Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,638
- Thread starter
- #21
SEHEM YA 15
Ananogewa na mchezo huo kiasi cha kuwamtumwa wa ngono, anaendelea na mchezohuo mpaka anapoingia mwaka wa tatu chuoni hapo. Msichana mdogo aliyekuwa akisomamwaka wa kwanza chuoni hapo, Neema,anatokea kumpenda Dickson, jambo ambalohalijawahi kumtokea. Hata hivyo , msichana huyo hayupo tayarikuanza kufanya mapenzi na Dickson , jambolinalosababisha kijana huyo aende tenakununua machangudoa bila kujua kuwa Neemaalikuwa akimfuatilia kwa nyuma .
Kwa macho yake anamshuhudia Dickson akinunua changudoa, jambo linalomuumiza sana.
Je , nini kitafuatia? SONGA NAYO
Baada ya Neema kumshuhudia kwa machoyake mwenyewe, Dickson akinunua changudoana kuelekea naye gesti , alijisikia maumivumakali mno ndani ya moyo wake. Licha yakujipa moyo kwamba afadhali ameujua ukwelimapema, bado maumivu makali yaliendeleakumtesa kiasi cha kuamua kuondoka kabisaeneo hilo, huku machozi yakimtoka.Akaelekea barabarani kwa lengo la kuvukaBarabara ya Shekilango ili atafute usafiri wakumrudisha chuoni, huku mawazo mengiyakizidi kukitesa kichwa chake, akawa anahisikama amebeba jiko la mkaa kichwani mwake .Machozi yakawa yanaendelea kumtoka nakuulowanisha uso wake mzuri.
Hata alipokuwa anavuka barabara ,hakukumbuka kuangalia magari huku na kulekabla ya kuvuka, akajikuta ameingiabarabarani huku akiendelea kulia kwauchungu.Penzi la Dickson lilimtesa mno , upandemwingine akawa anajilaumu kwamba kamamchana wa siku hiyo angekubali kufanyamapenzi na Dickson, huenda hayo yote yasingetokea.“ Lakini mimi sijawahi kufanya mapenzi nanimejiwekea nadhiri kwamba sitampa ruhusa mwanaume yeyote auguse mwili wangumpaka nitakapo …” Neema aliendelea kuwazalakini kabla hajamalizia, alishtukia honi kalizikipigwa upande wake wa kushoto, alipogeuka, gari dogo la kifahari, Toyota MarkX tayari lilishamfikia mwilini.
Licha ya dereva kujitahidi kufunga breki kali,gari hilo lilimgonga Neema na kumrusha mita kadhaa juu , akadondoka katikati ya lami nakusababisha taharuki kubwa eneo hilo.***Baada ya kukidhi haja zake, Dickson alitokaharakaharaka kwenye chumba cha gestialichoingia na changudoa yule kamailivyokuwa kawaida yake. Kwa kuwa kaziiliyomleta alishaimaliza, hakutaka kuendeleakukaa eneo hilo.
Akawa anaondoka kwa lengo la kuvuka barabara na kuchukua usafiri wa kumrudishachuoni lakini ghafla alipoikaribia barabara ,alishtushwa na umati wa watu uliokuwaumekusanyika barabarani huku watu wenginewengi wakikimbilia eneo hilo.“ Kuna nini kimetokea pale ?” Dickson alimuuliza mmoja kati ya watu wengi waliokuwa wanakimbilia eneo hilo.“ Amegonga mtu! Daah , sijui kama ataponayule dada , ” alisema mtu huyo huku akizidishamwendo, Dickson naye akaongeza mwendompaka mahali mtu aliyegongwa alipokuwaameangukia.“ Ooh my God! Neema , what happened to you?”(Mungu wangu ! Neema, nini kimekutokea?)“ Mnafahamiana?” Patrick Buzohela, mwandishimahiri kutoka Kituo cha Runinga cha GlobalTV , alimhoji Dickson huku akimsogezea‘ maikrofoni ’ mdomoni, mwandishi mwingineakiwa makini kuchukua picha za video kwaajili ya kurusha kwenye runinga hiyo.“ Ni mwanachuo mwenzangu, tunasoma nayeChuo Kikuu cha Dar es Salaam, ” alisemaDickson kwa sauti ya juu huku akiwasukumawatu wote na kwenda mpaka pale chinimsichana huyo alipokuwa ameangukia, damu nyingi zikimtoka puani, mdomoni na kwenyemajeraha mengi aliyoyapata .
Patrick na mwenzake waliendelea kuchukuapicha za tukio hilo kwa umakini mkubwa,wakawa wanarekodi kila kitu kilichokuwakinaendelea pamoja na kuwahoji baadhi yamashuhuda wa ajali hiyo .Bila kujali chochote, Dickson alimuinua nakuanza kuomba msaada kwa mtu yeyotemwenye usafiri ili wamkimbize hospitali .Bahati nzuri , gari lililomgonga halikuwa limeharibika sana, dereva akashuka hukuakitetemeka na kukubali kumkimbizahospitalini .Kwa kuwa askari wa usalama barabaranihawakuwa mbali na eneo hilo, walifika na kuchukua taarifa zote muhimu kishawakaruhusu mgonjwa akimbizwe hospitalini .Dickson akiwa kwenye siti ya nyuma ya garihilo, alimpakata Neema ambaye damu nyingizilikuwa zikiendelea kumvuja nakumlowanisha kijana huyo mwilini lakinimwenyewe hakujali.
Muda mfupi baadaye, tayari walikuwawamewasili kwenye Hospitali yaMwananyamala ambapo waliteremka nakupokelewa na wahudumu waliomlazamsichana huyo kwenye kitanda chamagurudumu na kumkimbiza wodini. Tayarigiza lilishaanza kuingia. Dickson akawasaidia mpaka walipofika kwenyemlango wa wodi ya wagonjwa mahututiambapo hakuruhusiwa kuingia. Msichana huyoambaye alishapoteza fahamu kuanzia mudauleule aliogongwa na gari , aliingizwa wodiniambapo madaktari walianza kuhangaikakuokoa maisha yake.“ Mgonjwa ni nani yako?”“ Ni mwanachuo mwenzangu. ”“ Mnasoma wapi?”“ Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ” alisemaDickson wakati akitoa maelekezo kwa mtualiyekuwepo mapokezi, kwa ajili ya kuandaafaili la mgonjwa. Baada ya kumaliza kutoamaelezo hayo , Dickson ambaye damu nyingizilizokuwa zimemvujia kwenye nguo zakezilikuwa zimeanza kukauka, alienda kukaakwenye benchi lililokuwa jirani na wodi yawagonjwa mahututi.
Tayari Kituo cha Runinga cha Global TVkilikuwa kikiirusha habari ya mwanachuo huyo kugongwa na gari na kueleza kila kitukilichokuwa kinaendelea mpaka muda huo .Watu wengi, wakiwemo wanachuo wenzakewakasikia taarifa hiyo na kuanza kukusanyanakuelekea hospitalini. Maswali mengi yaliyokosa majibu yaliendeleakupita kwenye kichwa cha Dickson, akiwahaelewi ilikuwaje mpaka Neema akafika eneohilo na kupata ajali mbaya kiasi hicho.Aliendelea kujiuliza maswali mengi ambayohakuna hata moja alilopata jibu lake.“ Au alikuwa ananifuatilia nini? Lakini haiwezekani, alijuaje kwamba nimekuja huku?” alijiuliza lakini akajipa moyo mwenyewe.
Aliendelea kukaa kwenye benchi hilo kwamuda mrefu mpaka baadaye aliposhtukiaviongozi wa serikali ya wanachuo na baadhiya wahadhiri wakija kwa wingi hospitalinihapo.“ Kumetokea nini Zinja ?”“ Neema kapata ajali mbaya , amegongwa nagari. ”“ Neema yupi ? Yule mwanachuo wa mwaka wakwanza mliyekuwa mmekaa naye jana wakatiwa chakula cha jioni ?”“ Ndiyo huyohuyo ,” alijibu Dickson nakuinamisha kichwa chake chini. Maswalialiyokuwa anaulizwa na wanachuo wenzakeyalizidi kumtia uchungu na kusababishamachozi yaanze kumlengalenga. Muda mfupi baadaye, mlango wa wodi yawagonjwa mahututi ulifunguliwa, watu wotewakasimama wakiwa na shauku kubwa yakusikia chochote juu ya hali ya mwanachuo mwenzao.
Je, nini kitafuatia?