Hadithi: Kisu chenye mpini mwekundu

Hadithi: Kisu chenye mpini mwekundu

mgh!!!!!..........sasa chuma kinaanza kukoli moto. Twende kazi Mkuu.
 
RIWAYA: KISU CHENYE MPINI MWEKUNDU
MTUNZI: Ahmad Mussa Mniachi
SEHEMU YA KUMI

Aliondoka pale nyumbani huku akikabiliwa na mtihani mgumu kwa mke wa Gervas.
Atampata vipi ili amweleze ukweli wa mambo. Iwapo atamueleza kweli haitamletea
matatizo. Aliona wazi kuwa kuna hatari ya kushtakiwa kwa kueneza maradhi wakati
anajua wazi kuwa yeye ni muathirika. Lakini kama angeweka wazi kweli angepata ule
msaada? Angeupata vipi wakati Gervas alikataahata fedha. Kwanini Gervas ambaye
kafunga ndoa kanisani atake liwazo lingine nje ya ndoa? Labda haya ni malipo mazuri
ya usaliti. Hapana lazima nimuokoe mkewe, nitajibu nini mbele ya Mungu kama yule
mwanamke atakufa kwa ajili yangu? Alijiuliza maswali mengi bila kupata njia sahihi ya
kumnusuru mwanamke mwenzake.
Maandishi makubwa ya shule ya Sekondari Mbagala yalimzindua kutoka kwenye lindi
la mawazo. Akatembea moja kwa moja kuelekea ofisi ya mkuu wa shule. Alikuwa hajui
kama afurahi au ahuzunike. Kitendo cha kupata nafasi ile baada ya kuudhalilisha utu
wake kilimuumiza sana. Alitamani amfanye jambo baya Gervas ambaye alimfanyia
mambo yale bila hiyari yake upande mwingine ukamwambia kuwa hakuwa na sababu
ya kufanya yote yale adhabu aliyoipata ilitosha.
Akaingia moja kwa moja kwenye ofisi ya walimu. Hakukuwa na mwalimu yeyote,
akafuata kidirisha kidogo kilichoandikwa MAPOKEZI.
“Habari yako dada.”
“Nzuri nikusaidie nini?”
“Naomba kuonana na mkuu wa shule.”
“Una tatizo gani?”
“kuna barua inabidi nimfikishie imetoka kwa Afsa elimu taaluma.”
“Ni barua ya kikazi au binafsi?”
“Ni barua ya kikazi.”
“Naomba hiyo barua.” Akampa. Yule dada akaisoma kisha akagonga muhuri.
“Nifuate.” Akafungua mlango na kuja kule nje aliko mama Beda. Akamfuata.
“kaa hapo.” Akakaa sehemu iliyoandikwa wageni.
Akaingia kwenye ofisi iliyoandikwa MKUU WA SHULE . Baada ya dakika kama kumi
na tano yule dada akatoka. Akampa karatasi nyingine zipatazo nne. “Mwanafunzi
amekubaliwa kujiunga lakini inabidi ujitahidi ndani ya wiki mbili awe amesharipoti.”
Aliongea yule dada.
“Ahsante.”Alisikika mama Beda huku akipiga hatua kuiacha ofisi ile.

* * *

Muda wa masomo ulikuwa umeisha wanafunzi wa Zanaki walianza kuondoka
madarasani. “Vick nisubiri nina maongezi kidogo na wewe.” Alisikika kijana mmoja wa
kidato cha nne akimsimamisha Vick. “Shikamoo.” Aliamkia Vick
“Aah. Noma hiyo hakuna mzee wa kuamkiwa hapa mambo.”
“Poa.” Alijibu Vick huku moyo ukienda mbio.
“Unajua Vick natafuta nafasi ya kuongea na wewe siku nyingi lakini siipati.”
“kwanza nani kakutajia jina langu?”
“Mtu ukimpenda tu lazima utajua jina lake.”
“unasema unatafuta nafasi ya kuongea na mimi, haya umeipata ongea basi?” alisikika
Vick huku akianza kushikwa na hasira.
“Neno langu ni fupi sana nakupenda Vick.” Vick hakujibu badala yake alitoka mbio.
“Vipi alikuwa anakuambia nini yule kaka mbona umetoka mbio?” Aliuliza Zuwena
mwanafunzi aliyekuwa anasoma nae darasa moja.
“Eti anasema ananipenda.”
“Mh. Mwenzangu kweli yule kaka ni fataki Ziada, Pili na mimi sote katutongoza
anataka amalize form one wote bora tumsemee kwa mkuu wa shule”
“Achana nae atatupotezea muda bure.”
Wakafika getini kila mmoja akaelekea upande wake. “Mbagalaa… Mbagalaa…” Konda
alimshitua vick ambaye alikuwa kwenye dimbwi la fikra. Akakimbilia lile gari.
Ilikuwa ni safari ya dakika arobaini na tano kufika rangi tatu. Aliteremka pale kituoni
na kupanda kwenye daladala lililokuwa linaelekea kongowe. Mawazo yake yote
yalikuwa kwa Beda. Alitaka kujua kama mpango wa kupata shule umefanikiwa. Hivyo
alipofika nyumbani tu alibadili nguo haraka na kuondoka. Hakukumbuka hata kula.
Ulikuwa ni umbali wa dakika kama Thelathini kwa miguu lakini alijikuta akitumia
dakika ishirini tu.
“Karibu Vick, ulikuwa unatamani kumuona mama yangu leo umemkuta.” Alisikika
Beda akimkaribisha.
“Oooh mwanangu huyo.” mama Beda akamkumbatia Vick kwa furaha.
“Karibu sana mwanangu.’
“Ahsante mama shikamoo.”
“Marahaba mwanangu hamjambo huko nyumbani?”
“hatujambo mama .” Alijibu Vick huku akiminyaminya vidole vyake kwa haya.
Akatembea taratibu hadi pale alipokaa Beda wakapeana mikono.
“Vipi umepata shule?”
“Nimepata Vick, Mungu atakulipa kwa wema ulionifanyia.” aliongea kwa sauti ya
kunong’ona lakini ilifika kwenye masikio ya mama yake.
“wapi?”
“Mbagala sekondari.”
“Hongera.”
“Ahsante.”
“Nilitaka kujua kama umepata shule, nashukuru kama umepata kwa heri.”
“Mbona mapema?”
“Hata chakula sijala nisije nikazusha maswali.”
“ Ahsante kwa moyo wako mwema” Akamuaga mama Beda, akaondoka

****

Alipanda ngazi taratibu kuelekea katika ofisi ya afisa elimu taaluma. Moyo wake
ulikuwa unapiga kwa kasi. Alijua wazi kuwa anayemwendea hayupo ofisini. Alikaa nje
ya ofisi muda mrefu akisubiri aondoke. Ni fursa hiyo ndiyo aliyoisubiri sana. Bahati
Ilikuwa upande wake kwani yule mtu aliondoka nusu saa kabla ya muda wa kazi
kumalizika. Hakutamani kabisa kuonana naye. Licha ya msaada aliompa bado
alimchukia kuliko mtu yeyote. Bila ridhaa yangu. Aliwaza kwa huku akisaga meno kwa
hasira.
Alikumbuka kuwa jana yake alikuwa hapa. Hakuwa na bahati kwani mlengwa alikuwa
miongoni mwa watu wa mwisho kutoka pale ofisini. Akafika hadi pale mapokezi
alipofikia siku ya kwanza. Ilikuwa ofisi ya mapokezi. Alimkumbuka vema yule dada
aliyempokea siku ya kwanza ingawa yule dada alimsahau mama Beda. “Habari dada.”
Alisalimia mama Beda.
“Nzuri nikusaidie nini?”
“Naweza kumuona Mr. Gervas?”
“Hapana ameondoka, mpaka kesho.”
“Unaweza kunielekeza nyumbani kwake?”
“Anaishi Kimara baruti, si mbali sana kutoka kituoni. Kama unatoka kariakoo ukishuka
kituoni nenda upande wa kushoto, fuata mtaa wenye maduka mwisho kabisa utakuta
saluni imeandikwa Mama K uliza hapo au nenda mbele kuna kanisa la mabati pia
unaweza kuuliza hapo kanisani kwani mkewe ni mwekahazina hapo kanisani.”
Sina swali amemaliza kazi. Aliwaza mama Beda huku moyoni akiwa na furaha kubwa.
Huyu dada kanisaidia sana sasa nina uhakika wa kumnusuru Mrs. Gervas. Aliendelea
kuwaza mama Beda. Akaondoka akiwa mwenye furaha kubwa sana.
Kimara baruti, kituo cha kwanza mtaa wenye maduka uliza Mama K saluni au kanisani,
kanisani ni kuzuri zaidi. Aliwaza huku akichukua beseni lake la matunda ambalo
aliliacha getini kwa mlinzi. Huyo, akaendelea kukata mitaa mbalimbali ya jiji hili lenye
kila aina ya raha na karaha. Akauza, akauza…. Alipofika Mtongani Beseni lilikuwa tupu.
Akapanda daladala ambalo lilimfikisha mbagala rangi tatu.

ITAENDELEA....
 
RIWAYA: KISU CHENYE MPINI MWEKUNDU
MTUNZI: Ahmad Mussa Mniachi
SEHEMU YA KUMI

Aliondoka pale nyumbani huku akikabiliwa na mtihani mgumu kwa mke wa Gervas.
Atampata vipi ili amweleze ukweli wa mambo. Iwapo atamueleza kweli haitamletea
matatizo. Aliona wazi kuwa kuna hatari ya kushtakiwa kwa kueneza maradhi wakati
anajua wazi kuwa yeye ni muathirika. Lakini kama angeweka wazi kweli angepata ule
msaada? Angeupata vipi wakati Gervas alikataahata fedha. Kwanini Gervas ambaye
kafunga ndoa kanisani atake liwazo lingine nje ya ndoa? Labda haya ni malipo mazuri
ya usaliti. Hapana lazima nimuokoe mkewe, nitajibu nini mbele ya Mungu kama yule
mwanamke atakufa kwa ajili yangu? Alijiuliza maswali mengi bila kupata njia sahihi ya
kumnusuru mwanamke mwenzake.
Maandishi makubwa ya shule ya Sekondari Mbagala yalimzindua kutoka kwenye lindi
la mawazo. Akatembea moja kwa moja kuelekea ofisi ya mkuu wa shule. Alikuwa hajui
kama afurahi au ahuzunike. Kitendo cha kupata nafasi ile baada ya kuudhalilisha utu
wake kilimuumiza sana. Alitamani amfanye jambo baya Gervas ambaye alimfanyia
mambo yale bila hiyari yake upande mwingine ukamwambia kuwa hakuwa na sababu
ya kufanya yote yale adhabu aliyoipata ilitosha.
Akaingia moja kwa moja kwenye ofisi ya walimu. Hakukuwa na mwalimu yeyote,
akafuata kidirisha kidogo kilichoandikwa MAPOKEZI.
“Habari yako dada.”
“Nzuri nikusaidie nini?”
“Naomba kuonana na mkuu wa shule.”
“Una tatizo gani?”
“kuna barua inabidi nimfikishie imetoka kwa Afsa elimu taaluma.”
“Ni barua ya kikazi au binafsi?”
“Ni barua ya kikazi.”
“Naomba hiyo barua.” Akampa. Yule dada akaisoma kisha akagonga muhuri.
“Nifuate.” Akafungua mlango na kuja kule nje aliko mama Beda. Akamfuata.
“kaa hapo.” Akakaa sehemu iliyoandikwa wageni.
Akaingia kwenye ofisi iliyoandikwa MKUU WA SHULE . Baada ya dakika kama kumi
na tano yule dada akatoka. Akampa karatasi nyingine zipatazo nne. “Mwanafunzi
amekubaliwa kujiunga lakini inabidi ujitahidi ndani ya wiki mbili awe amesharipoti.”
Aliongea yule dada.
“Ahsante.”Alisikika mama Beda huku akipiga hatua kuiacha ofisi ile.

* * *

Muda wa masomo ulikuwa umeisha wanafunzi wa Zanaki walianza kuondoka
madarasani. “Vick nisubiri nina maongezi kidogo na wewe.” Alisikika kijana mmoja wa
kidato cha nne akimsimamisha Vick. “Shikamoo.” Aliamkia Vick
“Aah. Noma hiyo hakuna mzee wa kuamkiwa hapa mambo.”
“Poa.” Alijibu Vick huku moyo ukienda mbio.
“Unajua Vick natafuta nafasi ya kuongea na wewe siku nyingi lakini siipati.”
“kwanza nani kakutajia jina langu?”
“Mtu ukimpenda tu lazima utajua jina lake.”
“unasema unatafuta nafasi ya kuongea na mimi, haya umeipata ongea basi?” alisikika
Vick huku akianza kushikwa na hasira.
“Neno langu ni fupi sana nakupenda Vick.” Vick hakujibu badala yake alitoka mbio.
“Vipi alikuwa anakuambia nini yule kaka mbona umetoka mbio?” Aliuliza Zuwena
mwanafunzi aliyekuwa anasoma nae darasa moja.
“Eti anasema ananipenda.”
“Mh. Mwenzangu kweli yule kaka ni fataki Ziada, Pili na mimi sote katutongoza
anataka amalize form one wote bora tumsemee kwa mkuu wa shule”
“Achana nae atatupotezea muda bure.”
Wakafika getini kila mmoja akaelekea upande wake. “Mbagalaa… Mbagalaa…” Konda
alimshitua vick ambaye alikuwa kwenye dimbwi la fikra. Akakimbilia lile gari.
Ilikuwa ni safari ya dakika arobaini na tano kufika rangi tatu. Aliteremka pale kituoni
na kupanda kwenye daladala lililokuwa linaelekea kongowe. Mawazo yake yote
yalikuwa kwa Beda. Alitaka kujua kama mpango wa kupata shule umefanikiwa. Hivyo
alipofika nyumbani tu alibadili nguo haraka na kuondoka. Hakukumbuka hata kula.
Ulikuwa ni umbali wa dakika kama Thelathini kwa miguu lakini alijikuta akitumia
dakika ishirini tu.
“Karibu Vick, ulikuwa unatamani kumuona mama yangu leo umemkuta.” Alisikika
Beda akimkaribisha.
“Oooh mwanangu huyo.” mama Beda akamkumbatia Vick kwa furaha.
“Karibu sana mwanangu.’
“Ahsante mama shikamoo.”
“Marahaba mwanangu hamjambo huko nyumbani?”
“hatujambo mama .” Alijibu Vick huku akiminyaminya vidole vyake kwa haya.
Akatembea taratibu hadi pale alipokaa Beda wakapeana mikono.
“Vipi umepata shule?”
“Nimepata Vick, Mungu atakulipa kwa wema ulionifanyia.” aliongea kwa sauti ya
kunong’ona lakini ilifika kwenye masikio ya mama yake.
“wapi?”
“Mbagala sekondari.”
“Hongera.”
“Ahsante.”
“Nilitaka kujua kama umepata shule, nashukuru kama umepata kwa heri.”
“Mbona mapema?”
“Hata chakula sijala nisije nikazusha maswali.”
“ Ahsante kwa moyo wako mwema” Akamuaga mama Beda, akaondoka

****

Alipanda ngazi taratibu kuelekea katika ofisi ya afisa elimu taaluma. Moyo wake
ulikuwa unapiga kwa kasi. Alijua wazi kuwa anayemwendea hayupo ofisini. Alikaa nje
ya ofisi muda mrefu akisubiri aondoke. Ni fursa hiyo ndiyo aliyoisubiri sana. Bahati
Ilikuwa upande wake kwani yule mtu aliondoka nusu saa kabla ya muda wa kazi
kumalizika. Hakutamani kabisa kuonana naye. Licha ya msaada aliompa bado
alimchukia kuliko mtu yeyote. Bila ridhaa yangu. Aliwaza kwa huku akisaga meno kwa
hasira.
Alikumbuka kuwa jana yake alikuwa hapa. Hakuwa na bahati kwani mlengwa alikuwa
miongoni mwa watu wa mwisho kutoka pale ofisini. Akafika hadi pale mapokezi
alipofikia siku ya kwanza. Ilikuwa ofisi ya mapokezi. Alimkumbuka vema yule dada
aliyempokea siku ya kwanza ingawa yule dada alimsahau mama Beda. “Habari dada.”
Alisalimia mama Beda.
“Nzuri nikusaidie nini?”
“Naweza kumuona Mr. Gervas?”
“Hapana ameondoka, mpaka kesho.”
“Unaweza kunielekeza nyumbani kwake?”
“Anaishi Kimara baruti, si mbali sana kutoka kituoni. Kama unatoka kariakoo ukishuka
kituoni nenda upande wa kushoto, fuata mtaa wenye maduka mwisho kabisa utakuta
saluni imeandikwa Mama K uliza hapo au nenda mbele kuna kanisa la mabati pia
unaweza kuuliza hapo kanisani kwani mkewe ni mwekahazina hapo kanisani.”
Sina swali amemaliza kazi. Aliwaza mama Beda huku moyoni akiwa na furaha kubwa.
Huyu dada kanisaidia sana sasa nina uhakika wa kumnusuru Mrs. Gervas. Aliendelea
kuwaza mama Beda. Akaondoka akiwa mwenye furaha kubwa sana.
Kimara baruti, kituo cha kwanza mtaa wenye maduka uliza Mama K saluni au kanisani,
kanisani ni kuzuri zaidi. Aliwaza huku akichukua beseni lake la matunda ambalo
aliliacha getini kwa mlinzi. Huyo, akaendelea kukata mitaa mbalimbali ya jiji hili lenye
kila aina ya raha na karaha. Akauza, akauza…. Alipofika Mtongani Beseni lilikuwa tupu.
Akapanda daladala ambalo lilimfikisha mbagala rangi tatu.

ITAENDELEA....

Vipi imekwisha?
 
Analyse kwema huko gheto????????????!!!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
****
Alipanda ngazi taratibu kuelekea katika ofisi ya
afisa elimu taaluma. Moyo wake ulikuwa unapiga
kwa kasi. Alijua wazi kuwa anayemwendea hayupo
ofisini. Alikaa nje ya ofisi muda mrefu akisubiri
aondoke. Ni fursa hiyo ndiyo aliyoisubiri sana.
Bahati Ilikuwa upande wake kwani yule mtu
aliondoka nusu saa kabla ya muda wa kazi
kumalizika. Hakutamani kabisa kuonana naye.
Licha ya msaada aliompa bado alimchukia kuliko
mtu yeyote. Bila ridhaa yangu. Aliwaza kwa huku
akisaga meno kwa hasira.
Alikumbuka kuwa jana yake alikuwa hapa. Hakuwa
na bahati kwani mlengwa alikuwa miongoni mwa
watu wa mwisho kutoka pale ofisini. Akafika hadi
pale mapokezi alipofikia siku ya kwanza. Ilikuwa
ofisi ya mapokezi. Alimkumbuka vema yule dada
aliyempokea siku ya kwanza ingawa yule dada
alimsahau mama Beda. “Habari dada.” Alisalimia
mama Beda.
“Nzuri nikusaidie nini?”
“Naweza kumuona Mr. Gervas?”
“Hapana ameondoka, mpaka kesho.”
“Unaweza kunielekeza nyumbani kwake?”
“Anaishi Kimara baruti, si mbali sana kutoka
kituoni. Kama unatoka kariakoo ukishuka kituoni
nenda upande wa kushoto, fuata mtaa wenye
maduka mwisho kabisa utakuta saluni imeandikwa
Mama K uliza hapo au nenda mbele kuna kanisa la
mabati pia unaweza kuuliza hapo kanisani kwani
mkewe ni mwekahazina hapo kanisani.”
Sina swali amemaliza kazi. Aliwaza mama Beda
huku moyoni akiwa na furaha kubwa.
Huyu dada kanisaidia sana sasa nina uhakika wa
kumnusuru Mrs. Gervas. Aliendelea kuwaza mama
Beda. Akaondoka akiwa mwenye furaha kubwa
sana.
Kimara baruti, kituo cha kwanza mtaa wenye
maduka uliza Mama K saluni au kanisani, kanisani
ni kuzuri zaidi. Aliwaza huku akichukua beseni lake
la matunda ambalo aliliacha getini kwa mlinzi.
Huyo, akaendelea kukata mitaa mbalimbali ya jiji
hili lenye kila aina ya raha na karaha. Akauza,
akauza…. Alipofika Mtongani Beseni lilikuwa tupu.
Akapanda daladala ambalo lilimfikisha mbagala
rangi tatu.
* * ************

Hakuhitaji daladala kumfikisha shuleni. Wiki hii ya
kwanza haikuwa ngumu sana kwake. Alifurahia
masomo ingawa shule aliyosoma ilikuwa na uhaba
wa walimu. Kwa kushirikiana na Vick aliweza
kupata vitu vingi zaidi. Ni kipindi hiki ambacho
uhusiano wake na Vick ulikua zaidi. Sasa
walitambuana rasmi kuwa ni wapenzi. Mapenzi yao
yalitambulika kwa mama Beda.
Kwa ujumla masomo yaliendelea vizuri. Siku moja
jioni akiwa chini ya mti pale nyumbani kwao Beda
alimuona Vick akimjia mbio.
“Vipi Vick mbona unanitisha?
“Usitishike Beda nimekuja kukufuata twende
twisheni.”
“Mbona sina hela ya kulipia hiyo twisheni?”
“Usijali nitakupa.” Aliongea kwa sauti ya
kunong’ona.
“wapi?”
“Rangi tatu kuna kituo kipya cha masomo ya jioni
kinachoendeshwa na wanafunzi wa chuo kikuu.”
Kisha wakaondoka kuelekea huko
* * ***********

Alianzisha tabia mpya kwenda kuuza matunda
maeneo ya Kimara baruti. Ni mitaa ambayo
hakuwa na mazoea nayo kabisa. Alilazimika. La
sivyo asingefanikiwa mpango wake. Ilikuwa siku ya
kumi sasa toka aanze kufanya biashara mitaa hii.
Ingawa alikuja maeneo haya kwa sababu tofauti na
biashara lakini alijikuta akipata wateja wengi na
faida kubwa. Kutokana na kuongezeka kwa idadi
ya wateja alilazimika kurudia mara mbili. Alileta
matunda asubuhi na jioni.
Kama zilivyo siku nyingine pia siku hii alipeleka
matunda pale saluni kwa Mama K. akiwa pale
saluni mara nyingi alipiga jicho nyumbani kwa
Gervas yule afisa elimu. Alifanya hivyo kwa siku
zote tisa. Alishaanza kukata tamaa ya kufanikiwa
mpango wake kitu kilichomfanya aanze kuzingatia
zaidi biashara. Wakati anaondoka pale saluni
akakutana na dada ambaye alikuwa amebeba begi
huku akiwa na mtoto mgongoni. Alikuwa
ameongozana na msukuma mkokoteni ambaye
alipakiza baadhi ya vitu kwenye mkokoteni wake.
Alitaka kumpuuza lakini mapokezi ya pale saluni
yakamshitua.
“Karibu Mama Gervas.” Alisikia sauti ya Mama
‘K’ yule mama mwenye saluni akimkaribisha yule
mgeni.
Mungu wangu ndiye yeye yule? Alijiuliza huku
moyo ukianza kupiga kwa nguvu. Ingawa dhamira
yake ilikuwa thabiti kwenye moyo wake hapa
alianza kuyumba. Alijiuliza kama amwambie au
aendelee kumficha. Msimamo wake ulianza
kuyumba. Akapiga moyo konde.
Ngoja amalize kuongea na wambeya wa pale
saluni kisha nitamfuata. Aliwaza mama Beda.
Baada ya kusalimiana na kina dada wa saluni
akaendelea na safari. Hakutaka kujiuliza akaanza
kumfuata nyuma taratibu. Alipofika pale nyumbani
kwake akasimama upande wa hatua kama kumi
kutoka nyumba ile akajifanya kuhesabu matunda
yake. Mtu mmoja aliyekuwa nyumba ya jirani
akamwita. “Matundaa.” akaenda kumuuzia. “Haya
maparachichi shilingi ngapi?” Aliuliza yule mteja.
Akamtajia bei kisha akamuuzia.
Baada ya hapo akajikuta ujasiri ukimwingia zaidi.
Akapiga hatua za haraka kuelekea kule nyumbani
kwa mke wa Gervas. Alishaamua kumwambia
ukweli wote.
Liwalo na liwe. Aliwaza kwenye nafsi yake huku
akilisogelea geti la nyumba ile. Kijasho chembamba
kilikuwa kinamtoka. Alihisi joto kuliko kawaida.
Pumzi zake aliona kama hazitoki vizuri. Alikuwa
anatetemeka lakini maji alishayavulia nguo. Aliona
utakuwa wehu kwenda bafuni na kurudi bila kuoga.
Huruma imewaponza wengi lakini sina jinsi.
Aliendelea kujifariji mwenyewe. Maadamu
nimeamua basi nifanye hayo mengine nimwachie
Mungu. Aliendelea kuupunguzia hofu moyo wake.
“Ngo.ngo.ngo.” aliendelea kubisha hodi kwa nguvu
ambayo ilisababishwa na hofu. Kama kungekuwa
na daktari ambaye angempima mapigo yake ya
moyo basi yalikuwa juu sana muda huu. Hofu hiyo
ilitokana na dhima iliyokuwa mbele yake. Alikuwa
na mambo mawili tu ya kuchagua: Anyamaze
amuue mwanamke asiye na hatia tena alishasikia
ni mlokole au atoboe ukweli avunje ndoa ya watu.
Uwezekano wa kuendelea kwa ndoa ya Gervas
na mkewe kama angetoa siri ile ulikuwa ni asilimia
kumi tu. Wapo wanawake wenye mioyo ya ajabu
ambao hukubali yote lakini sidhani kama ni hawa
wanawake wa kipindi hiki. Hata hao wa kipindi
hicho wengi wao ilikuwa ni simulizi ambazo hazina
uhakika kama ile simulizi ya wafalme wa nchi
fulani ambao ilikuwa ni sheria katika nchi yao
mfalme akifa kuzikwa na mkewe akiwa hai.
Nani yuko tayari kuyatoa sadaka maisha yake kwa
ajili ya mtu anayempenda? Watu huhatarisha
maisha yao kwa ajili ya fedha na si mapenzi. Hizi
ndizo zama tulizo nazo.

ITAENDELEA!!!!!
 
SEHEMU YA KUMI

Uwezekano wa kuendelea kwa ndoa ya Gervas
na mkewe kama angetoa siri ile ulikuwa ni asilimia
kumi tu. Wapo wanawake wenye mioyo ya ajabu
ambao hukubali yote lakini sidhani kama ni hawa
wanawake wa kipindi hiki. Hata hao wa kipindi
hicho wengi wao ilikuwa ni simulizi ambazo hazina
uhakika kama ile simulizi ya wafalme wa nchi
fulani ambao ilikuwa ni sheria katika nchi yao
mfalme akifa kuzikwa na mkewe akiwa hai.
Nani yuko tayari kuyatoa sadaka maisha yake kwa
ajili ya mtu anayempenda? Watu huhatarisha
maisha yao kwa ajili ya fedha na si mapenzi. Hizi
ndizo zama tulizo nazo.
“Karibu pita.” Sauti kutoka ndani ilimshitua. Ni
kana kwamba hakuitarajia hii sauti. Kwake ilitisha
kuliko simba. Alisahau kabisa kuwa ni yeye ndie
aliyebisha hodi. Upande mwingine akajilaumu
kwanini alikuja kutoa taarifa hii. Alikuwa hana
chaguo zaidi ya kuingia ndani. Kivumbi kilikuwa
hapo. Akakumbuka jinsi mtu anavyopewa taarifa
ya msiba wa kipenzi chake. Huanza kwa kufichwa
na kuliwazwa. Aanze vipi? Lilikuwa swali gumu
kwake. Kilichomtisha zaidi ni jinsi mke wa Gervas
atakavyolipokea.
“Ingiaaa.” sauti iliendelea kusisitiza huku mama
Beda akiwa ameganda pale getini. Kwa moyo
uliokosa ujasiri akasukuma lile geti na kuingia
ndani.
“Karibu dada, muda mrefu ulikuwa unabisha hodi
nakuambia ingia ulikuwa husikii?”
“Nilisikia. Kuna mtu nilikuwa namuuzia matunda.”
Alijitetea.
“Hapa ndani pako shaghalabaghala nyumba
ukimwacha mwanaume lazima ibadilike tu.”
“Sio wote dada unatuonea.” Msukuma mkokotena
alijitetea na kumfanya mke wa Gervas acheke.
Mama Beda alijaribu kulazimisha kucheka lakini
hakuweza. Asingeweza abadani. Kwani kucheka
sehemu kama ile ni sawa na kucheka mbele ya jaji
wakati una kesi ya mauaji.
“Ongea dada nataka kwenda kuoga.” Aliongea mke
wa Gervas.
“Nitaongea kwanza malizana na huyo mtu wa
mkokoteni nina maongezi muhimu sana.” Aliongea
kwa sauti ya msisitizo ambayo kidogo ilimtisha
Mrs Gervas ambaye alikuwa na mtoto mdogo
mgongoni.
“Karibu ukae ndani basi.” mama Beda akapita na
kukaa sebuleni. Hali ya sebuleni haikumpendeza
mke wa Gervas. Chupa za bia zilitawanywa hovyo,
baadhi ya glasi zilikuwa na mabaki ya bia.
Aliichukia sana tabia hii ya mumewe. Hakupenda
kabisa tabia ya ulevi. Kilichomshinda ni kuwa
walifunga ndoa kabla hajaokoka, hata yeye muda
huo alikuwa mnywaji. Hivyo alikosa mbinu nzuri ya
kumshawishi mumewe aache pombe wakati
anakumbuka wazi kuwa walikutana baa.
“Umesema shilingi elfu moja eeh.” Aliuliza mke wa
Gervas
“Ndiyo shangazi.” Alijibu kijana wa mkokoteni.
Akafungua zipu ya mkoba wake uliokuwa kwapani
akatoa noti ya shilingi elfu moja akampa.
Akaanza kupanga vitu kabla ya kwenda kuoga.
“Ni maongezi marefu?” aliuliza huku akiendelea
kupanga vitu pale sebuleni.
“Sana. Tena nitapenda tuongee baba mchungaji
akiwepo.”
“Mchungaji!” Diana mke wa Gervas akashituka
huku akiwa na mshangao wa wazi.
“Ni muhimu sana tena kwa faida yako.” Aliendelea
kuongea huku akihisi kupungukiwa na woga
alikokuwa nao hapo awali.
“Ngoja nimtume mtu aniitie.” Akatoka nje na
kumwacha mama Beda akijipongeza kwa mbinu
alizotumia. Alisikia kiu kikali lakini alishindwa
kunywa maji kwani mwenyeji wake alikuwa nje.
“Haya dada mi naenda kuoga wakati tunamsubiri
huyo mchungaji.” Aliongea Mrs Gervas.
“Hodi.” Sauti kali yenye mikwaruzo kiasi
ilimthibitishia mama Beda kuwa aliyeko nje ni
mchungaji.
“Karibu.” Alilazimika kukaribisha mama Beda kwani
mwenyeji wake alikuwa anaoga.
“Habari mama.” Alisalimia mchungaji.
“Nzuri baba shikamoo.”
“Marhaba.”
“Anakuja nafikiri anabadili nguo maana katoka
safari.”
Mchungaji akaitikia kwa kichwa huku na yeye
akijiuliza maswali mbalimbali maana alishazoea
waamini kwenda nyumbani kwake. Inapotokea
muamini akamuhitaji basi mara nyingi huwa ni
tatizo kubwa. Kuna tatizo gani kwa mtu huyu
ambaye ndio kwanza anatoka safari? Ni miongoni
mwa maswali ambayo yalipita kwenye kichwa cha
mchungaji.
Pangaboi lilikuwa linazunguka lakini mama Beda
hakuweza kuhisi kama kuna upepo ulikuwa
unamfikia pale alipokaa. Joto kwake lilikuwa kali
ingawa mchungaji alitamani ile swichi ya pangaboi
inayoruhusu kasi ya mzunguko ingepunguzwa.
“Karibu baba mchungaji.”
“Ahsante, Bwana asifiwe.”
“Ameen.” Wakapeana mikono kwa furaha.
Bado tu saa yenu ya kukatisha furaha. Aliwaza
mama Beda huku ujasiri wa kutimiza azma yake
ukianza kujirudia.
“Hongera sana, umepata mtoto gani?” Aliendele
kuuliza mchungaji.
“Wa kike amepewa jina la Merina na bibi yake.”
“Ooh Bwana ambariki sana na aibariki ndoa yenu.”
Hakuna ndoa na yule maluuni. Aliendelea kuwaza
mama Beda.
“Enhe nimesikia unaniita kuna maongezi muhimu.”
“Ni kweli nimekuita kwani kuna huyo mgeni hapo
anasema ana maongezi muhimu lakini kaweka
sharti la kuwepo mchungaji.”
“Enhe mama tunakusikiliza.” Alisikika mchungaji
huku akimgeukia mama Beda.
“Ni kweli nilikuwa nahitaji kuongea na Mrs Gervas
lakini nikaona si busara kutokana na uzito wa
mazungumzo niongee naye peke yake, ni
mazungumzo mazito mazito sana.” Alisisitiza na
kutulia kidogo jambo lililowatia hamu zaidi ya
kumsikiliza mchungaji na Mrs Gervas.
“Enhe.” Alisisitiza mchungaji huku akionyesha wazi
hamu ya kutaka kusikia hicho kilichosisitizwa kuwa
ni kizito.
“Nafikiri hatufahamiani, mimi naitwa Sakina
Msangi au mama Beda, mimi si mwenyeji mtaa
huu. Hii ni kama siku ya kumi toka nianze kujenga
mazoea ya huu mtaa lengo kuu ikiwa ni kuonana
na Mrs Gervas ili niongee jambo hili nililolikusudia
.” Akatulia na kusababisha hamasa ya kumsikiliza
izidi.
“Kama nilivyoeleza jambo lenyewe ni zito linahitaji
ujasiri kulieleza na kupokelewa kwake vile vile
unatakiwa ujasiri.”
Huyu mtu mbona hasemi maneno mengi tu kama
mshairi. Aliwaza mchungaji huku shauku yake
ikiongezeka maradufu.
“Kabla ya yot…………” hakuweza kumaliza
alilokusudia kuongea. Mlango ukagongwa kwa
nguvu huku sauti ya furaha ikifuatia. Sauti haikuwa
ngeni masikioni mwa mama Beda. Ni miongoni
mwa sauti zilizomkera sana, alimchukia sana
mwenye sauti hiyo. Alimkumbuka vema mtu huyo
ambaye ameuingiza utu wake kwenye idhilali
kubwa. Alikuwa ni mtu wa mwisho aliyehitaji
kumuona hapo. Afanyeje? Lilikuwa swali gumu
lililopita kwenye akili yake.
“Ooh karibu mke wangu.” Alifurahi Gervas huku
akimkumbatia mkewe.
Pale alipokaa mama Beda alikuwa
amechanganyikiwa, alijiuliza kama ataambiwa
aendelee na ile hadithi itakuwaje?
Eee Mungu ninusuru Sakina mimi. Aliomba moyoni
mwake.
“Twende chumbani mara moja nina maongezi
muhimu kidogo.” Aliongea kwa furaha Gervas huku
akisahau kuwasalimia wageni. Mchungaji
aliwasindikiza kwa macho mtu na mkewe wakati
wanaingia chumbani. Akaamua kurudisha macho
kwa mama Beda.
Hakuna mtu. Akapigwa na butwaa. Mama Beda
alikuwa ameshaondoka eneo lile. Yaani muda huu
huu? Alijiuliza mchungaji huku akishangazwa na
kitendo kile cha haraka.
* * *******

Alirudi nyumbani saa kumi na nusu. Siku hiyo
hakumuona kabisa Vick. Kuna mambo walikuwa
wanasimulia wanafunzi wenzake. Walisimulia
mambo mengi ambayo alikuwa hayajui. Alisimuliwa
raha ya kuwa na mpenzi. Siku ile alitamani sana
kujaribu kwa Vick yale mambo aliyosikia. Upande
mwingine nafsi yake ilisita. Lakini masimulizi yale
yalimhamasisha. Aah. Nisije kumuudhi Vick bure
nikakaosa msaada. aliwazaBeda. Akaendelea na
kazi ndogo ndogo za nyumbani.
Wakati akiendelea na kazi hizo mara akamuona
vick anakuja. Hakuwa Vick aliyemzoea. Vick
aliyemzoea alikuwa mtu mchangamfu tena mwenye
furaha. Leo Vick kaja mnyonge mwenye huzuni.
Kidogo hili lilimtatanisha Beda.
“Vipi vick mbona unanitisha?” alisikika Beda. Vick
hakujibu akaenda pale kwenye gogo la mnazi
alipokaa Beda. Akaanza kulia. Wakati analia mama
Beda naye akawasili. Akashangaa kumkuta Vick
analia.
“Enhe Beda, umemfanya nini mtoto wa watu.”
Aliuliza mama Beda huku akionyesha wazi
kutaharuki.
“Kaja sasa hivi tu mama sijui nini kinamliza.”
Mama Beda akambembeleza Vick ili aeleze
kinachomliza.
“Kuna mtu katoka hapa mtaani kaenda
kumwambia mama kuwa mimi nimejenga
mahusiano na familia ya wachawi eti ninyi ni
wachawi mama kanigombeza sana.” Mama Beda
hakupata tabu kumjua nani kapeleka taarifa hizo.
Alijua kuwa lazima atakuwa mke wa mzee Uwesu
kwani ndiye mwenye tabia za umbea kama huo.
“Pole sana mwanangu hiyo ndiyo dunia sisi
tumeishi hapa miaka mingi hatuna ugomvi na
yeyote lakini umaskini wetu ndio unaotutesa, labda
tungekuwa matajiri kama wao.” Mama Beda
aliongea kisha naye akaanza kulia.
“Usilie mama.” Kilio cha Vick kilikwisha akajikuta
akimhurumia zaidi mama Beda.
“Mama mimi nitakuwa nanyi muda wote wa
maisha yangu kwani nafahamu fika kwanini
unazushiwa hayo yote kama ni wekundu wa macho
mara nyingi naona jinsi unavyoshinda jikoni
ambako kuna moshi unaotokana na kuni za miti
mbalimbali usiwe na wasiwasi hata kama
nitafukuzwa nyumbani bado nitakuwa nanyi.”
Aliongea Vick kwa hisia kali jambo lililomfanya
mama Beda kutokwa na machozi zaidi.
* * *******

Gervas alipata taarifa kutoka kwa mfanyakazi
mwenzake kuwa amemuona mkewe kituo cha
daladala cha ubungo. Wakati huohuo alikuwa
amepata barua inayomtaka kwenda kwenye semina
ya uongozi chuo cha ADEM Bagamoyo. Semina
hiyo ilipangwa kufanyika siku inayofuata. Ilikuwa ni
semina ya siku saba. Akiwa mwenye furaha kwa
vyote viwili akaamua kupitia nyumbani ili
amsalimie na kumuaga mkewe kwanza.
“Nipeleke fasta si unajua tutaondoka jioni hii
kwenda Bagamoyo?” Alihimiza Gervas akiwa na
dereva wa gari lile la idara ya elimu katika
manispaa ya wilaya ya Temeke. Dereva akafanya
kama alivyoamrishwa na mkuu wake wa kazi.
Baada ya kuingia chumbani na mkewe akambusu
na kumshikashika mtoto huku akimbusu kwa
furaha.
“Vipi mume wangu mbona hujawasalimia wageni
pale sebuleni?”
“Ah. Samahani mke wangu furaha ilinizidia
nikashindwa hata kuwasalimia”
“Ina maana hata mchungaji hujamfahamu?”
“Yaishe mke wangu nimeshindwa kumfahamu
yeyote pale.”
“Eh. Nataka uniambie mbona unaonekana mwenye
haraka?” Aliuliza mke wa Gervas.
“Nimepata safari ya kikazi mke wangu, naenda
kwenye semina ya wiki moja bagamoyo.”
“Haya nakutakia safari njema.”
Wakatoka mle chumbani. Alipofika sebuleni
hakumuona mgeni mwingine wakapeana mikono na
baba mchungaji. Baada ya kusalimiana hakuuliza
kuhusu mgeni mwingine badala yake akaaga na
kuondoka.
Mchungaji alikuwa ametulia pale kwenye kiti.
“Mgeni yuko wapi?” Aliuliza Mrs Gervas.
“Ametoweka.”
“Ametoweka?”
“Ndiyo ni dakika chache za kufumba na kufumbua
sikumuona tena.”
“Mh. Makubwa tujaribu kumsubiri labda hajaenda
mbali”
Wakamsubiri mgeni hakutokea. Wakakata tamaa
kisha wakaagana.
* * *****

**Mama Beda ametoweka na bado hajasema
kilichomleta….
Je atafanikiwa kunusuru janga kwa mwanamke
mwenzake!!!!

ITAENDELEA!!!
 
SEHEMU YA KUMI NA MOJA

Mchungaji alikuwa ametulia pale kwenye kiti.
“Mgeni yuko wapi?” Aliuliza Mrs Gervas.
“Ametoweka.”
“Ametoweka?”
“Ndiyo ni dakika chache za kufumba na kufumbua
sikumuona tena.”
“Mh. Makubwa tujaribu kumsubiri labda hajaenda
mbali”
Wakamsubiri mgeni hakutokea. Wakakata tamaa
kisha wakaagana.
* * *

Zilikuwa zimepita siku tatu toka mgeni yule
atoweke. Mchungaji na Mrs Gervas walishaanza
kumsahau. Walijua ni mwehu au mtu aliyekuwa na
jambo fulani ambalo lilihusu pesa akashindwa
kuongea. Hawakulitilia maanani tena.
Siku hiyo mchungaji alikuwa kwenye mafundisho
ya kawaida ndani ya kanisa ndipo akatokea mtoto
mdogo ambaye alienda mbele moja kwa moja
akampa karatasi ambayo ilikuwa na ujumbe fulani.
Akaufungua na kuusoma.
Samahani mchungaji, niliondoka bila kukuaga ile
siku tuliyokutana nyumbani kwa Gervas kutokana
na sababu zisizoweza kuzuilika. Naomba tukutane
tena mahali palepale. Ulisomeka ujumbe huo na
kumfanya mchungaji akatishe somo. Akakumbuka
jinsi alivyovutiwa na mazungumzo ya yule dada
siku waliyokutana. Kutokana na shauku aliyokuwa
nayo hakutaka kupoteza muda akaingia kwenye
gari lake Prado nyeusi akaondoka kuelekea kwa
Mrs Gervas. Ulikuwa ni mwendo wa dakika tano
kwa gari kutoka kanisani hadi nyumbani kwa Mrs
Gervas.
Alipofika akashangaa kumkuta yule dada akiwa
amesimama mlangoni. Akasimamisha gari
wakasalimiana.
“Leo usitutoroke mama.” Alitania mchungaji huku
akicheka. Mama Beda hakucheka alikuwa ‘siriasi’.
Mchungaji akapiga honi mara tatu. Mrs Gervas
akaja kufungua geti. Akashituka baada ya
kumuona tena mama Beda akiwa pale getini. “Yesu
wangu.” Alishituka Mrs Gervas. Bado utashituka
sana. Aliwaza mama Beda huku akijikohoza
kuliandaa koo lake kwenda kulipua bomu zito.
Katika sebule ileile, tofauti ilikuwa ni mpangilio na
usafi wa ndani tu. Mama Beda alikaa akiwa
mwenye fikra nyingi hasa akihofia kutokea tena
mumewe yule dada mlokole.
“Haya nadhani tumekutana sasa.” Alianza
mchungaji mara tu baada ya kuhakikisha kuwa
wote wamesalimiana.
“Siri ya mkutano wetu unayo wewe bi Sakina au
mama Beda kama ulivyojitambulisha mwanzo lakini
kabla ya yote tunaomba maelezo kwanini
ulitutoroka.”
“Jambo nililotaka kuzungumza ndilo lililonifanya
nitoroke sikutaka Gervas awe hapa wakati
tunazungumza ni jambo zito ajabu.” akatulia
kidogo na kuwaangalia washiriki wenzake wa
mkutano ule ambao haukuwa na ajenda zilizo wazi
kwa wajumbe. “kabla ya kuendelea naomba nipate
uhakika kama Gervas yuko mbali na eneo hili.”
“Hilo usihofu kwani siku ileile Gervas alisafiri
kwenda Bagamoyo ambako wana semina ya siku
saba.”
“Ina maana hukuwahi kupata faragha na mumeo?”
Swali hili kidogo lilimkera Mrs Gervas.
“Faragha ipi unakusudia?” Aliuliza huku akionyesha
hasira kidogo.
“binti mbona unauliza maswali mazito?”
“Naomba nijibiwe kila ninachouliza na nafikiri
mutakubaliana na mimi kuanza na maswali
ambayo pengine munayaona ya kijinga nakusudia
faragha ya tendo la ndoa.”
“Hatujawahi kuipata hiyo faragha nafikiri mpaka
arudi.” Hakuwa na jinsi alilazimika kujibu.
“Sawa, sasa naona nieleze mkasa wote
uliosababisha tuwe hapa, awali ya yote naomba
uvumilivu mkubwa toka kwa Mrs Gervas.”
Akaanza kusimulia matatizo yake ya kimaisha
akianzia na la kufiwa na mumewe mpaka
kuhangaika juu ya ada ya mwanawe. Mrs Gervas
alikuwa analia kutokana na maelezo ya mama
Beda wakati mchungajia alilazimika kufuta machozi
kutokana na simulizi ile ya kusikitisha. Alitulia
kidogo na kuvuta pumzi kwani alikuwa anaelekea
kwenye kiini au ajenda kuu. Kisha akaanza kueleza
alivyohangaika kutafuta shule mpaka akakutana na
Gervas. Akatulia kidogo kwani mapigo ya moyo
yalishaanza kubadilika na kwenda kasi.
Kisha akaanza kusimulia jinsi alivyolazimishwa
kufanya mapenzi na Gervas. Mchungaji akamkazia
macho Mrs Gervas ambaye alitulia lakini
akionekana wazi kuhema kwa hasira. Alitaka
kuangua kilio lakini mchumgaji akawahi kumtuliza.
“kwa hiyo dada umetoka huko kuja kunitia
uchungu kwa kunisimulia uchafu wa mume
wangu?” Aliuliza Mrs Gervas kwa hasira akitamani
kumrukia mama Beda kwani alishasimama.
“Umemsumbua mchungaji kuja kusikia huo upuuzi
ili nidhalilike?”
“Tulia dada utanifanya chochote baada ya
kumaliza maneno yangu na sasa ninaelekea
ukingoni kwani nataka kueleza kile ambacho
sikupenda kukueleza ukiwa peke yako.” Akatulia na
kumkazia macho mwanamke yule ambaye
alijirudisha tena pale alipoketi na kuendelea
kumsikiliza mgeni yule.
“Mchungaji na Mrs Gervas, naomba niweke wazi
kuwa mimi ni muathirika wa virusi vya ukimwi na
mumeo alinilazimisha kukutana kimwili bila kinga
haikuwa hiyari yangu kama nilivyoeleza kuwa ni
kama alinibaka.” Hakuwa na haja ya kumaliza
maneno ya mwisho, neno lile lile kuwa yeye ni
muathirika liikuwa kama mkuki wa sumu uliopita
kwenye moyo wa Mrs Gervas. Alimkazia macho
mama Beda. Alikuwa mwenye bumbuwazi ya aina
yake. Hakujua kama alitakiwa kuhuzunika au
kufurahi.
Mchungaji naye pale alipokaa alikuwa amepigwa
na butwaa. Kwa dakika kadhaa hakuna aliyeongea,
hakuna aliyecheka na hata kulia pia. Hapo
mchungajia akaelewa kwanini yule mgeni aliuliza
kama Mrs Gervas na mumewe walishakutana
faragha. Moyoni alimsifu mwanamke yule kwa
ujasiri wa aina yake pia alipanga kulifanya tukio lile
kuwa moja ya masomo yake.
Akamgeukia mgeni na kumuuliza.
“Sina nia mbaya mama isipokuwa nataka kujua
lengo la kufanya yote haya ninini?”
“Nasikia huruma kwenye nafsi yangu sikutaka
mwanamke mwenzangu aingie kwenye matatizo
kama yangu. Nilihisi wazi nafsi ikinisuta ndio
maana nikaamua kufanya uchunguzi ili niweze
kujua aliko mke wa Gervas kwa bahati nikaelezwa
na mwenyewe Gervas kuwa mkewe amesafiri hivyo
nikaamua kufanya biashara maeneo haya ili kuvizia
isipatikane faragha ya ndoa kabla ya kupata
vipimo kutoka hospitali.” Mchungaji akatikisa
kichwa baada ya kusikia maelezo ya mama Beda.
Ingawa alikuwa kwenye taharuki bado Mrs Gervas
aliendelea kuwa mtulivu na kumsikiliza mama
Beda.
“Mama tunashukuru kwa maelezo yako; kimsingi
umefanya jambo la busara sana kulifikisha katika
namna nzuri kama hiyo. Pia napenda nikupe pole
kwa yote yaliyokukuta tena si vibaya
nikikupongeza kwa uamuzi wa kijasiri wa kukubali
kuja kuyapigania maisha ya mwenzako ingawa
hapo mwanzo tulianza kuchukizwa na maelezo
yako tukidhani kuwa wewe ni mshari lakini sasa
tunakubali kuwa Mungu ndiye aliyekuongoza
kufanya yote haya.”
Kabla hajaendelea kuongea Mrs Gevas akataka
kuanguka lakini mchungaji akawahi kumdaka.
Akamlaza vizuri pale kwenye kiti. Alikuwa
amepoteza fahamu. Mchungaji akaanza kumpepea.
Kama siku ya kwanza Mama Beda akatumia
mwanya huo kuondoka mle ndani.
Alikuwa amemaliza kazi, hakuwa na sababu ya
kuendelea kubaki pale. Akiwa na beseni lake la
matunda alitembea haraka kulekea kituo cha
daladala.
* * *

Jumamosi hii ilimkuta Beda akikusanya kokoto
kwa ajili ya kwenda kuuza. Kazi hii ilikuwa ngumu
lakini hakuwa na namna kwani kuna mahitaji
mengine madogo madogo aliona hakuna ulazima
wa kumwambia mama yake. Alikuwa na huzuni
kidogo kwani ni juma la pili alikuwa hajamuona
rafiki yake Vick. Hakujua nini kimemsibu. Yeye
ndiye aliyekuwa anampa fedha za matumizi.
Kukosekana kwake kwa hizo wiki mbili kulimfanya
atafute vibarua ambavyo vingemsaidia mahitaji
madogomadogo. Ndani ya wiki mbili alikuwa
amepasua mawe, amekusanya mchanga na
vibarua vingine ambavyo havikuendana na umri
wake.
Akiwa amebeba kiroba cha kokoto akakutana na
Happy mwanafunzi wanayesoma naye darasa
moja.
“Vipi Beda mambo.”
“Poa Happy unaenda wapi?”
“Nawahi twisheni vipi mbona wiki ya pili hii
hujaonekana twisheni?”
“Mambo ya fedha ndugu yangu, hapa naenda
kuuza hizi kokoto nipate chochote.” Alijibu.
“Haya wacha niwahi.” Alisema Happy huku
akiongeza mwendo.
“Ah. Samahani nilitaka kusahau.” Alirudi nyuma
Happy.
“Unajua Ijumaa umeondoka mapema sana kuna
mtu alikuja kukutafuta pale shuleni.”
“Yukoje?”
“Mbaba mmoja hivi mrefu wa wastani nasikia ni
afisa elimu.”
“Afisa elimu alikuwa ananitafuta mimi?”
“Ndiyo tena kauliza hadi nyumbani kwako lakini
wote tuliobaki hakuna aliyepafahamu.”
“Afisa Elimu?”
“Eeeh. Mbona unashangaa sana tena
nimekumbuka alijitambulisha kwa jina la Gervas
Msangi.”
“Hakueleza shida yake?”
“Hakuna aliyemuuliza kwani alionekana mtu
mwenye hasira huku macho yake yakiwa yameiva
kwa wekundu, nfikiri hata angekuwepo mtu
anayekufahamu asingethubutu kumuelekeza huko
kwako kutokana na hasira alizoonyesha.’
Beda akashituka baada ya maelezo hayo. Mtu
mwenye hasira ananitafuta nimekosa nini?
Alijiuliza Beda huku akianza kutawaliwa na hofu.
Hapy alikuwa ameshaondoka wakati Beda akiwa
ameishiwa nguvu za kubeba kile kiroba kutokana
na taarifa ile iliyomtatanisha. Likamjia wazo la
haraka, mapigo ya moyo yakaongeza kasi yake.
Alijua jinsi mama yake anavyoandamwa na mikosi.
Akarudi haraka nyumbani huku akikiacha kile
kiroba pale kilipo. Alipofika nyumbani akashituka
sana baada ya kukuta chanjo za gari pale
nyumbani kwao. Hofu ikazidi kuutawala moyo
wake. Alijua wazi kuwa mama yake yuko hatarini,
kwa kosa lipi? Alijiuliza.
Akakaa pale kwenye gogo akitafakari. Alikaa pale
kama masaa mawili ndipo akamuona mama yake
akirejea na beseni tupu.
“Vipi mwanangu mbona unaonekana huna raha?”
Aliuliza.
“Mama nahisi kuna matatizo yanatuandama tena.”
“Kwanini?”
“Nasikia kuna mtu mwenye hasira ambaye alikuja
kwa shari pale shuleni alikuwa ananitafuta,
wanasema ni afisa elimu alijitambulisha kwa jina la
Gervas Msangi.”
Akatulia na kumshangaa mama yake ambaye
aliyeonyesha kushitushwa na taarifa hiyo kuliko
alivyotarajia. Mama Beda alikaa chini akionyesha
kukosa nguvu kwa hofu.
“naomba unieleze ukweli mama umefanya nini?”
Mama Beda akainuka bila kusema lolote akamshika
mkono mwanawe kisha akaanza kumsimulia kila
kitu kuhusu Gervas mpaka siku aliyoenda
nyumbani kwake. Simulizi ile ilimfedhehesha sana
Beda. Alijisikia kudhalilika kwa mambo
aliyofanyiwa mama yake. Upande mwingine alijihisi
uchungu mkubwa baada ya kugundua kuwa mama
yake ni muathirika. Alishindwa kujua kama
ampongeze au amlaumu mama yake kwa hatua
alizochukua.
“Mama nakushauri uishi maisha ya kujificha
mpaka mambo yatakapopoa vinginevyo anaweza
kukuua huyu.”
“Mwanangu nimechoka haya maisha bora nife
siwezi kuendelea kuishi maisha ya mateso namna
hii.” Alisikika mama Beda huku akilia.
* * *

ITAENDELEA!!!
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI

“naomba unieleze ukweli mama umefanya nini?”
Mama Beda akainuka bila kusema lolote akamshika
mkono mwanawe kisha akaanza kumsimulia kila
kitu kuhusu Gervas mpaka siku aliyoenda
nyumbani kwake. Simulizi ile ilimfedhehesha sana
Beda. Alijisikia kudhalilika kwa mambo
aliyofanyiwa mama yake. Upande mwingine alijihisi
uchungu mkubwa baada ya kugundua kuwa mama
yake ni muathirika. Alishindwa kujua kama
ampongeze au amlaumu mama yake kwa hatua
alizochukua.
“Mama nakushauri uishi maisha ya kujificha
mpaka mambo yatakapopoa vinginevyo anaweza
kukuua huyu.”
“Mwanangu nimechoka haya maisha bora nife
siwezi kuendelea kuishi maisha ya mateso namna
hii.” Alisikika mama Beda huku akilia.
* * *

Semina ilikuwa imeisha. Gervas alirejea nyumbani
akiwa mwenye furaha kubwa. Alijua kuwa sasa
atapata muda wa kucheza na mtoto wake. Pia
alikuwa amemkosa mkewe kwa siku nyingi toka
alipoondoka akiwa mja mzito baada ya kujifungua
akaongeza miezi sita hukohuko. Gari lilisimama
mbele ya nyumba yake akaagana na dereva na
wanasemina wenzake ambao nao walikuwa na
hamu ya kufika majumbani kwao.
Akashangaa kuona akilakiwa na ukimya. Akafungua
mlango na kuingia ndani. Mkewe alikuwa amekaa
kwenye kiti bila kuonyesha hisia zozote za kuwa
aliyeingia ni nani kwake.”
“Vipi mke wangu mbona hivyo?” Mkewe hakujibu
akamkazia macho kama anaeyemuona mtu mgeni.
Gervas akashitushwa na hali ile. Akamsogelea
mkewe ili amshike.
“Usinishike.” Alifoka mkewe. “Eh. Una nini mke
wangu?” Aliuliza Gervas kwa mshangao.
“Sikiliza wewe baradhuli kuanzia leo, mimi sio
mkeo mpaka pale utakapopima na kuthibitishwa
kuwa ni mzima na huna maambukizi ya virusi vya
ukimwi.” Kauli hiyo ikamshitua na kumshangaza
Gervas.
“Umechanganyikiwa mke wangu?”
“Nani amechanganyikiwa mimi au wewe ambaye
husaidii watu mpaka uwadhalilishe.’
Hakugundua mapema nini maana ya kauli ile.
Akashika kichwa kisha akakaa.
“Mke wangu naomba unieleweshe vizuri maana
naona unazidi kunichanganya.”
“Kama kuchanganyikiwa basi mimi ni zaidi yako
kwani tunakoelekea ni kama kusema ndoa yetu
imefika mwisho.”
“Kwanini mke wangu mbona unaongea mambo
mazito?”
“hukumbuki wewe kama kuna mwanamke alikuja
kukuomba msaada kwa ajili ya mwanae aliyefaulu
ukaena nae gesti?” Gervas akatahayari baada ya
kusikia kauli ile.
“Mke wangu kwa nini unapenda kusikiliza
umbeya?”
“Sawa ni umbeya lakini siko tayari kuendelea na
wewe mpaka pale utakapopima.”
“Kwanini umeweka sharti la kupima.”
“Kwa sababu yule dada ni muathirika anaishi na
virusi vya ukimwi.”
Ikawa zamu ya Gervas kuchanganyikiwa. Akainuka
pale alipokaa. Akaanza kutembea tembea mle
ndani bila uelekeo. Kweli Gervas alikuwa
amechanganyikiwa kwani aliliona kaburi likiwa
mbele yake.
“Suala la msingi ni kwenda kupima huko
kuzunguka zunguka hakutasaidia kitu.” Aliendelea
kuongea Mrs Gervas. Akaingia chumbani kwake
akajitupa kitandani. Akaanza kulia. Hakuwepo wa
kumbembeleza kwani kutokana na kilio kile mkewe
alithibitisha kuwa ni kweli mumewe kafanya
kitendo hicho ambacho kinahatarisha ndoa yao.
“Muda umeenda mke wangu nitaenda kesho
kupima.” Sauti ya mumewe ilisikika kutoka
chumbani huku akilia.
Alijaribu kulala lakini usingizi haukuja. Akabaki
kukodoa macho huku akiwa na huzuni kubwa
kabisa. Hasira ilimjia kuhusu mama Beda. Alisahau
kabisa jinsi mama Beda alivyombembeleza kuhusu
kutumia kinga bila kukubali. Alijiuliza kwanini
hakuelezwa ukweli juu ya afya ya yule mama
ingawa kimsingi alijijua wazi kuwa asingeweza
kutoa msaada wowote bila malipo. Majuto ni
mjukuu na wakati wa kujuta ulikuwa umefika.
Upande mwingine alijilaumu kwanini alishindwa
kukubaliana na yule mama? Akaanza kulia tena
huku akikumbuka safari ya kwenda kupima siku
inayofuata.
Wakati yuko kwenye lindi la mawazo hakujua kama
mkewe alikuwa anapiga hatua kuiacha nyumba ile
akiwa na mtoto wake mchanga mgongoni. Begi
alishaliaandaa hivyo mumewe alipoingia chumbai
akaondoka na begi lake kuelekea nyumbani kwa
baba mchungaji. Hakutaka kulala pale mpaka
apate majibu ya mumewe.
Ingawa mumewe alikuwa kwenye wakati mgumu
hakukubali kubaki na kumliwaza kwani alijitia
kitanzi mwenyewe kwa kuisaliti ndoa yao. Kama
alitaka suluhu kwanza apime pili amfuate kwa
baba Mchungaji.
* * *

“Gervas Msangi.” Daktari wa hospitali ya wilaya ya
Temeke aliita. Akanyanyuka na kufuatiwa na
mkewe. Wote wakaingia kwenye chumba kile.
“Vipi mbona mmeingia wote wawili.” Alihoji daktari
“Huyu ni mume wangu.” Alijitetea mkewe.
“Bwana Gervas uko tayari kupokea matokeo mbele
ya mkeo?”
“Niko tayari alijibu.” huku akianza kubanwa pumzi
kutokana na hofu
“Vipimo vinaonyesha kuwa una maambukizi ya
virusi vya ukimwi hivyo….” Kuli ya dokta haikufika
mwisho Mrs Gervas aliinuka kwenye kiti na kutoka
nje haraka.
“Binti subiri….” Aliita dokta baada ya kumuona
akitoka mle ndani.
“Mke wangu nisubiri.” Alilalamika Gervas wakati
mkewe anakatisha kwenye kundi la watu mbio.
Msongamno wa watu pale hospitali ulimfanya
Gervas ashindwe kujua mkewe alikuwa amekimbilia
wapi. Akamtafuta pale hospitali hakumuona. Baada
ya kutafakari kwa muda akaamua kuchukua teksi
hadi nyumbani kwa baba Mchungaji.
“Ongeza mwendo dereva.” Alihimiza Gervas huku
akionekana wazi kuchanganyikiwa.
Gari ilikuwa kwenye kasi kikubwa kitendo
kilichowashawishi trafiki wa tazara kuwasimamisha
na kuanza kuwahoji. Kitendo hicho kilikuwa karaha
kubwa kwa Gervas ambaye alikuwa anajaribu
kuokoa ndoa yake. Moyoni alimchukia sana mama
Beda. Alimuona kuwa shetani mkubwa katika
maisha yake akiusahau ushetani alioufanya yeye.
“Naomba uturuhusu afande mke wangu anataka
kujifungua inabidi nimuwahi tumpeleke hospitali.’
Alibembeleza Gervas. Kwa jinsi alivyochanganyi
kiwa yule askari akamruhusu huku akiwahimiza
kuwa waangalifu.
Gari ikaongeza tena kasi yake hadi maeneo ya
kimara Baruti.
“Kata kushoto kisha nyoosha mpaka utakapoona
kanisa la mabati.” Alielekeza Gervas huku
akitamani kushika usukani. Gari ikafunga breki
mbele ya kanisa lile. Gervas akashangaa kuwakuta
waamini wa kanisa lile wakiwa nje
makundimakundi. Hakutaka kuuliza akatembea
hadi pale aliposimama baba mchungaji.
“Samahani mchungaji mke wangu amefika hapa?”
“Mke wako alikuwa hapa kama dakika kumi
zilizopita amechukua begi lake ameelekea huko
nyumbani kwako.”
“Akarudi tena kwenye teksi.”
“Anko utanilipa kweli?” Aliuliza dereva teksi.
“Kijana endesha gari tunachelewa.” Alifoka Gervas
huku akitoa noti kwa hasira. Dereva hakusema kitu
zaidi ya kupokea zile noti bila kuhesabu kwani kwa
macho tu zilikuwa nyingi kuliko malipo yoyote
ambayo angehitaji siku hiyo.
“Wapi?”
“Nyumba ile yenye geti jeusi.” Alielekeza Gervas.
Waliposimama gervas akakimbia kuelekea ndani.
Hakukuta mtu zaidi ya kuona wazi upungufu wa
baadhi ya vitu mle ndani. Alijua nini kimefanywa na
mkewe. Akaanza kulia kwani alijua wazi kuwa
hawezi tena kumpata mkewe. Akatoka nje huku
machozi yakimtoka. “Twende Ubungo bus
terminal.” Alihimiza Gervas huku akiingia kwenye
teksi.
Teksi iliondoka kwa kasi hadi ubungo. Wakati
wanataka kuingia wakakutana na basi lililokuwa
linatoka. Siti ya nyuma kabisa Mrs Gervas
alikutanisha macho na mumewe aliyekuwa kwenye
teksi. Akampungia mkono. Pingu ya maisha ilikuwa
imefunguka. Hakuna shaka huo ulikuwa ni mwisho
wa maisha matamu ya ndoa ambayo tamaa ya
Gervas ilimfanya ayatie sumu na kuyaharibu
mwenyewe. Alitikisa kichwa huku akitazamana na
mkewe ambaye naye alikuwa anatokwa na
machozi. Ulikuwa mwisho mchungu kama shubiri.
Akachungulia tena dirishani huku akilitazama kwa
uchungu jinsi basi lile lilivyokuwa linauacha mji wa
Dar es salaam. Kwa jinsi alivyochanganyikiwa
dereva hakutaka kuuliza akaamua kumpeleka
nyumbani kwake.
* * *

Miezi ikakatika mwaka ukaisha yule afisa elimu
hakuonekana tena. Hofu ya mama Beda ikaisha.
Tayari Beda alikuwa kidato cha pili. Hakukuwa na
mabadiliko katika maisha yao. Vick alikuwa
anakuja mara moja moja na kumpa msaada Beda.
Hakuwa na nafasi nzuri ya kupata fedha kama
alipokuwa kidato cha kwanza. Upotevu wa fedha
wa mara kwa mara ulimfanya baba yake ashindwe
kujua ni nani anahusika hivyo akaamua kubadilisha
namna ya utunzaji wa fedha. Beda alilazimika
kuingia mtaani siku za jumamosi na Jumapili na
kufanya vibarua mbalimbali.
Jumamosi moja Beda alikuwa amejipumzisha
nyumbani. Siku hiyo hakwenda kwenye vibarua
vyake. Akiwa kwenye lile gogo la mnazi alilozoea
kukaa akamwona Vick akimjia. “Karibu dear.”
Alikaribisha Beda kwa utani.
“Ahsante, mama nimemkuta?”
“Ameshaondoka kwenda kwenye biashara zake.”
“Leo baba na mama wamesafiri tena, nataka
kutoroka kama siku ile nije kulala kwako.”
“Poa tu unakaribishwa sana.”
“Leo sichelewi inabidi niwahi kuwawekea maji
kuku.”
“Kumbe munafuga kuku?”
“Ndio tuna kuku wa kisasa kama mia nne.”
Wakaagana na Vick.
Muda mfupi baada ya kuondoka Vick mama Beda
akawasili.
“Shikamoo mama.”
“Marahaba mwanangu habari za shule.”
“Mama leo jumamosi mara hii umesahau.’
“ah. Mwanangu mi naishi tu sijui hata siku” Kauli
hiyo ikamchekesha Beda.
* * *

“Beda, Beda……..” Sauti iliita kutoka Dirishani. Sauti
hiyo haikuwa ngeni katika masikio ya Beda.
Asingeweza kuishangaa sauti ya vick hata kidogo.
Akatembea kwa kunyata ili mama yake asisikie.
Akafungua mlango. Vick akiwa na kandambili zake
mkononi akazama ndani. Mlango ukafungwa
wakaingia chumbani kwa Beda. Kibatari
kikazimwa.
Saa kumi kamili wote walishitushwa na adhana.
“kumekucha Vick twende nikusindikize.”
Wakaondoka. Ulikuwa ni mwendo wa dakika
ishirini. Walipofika Beda akamwacha Vick pale
getini. Akamuona Vick akivuta geti ambalo
alilitegesha ili atakaporudi apate urahisi wa
kuingia. Akageuka na kurudi nymbani akiwa na
furaha ya kufungua ukurasa mpya na Vick. Ilikuwa
ni siku yao ya kwanza.
Baada ya miezi minne Vick alianza kusumbuliwa
na kichwa mara kwa mara. Si hivyo tu mara nyingi
alisinzia darasani na kulalamika kizunguzungu. Hali
hiyo ilimtia wasiwasi mwalimu wa darasa ambaye
aliamua kufuatilia afya ya mwanafunzi wake.
Akamchukua hadi zahanati ya shule.
“Vick, nimekuleta huku ili nipate uthibitisho wa
afya yako.” Aliongea mwalimu wake wa darasa.
“Muda wa vipimo ukafika.”
* * *

**Nini tena kinajiri kwa Vicky…..
ITAENDELEA!!!
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU

Baada ya miezi minne Vick alianza kusumbuliwa
na kichwa mara kwa mara. Si hivyo tu mara nyingi
alisinzia darasani na kulalamika kizunguzungu. Hali
hiyo ilimtia wasiwasi mwalimu wa darasa ambaye
aliamua kufuatilia afya ya mwanafunzi wake.
Akamchukua hadi zahanati ya shule.
“Vick, nimekuleta huku ili nipate uthibitisho wa
afya yako.” Aliongea mwalimu wake wa darasa.
“Muda wa vipimo ukafika.”
* * *

Moja ya furaha iliyokuwa inarindima katika kichwa
cha sajenti wa jeshi la wananchi Frank kilindo ni
barua ya likizo iliyokuwa pale mezani kwake.
Ilikuwa ni likizo ya miezi mitatu. Alikuwa
amepanga kuutumia muda wake wa likizo
nyumbani kwao Mahenge. Hakuweza kufikiria
kama kuna kitu kingekatisha furaha ile. Akiwa
kwenye mawazo hayo ya furaha ghafla, simu yake
ya kiganjani ikaanza kuita. Akaitoa ile simu
mfukoni kisha akaangalia mpigaji ni nani. Ilikuwa
namba mpya akaamua kupokea.
“Hallow unaongea na sajenti kilindo hapa nani
mwenzangu.”
“Naitwa mwalimu Mateka ni mwalimu hapa
zanaki” Ilijibu sauti upande wa pili kisha
ikaendelea.
“Kuna taarifa kuhusu mwanao Vick, tumempima
ameonekana ana ujauzito wa miezi miwili.”
“Uhfuuu.” akashusha pumzi sajenti.
Akatoka ofisini huku furaha yake yote ikimezwa na
hasira. Akaingia kwenye gari lake na kuliondoa
kwa kasi kuelekea nyumbani. Njia nzima alikuwa
anasonya kwa hasira huku akitamani kukutana na
Vick amrarue.
Alipofika nyumbani akafunguliwa geti na mkewe.
“Vipi baba Vick, mbona hivyo?” Aliuliza mkewe
baada ya kuona jinsi numewe alivyobadilika.
“Naomba maji baridi.” Hakutaka kujibu swali la
mkewe. Baada ya kunywa maji akaongea bila
kumtazama mkewe. Alikuwa kama anayeongea na
mtu amabye anamuona peke yake.
“Yaani nahangaika ili mwanangu asome leo
anakuja kuniletea mimba.”
“Nini?” Mama yake alipatwa na mshituko.
“Mwanao Vick ana mimba ya miezi miwili
nimepigiwa simu kutoka shuleni kwao.”
“Paaaa.” Chupa ya chai iliyokuwa mkononi ilimtoka
mama Vick kwa mshituko alioupata.
Akakaa kwenye kiti na kushika tama. Furaha ya
likizo ilikuwa imeyeyuka. Hakuna aliyefurahia tena
safari yao ya Mahenge.
Muda wa kumsubiri Vick ili amalize hasira zake
kwa kipigo atakachompa ulikuwa mrefu mno.
Alishauweka mezani ule mkanda wa jeshi tayari
kwa kipigo. Hasira kali ilirindima kwenye nafsi
yake.
Masaa yalizidi kuyoyoma Vick hakutokea
nyumbani. Subira ikamshinda Sajenti. Akaamua
kumfuatilia hukohuko shuleni. Jua lilikua linaanza
kuwaaga wakazi wa Dar. Haikuwa kawaida ya Vick
kurudi usiku lakini muelekeo ulionyesha kuwa
angerudi usiku. Licha ya uchungu kwa kitendo
kilichofanywa na mwanae bado mama Vick alikuwa
na wasi wasi na hatua itakayochukuliwa na
mumewe. Alijua jinsi gani mumewe anakuwa mtu
hatari akiwa na hasira. Aliogopa sana kuwa
anaweza kumuua mwanawe lakini aliogopa zaidi
kumzuia kwani kitendo hicho kingemfanya aone
kuwa walikuwa na ushirikiano pia aliogopa
kugeuziwa kibao na kupata kipigo cha paka mwizi.
Akaamua kutulia na kumwacha mumewe afanye
atakalo.
* * *

Baada ya kupata matokeo Vick aliondoka shuleni
akiwa kama aliyechananyikiwa. Alikuwa anajiuliza
nini atamwambia baba yake kwani alishapewa
barua ya kufukuzwa shule. Kila aina ya uongo
aliofikiria kutunga alijua wazi kuwa usingekubalika
mbele ya baba yake. Kilichomtia hofu zaidi ni
uwezekano wa baba yake kupata taarifa kutoka
shuleni moja kwa moja. Akaona hana sababu ya
kuongopa isipokuwa asubiri aone majaliwa yake
yatakuwaje. Hakutaka kwenda nyumbani moja kwa
moja akaamua kupitia kwa Beda. Hakukuta mtu.
Kwa kuwa alijua pale walipoficha funguo
akachukua na kufungua mlango kisha akajilaza
kwenye jamvi lililochoka pale sebuleni. Akashikwa
na usingizi akalala.
Saa kumi na mbili na nusu akaamshwa na Beda
ambaye aliingia ndani na kushangaa baada ya
kumuona Vick akiwa amelala pale.
“Vipi Vick kulikoni?” Aliuliza Beda. Akaamka
akafuta macho kwa mkono wake wa kuume.
“Kuna matatizo Beda.” Alianza kuongea huku
akitazama chini.
“Kuna nini?”
“Nimefukuzwa shule.”
“Umefanya kosa gani?”
“Nina ujauzito wa miezi miwili Beda.”
Kwanza alihisi tumbo likianza kuunguruma kisha
akakaa pale kwenye jamvi.
“Una mimba?” Aliuliza Beda kwa mshangao. Ni
kitu ambacho hakukitarajia kabisa.
Vick akaanza kulia. Ni wazi hakuna mtu
aliyemuogopa zaidi ya baba yake. Alikuwa
anajiuliza ni hatua gani itachukuliwa baada ya
kufukuzwa shule.
* * *

Sajenti Frank Kilindo aliamua kurejea nyumbani
baada ya kugundua kuwa hasira zilikuwa
zinamwendesha vibaya. Ni hasira tu zilizokuwa
zinamchanganya hata akashindwa kuvuta subira
na kumsubiri Vick.
Saa 1.32 Vick akawasili nyumbani. Alijitahidi
kuficha kilio na huzuni yake. Alipofika sebuleni
akamkuta baba yake akiwa amekaa mkao ambao
haukumpa shida kuutafsiri kuwa ameshapata
taarifa. Huku akitetemeka akakatisha pale sebuleni
hadi chumbani kwake bila kumsalimia baba yake
kama alivyozoea. Baba yake naye akajifanya kama
hajamuona.
Baada ya dakika chache Vick akajisalimisha pale
sebuleni kwani alijua kitendo cha kubaki chumbani
kingemfanya baba yake amfuate jambo ambalo
lingekuwa hatari zaidi kwake.
“Habari za shule mwanangu.”Alisalimia sajenti.
Anaigiza? Alijiuliza Vick.
“Nzuri shikamoo baba.”
“Marhaba vipi habari za shule.”
“Nzuri.” Alijibu Vick huku akijua wazi kabisa kuwa
maswali yote hayo yalikuwa ni mtego tu.
Asingeweza kudanganyika kabisa kuwa baba yake
alimsalimia katika hali ya kawaida.
“Mwanangu, najua kabisa kuwa una uja uzito.”
Aliongea kwa sauti tulivu ambayo ilimshangaza
hata Vick. Baada ya kupiga chafya akaendelea.
“Nilikuwa nimekuandalia adhabu kali sana, nafikiri
unauona huo mkanda hapo mezani. Nimefikiria
muda mrefu nimeona hakuna sababu ya
kukuadhibu kiasi hicho kwani ni kosa lako la
kwanza hivyo jiandae jumatatu twende hospitali
tukaitoe hiyo mimba.” Aliongea sajenti kwa sauti
tulivu ambayo ilimshangaza hata mkewe ambaye
alikaa karibu na dirisha ili kuweza kujua nini
kitatokea.
“Unaweza kwenda.” Vick akaondoka kurudi
chumbani huku akiwa haamini kabisa kilichotokea.
* * *

Jumatatu ilimkuta vick akiwa kwenye zahanati ya
Sakina ambayo iko Tandika sokoni. Zahanati hii
ilikuwa na kitu cha ziada kwa Vick. Asingeweza
kusahau jinsi mwanafunzi mwenzao Hawa
alivyopoteza maisha baada ya kujaribu kutoa
mimba katika hospitali hiihii. Ilikuwa ni baada ya
kupata sifa kuwa kuna daktari nzuri wa kukatisha
uhai wa watoto ambao bado hawajauona mwanga
wa dunia hii. Wazo likapita kichwani mwake,
kwanini atoe mimba? Mama yake alikuwa
ameingia chumba cha daktari. Jinsi mikasi na
vyombo vya hospitali vilivyokuwa vinagongana
vilimtia hofu sana.
Hakutaka kumsubiri mama yake, aliamua kuondoka
akiwa na uamuzi wa kutotoa mimba. Alishaamua
kuwa liwalo na liwe. Wakati mama yake akiongea
na daktari juu ya gharama za shughuli ile vick
alikuwa anapiga hatua kuelekea kituo cha daladala
pale Tandika. Akakatisha pale kituo cha polisi
akatokea barabarani. Huku akigongana na watu
kutokana na msongamano aliendelea kutembea
kasi. Mara kadhaa alilazimika kupokea matusi
kutoka kwa wanawake wenzake ambao aligongana
nao wakati wa kupishana. Wanaume ni watu wa
ajabu, hali ile ya kugongana na wanawake kwao
ilikuwa ni faraja ingawa nao walichukia pale
walipogongana na wanaume wenzao.
Aliyapuuza macho ya watu waliokuwa
wanamshangaa kwa haraka aliyokuwa nayo.
Akafika kituo cha daladala zinazoelekea Mbagala.
Akaingia kwenye daladala lililokuwa linakaribia
kujaza abiria.
Siku ya tukio alipata msamaha . Itakuwaje leo
baba yake atakapopewa taarifa za kukimbia kwa
daktari. Ni kweli inaweza kutokea miujiza kama ya
siku ile? Mkanda wa jeshi ulikuwa mezani lakini
ghafla sajenti yule wa jeshi la wananchi akabadili
mawazo. Kwa upole kabisa akampa nafasi
mwanawe. Ilikuwa ni nafasi ngumu ambayo
ilimuathiri Vick kifikra. Kwanza alikuwa anatakiwa
kuua kiumbe asiyekuwa na hatia, pili alikuwa
anahatarisha maisha yake. Hakuwa tayari kufanya
lolote kati ya hayo, Ujasiri ulikuwa mkubwa kwenye
nafsi yake. Alijiandaa kukabiliana na kipigo,
alijiandaa kuabiliana na lawama za aina yoyote.
Alikuwa siti ya dirishani huku akiangalia nje.
Alikuwa anaangalia nje lakini fikra zake zilikuwa
zimeondoa uwezo wa macho. Hakuweza kuona
chochote kule nje. Macho yake yaliona vitu tofauti
na vitu halisi vilivyokuwa mbele ya macho yake.
Aliweza kumuona baba yake akiwa na ule mkanda
wa jeshi, aliweza kumuona Beda akimbembeleza
na kumliwaza baada ya kupigwa kwa mkanda ule.
Pia aliweza kumuona mama yake akimtafuta pale
‘Dispensary’ bila mafanikio. Haiwezekani huu ni
uuaji. Aliwaza.
Saa 6.30 aliwasili Mbagala. Akaanza kutembea
kwa miguu huku akiwa hajitambui vema kutokana
na mawazo. Baada ya dakika kadhaa akafika
nyumbani . Moja kwa moja akaelekea chumbani
kwake ambako alijilaza kitandani na kuyaelekeza
macho yake juu.
Alilishika tumbo lake, bado lilikuwa dogo halikuwa
na dalili yoyote ya kuonyesha kuwa ni mja mzito.
Baada ya mawazo ya muda mrefu akapitiwa na
usingizi.
Akashtushwa na vishindo vya mtu aliyekuwa
anagonga mlango kwa nguvu. Alijua tu. Hakuwa
mwingine zaidi ya baba yake. Akaamka pale
kitandani na moja kwa moja akaenda kufungua
mlango.
Akakutana na sura ile ya simba aliyejeruhiwa.
“Vick sitaki nikupige kwa hasira nilizo nazo
naomba uondoke humu ndani najua utanipa kesi ya
mauaji. Pia nataka ujue kuanzia leo mimi sio baba
yako, nenda ukamtafute baba yako huko aliko.”
Ilikuwa ni hotuba fupi nzito iliyobeba ujumbe wa
kutisha. Aende wapi? Alijiuliza.
“Nakupa masaa mawili ya kukaa humu ndani,
nikirudi huku ninakoenda nisikukute.” Alifoka
Sajenti.
* * *

Sajenti Frank kilindo alikuwa anajiandaa kwenda
kumchukua mkewe na mwanawe ambaye
alimuacha pale zahanati Tandika. Huku
akijipongeza kwa kuweza kudhibiti hasira yake kwa
mwanae Sasa alijua mwanae ataendelea na
masomo baada ya kutoa mimba.
Aliendesha gari taratibu kuelekea Zahanati.
Alipofika akamkuta mkewe akiwa katika simanzi.
“Vipi?” Swali fupi lenye maana kubwa.
“Katoroka.”
“What?” Kimya.
“Ingia kwenye gari twende.” Ilikuwa amri.
“Hatusubiri?”
“Sina mtoto nisubiri nini?” Ukimya ukatawala
baada ya kauli hiyo huku kila mmoja akitafakari
tukio lililofanywa na Vick.
Alipofika nyumbani hakuwa na hatua nyingine zaidi
ya kumfukuza na kumkana mwanae. Mama Vick
alisikia uchungu sana lakini aliogopa kutia neno
lolote kwani lingemgharimu.
Baada ya baba yake kuondoka Vick alikusanya vitu
vyake kama alivyoamrishwa na baba yake
hatimaye akaondoka. Wakati anaondoka akageuka
na kuiangalia nyumba ile ambayo amekulia yeye na
kaka zake watatu ambao wote wameajiriwa na
jeshi la wananchi. Yeye ndiye mtoto wa mwisho
bado alikuwa mwanafunzi wa sekondari. Ndoto
zake zimeishia hapo. Huku akiwa na mizigo yake
hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda zaidi ya
nyumbani kwa Beda.
Alipofika akashangaa kuwakuta Beda na mama
yake wakiwa katika hali ya simanzi. Akashangaa
kuona wana nyuso zilizojaa woga.
Baada ya kusalimiana akakaa huku akijiandaa
kusimulia kile kilichomtokea. Ajabu. Hakuna
aliyeshangazwa na ujio wake. Hili lilimshangaza
zaidi.
“Mwanangu Vick.’ Alianza mama Vick huku
akionekana kusita kidogo kwa alichokusudia
kuongea kisha akaendelea. “Taarifa zako zote
tunazo baba yako alikuja hapa akatoa vitisho
vizito na kaapa kama tutathubutu kukupokea basi
kifo itakuwa halali yetu sote.”
Vick alishtushwa na kauli hiyo akajikuta akikosa
nguvu akalala pale kwenye jamvi.
Kilio kilichoambatana na kwikwi kikaanza kumtoka
Vick. Mama Beda naye akashindwa kuvumilia
akaingia ndani huku akilia. Asingeweza kuusahau
moyo wa huruma ulioonyeshwa na Vick. Vick ni
kama mwanae, pamoja na ujinga walioufanya alijua
ni utoto wa kutofikiria nini kitatokea mbele ya
safari. Kama si vitisho vya baba yake alikuwa
tayari kumtunza na kumuhudumia. Afanyeje?
Aliwaza. Akaendelea kulia huku kila alilolifikiria
akiliona kuwa zito upande wake. Kiio kilikuwa
kimetawala nyumba hii. Beda naye alikuwa analia
kwa matatizo yaliyokuwa yanamkuta Vick yeye
akiwa sababisho.
“Beda naomba uniwekee hili begi kubwa ndani.”
Aliongea Vick huku akijifuta machozi. Alionekana
kama aliyepata wazo jipya. Beda alipotoka ndani
hakumkuta Vick. Hakushtuka kwa sababu alihisi
kuwa huenda hayuko mbali. Lakini alishtuka baada
ya kuona masaa yanakatika
**Vicky amefukuzwa kwao huku mama Beda
akipewa onyo kali asithubutu kumuhifadhi…. VICKY
ANATOWEKA na hakuna ajuaye alipo…

ITAENDELEA!!!
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

Mama Beda naye akashindwa kuvumilia akaingia
ndani huku akilia. Asingeweza kuusahau moyo wa
huruma ulioonyeshwa na Vick. Vick ni kama
mwanae, pamoja na ujinga walioufanya alijua ni
utoto wa kutofikiria nini kitatokea mbele ya safari.
Kama si vitisho vya baba yake alikuwa tayari
kumtunza na kumuhudumia. Afanyeje? Aliwaza.
Akaendelea kulia huku kila alilolifikiria akiliona
kuwa zito upande wake. Kiio kilikuwa kimetawala
nyumba hii. Beda naye alikuwa analia kwa
matatizo yaliyokuwa yanamkuta Vick yeye akiwa
sababisho.
“Beda naomba uniwekee hili begi kubwa ndani.”
Aliongea Vick huku akijifuta machozi. Alionekana
kama aliyepata wazo jipya. Beda alipotoka ndani
hakumkuta Vick. Hakushtuka kwa sababu alihisi
kuwa huenda hayuko mbali. Lakini alishtuka baada
ya kuona masaa yanakatika.
Jua lilishaanza kupoteza nuru yake. Bado Vick
aliendelea kutembea. Alitembea hadi kiza
kilipoingia. Hakujua wapi anaelekea. Ingawa kwa
kufuata ramani ya nchi alikuwa ameshauacha
mkoa wa Dar es salaam na kuingia mkoa wa
Pwani. Hatimaye aliiacha ardhi ambayo ilikuwa na
majumba. Akaingia maeneo ambayo hakuiona
nyumba yoyote zaidi ya barabara ile ya lami.
Magari mengi yalikuwa yanapita kwa kasi eneo lile.
Hakupenda jinsi magari yalivyokuwa yanammulika
kwa taa zake. Alijua wazi wako madereva wenye
roho nzuri ambao watasimama na kutaka kumpa
msaada ambao hakuuhitaji wakati huo. Akaamua
kuacha barabara kuu inayoelekea wilaya ya
Mkuranga na mikoa ya kusini akaingia msituni.
Alianza kwenye mashamba hatimaye akaingia
kwenye msitu kamili. Hofu na mashaka na mateso
yalitawala katika safari yake. Alishaamua kufia
huko msituni. Alitembea mpaka akachoka.
Akaamua kulala chini ya mti mkubwa. Saa nane
usiku akashtuka ghafla kutoka usingizini.
Alipoangalia vizuri akagundua kile kilichokuwa
mbele yake. Ajabu. Ingawa kulikuwa na giza nyoka
yule mkubwa aling’aa na kuweza kuonekana.
Alikuwa anajiburuza taratibu kuelekea kule aliko
Vick. Alimtambua vizuri nyoka huyu. Ingawa
alikuwa hajawahi kumuona lakini alibaini moja kwa
moja kuwa ni chatu. Alitamani sana kufa lakini
kamwe hakutamani kifo hicho kitokane na chatu.
Alitetemeka lakini akawa mtulivu akisubiri kifo
chake. Alimfikiria sana yule aliyekuwa tumboni.
Hakujua itakuwaje. masikini nakufa na mwanangu
hata dunia hajaiona. Aliwaza Vick huku akianza
kutokwa na machozi.
*****************************

Nje ya jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam walisimama vijana wenye nyuso zilizojaa
wasiwasi. Miongoni mwao alikuwa ni Beda Sanga.
Huyu alikuwa miongoni mwa vijana waliomaliza
kidato cha sita ambao wamebahatika kuitwa
kwenye usaili wa kujiunga na jeshi la Polisi.
Pengine huyu ndiye mtu aliyekuwa na hofu zaidi,
kichwani mwake yalipita mambo mengi zaidi.
Kubwa zaidi ilikuwa ni ile fikra ya kulipa fadhila
alizofanyiwa na mama yake. Alikumbuka jinsi
mama yake alivyopata tabu kwenye malezi yake.
Miongoni mwa vitu ambavyo vilimuhuzunisha ni
kifo cha Vick. Kilichomsikitisha zaidi ni aina ya kifo
chake. Vick alitoweka Ghafla kwenye macho yake.
Dakika, saa…… hatimaye miaka Vick hajaonekana.
Mama Beda alimlilia sana licha ya vitisho kutoka
kwa baba mzazi wa vick kuwa iwapo atathubutu
kmpokea basi angewaua wote watatu. Vick
kachukua hatua ya kutoroka. Hatimaye
hakujulikana wapi aliko. Baada ya miaka mitatu
kupita kila mtu akapitisha kwenye fikra zake kuwa
Vick ni marehemu. Amejiua, ameuwawa au ame….
hakuna aliyeweza kufumbua fumbo hilo. Jambo la
ajabu baba yake hakujisughulisha tena na jambo
lolote kuhusu Vick kwake ukurasa ulikuwa
umefungwa ingawa alipata lawama kubwa kutoka
kwa ndugu na jamaa hakujali.
“Beda Sanga….” Alishtushwa na sauti iliyokuwa
inaita ndani.
“Nipo.” Aliitika kwa sauti huku akijitahidi kutembea
kwa ukakamavu kuelekea ndani. Alitembea
mwendo ambao alidhani ungewashawishi
wasimamizi wa usaili kumchagua.
Akasimama mbele ya meza ile ile iliyozungukwa na
watu waliokuwa ‘siriasi’ kiasi cha kumtia hofu mtu
wa kawaida.
“Kwanini unataka kuwa Polisi?” Alihoji mmoja. Aina
gani hii ya maswali. Alijiuliza Beda.
“Nataka kulitumikia Taifa langu.” Alijibu na kukaa
kimya.
“Huwezi kulitumikia taifa kwa njia nyingine
tofauti?” Aliuliza mwingine.
“Naweza.” Alijibu kwa mkato huku akimwangalia
yule aliyekuwa katikati jinsi alivyokuwa anakagua
vyeti vyake.
“Kwanini usilitumikie Taifa kwa njia nyingine.”
Aliendelea kuuliza
“Kwa sababu huu ni kama mgawanyo wa kazi
hivyo mimi nimechagua huku.”
“Kwa hiyo lengo lako ni kuitumikia nchi tu.”
“Si hivyo tu nahitaji pia mshahara ambao utaweza
kunifanya niendeshe maisha yangu ya awaida.”
“Unasema maisha ya kawaida unaweza kufafanua
ni maisha gani si ya kawaida?”
“Ndiyo. Ni maisha ya anasa na………..” Hakumaliza
akakatishwa na swali lililoulizwa na yule aliyekuwa
anakagua vyeti vyake.
“Kwanini umeghushi vyeti vya Elimu ya Sekondari.”
“Sijaghushi ni vyeti halisi.” Alijibu Beda kwa
kujiamini.
“Haya nenda.” Aliamrishwa.
Akaondoka huku akiwa hana uhakika nini
kitatokea.
* * **********

Ilikuwa kama ndoto. Beda hakuamini siku
aliyoripoti makao makuu ya jeshi la Polisi akiwa
askari aliyehitimu vema mafunzo hayo. Alianza
kazi yake kwa ufanisi mkubwa jambo
lililosababisha athaminiwe na kupewa majukumu
mengi zaidi. Aliamua kumuhamisha mama yake
kule Mbagala wakahamia maeneo ya Ubungo.
Hakuipenda nyumba ya Mbagala kwa sababu
ilimpa kumbukumbu mbaya katika maisha yake.
Ndipo alipoamua kwenda kutafuta chumba maeneo
mengine.
Siku moja Beda alikuwa kwenye mizunguko ya
kawaida pale Kariakoo. Ndipo akakutana na kitu
ambacho kilimshtua.
Ombaomba. Hakuwa ombaomba wa kawaida.
Alimwangalia kwa makini akajikuta moyo wake
ukienda mbio. Pumzi zikaanza kupanda na
kushuka haraka haraka. Akaamua kuondoka eneo
lile harakaharaka. Ni mzuka au sadifa? Alijiuliza
huku akiwa amesimama kwenye makutano ya
mtaa wa Swahili na Sikukuu. Akakaa pale kama
dakika kumi bila kujua afanye nini. Ndipo
alipoamua kupiga moyo konde na kurudi tena
nyuma. Huku anatetemeka akaita.
“Vick.”
“Bee.” Yule ombaomba aliitika na kuzidi kumtisha
Beda. Ni yeye. Kama alikuwa Vick kweli basi
kidogo alionyesha kumsahau Beda. “Naomba
shilingi mia baba mwanangu ana njaa si
unamuona.” Aliongea yule mwanamke ombaomba
huku akimuonyesha Beda kwa kidole mtoto
aliyekuwa ameegemea ukuta. Beda akamuona yule
mtoto, alikuwa na miaka kati ya sita na minane.
Mungu wangu. Alishtuka Beda baada ya kumuona
kiumbe aliyefanana na mama yake mzazi akiwa
kwenye kundi la ombaomba. Machozi yakaanza
kumtoka.
“Vick unanikumbuka?” Aliuliza Beda. Hapo Vick
akamtazama vizuri aliyekuwa anaongea naye.
“Beda.” Alishtuka Vick na kumkazia macho Beda
kwa mshangao. Wakakumbatiana huku
wakiendelea kulia. Kilio chao kilivuta hisia za
ombaomba wengine na wapita njia ambao walitaka
kufahamu kulikoni Kijana yule mtanashati
akumbatiane na ombaomba tena kubwa zaidi
wakikipamba kitendo kile kwa kilio. Wengi
walisimama wakisubiri kusimuliwa. Hakutokea wa
kusimulia mkasa ule. Ili mradi kila mmoja aligeuka
na kumuuliza jirani yake. Jibu halikupatikana na
watu hawakuondoka walizidi kujaa na kusababisha
usumbufu mkubwa kwa wapita njia wenye haraka.
“Twende.” Aliamrisha Beda baada ya kuona watu
wanazidi kuongezeka.
Wakatembea hadi kituo cha teksi cha sikukuu.
“Nipeleke Ubungo maziwa.” Alisikika Beda huku
akiingia kwenye teksi.
Beda alikuwa amepanga vyumba viwili na sebule.
Baada ya kumlipa dereva wa ile teksi wakateremka
na kuingia ndani. Mama Beda ambaye alikuwa nje
hakujishughulisha sana na wageni wale kwani
alishazoea kupata wageni wengi toka mwanawe
alipoajiriwa na jeshi la polisi. Maisha yake
yalibadilika unafuu ulikuwepo. Angalau alianza
kuonja ladha ya elimu ya mwanae.
“Karibu Vick.”
“Ahsante.”
Aliitikia Vick. Vick mchovu sio yule aliyetoroka kwa
baba yake wakati anang’aa. Nyuma alifuatiwa na
binti aliyevaa kanga na kuifunga shingoni kama
mtoto wa kijijini. Alikuwa na kila dalili ya umaskini.
“Huyu ni nani?” Aliuliza Beda huku akimkazia
macho yule binti wa miaka sita au saba.
“Ni mwanao Beda huoni jinsi alivyofanana na
mama yako?”
Beda akainamisha kichwa chini kwa uchungu.
Hakuwa na sababu ya kukataa, yule mtoto
alifanana kila kitu na mama yake mzazi. Yule
mtoto alionyesha utulivu mkubwa sana. Kwanza
alijua kuwa ameletwa pale kuja kusaidiwa tu.
Haikumuingia akilini kuwa yule aliyeko mbele yake
ni baba yake mzazi. Asingeweza kuamini kabisa na
pengine ni kitu ambacho hakuwahi kukifikiria.
Alijua kuna watu walistahili maisha fulani lakini sio
yeye. Alijiweka katika kundi ambalo aliona ni halali
kuishi maisha ya kuomba.
“Mama, mama.” Aliita Beda baada ya kuinua
kichwa chake.
Mama yake akaja. Akakaa kwenye kiti pembeni
kidogo na pale alipokaa Vick na mwanae.
“Unamfahamu huyu.” Aliuliza huku akimuonyesha
yule binti mdogo. Mama yake alimtazama kwa
makini yule binti kisha akashituka. Hii sura si ngeni
nilimuona wapi? Alijiuliza mama Beda. Kuna kitu
kikamshangaza katika uso wa yule binti mdogo.
Kulikuwa na alama ndogo nyeusi ambayo
aliifahamu sana. Aliiona wapi? Alishituka alipokuja
kubaini kuwa sura anayoiangalia haikuwa na
tofauti na sura mbili anazozifahamu sana. Sura ya
kwanza ni ya marehemu mama yake mzazi na sura
ya pili ni ya kwake mwenyewe. Mungu wangu
kama najitazama kwenye kioo nani huyu?
Akamgeukia Beda na kumtazama kama mtu
anayetaka majibu ya maswali ambayo yanapita
kichwani mwake.
“Unamfahamu?” Beda alirudia swali lake.
“Simfahamu lakini kwa kuwa hujawahi kumuona
bibi yako basi mtazame huyu mtoto.” Aliongea
mama Beda huku mshangao ukiwa haujafutika
usoni kwake.
“Na huyu mama yake unamfahamu?” Akamkazia
macho mgeni yule dhaifu, mchafu. Hakukumbuka
alimuona wapi.
“Simfahamu.”
Alijibu kwa mkato.
“Huyu ndiye ambaye umelitunza begi lake karibu
miaka sita sasa.”
“Begi?”
“Ndiyo hakuna mtu alituachia begi lake miaka sita
au saba iliyopita?”
“Mungu wangu, Vick.” Alishituka mama Beda.
Hakuweza kuvumilia mbele ya miujiza ile, akajikuta
akiangua kilio kikubwa.

**Amakweli ni MUUJIZA………
Nini kitaendelea!!!!
 
SEHEMU YA KUMI NA TANO

“Na huyu mama yake unamfahamu?” Akamkazia
macho mgeni yule dhaifu, mchafu. Hakukumbuka
alimuona wapi.
“Simfahamu.”
Alijibu kwa mkato.
“Huyu ndiye ambaye umelitunza begi lake karibu
miaka sita sasa.”
“Begi?”
“Ndiyo hakuna mtu alituachia begi lake miaka sita
au saba iliyopita?”
“Mungu wangu, Vick.” Alishituka mama Beda.
Hakuweza kuvumilia mbele ya miujiza ile, akajikuta
akiangua kilio kikubwa. Majirani wakaanza
kukusanyika wakiwa na wasiwasi huenda kuna
msiba. Beda alijitahidi kuwarudisha na kuwaambia
hakuna tatizo ni mambo ya kifamilia tu. Majirani
wabishi walisimama madirishani kutaka kujua
kulikoni. Kwa kutambua hilo hawakuanza mapema
kuongea juu ya jambo hilo. Beda alikuwa na hamu
kubwa kutaka kujua Vick alipotelea wapi mpaka
leo anarudi mikononi mwake akiwa na mtoto yule.
Hakutaka kuuliza hilo mapema kabla hajahakikisha
kuwa hakuna mtu asiyehusika atakayenasa
mazungumzo yale.
“Mtoto anaitwa nani.”
“Anaitwa Veronica.” Alijibu Vick kwa mkato.
Mama Beda huku machozi yakimtoka akamchukua
Vero na kumpakata. Vero alishangaa kwani alikuwa
hajawahi kupata mapenzi zaidi ya yale ya mama
yake mzazi. Alikumbuka maisha ya mateso
aliyoishi kwenye mitaa mbalimbali ya kariakoo.
Baadhi ya maeneo walitukanwa pia kuna wakati
waliambiwa wanafanya makusudi. Alikumbuka pia
jinsi walivyopigwa makofi na baadhi ya wenye
maduka. Nani huyu ambaye leo anathubutu
kumkumbatia kwa hisia kali za mapenzi ya kweli
kama yale aliyoyapata kutoka kwa mama yake? Ni
nani huyu ambaye hajali hata haya mavazi yangu
yenye harufu mbaya?
Kulikuwa na utulivu mkubwa. Akachungulia
dirishani, hakukuwa na mtu tena. Akafungua friji
akatoa Soda. Moja akampa Vero nyingine akampa
mama yake Vero. Shauku aliyokuwa nayo
isingemfanya asubiri muda zaidi kujua kile
alichohitaji kutoka kwa Vick.
“Please naomba unieleze nini kilitokea. Anzia siku
uliyotoroka mpaka kufikia leo.”
Vick akainua kichwa juu.
* * *&&&***

“Ng’aa, nng’aa, nng’aa.” Saa 6.00 sauti ya mtoto
mchanga ilisikika kutoka ndani ya nyumba ndogo
ya nyasi. Kibatari chenye mwanga hafifu
kiliwasaidia wakunga wa jadi kumsaidia Vick
kujifungua salama. Mwanga wa kibatari ulizidi
kufifia, mabibi wale wenye kila dalili za umaskini
walitazamana wakashindwa kujua nini wafanye.
Bibi mmoja akatoka nje, akachukua kuni na kuja
nazo ndani. Akaziweka kwenye jiko lile la mafiga.
Baada ya kuhangaika kwa dakika tano moto
ukawaka. Mwanga ule ukaumeza mwanga wa
kibatari. Baada ya dakika chache wakaja kina
mama wengine kutoka nyumba za jirani. Kila
mmoja akafanya kazi aliyoona inafaa ili kumsaidia
mzazi. Vick alishukuru sana baada ya kupata
ushirikiano nzuri kutoka kwa wanakijiji.
Pamoja na umasikini waliokuwa nao alibaini kuwa
ni watu wenye mapenzi ya kweli. Alikumbuka jinsi
alivyookotwa msituni na kisha kutunzwa katika
kijiji hiki cha Jaribu mpakani kilichopo katika mkoa
wa Pwani. Asingeweza kusahau jinsi alivyonusurika
kumezwa na chatu. Alijiuliza jinsi chatu yule
alivyoweza kupita karibu yake bila kujishughulisha
nae. Alikuwa ameshiba? Alijiuliza Vick. Lakini
alikuwa amesikia simulizi mbalimbali kuwa chatu
akishiba hukaa sehemu moja mpaka shibe yake
iishe. Hakuwa na uhakika na simulizi hizo kwani
wote walioongea hakukuwa na mtaalamu wa
mambo ya viumbe.
Baada ya chatu kumsogelea zaidi Vick alipoteza
fahamu.
****&&&&****

Siku ya pili ilimkuta mama Tatu akitafuta kuni kule
porini, ndipo alipomuona Vick akiwa amepoteza
fahamu. Alikimbia hadi kijijini ambako alitoa taarifa
juu ya kuonekana kwa binti yule. Wanakijiji kadhaa
wakashirikiana kumbeba hadi kijijini ambako
alipewa huduma za awali hadi aliporudiwa na
fahamu. Akawaeleza mkasa wake wote bila
kusahau dhamira yake ya kujiua. Wanakijiji
walisikitika sana wakampokea na kuanza kuishi
naye.
Miezi ya kujifungua ikafika. Akajifungua mtoto wa
kike ambaye alipewa jina la Veronika. Siku, saa na
hatimaye miaka ikakatika Vick akaamua kurudi
kwa baba yake kuomba msamaha. Wanakijiji
wakamchangia nauli. Si mbali sana kutoka kijijini
Jaribu mpakani hadi Dar es salaam.
Aliwasili Dar akiwa na Vero ambaye alishakuwa
mkubwa. Miaka sita aliyokaa kijijini haikuweza
kumsahaulisha mazingira ya Dar. Akafika pale
kweye nyumba yao. Akakuta nyumba mbili kubwa
zikiwa jirani na nyumba yao. Nyumba hizi zilikuwa
zimejengwa eneo ambalo lilikuwa na nyumba
ndogo ndogo.
Aligonga geti huku akiwa na hamu kubwa ya
kumuona mama yake. Alishangaa kuona akitoka
mtu tofauti kabisa na familia yao.
“Habari yako.”
“Nzuri shikamoo mama.”
“Marhaba nikusaidie nini.”
“Naweza kumuona mzee Kilindo?”
“Yule mzee mwanajeshi?”
“Ndiyo.”
“He.Ina maana huna habari kuwa yule mzee alikufa
yeye na mkewe kutokana na ajali ya gari iliyotokea
mwaka juzi?” Alijibu yule mama. Lilikuwa ni pigo
kubwa kwake.
Akaondoka akiwa na huzuni kubwa. Aliijua vema
historia ya baba yake ambaye hakuwa mtanzania.
Aliingia hapa nchini kiujanja ujanja na hatimaye
kujipatia ajira katika jeshi la wananchi kwa njia
alizozijua mwenyewe. Mama yake alikuwa mtu wa
Mahenge ambako hajawahi kufika. Hakuwa na
mahusiano mazuri na kaka zake ambao hawakuwa
wa mama mmoja.
Akaamua kuondoka na kwenda nyumbani kwa
Beda. Akiwa na matumaini makubwa ya kupata
masaada huko alipigwa na butwaa baada ya
kukuta nyumba hiyo ikiwa gofu.
Hakuwa na njia nyingine zaidi ya kuingia mtaani na
kuwa ombaomba. Maisha yalikuwa magumu sana.
Ni kipindi ambacho kilikuwa na mateso makubwa
zaidi ya kipindi chochote katika maisha yake.
Alidhalilika akadharaulika.
Hakuamini alipojikuta tena kwenye mikono ya
Beda. Ukawa mwanzo wa maisha mapya. Furaha
ikarejea tena kwenye nafsi yake.
******&&&&*****

Kutokana na juhudi kubwa na ujasiri wa aina yake
Beda alijikuta akipandishwa vyeo na hatimaye
kuwa Inspekta. Fedha haikuwa tatizo tena.
Alinunua nyumba kinondoni baada ya kupata
mkopo mnono kutoka moja ya benki za hapa
nchini.
Jumatatu moja Inspekta Beda alikuwa katika
semina ya maafisa wa jeshi la polisi. Semina hiyo
ilikuwa nzuri kwa sababu ilidhaminiwa na moja ya
makampuni makubwa ya simu. Baada ya semina
kwisha ulifika muda wa kujipongeza.
“Aaah. Afande onja kidogo hii bia.” Alibembeleza
Inspekta Makenzi.
“Mh. Chungu afande.’ alilalamika Inspekta Beda
baada ya kujaribu kumeza funda moja la bia ile.
“Jaribu tena utazoea tu.”
“Kwa hiyo unataka nizoee ulevi.”
“Acha hizo afande. We hutaki kuvumbua dhahabu.”
Inspekta akacheka huku akijimiminia funda lingine.
Hatimaye akamaliza chupa nzima ya bia ile.
Semina iliisha kila mmoja akarudi kwenye kituo
chake cha kazi.
Siku iliyofuata mara baada ya kazi akaenda
maeneo ya Manzese. Akatafuta sehemu ambayo
ilikuwa tulivu kidogo.
“Naomba bia baridi.”
“Bia gani boss.”
“Naomba yoyote ambayo si kali sana.” Alijibu huku
akiona aibu kwa kutojua majina ya bia.
Alikumbuka kuwa bia hizi hutangazwa redioni mara
kwa mara lakini alisikia kuwa hutofautiana ukali.
Alijimiminia kinywaji kile, akaanza kunywa taratibu
mpaka alipomaliza chupa ya kwanza hatimaye
akaagiza ya pili.
Ile ya pili hakumaliza akainuka pale kwenye kiti
baada ya kuhakikisha amelipa kiasi anachodaiwa.
Akachukua teksi iliyompeleka nyumbani kwake
Kinondoni. Saa 6.32 aliwasili nyumbani kwake.
“Vipi dear mbona umechelewa sana?” Aliuliza Vick.
“Si unajua majukumu yetu ya kazi.”
“Na hiyo pombe mlikuwa mnakunywa kazini?”
Hakuwa na jibu. Akaingia bafuni kwenda kuoga
kisha akatoka na kukaa mezani. Vick alimuangalia
Beda bila kuongea lolote.
“Mh.” Aliguna bila kuongea neno lolote kisha
akaingia chumbani kwenda kulala.
“Vipi mtoto alienda shule leo?” Aliuliza Beda baada
ya kuingia chumbani.
“Alienda walimu wake wanamsifia sana wanasema
ni mwepesi wa kuelewa.”
Baada ya hapo wote wakawa kimya.
* * ************

Ulikuwa ni mwezi wa nne toka Inspekta Beda
aanze kuwa mnywaji wa pombe mara nyingi
aligombana na mkewe. Maelewano yalianza
kupungua nyumbani siku nyingine aligombana na
mama yake ambaye hakupenda kabisa tabia hiyo
mpya ya ulevi.
Siku moja Ispekta Beda alikuwa amejipumzisha
kwenye baa moja iliyoko maeneo ya Majumba sita.
Akiwa hapo aliagiza pombe kama kawaida yake.
Mara akaingia mwanamke ambaye alienda kukaa
kwenye meza moja na Beda. Baada ya kuagiza
vinywaji alivyohitaji akaanzisha mazungumzo na
Beda.
“Kaka unaonekana una mawazo mengi sana.”
“Ah. Hapana labda ndo’ nilivyo.” Wote wakacheka
kisha wakaendelea na maongezi mengine. Muda
wa saa nzima waliokaa pale uliwatosha Beda na
yule mama kuanzisha uhusiano. Maongeza
yalikuwa motomoto huku yakisindikizwa na muziki
ndani ya ile baa.
Mwisho wa yote wakakubaliana kwenda kulala
gesti.
“Una mke.” Aliuliza yule mwanamke huku akiwa
amelaza kichwa chake katika kifua cha Inspekta
Beda.
“Ndiyo.” Alijibu kwa mkato akionekana kukerwa na
swali hilo.
“Unajua kwa nini nakuuliza……” Aliongea huku
akionyesha wazi kukolewa na kilevi.
“Nataka tufanye mapenzi ya heshima ambayo
hayatamfanya mkeo abaini jambo lolote.’
“Poa.” Alijibu Inspekta huku akitembeza mkono
wake katika mwili wa yule mwanamke.
Inspekta alionekana kulewa kweli kweli kwa
mapenzi ya yule mama. Siku moja tu. Lilikuwa
jambo la ajabu kwa mtu aliyemtambua vizuri
Inspekta Beda jinsi alivyotekwa na kuweza
kubadilishwa na pombe kwa muda mfupi namna ile
hata akawa hana maamuzi sahihi.
Asubuhi ilimkuta Inspekta akiwa amelala na yule
mwanamke. Aliamka akavaa nguo zake tayari kwa
safari ya nyumbani.
“Unaenda wapi tena dear si uliniambia kuwa leo
utakuwa Off.” Aliuliza yule mwanamke. Sauti yake
laini ikamfanya Inspekta arudi tena kitandani.
Akashangaa ni saa ngapi alimwambia kuwa
atakuwa off. Ni kweli alikuwa Off lakini
hakukumbuka kutoa kauli hiyo. Kweli pombe si
chai. Aliwaza huku akihisi kuongea mengi ambayo
hakutakiwa kuongea na mwanamke yule
aiyekutana naye kwa mara ya kwanza.
“Beda.” Aliita yule mwanamke.
“Hivi kweli unanipenda?”
“Nakupenda sana.” Alijibu Beda huku kiasi fulani
akishangazwa na swali lile kwani ni pombe tu ndio
zimewafanya wajumuike pale kitandani.
“Nitahakikisha vipi kuwa unanipenda?”
“Labda ulitaka nikuthibitishie vipi?” Aliuliza Beda
huku kiasi fulani akilisanifu na kulisifia moyoni
mwake umbo la yule mwanamke.
“Nataka unioe.”
Beda akashusha pumzi bila kuongea lolote.
“Usijali lakini kwanza inabidi nipate mbinu nzuri ya
kumuondoa mke wangu.” Akaongea baada ya
kukaa kimya dakika kadhaa, huku akishangaa jinsi
siku moja ilivyotosha kumfanya awe dhaifu kwa
mwanamke aliyeokotana naye baa. Akashangaa
zaidi baada ya kugundua kuwa alikuwa na dhamira
ya dhati ya kumuondoa mkewe Vick pale
nyumbani.
* * *

**BEDA????? Kulikoni kusahau yaliyopita na
kujiingiza katika ulimwengu huo!!!!!
Pesa…. Pesa mbaya sana ukiitumia vibaya!!!
ITAENDELEA!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom