Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 8,288
- 18,579
- Thread starter
- #121
MAISHA YANGU NYUMA YA PAZIA JEUSI
SEHEMU YA 20
Ilipoishia
Nikiwa katikati ya kilio mara nikasikia mtu akiita kutoka dirishani. Niligeuka kwa hamaki kubwa kuangalia alikuwa ni nani. Lahaula..! alikuwa ni mlinzi mkuu wa shule.
“unafanya nini huku peke yako? Eeh?” alisema kwa ukali. Mwili ulizidi kuishiwa nguvu. Nilikuwa katikati ya majonzi lakini hili nalo lilikuwa ni tatizo jipya tena. Hakika siwezi kukisahau kipindi hiki katika siku zite ya maisha yangu. Ni kipindi ambacho moyo wangu ulibeba mzingo wa maumivu na huzini kupita kiasi.
Nikiwa bado sijui ni nini nifaye, nilisikia mlinzi akifoka tena.
“we mwanafunzi nakuomba hivyo hivyo ulivyo nyanyuka uje hapa.” Kauli hii ilikuwa ni msiba mwingine kwangu. Kwa hakika nilijua kuwa ile siri iliyokuwa imejificha nyuma ya kifo cha Jennifer ingeenda kufichuka punde.
Endelea…..
Nilikuwa katika kipindi cha majuto na uchungu mkali kwa kufanya jenifer aamue kujiua kwa sababu yangu na wakati bado jeraha hili likiwa bichi kabisa kuna jeraha lingine lilikuwa linaningojea. Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwangu.
Nilibaki nimetoa macho nikimwangalia mlinzi aliyekuwa ananiangalia kupitia dirishani nikiwa sijui ni lipi la kufanya.
“hivi husikii ninachokwambia? Nakwambia njoo haraka sana. Beba na hivyo ulivyovishika” mlinzi alizidi kusisitiza kwa sauti ya ukali.
Kulingana na tukio lililokuwa limetokea usiku ule pale shuleni, jambo dogo tu lingeweza kufanya uhisiwe vibaya. Na kwa kuwa mimi nilikua msababishi mkuu wa Jennifer kufikia maamuzi ya kujitoa uhai, kitendo cha mimi kukutwa darasani usiku nikilia huku nikiwa nimeshika vithibitisho vya uhusika wangu, hivi kwa pamoja vingeweza kusababisha mimi kutiliwa shaka na kugundulika kuwa mimi ndiye msababishi wa yote, jambo ambalo lingekuwa na madhara makubwa sana kwangu, wazazi wangu na hata wazazi wa Jennifer. hivyo japokuwa nilikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa lakini nilitakiwa kufanya kila njia ili tu vitu hivyo visiweze kuonekana.
Mlinzi alizidi kuniamrisha nitoke nje haraka sana bila kuacha kitu chochote nilichokuwa nimeshika. Japokuwa nilikuwa katika wakati mguu, ilinilazimu kufikiri vema ili nisiweze kuingia katika matatizo makubwa zaidi. nikaamua kuwa nisinyanyuke kutoka nje. Mlinzi aliendelea kuniamuru nitoke lakini mimi sikutii, niliendelea kukaa.
Mlinzi alipoona kuwa sinyanyuki alianza kupiga hatua kuingia darasani. Na mimi nikaona hiyo ndiyo nafasi pekee ya kuficha ushahidi. Nilisubiri alipofika katika ukuta unaotenganisha dirisha na dirisha sehemu ambayo yeye hawezi kuniona na mimi siwezi kumwona, nikachukua ile picha na barua kisha kwa kasi ya aina yake nikanyanyua mkono na kuvitupa nje ya darasa kupitia dirishani lililokuwa jinani yangu kisha nikaendelea kukaa vile vile kama nilivyokuwa nimekaa awali. Milizi aliingia ndani ya darasa huku akiwa sura ya ukali ulio dhahiri kabisa.
“nakuuliza unafanya nini humu peke yako usiku huu?” alisema huku akininyoshea kirungu chake. Nilimwangalia huku nikijaribu kujikausha ili nisionekane kuwa nilikuwa nalia.
“babu, mimi nilikuwa nimekuja kuchukua daftari tu” nilijitetea huku sauti yangu ikionyesha wazi nilikuwa nimetoka kulia muda sio mrefu.
“daftari la kazi gani usiku huu, ninyi si mmetangaziwa kuwa mnatakiwa kuwa mabwenini muda huu. Halafu nimekuona tangu muda unalia huku umeshika karatasi. Hebu nionyeshe hiyo karatasi”
“babu, kwenye kulia sikatai…ila hilo la kushika karatasi hapana. Unatakuwa uliona vibaya. Nilikuwa nimeshika daftari” niliongea huku nikionyesha daftari lililokuwa juu ya meza.
“kwa hiyo unanifanya mimi sina akili sio? Nimekuona muda mrefu sana umeshika kitu kama barua hivi unakiangalia huku unalia. Bila shaka wewe utakuwa unajua kilicho nyuma ya Yule msichana kujinyonga” alisema kwa sauti ya juu na ukali ili kunitisha.
“nini unataka kusema we mzee, kuwa mimi ndiye niliyemnyonga Jennifer sivyo…nipeleke polisi basi. Watu tuna majonzi, tunaamua kukaa sehemu zenye upweke ili tutulize akili na kupunguza uchungu. Wewe unakuja na mambo yako ya ajabu hapa” niliongea huku nikiambatanisha na kilio. Sikulia ili kufanya Yule mlinzi anione sina hatia, bali nililia kwa hisia za kweli juu ya kuondoka kwa Jennifer. Kilio kilikuwa cha kweli kwa asilimia zote.
“we mtoto unanijibu jeuri mimi! Nakuuliza unanijibu jeuri?” aliuliza mlizi kwa sauti ya ukali sana. Ni wazi alikuwa amekereka na majibu yangu hivyo nikaamua kukaa kimya ili nisikuze mambo zaidi. “ haya nyanyuka haraka” alisema baada ya kuona sijibu kitu. Nilipsimama alianza kunipekua. Alinipekuwa kwenye mifuko yote ya suruali, hakuambulia chochote. Hakuridhika, akaanza kupekua kwenye meza yangu, aliiona ile leso lakini hakuitilia maanani. Akaendelea na kupekua meza za jirani lakini pia hakupata chochote cha kuthibitisha madai yake. alipoona amekosa pa kunikamatia alisogea pale nilipokuwa nimesimama kisha akaongea kwa sauti ya chini;
“nenda bwenini, ila usidhani umeshinda katika hili. Bado nina sababu nyingi za kukutilia shaka juu ya tukio la Yule binti kujinyonga. Nafikiri kesho tutakutana kituo cha polisi” alisema Yule mlinzi kisha akaniamuru niende bwenini haraka sana.
Nilishukuru angalau kwa kupata nafasi ya kuliepuka hilo japo kwa muda kidogo. Nilianza kupiga hatua kutoka nje ya darasa huku akili yangu ikiwa inawaza juu ya vile vitu nilivyovitupa nje kupitia dirishani. Vilikuwa ni vitu vilivyobeba ushahidi wote juu ya kifo cha Jennifer. Japo katika kesi kama ile ya kujiua nisingekuwa na hatia lakini ni wazi kama vitu hivyo vingeonekana kwa watu, jamii inayonizunguka ingenitazama kwa jicho baya sana, hasa wanafamilia wa Jennifer. Hivyo nilikuwa natoka nje ya darasa nikifikiria ni vipi kama vingepeperushwa na upepo na kwenda mahali ambapo mimi siwezi kuvipata na vikatua katika mikono ya watu wengine? Nilikuwa natamani sana niende nikavichukue muda ule ule ila nilikuwa nahofia kuonekana na mlinzi. Hivyo nikapitisha uamuzi kuwa nienda bwenini nikakae kwa muda kisha niende tena kwenda kuvichukua.
Nilifika bwenini na kukuta wanafunzi wengine katika mabweni yote wakiwa macho wakiongea mambo tofauti tofauti kuhusu tukio ambalo lilikuwa limetokea. Hali ile ilinifanya nizidi kuumia ndani ya nafsi yangu kwa sababu kuwa mimi ndiye nilikuwa chanzo yote hayo. Ama kwa hakika mzigo niliokuwa nao nafsini mwangu ulikuwa mzito sana.
Niliendelea kupiga hatua za kinyonge nikikaribia chumba nilichokuwa nalala. Nikafika ndani ya chumba na kuwakuta wanafunzi wenzangu wakijadili kifo cha Jennifer.
“barry ulikuwa wapi wewe?” lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa mwanafunzi mwenzangu baada tu ya mimi kuingia mule chumbani, na wanafunzi wengine nao walitulia na kuniangalia mimi. Ni kama vile walikuwa wanahisi kuwa mimi nafahamu chochote kuhusu tukio hilo. Kwa hali niliyokuwa nayo nisingeweza kuongea chochote na kama ningethubutu basi ningeweza kuharibu kila kitu. Sikutaka watu wajue hadithi iliyokuwa kati yetu kiasi ya kumfanya Jennifer afikie maamuzi ya kujiua. Hivyo sikujibu lolote, nilipanda zangu kitandani na kujifunika shuka mwili mzima.
Japokuwa niliamua kuwa kimya, lakini wanachumba wenzangu waliendelea kuongea kuhusu tukio hilo. Wengi wao walionyesha kutaka kusikia chochote kutoka kwangu kwa maana hadi umauti unamkuta Jennifer, mimi ndiye niliyekuwa mtu wake wa karibu, hapakuwa na siri katika hilo. Lakini mimi sikutaka kuongea kitu, nilibaki kimya ndani ya shuka huku nikiugulia maumivu.
Mimi kupanda kitandani ni kama nilikuwa nimefika eneo la kumkumbuka Jennifer, nilikumbuka siku ya kwanza kufika shule na kukuta wavulana wenzangu walimwongelea kiasi nikashikwa na shauku ya kumfahamu, nikakumbuka siku ya kwanza kumwona alipokuwa akijibu swali, nikakumbuka migogororo yote ambayo tulipitia kwa pamoja, nikakumbuka jinsi tulivyopatana, nikakumbuka jitihada zangu za kujiweka mbali na yeye ambazo zilishindwa na kufanya tudondokee penzini, penzi ambalo lilikuwa la upande mmoja. Yote hayo yakaja kuhitimishwa kuwa kwa wakati huo Jennifer hakuwa nasi tena. Yalikuwa ni majuto makubwa sana kwangu.
Mawazo lukuki yaliendelea kupita kwenye kichwa changu huku nikisubiri watu wengine walale kisha niende kuangalia kama ningeweza kuzipata zipata picha na ile barua. Nilihofu kutoka ikiwa wengine wangali macho kwani kufanya hivyo kungefanya nitiliwe shaka. Nao wanachumba walikuwa kama wanajua ni nini nilikuwa nawaza na hivyo wakaamua kunikomoa, waliongea kwa muda mrefu sana kiasi nikawa natamani niwaambie walale. Ila niliamua kujivika roho ya uvumilivu ili nisiharibu mambo.
Baada ya muda mrefu sana, kukawa kimya. nikatoa kichwa nje ya shuka ili kuhakikisha kuwa wote wamelala, kweli..wote walionekana kuwa wamelala. Hivyo nikaona huo ndiyo ulikuwa wakati wangu wa kutoka kwenda kuvitafuta vile vitu nilivyovitupa nje. Kwa taratibu sana ili nisisikike, nilinyanyuka kitandani na kushuka na kisha kwa mtindo wa kunyata nikatoka nje ya chumba na kuelekea lilipo darasa letu. Nilikuwa natembea kwa tahadhani kubwa ili nisionekane na watu hasa Yule mlinzi kwa maana kama angeniona tena nazurura usiku ingekuwa kesi nyingine.
Nilifanikiwa kufika nyuma ya darasa letu kwa upande wa nje kwenye usawa wa dirisha ambalo nililitumia kuvirusha vile vitu nje. Niliangalia pale chini ila sikuweza kuona chochote. Mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio, akili ikaanza kuvurugika zaidi. nilianza kuangalia kwa papara maeneo ya jirani na pale lakini sikuweza kuona chochote zaidi ya makaratasi ya madaftari ambayo yalikuwa yamezagaa zagaa.
“au Yule mlinzi amepita huku na kuviona…ahh, mbona mambo ya kis***e haya dah” nilijikuta naropoka kwa sauti yenye kusikika vyema huku ikiambatana na kilio. Yaani ilikuwa ni matatizo juu ya matazito. Na kama ingekuwa hivyo kuwa Yule mlinzi aliiona ile barua na picha na kuvichukua, basi habari yangu ingekuwa imeishia hapo. Kila mtu angejua kuwa mimi ndiye niliyefanya Jennifer ajiue. Je, ni wapi ningeificha sura yangu?
Niliendelea kutafuta katika maeneo yote yaliyokuwa jirani, sikuwa najali tena kuonekana na mlinzi au mtu yeyote Yule. Kitu pekee nilichokuwa najali ni niipate barua na picha, basi. Kadri muda ulivyokuwa unaenda, jitahada zangu zilionekana kugonga mwamba. Nikakaa chini huku nikimlaumu Mungu ni kwanini aliamua kunipitisha katika matatizo mengi katika usiku ule tu mmoja.
Nikiwa katika hali ya kukata tamaa niliona kitu kama karatasi kikipeperushwa na upepo. Sikujishughulisha kukifutilia kwa maana katika eneo hilo kulikuwa na makatarasi mengi ya aina hiyo. Karatasi hiyo ilipeperuka na kwenda kunasa kwenye maua yaliyokuwa jirani nami. Akili yangu akinisukuma kwenda kukiangalia pengine muujiza ungetokea. Kwa kujivuta nikanyanyuka na kwenda kukiangalia. Niliinama na kukiokota. Sikuamini macho yangu, ilikuwa ni barua ya Jennifer.
“asante Mungu” nilijikuta naongea pasipo kujielewa. Akili ikachangamka kidogo, nikaanza kuangaza mcho tena kutafuta picha ambayo nayo niliiona muda kidogo baadaye katika ameneo jirani na yale nilipoiokota barua.
*********
“kuna mengi saa yalitokea baada ya hapo ila kwa ufupi hicho ndicho nilitaka ukifahamu” niliongea huku nikiwa nimetazama mbele nikiangalia mawimbi ya bahari yalivyokuwa yanapiga ufuoni.
"pole barry...inasikitisha sana. sikuwahi kujua kuwa ulikuwa umekutwa na tukio kubwa namna hii." alisema ingrid huku akiweka mkono wake mgongoni kwangu kama ishara ya kunifariji...japokuwa hata yeye alikuwa ni mwenye huzuni muda huo.
"ingrid...hakuna kipindi ambacho kilikuwa kigumu kwangu kama kile, na sidhani kama kitakuja kutokea kingine kukizidi. Huwa najihisi mkosaji sana kila nikilikumbuka tukio hili. Ni kweli jennifer alikuwa na mapungufu yake lakini hakustahili kile nilichokuwa namfanyia. Nimekuwa nikisema RIP kila ninapokumbuka kuondoka kwake..lakini h huwa simaanishi Rest In Peace..bali huwa namaanisha Return If Possible...nataka kutubu mbele yake..nataka kumpa thamani yake aliyostahili japo kwa mara moja tu.” Niliongea kisha nikatulia kuvuta pumzi, kisha nikaendelea.
"baada ya mazishii ya Jennifer maisha yangu pale shuleni yalikuwa magumu sana. Kila nilipokuwa naona kiti na meza aliyokuwa akiitumia Jennifer nilikuwa nakosa amani kabisa. Japo kilichotokea kilikuwa ni siri yangu na yeye, lakini minong’ono kunihusu ilikuwa ni mingi sana. Minong’ono hii ilinifanya nizidi kuwa na majuto maana vingi vilivykuwa vinasemwa vilikuwa vya ukweli. Maisha yangu yote yalitawaliwa na huzuni na majuto. Lakini siku zote, majuto ni mjukuu. Kwa kweli nilishindwa kuendelea na shule, nikaamua kuacha ili angalau nikae mbali na eneo ambalo lilikuwa linanikumbusha machungu kila ninapokuwapo. Wazazi walishangazwa na uamuzi wangu na kunilazimisha kwa nguvu nirudi shule lakini nilikataa kata kata. Sikutaka tena kusikia kitu kinaitwa shule katika maisha yangu. niliona bora tu niendelee kukaa nyumbani au nitokomee mahali pasipojulikana kuliko kwenda shule. baada ya kunisisitiza sana hatimaye alishindwa na kuniacha tu." Niliendelea kumsimulia Ingrid huku macho yangu yakiwa yanatazama baharini.
"barry, pole sana..." alisema kwa sauti ya huzuni.
"kutoka siku ile Jennifer alipofariki, niliapa kuwa jennifer ndiye alikuwa mke wangu halali kwa maisha yangu yote..niliamua kuitunza heshima yake...nawaogopa wasichana..nawahofia sana..kila ninapopata hisia za kumpenda yeyote ghafla kumbukumbu za tukio la jennifer hunirudia na kufanya nikose matamanio ya kuwa na msichana maishani mwangu. ingrid, give me up....acha niendelee kuugua na hili maana sitaki tena kuja kutokewa na mengine ambayo sitoweza kuyahimili. hili lililonipata linatosha. niache tu mimi niwe rafiki yako na nakuahidi nitakuwa rafiki mzuri kupata kutokea kwako, lakini suala la mapenzi kati yetu achana nalo. Acha niendelee kubaki na Jennifer wangu. Nimekwambia haya yote nikitegemea kuwa utanielewa." nilimaliza kuongea.
"barry nimekuelewa..na pole sana kwako pia I'm very sory kwa jennifer, may her soul rest in peace. barry, naingiwa na wasiwasi kuendelea kukupenda kutokana na hiki ulichoniambia leo lakini naamini ulijifunza mengi. Mimi naamini kuwa unapokosea sana ndipo unapojifunza sana. Sidhani kama bado utaweza kufanya yale uliyokuwa ukimfanyia jennifer kwa kuwa tayari unajua matokeo yake yanaweza kuwa ni nini. Pia unahitaji mtu wa kukurudisha kisaikolojia katika hali yako ya zamani..japokuwa unaweza kuwa unahisi upo sawa lakini ni lazima kuna vitu vitakuwa haviko sawa. Unahitaji mtu wa kukuliwaza..barry hivi haujisikii faraja wakati ambao ulikuwa ukikaa na kukumbuka kumbukumbu hii mbaya uutumie kuwa na mimi pembeni yako?, amini nakwambia hautokaa ujutie kuwa namimi. Barry, nakupenda sana. pia huenda uliyafanya yale kwa sababu jennifer alikuwa akikutendea vibaya nyakati za mwanzoni..lakini vipi kuhusu mimi, nilishawahi kukukosea chochote?..eeh eti barry. jennifer alikufa kwa ajili yako basi acha niishi nawe badala yake.. hata kama ukitaka kuniita jennifer ni sawa tu, barry. please nakuomba sana...nipe muda nijaribu kukuonyesha uhalisi wa mapenzi yangu kwako, nikikushindwa nitaondoka zangu kwa amani lakini nipe nafasi kwanza" alisema ingrid kwa sauti ya mahaba mazito.
Nilianza kuhisi kama damu ilikuwa inapanda na kuja kujaa kifuani. Nikajikuta napandwa na hasira sana maana sasa huu ulikuwa ni usumbufu ulikuwa unavuka mipaka yote. Nilikuwa kila siku namwambia kuwa isingewezekana mimi na yeye kuwa katika mahusiano lakini akawa mgumu kuelewa. Nikaamua kuumpa hadithi ile kati yangu na jennifer nikiamini kuwa huenda angeelewa kwa nini nilikuwa sitaki kuwa na yeye lakini ilikuwa ni kama sikufanya kitu. Nilikuwa nimetumia muda mwingi kujieleza nikitarajia angenielewa na kuniacha huru lakini alikuwa bado ameng'ang'ana na mimi tu. Nilianza kuhisi ananifanyia makusudi. Nilikasirika sana.
Nikiwa katika hali ya huzuni baada ya kujikumbusha kifo cha jennifer na hasira za kukasirishwa na ukichwa ngumu wa Ingrid, nilijikuta nanyanyuka na nikamkata ingrid. kisha nikamnyanyua na kumkwida, mishipa yangu ya damu ilikuwa imevimba kwa hasira, macho yakitoa mchozi. nilianza kumuongelesha ingrid huku nikimtikisatikisa.
"ingrid, una kichaa..eti nakuuliza una kichaa?"
"barry..unataka kunipiga kisa nakwambia hisia zangu..barry wewe ni mtu wa ina gani usiyeelewa" alisema kwa sauti ya kelele iliyoambatana na kilio Fulani hivi.
"kila siku nakwambia kuwa haiwezekani lakini wewe unga'ang'ana tu...huoni watu wengine hadi usumbuane na mimi tu. Ni mimi ndo ndiye mwenye m**o hapa duniani? eeh" nilisema huku nikiwa bado nikemkwida kwa hasira zaidi ya mwanzoni. ingrid alikaa kimya lakini alikuwa akitoa kilio kwa chinichini. Nikamwachia kwa kumsukuma, akapepesuka na kudondoka kwenye mchanga, sikujali chochote, niligeuka na kuanza kuondoka.
"barry...this is too much...niambie tu kama wewe ni hanithi nijue...mwanaume aliyekamilika hawezi kufanya unayoyafanya. usitake kuleta visingizio.. na nina wasiwasi na hii hadithi yako uliyonisimulia, inawezekana kuwa ni ya uongo. Umeamua kutunga uongo ili kuficha uhanithi wako. hakuna mtu anaitwa jennifer uliwahi kuwa naye..wewe ni muongo. Barry wewe ni joka la kibisa, kwenda zako ms***e wewe" ilikuwa ni sauti ya ingrid akinitamkia maneno yale. Sikuwahi kufikiri kama ingetokea siku Ingrid angenitamkia maneno kama yale. ingrid alikuwa amevuka mipaka...alikuwa amevuka mipaka kwa ambayo kila mwanamme huiheshimu na kuilinda. nilijikuta nageuka kisha nikaaza kumfuata ingrid alipokuwa amekaa.
Nilifika nikamkamata na kumyanyua huku nikiwa nahema kwa hasira.
“unasemaje wewe Malaya mmoja? Mimi ni hanithi! Mimi ni ms***e sio!” niliongea kwa sauti ya chini lakini iliyoshiba hasira kali.
“ndiyo, we ms***e tu. Huna lolote. Unaleta usanii eti ‘jennifer, Jennifer’” aliongea Ingrid kwa kujiamini huku hiyo ‘jennifer’ alitamka kwa kubana pua. Sijui hizi akili alizitoa wapi. Kwa muda ule nilisahau kila kitu kizuri tulichokuwa tumewahi kufanya na yeye. hata kile chakula kitamu alichoniletea siku ile ya kwanza kumuona sikukikumbuka tena. kwa muda ule ingrid alikuwa ni adui yangu namba moja. Bila hata ya kujiuliza mara mbili, nilimtandika ngumi nzito ya shavuni iliyosababisha adondoke chini.
Itaendelea…