Prince Naahjum_
Senior Member
- Jun 13, 2016
- 139
- 125
- Thread starter
- #21
SEHEMU YA 5
Upande wa pili alionekana Asunta akijitahidi kuendeesha gari kwa speed sana ili aweze kuwahi ubungo na kugeuka kurudi nyumbani kwani alishahisi kuwa anatafutwa kwenye simu kwa kuwa alikuwa nyuma ya muda kwa zaidi ya masaa mawili na kwa kuwa haikuwa kawaida yake na alivyowaelewa wazazi wake walivyo juu yake alihisi tu lazima watakuwa wamepata wasiwasi tayari.
Alilifikia geti la kuingilia mule ndani na alipokuwa anapaki gari yake alishangaa kuiona gari aliyopenda kutembelea babaake ikiwa eneo lile na zaidi kilichomuaminisha ni baada ya kumuona dereva wa babaake akiwa kasimama nje ya ile gari na hata nae alipoiona gari ya Asunta alitabasam na kumuashilia kuwa akipaki aende.
"Mh! mbona leo kivumbi, sijui kaja na baba!"
Alijisemea moyoni Asunta na mapigo kuanza kumuenda kasi na aliposhuka kwenye gari kumfata yule dereva na baada ya kusalimiana kabla hajauliza chochote moyo ulimripuka mara baada ya kusikia sauti ya babaake sambamba na mwalimu wake wakijia pale walipo.
"Si huyu hapa Asunta!!? aaah mwanangu nini kimekupata tena"
Aliongea kwa taharuki Pastor George na kumsogelea Asunta ambae alikosa cha kujibu harakaharaka kwani aliogopa sana kumdanganya babaake lakini pia alijua si vyema wala si busara kumwambia mzazi wake kuwa alikuwa na mwanaume huko atokapo ambae wanapendana.
Hali ile ilimfanya Asunta abaki amejiinamia kichwa huku akivunjavunja vidole na ndipo Pastor George alipofika jirani yake tu alimuekea mwanae mikono kichwani na kuanza kumuombea palepale.
"......Baba naomba katika jina la Yesu vunja na teketeza nguvu zote na mapepo mabaya yanayoanza kumnyemerea bint yangu... Jehova nakutumaini wewe baba ingia na uusafishe moyo wa bint angu Asunta umuondolee hofu ya kumficha shetani na kuogopa kusema ukweli ... Naamuru sasa katika Jina la Yesu Kristo alie haaaii.... Nateketeza na kuchoma nguvu zote za giza na ushawishi wa shetani ... ktk jina la Yesu nasema Asante baba maana najua kazi yako unaenda kuifanya sasa.. aashgamaloga bbautih a ngghikjhhgaamaa... Aaamen.."
Aliomba hadi Asunta nae alijikuta anafumba macho na baada ya maombi yale alimuamuru aingie kwenye gari wageuze kurudi nyumbani kwani hayo mengine watayazungumza watapofika nyumbani.
Aliendeesha gari Asunta huku akijua fika sasa kimenuka na babaake aliheshimu tu mazingira ya pale ndio maana hakumsema sana lakini vilevile moyo wake ulifurahi kuwa ktk mahusiano na Dullah japo alijua hawezi kumwambia yeyote kwa muda ule mpaka hapo baadae taratibu zitapofatwa.
Walifika nyumbani na kweli kama alivyowazia Asunta baabaake alikuwa bado kakasilika mno.
"Haya mama twambie ulikuwa wapi"
Aliuliza pastor George baada ya kueka kikao cha dharula na kumwita mkewe sambamba wamuhoji na kumsikiliza biti yao Asunta wapi alipokuwa na kwanini amechelewa.
Asunta alibaki tumbo joto akifikiri aanzie wapi amalizie wapi ili awalidhishe wazazi na ndipo kwa haraka ilimjia mbinu kichwani na kuamua kuitumia.
"Naomba mnisamehe sana wazazi wangu lakini nilipokuwa njiani asubuhi naelekea mazoezini Vero alinipigia na kunambia anaumwa hivyo nilijikuta napitiliza mpaka kwao kwanza kumuona na kwa bahati mbaya simu ilizima chaji na nikasahau kuichaji ndio maana sikuwataarifu mapema"
Alijitetea Asunta kwa kutunga uongo wa pale pale lakini Pastor George alikuwa na mbinu sana za kumsoma mwanae pindi aongeapo kweli.
"Ahaa kwa hiyo ulipitia kwa Vero, vipi ulimkuta?"
"Ee nilimkuta baba"
"anaendeleaje?"
"hali yake si nzuri sana ila hajambo."
"oke sawa, mama Asunta chukua simu ya Asunta ichomeke chaji tumpigie Vero sasa hivi"
Kauli ile ya kuwa apigiwe Vero ilisababisha moyo wa Asunta kulipuka na kuanza kuhofia zaidi jinsi Vero atavyomponza kwani walikuwa na siku kadhaa hawakuonana pia hakumpigia simu kumpanga kwa jambo lile alilolitunga.
"Asunta mwanangu, ninavyokutazama tu roho mtakatifu ananionesha kuwa unachokisema sio cha kweli.. hebu kuwa muwazi kwani huoni kama ni aibu na dhambi kubwa kusema uongo tena mbele ya wazazi wako?"
Aliongea tena Pastor George maneno yaliyomchoma kidogo Asunta na kujikuta anapata kigugumizi kwani alihofia mno kusema ukweli mapema ile pia alihofia kuendelea kung'ang'aniza uongo wake kwani aliamini endapo atapigiwa kweli Vero basi ataumbuka.
Alifikilia mno na kubaki kainama bila kusema chochote hali iliyozidi kumuimanisha Pator George kile akisemacho na moyoni alijikuta anahuzunika kidogo Pastor na kubaki wanatazamana na mkewe wakisemezana kwa macho wamfanyeje mtoto wao kipenzi kwani walimpenda mno na hawakuwa tayari apotee mapema ile na walishamuekea mikakati mizuri sana ya baadae ili asije kuwa tegemezi.
Akiwa bado katulia Asunta safari hii mamaake alimsihi na kumuomba aseme ukweli tu wala asiogope kwani wao ni wazazi wake hivyo asiwaogope wala asiwafiche kitu.
Ndipo alipoinua uso wake Asunta na kumuangalia mamaake kipenzi aliyemzoea kama rafiki pia kwa vile walivyoishi na kupewa uhuru wa mawazo na kujadili mambo muda mwingi ya kimaisha pamoja.
Safari hii Asunta alipiga moyo konde na kutaka kuongea kitu lakini kabla hajafanya hivyo mara simu yake iliyokuwa imechomekwa kwenye chaji na ilishawashwa muda kwa dhumuni la kumpigia Vero ghafra iliita na ndipo mamaake alipoitazama kwenye kusoma jina la aliyekuwa anapiga na kumuangalia mwanae kwa mshangao kisha akamkabidhi simu yake.
"Nani huyo anaempigia?"
Aliuliza Pastor George akiitilia mashaka simu ile kuhusiana na safari ya mwanae.
na mara baada ya Asunta kuiangalia jina lililotokea kwenye Screen liliseviwa My D.
Moyo ulimripuka sana Asunta hasa pale babaake alipomfokea pindi alipositasita kuipokea ile simu.
"Pokea basi uzungumze na huyo mtu, tena uweke Loud speeker..!"
Alifoka Pastor George na kunyanyuka hali iliyomtisha zaidi Asunta na kujua sasa akizembea atapigwa vibao kwani alimuelewa vizuri pia babaake japo hakuwahi kumpiga mara kwa mara lakini sifa zake za ugomvi hapo zamani na kutopenda ujinga alishahadithiwa na mamaake na kumtahadhalisha kuwa licha ya babaake kuwa mtumishi mzuri wa mungu lakini hasira zinapomzidi sana huwa anabadilika mno.
Kwa hofu kubwa Asunta alikielekeza kidole gumba sehemu ya batani ya kijani ya simu yake na kuipokea.
"Hallow baby, samahani ushafika nyumbani? naomba nikwambie kitu Asunta mamy... ukweli tangia tumeachana mida ile mpaka sasa nahisi ubongo wangu umeganda na kushindwa kuingiza vitu vipya nikitafakari hivi hiki kilichotokea ni ndotooo au ni picha halisi?!! Haloo.. Halooooooo .. Asunta halooo!!!?"
Naam ilikuwa ni sauti ya maneno ya Dullah kutokea simuni pindi ilipoekwa loud speeker baada ya kupokelewa na yalisikiwa vizuri na kila mmoja si Asunta, mamaake wala Pastor George huku Asunta akiwa kaganda bila ya kujibu chochote hadi Dullah alipoamua kukata simu baada ya kuona upande wapili kimya kimeshamiri.
Alisimama Pastor George na kuanza kufoka huku Asunta akibaki amejiinamia analia kwa kwikwi pale chini na kuomba msamaha kwa wazazi wake kwani tayari siri yote ilishabumbuluka na hakuwa na jipya tena.
"Umeonaa!!? umesikia mama Asunta ujinga wa mwanao.!!! na haya ndio mazoezi mapya aliyoanza siku hizi, mazoezi ya kuidhalilisha na kuitia nuksi nyumba yangu takatifu.
Asunta mwanangu kwanini unataka kututia aibu hivi? Eee Yesu baba muokoe huyu mwana kondoo wako hapa chini na unipe moyo wa uvumilivu nisije kumvunja heee!! Mwanangu Asunta!? mafundisho yoooootee kanisani imekuwa bure? sasa hivi ushakuwa baby wa mtu..!? nilichotaka usome mwanangu au kama hutaki kusoma fine naomba unijibu ukweli wote kabla sijaondoka kuhusu huyo aliyepiga simu.
Maana aibu sitaki kuikaribisha ndani ya nyumba yangu, unataka mume?? sema ifatwe sheria twende ngazi kwa ngazi sio hivyo unavyoenda wewee mwananguuu Aaaaagh"
Aliwaka sana Pastor George hadi mate yalikuwa yanamtoka mdomoni kutokana na hasira na kupanua mno mdomo kipindi anafoka.
"Naomba mnisamehe sana wazazi wangu ila sikupanga kuwaficha kabisa nilikuwa nasubiri muda rasmi ufike niwaambie habari hizi"
"Utuambie wewe ndie mshenga?.. hebu acha ujinga wako kama unataka kuolewa na umepata mtu uliyempenda mama sawaaa ila kwa masharti na vigezo vya roho mtakatifu mwenye kuleta amani na utulivu ndani ya nyumba, kwanza huyo mtu wako uliyepanga kutwambia habari zake si ndio huyo aliyepiga simu?
"Ndio."
"Anaitwa nani..?"
"Dullah baba"
"Dullah Dullah Dullaaaah!! okeeeei yaani Abdallah!!?!!.. Eee bwana Yesu ulie mbinguni, mbona shetani anamuandama kiasi hiki binti angu?!!
sasa sikiliza Asunta mimi naondoka ila kuanzia muda huu sahau kabisa juu ya huyo Shetani asije kukupoteza. na Sitotaka tena kumsikia mtu kama huyo ndani ya nyumba yangu takatifu. Nadhani umenisikia mama Asunta..
Amani ya bwana iwe nawe'
Aliongea kwa hasira Pastor George baada ya kulitafakali jina la Dullah na kugundua kirefu chake kisha akatoka na kuingia chumbani kulipokuwa begi lake na kutoka nje ambapo tayari msafara wa magari mawili kutoka kanisani kwao ulikuwa unamsubiri kwaajili ya kumpeleka uwanja wa ndege kwa safari yake jijini Nairobi.
Kwa upande wa Asunta hakuelewa kwanini babaake ameongea maneno yale na kwa hasira vile na baada ya kutoka na kuondoka Asunta alirudi ndani na kujifungia chumbani kwake na kuanza kulia kwa uchungu hadi mlango wa chumba chake ulipofunguliwa na hakuwa mwengine aliyeingia bali ni mamaake kipenzi ambae alikuwa mpole sana na mwenye busara pia.
ITAENDELEA