokuja Nairobi lakini kwa kuwa mmerudi basi kwa sasa natokea Nigeria na sitofika nyumbani kwanza nitafika huko. Nguvu ya bwana imefanya kazi yake. amani izidi kudumu miongoni mwetu baba Askofu, mpe pole sana kijana wetu')(
Alitabasam Pastor George na kujiona yeye ni mshindi pindi alipomaliza kuiandika ile msg na kuituma kwa Askofu Mbukinyo.

* * * * *
TANGA - TANZANIA
___________________

)('Mama, mi najuta kwa kweli najuta sana, sikutegemea kama mtu ninayempenda ndugu zake wanaweza kunifanyia hivi.')(
))(('Pole mwanangu, ndio ukisikia asiesikia la mkuu ndio kama hivyo. Tulishakwambia waislam si watu'))((
)('Kweli mama Nimeamini, naomba mnisamehe sana, nimeteseka vya kutosha mamaangu')(
))(('Wala usijali mwanangu, bwana yuko nawe atakufikisha salama'))((
)('Sawa mamaangu')(

Zilikuwa ni sms charting baina ya Asunta na mamaake kipindi hiko alikuwa kwenye Coaster ya kuelekea Tanga mjini ili awahi basi la kumrudisha Dar baada ya kuchoshwa ghafra na maisha ya kina Dullah pale kijijini Muheza.
Akili na moyo wake ulitibuka kabisa Asunta kuhusu kukaa na Dullah hasa akiangalia mazingira ya kwao vile alivyowaona ndugu zake na alitokea kumchukia sana Ilham mdogo ake Dullah ambae alimkunja na kutaka kumpiga masaa machache kabla hajaondoka kwa hasira.
Lakini akiwa kwenye basi kuna muda akili za kawaida zilirudi kichwani mwa Asu na kujishangaa kwanini anaondoka na kumuacha mtu aliyempenda? lakini alipojiuliza hivi tu ndipo moyo ulipotibuka ghafra baada ya kumjia picha ya sura ya Ilham machoni mwake na ya mamaake Dullah na hapo anamuona kinyaa hadi Dullah moyoni mwake na kujiona yuko sahihi kabisa kuondoka.

Coaster ilifika Tanga mjini na kama bahati aliikuta Dar Expless ikiwa ndio inataka kutoka stendi na kuiwahi hiyo hatimae safari ya kurudi jijini Dar ilianza huku akiyaangalia mazingira ya jiji la Tanga na kujisemea moyoni kuwa pale alikosea wala hakutakiwa mtu kama yeye kuishi kule.

<< UPANDE WA PILI >>

"Asuuu, Asuntaaa AAH!! Asu wanguuuu"
alionekana Dullah akikimbilia maeneo ya stend huku akiita jina la Asunta mpaka alipofika pale kenye kijiwe cha boda boda na kuwauliza watu maswali ovyo ambayo hawakujua waanze kumjibu vipi.
"Jamani Asu wangu amefika hapa? .. Eeeh! kaka umemuona Asu wangu?"
maswali ya Dullah yaliwafanya wale vijana wapanda pikipiki wamshangae tu kwa jinsi anavyoonekana na kuhisi au ameanza kuchanganyikiwa?
"Zidanee, unamuulizia Shem nini?"
ilisikika sauti ya kijana mmoja aliyekuwa anarudi na boda boda akitokea njia ya mjini.
"Ndio Pius vipi umemuona?"
"Nilipishana na pikipiki ya Jof kama nusu saa hivi alikuwa kampakia"
majibu ya Pius yalimfanya Dullah akodi pikipiki haraka kumfatilia Asunta lakini hadi amefika Muheza mjini alizunguka bila kuona dariri yake na kwa msaada na maneno ya Pius ndio yaliweza kumfanya Dullah akubali tena kurudi nyumbani kwanza.
"Sikia Zidane, mtu mzima hatafutwi hivi ndugu yangu usichanganyikiwe twende kwanza nyumbani ndipo utapata njia nzuri ya kufanya"
aliongea Pius baada ya kumsihi sana Dullah aliyekuwa anang'ang'ania wafike hata Tanga mjini huenda wangemkuta huko.
Alipanda kwenye pikipiki huku akiwa kachanganyikiwa Dullah akili moja haikai mbili haipo kipindi hiko Pius alikuwa anakandamiza gea kurejea Muheza kule kijijini.

Walipofika kijijini pale kwenye kituo cha bodaboda ajabu walikuta watu wengi wengi huku kila mtu akishangaa na wengine wakiwa wanatokea kule kwenye nyumba ya kina Dullah kila mtu akisema lake na hasa walipomuona Dullah walianza kumnyooshea vidole.
"Si yuleeee, tuwe makini sasa ikiwezekana nae tumkamate kabla hajaanza kutuaibisha wanaume jamani, hawa watoto wote wamewehuka ghafra."
"Kweli kabisa Mjumbe mi mwenyewe nilimuona huyu kijana akikimbia huku akisema ovyo"
"haya jiandaeni anatusogelea, si mmeona mwendo wake?"

Yalikuwa ni maneno ya watu waliokuwa wanatokea kule kwa kina Dullah wakiwa wamefatana na mjumbe wa kijiji kutokana na tukio lililojitokeza muda mfupi pindi walipomkamata Ilham dadaake Dullah akiwa uchi wa mnyama huku nguo kazifungafunga mgongoni kama mtoto.
Ilionekana dhahiri Ilham alirukwa na akili kabisa na kuwa chizi hivyo walifanya jitihada za kumfukuza hadi wakafanikiwa kumkamata na kumrudisha kwao huku wakiwa wamemfunga kamba za mikono na miguu na katika maongezi ya sintofaham toka kwa watu mbalimbali ndipo ilipozuka mada kuwa hata kakaake alionekana kukimbia ovyo huku akipiga kelele zisizoeleweka na hivyo kuhisi hata yeye huenda akawa karukwa na akili kama mdogoake na ndio sababu walipomuacha Ilham ndani walitoka kwa lengo la kwenda kumtafuta Dullah wajue wapi alipokimbilia na ndio ikawa sababu walipomuona mbele yao akija na njia ile ile waliyokuwa wanapita wao ndiopo walijiandaa kwa nia ya kumkamata kabla nae hajaanza kuvua nguo kama dadaake.
"Jumbe jiandae anakaribia huyo"
aliongea mjumbe na kumpa tahadhali kijana mwengine aliyekuwa upande wa kulia.
Wakati huo Dullah aliongeza mwendo kutaka kuwahi nyumbani kujua kulikoni mbona watu wamekuwa wengi vile, ukijumlisha na mawazo juu ya Asunta ilitosha kabisa kwa mtu kumuhisi vibaya Dullah kuanzia uso jinsi alivyouweka ukijumlisha na mwendo ndio kabisaaaa.

"Vipi jamaaani?!!! mbona siwaelewoiiiii!?"
alihamaki Dullah mara baada ya kudakwa na wanakijiji na palepale mjumbe alitoa kamba ile ya katani iliyobaki.
"Mzuieni vizuri"
alitoa amri mjumbe kipindi Dullah akipapatika kutaka kujinasua huku akishangaa kwanini wameamua kumkamata namna ile.
"Mjumbee!1 Mbona siwaelewiii... We Jumbeee aaaagh!"
alizidi kuita Dullah wakati huo walifanikiwa kumfunga vizuri kamba na kum beba sasa kumpeleka kule kwao.
"Jamaani nishusheenii Nifunguueniii mie sio Chiziii Jamaaa !!!! Mjumbeeee aaaaah Nifungueniiiiiiiii"
Alizidi kupiga kelele Dullah na kufurukuta ili afunguliwe hali ile ilizidi kuwafanya waamini kuwa huenda kweli Dullah amechanganyikiwa kwani hata chizi hujiona sawa tu.
"Dickson, wahi haraka kwa mzee Makatapila aje aangalie tatizo hapa"
aliagiza yule Mjumbe wakati huo tayari walikuwa wanafika maeneo ya nyumbani kwao ambapo watu walikuwa wanakusanyana kuja kuangalia kinachoendelea baada ya taarifa ya mdogoake Dullah ambae alikuwa maarufu pale kijijini kwa jina la Zidane kuwa amepatwa kichaa sambamba na Zidane (Dullah) mwenyewe.
Kipindi wanafika mama Dullah ambae muda wote alikuwa haamini kama kweli mwanae Ilham amebadilika ghafra na kufikia hadi hatua ya kuvua nguo alibaki akilia na kumlaumu Asunta hadhalani japo watu walikuwa hawaelewi nini anachomaanisha.
"Huu uhawi tuuu, Ilham mwanaaangu nilikwambiaaa muacheee ona sasa? bint yule mchawiii...hiiii"
alilia mama Dullah lakini mara alipowaona watu wakija huku wamem beba na Dullah ndipo maumivu yalimzidi kabisa na kujikuta anadondoka ghafra.

* * * *




ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 38


* * * *

Wakati yale yakiendelea kwa kina Dullah upande wa pili alionekana Asunta akiwa kwenye basi iliyokuwa ikizidi kusonga mbele na kuzidi kuuacha mkoa wa Tanga na kuanza kuukaribia mkoa wa pwani.
Alijiona ni mwenye bahati kwani muda wote alipokuwa anachart na mamaake alijisikia faraja na alijipongeza kwa maamuzi aliyochukua kuwa ni bora na sahihi kabisa kuliko angeendelea kusubiri na kupoteza muda kule kijijini kwa kina Dullah.
Japo alijijua kuwa tayari yu mjamzito lakini haikumuumiza akili wala moyo kwa kujiamini na kuamini utajiri waliokuwa nao hauwezi kumpa mawazo hata atapojifungua alijua mtoto atalelewa tu, tena katika mazingira bora zaidi na salama kuliko yale ambayo aliyaona pale.

Lakini kuna kitu kimoja cha mazingara ambacho kilikuwa kinacheza mwilini na akilini mwa Asunta na ndicho kilichokuwa kinampa muongozo pasi na yeye kujijua hadi kufikia hatua ya kupiga simu na kuongea maneno ambayo kiukweli hayakuwa na ustaarabu hata kidogo kwani yaliwajengea sifa mbaya kina Ilham na mamaake japo kwa muda huo Asu hakuona ubaya wowote alioutenda kule zaidi ya kuamini kuwa alikuwa anaingia kwenye familia mbaya, masikini na yenye uchawi ndani yake pasi na kujua kuwa babaake mzazi ndie aliyekuwa anaingiza mambo ya uchawi na mazingaombwe kwenye maisha yao hasa yale aliyoyaita ya kiroho ili azidi kutengeneza jina na pesa nyingi.

Na kuna wakati pia Asu akili zake zilipokaa sawa kidogo na kuanza kumkumbuka Dullah ndipo kile kitu cha mazingara kinapomvaa tena pasi yeye kugundua wala mtu yeyote kuona na hapo kinambadilishia taswira na kumtengenezea imani mbovu juu yao na kumzidishia chuki kwa familia ya kina Dullah.
Mwenyewe Asu alijiona yuko sawa kabisa lakini hakujua kuwa sasa mwili wake unaendeeshwa na nguvu za giza kutoka kwa Chinedu na msababishaji wa yote ni babaake mzazi ambae ni Pastor George.

* * * *
LAGOS - NIGERIA
________________

Zilipita siku tatu baada ya kuwasiliana na Askofu Mbukinyo na kuaidiana kukutana nae huko Kenya kwa maongezi zaidi na kujadili hatima ya watoto wao ambapo katika maongezi safari hii kila mtu alikuwa na wazo kichwani la kuwaunganisha watoto wao kuwa mke na mume ili hata ukaribu wao uzidi kudumu na kuwa na nguvu zaidi.
Japo ilikuwa bado hawajaekana wazi swala lile lakini tayari Askofu alishaeka nia pindi Pastor George atapowasili Kenya na kuongea mengi atalichomekea na suala hilo kisha kuona mtazamo wa Pastor George upoje, lakini alijipa imani Askofu kuhusu ufanikishaji wa suala hilo.

Alionekana asubuhi na mapema Pastor George akitoka pale hotelini na kurudisha kila kitu ikiwa na maana uwepo wake ulikuwa umeisha na alitaraji kuondoka siku hiyo.
Alitoka nje na kukutana na rafiki ake Chinedu aliekuwa anamsubiria na kuongoza wote mpaka kwenye gari kwa mazungumzo zaidi.
"Pastor George, sasa kila kitu nakuwa Supa. Chukua hii mupete"
aliongea Chinedu na kumpatia pete aliyomuahidi Pastor George ambayo ilikuwa na kito cha mchoro wa nyoka wa kijani.
"Hiyo hapana kabisa chezea hahahaaa, kipindi nakua Kongo kwa mwalimu aliwahi tengenezea Rais yenu ilee hahahahaaa Ona nakuwa mutu ya kuogopwa sanaaa. hahahaa hiyo hapo muchechee"
aliongea Chinedu ambae uchawi wake alijifunzia zaidi huko Congo alipoishi zaidi ya miaka kumi na tano kutokana na mamaake kuwa raia wa huko ila babaake ndie alikuwa Mnigeria.
Baada ya Pastor kumalizana na Chinedu ndipo safari ya kuelekea uwanja wa ndege ambao haukuwa mbali na pale ilianza huku Pastor George akiwa anajiona kama shujaa anayerudi toka vitani na ushindi mnono mkononi.

**********

Ndege ilitua kwenye uwanja wa Nairobi na Pastor akiwa mwenye furaha alipokewa kwa heshima na wenyeji wake wakiongozwa na Askofu mwenyewe ambapo baada ya salamu za hapa na pale waliingia kwenye magari na safari ya kuelekea Nyumbani kwa Askofu ilianza.

"Vipi Fredy mwanangu sasa maendeleo yako?"
aliuliza Pastor George pindi wakiwa njiani ambapo kule nyuma alipokaa alikaa na Fredy ambae nae alienda kumpokea sambamba na Askofu.
"Nashukuru sana baba, kama unavyoniona sasa niko buheri wa afya"
alijibu Fredy huku kichwa akiwa kakiinamisha chini mithili ya mtu aliyejawa soni mara baada ya kufumwa akifanya kitendo cha aibu na watu anaowaheshimu.
"Mungu akubariki sana"
aliongea Pastor huku akiisugua sugua pete aliyovaa aliyopewa na Chinedu sehemu zile za kito na moyoni akinuia mambo aliyokuwa anayajua mwenyewe pindi gari ilipokuwa inaingia getini kwenye jumba la Askofu Mbukinyo.

Baada ya kushuka na kuingia ndani kwa pamoja walikaa sebuleni ambapo kulipambwa maradufu huku kila mtu aliyemuona Pastor George alimpa heshima tofauti kabisa na ilivyokuwa awali safari hii walimpa heshima ya kumuogopa zaidi na hata mama Fredy ambae aligoma kwenda uwanja wa ndege kumpokea Pastor George kwa sababu zake binafsi alizozificha moyoni kutokana na chuki aliyoijenga mwanzo kabla Fredy hajapasua ukweli lakini bado hakuwa na upendo wala kujali ujio wa Pastor George ila ajabu Pastor alipofika na kusikia sauti yake alitoka haraka na kwenda kumlaki huku akimsalimia kwa heshima kubwa kabisa.

"Naamini bwana amekuongoza na kuwa na moyo wa kipekee sana Pastor japo awali tulikukwaza kwa kukukasilikia pasi na sababu ya msingi, naamini sasa shetani ameshindwa na damu ya bwana imetulinda leo hii tuko pamoja. Narudia kusema utusamehe kwa yote. Karibu sana na sana"
alifungua maongezi Askofu baada ya kupata chakula kwa pamoja na kukaa na Pastor pale sebuleni kwa lengo la kujadili zaidi.
"Usiwe na hofu kabisa baba Askofu kwa hilo, wala sijaona wapi mmenikosea mi najua ni mitihani ya bwana pindi anapotaka kupima mizizi ya imani ya watu wake ambao shetani anawasumbua kila siku. Hakuna tatizo kabisa."
alijibu kwa kujiamini Pastor George na baada ya hapo ndipo Askofu alipomuhadithia kisa na mkasa kilichopelekea mtoto wao kupatwa matatizo yale hadi kufikishwa London alipoenda kupatia nafuu.
"Daa! aisee mi nilihisi hiko kitu kwa kuwa namjua vizuri mwanangu hata kipindi amezaliwa nilimuombea na kumshikisha biblia, lakini hakuna tabu wala sioni kama kuna tatizo tena endapo Fredy mwenyewe amekiri makosa naamini bwana kamsamehe na hata Asu mwanangu alishamsamehe ila najua kilichomfanya atoroke ni hofu juu yenu kwani roho mtakatifu alishamuonesha kuwa hamtamuelewa hadi aje awaeleweshe Fredy mwenyewe. Aaaah! Mungu ashukuliwe sana."
alizidi kukazia Pastor huku akijipamba na kumpamba mwanae kwa maneno matamu.
"Vipi lakini Asunta mlimpata?"
"Ndio amerudi leo hii huko nyumbani."
Ndipo hapo sasa Askofu alipoliingizia swala alilolifikiria muda mrefu baada ya kujua ukweli juu ya kilichotokea sambamba na ombi la mwanae bila kujua kumbe hata Pastor nae alikuwa na fikra hizohizo na kutokana na fikra zao kufanana swala lile lilipitishwa mara moja kwao wote kwa moyo mmoja.
"Basi hakuna shaka kabisa baba Askofu, Asu ni wakumwambia tu, na hatoleta upinzani wowote dhidi yetu, naamini kila kitu kitaenda sawa tu."

* * * * *
MUHEZA - TANZANIA
__________________

"Mpepeeni haraka mwenzenu hapo kina mama"
"Jamani mbona hivyoo!"
"We, kijana kaite wale vijana waliokaa kule barabarani tusaidiane hapa"
"Oooh! afadhali bwana Makatapila umefika usaidie hii familia"
yalikuwa ni maneno ya wanakijiji mara baada ya mama Dullah kudondoka pale chini na kupoteza fahamu kabisa.
"Mamaaaaa mamaaaaa . nifungueni jamaaani mamaaangu kafanyaje?!! Mamamamaaaaaaaaaaaaaaa"
Alipiga kelele Dullah huku akijitupa tupa pale chini alipowekwa kwenye mlango wa kuingilia ndani kwao.
"Makatapila wahi na huku jamani huyu yanampanda sasa hivi"
alisikika yule mjumbe akimwita Makatapila ambae alikuwa ni mganga maarufu wa kile kijiji na aliaminika na wengi kutokana na kazi zake za kutibu na kusaidia watu mbalimbali na kuna wengine walisafiri kutoka mbali kabisa kwaajili ya kupata tiba kwa Makatapila kutokana na sifa zake zilizosambaa sehemu nyingi.

Mganga Makatapila ambae yeye huwa anatembea na usinga muda wote anapopita na kijiji kizima kilimtambua na kumzoea kwa hilo alifanya jitihada zake za kumzindua mama Dullah na hatimae aliweza na ndipo alipomsogelea Dullah pale alipofungwa huku akiimba nyimbo anazozijua yeye akiongozwa na ule msinga wake.
"Khaa! huyu mmemfungia nini sasa?!"
aliuliza kwa sauti mganga Makatapila
"Huyo nae tulimuona wazimu unamuanza."
alijibu mjumbe lakini Makatapila kila alivyofanya kuona wapi alipochezewa mchezo Dullah aliona hakuna mchezo wowote wa mazingaombwe uliofanywa katika akili za Dullah za kumfanya afungwe kamba ama kuitwa chizi.
"Mfungueniii... Mfungueniii"
alitoa amri Makatapila na ndipo walipokuja vijana na kumfungua kamba Dullah ambae alikuwa kakasilika mno kwa vile alivyodhalilishwa kwa kufungwa kama kichaa wakati ni mtu na akili zake.
"Haya nambieni dadaangu kipi kimemkutaa?"
aliuliza kwa uchungu Dullah mara baada ya kusikia kauli za watu muda mbao alikuwa kafungwa kamba, wakihadithiana kuhusu aliyokuwa ameyafanya dadaake kipenzi Ilham pindi uchizi wa ghafra ulipomvaa.
Makatapila kama kawaida yake akiongozwa na msinga wake uliofungwa shanga nyingi nyingi sehemu za mpini. aliongozwa alipowekwa Ilham ambapo alipoingia tu aligundua kitu kichwani mwa Ilham na kuanza kufanya mambo yake ya kutibu kimazingara ili amsaidie bint yule.

Wakati huo Dullah akili na mawazo yote juu ya Asu yalimtoka na kubaki na taharuki kubwa ukijumlisha maumivu mazito aliyokuwa anayapata muda ule huku akijiona kama yuko ndotoni pindi alipokua anasikia dadaake akiunguruma huko chumbani wakati mganga Makatapila akifanya yake.
"Haa! haa! haaa!!! huu ni uchawi wa hali ya juu sana aliofanyiwa huyu bint haaa !! huu si uchawi wa pwani ya afrika mashariki wala bara."
alishangaa na kuongea maneno yale mganga Makatapila mara alipojiona kuwa hana uwezo wa kupambana na uchawi uliowekwa kwenye kichwa cha yule bint Ilham.
"Mjumbee tafadhali mwambie mganga amsaidie dadaangu?"
aliomba Dullah akiwa nje mara baada ya kusikia kauli ya Makatapila kwa ndani.
"hahahahaaa. Huu ni uchawi wa mbali sana. Huu ni uchawi wa Mawingu hahahahaaa .. Amegongwa kwa mawingu ya kichawi hahahaaa ni mawingu ya kichawi yamesafiri kutoka mbali sana, huu ujanja wa kutegua haya mawingu mimi sinaaaaa"
Kauli hii ya mzee Makatapila ilimfanya hata Dullah akose nguvu na kukaa chini pale nje huku akilia kwa uchungu mkubwa.


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 39

"Eeee Mungu huhuuuu Aaaaagh!!! Kwaninii imekuwa hiviiii..!! Eee Mungu babaaaa kwaniniiii"
alisikika Dullah akilia kwa sauti na mara alinyamaza ghafra na kuingia mule ndani alipokuwa mganga Makatapila.
"Mganga, sitaki kuamini kama wewe umeshindwa kuwa ndio basi tena dadaangu hawezi kupona. Naomba unielekeze kama una rafikiako mganga mwenzio unayemtambua ambae amekuzidi uwezo nimpeleke dadaangu akatibiwe."
aliongea Dullah akiwa serious kabisa mara baada ya kuingia ghafra mule ndani na kuwastua hadi baadhi ya waliokuwa na mganga Makatapila mule ndani.
"hahaha Dullah Dullah mjukuu wa Kombo, usijifanyie hasira wakati wewe ndie msababishaji wa haya."
aliongea Makatapila huku akinusa msinga wake pindi alipokuwa amemuekea kichwani Ilham ambae alikuwa katulia huku kashikwa na watu akiwaangalia kama zimo vile kumbe hakuna hata moja analolielewa wala kujua kinachotendeka pale.
Kauli ya mganga Makatapila kuwa Dullah ndie msababishaji wa matatizo yaliyompata dadake, ilimchoma na kumstua sana Dullah na kumuuliza mganga kwa taharuki kubwa.
"Mimi!!? Nimesababisha nini sasa!!?"
"hahaha, Nimeona hapa tatizo umelisababisha wewe Dullah japo si wewe uliyemroga Ilham ila sababu za kurogwa kwake zimetokana na wewe kwanza hahahaha"
maneno ya Makatapila yalizidi kumchanganya Dullah.
"Bao sikuelewi babu.!!"
"Utanielewa tu Dullah ila tuliza akili kwanza ujiulize huyo mchumbaako uliyekuja nae hapa huko mlipotoka mlitokatoka vipi? Basi kama mlitoka kwa shari ndio maana shari na huku limetokea ila mngetoka kwa heri na huku heri ingetokea haahahaa"
maneno ya safari hii sasa yalianza kumuingia Dullah na kugundua kuwa kumbe sababu na kosa kubwa alilolifanya ni kutoroka na Asunta.
Lakini alishangaa pia, kwani mazingira ya kina Asu ni ya kiroho na imani ndivyo alivyokuwa anajua sasa kuhusu uchawi na kuroga umekuja kujaje pale? lakini hilo alilipuuzia kwanza akili na macho yake yalitaka kuona dadaake anakuwa sawa.
"Kuna kitu nimekumbuka Dullah .. Kuna kitu mizimu imenikumbushaaaaaa"
aliongea kwa sauti Makatapila
"Ndio babu nambie nakusikiliza, nipo hapa."
alijibu Dullah na kusogea jilani na pale alipokuwa Makatapila
"Ni hivi... Kuna mganga mmoja rafiki angu wa zamani yeye ni raia wa Kenya ila alikaa sana Kongo naamini ni yeye tu kwa haraka atayeweza kukusaidia. Yupo Mombasa Kenya anaitwa MAKUMBI ni maarufu sana na uzuri yeye anatibu karibu magonjwa yote. Utapokuwa tayari utanambia"
aliongea yule mganga Makatapila na kumfanya Dullaha azidi kusugua kichwa kwa mshtuko baada ya kugundua na kuufikiria umbali wa Kenya na isitoshe hakuwa na akiba yoyote ya pesa ambayo angeitumia.

Alitoka nje baada ya watu wengine kuanza kupungua huku kila mtu akiondoka eneo lile akiwa ameshika tama hata wale wachezaji wenzake wa kijijini aliowaacha kwenye mechi kumbe walikuja kumuona pale na kukuta kile kituko kilichowafanya wasikitike sana na kumpa pole huku akiwa kajiinamia nyuma ya ukuta wa nyumba yao akiwa haamini kile kilichomkuta dadaake mara kuna mtu mwengine alisogea na kumshika bega na pindi alipoinua kichwa kumtazama ni nani, hakuamini kabisa macho yake.
Kidogo moyo uliingia tumaini baada ya kumtazama mtu yule ambae alisaidiwa vizuri na mwanga wa mbaramwezi kuiona kwa ufasaha sura yake ambapo pembeni yake alikuwapo mwenzake mwengine mfupi kidogo ambae hakuwahi kumuona lakini aliamini ni watu wamoja kutokana na tishirt zao walizovaa zilizokuwa na maandishi sawa yaliyosomeka CLOUDS MEDIA.
Hakuelewa haraka haraka wamefikaje pale lakini ilimbidi asimame kusalimiana nao na alijisikia amani asiijue ilipotokea hasa baada ya kupeana mikono kwa mara ya pili na yule mwengine ambae alimkumbuka vizuri tu hasa kutokana na sauti yake ya upekee masikioni mwake, na huyo alikuwa ni MBWIGA WA MBWIGUKE akiwa na dereva wake waliokuja Tanga kwa kazi maalum ya kufatilia matokeo ya live ya kombe lililokuwa limeanzishwa na wao wenyewe Clouds ambalo hadi ile timu ya kina Dullah ilishiriki kwa mara ya kwanza, kombe lililokuwa na jina maarufu kama NDONDO CUP.

* * * *
DAR - TANZANIA
__________________

Majira ya usiku basi iliyokuwa imem beba Asunta iliwasili ubongo ambapo baada ya wasafiri kushuka Asu akiwa anatumiana msg na mamaake nae alishuka na hakuamini mara alipopokewa kijibegi chake na mtu ambae alipomtazama sura alimtambua vizuri kwani alikuwa ni dereva wao wa nyumbani na kumbe alifika pale sambamba na maake Asu mara baada ya kujua ujio wake na wote hawakuamini mama na mwana mara pale walipoonana walikumbatiana kwa nguvu huku Asu akiongea na machozi yakimtoka.
"mamaaaa,haaaaa!! Asante Yesu"
aliongea Asu huku akilia wakati amekumbatiana na mamaake nje ya gari yao pale ubungo na kumfanya mama nae atokwe machozi kwa uchungu akijua kweli mwanae huko alipotoka ameteseka sana.
"Usilie mwanangu Asunta, kikubwa bwana amekufikisha salama basi hayo mengine yote muachie yeye"
aliongea mama Asu na kumshika mkono mwanae kumuongoza kwenye gari yao wakati huo dereva alikuwa anawasubiri wao tu ili safari ya kurudi nyumbani ianze.

Baada ya kufika nyumbani ambapo usiku huo hakukuwa na mwenye lepe la usingizi baina yao Asu na mamaake kutokana na kila mmoja kutaka kujua habari zaidi juu ya alipotoka na maendeleo ya mwenzake, hususan mama Asunta.
"Mh! mwanangu ona ngozi yako ilivyokuwa. aaah! walikuwa kweli umeumia mama enhee na huyo mshenzi aliyekupiga! hajakuumiza kweli tupeleke Difenda ikamfunze adabu?"
"aaah! mama achana nae ni kijisokwe kimoja hivi hata mkononi hakijai, kweli nimeamini kwanini baba anawachukia waislam"
"umeona eeh"
"yaani mama, kwanza muda wote ukiwaona hao mabint wao wanajifunika kama mavanpire juani wanaogopa kuungua yaani duh! harafu wanaume ukiwatazama hasa vile vizee vimekaa kichawi kichawi"
"heheee aaaah! mwanangu Asu usinichekeshe kilazima mama, enhee na huyo bwana aliekutia wazimu nina wasiwasi dawa aliyokurogea imekufa au imepotezwa makali na roho mtakatifu"
aliongea mama Asu, lakini kauli ile ya kumuingizia Dullah kwenye yale maongezi kama iliustua moyo wa Asunta na kujishika tumbo huku akimtazama sana mamaake kwa mshangao kidogo na kujikuta anakuwa mwenye kustuka kama mtu aliyepoteza fahamu au aliyesikia kitu cha matumaini ambacho alishakata tamaa ya kukiona.
Na hii yote ilitokana na mapenzi ya dhati na ya kweli yaliyokuwa moyoni mwake dhidi ya Dullah lakini hakujua kama kulikuwa na kitu cha ziada kilichoingia mwilini mwake ambacho kilikuwa kinayumbisha akili zake na kuwachukia wazazi wa Dullah na hata Dullah mwenyewe japo muda mwengine nguvu ya mapenzi na uchawi uliokuwa mwilini mwake vilikinzana.

_______________

Baada ya mama Asu kuona mwanae kawa kama ameganda kidogo pindi alipomuulizia kuhusu Dullah ikabidi abadilishe mada haraka na kuongea habari nyengine kabla hajamuacha mwanae apumzike mule chumbani huku wakiagana kuwa kutapokucha watazungumza mengi zaidi.

* * * *
NAIROBI - KENYA
________________

Ilikuwa ni asubuhi sana mapema Pastor aliamka na kuwa wa kwanza kukaa sebuleni akiimba na kumsifu Yesu hali iliyowaamsha na wengine hususani baba Askofu na mkewe pamoja na Fredy ambao waliamua kuungana nae kwanza katika kuimba na kusifu japo hawajajua kama ndio desturi moya ya Pastor George au kuna maono kaoneshwa maana hata nyimbo alizokuwa anaimba ziligusa sana kwenye mtima wake kwa jinsi alivyokuwa anasifu mpaka anatokwa machozi.

Baada ya kuimba sana na kusifu ndipo Pastor alipoongoza maombi ya asubuhi kisha kusalimiana baadae na kuwaita wote pale sebuleni kwa lengo la kuwapa habari na kuwajuza kilichopo.
"Jamani baba Askofu, mama Askofu, Fredy na nyinyi wanangu.. Leo nina habari kubwa sana. Habari ambayo hata mimi mwenyewe sijawahi kuiota wala kudhani kama kuna siku yatanitokea haya yaliyonitokea leo, Aaaaaaagh! Uhimidiwe ewe Yehovaaaa."
alianza kwa utulivu kabisa Pastor George maongezi yale aliyoyaitisha yeye mwenyewe na kuwafanya wote wamsikilize kwa umakini.
"baba Askofu, kwanza honera sana bwana amekubariki na nyumba yako leo imekuwa moja ya nyumba za wabarikiwa"
"Asante sana Pastor."
"Usinishukuru mimi bali wakushukuriwa ni yule aliyepaa mbinguni bila mbawa na leo usiku katika nyumba yako hii amenishukia na kuongea nae live kabisa na wala sikuwa kwenye ndoto."
maneno haya ya Pastor George yaliwafanya wataharuki wote na kustuka hasa pale aliposema eti ameshukiwa na yule aliyepaa bila mbawa (Yesu) usiku ule na kuongea nae live pale kwa Askofu Mbukinyo.
"Najua ni vigumu sana kuamini kwa mioyo ya kawaida ila kama utazama zaidi kiroho na imani ya moyo kwa roho mtakatifu, najua hiki nitachoongea hapa hakitakua ajabu sana masikioni mwenu na kwenye akili zenu. Ukweli ni kwamba leo nimetokewa na bwana Yesu mwenyewe na amenielezea kila kitu kuhusu Asunta na Fredy pia amenibariki kwa kunipa nguvu mpya za miujiza mikubwa kabisa kwaajili ya kuponya na kusaidia watu."
aliongea Pastor George maneno ambayo ukweli yalikuwa yanatoka kichwani mwake tu.
Hakukuwa na ukweli wowote kwenye maneno yake lakini aliamua kutunga uongo ili aweze kutumia vizuri pete yake ya kichawi aliyopewa na Chinedu pia kuogopwa na kusikilizwa na kila mtu na kujikuta anazidi kukufuru na kupata dhambi mbele za Mungu kwa ajili ya sifa na maslahi ya kidunia.

Maneno yale tu aliyoongea Pastor George palepale yaliwafanya wote wasiamame na kuanza kuimba nyimbo maalum ya kutukuza na kusifu kwa yule aliyebarikiwa na baada ya hapo walikaa tena kumsikiliza huku safari hii kila mmoja alimuangalia tofauti kidogo na kumuona ni mtu mwenye bahati ya aina yake na mwenye utofauti mkubewa sana na wao.

"Na katika maelezo ya bwana wetu Yesu amenambia kuwa Fredy ndie mwanaume wa kumuoza bint angu na pia roho mtakatifu ameshamuongoza Asunta usiku wa jana toka huko alipokuwa ambapo hapakumfaa kabisa kuishi. Nami katika kuthibitisha hili mbele yenu napiga namba za mke wangu atuambie nini kinaendelea huko kwani naamini kabisa akama Asu hajarudi basi atakuwa anakaribia kurudi na yote yanafanywa ili aweze kuja kuolewa na Fredy kwa baraka za bwana mwenyewe pia ameniwezesha kutibu maradhi sugu zaidi kwa njia ya kushika tu."

Aliwamaliza kabisa akili Pastor kwa uongo wake ulioenda shule ambao wote waliupokea kwa mikono miwili na waliamini zaidi pindi alipopigiwa mama Asu ambae alikuwa anaongea kwa sauti ya uoga awali lakini mwishoe alifunguka na kuthibitisha uwepo wa Ausunta baada ua kurudi jana yake usiku, na hapo sasa Waliamini zaidi na zaidi kuwa Pastor George ni m barikiwa mpya atayepaswa kunyenyekewa zaidi.

* * * *
MUHEZA - TANGA
___________________

"Daaah! Pole sana Rasta kwa yaliyokukuta, kama sikosei wewe si ndie yuleyule Dullah Rasta mshambiliaji muongo muongo wa Tandale fc?"
"Ndio kaka"
"Sasa dah! kumbe tetesi zilienea umekula kitita cha watu na kuikimbia Tandale huku Tusker ukiwaacha kwenye mataa kumbe una matatizo mazito namna hii?"
"Yaani kaka, we acha tu. Kwanza napenda kuwaomba radhi wana Tandale na Tusker fc kwa kilichotokea nilichanganyikiwa kwakweli sikumuaga hata rafiki angu wa karibu."
"Pole sana, na vipi kuhusu bint uliyeoneka umetimka nae mara ya mwisho Tandale?"
"Huyo yupo kwao, ni msichana niliyempenda lakini imeshindikana kuwa nae, wala haikua sababu iliyonifanya nitoroke."
"sawa sawa na je, endapo Tusker wakikuhitaji sasa hivi na kukupatia kiasi cha pesa kwaajili ya matibabu ya dada utakuwa tayari kujiunga nayo?"
"Kwa moyo mmoja kaka Mbwiga niko tayari."
Yalikuwa ni maongezi ya mahojiano baina ya Mbwiga na Dullah ambayo yalikuwa yanarekodiwa na yule mwenzake Mbwiga ambae pia ni dereva wake na hayo yote waliyafanya baada ya mazungumzo marefu ya awali.

Dullah alihadithia ukweli wote na ukichangia vile mganga alivyothibitisha kuwa tatizo limetokana na kwa yule mwanamke aliyekuja nae na kwa kuwa Mbwiga pia alikuwa mtu wa uswahilini aliijua ile michezo na kuamini kuwa ipo. Hivyo alimpa ushuri wa maneno ya kina kabisa Dullah na kumpanga cha kuongea pindi watapowasha voice record yao ambayo ataenda kuitumia kwenye kipindi chao cha michezo Extra pia alimuahidi kuongea na Shafii kwa pamoja wamsaidie ili aweze kujiunga na timu ile ya Kenya ambayo itakuwa rahisi pia kusafiri na dadaake hata kwa gari maalum ili akatibiwe.
"Usijali kabisa mdogo wangu Dullah, haya mambo yapo hasa kwetu wanaume inatupasa tuwe makini sana. Mi nitaenda kulifnyia kazi suala lako ila we baki na msimamo kuwa ulisafiri ghafra kurudi kijijini pasi na kutoa taarifa kutokana na habari ulizozipata za ugonjwa wa ajabu uliomkumba dadaako. Na simu pia waambie ulipoteza usiku huo huo na hadi sasa mshahangaika sana bado dada hajapata nafuu. Usiogope kabisa Clouds sisi ndo tunasikilizwa na watu wengi sana katika vipindi vyetu hususani vya michezo, tutasafisha safisha mambo yataenda sawa.
Ila kikubwa kwanza mdogo angu tengeneza heshima na jina, achana na mawazo kuhusu huyo mwanamke kwani wazazi wake washakuwa chui kwako. Amini nikwaambiayo ona hali ya mama, ona hali ya dada. Simama kiume pambana kwaajili ya maisha yako kwanza pengine chuki na ushirikina wote wa huyo mdingi unachochewa na hali halisi ya wewe mwenyewe."
aliongea Mbwiga na kumpa moyo Dullah huku akimsisitiza cha kufanya juu ya Asunta na kumuahidi watalisimamia suala lake ili ikiwezekana uhamisho wake kwa Tusker uwepo tena akiwa mchezaji huru kabisa ili pesa atazopewa zisaidie kutibu matatizo ya dadaake nchini Kenya kwa huyo mganga maarufu ambae kumbe hata Mbwiga alimjua na kuwataarifu kuwa kwa sasa huyo mganga ajulikanaye kwa jina la MAKUMBI ofisi yake kuu na anapoishi ni NAIROBI na si MOMBASA kama walivyojua awali.



ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 40

WIKI MOJA BAADAE
_________________

Na kweli mara baada ya Mbwiga kuondoka ilimchukua wiki moja tu karibu kila kona ya nchi hasa kwa vijana wapenda michezo walizisikia habari za matatizo ya ajabu yaliyoikumbuka familia ya mchezaji mchanga mwenye kipaji cha aina yake na hata kuweza habari zile kutapakaa zaidi na zaidi hadi katika club ya Tusker fc ya Kenya ambayo walifanya mawasiliano na clouds hususani Mbwiga aliyeongea nao kirefu na kutokana na uwezo wa kipekee aliokuwa nao Mbwiga katika kushawishi na kweli Tusker waliingia kwenye mstari kwa mara ya pili na hapo ndipo Clouds chini ya usimamizi wa Mbwiga wakiwa na muwakilishi mmoja wa Tusker walipofunga safari hadi kijijini kwa kina Dullah na kumaliza nae mazungumzo na katika hali ya kiubinaadam kabisa Tusker walijitolea usafiri wa gari ya moja kwa moja itayoibeba familia nzima ya Dullah mpaka Nairobi Kenya.

Mambo yalikuwa kama hadithi lakini ndio yalivyokuwa hatimae Dullah sambamba na familia yake ambapo hadi wakati huo mdogo wake alikuwa hajitambui kabisa japo alifungwa dawa maalum ya kutuliza ile hali na mganga Makatapila ili asiwape usumbufu kipindi wanasafiri kwenda Kenya.

* * *

Habari ya Asunta kurudi tena Kenya awali alizipokea kwa masikitiko makubwa kwani hakutaka kabisa kuonana na ile familia aliyoijengea hasira baada ya heshima ya muda mrefu.
Lakini kwa maneno ya Pastor George ambae sasa aliheshimika mno na kwa kisingizio cha kutokewa na Yesu ilikuwa ndio silaha iliyomshawishi Asu kukubali kwenda Kenya na hata alipofika baada ya mazungumzo kadha wa kadha alishawishiwa na kukubali kuolewa na Fredy japo alijijua kuwa yeye ni mjamzito tayari.

Lakini ikumbukwe hayo yote yalifanikiwa kiurahisi kutokana na pete aliyokuwa nayo Pastor George ambayo akiwa anaongea kitu huku akiisugua sugua basi lazima na yule anayeongea nae asugulike akili zake zikubaliane na akili zake yeye, na ndivyo hivyo ilivyokuwa kwa Asu hadi kumkubali Fredy ambae awali moyo wake ulikuwa na kinyongo mno na alimuheshimu kama kaka wa uzaliwa nae.

Katika hali ya furaha siku hiyo familia nzima bada ya mama Asunta nae kuwasili Kenya kwa sherehe maalum iliyoandaliwa na Askofu kwaajili ya mwanae kipenzi na wa pekee Fredy, ili kumshukuru Mungu kwa kile alichokiepusha na ndani yake kulikuwa na suprise kubwa ilipangwa kufanyoika siku hiyo na kabla ya sherehe rasmi kuanza mc alitangaza jambo lililoshangaza kwanza umati.
"Jamani mabibi na mabwana katika Kristo na wengineo, karibuni sana katika siku hii ambayo Mungu kuna neema nyengine ya ziada ametuletea, na kabla ya kuwaambia ni Neema ipi hiyo najua kila mtu hapa ana matatizo yake lakini kuna wale ambao wana matatizo sugu.
Basi na kwa kuwa Mungu wetu ni mwingi wa upendo ameamua kumtembelea ndugu yetu na kumpa baraka zake nyingi na kumfanya kuwa mponyaji wetu hasa kwa wale wenye matatizo mazito.
Basi mabibi na bwana napenda kumkaribisha kwenu Pastor George kutoka Tanzania aliyetokewa na Yesu live na sio usingizini. Leo hii anataka kusaidia mkusanyiko wa watu wote hapa."
Basi baada ya mc kunogesha ujio wa Pastor George jukwaani kila mtu alikaa kwa umakini kumtazama na kumsikiliza asemacho na zaidi kushuhudia hiyo miujiza aliyoshushiwa na bwana Yesu.

Na kweli kwa nguvu ya pete yake ya kichawi Pastor alianza kuhubiri kwa mbwembwe na nguvu nyingi na hali iliyoanza kuwashangaza watu na kuamini kweli alikuwa na miujiza mikubwa na baada ya kuanza kuwaangusha watu bila hata kuwashika kama ilivyokuwa kawaida ya mapastor wengi wenye miujiza ya maombezi.
Karibni nusu nzima ya watu waliokuwa ukumbini walianguka na wengine walichanganyikiwa kabisa na kusababisha heshima kupanda kiwango kwa yale aliyokuwa anayaonesha Pastor George.
"Mimi ndie Mtume na Nabii mpya niliyetumwa na Bana kusaidia wananchiiii"
alijinadi Pastor huku akinyoosha kwa mbele ule mkono uliokuwa na kidole kilichovikwa ile pete ambayo bila watu kujua kuwa pindi mkono wa Pastor unaponyooshwa ile pete inatoa nguvu furani kama za mionzi na kwenda kuwaingia watu na kubadilisha akili zao na wale waliokuwa na vichwa vyepesi zaidi basi walidondoka.
Ilimradi tu ilikuwa hatari na maajabu pale ukumbini hadi Pastor alipotulia na kunuia moyoni mwake ile mionzi yote irudi ilipotoka na kweli ilirudi na kila mtu alirudiwa na akili za kawaida huku wakiamini kweli wameponywa na wamesafishwa kwa baraka za Pastor George ambae sasa alikuwa anataka wamwite mtume na Nabii.

Baada ya maombezi ya Pastor George ndipo taratibu za kuwasaidia watu wengine ziliendelea hadi kila kitu kilipokuwa sawa ambapo mc aliwatangazia watu kuhusu ugeni uliokuwa unaingia muda ule wa watu waliokuwa wamevaa suti maalum kuwa ni wachezaji wa club ya Tusker fc waliopewa mualiko maalum.

* * *

Hakuamini masikio yake Roja akiwa mazoezini na Tusker fc kuwa yule mchezaji aliekuwa pacha wake Tandale sasa yuko mbioni kujiunga nao pale.
Hata hivyo Roja ambae sasa alishaanza kuwa mwenyeji pale ilimuwia vigumu kuamini hadi siku ambayo anaonana na Dullah uso kwa uso mara baada ya kufika Nairobi na kupelekwa kwenye makazi alivyoandaliwa na Tusker ndipo alipochukuliwa kwenda kukutana na wenzake mara baada ya kusainishwa kuwa mchezaji mpya wa club ile.
"Siamini kabisa kama leo tumekutana tena pacha wangu."
"Haaaaa!! Rojaaaaa"
Ilikuwa ni furaha kubwa baina yao kuonana tena siku hiyo mara baada ya kutambulishwa na katika club ya Tuske kwa muda huo Roja ndie aliyeonekana mchezaji hodari aliyetokea kupendwa sana na mashabiki kwa muda mfupi mno toka ajiunge na ile club.
"Naamini sasa mzunguko huu wa pili tutawaonesha na kuwafunza adabu wakenya."
aliongea Roja kwa furaha na kutoamini kama ile Road to Kenya leo hii imefanya kazi nzuri na imewanufaisha wote wawili.

Lakini suala alilokuwa nalo Dullah kichwani sasa ni yale maneno ya Mbwiga ambae alimsihi kuwa aoneshe kiwango siku hadi siku ili aweze kujitengenezea heshima na iwe njia rahisi kumuoneha Pastor kuwa pesa zinatafutwa kama kumkataa kwake kisa umasikini na kueka kigezo cha dini.
Alimuhadithia kila kitu kilivyokuwa rafiki yake Roja ambae alisikitishwa mno na habari zile na kama kawaida alichokifanya Roja ni kumpa moyo Dullah.
"D wewe ni Star na mtu hodari na tegemeo kwa Taifa hapo baadae, nakushauri rafiki angu achana na kuumiza kichwa sasa kuhusu yule mwanamke amini usiamini kama unavyosema kuna damu yako tumboni mwake basi kamwe haiwezi kupotea. sasa hivi usimtafute tena ila mfanye akutafute tena lakini zaidi ya yote mke bora ni yule anayetoka kwenye familia bora, mi naamini Asunta mlipendana lakini bado si mke bora."
maneno ya Roja yalimuumiza Dullah lakini aliyamezea hasa kila akikumbuka na maneno ya mamaake pindi alipokuwa analia na kumwambia kuwa asije akathubutu kumtafuta yule mwanamke tena wala kwenda kwao kwa kile kilichotokea.
Alimpenda sana Asu na moyo wake ulisema hivyo kila siku.
Lakini kwa matukio yanayotokea na kauli za watu wanaomthamini kama mamaake kipenzi zilimfanya abaki njia panda.

Siku hiyo club nzima ya Tusker walikuwa na mualiko maalum kutoka kwenye kampuni ambayo ndio walikuwa wadhamini wakuu wa ile club nao si Wengine ni MBUKINYO INTERPRICES wauzaji na watengenezaji wa Ving'amuzi maarufu sana nchini Kenya.
Ilikuwa ni sherehe maalum ya meneja wao ambapo siku hiyo wachezaji na viongozi wote walinunuliwa Suti maalum kama sare yao special kwenye hiyo sherehe.
Dullah nae alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliohudhulia sambamba na rafiki ake kipendzi Roja.
Na mara walipofika pale ukumbini muda wa jioni walishangaa kukuta kila mtu anahadithia juu ya mchungaji wa kitanzani ambae sasa kawa mtume na nabii baada ya kutokewa na Yesu, na alilithibitisha hilo muda mfupi uliopita kwa maombezi yake ya ajabu.
Basi kipindi sherehe inaendelea ndipo meneja wao alipoingia rasmi ukumbini sambamba na wapambe wake na kila mtu aligeuza macho kumtazama kipindi anapita.
"Yupi sasa ndio yule nini?"
aliuliza Dullah kwa Roja na kuoneshwa meneja mwenyewe ambae hakuwa mwengine bali ni Fredy.

"Mabibi na mabwana kabla mambo mengine kuendelea napenda kuwaletea jambo na habari kubwa inayoenda kutokea sasa ambayo iliekwa kwenye mabano haikutangazwa ili iwe suprise kwenu.
Ni hiviiiiii kwa mara ya kwanza Meneja wetu muheshimiwa Fredy anamtambulisha rasmi mkewe mtarajiwa na leo hii atamvisha pete ya uchumba hapahapa mbele ya mcho yenu wote mliohushuliaaaaaa... Napenda kuwakaribisha bwana Fredy Mbukinyoooo na bibi Asuntaaaa Georgeeee"
Maneno ya MC na kile alichokiona Dullah pale mbele kilimfanya adondoshe hadi glasi ya Juice aliyoishika pasi na kutambua na hakuamini kabisa aliona kuwa lile tukio linalotokea pale labda ni ndoto anayoiota wakiwa safarini kuja Kenya kwa mara ya kwanza.

__________________

"Naam vizuri kabisaaaa, huyo ndie Mh Fredy sambamba na ua la moyo wake, mtoto wa mchungaji aliyebarikiwa na kupewa unabii na bwana wetu Yesu Kristo, leo hii pia Mungu amewakutanisha watu hawa wataokuja kuungana na kuwa mke na mume rasmi siku si nyingi, narudia tena anaitwa Asunta George. hahahaaa Waliopatanishwa na Mungu hakuna wa Kuwapotoshaaaaaa.. Jamani wamependeza hawajapendezaaaaaa?.."
"WAMEPENDEZAAAAAAA"

Maneno ya Mc sambamba na kelel za watu pale ukumbini waliokuwa wakiripuka kwa shangwe na furaha tele yalizidi kuchanganya akili ya Dullah na kubaki kaganda kama mtu aliyekaushwa kwa shoti ya umeme akiwa hayaamini macho na masikio yake.
"Usipanick kaka, usipaniki kabisaaa D achana na hayo mambo."
alikuwa ni Roja akimsihi Dullah kwa sauti ya chini mara tu nae alipomuona Asunta na kustushwa na mlio wa mvunjiko wa glasi ambao wengi hawakuusikia kutokana na kelele zilizokuwepo na kutokuwa karibu na Dullah.

Alishangaa hadi machozi kuanza kumtoka Dullah na hapo ndipo Roja alipomsihi wainamishe vichwa pale kwenye kiti walipokaa wawe kama watu waliokwa wakijadili jambo la kina ili wengine wasiweze kugundua kama Dullah alikuwa analia.
"Wewe ni mwanaume, tambua maana ya mwanaume Dullah, Mwanaume hatakiwi kumlilia mwanamke ila mwanamke ndie anayetakiwa kumlilia mwanaume. Alichokuzidi Fredy nadhani unakiona... kwanza ana pesa chafu, pili wazazi wake nao matajiri na ndio sababu hata mzee aliyekukazia wewe huku amerainika kabisaaa, kikubwa kuwa na hasira ya maisha na kama vile ulivyomuahidi mama siku unaondoka kule kijijini kuja Dar sasa unatakiwa kumuonesha mama ulichokuwa unakitafuta. Mungu amekufanya umezaliwa kwenye familia masikini lakini hekma yake ndani yake amekuekea kipaji hadimu ambacho wengi wanakitamani sana lakini amekupa wewe ili uweze kuyaongoza maisha yako na kusaidia ndugu zako hadi leo hii kumbuka umefika hapa Tusker kwaajili ya soka na kupata pesa za kumtibu dada, na huyo mtu anayekuchanganya sasa kumbuka ndie sababu ya matatizo ya dada na mengineyo... Tuliza kichwa D usije kuibua mazito tusiyoyajua>"
Maneno ya Roja yalimfanya Dullah ajikaze kiume na kuacha kulia kabla hajainua tena kichwa chake kuendelea kuangalia kile kilichokuwa kinaendelea jukwaani.

Na kweli aliwashuhudia watu wale wawili wakiwa na nyuso zenye furaha wakivishana pete ya uchumba kabla ya kubarikiwa kwa sala maalum kutoka kwa Pastor George mwenyewe ambae sasa alikuwa anajiona yeye kama Nabii au Mtume.
Kwa wengi ilikuwa furaha lakini kwa Dullah yalikuwa ni maumivu makali sana.
("Mpira wewe ndie mwanamke wangu wa ukweli, nitakupenda daima ili tuzidi kuliwazana uwanjani.")
aliapia ndani ya nafsi yake Dullah na palepale ule moyo wa upendo uliopitiliza juu ya Asunta ulianza kuingia doa la chuki lililoanza kuuchafua taratibu upendo wake juu ya Asu.


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 41



* * * *
SIKU TATU BAADAE
__________________

Walionekana Dullah, mamaake sambamba na Roja wakiwa ndani ya jengo moja la tiba asilia ambalo lilikuwa linamilikiwa na mganga maarufu sana Kenya aliyeitwa Makumbi.
Walikuwa wamekaa wakisubiria majibu mara baada ya kumfikisha Ilham siku hiyo na kutakiwa kumuacha kwenye chumba kimoja maalum cha mizimu kisha wao kuelekezwa kusubiri pale kwenye jengo lile kulipokuwa na mabench mengi huku kukionekana wateja mbali mbali wakiingi na kutoka pia wahudumu wa mganga Makumbi walikuwa shapu kuwahudumia watja na kuwakabidhi namba maalum zilizokuwa zinaitwa kwa zamu kwa wale walioleta wagonjwa ambapo kulikuwa na nyumba nyengine ilitengenezwa kama wodi kabisa iliyokuwa na vigodoro na kadhalika.
Mganga Makumbi alikuwa tofauti sana na waganga wengi kwa jinsi alivyojitengenezea mazingira yake ya utabibu na aliaminika sana kuwa ni mganga hodari mno.

Mara baada ya kusubiri sana hatimae zamu yao iliwadia na waliitwa kisha kutakiwa mmoja wao aingie kwenye kile chumba akazungumze na mganga Makumbi na hapo ndipo Dullah alipoteuliwa na mamaake kisha nae bila kusita wala kupinga aliingia kukutana na Makumbi ili apate kujua kulikono, na kuhusu hatma ya dadaake kipenzi.
Mara baada ya kuingia ndani na kukutana na Makumbi ambae alisifika pia kwa kupenda vitendo kuliko maneno na hilo lilijidhihirisha pindi Dulla alipoingia alishangaa kuona Makumbi ametengeneza moshi wa ajabu uliokuwa unaonekana kichwani mwa Ilham ambapo ule moshi ulijitengeneza kama tv na hapo ukaanza kuonesha matukio yalivyokuwa kuanzia kule Nigeria hadi pale nyumbni kwao Tanga na aliona kijiwingu cha moshi kilichofungamana kama kirungu kikienda kumgonga Ilham pindi alipokuwa anataka kumpiga Asunta baada ya kuongea maneno ya uchonganishi kwa njia ya simu na mamaake.
"Umeona tatizoooo? Umeonaaa kijanaaa.. Hili ni tatizo dogo sana na ni lamuda mfupi kulitengeneza kijanaaaa hahaha lakiniii!!! ni gumu sana kuliondoa na linachukua muda mrefu kidogo"
aliongea mganga mara baada ya ile luninga ya kimaajabu kuzima na kumfanya Dullah abaki ameshika tama akiwa haamini amini kile anachokiona na kupata hasira mno dhidi ya Pastor George.
("Huyu mshenzi anaongopa mbele ya umati eti katokewa na Yesu wakati kumbe ni mchawi kiasi hiki?")
aliwaza na kuongea ndani kwa ndani ya moyo wake Dullah na kumgeukia mganga kumuuliza.
"Lakini ndugu Mganga si una uwezo wa kumsaidia dadaangu na kumtibu arudi kama awali.?"
"Haswaaa, ila tiba yake hadi akae sawa kabisa kabisa ni miezi sita na atatakiwa kulala hapahapa mpaka matibabu yatakapomalizika."
"Hilo halina shidaa.. Halina shida kabisaaaa. Nakuomba sana mganga msaidie dadaangu apate kupona mapema... aaaaagh"
aliongea Dullah na ilitakiwa alipe Ksh 500 kwa kila mwezi kwaajili ya malipo ya kulala pale kwenye wodi maalum na malipo kwa niaba ya mganga Mkumbi yalikuwa ni baada ya tiba.

Baada ya kumalizana na mganga Dullah alitoka huku akiwa kidogo na matumaini mapya moyoni mwake juu ya dadaake na aliwajuza kila kitu mamaake na rafikiake kipenzi na wa ukweli Roja.

* * * * *
WIKI MBILI BAADAE
____________________

Mzunguko wa ligi kuu Kenya uliendelea huku ikiwa ndio mechi ya kwanza kwa Dullah na uwanja wa Tusker ulifurika vya kutosha siku hiyo kwa lengo la kuja kuuona huo uwezo wa mchezaji ambae almanusura kuatia hasara kubwa timu yao baada ya usaili wake wa awali kuwa na zongo.

"D, unatakiwa leo leo uwaoneshe hawa wakenya wewe ni nani naamini watapokukubali, utayaona matunda makubwa sana kwani hawa ni zaidi ya mashabiki wa Tandale."
Yalikuwa ni maneno ya Roja pindi walipokuwa wanajiandaa kuingia uwanjani na jina la Dullah liliekwa kwenye majina ya wachezaji wa akiba siku hiyo.
"Sitokuangusha Roja, Sitowaangusha mashabiki, wala sitojiangusha mwenyewe... Najisikia kucheza mpira sasa kuliko nyakati zote."
alijibu Dullah na kumfurahisha Roja.

Mechi ilianza hadi kipindi cha kwanza kinaisha tayari Tusker walikuwa nyuma kwa gori moja.
Kipindi cha pili mpira ulikuwa na kasi pande zote mbilina hadi inafika dakika ya sabini bado matokeo yalikuwa Tusker wako nyuma kwa gori moja na ndipo hapo Dullah alipoambiwa avae jezi na kila shabiki aliyekuwa uwanjani walianza kumnyooshea kidole kuambizana kuwa yule mtu aliyewasumbua katika usajili ndie yule Rasta anayeingia muda ule.

ITAENDELEA


MTOTO WA PASTOR (51)
BY - MTOTO WA BECKER (The Special Thinker)
________________________
________________

("Nimerudi tena kwenye kitanda chetu mpenzi wangu mpira, naomba tuliwazane pamoja katika kitanda hiki kinachotazamwa na watu wengi pindi tunapokuwa tunaliwazana.. Naomba usinibanie kaa na mimi tuushangaze umati na kuudhihilishia kiasi gani Tunapendana")
aliongea moyoni mwake Dullah pindi alipokuwa aningia uwanjani huku akimaanisha kuwa kile anachoongea kinasikiwa vizuri na anayeongea nae ambae hakuwa mtu bali ni mpira ule alioingia ili kuucheza.

Kwa mazingira ambayo wengi hawakuyatarajia baada ya Dullah kuingia tu mpira wa kwanza kuugusa aliupasia moja kwa moja wavuni na kuufanya uwanja mzima ubaki kimya wakiwa hawaelewi au kama hakijatokea kitu pindi Dullah alipoisawazishia Tusker kwa shuti kali alilopiga zaidi ya mita 25 kuunganisha mpira ambao ulionekana kupoteza muelekeo na kumuacha kipa wa timu pinzani akiwa nae haamini kilichotokea pindi aliposhuhudia nyavu zake zikitingishwa vibaya na mpira uliokuwa unacheza cheza na kuzunguka wavuni.
Watu wengi walichukulia ile ilikuwa ni nguvu ya soda tu aliyoanza nayo rasta yule na ndio sababu japo gori liliwakuna lakini ule moyo wa hasira dhidi ya Dullah bado ulikuwa haujalainika kwa mashabiki wa Tusker lakini kama hiyo haitoshi dakika tano badae Dullah aliwaonesha kitu chengine cha ziada baada ya kupokea pasi kwenye mazingira magumu lakini aliweza kuudhibiti mpira na kuwadanganya mabeki wa timu pinzani hatimae aliweza kuachia kombola kali lililoenda kugonga besela na kuufanya umati mzima hususani mashabiki wa Tusker kunyanyuka na kushika vichwa vyao kabla ya dakika tatu baadae Dullah huyo huyo kuuzamisha tena mpira wavuni baada ya kupokea pasi maridadi kutoka kwa Roja na hapo alimtoka mpaka goli kipa na kufunga kiulaini kabisa.
Hapo sasa watu walijikuta wakilipuka shangwe na kumuangalia kiupendo vile vitu alivyokuwa nafanya mara baada ya kuhitimisha kalamu ya mabao dakika tatu kabla mpira kuisha pindi ilipopigwa kona nae kujitwisha mpira ule kwa kichwa kilichopigwa kiufundi kwa jinsi alivyouhamishia kwenye kona kabisa ya goli.

Na huyo ndie Dullah mchezaji mpya wa Tusker fc aliyekuja kupewa tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa msimu huo na chama cha mpira wa miguu cha Kenya richa ya kwamba aliukutia msimu kati lakini uhodari wake uwanjani ulimuwezesha kuwa namba mbili katika ufungaji wa msimu huo na kuisaidia Tusker kushiriki ligi ya mabingwa Afrika mara baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Kenya ambao hakukuwa na shabiki wala kiongozi yeyote wa Tusker aliyeota kuwa wangeweza kufanya maajabu yale msimu huo mara baada ya kuboronga kupita maelezo msimu ulioisha.
Nani ambae hakutaka kumjua mchezaji mpya wa Tusker?
Nani ambae aliacha kusimulia maajabu ya mchezaji yule wa Tusker pindi awapo na mpira?
Nani ambae hakutamani kukaa nae jirani na kujua siri ya mafanikio yake uwanjani?
Nani ambae hakukiri kuwa namba tisa na kumi ambayo walicheza Dullah na Roja ndio ilikuwa safu hatari zaidi ya ushambuliaji msimu huo?
Yaani kwa muda wa miezi minne tu aliyokaa Kenya ilitosha kabisa kubadilisha historia ya Dullah kutoka bwege wa mapenzi kwa Asu mpaka kufikia kuwa bwege wa mapenzi kwa mpira, na ubwege wa mapenzi kwa mpira ndio uliokuja kumuinua na kuzidi kumuonesha yeye ni zaidi ya mchezaji japo mwenyewe alikuwa anacheza kama kuliwazika na kuyatoa mawazo mengine yooote kuhusu mapenzi hususani kwa Penzi la Mtoto wa Pastor.

Ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa lilikuwa si jambo dogo na Kampuni ya Mbukinyo ambao ndio walikuwa wadhamini wa Tusker walituma zawadi maalum kwa wachezaji wao zilizotoka kwa meneja wa Mbukinyo ambae tetesi zilisemekana kuwa alihamia uingereza miezi mitatu iliyopita na huko ndipo alipofunga ndoa na bint wa mchungaji ambae alikuwa anakuja juu kupita maelezo huko Tanzania na nchi jilani huku akijinadi unabii aliotawazwa na bwana Yesu mwenyewe aliyemtokea miezi michache iliyopita.
Zawadi hizo ambazo zilikuwa ni pesa zaidi ya laki moja za Kenya kwa kila mchezaji mmoja na kwa upande wa Dullah zilizidi kumueka pazuri hata kumuhudumia zaidi dadaake ambae alikuwa bado anapatiwa matibabu kule kwa mganga Makumbi.

* * * *
LONDON - UINGEREZA
_____________________

Mimba changa aliyokuwa nayo Asu ndio ilikuwa sababu kuu iliyowafanya wahamie London na kufunga ndoa katika kanisa kuu la Anglikana, ndoa ambayo ilihudhuliwa na watu kadhaa hususani wale waliokuwa karibu sana nao kifamilia.
Zaidi ya Fredy hakukuwa na mtu mwengine aliyebaini kuwa Asu ni mjamzito kipindi ndoa ile inafungwa kutokana na siri iliyokuwepo juu ya ujauzito ule ambao Fredy hakujua ni wanani lakini alijua si wake na kwa kuwa alimpenda sana Asu hakuona tatizo juu ya hilo alikubali kwa moyo mmoja kujifanya mtoto ataezaliwa ni wa kwake japo mimba ilimtangulia kwa miezi miwili.
udogo wa tumbo la Asu ilikuwa ni sababu nyengine iliyozidi kuwapofua watu wengi wasijue hata mamaake mzazi na babaake hakuwaambia sual lile lakini hadi wanafunga ndoa tayari Asu alikuwa na mimba ya miezi mitatu.

Waliishi London karibu na mtaa wa Fulham ambapo walikuwa pia jilani na uwanja wa Stamford bridge uliokuwa unamilikiwa club maarufu ya Chelsea na hiyo ikawa sababu ya kila mwisho wa wiki waelekee uwanjani pale kuangalia mehi mbalimbali za Chelsea na kujikuta Asu akitamani kuwa mwanachama kabisa wa ile timu kutokana na moyo wake kupenda sana mpira kupita kawaida kadri ile mimba ilivyozidi kukua.
Hata Fredy nae alipenda michezo hususani ule wa mpira wa miguu na ndio sababu mapenzi ya Fredy na mpira ilikuwa ndio sababu hata alimshawishi babaake waidhamini Tusker msimu ule ilipoonekana kuyumba sana kiuchumi na habari za ubingwa wa kushangaza kutoka kwa Tusker ziliustua mno moyo wa Fredy kipindi hiko ambapo mimba ya Asunta ilikuwa tayari inakwendea mwezi wa sita na ikawa sababu tosha ya Fredy kutosafiri kwenda Kenya zaidi ya kuwatumia zawadi za aina yake wachezaji na viongozi wa Tusker fc huku yeye alipoamua kufatilia sherehe za ubingwa na kila kitu kupitia compyuta ambapo katika mtandao wa Supersport alizungumziwa sana mchezaji bora chipukizi wa ile ligi raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 23 aliyitwa Dullah Kombo mara baada ya kuwa mfungaji bora namba mbili pia wa msimu mbali ya kuwa alihamia nusu ya msimu.
Habari zile zilimfurahisha sana Fredy na kwa kuwa hata mkewe mimba yake ilikuwa inamperekesha sana kwenye mpira... aliona ni vyema waangalie pamoja hilight za msimu zilizorekodiwa na Supersport kwenye ile ligi hasa vile vipande vya huyo mchezaji mpya wa Tusker ambae wakenya walimpachika jina la African Messi.
Lakini mara Asunta alipoziona picha tu za mchezaji mwenyewe alijikuta mapigo ya moyo yakibadili kasi na macho yake kutoamini kile akionacho hadi Fredy alishangaa kutokana na ustaajabu wa hali ya juu aliokuwa anauonesha Asu mbele yake.
"Asu mke wangu, vipi?!"
aliuliza Fredy kwa mshangao mara baada ya kumtazama Asu aliyekuwa amebadilika aina ya uhemaji mara baada ya kutokea picha za Dullah na kunasa machoni mwake kupitia Compyuta.


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 42


"Asu mbona hivyo?!"
Aliuliza kwa mshangao zaidi Fredy mara baada ya kuona Asu akiwa kaganda vile vile bila kusema kitu.
"Aaaaah! najisikia vibaya Fredy mume wanguu aaagg"
aliugulia Asu hali iliyomfanya Fredy akurupuke haraka na kumpigia simu daktari wao aliyekuwa anakuja mara kwa mara kuangalia hali ya maendeleo ya mkewe.
["wahi sasa hivi tafadhali"]
aliongea kwa msisitizo Fredy pindi simu ilipopokelewa upande wa pili na kurudi alipokuwa amesimama Asu huku akiwa kajishika tumboni akitaka kuchuchumaa ambapo Fredy alimuwahi na kumlaza kwenye sofa huku akiwa na wasiwasi.
"Asunta mke wangu unajisikiaje kwani?"
"Tumbo tu mume wanguu aaaaggg"
alizidi kuugulia Asu na kumtisha Fredy asijue afanye nini ili kuyazuia maumivu ya tumbo yaliyomkumba mkewe ghafra namna ile.
Aliona yule daktari anachelewa sana na alianza kufikiria kutoka nae ampeleke mwenyewe hospitali huku akiwa kajisahau kabisa kama hazijapita hata dakika tatu toka aongee na huyo Daktari wao ambae alikuwa jengo lilelile walilokuwa wanaishi wao tofauti yeye na Asu walichukua vyumba gorofa ya nane na yule daktari alikuwa anaishi ghorofa ya arobaini.

Ukweli ni kwamba Asunta pindi alipoiona picha ya Dullah mtoto aliekuwa tumboni aliruka mno na kumuumiza tumbo hali iliyomfanya azidi kuishangaa ile picha pamoja na ile hali iliyomtokea na ndipo hapo maumivu ya tumbo yalipoanza na kweli yalikuwa makali lakini hofu na mshangao wa Asu ndio uliochochea kuhisi maumivu makali zaidi.
Wakati uleule kengere ya mlangoni ilisikika na Fredy alienda kufungua mlango haraka na ndipo alipoingia yule Daktari akiwa na begi dogo lililokuwa na vifaa vyake vya kazi na moja kwa moja alianza kazi ya kumkagua Asu kwa umakini mkubwa na kugundua kuwa hakuwa na tatizo lolote zaidi ya mtoto kucheza sana ambapo ilionesha mama kuna kitu kilimstua au kumtisha.
Fredy hakutaka kufikiri sana wala kuchunguza kitu gani kilimstua au kumtisha mkewe na halikumjia wazo hata chembe kuwa labda zile picha walizokuwa wanaangalia ndio sababu, zaidi yeye alipuuzia na alichokiomba kwa Mungu mkewe abaki salama na ajifungue salama kabisa usalimini.

* * * * *
DAR ES SALAAM - TANZANIA
_______________________

''
" ........... Yeeeeyee Ndieee Mwenye kutoa Mamlakaaaa na humpa yuuuulee aliyem'bariki... Hana mpinzaaaniiiii chinii katika Jua mpaka juu mawinguniiiiii. Namwita Yehovaaa leo hiiiii hapa hapaaa kwa barakaaaa alizonipaa amini wewee mwenye Magonjwa sugu kama Ukoma, Ukimwi, Kisukari, Ebola na yooote yaliyokosa majina amini leo sasaaa ukombozi umekufikiaaaa.... Kikubwaaa hutakiwi kuwa Bahiri kumtolea Bwanaaa.. Kwani bwana anasema ukijinyima na kutoa kitu kikubwa chenye thamani kwako kwaajili yangu kupitia kwa mtumishi wangu niliyemchaguaaaaa baaasiii na mimi nitakulipa kubwa zaidi ya hilo kwani utakuwa umenionyesha upendo kama nilivyowaonesha kwa kumtoa mwanangu kipenzi na wa pekee kwenu... Halleluyaaaaaajee hampendi kwenda kukutana na Bwana wetu Yesu Kristo?.... Basi kama hupendi na una urafiki na Shetani pia unafurahishwa na matatizo yanayokuandama, basi nakuomba usinyanyuke hapo ulipo kuja kutoa sadaka kwaajili ya Mungu ila wana wa Mungu wenye mioyo ya kujinyima na kujitolea Nawakaribisha sana hapo mbele kwenye vikapu vya sadaakaaaaa....."
''
Alikuwa ni Pastor George ambae sasa alikuwa anajiita mtume na nabii pindi alipokuwa anafanya yake katika ukumbi wa Dimond Jubelee ambao ulikuwa umefurika kupita kawaida kila mtu akisafiri ili apate kuombewa na huyo nabii mpya aliyetokewa na Yesu na kupewa miujiza ya ajabu.

Watu wengi walimuamini mno George siku hadi siku na anapokuwa kwenye ibada ya maombezi popote pale unapofika muda wa sadaka aliweza kuwavuta watu karibia wote waliofika kwenye maombezi siku hiyo na kutoa pesa walizoziandaa ama walizokuwa na bajeti nazo nyengine lakini walijikuta imani inawaingia na kwenda kuziweka kwenye makapo makubwa 12 ambayo ndio hutembeza kwenye maombi yake Pastor akinadi kuwa kila kapu moja ni kwa niaba ya mwanafunzi mmoja wa Yesu na mbele anaposimama hueka Bluefcase ambayo muda wote hukaa wazi akimaanisha ile bluefcase ndiyo kwa niaba ya Yesu mwenyewe hivyo wengi walikuwa wanapitakwenye makapu na kudondosha elfu tano elfu kumi lakini wanapofika pale kwenye Bluefcase yenye nembo ya msalanba na picha ya Yesu hujikuta wanatumbukiza karibu pesa zote walizojaliwa kuja nazo siku hiyo huku wengine walijikuta wakiacha hadi funguo za magari yao sambamba na kadi ili tu kuonesha jinsi gani wapo tayari kukitoa kitu kikubwa na cha thamani kwao kwaajili ya Mungu kupitia mtumishia aliyemchagua mwenyewe na kumtakasa mbele zao kwa kumpa miujiza.

Na hivyo ndivyo George alivyozidi kujikusanyia utajiri ambapo kila wiki kupitia pesa ya sadaka aliingiza zaidi ya milioni 50 kutoka kwa waumini mbalimbali na kuzidi kuonekana tishio huku akizidisha uaminifu kwa mganga wake wa Nigeria kwa kumfanyia suprise kibao ili nae azidi kumuongezea nyota ambayo nguvu zake zote zilipita kichawi kupitia pete ya kijini aliyopewa na Chinedu.

* * * *
NAIROBI - KENYA
________________

Matunda yalianza kuonekana kwa Dullah na Roja mara baada ya sherehe za ubingwa kumalizika alijitokeza mdau wa Tusker fc aliyekuwa anaishi Afrika ya kusini na kujitolea gari mbili za kutembelea moja ikiwa kwa niaba ya Dullah na nyengine kwa niaba ya Roja huku wachezaji wengine wakiambulia pesa tasilimu na kupewa motisha kuwa kama watazidisha juhudi basi masimu ujao na wengine apia wanaweza kuzawadiwa vitu vikubwa kama hivyo.

Lilikuwa ni jambo ambalo awali hakuwahi kulitarajia Dullah kama mpira ungeweza kumfikisha pale na kumletea heshima ile ambayo alikuwa anaona haistahili kwake pindi alivyokuwa anapendwa na kunyenyekewa na wakenya hususani uongozi wa Tusker fc.
"hizi ni rasha rasha D mvua bado zinakuja mwanangu tupige kazi."
yalikuwa ni maneno ya Roja siku hiyo alipokuwa anamfundisha gari Dullah ili afanikiwe kupata leseni ya uendeshaji kwani Dullah ukweli alikuwa ahajui lolote kuhusu gari.
Maisha sasa yalikuwa mazuri hata mamaake alianza kunawili mara baada ya Tusker kujitolea na kumpangia nyumba nyengine yenye hadhi zaidi Dullah na familia yake na hata kwa Roja pia alifanyiwa hivyo na kama kawaida yao umoja wao ulizidi kukomaa ndani na nje ya uwanja.
"sasa ushaanza kuwa dereva mzuri sana, huu ndio wakati wa kukata leseni sasa. Itapendeza sana siku moja unarudi Tanga ukiwa na usafiri wako mkali kama huu"
aliongea Roja mara baada ya siku kadhaa kupita toka aanze kumfunza gari Dullah ambae sasa alionesha kuwa na wezo nalo wa kuliendeesha vizuri.
"hahahahaaaa Roja, yaani hapa ndio kama vile wamemwagia petroli kwenye moto mkubwa, naitamani hiyo ligi ya mabingwa nikakutane na hao makipa wa mabingaaaaa...."
aliongea Dullah na wote kucheka kwa furaha.

Hali ya Ilham ilizidi kutengemaa kule kwa mganga Makumbi na sasa akili zake za utambuzi zilianza kurudi pindi hata kina Dullah walipoenda kumtembelea na kumuangalia aliwatambua na alimpenda sana Fredy ambae alikuwa haishi kumpigisha story za vichekesho na kumfanya ubongo wake ku relax bila kufuga mawazo mengi ya kujiuliza kulikoni ambayo yangemuumiza kichwa na kumfanya achelewe zaidi kupona.

Hata mamaake Dullah alitokea kumpenda sana Roja siku baada ya siku kwa tabia zake na vile alivyo pia.
("Eee, Mungu saidia huyu kijana aje kuwa mkwe wangu, dah! mwanangu Ilham kama akipona harafu akapata mwanaume wa kumuoa kama Roja atakuwa amepata bahati kubwa sana.")
yalikuwa ni mawazo ya kila siku yaliyokuwa kichwani mwa mama Dullah pindi alipomuona Roja na mara nyingi katika maombi yake aliombea sana jambo hilo lakini hakujua nini afanye na alijua si rahisi kwa dunia ya sasa kumshawishi mtoto kuolewa au kuoa kwa mtu ambae unampenda wewe bila kujua wala kuchunguza kama moyo wa mwanao na wa mtu unayetaka awe nae umeridhia? je wao wenyewe waliwahi kutamkiana maneno hayo ya kuishi? je hakuwezi kuja kutokea uhasama baadae baina yao na kuishi pasi na amani?
Maswali haya ndio yalimfanya mama Dullah kubaki na lake moyoni na kushindwa kumgusia yeyote kati yao juu ya kile alichokuwa anachokifikiria na hatimae siku zilienda na baada ya miezi sita kama alivyosema mganga Makumbi, Ilham alipona kabisa na kuwa kama zamani na siku alipokuwa anatolewa kule kwa mganga alishangaa mno kuona wanaingia kwenye gari nzuri aina ya prado ambayo alikuwa hajawahi kupanda toka kuzaliwa kwake na alichoshanaa zaidi kuona kakaake Dullah ndie aliyekuwa dereva wa gari ile na kuona kama ndoto mara alipouliza na kuambiwa ile ilikuwa ni gari ya kakaake na zaidi ya yote walipofika kwenye nyumba waliyopangiwa na ile club ya Tusker alijikuta Ilham akiwa haamini kama ni mpira pekee ndio uliowabadirisha na kuingia kwenye maisha yale ambapo leo hii wanaingia kwenye nyumba nzuri tena wakiwa na gari ya kwao kabisa!?!!

* * * *
LONDON - UINGEREZA
___________________

Tokea siku Asunta alipoiona picha ya Dullah kupitia compyuta alipokuwa na mumewe Fredy aliyemwita kumuonesha wachezaji wa timu yao waliobeba ubingwa hususani Messi wa Afrika ambae ndie alikuwa Dullah wake, moyo ulianza kumuuma taratibu na kumkumbuka Dullah siku hadi siku japo alikuwa hana la kufanya lakini kuna muda alipomtazama Fredy alijikuta anajiuliza moyoni kuwa alikubalikubali vipi kumsariti mtu aliyempenda kweli ambae ni Dullah na kukubali kuolewa na Fredy..!!?
("Mh! mbona hii ndoa imekuwa kama ya muujiza...! yaani mimi leo nimekuwa mke wa Fredy? He!")
alijiuliza Asunta siku moja majira ya usiku akiwa kalala na Fredy mara baada ya kuota ndoto akifanya madude (mapenzi) ya nguvu na Dullah.
Alijisikia raha sana na alikumbuka zile raha alizokuwa anazipata kwa Dullah kwani aliweza kukunwa vizuri hadi akajisikia kuliko tangia aolewe na Fredy ambae alikuwa mvivu mno kitandani na kutokana na kitambi kilichokuwa kimemtoka Fredy na kuongezeka siku hadi siku ndivyo alivyozidi kuwa mvivu ukizingatia hata maumbile yake yalikuwa madogo sana tena yalikuwa hayasimami vizuri na katika tendo hakuweza Fredy kuvumilia walau dakika mbili ziishe alijikuta akifika mwisho na kuregea mwili mzima na haikuwa kazi rahisi hata kidogo pindi Fredy anapopiga mshindo wa kwanza kuja kusimama tena ni shughuli, mbali ya Asu kumfanyia vituko na kumuandalia vyakula vya aina tofauti ili kuzidi kumpa nguvu pindi awapo uwanjani lakini ndio kwanza uzorota wa Fredy ulizidi kuongezeka na kugeuka kero kubwa moyoni mwa Asu.

Alifikiria mengi siku hiyo na kitu kimoja ambacho kilikuwa chaajabu kwa Asunta ni pale akili zake zinapomkumbuka Dullah tu basi na mtoto tumboni anacheza kwa nguvu na kumsababishia maumivu ambayo baada ya dakika kadhaa hupotea na kuwa katika hali ya kawaida.
Safari hii hali ile ya kuogopa maumivu ya tumbo alikuwa anaipotezea na kuvumilia pasi na kumwambia mtu hadi tumbo linapokaa sawa mwenyewe.
("D, nimekukosea sana mme wangu lakini hiki kiumbe ni chako kabisa na atapozaliwa nitakutafuta umuone mwanao na wewe ndie utayepaswa utoe jina. Sasa niliondokajeee? eee!! Kweli nilimkosea na mamaaa na wifiiii aagh!! kwanini sasaaa nilikuwa siwapendi vile?!! daah! ")
aliwaza na kujiuliza moyoni kwa maumivu makubwa Asunta huku akijenga taswira kama Dullah ndie aliyelala nae pale kitandani na hakuwahi kutaraji kama ipo siku atakuja kuachana na Dullah na kuolewa na mwanaume mwengine tena akiwa ana ujauzoito wa mwanaume mwengine?!!
aliwaza pia na kujiona kumbe alifanya kosa kubwa sana kuolewa na Fredy na amevunja viapo vyake vingi alivyojiekea kikiwemo kiapo kwamba hatarajii wala kifikiria kuja kuzaa watoto wenye baba tofauti jambo ambalo sasa aliona ndilo alilosimamia kwa mbele anapoelekea kwani tayari ana mimba ya Dullah na mumewe atapohitaji wazae tayari atakuwa kashachanganya damu na kuvunja agano la kiapo chake.

* * * *
DAR - TANZANIA
_____________

Ilikuwa ni usiku wa manane akiwa ni mwenye furaha siku hiyo Pastor George baada ya kuvuna pesa nyingi kuliko siku zote kwenye ukumbi wa Diamond jubelee na mara baada ya malipo mengine ya ukumbi na kadhalika, aliingia kwenye chumba maalum alichokitenga mule ndani toka aliposema kuwa ametokewa na Yesu na kumuelekeza chumba kile ambacho awali kilitengwa kwaajili ya wageni wa kiume sasa kimekuwa chumba maalum cha kupokea maono nyakati za usiku sana na haikutakiwa mtu yeyote kuingia kwenye kile chumba hata mkewe pia.

Aliingia akiwa na bluefcase la pesa alilokuwa nalo kwenye maombi mchana wake achilia mbali vile vikapu ambavyo pesa yake hupelekwa bank moja kwa moja, alifungua na kuanza kuhesabu maburungutu ya noti za waumini huku mate yakimtoka na moyo wake ukiwa umefurika furaha isiyo na kifani.

Jumla ya noti zilizojaa kwenye bluefcase lile kubwa siku hiyo ilikuwa milioni 53 ukiachilia mbali zile zilizokuwa kwenye makapu.
"hahahahahaaaaaaa Chineduuuuuu Iiigweeeeeeeeeee"
alifurahi sana Pastor na mule kwenye kile chumba kulikuwa na simu maalum ambayo ndiyo aliyokuwa anawasiliana na Chinedu mganga wake yule wa Nigeria,
Alichukua simu kama kawaida na kumpigia Chinedu akiwa mwenye tabasamu zito hasa mara baada ya Chinedu kupokea simu na kusalimiana lakini ajabu siku hiyo Chinedu alionekana kupooza kidogo hali iliyomtisha Pastor na kumuuliza kulikoni? ila jibu alilotoa Chinedu lilimfanya kwanza Pastor anyamaze kwa muda akiwa kataharuki.

ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom