Hadithi: Kizuizi

Hadithi: Kizuizi

Haijawekwa wazi ila mizambwa ndiye baba yake james,hivyo amesharestinpisi hivyo story imeishia hapo
 
kila sehemu moja inaushawishi wa kutaka kujua nini kinaendelea sehemu iliofuata
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU
Alipumzika kwa siku moja
nyumbani kujiandaa na safari ya
kurejea jijini Dar es salaam.
Tayari kwa kuanza maisha mapya
katika jiji hilo.
Safari hii hakupokelewa na Emmy
kama ilivyokuwa awali bali
walifika watu walioagizwa.
Alivyowauliza kulikoni Emmy
hajafika ndipo alikutana na taarifa
ya kusisimua.
Msiba!
Emmy alikuwa amefiwa na
babamkwe wake.
Waliompa taarifa hii hawakujua
kama Jose B anamfahamu vyema
mzee yule mwenye hekima.
Ameuwawa kwa kupigwa na kitu
kizito kichwani kabla ya
kuchomwa visu tumboni na
kifuani.
Kifo cha kustaajabisha na
kusikitisha sana.
Kulikoni! Jose B alijiuliza.
Walioagizwa kumchukua Jose B
waukweli walielekezwa mahali pa
kumpeleka ambapo atakaa na
kumngoja mwenyeji wake.
Jose B aliwaza kuwa huenda
anapelekwa hotelini tena. Lakini
haikuwa hoteli mara hii bali
nyumba nzuri ambayo ilitawaliwa
na samani mpya mpya.
Akakaribishwa.
“Sisi tunatoka kidogo amesema
atakukuta hapa.” Waliaga wale
wenyeji, Jose B akabaki peke
yake.
Maswali lukuki yakapita katika
kichwa chake. Kuhusu kifo cha
mzee Magayane pamoja na uwepo
wake katika nyumba hii.
Hakuamini kirahisi rahisi kuwa
yule mtoto wa kike alikuwa
ametimiza mara moja kile
ambacho Jose B alikuwa
amekihitaji.
Majibu yake aliyapata usiku wa
saa mbili, baada ya Emmy
kuwasili nyumbani pale na
kumkabidhi rasmi nyumba ile.
“Imelipiwa kodi ya mwaka mzima
pliiz Sam wa pili nakuomba sana
usiniangushe ndoa yangu bado
change sana.” Alizungumza kwa
huzuni kuu huku macho yake
yakiwa mekundu sana kutokana
na kilio kikubwa baada ya taarifa
ya kifo cha baba mkwe.
Jose B akashikwa na imani huku
udhaifu nao ukichangia
akamhakikishia kuwa atakuwa
naye bega kwa bega.
Wakaagana, kwa mara ya kwanza
Jose B akalala katika nyumba ya
kifahari. Ikiwa katika milki yake.
“Natamani mama angeniona hapa
nilipo.” Aliwaza.
Usingizi mwanana ukampitia.
Afajiri alidamka akiwa na wazo la
kumpigia Emmy simu aweze
kumuuliza kiundani juu ya msiba
ule wa ghafla. Jose B alitaka
kufahamu mawili matatu ili atii
kiu yake.
Alipopiga simu ya Emmy haikuwa
inapatikana.
Alijaribu tena na tena hali ikawa
ileile.
Wakati Jose akifanya jitihada za
kumtafuta Emmy, mwanadada
huyu alikuwa mkimya kabisa
katika ndege iendayo Mwanza.
Mambo kadhaa yakipita kichwani
mwake, alikuwa akimuwazia Jose
B waukweli kama ni kweli
ataitunza siri ile kwa muda mrefu
bila kuivujisha popote.
Alimchukulia Jose B ama Sam wa
pili kwa alivyojitambulisha kama
mwanadamu pekee anayeweza
kuiacha ndoa yake salama ama
kuisambaratishia mbali.
Kimya kimya akafanya dua huku
akimwombea kijana huyu awe na
moyo wa chuma.
Kijana mtanashati aliyeketi kiti
cha pembeni ya Emmy naye
alikuwa amejikita katika kusoma
jarida lililoandikwa katika lugha
ya kiingereza, lakini cha
kustaajabisha hakufunua kurasa
kuendelea mbele. Alikuwa
amekodolea macho ukurasa
mmoja pekee. Akili yake haikuwa
pale kabisa alikuwa anawaza
mengi zaidi ya yule mwanamke.
Alikiwaza kifo cha ghafla cha
baba yake, tena kilichotokana na
shambulio la kisu na kitu kizito.
Atakuwa nani huyu? Alijiuliza.
Akajaribu kufanya makisio lakini
hakupata majibu. Ni sura gani
ambayo mzee ameiona na
kunipigia simu usiku? Alizidi
kujiuliza.
Ghafla akamkumbuka kijana
aliyemuuzia siri ya kizuizi.
Alimkumbuka kwa sababu
alikuwa ni mpenda kujua mengi
hata yale yasiyomuhusu.
Jose B waukweli.
Nikifika Mwanza namtafuta.
Huenda anajua chochote.
James alifikia maamuzi ya
kujaribu kama atapata lolote kwa
kijana yule.
Mtu na mkewe kwa wakati
mmoja wanamuwaza mtu mmoja.
****
Sura iliyopita mbele yake
ilifanana na sura ambayo tayari
alianza kuisahau. Hakuitilia
manani sana na aliamini kuwa
hakuna kilichotokea zaidi ya hisia
zake.
Wakati anapata chakula cha usiku
na wanafamilia akaikumbuka tena
sura ile ambayo hata
angewashirikisha bado
wasingeweza kumtambua kwani
ni yeye na mwanaye wa kiume
pekee walikuwa wanaitambua
sura ile ambayo ilipotea machoni
mwao miaka kadhaa.
Sura ya mwanamke.
Baada ya kupata chakula mzee
Magayane alitoka nje ili aweze
kumpigia simu James na
kumueleza juu ya ndoto hiyo ya
mchana ya kuiona sura ile.
Alipompigia James, kwanza
alikuwa anaongea na mtu. Mzee
akafanya subira kisha akapiga
tena.
Ikapokelewa. Wakapeana salamu
za kila siku kisha mzee Magayane
akataka kutiririka.
“Huwezi amini bwana yaani leo
nimeota ndoto ya mchana sijui ni
watu wanafanana ama
vipi....hebu otea nimeona kitu
gani au nimeona sura ya nani
hapa mjini.” Mzee Magayane
alimuuliza mwanaye.
Kwa kuwa usiku ulikuwa
umeenda. Hata gharama za
kupiga simu zilikuwa chini.
James akakosa la kumjibu baba
yake.
“Vipi mbona kimya..we bashiri tu,
nimeonana na nani leo?”
James kimya. Akifanya tafakari
bila mafanikio.
“Samahani mzee mwanao ananiita
kidogo, nikimaliza nakupigia na
jibu nitakuwa nimepata...iwapo
nitakosa basi nitakupa mji ili
unipe jibu sahihi.” James aliaga,
mzee akakubali.
Hayo yalikuwa mazungumzo ya
mwisho kati ya mzee Magayane
pamoja na mwanaye.
Akiwa katika kusubiri simu
ipigwe, akiwa mbele ya nyumba
yake.
Mara ikapita taksi katika mwendo
wa taratibu.
“Samahani mzee naomba
kuuliza..”
“Bila shaka waweza kuuliza.”
Alijibu mzee Magayane.
“Huku mbele ni njia gani inatoka
kuifikia barabara ya lami?”
akauliza bwana mmoja ambaye
alikuwa anaendesha ile taksi ya
kukodi.
Swali lile likamvutia yule mzee,
akajisogeza tayari kwa kutoa
maelekezo.
Ghafla akadakwa, na kutupwa
garini kisha wale wazoefu wa
matukio wakaondoa gari kwa
mwendo wa kasi huku
wakionekana kuitambua njia zaidi
ya mzee Magayane alivyoweza
kudhani.
Ndani ya gari lile alikuwepo
mwanadada ambaye alikuwa
amevaa baibui nyeusi iliyomficha
hadi sura yake.
Safari fupi mwendo wa nusu saa.
Gari ikasimama.
Lilikuwa ni pori dogo sana
maeneo ya Buswelu. Taa za ndani
ya gari zikawashwa, yule
mwanamama akavua juba lake.
Ana kwa ana na mzee Magayane.
Ile ndoto aliyodhani ameiota
ikageuka kweli, alikuwa
anatazamana na mwanamke
ambaye hakutegemea kuwa ipo
siku watakutana katika mazingira
hayo.
Yeye na mwanaye walikuwa na
hatia kubwa sana juu ya
mwanamama huyu na adhabu
waliyostahili haikuweza
kusemekana.
Hapakuwa na maongezi marefu
sana.
Mzee Magayane hakuwa na cha
kujibu.
Umauti ukamkumba katika namna
ya kusikitisha.
Kwanza alipigwa na rungu
kichwani, akapoteza fahamu.
Hakuweza kuzinduka tena. Visu
vilipenyeza akiwa ametulia tuli.
Hatimaye akatambulika na
wanafunzi waliokuwa wanawahi
shuleni kuhesabu namba akiwa
mfu.
James ambaye alikuwa ameandaa
majibu kadhaa ya kumpa baba
yake kwa lile swali alilouliza
hakuipata tena nafasih hiyo ya
kujaribu kujibu.
Na kamwe hakujua ni jibu gani
baba yake alikuwa anataka
kumpa.
Siku iliyofuata anapokea taarifa
hiyo mbaya.
Sasa yupo ndani ya ndege
akikaribia kutua jiji la Mwanza
kwa ajili ya mazishi.
****
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE
Ile ndoto aliyodhani ameiota
ikageuka kweli, alikuwa
anatazamana na mwanamke
ambaye hakutegemea kuwa ipo
siku watakutana katika mazingira
hayo.
Yeye na mwanaye walikuwa na
hatia kubwa sana juu ya
mwanamama huyu na adhabu
waliyostahili haikuweza
kusemekana.
Hapakuwa na maongezi marefu
sana.
Mzee Magayane hakuwa na cha
kujibu.
Umauti ukamkumba katika namna
ya kusikitisha.
Kwanza alipigwa na rungu
kichwani, akapoteza fahamu.
Hakuweza kuzinduka tena. Visu
vilipenyeza akiwa ametulia tuli.
Hatimaye akatambulika na
wanafunzi waliokuwa wanawahi
shuleni kuhesabu namba akiwa
mfu.
James ambaye alikuwa ameandaa
majibu kadhaa ya kumpa baba
yake kwa lile swali alilouliza
hakuipata tena nafasi hiyo ya
kujaribu kujibu.
Na kamwe hakujua ni jibu gani
baba yake alikuwa anataka
kumpa.
Siku iliyofuata anapokea taarifa
hiyo mbaya.
Sasa yupo ndani ya ndege
akikaribia kutua jiji la Mwanza
kwa ajili ya mazishi.
****
Kila mtu alikuwa na jibu lake juu
ya kifo cha bwana Magayane,
mzazi wa James, wapo
waliohusisha ujambazi na wengine
wakihisi kuwa kuna kisasi
kimejificha.
James na mkewe walibaki katika
sintofahamu. Hawakujua waseme
nini.
Ilikuwa inasikitisha.
Hatimaye maziko yakafanyika
huku baadhi ya ndugu wa karibu
wakiwa hawaamini kama ni kweli
bwana Magayane amekufa.
Akina mama walikuwa
wamejitanda kanga na vitenge
vyao wakiomboleza kwa kila aina
ya vilio.
Hatimaye mwili wa mzee
Magayane ukahifadhiwa katika
nyumba yake ya milele.
Akina mama wengi walilia kwa
uchungu, lakini kuna mmoja kati
yao hakuwa akilia kwa uchungu
bali alilia kutimiza wajibu.
Alikuwa amevalia miwani nyeusi
na alikuwa amejitanda kama
wanawake wengine. Na alikuwa
anafurahia jinsi shughuli ile
ilivyokuwa inaendelea. Alifurahi
kwa kuwa alipenda iwe hivyo na
imekuwa.
Mzee Magayane alizikwa nyuma
ya mbele ya nyumba yake jijini
Mwanza. Ndugu wa karibu na
majirani walilala hapo kwa siku
kadhaa.
Mwanamama mwenye miwani
nyeusi naye alibaki pale si kwa
ajili ya kulala lakini kuna jambo
alikuwa analihitaji.
Majira ya saa sita usiku aliondoka
baada ya kulitimiza.
Waliobaki kwa ajili ya kulala
hawakujua lolote. Hata
mwanamama aliyemuagiza kwa
jirani mdogo wa mwisho wa
James hakukumbuka kama
aliwahi kumtuma kwani alipitiwa
na usingizi na kisha kusahau,
huenda alichomuagiza hakikuwa
cha msingi sana.
Majira ya saa nne ukazuka msiba
mpya kabisa wa kushtukiza.
Castor, mdogo wa mwisho wa
James alikutwa ameuwawa kwa
kunyongwa shingo kisha mwili
wake kutupwa mtaroni.
Wasiwasi ukatanda. James
akapagawa.
Hofu ikamvagaa na kuanza
kumsulubisha, swali ambalo
marehemu baba yake alimuuliza
bila kumpa jibu likaanza kujirudia
kichwani.
Ni nani aliyeonekana Mwanza? Je
ndiye anayeua? Hakupata jibu.
Uchunguzi wa polisi uliishia
kubaini kuwa kuna alama za
mikono katika shingo ya
marehemu.
Alama hizo zilitakiwa kutumwa
jijini Dar es salaam kwa
uchunguzi zaidi.
Haikufahamika kama zilitumwa
ama la.
Castor naye akazikwa huku msiba
huu ukivuta watu wengi zaidi
kutokana na aina yenyewe ya kifo,
aliyetoka kumzika baba yake naye
amezikwa. Ilileta mvuto flani wa
kusikitisha.
Emmy akaanza kukosa imani na
familia iliyomuoa, akaanza
kujiuliza wana kisa gani na watu
gani hadi haya yanawatokea?
Wasije wakaniua na mimi? Alijipa
tahadhari lakini hakutaka
kumwomba James ruhusa ya
kutoweka jijini Mwanza na
kurejea Dar. Alihofia kumkwaza.
Mbaya zaidi alikuwa na pete
kidoleni tayari.
Eeh Mungu kwa nini haya
hayakutokea nikiwa katika
uchumba ili nigaili? Alisali kimya
kimya.
Emmy hakuwa amekomaa sana
kiakili katika suala la mahusiano,
kwanza ilikuwa ni mara yake ya
kwanza kumilikiwa na
mwanaume kwa ukaribu kiasi kile
tofauti na baba yake mdogo,
Lameck. Pili alikuwa na muda
mfupi sana katika ndoa.
Emmy akawaza kuachana na
James, hofu ikamtuma kufanya
hivyo.
Alikiri katika nafsi yake kuwa
katu hawezi kuamua kwa mdomo
wake kumtamkia kuwa waachane,
kwani hakuwa na sababu kubwa
ya kufanya vile.
Akiwa katika mawazo hayo
akamfikiria Jose B ambaye yeye
alimtambua kwa jina la Sam wa
pili. Aliamini kuwa iwapo
atakiuka masharti aliyoagizwa
ayatii basi utakuwa mwanzo wa
kijana huyu kutoboa siri ile
inayomkabili. Siri ya kufumaniwa
akiwa nyumba za kulala wageni
na mwanaume.
Emmy akaona kuwa hilo lilikuwa
jibu sahihi.
Akafanya tabasamu, akashika
simu yake aanze kumchanganya
Jose B.
Kabla hajafanya lolote akasikia
sauti ikinong’ona naye na
kumwambia.. ‘Lameck ni baba
yako.....aibu ya maisha’...kijasho
kikamtiririka na kugundua kuwa
alikuwa anataka kufanya jaribio la
kujisulubu mwenyewe.
Iwapo Lameck atagundulika kuwa
ndiye mwanaume ambaye alikuwa
naye katika chumba hicho
wakizini, jamii itawachukuliaje
ndugu hawa wa karibu.
Mama na baba watanitazama
vipi? Alijiuliza huku akiirudisha
simu mahala pake na kuuvunja
rasmi mpango wake wa kumtibua
Jose B ili aivuruge ndoa yake.
Jose B alikuwa ametulia tuli
katika nyumba ile ambayo
alikuwa ametimiza juma moja
tangu aimiliki.
Alikuwa akifanya utafiti wa kina
juu ya vifo viwili vya mfululizo.
Baba na mwana jijini Mwanza.
Taarifa za msiba huu Jose B
alizipata akiwa jijini Dar es
salaam katika nyumba ambayo
alikuwa amepangishiwa na Emmy
kutokana na kumiliki siri nzito
inayomuhusu mwanadada huyo.
Jose B akaweka hisia zake kwa
aidha ndugu wa karibu wa
Bibiana ama ndugu wa Deo wapo
katika kulipa kisasi. Aliamini
hivyo kutokana na tukio la James
kufanya mauaji jijini Mwanza.
Baada ya kuuziwa Kizuizi.
Jose B akatamani sana kuwajua
hawa ndugu wa Deo ama Bibiana
ili aingie nao katika biashara kwa
sababu tayari anaijua siri ya wao
kufanya mauaji.
Alijaribu kuvuta kumbukumbu
akakosa ndugu wa karibu wa
wawili hawa. Akasikitika kuikosa
biashara hii.
Ghafla akamkumbuka tena James,
akatamani kufanya naye biashara
nyingine lakini akaingiwa hofu
juu ya biashara ya kwanza
ambayo haikukamilika. Pia hii
misiba miwili mizito huenda
hatakuwa katika nafasi ya
kufanya biashara.
Akaamua kumpuuzia na kuwaza
mambo mengine.
****
BAADA YA MIEZI MIWILI.
Misiba ilianza kusahaulika,
familia ikaanza kujengeka katika
furaha tena. James aliondoka na
mdogo wake mmoja Mwanza na
kuishi naye jijini Dar es salaam.
Emmy naye akamchukua binamu
yake mdogo wakaishi naye.
Ikawa familia ya watu wanne.
Familia yenye furaha.
Emmy alikuwa ametimiza kila
kitu kwa Jose B wa ukweli
ikiwemo kumfungulia banda la
tigo pesa na Mpesa kandokando
ya jiji.
Jose B akajikita katika biashara
muda wa kufuatilia ya watu
ukapungua. Japo alipokuwa kazini
pia alijaribu kujua mawili matatu.
Jina lake likaendelea kukua japo
wanaomuita hawakujua kwanini
anaitwa Jose B waukweli.
Usumbufu wake kwa mke wa
James ukapungua kwa kiasi
kikubwa baada ya kuwa na uwezo
wa kujiingizia kipato.
James kwa upande wake, kupita
miezi miwili bila kusikia mauaji
yoyote yale walau alipata amani
katika moyo wake.
Mawazo yake juu ya kisasi
kinacholipwa yalianza kufutika
japo maswali ya kujiuliza
hayakuisha.
Kitumbo cha Emmy kilizidisha
furaha ndani ya nyumba.
Mama kitumbo. James alimtania
mkewe kila mara na walicheka.
Kasoro siku moja tu, James
alimtania mkewe na wala
hakucheka, mbaya zaidi alikuwa
ameegemea kochi katika namna
ya kuinama.
“Mama kitumbo.” James aliita.
Emmy kimya.
“We mama kitumbo
wewe....amka...” alisisitiza lakini
hakupata majibu bado palikuwa
kimya.
Watoto walikuwa shuleni pale
nyumbani alibakia Emmy peke
yake na sasa alikuwa hazungumzi,
japo alikuwa anapumua.
James akamkabili na kuanza
kumpapasa huku na kule. Emmy
alikuwa na kila dalili ya mtu
aliyezimia.
Mwanaume akachukua maamuzi.
Akambeba mkewe hadi katika
gari yake, hakutaka kupaparuka
wala kutaharuki maana kwa
kufanya hivyo angeweza kufanya
maamuzi mabovu kabisa.
Emmy akafikishwa hospitali ya
jirani.
Baada ya nusu saa alirejewa na
fahamu.
“Mama...mama...” alianza kuita.
James akashangaa kulikoni.
Emmy aliendelea kuangaza huku
na huko.
James alidhani ni
mang’amung’amu baada ya
kuzinduka, lakini Emmy alizidi
kuita mama.
Alipotulia alisimulia juu ya mkasa
aliokumbana nao kabla ya
kupoteza fahamu, mkasa wa
kustaajabisha. Mkasa wa
kusikitisha.
Mkasa unaoisha mama yake mzazi
akiwa ameupoteza uhai.
Kifo cha kutatanisha.
Baada ya kupigiwa simu
akaondoka na furaha bila
kumweleza mtu yeyote kitu, lakini
sasa yu katika jokofu linalopuliza
baridi kali, baridi isiyoweza
kustahimiliwa na yeyote aliye hai,
bali maiti tu.
Mama Emmy naye alikuwa maiti.
****
Hali ya joto kali la jijini Dar es
salaam lilimfanya aone hata
pangaboi lililokuwa linazunguka
kwa kasi kubwa halikuwa na
msaada wowote.
Alilitazama kwa makini jinsi
linavyojitahidi kuzunguka kwa
kasi ili mmiliki wake ajivunie
kuwa nalo lakini jitihada ziligonga
mwamba.
Ile hali ya kufananisha lile panga
boi na kitu hai zikamrudisha
nyuma na kuzitazama jitihada za
madaktari zilivyogonga mwamba
hadi hapo alipo kuwa kama
pangaboi lisilokuwa na maana.
Alijaribu kuyatumia vyema
maneno aliyoambiwa na
mwanasaikolojia, kiasi fulani
yalimsaidia lakini bado aliumia
moyoni.
Alijiona kuwa hana manufaa
kabisa katika jamii.
Akiwa kifua wazi alitoka nje na
kwenda kujiegesha katika pembe
moja chini ya mti wenye kivuli.
Akiwa chini ya mti huo jicho lake
likasafiri mita kadhaa akamuona
mwanadada akiwa amejisitiri kwa
kanga moja pekee akiwa anaanika
nguo. Kanga yake ilikuwa
imelowana na kunatiana na mwili
wake katika hali ambayo inaleta
matamanio kuitazama.
Hasira zikamzidia kwa hali hiyo
akajipigapiga kichwa chake
ukutani. Hasira zikatulia kidogo,
akahamisha macho na kutazama
upande mwingine, huku
akakutanisha macho yake na
rafiki yake wa siku nyingi.
Alikuwa amebeba mtoto.
Mtoto alionekana kuwa katika
mikono salama kabisa na alikuwa
anatabasamu kila aliporushwa juu
kisha kudakwa.
Hili nalo likamuumiza zaidi.
Akauma meno yake ili kuikabili
hasira, akafanikiwa.
Hakutaka kuendelea tena kukaa
pale nje. Akarejea katika pangaboi
lisilokuwa na msaada wa
kukabiliana na joto.
Akajifunika gubigubi akaanza
kulia.
Kilio cha mtu mzima.
Baadaye akapitiwa na usingizi.
Katika usingizi huo usiokuwa na
ladha aliwaza mambo kadhaa,
mambo yanayoweza kumpa amani
katika moyo wake.
Akafikiria jinsi ya kuipigania
furaha yake.
Akamkumbuka Devotha.
Devotha angeweza kuwa mwanzo
mzuri wa kuirejesha furaha yake.
Akasimama wima akavaa nguo
zake nadhifu. Hakuaga mtu
akatoweka.
Alipofika mahali pazuri kabisa
akatoa kitabu chake kidogo
akaibuka na namba za simu
akabofya zikaita.
Hakujitambulisha mapema.
Akatumia uumbaji wa maneno.
Devotha akaingia mtegoni.
Baada ya masaa mawili walikuwa
katika mazungumzo.
Mazungumzo yaliyoanza kwa
furaha tele, lakini baadaye
yakaleta msuguano. Devotha
hayupo tayari kukubaliana na
ukweli wakati mwanaume
anasisitiza kuwa lazima iwe vile.
Devotha anataharuki.
Mwanaume anaposhindwa kuizuia
taharuki ile, anaamua kuchukua
hatua.
Anamkubalia Devotha kwa lile
analolitaka, mwisho wanaagana.
Laiti Devotha angejua, asingefanya
maagano kwa kushikana mikono.
Kwa kutojua hili basi akaibariki
safari yake.
Hatimaye yule dereva taksi
aliyemchukua kumrejesha
nyumbani anatiwa hatiani, kwani
Devotha alikufa akiwa katika
teksi yake.
Taarifa inamfikia Emmy, taarifa
yenye utata.
Mwanamama aliyefahamika kwa
jina la Devotha John amekutwa
amekufa katika taksi. Hilo jina ni
sawa na la mama yake mzazi.
Taarifa ya pili kutoka kwa ndugu
wa karibu ikatoa uhakika,
Devotha aliyetajwa ni yuleyule
mama mzazi na rafiki kipenzi wa
Emmy, mama kitumbo akazimia.
James akamkuta katika hali ile.
Sasa wapo hospitali na Emmy
anasimulia.
UTATA MWINGINE...........
***Baada ya Baba James, na
mdogo wake James kutangulia
katika haki.......sasa ni mama
yake Emmy: Devotha. Anakufa
baada ya kugoma kukubaliana na
muuaji.....Muuaji alitaka nini??
Na kivipi awe na makubaliano na
muuaji??
***Je muuaji huyu ana mahusiano
na muuaji wa kwanza??
***Jose B amejipumzisha na
umbea na ushakunaku....huenda
kwa kuwa yupo mbali na
Mwanza....haya tukio hili
linatokea jijini alipo...kipi
kitakuwa bora kwake..banda la
biashara ama umbea huu
unaomuingizia mamilioni KILA
KUKICHA??
***Mwanamke aliyeua jijini
Mwanza...anataka nini?? Na
mbona yu kimya tena???
Unataka kujua kuna siri gani
katika KIZUIZI.....usikose hata
episode moja utapata majibu........
ITAENDELEA..
 
SEHEMU YA KUMI NA TANO
Alipofika mahali pazuri kabisa
akatoa kitabu chake kidogo
akaibuka na namba za simu
akabofya zikaita.
Hakujitambulisha mapema.
Akatumia uumbaji wa maneno.
Devotha akaingia mtegoni.
Baada ya masaa mawili walikuwa
katika mazungumzo.
Mazungumzo yaliyoanza kwa
furaha tele, lakini baadaye
yakaleta msuguano. Devotha
hayupo tayari kukubaliana na
ukweli wakati mwanaume
anasisitiza kuwa lazima iwe vile.
Devotha anataharuki.
Mwanaume anaposhindwa kuizuia
taharuki ile, anaamua
kuchukua hatua.
Anamkubalia Devotha kwa lile
analolitaka, mwisho wanaagana.
Laiti Devotha angejua, asingefanya
maagano kwa kushikana mikono.
Kwa kutojua hili basi akaibariki
safari yake.
Hatimaye yule dereva taksi
aliyemchukua kumrejesha
nyumbani anatiwa hatiani, kwani
Devotha alikufa akiwa katika
teksi yake.
Taarifa inamfikia Emmy, taarifa
yenye utata.
Mwanamama aliyefahamika kwa
jina la Devotha John amekutwa
amekufa katika taksi. Hilo jina ni
sawa na la mama yake mzazi.
Taarifa ya pili kutoka kwa ndugu
wa karibu ikatoa uhakika,
Devotha aliyetajwa ni yuleyule
mama mzazi na rafiki kipenzi wa
Emmy, mama kitumbo akazimia.
James akamkuta katika hali ile.
Sasa wapo hospitali na Emmy
anasimulia.
UTATA MWINGINE...........
****
Hakuna chozi linaloweza kubadili
msiba kuwa sherehe, na hakuna
kilio kinachoweza kumbadili
aliyekufa aweze kurejea.
Kilio huwa ishara ya uchungu,
kisha maisha yanaendelea katika
hali ya utofauti kwa muda mrefu
kisha huzoeleka.
Emmy hakupata mtu sahihi wa
kumtuliza, kila aliyejaribu
kumtuliza ni sawasawa alikuwa
anampigia Kondoo zeze ili akate
mauno, jambo lisilowezekanika.
Mama yake alikuwa amekufa kwa
kushambuliwa na sumu kali iuayo
mara moja baada ya kupenya
katika ngozi.
Mtu aliyejaribu kwa kiasi fulani
kumtuliza Emmy japokuwa sio
sana alikuwa ni mwanaume
shujaa aliyeyakabidhi maisha yake
kutetea wengine na kuwalinda.
Mwanajeshi kamili Lameck John
Sulube.
Emmy alitulia kwa sababu
hakuwa na taarifa ya marejeo ya
mwanajeshi huyo, na pia ile hatia
ya kuzini nje ya ndoa ikaibuka
upya. Akausahau msiba kwa
sekunde kadhaa. Maneno ya
Lameck yalikuwa yaleyale ‘Ni
mipango ya Mungu!! Usilie sana
utakufuru!!, Bwana ametoa na
bwana ametwaa!!’. Maneno
ambayo huwa hayana maana kwa
mfiwa.
Ukaribu wa Emmy na Lameck
Sulube haukumshtua mtu yeyote
ambaye aliijua kwa uchache
familia ile. Waliwatambua hawa
kuwa ni mtu na baba yake
mdogo.
Hata James mumewe hakutilia
mashaka yoyote. Alikuwa anamjua
vyema Lameck, anamfahamu fika
kwani wakati anamrandiarandia
Emmy aliwahi kukunjana mashati
na huyu bwana. Lakini hakuchoka
hadi alipofanikiwa kumuoa na
sasa ni mjamzito.
Ila jicho moja lilikuwa na
mashaka na ukaribu ule.
Akiwa amejivika suti nyeusi
iliyomkaa vyema kijana huyu
anayekimbilia miaka ishirini na
mbili, kichwa chake kikiwa na
nywele fupi zilizopakwa mafuta
ya kung’ara, kiatu cha bei ghali
kikiuvaa mguu wake. Kijana huyu
alikuwa mtulivu sana, leso yake
mkononi akipambana na jasho
ambalo linataka kumharibia
mwonekano wake. Mkono mmoja
alikuwa na funguo zilizofanana na
za gari.nani anajua huenda
nayeye alikuwa ameegesha gari
lake nje ya nyumba.
Kwa kumtazama usingeweza
kudhania yupo katika dunia
nyingine, akijadili mambo yake
tofauti kabisa na msiba
unaoendelea.
Zilipigwa nyimbo za kusihi watu
waandae nyoyo zao kwa sababu
hatujui saa wala dakika ya
mwisho wetu, yeye hakuzisikia
bali alihisi anapigiwa makelele na
wachina wanaoimba nyimbo zao
kwa lugha yao ngumu.
Hatimaye ukafika wakati wa
kutoa heshima za mwisho kwa
marehemu.
Kutokana na uwingi wa watu
katika msiba huu, ilibidi
mwongozaji atoe utaratibu
maalumu kabisa wa kuuaga mwili
wa marehemu Devotha.
Alianza kwa kuiita familia ya
marehemu, hapa akawaita watoto
na baba. Wakaaga.
Dada, mawifi, shangazi, mama
wadogo. Wakaaga.
Baba wadogo, baba wakubwa,
mashemeji, wajomba, kaka. Nao
wakajongea waweze kuaga.
Yule kijana aliyekuwa amejikita
katika kujipangusa jasho
akasitisha zoezi lile, akaiacha
jasho itiririke, akajisahau kuwa
alikuwa amevaa suti, akaanza
kuhaha huku na huko.
Akazidi kujiuliza ile sura kwa nini
inamvutia.
Mwanzoni alidhani kuwa ni mteja
mmojawapo aliyewahi kufika
katika banda lake kwa ajili ya
huduma za kuweka na kutoa
pesa.
Lakini sasa akili ikamruka
hakutaka kuamini kuwa yule ni
kama anavyomdhani.
“Samahani kaka mambo vipi. U
mwenyeji wa maeneo haya.”
Aliuliza kwa sauti tulivu, akiwa
amelitoa koti la suti na kulitupia
begani.
Jose B waukweli anaingia kazini.
“Kiasi fulani kwani vipi?.”
“Hivi yule jamaa aliyevaa kadeti
ndiye Thomas, mdogo wake na
marehemu?” alihoji kiujanja Jose
B.
Mng’aro wake na mavazi yake
yakamfanya aheshimike.
Yule bwana hakuwa anajua sana
juu ya ile familia. Lakini alimuita
mwenye ukaribu na familia ile.
Jose B akauliza swali lilelile.
Akapatiwa jibu kuwa yule anaitwa
Lameck, ni shemeji wa
marehemu.
“Na yule mwanamke
waliyekuwanaye ni kama mtoto
wake.” Alijibu hata ambayo
hajaulizwa.
Na hivyo ndivyo Jose B alikuwa
anapenda. Ili ajue mengi.
Kuna jambo hapa!! Si bure.
Aliwazua Jose, huku akijituliza na
kujiuliza inakuwaje amhisi vibaya
yule bwana.
Baada ya ndugu wa karibu
kumaliza kuaga. Wasindikizaji
wengine nao waliaga.
Jose B hakwenda kuaga, akabaki
kumfuatilia Lameck na nyendo
zake.
Mara Lameck akakutana na
kipande cha mtu, kilikuwa
kinampa pole.
Jose B akashtuka, kile kipande
alikuwa anakifahamu vyema.
Aliwahi kukiona maeneo fulani
jijini Dar es salaam.
Ubungo. Zamzam guest house.
Kipande kile cha mtu kilikuja
kumpokea Emmy, kikamuingiza
ndani kisha kikatoka nje.
Sasa ikajengeka picha ya mwisho
ya kumaliza utata kwa Jose B
waukweli mshakunaku wa
kimataifa. Yule aliyebaki ndani
pamoja na Emmy ndiye huyu
anayeitwa baba mdogo.
Jose B akacheka kisha
akamshukuru Mungu kwa
kumbariki na kipaji hicho cha
kipekee.
Kwa hiyo baba na mwana
wanamahusiano ya
kimapenzi....eeh!! Mungu
ameumba dunia na maajabu yake,
ndo maana nikashangaa kivipi
napewa malipo makubwa hivyo.
Kumbe ni baba na mwana. Jose B
akamaliza kwa kicheko kifupi.
Safari ya kuelekea kuzika
ikafuata.
Jose B alikuwa amekuja na gari
ndogo, ilikuwa ngumu kujua
iwapo ni yake ama amekodi,
aliingia katika gari na kumuamuru
dereva aondoe.
Alifungulia mziki wa taratibu kwa
sauti ya chini.
Wakati mziki ukiendelea, Jose B
akaanza kumfikiria upya Emmy,
akajisahaul,isha kuwa
mwanamama huyu kwa sasa yupo
katika machungu makubwa ya
kumpoteza mama yake mpenzi.
Jose B akamuwaza kama
mwanamke ambaye amejaribu
kumtapeli ama wamefanya
biashara isiyokuwa sahihi.
“Mimi nilielewana naye kuwa
anipe milioni saba ama nyumba
nikidhani kuwa alikuwa na mtu
wa kawaida tu wakimsaliti James,
lakini kumbe alikuwa na baba
mdogo? Hii biashara kamwe
nisingeweza kuifanya kwa milioni
saba au kinyumba kile, hii ni
hasara tena hasara kubwa tu.
Yaani mtu na baba yake niiuze
kwa milioni saba? Si bora hata
nisingeiuza kabisa. Mtu na baba
yake unadhani mchezo!! Yaani
hapa sikubali kudhulumiwa
kiwepesi wepesi. Lazima haki
itendeke hapa.” Aliwaza Jose B
kwa hisia kali sana kama mtu
aliyewekeza mahali kisha
akadhulumiwa pesa yake halali.
Jose B hakuwekeza chochote!! Cha
ajabu analalamika.
Au huyo baba mdogo amsaidie
huu mzigo, kweli ngoja nimtwike
na yeye mzigo wa kulipia hasara
niliyoingia. Alibadili mawazo yake
Jose B, akaugeuzia upepo kwa
Lameck Sulube.
****
Laiti usingekuwa ukakamavu wa
jeshi, huenda Lameck angeweza
kuanguka wakati wa kutupia
mchanga wa mwisho katika
kaburi la Devotha, mama yake
Emmy.
Ama hakika damu ni nzito
kushinda maji.
Lameck kwa mkono wake alikuwa
ameteketeza maadui wengi
waliothubutu kukatiza mbele
yake katika vita huko Sudani.
Wengine aliwalipua vichwani na
wengine aliwapasua matumbo
kwa bunduki. Hayo yote yalikuwa
ya kawaida kwake, iweje kifo cha
mtu huyu kimguse kwa kiasi
hicho.
Alikuwa nyumbani kwake wakati
akiwaza haya.
Lakini ni ubishi wake..
Lameck aliyakumbuka
mazungumzo yake ya mwisho na
mama yake Emmy katika hoteli
iliyopo pembebi kidogo ya jiji.
Mazungumzo nyororo yaliyoishia
pabaya baada ya mada mpya
kuletwa mezani.
Mtu na shemeji yake wakaanza
kulumbana baada ya Lameck
kumgusia mama Emmy kuwa
anampenda mwanaye sana.
Kumpenda halikuwa tatizo,
Lameck akaleta hoja ya nyongeza
kuwa wamewahi kuwa na
mahusiano ya kimapenzi tangu
wakiwa watoto.
“Mnaendelea hadi sasa?” Devotha
alimuuliza.
Lameck akapinga. Devotha
akashusha pumzi kali.
Lameck akaendelea kuikaribia
maana aliyoitaka.
Akamgusia Devotha kuwa Emmy
ameolewa akiwa si bikra.
“Acha upumbavu wewe...mbona
mumewe alileta shukrani ng’ombe
mbili nyumbani kwa kumkuta
Emmy akiwa mzima na usichana
wake huko Uganda?” Alijibu kwa
kebehi kiasi fulani huku taharuki
ikianza kuchukua mkondo.
Lameck akashtuka, hakutegemea
kusikia hayo kutoka kwa yule
mama. Kumbe James alienda
kujisifu. Kujisifu kwa Bikra feki
iliyotengenezwa na daktari
mashuhuri Lameck John Sulube,
kwa kutumia Shabu, Ndimu na
kisha kuiweka makini zaidi
ikawekewa dondoo za sabuni aina
ya KAISIKI. James akadanganyika
na kutoa ng’ombe mbili.
“Au nimpigie James simu hapa
akuumbue??” aliongezea yule
mama Lameck akiwa bado kimya.
“Haina maana shemeji kufanya
hivyo” Lameck aliweka nidhamu
mbele.
“Kumbe ulichoniitia.”
“Kuna jambo la ziada....”
“Lipi?” aliuliza kisharishari.
“Ni kuhusu Emmy na mimi,
nimeamua nianze kujadili na
wewe kiutu uzima kisha
tutamuita Emmy.......” kabla
hajaendelea yule mama mweupe
ambaye uso wake ulikuwa
umeanza kuwa mwekundu
kutokana na hasira alimkatisha,
“Shem Lameck naomba
tusivunjiane heshima, yaani mimi
wewe na mwanangu tukae
kuzungumzia bikra mara sijui
mlikuwa na mahusiano utotoni,
unamshutumu mwanangu hana
bikra, hiyo bikra uliitoa wewe
mpuuzi mkubwa, na kwa taarifa
yako ni kwamba Emmy ni mama
mtarajiwa, ana kitoto kinaimba
kwa furaha tumboni, sitaki kabisa
umkere mwanangu, nenda
ukapambane na wanajeshi
wenzako huko si mwanangu....jitu
zima hata aibu huna na nitaenda
kumwambia mume
wake....mshenzi wewe....yaani
umekosa wanawake mtaani huko
unakuja kujishebedua kwa mtoto
wako loooh aibu kweli na
nitakushtaki ukiendelea nasema
nitakushtaki Lameck...ukome,
umkome mwanangu” mama
alipaza sauti, ikawa kazi ya
Lameck kumsihi mama huyu
asiongee sauti ya juu.
Mara akasimama aweze
kuondoka. Lameck akamdaka
mkono, akaanza kumlaghai kuwa
alikuwa anatania, lakini yule
mama alikubali kinafiki tu kuwa
hawezi kuyafikisha mahali popote
maneno yale.
Lameck kwa kumsoma macho
yake akaugundua unafiki wake.
Lameck alikuwa amechukizwa
sana na maneno makali kutoka
kwa yule mama, hasahasa maneno
ya mwisho ya kumtishia
kumshtaki. Lameck akaongozwa
na hasira, na kwa kujilinda siri ile
isitoke mapema.
Akatumia msemo wa heri mmoja
afe wengi wapone.
Kitendo cha sekunde kadhaa
kutoka kwa mwanajeshi huyu.
Sumu ikaugusa mwili wa mama
Emmy.
Yeye akanawa upesi upesi.
Akarejea nyumbani, taarifa
aliyoitegemea ndiyo ambayo
aliipata kuwa mama Emmy
alikufa akiwa katika gari
iliyokuwa inamrudisha nyumbani
akitokea hotelini. Bila kujulikana
na nini alikuwa anafanya.
Sasa amezikwa tayari na ni usiku
mwingine Lameck anawaza
yaliyotokea.
Lameck ameua.
***LAMECK amemuua DEVOTHA
ili kujilinda
asichafuliwe...amemuua kabla
hajamwambia ni kipi alichomwitia
wajadili.
***JOSE B anapata kitu kipya
kabisa msibani, kumbe LAMECK
na EMMY ni ndugu wa karibu.
Dili jingine!!
***LAMECK anataka nini kwa
EMMY.....na nini hatma ya JOSE B
kumpa mzigo LAMECK aubebe,
kumbuka JOSE B hajui iwapo
LAMECK ni mwanajeshi.Itaendelea
 
Back
Top Bottom