Hadithi: Kisu chenye mpini mwekundu

Hadithi: Kisu chenye mpini mwekundu

SEHEMU YA KUMI NA SITA
Beda akashusha pumzi bila kuongea lolote.
“Usijali lakini kwanza inabidi nipate mbinu nzuri ya
kumuondoa mke wangu.” Akaongea baada ya
kukaa kimya dakika kadhaa, huku akishangaa jinsi
siku moja ilivyotosha kumfanya awe dhaifu kwa
mwanamke aliyeokotana naye baa. Akashangaa
zaidi baada ya kugundua kuwa alikuwa na dhamira
ya dhati ya kumuondoa mkewe Vick pale
nyumbani.
* * *

Siku ya tatu Vick alikuwa hajamtia Beda machoni.
Mabadiliko haya ya Beda hayakumuudhi Vick tu,
bali hata mama yake alichukia. Saa 1.36 Usiku
Beda alifika nyumbani. Hakuzungumza na yeyote
akaacha fedha za matumizi mezani kisha
akaondoka huku akiwa na kimkoba ambacho
aliweka sare zake za kazi. Vick alianza kulia.
Kilikuwa kilio kipya mtu ambaye amempigania
maisha yake yote leo anamgeuka? Alijiuliza huku
akisikia uchungu. Mama yake Beda alikuwa
anajitahidi kumbembeleza Vick. Vero hakuelewa
kitu, umri wake mdogo ulimuwezesha kutafsiri
baadhi ya mambo huku mengine yakiwa kama
fumbo kwake.
Maisha yalibadilika. Hakuna alichokosa, lakini
mumewe hakuonekana nyumbani. Alihuzunika kwa
kukosa mapenzi ya mume wake. Mapenzi haya
aliyoyapigania miaka na miaka leo yamegeuka
shubiri. Alilia kwa nguvu zake zote, kilio
hakikusaidia kitu. Alihuzunika lakini bado huzuni
yake haikuwa suluhisho la matatizo yake Mwisho
akaamua kukaa kimya ili aone matokeo yake.
Upande wa pili Inspekta Beda alikuwa amezama
kwenye penzi jipya la Mwanamke yule ambaye
kiumri alikaribiana na mama yake mzazi.
Hakukuwa na uwiano wa umri kati yao. Yule mama
alikuwa na watoto watatu. Lucy, Koku na Fredi.
“Hivi unaonaje tukihamia kwenye nyumba yako
kule Kinondoni?” Aliuliza mama Lucy.
“Utaweza kukaa na mke mwenzio?” Aliuliza
Inspekta Beda.
“Hakuna tatizo kuliko kukaa huku kwenye nyumba
ya kupanga nimechoka maneno na masimango.”
“Mh. Sawa lakini ngoja kwanza nijadiliane na mke
mwenzio.” Alijibu Inspekta Beda.
Mama Lucy alifurahi moyoni mwake huku akiwa na
dhamira ya kumteka kabisa Beda.
“Hivi unafikiri atakubali?” Aliuliza mama Lucy.
“Sina uhakika lakini wacha nijaribu.”
“Inaelekea unampenda sana mkeo.”
“Si kwamba nampenda ni yeye ndio kajipendekeza
kwangu nilimsaidia kutoka kwenye kundi la
ombaomba nikamhurumia nikaamua nimuoe.”
“Kwani yule mtoto si wako?”
“Ni wa kwangu nilimpa ujauzito kabla hajawa
ombaomba.”
“Kwani ilikuwaje mpaka akawa ombaomba.”
“Tuache hizo stori dear kwani kwa sasa hazina
maana.” Aliongea hivyo huku akiwa amesimama
tena na kujiandaa kuondoka.
Baada ya kuondoka kwa mama Lucy akaenda moja
kwa moja nyumbani kwake ambako alikutana na
mkewe na kumweleza mpango mzima.
“Vick mpenzi nina neno nataka kuongea na wewe.”
“Ongea tu mume wangu.”
“Nataka ujue wazi kuwa nakupenda lakini pamoja
na hilo nimeamua nikuletee dada yako hapa
nyumbai.”
“Dada yangu yupi?.” Aliuliza Vick huku akionyesha
wazi kushangazwa na kauli hiyo.
“Namaanisha kuwa nataka kumleta mwanamke
mwenzio hapa nyumbani.”
“Mh. Ndio maana ukatanguliza maneno ya
kunilaghai mara nakupenda sijui hivi na vile……
sawa lakini kumbuka tulikotoka Beda.”
“Najua tumetoka mbali lakini lazima ujue maisha ni
safari na hii ni sehemu ya safari.”
“Kwa hiyo ikiwa safari unaweza kulifanya lolote
linalokufurahisha huku ukiwakera wenzio?”
“Sio hivyo mpenzi najua unahisi kuwa sitafanya
usawa. Naomba uelewe wazi kuwa nitakujali na
kukuthamini.”
“Ndio najua utanithamini kwani dalili si nimeanza
kuziona, umelala nje siku tatu bila taarifa nafikiri
ndio thamani unayoikusudia.”
Inspekta akainamisha kichwa kwa hasira.
Vick akaenda kwa mama Beda na kumsimulia
mawazo ya mwanawe. Mama Beda huku akiwa
mwenye hasira aliamua kumwita mwanawe na
kumkalisha.
“Mwanangu Beda, naomba ukae unisikilize…”Al
iongea mama Beda mbele ya mwanae na Vick.
“Hii dunia mwanangu…..”
“Ongea basi mama si unanichanganya tu. Hii dunia
kuna asiyeijua?” Alikuja juu Beda bila kujua
anayeongea naye ni mama yake.
“Mwanangu mimi mama yako hutakiwi kunijibu
hivyo.”
“Kama unaongea upuuzi lazima nikujibu vibaya
lazima ujue kuwa wewe ni mama yangu una
mipaka yako najua sana Vick kakusimulia kila kitu
na hayo ni maamuzi yangu kama hataki huyo Vick
aondoke aniachie nyumba yangu hajachangia hata
shilingi.” Aliongea Inspekta Beda kwa hasira.
“Mwanangu mbona umebadilika.”
“Mama, kama umechoka kukaa hapa ndani na
wewe ondoka, sikujua kama mama yangu ni
mkorofi kiasi hiki kumbe ndio maana ulikuwa
uligombana na majirani kipindi kile na inawezekana
kuna ukweli wewe ndio umesababisha kifo cha
baba yangu.”
“Mwanangu maneno gani hayo unaniambia?”
Aliuliza mama Beda huku akianza kutokwa
machozi. Bila kujali Beda akaendelea kumshushia
mvua ya maneno yaliyomtia uchungu.
Mama Beda akashindwa kuvumilia maneno
yalikuwa makali sana. Akaanza kulia huku
akirudiwa na kumbukumbu za kipindi cha maisha
magumu alichomlea Beda. Ikawa zamu ya Vick
kumbembeleza mama Beda. Beda alikuwa
amebadilika sana.
* * *

“Vipi dear umefanikisha.” Aliuliza Mama Lucy huku
akimrembulia macho Beda.
“Amekataa tena hata mama amekataa.” Alijibu
Beda huku akikuna kichwa.
“Kina mama si watu wa kuwasikiliza sana kwani
umri wao unawafanya wawe hivyo.”
“Nimemfokea sana nimemwambia aache kuingilia
mambo yangu.”
“Wewe ndio mwanaume bwana, askari unatakiwa
kuwa mkakamavu hata nyumbani kwako.”
Aliendelea kusisitiza Mama Lucy.
“Kwa hiyo tujiandae kuhamia huko?”
“Eeh. Weka kila kitu sawa siku ikifika tunakuja
kukusanya na kupeleka nyumbani.” Alisisitiza Beda
huku akionyesha wazi kufurahia.
“Ndiyo maana nakupenda ooh, kumbe unanijali
mpenzi.” Aliongea mama Lucy huku akimkumbatia
na kumpiga busu la kinafiki Beda.
“Nisubiri mpenzi natoka kidogo.” Alisikika mama
Lucy huku akitoka mle chumbani.
Akaenda moja kwa moja chumbani kwa Lucy na
Koku, wote wawili walikuwa wanasoma shule ya
sekondari ya Jangwani. Watoto wa mama Lucy
wote watatu walikuwa wa baba tofauti huku
kukiwa hakuna uhakika kuhusu baba wa watoto
wale. Isingeweza kusahaulika jinsi mama Lucy
alivyogonganisha wanaume wawili huku kila mmoja
akifahamu kuwa yeye ndiye baba wa Lucy, baada
ya kufahamiana wale wanaume hawakuwa na
sababu ya kugombana kila mmoja akaingia njia
yake huku wakimwachia mama Lucy jukumu la
kumlea mwanae peke yake.
Ni huyu mama Lucy ambaye kwa tamaa yake ya
fedha alithubutu kumuua baba wa kifungua mimba
wake Fredi kwa matumaini ya kurithi mali zake,
hakuamini pale alipowaona ndugu wakija na kuuza
nyumba baada ya kufuatilia ikabainika kuwa ile
nyumba haikuwa ya mumewe ilikuwa ni ya mama
yake mdogo mumewe, akakosa vyote.
Huyu ndiye mama Lucy ambaye historia yake
imejaa machafu huku mikono yake ikiwa na damu
ya baba Fredi. Mtoto wake wa mwisho alikuwa
hajulikani kabisa baba yake. Aibu.
“Lucy…lucy…” Aliita mama Lucy alipofika mlangoni.
“Bee mama.” Aliitika Lucy huku akishtushwa na
ujio huo wa mama yake kwani ilikuwa saa nane
usiku. Lucy akasogea mlangoni na kuanza kuongea
na mama yake.
“Mwanangu hili ----- limekubali kunihamishia
nyumbani kwake, kesho mwambieni kaka yenu
arudishe chumba kwani tumepata sehemu ya
kula.” Lucy akatabasamu huku akipeana mkono na
mama yake.
“Poa mama.” Alisikika Lucy huku akirudi chumbani.
* * *

Baada ya mwezi mmoja Vick alianza kuhisi dalili
za uja uzito. Hali hiyo ilimsumbua sana kwani
hakupata mapenzi yaliyotakiwa kutoka kwa
mumewe. Ni siku hii ambayo ilikuwa pigo
lisiloweza kusahaulika katika maisha ya Vick.
Akiwa amekaa barazani na mama Beda Akaliona
lori kubwa likifika pale nyumbani kwao. Inspekta
Beda aliteremka akiongozana na mwanamke
mweupe.
“Mama Vero. Nafikiri nilikueleza mapema kuwa
kuna mwenzako anakuja hapa….” Vero hakuweza
kumaliza kusikiliza ile kauli akaangua kilio kikubwa
ambacho hata hivyo kwa Beda ilikuwa kama
kumpigia mbuzi gitaa. Mama Beda hakuongea kitu
aliogopa sana matusi ya mwanae. Akawa
anatazama kila linalotendeka kwa uchungu
mkubwa. Vyombo vya Vick vikahamishwa na
kuwekwa chumba cha uani. Ilikuwa ni dharau
kubwa kabisa. Hata Vero alilia akaambulia makofi
mawili matatu kutoka kwa baba yake.
Furaha ilipotea kabisa ndani ya familia hii baada
ya kuhamia mwanamke huyu ambaye alionekana
wazi kuwa mshari.
Kadri miezi ilivyozidi kusonga mbele ndivyo mama
Beda alivyoendelea kukosa uvumilivu. Alianza
kupata upya mateso ambayo alishayasahau. Kila
alipokumbuka shida alizozipata ili mwanae asome
machozi yalimtoka. Hali yake kiafya ikaanza
kubadilika. Mara kwa mara alisumbuliwa na tatizo
la kifua na malaria. Beda hakuwa na muda wa
kujua afya ya mama yake wala Vick ambaye
alikuwa mjamzito.
Siku za kujifungua zikafika. Vick akajifungua
salama mtoto wa kike ambaye aliitwa Sara. Bado
Beda hakuonyesha mapenzi yoyote. Mara nyingi
aliacha fedha za matumizi bila hata kumuona
mtoto.
Watoto wa yule mama wakahamia pale nyumbani
kwa Beda. Toka wahamie wale watoto chuki
ikazidi. Ajabu. Beda akaonyesha mapenzi makubwa
kwa wale watoto kuliko Vero ambaye ni mtoto
wake wa kumzaa.
* * *
Ingawa alikuwa mdogo lakini alikuwa na uwezo wa
kuelewa mambo. Vero alikuwa akiliona kila
lililokuwa linatendeka. Mara nyingi wale watoto
watatu walipenda kukaa faragha na mama yao.
Hali hii ilisababisha Vero aanze mtindo wa
kuwavizia na kuwasikiliza kwa siri walichokuwa
wananong’ona. Mara nyingi alikuwa anamfikishia
mama yake. Mengi yalikuwa ni maneno mabaya na
ya kashfa.
Mama Beda alishachoka mazingira ya pale
akanong’ona kitu na Vick kisha akabeba mizigo
yake akaondoka pale nyumbani. Hali yake ya
kiafya haikuwa nzuri lakini alilazimika kuondoka.
Akaenda alikokujua yeye na Vick ambaye alimuaga.
Alishindwa kwa sababu alikuwa anafanyiwa vitimbi
vya chini chini na mwanamke aliyemleta Beda.
Kilichomkera zaidi ni kuhisi kudhalilika kwani
kiumri alihisi kutotofautiana sana na yule
mwanamke. Labda tofauti ni mfumo wa
kulazimisha ujana kwa kutumia vipodozi ndio
uliomfanya mama Lucy aonekane kama msichana.
Ajabu. Kuondoka kwa mama yake bado
hakukumzindua Beda. Mara nyingi alifurahia
maisha na mama Lucy kwa vinywaji na starehe
mbalimbali. Ilikuwa ni kawaida yake kwenda
kwenye baa maarufu na sehemu nyinginezo
zilizosifika kwa starehe.
Siku moja Vero alipita karibu na chumba
alichokuwa analala Koku na Lucy akawasikia
wakinong’ona na mama yao.
“Kwa hiyo itakuwaje?”Alisikia sauti ya Koku
ikiuliza.
“Tumemwagiza Fred akanunue ile sumu kisha
tutamwekea yule mama, tukizubaa atatuzidi kete.”
“Eee. Dunia yenyewe tunatakiwa kuchangamka
tukilaza damu yule mama atatusumbua baadaye si
unaona anazidi kuongeza vitoto hapa.” Alilalamika
Lucy.
Kauli ile ilimchanganya kidogo Vero lakini kutokana
na utoto akajikuta akiipuuza.
Siku zikakatika, hatimaye ikafika ile siku mbaya
kuliko zote. Mama Vero alikuwa anaoga bafuni.
Aliporudi akafunua ndoo yake ya maji ya kunywa.
Alipokunywa tu akaanza kuhisi tofauti. Hali ilikuwa
mbaya. Inspekta Beda alipofika bado hakumjali.
Kama alivyofanya mama Beda, naye akaamua
kuondoka pale ndani. Akatoroka na mwanae Vero
na Sara ambaye alikuwa na umri wa miezi miwili
tu. Lakini wakati anatoroka alikuwa anasumbuliwa
na tumbo ambalo alihisi kuwa ni sumu baada ya
kudokezwa na Vero wakati tukio limeshatokea.

ITAENDELEA!!!
 
RIWAYA: KISU CHENYE MPINI MWEKUNDU

SEHEMU YA KUMI NA SABA

Inspekta Beda alipofika bado hakumjali. Kama
alivyofanya mama Beda, naye akaamua kuondoka
pale ndani. Akatoroka na mwanae Vero na Sara
ambaye alikuwa na umri wa miezi miwili tu. Lakini
wakati anatoroka alikuwa anasumbuliwa na tumbo
ambalo alihisi kuwa ni sumu baada ya kudokezwa
na Vero wakati tukio limeshatokea.
*****

Veronika akaacha kusimulia na kumgeukia Sara
ambaye alikuwa analia. “Nafikiri sasa utakuwa
umejua kwanini nimemuua Lucy.”
“Kuhusu Lucy nimejua, bado sijajua mama yangu
na bibi yangu ilikuwaje na pia ningependa
kufahamu kwanini ulimuua mama Pili”
“Swali zuri, lakini kwanza naomba nikueleze jinsi
nilivyoingia kwenye maisha ya uchangudoa mpaka
nikafikia uamuzi wa kuwa muuaji na kumuua
mama Pili.” Akatulia kidogo na kumkazia macho
mdogo wake ambaye alishaanza kumuamini na
kumuelewa dada yake.
“Habari ya mama na bibi naomba niiweke kiporo
kwanza. Katika kutafuta maisha ndipo nikahamia
kwa mama mmoja mfanyabiashara aliyekuwa
anaishi Kawe. Nikafanya kazi za ndani huko huku
wewe ukiwa mgongoni kwangu nililazimika
kuwaongopea kuwa sisi ni watoto yatima bahati
yule mama hakuwa mdadisi......”
“…….Nikakaa kwa yule mama hadi ulipotimiza
miaka mitano nikaagana na yule mama baada ya
kupata ahadi ya ajira yenye malipo zaidi kutoka
kwa mama mwingine ambaye alikuwa nyumba ya
jirani, sikujua nasema sikujua kumbe yule mama
alikuwa nyoka kabisa tena nyoka mwenye sumu
kali kwani sikuwa wa kwanza kuangukia katika
mikono ya mama pili kupitia ushawishi wa huyu
mama.”
“…..Namkumbuka vizuri yule mama anaitwa mama
Mwazani naye pia yupo kwenye mpango wangu
akipona bahati yake, huyu ndiye aliyenikutanisha
na mama Pili huku akifahamu fika lengo la mama
Pili. Nakumbuka siku aliyonipeleka mama Pili
alifurahi sana. Akampa pesa ambazo zilikuwa ni
ujira wake kwa kunipeleka pale. Sikumbuki ni
miaka mingapi nilifanya kazi kabla ya kuingizwa
rasmi kwenye mtandao wa machangudoa.
Ninachokumbuka huu ni mwaka wa tano au wa
sita toka niingie kwenye biashara hii.”
“Lakini dada hujanipa sababu za kutosha za
kumuua Mama Pili.”
“Bado sijamaliza mdogo wangu, nina sababu zaidi
ya moja za kumuua mama Pili….”
“……Kama unakumbukumbu ukiwa na miaka saba
uliwahi kutekwa na wanaume watatu wakakufanyia
mambo machafu ambayo yalikuathiri sana
kisaikolojia ule ulikuwa ni mpango wa mama Pili na
alilipwa pesa nyingi sana, pili tulikubaliana
akusomeshe, nasikitika hajatekeleza nasikia
uchungu mdogo wangu kama si kukufundisha
mwenyewe basi hata kusoma na kuandika
ungekuwa hujui. Tatu ni yeye ndiye aliyenilazimisha
kwa nguvu kuingia kwenye biashara ya ukahaba
kwani alitafuta watu wakanifungia chumbani kwa
kushirikiana na mwanae Pili.(kipande hicho
akashindwa kujizuia akatulia kidogo na kujifuta
machozi ambayo yalikuwa yanamwagika kwa
wingi) Vile vile naomba ufahamu kuwa nilipofika
pale niliwakuta mabinti wengine ambao alikuwa
anajinufaisha nao kwa mtindo huo, cha kusikitisha
zaidi ni pale alipomlazimisha binti mmoja
kutembea na mwanaume ambaye ni muathirika
wakati akijua wazi. Baada ya kuathirika kutokana
na matunzo duni yule dada alisumbuliwa na homa
za mara kwa mara. Mama pili hakutaka kuingia
gharama tena akatumia njama ya kumuwekea
sumu na kumuua. Kijana yule yule ambaye
alimlazimisha yule binti akanilazimisha na mimi
pia. Nikakataa lakini wakatumia ubabe kuhakikisha
nafanya mapenzi na yule kijana kwani alilipwa
pesa nyingi. Ndio maana nilipoenda kupima
nilikuwa na uhakika mkubwa kuwa majibu
hayatakuwa mazuri kwa sababu yule kijana
alilazimisha kufanya mapenzi bila kinga.”
Akatulia na kumkazia macho mdogo wake ambaye
alikuwa makini kumsikiliza dada yake.
“Naomba tulale nina kazi ya kufanya kesho.”
Alimaliza kisha akajivutia shuka akalala.
“Samahani lakini kwa usumbufu huyo kijana
unamfahamu vizuri?”
“Ndiyo. Anafanya kazi kampuni ya mafuta BP mtaa
wa jamhuri, sitaki swali tena mdogo wangu
nimechoka pengine unataka kujua jina lake anaitwa
Samson Masanja.” Hakuongea tena akajivutia
shuka akalala.
********

Alitembea kwa wasiwasi mkubwa kwani eneo
alilokuwepo ni eneo analofahamika sana. Pia
aliogopa kwa sababu alikuwa anatafutwa na polisi.
Kilichomsaidia hakuacha alama yoyote ya picha
ambayo ingewafanya polisi waitoe magazetini na
kuhatarisha maficho yake. Alishaifikia nyumba ile
aliyokusudia. Hakuwa na haraka. Akabana sehemu
ambayo ilikuwa inatumika kuhifadi magunia ya
mkaa. Ilikuwa ni siku ya tatu anakuja kujificha
hapo bila kufanikisha kulipata windo lake. Akakaa
hapo kwa masaa mawili bila kutokea kile
alichokitarajia. Akiwa amekata tamaa ndipo
alipoushuhudia mlango ukifunguliwa. Akamtazama
vizuri aliyetoka. Ni yeye. Aliwaza kwa furaha huku
akijiandaa kwa shambulizi.
Pili aliingia chooni baada ya dakika chache
akatoka. Hakufika mbali. Vero akampiga kwa
gongo zito kichwani akataka kudondoka lakini vero
akamuwahi ili asitoe kishindo. Kisha akammalizia
kwa kudidimiza kisu che mpini mwekundu upande
ambao alihisi kuwa ndiko yaliko makao ya moyo.
Akamshikilia taratibu hadi alipohakikisha mwili
wake ameulaza chini. Moyoni alifurahi sana jinsi
alivyoifanya kwa umahiri mkubwa kazi hiyo.
Taratibu akaondoka eneo la tukio. Tofauti na wale
wengine huyu alimuua kwa utulivu zaidi. Mama
Mwazani ndiye aliyenileta huku sasa ni zamu yake.
Aliwaza huku akiondoka kifua mbele baada ya
kutekeleza jukumu lile. Akapita kwenye vichochoro
mbalimbali ambako alipishana na makahaba
aliowafahamu sana. Hakuna hata mmoja aliyeweza
kumtambua Vero. Alijitahidi kubadilisha mwendo
na chochote ambacho kingemfanya mtu aweze
kumtambua.
Salum, mpenzi wake Pili alikuwa amechoka kusubiri
kule ndani. “We pili vipi huko nje?” Aliuliza kwa
hasira kidogo. Alipoona hajibiwi ndipo alipoamua
kutoka nje. “He. Vipi tena mpenzi.” Alishtuka
baada ya kumuona Pili akiwa amelala chini. Kwa
kuwa kulikuwa na giza akaingia ndani na kuchukua
kibatari.
“Damu.” Alishituka salum kabla ya kutimua mbio
akiogopa ushahidi ambao ungekuja baada ya
kuonja mvua ya makofi pengine na virungu kutoka
kwa polisi.
* * *

Kachero Dadi Kasweyaga alikuwa anajiandaa
kunyofoa laini yake ya mtandao ambao
unafahamika ofisini kwake ili aweke ile
inayofahamika zaidi na ndugu na marafiki. Ilikuwa
ni kawaida yake kwa siku anazochoka kubadili laini
kwa kuchelea kupigiwa usiku. Leo ilikuwa ni moja
ya siku hizo. Wakati anataka kuzima ikaingia simu.
Safari hii ilipigwa na bosi wake Inspekta Beda.
“halloo habari afande.”
“Nzuri za nyumbani.”
“Salama kwani umemaliza likizo afande?”
“Ndiyo na hivi ninavyoongea nakuhitaji ofisini kuna
dharura.”
“Sawa afande.” Akajibu huku akijifanya
kuchekacheka kumbe alikuwa amekunja uso kwa
hasira. Akamkazia macho mkewe mama Tunu.
Akasikitika kwani alikuwa anakaribia kuanza safari
yake ambayo imemfanya awe pamoja na mama
Tunu.
Akainuka kitandani kivivuvivu.
“Vipi baba Tunu.” Mkewe alishituka usingizini
baada ya purukshani za mumewe wakati
anajiandaa kuondoka.
“Kuna imejensi nimeitwa ofisini.”
“Mh. Haya .” Alinung’unika mkewe huku akiinuka
kutoka kitandani kwenda kufunga mlango.
Akafungua mlango na kutoka, mkewe akaubamiza
mlango kwa nguvu kitendo kilichomfanya kachero
atambue kuwa mkewe kakasirika.
Hakuishi mbali sana na kituo cha polisi cha
Buguruni. Akatembea moja kwa hadi kituoni.
“Vipi peter kumbe na wewe umeitwa?” Aliuliza
kachero Dadi baada ya kumkuta koplo Peter
Mkwabi akiwa pale kituoni.
“Ee. Kuna mauaji mengine afande.”
“Yanafanana na yale ya kwanza.”
“Siyo kufanana tu. Aliyeuwawa safari hii ni mtoto
wa yule mama.”
“Nini? Ina maana Pili naye kauwawa?”
“Yes. Tofauti na mauaji ya kwanza safari hii
muuaji katumia kitu kizito kisha akamalizia na kisu
kama kilekile.”
“Kina mpini mwekundu nacho?”
“Ndiyo afande, ni muuaji wa ajabu kabisa kwani
kitu alichotumia kilitosha bila kuhitajika kile kisu.
Nilikuwa nakusubiri kwani afande yuko eneo la
tukio.”
Kwa kuwa kulikuwa na hatua chache kutoka
kituoni hadi eneo la tukio walilazimika kutembea
kwa miguu.
* * *

Hasira kali ilikuwa inarindima katika kichwa cha
Inspekta Beda. Aliapa kumuua kwa mkono wake
mtu aliyemuua Lucy. Lakini alishangazwa na
kitendo cha muuaji huyo kufanya mauaji hayo
kwani hakuwa na uhusiano wowote na familia ya
mama Pili. Alijaribu kuchunguza kama kuliwahi
kuwa na uhusiano fulani kati ya Lucy na familia ya
mama Pili lakini akagundua hakuna uhusiano wa
aina hiyo.
Ripoti ya wataalamu wa vidole ilikuwa mbele yake.
Bado ilionyesha kuwa muuaji wa watu wote watatu
alikuwa mmoja. Anataka nini? Hili lilikuwa swali
gumu kabisa lililopita kwenye kichwa cha Inspekta
Beda. Alisaga meno kwa hasira. Haikuwa kawaida
kwake kufanya kazi siku tatu kabla hajapata
ufumbuzi au mwelekeo wa ufumbuzi lakini safari
hii mambo yalionekana kutatanisha.
Hata pale alipotajiwa Vero ndiye muuaji hakuweza
kufikiria kabisa kuwa Vero huyo atakuwa ni
mwanawe wa kumzaa ambaye amemtelekeza. Vero
wake alikuwa mpole mwenye huruma. Huyu
anayemsoma kwenye faili ni Vero kahaba tena
muuaji. Hakuipa akili yake nafasi ya kupitisha
wazo juu ya mwanawe.
Akiwa kwenye lindi la mawazo simu ya kiganjani
ikaita. Akaitazama vizuri. Ilikuwa inapigwa na
Kachero Dadi, akashtuka kwani alishazoea simu za
kachero yule mara nyingi hazikuwa na taarifa
nzuri.
“…. Kama yale ya kwanza lakini safari hii ni
Kawe…”
“…Nilipigiwa simu na mkuu wa kituo cha huku kwa
sababu alipata taarifa kuwa tumeshikilia upelelezi
wa mauaji yanayofanana na haya.”
“Uko wapi sasa?”
“Niko Kawe nimeshamaliza uchunguzi.”
“Umegundua nini?”
“Kuna uhusiano wa karibu kati ya mama Pili na
marehemu.”
“Mh. Haya mauaji yanaweza kuwa ni ya kisasi.”
Aliongea Inspekta huku akishusha pumzi.
“Vipi kuhusu Vero umejaribu kuhoji hapo.”
“Ndiyo. Vero alikuwa house girl nyumba ya jirani
huyu mama ndiye aliyemtoa na kumpeleka kwa
mama Pili.”
“Enhee. Angalau mwanga naanza kuupata huyo
Vero alitokea wapi?”
“Hapo pana ugumu afande kwani aliyemwajiri Vero
kwa mara ya kwanza kwa sasa ni marehemu.”
“He. Na yeye kauwawa?”
“No. Huyu amekufa kwa ajali ya gari wakati
anaelekea Morogoro.”
“Duh. Mbona mambo yanazidi kuwa magumu?”
“Sana. Maana huyu vero hafahamiki kabisa ni mtu
wa aina gani maana anakuwa kama mzuka.
Inspekta Beda aligonga meza kwa hasira.
Matumaini ya kumpata muuaji yalikuwa madogo.
Ili muuaji apatikane ilitakiwa aeendelee kuua jambo
ambalo lingekuwa hatari zaidi. Vitu viwili
vilimfanya Inspekta aone ugumu uliopo wa
kumpata muuaji, Kulikuwa hakuna picha yoyote ya
muuaji pia alikuwa hajulikani hata ndugu yake
mmoja ambaye wangeweza kumdadisi mambo
kadhaa. Ilikuwa ni ajabu kwake kwa mshukiwa
kutojulikana kabisa hata maelezo ya awali.
Alipitia kumbukumbu mbalimbali za kipolisi lakini
bado hakufanikiwa kupata lolote kuhusu Vero.
Katika orodha ya wahalifu aliyokuwa nayo
wanawake walikuwa watatu tu tena wawili kati yao
walishauwawa na Polisi wakati wa jaribio la kupora
gari la mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya
kiasia.
* * *
ITAENDELEA!!!
 
SEHEMU YA MWISHO PART 1

Ilikuwa ni ajabu kwake kwa mshukiwa kutojulikana
kabisa hata maelezo ya awali.
Alipitia kumbukumbu mbalimbali za kipolisi lakini
bado hakufanikiwa kupata lolote kuhusu Vero.
Katika orodha ya wahalifu aliyokuwa nayo
wanawake walikuwa watatu tu tena wawili kati yao
walishauwawa na Polisi wakati wa jaribio la kupora
gari la mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya
kiasia.
* * *

“Vipi dada umemaliza kazi?” Aliuliza Sara huku
akimkazia macho dada yake.
“Angalia idadi ya visu kwenye begi.” Alijibu huku
akijilaza pale kitandani.
Sara alifungua begi la dada yake na kuanza
kuhesabu idadi ya visu vilivypo.
“Viko vinne.”
“Wanaume wawili wanawake wawili.” Aliongea
huku akijilaza kitandani na kujipongeza kwa jinsi
alivyomuua mama Mwazani kule Kawe na
kuwaachia kazi ngumu Polisi. Wakati akiwa pale
kitandani akafungua Mkoba wake na kuchungulia
akiba iliyopo. Ilikuwa inatosha kuendesha maisha
yake kwa mwezi mmoja zaidi. Hizi zilikuwa fedha
alizozipata baada ya kumuua Lucy. Akatabasamu.
Alishanogewa na mchezo wa kifo. Alitamani kuua
zaidi na zaidi…….
Vero aliamka saa 1.21 akafungua mkoba wake kwa
mara nyingine akatoa simu ya marehemu Lucy
kisha akaiwasha ile. Ilipowaka tu ukaanza kuingia
mfululizo wa meseji ambazo hazikupungua saba.
Akafungua na kuanza kuzisoma. Moja ilimvutia
zaidi. …… Lucy rafiki yangu uko wapi ukifungua
simu naomba unipigie nime kumiss sana kila
nikikutafuta hupatikani. Habiba. Akaamua kuijibu
ile meseji. …… Pole Habiba mwenzio nishakufa siku
nyingi naandika nikiwa kaburini jitahidi kuwafanyia
wema binadamu wengine huku mambo ni magumu
kuna mateso makubwa sana… Akaituma. Ukaja
mlio ambao ulimuashiria kuwa meseji
imepokelewa. Baada ya dakika kumi ikaingia
meseji nyingine. ….Acha utani Lucy hayo masihara
siyo mazuri….. Yalikuwa ni majibu ya ile meseji ya
Vero. Kama huamini chukua hii namba ya mama
kisha umpigie umuulize, sasa siwezi kuendelea
kwani malaika wa adhabu yuko mbele yangu subiri
niadhibiwe kama nitapewa tena nafasi
nitakupigia…… Alijibu ile meseji kisha akazima
simu.
Moyoni alicheka kwa mzaha alioufanya. Alijua wazi
jinsi gani yule binti atachanganyikiwa baada ya
kupata taarifa kutoka kwa mama mzazi wa Lucy.
Lucy ni marehemu kweli lakini hii meseji kutoka
kaburini kiboko…. Alicheka tena safari hii kwa sauti
huku akimshangaza Sara ambaye muda mwingi
alikuwa kimya akitafakari kuhusu mlolongo wa
maisha yake.
“Vipi mbona unacheka.”
“Acha nicheke mdogo wangu.” Alisema kisha
akamsimulia kuhusu zile meseji.
Wote wakacheka.
“Leo utaenda?”
“Hapana, waliobaki natakiwa kuwa makini kwanza
kuna wanaume wawili halafu Koku na mama yake.”
“Kwa nini usiwasamehe.”
“Hapana mdogo wangu, machungu ya ubaya wao
hayawezi kuondoka kama wataendelea kuwa hai.
Tone la mwisho la damu ndilo litakalo nifanya
nijisalimishe mbele ya mikono ya sheria.”
“Kwa hiyo utafanyaje kuhusu waliobaki?”
“Natakiwa kupumzisha kichwa changu kwa siku
mbili zaidi nikitafakari nini cha kufanya.”
“Sawa.” Aliongea Vero kwa upole zaidi.
“Halafu kwa nini unapenda kutumia kisu chenye
mpini mwekundu?” Aliuliza Sara.
“Ni rangi ambayo ninapoiona inanikumbusha
wajibu wangu kwani ni rangi ya hatari pia kuna
dhana kuwa ni rangi ya ukombozi, ndio maana
nchi nyingi zilizokombolewa kwa vita bendera zake
ni nyekundu.”
“Mh. Dada una mambo, ungekuwa mwanasiasa
sijui ingekuwaje.”
“Mungu aninusuru, siasa ni kitu ambacho sitaki
kukisikia kabisa katika maisha yangu.”
“Kwanini?”
“Sijaona watu madhalimu na wanafiki wakubwa
kama wanasiasa usinitajie kabisa nasikia
kichefuchefu.”
* * *
“Enhe. Amesema alikuwa anaongea kutoka
kaburini?” Alihoji tena kachero Dadi huku Inspekta
ambaye alikuwa kando yake akiwa amefura kwa
hasira. “Ndiyo.” Alijibu Habiba huku akitoa ile simu
yake na kufungua sehemu ya meseji.
“Uliwahi kuongea naye.” Aliuliza tena kachero.
“Hapana. Kwani baada ya kuniambia kuwa malaika
wa adhabu amefika alizima simu.”
Kachero Dadi alitamani kucheka lakini akajizuia
kwa kuwa Inspekta alikuwa kando.
Inspekta akaichukua simu ya yule binti, akaanza
kusoma ile meseji. Akatikisa kichwa.
“Sidhani kama huyu mtu ni mwanamke.”
“Kwanini?”Aliuliza kachero
“Si kawaida kuwa na mwanamke mjanja namna hii
ambaye haogopi hata polisi.”
“Umejuaje kuwa haogopi polisi?”
“Angekuwa mtu mwenye woga asingethubutu
kutumia simu ya marehemu wakati anajua wazi
kuwa anatafutwa.”
“Unajuaje kama muuaji ndiye anayetumia simu ya
marehemu?” Aliuliza kachero.
“Angekuwa mtu mwingine angetoa laini kisha
akapachika ya kwake habari zingekuwa zimeisha.”
“Mh. Aliguna kachero huku akikuna kichwa.”
Baada ya dakika chache simu ya Inspekta ikaanza
kuita. Akaangalia jina kabla ya kupokea. Moyo
ukamlipuka kwa hofu.
“Shikamoo baba.”
“Wewe nani?” Alifoka Inspekta badala ya kujibu.
“Ina maana toka niende kaburini mmeamua kufuta
hata namba zangu?” Uliuliza upande wa pili.
“Kwanza niambie wewe ni nani?”
“Mimi ni Lucy baba.”
“Uko wapi?”
“Niko makaburini hapa Kinondoni nimepewa
upendeleo wa kipekee kuongea na binadamu
wenzangu.”
“Sikiliza wewe ndama, siku nikikutia mikononi
mwangu utajuta kuzaliwa.”
“Usijitukane baba kama mimi ni ndama basi wewe
utakuwa ng’ombe kamili kwa sabau wewe ndio
baba yangu na hilo la kujuta kuzaliwa lisikupe tabu
kwani siwezi kujuta mara mbili nimeshajuta na
huku niliko bado naendelea kujuta, naona malaika
anakuja kuniuliza maswali….”
“Wewe usikate…” Alishachelewa kwani simu
ilikatwa.
“Mruhusu huyo binti aende kwani ishakuwa balaa
hapa.” Aliongea Inspekta huku akiegemea kwenye
kiti chake. Hakuna aliyetaka kujua Inspekta alikuwa
anaongea na nani kwani simu yake ilikuwa kwenye
mfumo wa ‘loud speaker’ Kachero alikuwa hoi
kutokana na kujizuia na kicheko baada ya tukio lile
la simu kutoka kaburini.
“Unafikiri kwa nini ameamua kukupigia?” Aliuliza
kachero huku akizidi kupata mateso ya kubana
kicheko kilichokuwa kinamvizia.
“Siwezi kujua lakini muuaji ni mtu anayejua nini
anachokifanya.”
“Una maana gani?”
“Jinsi nilivyoongea nae ni wazi kuwa anajua
anachokifanya pia kuna fumbo zito nahisi liko
ndani yake…..”
“….. kuna uwezekano mkubwa wa mahusiano kati
ya mama Pili na Lucy, siwezi kujua ni uhusiano
gani lakini nahisi upo kwani watu wote watatu
aliowaua wana uhusiano isipokuwa huyu Lucy
ambaye kuna kitu kama uhusiano ambao
ulijificha.”
“Tutawezaje kufahamu hilo.”
“Ni vigumu kwani marehemu wameondoka na siri
hii.”
“Kwa upande fulani nataka kukubaliana na wewe
hasa nikifikiria kitendo cha muuaji kuondoka na
Lucy toka ofisini kwake hadi pale alipouwawa.”
Simu ya Inspekta ikaanza kuita tena. Akaiangalia
tena ile namba, safari hii alikuwa mkewe.
“Enhe.” Aliuliza huku akijitayarisha kusikia taarifa
za kuchukiza tena.
“Kapiga tena yule mtu anatusalimia sana na
anasema eti karibuni atatufuata tujumuike wote
kaburini.”Aliongea mkewe. Inspekta alisikiliza bila
kuongea lolote. Kuna nini mbona huyu muuaji
anatuchezea sana? Alijiuliza Inspekta.
Kama aliyezinduka usingizini akauliza.
“Anasemaje nani atamfuata?” Aliuliza Inspekta
huku hali ya hasira ikiwa imepotea kwani aliona
wazi kuna tishio la mauaji mbele yake.
“Atatufuata sisi.”
“Achana nae mpumbavu bado kidogo nitamtia
mikononi.”
“Huuu.” Mkewe alishusha pumzi kisha akakata
simu.
“Unaona jinsi muuaji anavyonichezea?” Aliuliza
Inspekta.
“Mh. Afande hata mimi huyu mtu ananitatanisha
sana.”
“Ngoja niende nyumbani nikaongee na mke wangu
huenda kuna kitu atakuwa anafahamu.”
* * *

“Mbona unachukua visu viwili.” Aliuliza sara.
“Huenda nikafanya mambo kulingana na idadi ya
visu.’
“Mh. Dada unatisha huogopi?”
“Matatizo yanaondoa uoga.”
“Mbona watanzania wana matatizo mengi lakini ni
waoga.”
“We hujui tu. Akitokea mpumbavu mmoja tu
akawahamasisha waandamane ili wachome moto
ikulu wataandamana tu kwani hawana cha
kupoteza ndio maana ukichunguza waandamanaji
wengi ni watu wenye maisha magumu hata siku
moja huwezi kumshawishi tajiri aandamane.”
“Mh. Dada una maneno kama msomi.”
Akaweka visu vyake vizuri kwenye mkoba wake.
Akampungia mkono mdogo wake akaondoka.
Tofauti na mauaji mengine aliyoyafanya safari hii
aliondoka akiwa na hofu kubwa. Wakati anataka
kutoka mle ndani akakumbuka kitu. Ilikuwa ni
hatari kwake kuondoka namna ile. Alijua wazi
kuwa kulikuwa na ugumu mkubwa wa kazi
iliyomkabili mbele yake.
“Mbona unarudi? Aliuliza Sara.
“Natakiwa kubadilisha mfumo wa kazi kwani iwapo
nitaendelea na mfumo wa kawaida naweza kujikuta
kwenye mikono ya dola kabla ya kumaliza kazi.”
“Kivipi.”
“Utaona.”
Akarudisha vile visu kwenye begi kisha akaondoka
na kwenda maeneo ya dampo.
Akaanza kupekua pekua hatimaye akazipata nguo
chafu zilizochanikachanika ambazo asingeweza
kuvaa zaidi ya mwendawazimu. Akazichukua na
kuziweka kwenye mfuko wake wa nailoni.
Akatembea hadi sehemu alipolikuta gofu la
nyumba. Akaangalia pande zote kuhakikisha
usalama, hakukuwa na mtu aliyemuona wakati
anaingia mle ndani. Akaingia na kuvaa yale
mavazi. Chizi. Alikuwa kichaa kamili kama si ngozi
yake ambayo bado ilikuwa na mng’ao wake wa
kuvutia. Hakutaka chohote kimuumbue akatoka nje
haraka, akatembea mpaka pale alipoona
yamemwagwa mabaki ya mkaa. Hakutaka kujiuliza
akaanza kujipaka vumbi lile la mkaa. Sasa
alikamilika kama kichaa, akazidi kujitia uchafu kila
alipouona………
* * *

“Mama aomba maji, mimi aa njaa ataka kula.”
Kichaa aliendelea kumkera mke wa Inspekta
ambaye tayari alikuwa na mawazo mengi kutokana
na simu ya ajabu aliyoipata. Huku bado moyoni
akiendelea kuuguza kidonda cha kufiwa na mwanae
ambae alimpenda sana.
“Njoo unywe na uondoke kabisa sitaki kukuona
hapa unatia kichefu chefu.” Alilalamika mke wa
Inspekta Beda. Akaanza kutembea kwa haraka
kwenda ndani kumchukulia yule mwendawazimu
maji ya kunywa. Mwendawazimu akiwa mwenye
njaa na kiu alimfuata mama yule huku udenda
ukimtoka hovyo. Mama Lucy akaingia kwenye
chumba ambacho ndoo za maji zilikuwa
zinahifadhiwa. Akafunua moja ya ndoo zilizopo mle
chumbani. Hakuwahi kuchota yale maji. Mlango
ukafungwa nyuma yake. Alipoangalia nyuma yake
alisimama yule mwenda wazimu akiwa na bisu
kubwa lenye mpini mwekundu. Ule udenda
uliokuwa unamtoka haukuwepo tena.
“We. Kichaa unataka nini?” Aliongea Mrs Beda kwa
Kihoro.
“Roho yako.” Alijibu yule kichaa kwa mkato.
“Unanikumbuka?” Aliuliza yule kichaa huku
akimkazia macho mama Lucy kwa namna ambayo
ilimtisha.
“Ha..ha..hapa..pana sikujui toka humu ndani.”
Alifoka mama Lucy kwa ukali uliochanganyika na
woga.
“Unakumbuka kuna siku uliwahi kushirikiana wewe
Lucy , Koku na Fred kununua sumu kwa ajili ya
kumuua mtu fulani?”
“Hapana.” Alikataa huku akionyesha mshituko
mkubwa zaidi.
“Najua unakumbuka vizuri sana, pengine ambacho
huwezi kukumbuka ni kuwa mimi ndiye Vero mtoto
wa yule mama na pia ni mtoto wa Inspekta Beda.”
alitulia na kumwangalia yule mama ambaye
alitokwa na haja ndogo kutokana na woga
uliomkuta.
“Sitaki niamini kuwa kuna mambo ya kishirikina
umemfanyia baba yangu hata akaitelekeza familia
yake lakini nataka nikudhihirishie kuwa nilikuwa
nimejificha sehemu fulani siku mliyokuwa
mnapanga kumuwekea sumu mama yangu. Ingawa
miaka mingi imepita bado kumbukumbu yangu
haiwezi kufutika mpaka pale sura yako na wenzako
zitakapofutika kwenye uso wa dunia, pia naomba
uelewe wazi kuwa mimi ndiye muuaji wa
Lucy………” Hakumaliza hotuba ile ambayo haikuwa
rasmi kwani yule mama alianguka kutokana na
mshituko mkubwa alioupata. Haikuwa kazi kubwa
kwa Vero bila huruma akakipitisha kisu katika
shingo la yule mama. Damu zikamwagika na
kutapakaa eneo lile. Hakukihitaji tena kile kisu.
Akakiacha kisu pale pale.

**VERO anakiendeleza kisasi…..
ITAENDELEA!!!
 
SEHEMU YA MWISHO PART 2

Damu zikamwagika na kutapakaa eneo lile.
Hakukihitaji tena kile kisu. Akakiacha kisu pale
pale. Akaichukua simu ya yule mama ambayo
alikuwa ameivaa shingoni kwa kamba maalum.
Akatafuta namba fulani fulani. Akaipata namba ya
Koku. Akaanza kupiga namba ikawa inaita bila
kupokelewa. Bahati ilikuwa upande wake ile simu
ikakatwa kisha ikatumwa meseji niko getini nakuja.
Mjinga amejileta mwenyewe. Aliwaza Vero.
Akasimama nyuma ya mlango kwa umakini
mkubwa. Koku akafungua mlango huku macho
yake yakiwa kwenye simu. Alikuwa anaandika
meseji. Hakupata nafasi ya kumaliza kuandika
meseji kisu kikali kikapenya kwenye shingo lake.
Akatapatapa bila kupiga kelele, hatimaye akakata
roho.
Akamshukuru Mungu kwa kumaliza kazi ile
salama. Kazi iliyobaki hakuiiona kuwa kubwa sana
kwani hata kama asingeimaliza bado alikuwa na
furaha ya kumaliza robo tatu ya kazi yake.
Akaandika meseji akamtumia Inspekta Beda.
Bado wawili tu utapumzika.
Akaanza kuondoka mle ndani taratibu lakini kabla
hajafika getini akasikia mlio wa gari nje. Akarudi
haraka ndani. Akaanza kuchungulia dirishani.
Mungu wangu. Alishituka Vero baada ya kumuona
Inspekta Beda akifungua geti huku akiwa
ameongozana na askari wengine wawili.
Nimekwisha.
* * *

Hofu iliyokuwa imetanda katika jiji la Dar es
salaam ilianza kupungua baada ya taarifa za
kukamatwa Vero. Magazeti karibu yote yalibeba
taarifa hizi za kusisimua. Waandishi wa magazeti
walikuwa na kazi ya ziada kuripoti mauaji haya.
Watu sita walikuwa wameuwawa katika staili
inayofanana, kilichosisimua zaidi ni mauaji ya
familia ya Inspekta Beda. Hata waandishi
walishindwa angalau kutia uongo kuwa mauaji
haya yanahusiana na jambo lipi.
Gumzo kubwa katika vijiwe vya kahawa lilikuwa ni
juu ya muuaji huyu ambaye hutumia kisu chenye
mpini mwekundu. Miongoni mwa watu waliokuwa
kwenye wakati mgumu ni kachero Dadi Kasweyaga
ambaye katika maisha yake ya kazi hakuwahi
kukutana na tukio kama hili. Leo kidogo alikuwa
kwenye ahueni baada ya Vero kukamatwa.
Watu wengi walikuwa maeneo ya polisi
chang’ombe wakijaribu kuchungulia ili waweze
kumwona mwanamke aliyetikisa jiji la dar es
salaam. Kukamatwa kwake kulikuwa gumzo kwa
sababu alikuwa msichana mpole ambaye
hakutegemewa kuweza kulitikisa jiji kubwa namna
hii. Hofu ilikuwa imepunguwa watu wengi walikuwa
na furaha.
“Umesema unaitwa nani?”
“Veronika Charles.”
“Nataka kujua kwanini umefanya mauaji ya kutisha
na kulitikisa jiji.” Aliendelea kuhoji Kachero Dadi.
“Mimi?”
“Kumbe naongea na nani?”
“Nimemuua nani?”
“Ebo. Unajifanya kushangaa sio?”
“Unajua mnanichanganya sana mimi nimeuwa
mtu.” Alishangaa Vero.
“Swala sio kukataa kama umeua au hujaua
tunachotaka kujua kwanza kwa nini ulimuua mama
Pili kisha utamaliza kuhusu hao wengine.”
“Mama Pili ninayemjua ni mmoja tu ambaye ni
jirani yangu pale kinondon naye ni mzima.”
Aliendelea kukanusha Vero. Kiasi fulani kachero
Dadi aliaanza kushangazwa na jinsi huyu
mwanamke anavyoongea kwa kujiamini huku akiwa
na uhakika wa asilimia mia kwa kauli zake. Lakini
asingeweza kusahau jinsi mwanamke huyu
alivyokuwa mjanja kiasi cha kuwachachafya na
kuwakejeli kwa kutumia simu.”
* * *

Huyu hakuwa na furaha. Taarifa za kukamatwa
kwa Vero hazikumfurahisha hata kidogo. Alijua
kuna makosa yamefanywa na polisi. Ni kweli
aliyekamatwa ni Vero lakini si Vero muuaji ambaye
anasakwa na jeshi hilo. Pengine ni jina tu ndio
ambalo limemponza. Halafu alihisi kuwa huenda
alipita eneo la tukio muda mfupi baada ya mauaji.
Akaanza kurudiwa na fikra juu ya tukio lile.
Baada ya kumuona Inspekta anakuja na askari
wawili aliamua kujificha nyuma ya sofa lililoko pale
sebuleni. Askari walishtushwa na mauaji yale lakini
Ghafla, Inspekta akatoa amri mlango ufungwe
askari waingie vyumbani waanze kumtafuta
muuaji. Hapo Vero alijua kuwa amekwisha. Lakini
akajiwa na wazo la ghafla. Akaiwasha ile simu ya
marehemu na kuamua kujaribu bahati yake kwa
kupiga namba ya Inspekta.
Inspekta alipokea haraka haraka huku akipatwa na
mshangao mkubwa.
Akiwa kule nyuma ya sofa Vero aliamua kucheza
karata ya mwisho, ilikuwa ni karata hatari kwani
hakuwa na uhakika kama pale sebuleni kulikuwa
na mtu amebaki au la.
“Hallow afande nimefurahi sana kupishana na
wewe wakati unaenda nyumbani kwako nafikiri
umeshajionea mambo niliyoyafanya Mungu
akipenda nitarudi tena kesho kuja kummalizia aliye
baki.” Inspekta akapatwa na mshituko baada ya
kupata simu hiyo. Akakosa umakini.
“Nafikiri utafurahia kazi nzuri niliyoifanya hapo
ndani kwani itakupa changamoto kubwa zaidi na
kuchangamsha akili yako.” Akatulia kidogo kisha
akakata na kuzima simu.
“hallow twendeni haraka muuaji yuko nje tunaweza
kumuwahi.” Wakatoka haraka haraka baada ya
kupewa taarifa ya simu ile.
Hakuwa na muda wa kupoteza hiyo ilikuwa karata
yake ya mwisho. Walipotoka tu naye akatoka mle
ndani. Akapita palepale getini. Akaanza kuimba na
kutukana hovyo baada ya kutoka mle ndani.
Hakuna aliyemjali, chizi nani angejishugulisha
naye?
Alipofika mbele kidogo akamkuta Inspekta na
wenzake wakimuhoji dada mmoja ambaye ni wazi
alikuwa katika mizunguko ya kawaida. Akapishana
nao bila kutiliwa mmashaka. Akashangaa kuona
yule dada akifungwa pingu. Mwendawazimu
huyooo akatokomea.
Saa mbili na nusu usiku akaingia ndani ya gofu lile
ambalo alificha nguo zake. Akabadili na kuvaa
hijabu nzuri iliyomfanya afanane na mwanamke wa
kiarabu au kisomali. Akatabasamu, ni wazi alikuwa
anasherehekea ushindi wake Mkubwa alioupata.
Alijishangaa hata yeye mwenyewe. Ni wapi alipata
uwezo wa kufanya mambo makubwa kama yale.
Akatembea taratibu kuelekea kule gesti. Alisikia
raha, raha kubwa kabisa ndani ya moyo wake.
Vilibaki visu viwili tu. Ilikuwa lazima avitumie.
Aliingia chumbani na kumkuta Sara akiwa amelala.
“Vipi mbona hujafunga mlango?” Aliuliza Vero.
“Nilitaka usipate shida ya kubisha hodi.”
“Kuwa makini, usirudie tena ni hatari.” Aliongea
huku akipekua kwenye begi lake na kutoa taulo.
“Vipi umemaliza?”
“Bado wawili mmoja nitahitaji msaada wako.”
“Kivipi?”
“Nahitaji umvute hadi hapa ili nimalizie kazi
yangu.”
“Nitawezaje dada?”
“Wanaume ni watu dhaifu sana tofauti na
unavyofikiri, ukitumia nguvu watakushinda.
Maneno mazuri tena yanayosindikizwa kwa sauti
laini ya mahaba ni silaha tosha ya kumshawishi
hata mkuu wa majeshi akainuka kitini na kukupigia
saluti?”
“Unafikiri wanaume wote ni dhaifu kiasi hicho?”
“No. kuna wanaume wachache wenye uwezo
mkubwa kifikra. Hawa ni hatari sana kwani huwezi
kuwaangusha kwa maneno wala tabasamu lako
lakini hawa ninaowakusudia ni walewale wa
kawaida……..”
“Samahani dada visu vimebaki viwili lakini
nimegundua cha tatu ambacho si chekundu kama
vile vingine….” Akamkatisha kabla hajamaliza
kuongea.
“Hicho sikutaka ukione lakini kuna shujaa
mwanamapinduzi ambaye atakuwa wa mwisho
kuuwawa kwa mkono wangu.” Alijibu na kuondoka
huku akionekana wazi kutotaka maswali zaidi
kuhusu hilo.
* * *

Fred alikuwa na huzuni kubwa kutokana na kifo
cha mama yake na dada zake. Mara nyingi
aliogopa kulala mle ndani peke yake kwani
Inspekta hakurudi nyumbani kutokana na uzito wa
majukumu yaliyomkabili. Mara nyingi alirudi
nyumbani na kulala mchana kisha kukesha kazini
usiku. Vitu viwili vilimpa moyo Fred, kwanza muaji
alikuwa anaua wanawake tu pili alikuwa
amekamatwa. Haikumwingia akilini kuwa muuaji
anaweza kuendeleza tena kazi yake.
Akaingia ndani na kukaa pale sebuleni. Mama yake
alikuwa amezikwa yalibaki maombolezo tu. Alijua
wazi kuwa ni yeye ndiye mrithi wa Inspekta Beda,
lakini wazo moja lilimtisha je. kama Inspekta ataoa
si itakuwa balaa. Akaanza kulia upya.
Kilio chake kikakatishwa na mtu aliyekuwa
anagonga mlango. Akafungua mlango. Akaingia
msichana mwenye hijabu nyeusi.
“Habari kaka Fredi.”
“Nzuri za nyumbani.” Alijibu Fred huku akijaribu
kukumbuka ni wapi alimuona huyo msichana bila
kupata jibu.
“Vipi mbona pako kimya sana Koku nimemkuta?”
Swali hilo likazidi kumshangaza fredi kwani
aliyekuwa anauliziwa hapo alikuwa marehemu.
“Wewe ni nani?.” Aliuliza Fredi kwa mshangao
mkubwa kabisa.
“Hee. Mara hii umenisahau kaka Fred, mimi ni
rafiki yake naitwa Mary nilikuwa masomoni
Uganda.”
“Duh. Samahani sana unajua nilikuwa najiuliza
mbona sura yako kama niliiona mahali fulani, yaani
si ngeni kabisa tena nilihisi kuwa kama nilikuona
hapa nyumbani.”
“Miaka miwili tu niliyokaa Kampala umenisahau
hivi, ningekaa miaka kumi si ingekuwa balaa.”
“Samahani sana Mary lakini Koku amekufa.”
“Koku amekufa.” Alishituka akaanza kulia. Akalia
kiasi ambacho Fredi alishikwa na huruma akaanza
kumbembeleza. Kwa kisingizio cha kumbembeleza
akawa anamshika maeneo ambayo kimaadili
hakuruhusiwa. Kosa. Alishituka baada ya kuona
yule mwanamke akiwa ameshikilia kisu chenye
mpini mwekundu. Alikuwa anatafuta namna ya
kujiokoa lakini alishachelewa kwani hakupewa
muda wa kufikiria zaidi kisu kile kikapenya kwa
nguvu upande wa kushoto wa kifua chake.
“Naitwa Veronika Beda.” Alitamka huku akimkazia
macho fred ambaye alikuwa anatapatapa
kuipigania roho yake. Ingawa alikuwa anakata roho
alishituka baada ya kutajiwa jina hilo.
Wakakutanisha macho yao. Alitaka kuongea kitu…
aliendelea kujaribu kuongea akaishia kwenye
miguno ya mauti… Macho yake yakapoteza nuru ya
uhai. Akakata roho.
Akaangalia saa kubwa ya ukutani. Ilikuwa saa
nane na nusu mchana. Akashituka, muda wa
Samson Masanja kutoka kazini ulikuwa
umekaribia. Akajikagua mwilini akagundua matone
ya damu ambayo yalimezwa na weusi wa nguo
yake. Hakuna ambaye angeweza kugundua kuwa ni
matone ya damu kwani yalikuwa na rangi nyeusi
kama nguo yenyewe.
Akatembea hadi kituo cha magari ambacho
kinajulikana kwa jina maarufu Studio. Akapanda
daladala lililokuwa linaelekea Kariaoo. Kijana
aliyekaa naye siti moja alijaribu kumchombeza kwa
hili na lile lakini alikuwa kimya hakumjibu chochote
na wala hakumsikia kwani mawazo yake yalikuwa
hatua kadhaa nje kabisa ya daladala. Yule kijana
alianza kuongea maneno ya kashfa. Vero akageuka
wakakutanisha macho yao. Hakuendelea tena
kuongea. Sura ya Vero ilitisha. Ilikuwa sura yenye
ujumbe mzito ambao yule kijana alishindwa
kuutafsiri lakini alijua ni ujumbe hatari. Sura
ambayo haikutaka mchezo wala utani. Haikuwa
sura ya kawaida ya kike. Yule kijana alijikuta
akikosa amani pale alipokaa. Alitamani gari lifike
ateremke. Alishaona balaa.
Baada ya kuteremka Vero alitembea kwa kasi huku
akikatiza mitaa mbalimbali ya Kariakoo. Baadae
akafika katika viwanja vya mnazi mmoja,
akaendelea kutembea kwa kasi huku akijitahidi
kuwa makini na magari katika kituo cha mnazi
mmoja. Akavuka salama, akaingia mtaa wa
Jamhuri.
Akatembea kwa kasi hadi alipokifikia kituo cha
mafuta cha BP.
“Habari yako dada.”
“Nzuri nikusaidie nini?”
“Naweza kumpata Samson Masanja.”
“Mh. Wiki ya pili sasa Samson kalazwa katika
Hospitali ya Amana.”
“Unaweza kunielekeza chumba alicholazwa?”
“Ukiingia pale Receiption uliza VIP wakikuelekeza
nenda chumba namba 9 ndiko alikolazwa.”
Akaondoka huku akimshukuru yule dada.
* * *
 
SEHEMU YA MWISHO

Akatembea kwa kasi hadi alipokifikia kituo cha
mafuta cha BP.
“Habari yako dada.”
“Nzuri nikusaidie nini?”
“Naweza kumpata Samson Masanja.”
“Mh. Wiki ya pili sasa Samson kalazwa katika
Hospitali ya Amana.”
“Unaweza kunielekeza chumba alicholazwa?”
“Ukiingia pale Receiption uliza VIP wakikuelekeza
nenda chumba namba 9 ndiko alikolazwa.”
Akaondoka huku akimshukuru yule dada.
* * *

DUKA LA VIFAA VYA HOSPITALI. Maandishi hayo
yalimvutia Vero ambaye moja kwa moja aliingia
mle dukani.
“Hili shilingi ngapi?” Aliuliza huku akishika koti
jeupe la hospitali.
“Elfu kumi na tano.” Alijibu yule muuzaji huku
akilitoa lile koti kwa mti maalum.
“Nipatie hilo.” Alisikika huku akitoa kiasi
alichoambiwa.
Akaliweka kwenye mfuko wake kisha akaondoka.
Baada ya nusu saa alikuwa maeneo ya Ilala.
Akaingia moja kwa moja pale hospitali. Akatembea
moja kwa moja hadi mapokezi.
“Habari dada.”
“Salama nikusaidie nini?”
“Naomba unielekeze VIP.”
“VIP ni huku (huku akinyoosha kidole) lakini kwa
sasa huruhusiwi kwa sababu huu si muda wa
kuona wagonjwa.” Alijibu yule dada wa mapokezi
ambaye kabla ya kufika Vero alikuwa anasinzia
pale dirishani.
Vero akaondoka pale dirishani na kuelekea upande
alioelekezwa. Bila kujali onyo alilopewa. Yule dada
wa mapokezi hakumwangalia Vero wakati anaingia
kule viliko vyumba vya VIP. Hakuingia moja kwa
moja. Akaingia chooni na kuvaa koti lile jeupe ili
asiweze kusumbuliwa kwani korido ilikuwa ndefu
mpaka kukifikia chumba namba 9.
Alipishana na manesi wawili ambao walionekana
kuwa busy huku wakitoka chumba kilekile
alichotaka kuingia. Akaingia mle chumbani.
Chumba kilikuwa na vitanda viwili lakini mgonjwa
alikuwa mmoja.
“Samson.” Aliita Vero
Mgonjwa dhaifu aliitika kwa sauti yenye
mikwaruzo.
“Nani.” Aliuliza mgonjwa huku akikohoa.
“mimi ni Vero unanikumbuka?”
“Sogea nikuone macho yangu hayaoni mbali.”
Vero akasogea karibu na mgonjwa.
“Umenikumbuka?” Aliuliza Vero huku akianza
kuingiwa na huruma kutokana na hali ya samson
Masanja.
“Bado.”
“Unamkumbuka mama Pili, yule mama wa
Buguruni ambaye alikuwa anafuga machangudoa?”
Aliuliza huku huruma aliyokuwa nayo ikianza
kupotea. Akamuona mgonjwa akishtuka kidogo.
“Sina muda wa kupoteza mimi ni mmoja wa watu
ambao kwa kutumia fedha zako uliweza
kutuambukiza virusi, Nimekuja kuchukua roho
yako. Kwani hustahili kifo cha kiungwana kama hiki
cha hospitali.” Alimaliza na kuchomoa kisu chake
chenye mpini mwekundu.
*****

Alikuwa anakaribia kupatwa na wazimu kwa
mshituko alioupata baada a kifo cha Fredi.
Veronika alikuwa amekamatwa. HUYU
ANAYEFANYA MAUAJI NI NANI? Lilikuwa swali
lisilojibika. Alifungua tena tepu ndogo ambayo
ilikuwa imerekodiwa wakati makachero wanamuhoji
Veronika.
“Nimeshindwa sasa kama munataka kunua niueni
tu…..” Alifoka Vero kwenye kinasa sauti kile.
Akasimama na kuanza kuzunguka zunguka huku
akikuna kichwa chake.
Ni muda huu ambao akili yake ilikuwa kama
imerudi. Akaanza kumkumbuka mkewe Vick na
mama yake. Alishangaa kugundua kuwa siku zote
hizo hakupata hata fursa ya kujiuliza wako wapi.
Upweke uliotawala kwenye nyumba yake ulimfanya
atokwe na machozi mara kadhaa.
UKO WAPI MAMA. Aliwaza huku akimkumbuka
mama yake mzazi, mama ambaye alikuwa na
huruma ya kweli mama ambaye aliyatoa maisha
yake kwa ajili ya manufaa ya mwanae. Alianza
kutokwa na machozi baada ya kuikumbuka familia
yake.
Akakumbuka kuwa mkewe alikuwa mjamzito.
Amejifungua? Au ameolewa na mwanaume
mwingine? Akainama pale mezani. Upweke ulikuwa
unamsulubu fikra zikarudi nyuma akakumbuka jinsi
alivyomfokea mkewe mpaka akaamua kutoroka.
Aliowathamini wote wamerudi mchangani.
Wakati akiwa kwenye dimbwi la mawazo simu yake
ikaanza kuita. Akaitazama ile namba akazidi
kuchanganyikiwa. Namba ya marehemu Lucy ndiyo
iliyoingia.
“Hallow habari Inspekta.”
“Ongea unachotaka kuongea.”
“Bila salamu?”
“Haya nzuri ongea.”
“Nataka ufahamu kuwa mimi ni muuaji mwenye
huruma kama mama yako mzazi. Kama una
kumbukumbu mama yako aliwahi kwenda mahali
kumuokoa dada ambaye alikuwa anakaribia
kuambukizwa virusi vya ukimwi na mumewe. Hivyo
kwa kufuata moyo nzuri wa mama yako na mimi
napenda kumuokoa huyo dada munayemshikilia
hapo. Moja napenda utambue kuwa mimi ndiyo
Vero, pili naona kazi zenu hamfanyi kitaalamu hivi
askari wakubwa kama nyinyi mnashindwa
kuoanisha alama za vidole za mtu munayemshuku
na zile zilizoko kwenye visu, huyo dada
mnamuonea tu kama unakumbuka vizuri siku ya
tukio ulipishana na mwendawazimu ambaye ndio
mimi, pia napenda kukufahamisha kuwa tayari
nimemaliza kazi kwa mtu wa mwisho nenda
chumba namba 9 upande wa VIP katika hospitali
ya Amana.”
Simu ilikatwa Inspekta akainua simu yake ya
mezani. Akiwa amechanganyikiwa kabisa
akampigia kachero Dadi kasweyaga.
“Hallow vipi afande.” Ilisikika simu upande wapili
“kuna mauaji mengine Amana.”
“Tumeshapata taarifa na maiti yake pamoja na ile
ya Fredi zote ziko hospitali ya Taifa ya Muhimbili
nilikuwa nakuja kukupa taarifa.”
“Halafu naomba huyo Vero aachiwe nafikiri
mahojiano na aina ya matukio yanayotokea
hahusiki kabisa.” Alimaliza Inspekta kisha
akaegemea kiti chake tena.
Akili yake ilifanya kazi kuliko uwezo wake wa
kawaida. Swali moja alilojiuliza ni kuhusu muuaji
ambaye ameweza kutoa historia ya maisha ya
mama yake siku za nyuma. Huyu mtu ni nani na
anataka nini. Hilo ni swali lililopita katika kichwa
cha Inspekta. Akatoa simu yake akajaribu kupiga
katika namba za Lucy. Simu ilikuwa
inaita.Hatimaye ikapokelewa.
“Enhe.” Iliuliza sauti kwa dharau kidogo.
“Nataka kujua ni kwanini umefanya mauaji mengi
kiasi hicho?”
“Kwa kuwa muda wangu wa kuishi umekwisha
nitakufahamisha kila kitu.”
“Tutaonana vipi?”
“Unakumbuka vizuri pale ulipokulia?”
“Una maanisha nini?”
“Unaikumbuka ile nyumba ya mbagala ambayo
ilikuwa ya marehemu baba yako?”
“Ndiyo nakumbuka vizuri.”
“Tukutane pale saa 12.30 Jioni.”
“Sawa.” Simu ikakatwa.
* * *
Huku hofu ikiwa imeutawala moyo wake Inspekta
alitembea Taratibu kuelekea eneo walilokubaliana
kukutana. Alipapasa mfuko wake wa kushoto.
Bado bastola yake ilikuwepo. Alikuwa amedhamiria
kuua ingawa alijiuliza sana kwa nini muuaji
ametaka wakutane eneo lile. Siku hii hakuvaa sare
zake za kazi. Alipofika eneo lile la kihistoria kwake
akashangaa kuona jinsi lilivyochakaa huku likiwa
limezungukwa na majumba makubwa ya kisasa.
Nyumba yao ilikuwa imeanguka upande mmoja.
Alipoangalia vizuri ndipo akashtuka baada ya
kuwaona mabinti wawili waliokuwa wamekaa
kwenye gogo lile la mnazi ambalo alikuwa
anapenda kukaa miaka mingi iliyopita.
“karibu.” sauti tulivu ya Vero ilimkaribisha.
Ulikuwa mshtuko wa mwaka. Asingeweza
kumsahau Vero kwani alifanana sana na mama
yake mzazi. Aliyemshangaa pale ni yule binti
mwingine ambaye alifanana na mkewe Vick.
“Vero. Unafanya nini hapa?” Aliuliza Inspekta huku
akionekana wazi kuchanganyikiwa na kusahau
dhamira yake ya kumuua muuaji.
“Baba, si unamtaka muuaji. Niko mbele yako
nifanye utakacho lakini kabla ya yote naomba
nikusimulie kila kitu kuhusu mauaji yale.” Huku
machozi yakimtoka akasimama na kuanza
kumsimulia Inspekta.
“…….. kutokana na ile sumu mama yangu aliishi
siku chache hatimaye akapoteza maisha akaniacha
mimi, Sara na bibi yetu ambaye alipoteza maisha
kutokana na kuzidiwa na homa za mara kwa mara
ambazo zilisababishwa zaidi na ukosefu wa
chakula bora. Baba tazama hayo makaburi….”
Inspekta akaangalia kule alikoelekezwa kidole. Ndio
kwanza akagundua kuwa kulikuwa na makaburi
mawili. Hilo la kwanza ni la mama yangu Vick
ambaye alikupenda akayapigania maisha yako kwa
nguvu zake zote lakini ukamtesa na kumnyanyasa
na hilo la pili ni la mama yako mzazi, amekufa
hata mazishi yake hujahudhuria………. Narudia tena
mimi ndio muuaji na sababu zangu nishakueleza.”
Sara na Inspekta walikuwa wanamwaga machozi.
Sara alikuwa analia kwa kuliona kaburi la mama
yake. Inspekta alikuwa analia kutokana na mjeledi
aliopigwa katika maisha yake.
“Baba sioni tena thamani ya kuendelea kuishi mimi
ni muathirika yanipasa kumfuata mama na bibi,
naomba umtunze huyo sara….”
“Hapana mwanangu usiniache peke yangu….”
Inspekta alilia kama mtoto mdogo huku
akimbembeleza Vero ambaye alikuwa ameshika
kisu mkononi.
“Hapana Vero mwanangu usifanye hivyo dawa ya
ukimwi ishagunduliwa mwanangu.” Alibembeleza
Inspekta huku akimnyooshea mkono mwanawe
asithubutu kujiua.
“Dada utaniacha na nani kama utakufa.” Sara naye
alilia akimbembeleza dada yake asijiue.
“Usijali Sara nimekufikisha mbele ya baba yako
atakutunza mimi naondoka.”
“Veroooooooooo.” Aligumia Sara kwa uchungu
wakati akimshuhudia dada yake akididimiza kisu
kifuani kwake mwenyewe.
Damu ziliruka zikarukia kwenye blauzi nyeupe ya
Sara. Vero alikuwa anakata roho huku
akimwangalia mdogo wake kwa macho yaliyojaa
huruma. Sara aliinama pale alipolala dada yake na
kumshikilia mabegani huku akilia kwa uchungu.
“Kwanini dada, kwa nini ufe.” Aliendelea kulalamika
Vero.
Inspekta naye aliendelea kulia kwa sauti kubwa.
Huku akimwangalia mwanae alivyokuwa anakata
roho. “Sara.” Aliita Vero. “Nakk…..kk..mh….”
Haijulikani alitaka kuongea nini akakata roho.
MWISHO
 
Ulikuwa uhondo bandika bandua pamoja sana na udumu mleta uzi.
 
SEHEMU YA MWISHO

Akatembea kwa kasi hadi alipokifikia kituo cha
mafuta cha BP.
“Habari yako dada.”
“Nzuri nikusaidie nini?”
“Naweza kumpata Samson Masanja.”
“Mh. Wiki ya pili sasa Samson kalazwa katika
Hospitali ya Amana.”
“Unaweza kunielekeza chumba alicholazwa?”
“Ukiingia pale Receiption uliza VIP wakikuelekeza
nenda chumba namba 9 ndiko alikolazwa.”
Akaondoka huku akimshukuru yule dada.
* * *

DUKA LA VIFAA VYA HOSPITALI. Maandishi hayo
yalimvutia Vero ambaye moja kwa moja aliingia
mle dukani.
“Hili shilingi ngapi?” Aliuliza huku akishika koti
jeupe la hospitali.
“Elfu kumi na tano.” Alijibu yule muuzaji huku
akilitoa lile koti kwa mti maalum.
“Nipatie hilo.” Alisikika huku akitoa kiasi
alichoambiwa.
Akaliweka kwenye mfuko wake kisha akaondoka.
Baada ya nusu saa alikuwa maeneo ya Ilala.
Akaingia moja kwa moja pale hospitali. Akatembea
moja kwa moja hadi mapokezi.
“Habari dada.”
“Salama nikusaidie nini?”
“Naomba unielekeze VIP.”
“VIP ni huku (huku akinyoosha kidole) lakini kwa
sasa huruhusiwi kwa sababu huu si muda wa
kuona wagonjwa.” Alijibu yule dada wa mapokezi
ambaye kabla ya kufika Vero alikuwa anasinzia
pale dirishani.
Vero akaondoka pale dirishani na kuelekea upande
alioelekezwa. Bila kujali onyo alilopewa. Yule dada
wa mapokezi hakumwangalia Vero wakati anaingia
kule viliko vyumba vya VIP. Hakuingia moja kwa
moja. Akaingia chooni na kuvaa koti lile jeupe ili
asiweze kusumbuliwa kwani korido ilikuwa ndefu
mpaka kukifikia chumba namba 9.
Alipishana na manesi wawili ambao walionekana
kuwa busy huku wakitoka chumba kilekile
alichotaka kuingia. Akaingia mle chumbani.
Chumba kilikuwa na vitanda viwili lakini mgonjwa
alikuwa mmoja.
“Samson.” Aliita Vero
Mgonjwa dhaifu aliitika kwa sauti yenye
mikwaruzo.
“Nani.” Aliuliza mgonjwa huku akikohoa.
“mimi ni Vero unanikumbuka?”
“Sogea nikuone macho yangu hayaoni mbali.”
Vero akasogea karibu na mgonjwa.
“Umenikumbuka?” Aliuliza Vero huku akianza
kuingiwa na huruma kutokana na hali ya samson
Masanja.
“Bado.”
“Unamkumbuka mama Pili, yule mama wa
Buguruni ambaye alikuwa anafuga machangudoa?”
Aliuliza huku huruma aliyokuwa nayo ikianza
kupotea. Akamuona mgonjwa akishtuka kidogo.
“Sina muda wa kupoteza mimi ni mmoja wa watu
ambao kwa kutumia fedha zako uliweza
kutuambukiza virusi, Nimekuja kuchukua roho
yako. Kwani hustahili kifo cha kiungwana kama hiki
cha hospitali.” Alimaliza na kuchomoa kisu chake
chenye mpini mwekundu.
*****

Alikuwa anakaribia kupatwa na wazimu kwa
mshituko alioupata baada a kifo cha Fredi.
Veronika alikuwa amekamatwa. HUYU
ANAYEFANYA MAUAJI NI NANI? Lilikuwa swali
lisilojibika. Alifungua tena tepu ndogo ambayo
ilikuwa imerekodiwa wakati makachero wanamuhoji
Veronika.
“Nimeshindwa sasa kama munataka kunua niueni
tu…..” Alifoka Vero kwenye kinasa sauti kile.
Akasimama na kuanza kuzunguka zunguka huku
akikuna kichwa chake.
Ni muda huu ambao akili yake ilikuwa kama
imerudi. Akaanza kumkumbuka mkewe Vick na
mama yake. Alishangaa kugundua kuwa siku zote
hizo hakupata hata fursa ya kujiuliza wako wapi.
Upweke uliotawala kwenye nyumba yake ulimfanya
atokwe na machozi mara kadhaa.
UKO WAPI MAMA. Aliwaza huku akimkumbuka
mama yake mzazi, mama ambaye alikuwa na
huruma ya kweli mama ambaye aliyatoa maisha
yake kwa ajili ya manufaa ya mwanae. Alianza
kutokwa na machozi baada ya kuikumbuka familia
yake.
Akakumbuka kuwa mkewe alikuwa mjamzito.
Amejifungua? Au ameolewa na mwanaume
mwingine? Akainama pale mezani. Upweke ulikuwa
unamsulubu fikra zikarudi nyuma akakumbuka jinsi
alivyomfokea mkewe mpaka akaamua kutoroka.
Aliowathamini wote wamerudi mchangani.
Wakati akiwa kwenye dimbwi la mawazo simu yake
ikaanza kuita. Akaitazama ile namba akazidi
kuchanganyikiwa. Namba ya marehemu Lucy ndiyo
iliyoingia.
“Hallow habari Inspekta.”
“Ongea unachotaka kuongea.”
“Bila salamu?”
“Haya nzuri ongea.”
“Nataka ufahamu kuwa mimi ni muuaji mwenye
huruma kama mama yako mzazi. Kama una
kumbukumbu mama yako aliwahi kwenda mahali
kumuokoa dada ambaye alikuwa anakaribia
kuambukizwa virusi vya ukimwi na mumewe. Hivyo
kwa kufuata moyo nzuri wa mama yako na mimi
napenda kumuokoa huyo dada munayemshikilia
hapo. Moja napenda utambue kuwa mimi ndiyo
Vero, pili naona kazi zenu hamfanyi kitaalamu hivi
askari wakubwa kama nyinyi mnashindwa
kuoanisha alama za vidole za mtu munayemshuku
na zile zilizoko kwenye visu, huyo dada
mnamuonea tu kama unakumbuka vizuri siku ya
tukio ulipishana na mwendawazimu ambaye ndio
mimi, pia napenda kukufahamisha kuwa tayari
nimemaliza kazi kwa mtu wa mwisho nenda
chumba namba 9 upande wa VIP katika hospitali
ya Amana.”
Simu ilikatwa Inspekta akainua simu yake ya
mezani. Akiwa amechanganyikiwa kabisa
akampigia kachero Dadi kasweyaga.
“Hallow vipi afande.” Ilisikika simu upande wapili
“kuna mauaji mengine Amana.”
“Tumeshapata taarifa na maiti yake pamoja na ile
ya Fredi zote ziko hospitali ya Taifa ya Muhimbili
nilikuwa nakuja kukupa taarifa.”
“Halafu naomba huyo Vero aachiwe nafikiri
mahojiano na aina ya matukio yanayotokea
hahusiki kabisa.” Alimaliza Inspekta kisha
akaegemea kiti chake tena.
Akili yake ilifanya kazi kuliko uwezo wake wa
kawaida. Swali moja alilojiuliza ni kuhusu muuaji
ambaye ameweza kutoa historia ya maisha ya
mama yake siku za nyuma. Huyu mtu ni nani na
anataka nini. Hilo ni swali lililopita katika kichwa
cha Inspekta. Akatoa simu yake akajaribu kupiga
katika namba za Lucy. Simu ilikuwa
inaita.Hatimaye ikapokelewa.
“Enhe.” Iliuliza sauti kwa dharau kidogo.
“Nataka kujua ni kwanini umefanya mauaji mengi
kiasi hicho?”
“Kwa kuwa muda wangu wa kuishi umekwisha
nitakufahamisha kila kitu.”
“Tutaonana vipi?”
“Unakumbuka vizuri pale ulipokulia?”
“Una maanisha nini?”
“Unaikumbuka ile nyumba ya mbagala ambayo
ilikuwa ya marehemu baba yako?”
“Ndiyo nakumbuka vizuri.”
“Tukutane pale saa 12.30 Jioni.”
“Sawa.” Simu ikakatwa.
* * *
Huku hofu ikiwa imeutawala moyo wake Inspekta
alitembea Taratibu kuelekea eneo walilokubaliana
kukutana. Alipapasa mfuko wake wa kushoto.
Bado bastola yake ilikuwepo. Alikuwa amedhamiria
kuua ingawa alijiuliza sana kwa nini muuaji
ametaka wakutane eneo lile. Siku hii hakuvaa sare
zake za kazi. Alipofika eneo lile la kihistoria kwake
akashangaa kuona jinsi lilivyochakaa huku likiwa
limezungukwa na majumba makubwa ya kisasa.
Nyumba yao ilikuwa imeanguka upande mmoja.
Alipoangalia vizuri ndipo akashtuka baada ya
kuwaona mabinti wawili waliokuwa wamekaa
kwenye gogo lile la mnazi ambalo alikuwa
anapenda kukaa miaka mingi iliyopita.
“karibu.” sauti tulivu ya Vero ilimkaribisha.
Ulikuwa mshtuko wa mwaka. Asingeweza
kumsahau Vero kwani alifanana sana na mama
yake mzazi. Aliyemshangaa pale ni yule binti
mwingine ambaye alifanana na mkewe Vick.
“Vero. Unafanya nini hapa?” Aliuliza Inspekta huku
akionekana wazi kuchanganyikiwa na kusahau
dhamira yake ya kumuua muuaji.
“Baba, si unamtaka muuaji. Niko mbele yako
nifanye utakacho lakini kabla ya yote naomba
nikusimulie kila kitu kuhusu mauaji yale.” Huku
machozi yakimtoka akasimama na kuanza
kumsimulia Inspekta.
“…….. kutokana na ile sumu mama yangu aliishi
siku chache hatimaye akapoteza maisha akaniacha
mimi, Sara na bibi yetu ambaye alipoteza maisha
kutokana na kuzidiwa na homa za mara kwa mara
ambazo zilisababishwa zaidi na ukosefu wa
chakula bora. Baba tazama hayo makaburi….”
Inspekta akaangalia kule alikoelekezwa kidole. Ndio
kwanza akagundua kuwa kulikuwa na makaburi
mawili. Hilo la kwanza ni la mama yangu Vick
ambaye alikupenda akayapigania maisha yako kwa
nguvu zake zote lakini ukamtesa na kumnyanyasa
na hilo la pili ni la mama yako mzazi, amekufa
hata mazishi yake hujahudhuria………. Narudia tena
mimi ndio muuaji na sababu zangu nishakueleza.”
Sara na Inspekta walikuwa wanamwaga machozi.
Sara alikuwa analia kwa kuliona kaburi la mama
yake. Inspekta alikuwa analia kutokana na mjeledi
aliopigwa katika maisha yake.
“Baba sioni tena thamani ya kuendelea kuishi mimi
ni muathirika yanipasa kumfuata mama na bibi,
naomba umtunze huyo sara….”
“Hapana mwanangu usiniache peke yangu….”
Inspekta alilia kama mtoto mdogo huku
akimbembeleza Vero ambaye alikuwa ameshika
kisu mkononi.
“Hapana Vero mwanangu usifanye hivyo dawa ya
ukimwi ishagunduliwa mwanangu.” Alibembeleza
Inspekta huku akimnyooshea mkono mwanawe
asithubutu kujiua.
“Dada utaniacha na nani kama utakufa.” Sara naye
alilia akimbembeleza dada yake asijiue.
“Usijali Sara nimekufikisha mbele ya baba yako
atakutunza mimi naondoka.”
“Veroooooooooo.” Aligumia Sara kwa uchungu
wakati akimshuhudia dada yake akididimiza kisu
kifuani kwake mwenyewe.
Damu ziliruka zikarukia kwenye blauzi nyeupe ya
Sara. Vero alikuwa anakata roho huku
akimwangalia mdogo wake kwa macho yaliyojaa
huruma. Sara aliinama pale alipolala dada yake na
kumshikilia mabegani huku akilia kwa uchungu.
“Kwanini dada, kwa nini ufe.” Aliendelea kulalamika
Vero.
Inspekta naye aliendelea kulia kwa sauti kubwa.
Huku akimwangalia mwanae alivyokuwa anakata
roho. “Sara.” Aliita Vero. “Nakk…..kk..mh….”
Haijulikani alitaka kuongea nini akakata roho.
MWISHO

willy nimeamini unahusika na id zote. we ndo mareche, kidi kudi, na analyse.

Tafadhali malizia Uchu
 
Hahaaa mkuu nimeisoma hii comment nimefurahi sana kwa sababu usilolijua daima litakusumbua.

Nashkuru Mkuu Willy Gamba kwa kumalizia mwendelezo wa hafithi hii.Maana nilitingwa na majukumu mengi

Hakika umefanya kazi nzuri


willy nimeamini unahusika na id zote. we ndo mareche, kidi kudi, na analyse.

Tafadhali malizia Uchu

Mkuu Ntamanolo naomba nikuhakikishie mm na Willy Gamba ni watu wawili tofauti.Wala husiwe na mashaka
 
Nashkuru Mkuu Willy Gamba kwa kumalizia mwendelezo wa hafithi hii.Maana nilitingwa na majukumu mengi

Hakika umefanya kazi nzuri
Tuko pamoja mkuu kusaidia pale panapohitaji msaada ni kitu kizuri ikizingatiwa wagonjwa wa riwaya kama mimi kukatishwa uhondo ni huzuni kubwaaa
 
Hahaha arosto imeisha!
Asnt sn mkuu,bonge la story
e31bda31da4e17f26fd2539333ab641f(0).jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom