Hadithi: Jini Mweusi

SEHEMU YA 35

Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea. Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.

Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anaendelea na tabia yake ya kununua machangudoa pasipo watu kufahamu kwamba yeye ndiye aliyekuwa amefanya mauaji ya msichana aliyeuawa siku kadhaa zilizopita.

Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

Mzuka wa kufanya mapenzi ulikwishampanda Dickson, alimchukua changudoa yule na kumvuta kitandani pale, akili yake ilichanganyikiwa, umbo zuri na ngozi nyororo aliyokuwa nayo msichana yule ilizidi kumhamasisha kufanya naye mapenzi mle chumbani.
“Subiri kwanza,” alisema msichana yule.
“Kuna nini?”
“Mbona una haraka?”
“Sasa si tumelipia short time, tufanye fasta,” alisema Dickson, hata sauti aliyoitoa chumbani hapo ilionesha ni jinsi gani alikuwa kwenye mhemko mkubwa wa kufanya mapenzi. Dickson hakutaka kusikia kitu chochote kile, alichokuwa akikitaka ni kufanya mapenzi tu. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi, damu ilizunguka kwa kasi mno, kilipita kipindi kirefu kufanya mapenzi kabla ya siku hiyo, ule mzuka wa wiki mbili zote alikuwa nao ulimzidi nguvu.
Alimchojoa changudoa nguo zake katika haraka ambayo hata yeye mwenyewe aliishangaa, alipomaliza, akamlaza kitandani. Katika kila kitu alichokuwa akikifanya mahali hapo hakutaka kugundulika kama alikuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kila alipomgeuza huku na kule, alihakikisha kwamba mwanga wa taa iliyokuwa nje haimpigi usoni mwake.

Walitumia muda huo vilivyo, baada ya saa mbili baadaye, kila mmoja alikuwa hoi, Dickson alibaki akimwangalia changudoa yule huku hata hamu ya kuendelea hakuwa nayo kabisa.
“Kiasi gani?”
“Unataka unilipe ipi? Ya mpaka asubuhi au short time?” aliuliza changudoa yule.
“Mpaka asubuhi japokuwa nataka kuondoka.”
“Laki moja na nusu.”
“Hakuna tatizo.”
Dickson akaivuta suruali yake na kutoa pochi yake ambapo akaifungua na kuanza kuhesabu fedha zake. Hakukuwa na hela ndogo, noti zote zilizokuwa ndani ya pochi ile zilikuwa ni elfu kumi tu, hivyo akazihesabu mpaka zilipofika kiasi hicho akamgawia msichana yule.
“Laki moja na nusu hii?” aliuliza msichana yule.
“Ndiyo!”
“Mmmh! Usije ukawa umenipiga changa la macho, ngoja niwashe taa nizihakikishe,” alisema msichana yule huku akisimama kitandani pale. Dickson akamshika mkono.
“Baby...”
“Abee kipenzi!”
“Huniamini?”
“Kwenye suala la fedha, hautakiwi kumuamini mtu, hata shemasi tu anaiba sadaka kanisani” alijibu msichana yule.
“Siwezi kukufanyia mchezo huo, niamini kipenzi. Kwanza hebu andika namba yako hapa,” alisema Dickson, aliamua kuliingizia suala la namba kwani hakutaka changudoa yule aendelee kuweka msisitizo wake juu ya kuwasha taa ile.
Dickson akafanikiwa kumlaghai msichana yule na mwisho wa siku hakuweza kabisa kuwasha taa ile kitu kilichomfurahisha sana Dickson. Mpaka alipoamua kuondoka na kumuachia changudoa yule fedha za kutosha zaidi, wakaahidiana kwamba kuanzia siku hiyo angekuwa mteja wake, yaani kuhusu suala la fedha hakutakiwa kuwa na wasiwasi kabisa.

Kila siku usiku Dickson alipokuwa akifika Sinza Mori, hakutaka kumchukua msichana mwingine zaidi ya huyohuyo aliyejitambulisha kwa jina la Magreth, ila awapo kazini alipenda sana kuitwa Mage. Uwepo wa Dickson ukawa gumzo mahali hapo, machangudoa wengi wakamfahamu kama mwanaume aliyekuwa akija na gari jeusi, kila walipoliona usiku mahali hapo, walijua fika kwamba alifika mahali hapo kwa ajili ya kumchukua Magreth, hivyo hawakutaka kumuingilia.

Katika kipindi cha wiki mbili, Magreth hakuweza kugundua kwamba yule mtu aliyekuwa akimchukua kila usiku alikuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam. Siku zikaendelea kukatika, kutokana na fedha alizokuwa akizipata Magreth, akawa changudoa aliyekuwa na maendeleo kuliko yeyote mahali hapo.
“Niitie Magreth...” alisema Dickson, kama kawaida alikuwa amefika Sinza Mori kwa ajili ya kumchukua Magreth na kuondoka naye kama kawaida yake.
“Hajafika!” alijibu msichana mmoja aliyevalia kimini.
“Amekwenda wapi?”
“Hajafika. Anaumwa tumbo!”
“Sawa! Asante.”
“Hutaki huduma?”
“Nataka, ila kama ye....”
“Hata mimi naweza kukupa huduma, tena zaidi ya huyo Mage,” alisema msichana huyo.
“Kweli?”
“Kweli kabisa.”
“Basi ingia twende nikaone,” alisema Dickson.
Kutokuwepo kwa Magreth hakukuwa na tatizo lolote lile, alichokuwa akikitaka mahali hapo ni kufanya mapenzi tu, hakujali chochote kile, akamchukua msichana yule na kuanza kuondoka naye mpaka kwenye gesti bubu ya Chenchebe iliyokuwa maeneo ya Mwananyamala. Walipofika, wakateremka na kuingia ndani pasipo dada wa mapokezi kuhoji sana kwani alikuwa mteja wake ambaye hakuwahi hatakumuona uso, alimzoea mno na hata wakati mwingine aliachiwa kiasi fulani cha fedha.

“Nataka unionyeshee ulichonacho sasa,” alisema Dickson. “Usijali,” alisema msichana yule, akakifuata kitanda na kuanza kujinyonganyonga maungo yake, alipomaliza akazivua nguo zake na Dickson kumfuata pale kitandani.
“Anza na kifua changu kwanza,” alisema msichana yule, kwa haraka pasipo kuuliza chochote Dickson akafanya kama alivyoambiwa pasipo kujua kwamba huo ulikuwa mtego mkubwa, msichana yule alitaka kumlevya na madawa ya usingizi aliyoyapaka kifuani.

Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 36

Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.

Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.

Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.

Huko, tabia yake ya kununua machangudoa inaendelea kama kawaida. Akaweka mazoea na changudoa mmoja aitwaye Magreth, kila alipokuwa akimhitaji, alimchukua. Siku moja anapokwend hapo, anaambiwa kwamba Magreth ni mgonjwa hivyo anamchukua changudoa mwingine ambaye alikuwa na lengo la kumlevya chumbani pasipo kujua kama yule ni Kamanda Dickson.

Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

Usiku ulikuwa mkubwa, milio ya risasi ilisikika kila sehemu, watu waliokuwa ndani ya nyumba zao, wakafunga milango na madirisha ili kuyaokoa maisha yao. Wale waliokuwa wakipita njia kuelekea kule kulipokuwa na kituo kikubwa cha polisi ambapo milio kadhaa ya risasi ilisikika, wakasimama na kurudi walipotoka, tena wakikimbia kwa mwendo wa kasi.

Polisi walikuwa wakishambuliana na watu waliokisiwa kuwa majambazi. Walifika kituoni hapo kwa malengo mawili tu, kuwaua polisi kisha kuiba silaha kama walivyofanya katika vituo vingine vilivyokuwa katika mikoa mingine.

Polisi hawakukubali, kwa kuwa nao walikuwa na silaha nzito, wakaanza kushambuliana na majambazi hao walioonekana moto wa kuotea mbali katika kutumia silaha hizo na hata ukwepaji wao. Polisi walidondoka chini, damu ziliwatoka, risasi zilipenya miilini mwao, hakukuwa na aliyemuokoa mwenzake wakati huo, kila mmoja alikuwa bize kutetea nafsi yake, majambazi wale waliendelea kuwamiminia risasi mfululizo.

“Wanakuja…” alisema polisi mmoja, alionekana kuchanganyikiwa mno.

“Wapigie simu makao makuu uwaambie tunahitaji msaada,” alisema polisi mwingine.

Hakukuwa na muda wa kupoteza, hapohapo akapiga simu, jina la mtu lililomjia kichwani mwake ni Kamanda Dickson, hapohapo akampigia simu, simu ikaanza kuita. Majambazi wale waliokuwa wamevaa kininja waliendelea kuwasogelea polisi wale, eneo zima la kituo hicho likabadilika na kuwa uwanja wa vita. Ni polisi watano ndiyo waliobakia kati ya polisi kumi waliokuwepo kituoni hapo.

* * *

Dickson alikuwa na mhemko mkubwa, alipoambiwa kwamba kifua cha changudoa yule kiliachwa kwa ajili yake, akaanza kukisogelea pasipo kujua kwamba kilikuwa kimepakwa dawa ya usingizi, ili alewe na kukombwa kila kitu.

Wakati akiwa tayari amekikaribia, mara akaanza kusikia simu yake ikiita. Haikuwa kawaida kupigiwa simu usiku, hakuwa na familia, hakuwa na marafiki wa karibu kutokana na ukali wake na hata polisi wake alikwishawaambia kwamba hataki kupigiwa simu usiku mpaka kuwe na kazi kubwa hasa majambazi.

Alihitaji muda wa kupumzika kutokana na kazi ngumu alizokuwa akizifanya kila siku. Kitendo cha kusikia simu yake ikiita, alijua kwamba kulikuwa na tatizo sehemu, hakutaka kuendelea, aliheshimu sana kazi kuliko mapenzi, alichokifanya, huku akionekana kama mtu aliyeshtuka, akaifuata suruali yake na kuichukua simu.

“Nani wewe?” aliuliza kibabe.

“Mkuu! Tumevamiwa hapa Kituo cha Polisi cha Jangwani, tunaomba utusaidie…” ilisikika sauti ya polisi mmoja simuni huku milio ya risasi ikiendelea kusikika mahali hapo.

Hakutaka kuuliza kitu chochote kile, tayari akajua kwamba kulikuwa na majambazi yaliyokuwa yamevamia kituo hicho. Hiyo ndiyo hali iliyokuwa ikiendelea nchini Tanzania, vituo mbalimbali vilivamiwa na polisi kuuawa kisha bunduki kuibwa, alichokifanya ni kuanza kuvaa harakaharaka.

“Nini tena mpenzi?” aliuliza changudoa yule, wakati huo alikuwa akimalizia kuvaa shati lake.

“Chukua hiyo,” alimwambia changudoa yule huku akimtupia noti za shilingi elfu kumi kitandani, ilikuwa elfu sabini.

Hakutaka kuchelewa, akatoka mle chumbani huku akikimbia kiasi kwamba hata dada wa mapokezi alimshangaa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea chumbani mpaka Dickson kukimbia, alipojaribu kumuita, Dickson hakugeuka, akalifuata gari lake, kitu cha kwanza kabisa akaangalia kama bastola yake ilikuwepo pale alipokuwa akiiweka, akaiona, akawasha gari na kuanza kuelekea huko.

Kutoka Mwananyamala mpaka Jangwani hakukuwa mbali, tena kwa sababu alitumia gari binafsi huku ikiwa ni usiku sana ambapo hakukuwa na magari mengi barabarani, aliendesha kwa mwendo wa kasi kiasi kwamba baadhi ya watu waliokuwa barabarani walimshangaa.

Alipofika Magomeni, kitu cha kwanza akazima taa za gari lake na kuendelea kusogea kule kulipokuwa na kituo kile. Bado milio ya risasi iliendelea kusikika mahali hapo, alipokaribia zaidi, akasimamisha gari lake kisha kuteremka na kuanza kutembea kwa mwendo wa kunyata tena kwa kuinamainama huku akisogea kule kulipokuwa na kituo.

Mbele kabisa, aliwaona wanaume watano wakitembea kuelekea kituoni huku wakiwa na bunduki mikononi mwao. Hakutaka kujiuliza mara mbilimbili, akajua wale ndiyo walikuwa majambazi na walikuwa wakikisogelea kituo huku wakipiga risasi, hakukuwa na majibu kutoka kwa polisi hali iliyoonesha walikuwa wameishiwa risasi.

“Paaa…paaa…paaa…” ilisikika milio mingine ya risasi mahali hapo, alifyatua risasi tatu mfululizo, kutokana na shabaha aliyokuwa nayo, hapohapo majambazi watatu wakaanguka chini, damu zikaanza kuwatoka shingoni na vichwani mwao.

Wale wengine wawili wakaonekana kuchanganyikiwa, wenzao walikuwa chini, hawakujua risasi zilitoka upande gani, walichokifanya ni kuanza kurudi nyuma.

Mpaka kufikia hapo, Dickson akaona hiyo ndiyo ilikuwa nafasi pekee, alichokifanya ni kuwasogelea kwa mwendo wa kuinama tena kwa kasi. Majambazi wale waliokuwa wamepaki pikipiki zao pembeni, wakazichukua na kuziwasha kwa lengo la kukimbia.

“Paaa…” ulisikika mlio mmoja wa risasi, jambazi mmoja akadondoka chini.

Dickson hakutaka kuchelewa, kwa mwendo wa kasi akamfuata jambazi aliyetaka kutimua mbio na pikipiki, alipomkaribia, kama ndege, akamrukia kwa nyuma, wote wakadondoka chini.

Jambazi akachukua bunduki yake ili amfyatulie risasi Dickson, bunduki haikuwa na risasi, Dickson alipoichukua bunduki yake na kujaribu kumfyatulia risasi jambazi yule, nayo haikuwa na risasi. Wakabaki wakiangaliana, kilichobakia ni kuoneshana kazi kama wanaume, kila mmoja akakunja ngumi. Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi ya kila mmoja kuiokoa nafsi yake.

“Fight like a man,” (Pigana kama mwanaume) Dickson alimwambia jambazi yule.

Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 37

Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.

Huko, tabia yake ya kununua machangudoa inaendelea kama kawaida. Akaweka mazoea na changudoa mmoja aitwaye Magreth, kila alipokuwa akimhitaji, alimchukua. Siku moja alipokwenda hapo, anaambiwa kwamba Magreth ni mgonjwa hivyo anamchukua changudoa mwingine ambaye alikuwa na lengo la kumlevya chumbani pasipo kujua kama yule ni Kamanda Dickson. Hata kabla hajafanya mapenzi na changudoa huyo, anapigiwa simu na kuambiwa kituo kimoja cha polisi kimevamiwa.

Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

Walibaki wakiangaliana tu, hali ya ukimya ilikuwa imetawala mahali hapo mara baada ya milio ya risasi kutawala sekunde chache zilizopita. Dickson akabaki akimwangalia jambazi yule kwa umakini mkubwa huku akionekana kuwa na hasira mno.

Tayari alikunja ngumi, kilichofuata ni kumsogelea na kuanza kupigana. Mpaka kufikia hatua ya kuwa DCP wa Kanda ya Dar es Salaam, alifanikiwa kupitia mafunzo mengi, kupambana kwa kutumia risasi au kwa kutumia mikono na miguu.

Hakutaka kuchelewa, mara baada ya kumsogelea jambazi yule ambaye alionekana kutokuwa na mafunzo yoyote ya mapigano, akampiga teke moja zito la mbavu ambalo lilimfanya kupepesuka huku kabla hajaamua nini cha kufanya akapigwa ngumi moja ya shavu ambayo ilimpeleka chini moja kwa moja na kuanza kugaragara kwa maumivu makali.

Haikuwa kazi kubwa, ni ndani ya sekunde thelathini, kila kitu kilikuwa tayari alichokifanya ni kulichukua jambazi lile na kulipeleka kituoni ambapo askari wenzake bado walikuwa wamejificha wakiogopa kupigwa risasi.

“Kamanda..” aliita polisi mmoja aliyekuwa amejificha nyuma ya meza kubwa ya kaunta, alikuwa na wenzake wawili, wakasimama na kuanza kupiga saluti.

“Hebu liwekeni ndani kwanza,” alisema Dickson.

Mara baada ya ukimya mkubwa kutawala hapo ndipo watu waliokuwa ndani ya nyumba zao wakafungua milango na kutoka ndani kuona ni kitu gani kilichokuwa kimetokea. Macho yao yakatua katika miili ya majambazi na polisi iliyokuwa chini huku damu zikionekana kukauka.

Polisi waliokuwa mahali hapo wakaanza kuwazuia raia wasisogee kule ilipokuwa miili ile. Ni ndani ya dakika kadhaa, tayari polisi wengine wakafika kituoni hapo wakaichukua miili ya majambazi wengine na kuondoka nayo.

“Nani kafanya haya yote?” aliuliza raia mmoja, alionekana kutokuamini kilichotokea.

“Nilisikia polisi mmoja akisema ni kamanda Dickson,” alijibu raia mwingine.

“Kamanda Dickson?”

“Ndiyo! Kama kweli ni yeye, huyu mtu kweli hatari, tukipata makamanda watano tu kama yeye, mbona amani itakuwepo,” alidakia raia mwingine.

Siku iliyofuata, vyombo mbalimbali vya habari vikaanza kutangaza kilichotokea katika Kituo cha Polisi cha Jangwani, kila aliyesikia hakuamini, kitendo cha kishujaa alichokifanya kamanda Dickson kiliendelea kuwaonesha watu ni jinsi gani alikuwa shupafu.

Sifa zake ziliendelea kutapakaa kila kona, kila alipoitwa alipongezwa kwa kazi kubwa aliyokuwa ameifanya ambayo kwa namna moja au nyingine ilionesha namna alivyo hatarisha maisha yake kwa ajili ya kuleta heshima katika kazi ngumu ya kipolisi.

Japokuwa alionekana kuwa mwanaume shupavu, mwenye umakini mkubwa awapo kazini lakini bado tatizo lake lilikuwa palepale kwamba alikuwa mtu wa kupenda kununua mno machangudoa barabarani pasipo kujulikana.

Sura yake ikamfanya kukosa mke, hakupendwa na wanawake wengi kwani pamoja na sura yake mbaya bado wengine walimuogopa kutokana na matukio aliyokuwa akiyafanya kila majambazi walipokuwa wakifanya uhalifu sehemu fulani.

* * *

Alikuwa miongoni mwa wanawake wazuri, waliojaliwa kuwa na umbo zuri ambalo watu wanaojua jinsi mwanamke alivyo, wangeliita umbo namba nane. Uzuri wake ulimvutia kila mtu aliyekuwa akimwangalia, alikuwa na sura nyembamba, lipsi nene huku macho yake muda wote yakionekana kuwa mazito kama mtu aliyekuwa na usingizi mzito.

Kwa jina aliitwa Pamela Samsoni, msichana mwenye kimo cha wastani, mweupe na mwenye mwendo wa maringo mithili ya twiga. Katika Mtaa wa Sakina jijini Arusha alipokuwa akiishi, Pamela alikuwa gumzo kila kona, alipendwa na wanaume wengi, kila alipopita, alipokuwa akipigiwa miluzi, kwa kasi ya ajabu kama feni izungukayo, aligeuka na kuangalia mluzi ulipotoka.

Japokuwa alikuwa mzuri mno aliyewatetemesha wanaume wengi lakini hakuuthamini uzuri wake, alikuwa radhi kulala na mwanaume kwa kuwa tu alichokiangalia ni pesa. Alipendwa na watu wenye fedha, hakutaka kujua mwanaume alikuwa mzuri kiasi gani, kitu cha kwanza alichokuwa akitaka kuona ni mifuko na pochi, zilikuwa zimetuna au zilidhoofika.

“Umeumbika vizuri, una sura nzuri, kwa nini usiolewe?” aliuliza mwanaume mmoja, alikuwa akimwangalia Pamela kwa macho ya matamanio.

“Una sura nzuri, kifua kipana, kwa nini usioe?” naye alimrudishia swali mwanaume huyo.

“Mmh! Aya nimeelewa unamaanisha nini.”

Alikubalika mitaani, alipendwa kila kona, si kwa wanaume tu bali hata wanawake waliokuwa wakimwangalia Pamela walisema wazi kwamba alikuwa miongoni mwa wasichana wazuri mno. Mbali na uzuri aliokuwa nao, tabia ya kujiuza kwa wanaume mbalimbali, Pamela alikuwa na udhaifu mmoja tu.

Alipokuwa akimpenda mwanaume, alimpenda haswa, katika mapenzi, alikuwa na hasira za karibu, kumshambulia mtu kwa ajili ya mapenzi ilikuwa moja ya sehemu ya maisha yake. Wanawake wengi walilifahamu hilo, kila mwanaume aliyekuwa akimpata, hakukuwa na mtu aliyemuingilia kwani waliujua fika ukorofi wake, walijua namna ambavyo binti huyo alikuwa radhi kukurushia chupa ilimradi mwisho wa siku ujutie kitendo cha kumchukulia mwanaume wake.

Siku zikaendelea kukatika huku Pamela akiendelea kujiuza kwa mteja mmojammoja lakini baada ya kipindi cha miezi sita, hapo ndipo alipoanza kujiuza karibu na Hoteli ya Chibuchibu iliyokuwa jijini Arusha ambapo hapo alipata wateja wengi.

“Twende Mererani,” alisema rafiki yake mmoja.

“Kufanya nini?”

“Sasa swali gani hilo Pamela? Kwani unaweza kuchimba madini?” aliuliza rafiki yake huyo.

“Kuchimba madini?”

“Sasa umeniuliza kufanya nini kwani hujui kazi yako inayokuweka mjini?’ aliuliza rafiki yake huyo kwa sauti ya chini.

Siku iliyofuata wakaanza safari ya kuelekea Mererani, bado maisha ya kujiuza yalimsumbua, alikuwa radhi kuzunguka sehemu yoyote ile lakini mwisho wa siku aweze kuingiza kiasi kikubwa cha fedha.

Huko alipokuwa akienda na rafiki yake huyo, walikuwa na kazi moja tu, kujiuza kwa wanaume waliokuwa na fedha nyingi baada ya kuuza madini yao. Kwake, hivyo ndivyo maisha yalivyokwenda.

Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 38

Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.

Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.

Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.

Huko, tabia yake ya kununua machangudoa inaendelea kama kawaida. Akaweka mazoea na changudoa mmoja aitwaye Magreth, kila alipokuwa akimhitaji, alimchukua. Siku moja anapokwenda hapo, anaambiwa kwamba Magreth ni mgonjwa hivyo anamchukua changudoa mwingine ambaye alikuwa na lengo la kumlevya chumbani pasipo kujua kama yule ni Kamanda Dickson.

Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

Hata kabla Pamela na rafiki yake hawajafika Mererani, tayari watu wenye fedha zao wakapata taarifa juu ya ujio wao, stori iliyokuwa ikienea tena kwa kasi kubwa ni kwamba msichana mrembo, mwenye umbo matata aliyekuwa akikaa katika Mtaa wa Sakina, leo hii alikuwa akiingia Mererani kwa ajili ya kuwasalimia wanaume wa sehemu hiyo.

Waliokuwa na fedha zao, wakaziweka tayari, walikuwa tayari kwa kila kitu, hawakutaka kuona msichana huyo akifika na kuondoka huku wakiwa hawajafanya kitu chochote kile, hivyo wakamsubiria kwa hamu kubwa kama walivyomsubiria mbunge wao.

Ilipofika majira ya saa nane mchana, Pamela akafika hapo Mererani, wanaume walipomuona tu, wakakiri kwamba kweli msichana huyo alikuwa mrembo mno na alistahili kulitingisha Jiji la Arusha.

Watu wenye pesa zao, waliopata mzigo wa maana wakaanza kuwekeana madau wao wenyewe, kwa Pamela, ilikuwa furaha yake, alichokifuata Mererani hakikuwa kitu kingine zaidi ya pesa tu. Alizaliwa akiwa maskini, aliwalaumu sana wazazi wake na hivyo kupambana huku akijiahidi kwamba siku atakapokufa, awe ameweka kiasi kikubwa sana cha fedha katika akaunti yake.

Wanaume wakapangwa kwa zamu, leo Pamela alikuwa akilala na huyu kesho na yule. Hayo yalikuwa maisha yake ya kila siku, hayakuanzia hapo Mererani bali tangu alipokuwa Arusha Mjini alilala na wanaume mbalimbali.

Baada ya kukaa kipindi cha mwezi tena huku akiwa amepata kiasi kikubwa cha fedha, hapo ndipo alipopanga kwenda jijini Dar es Salaam. Hakuwahi kufika katika jiji hilo, alisikia sifa nyingi kwamba lilikuwa jiji zuri, lenye starehe za kila aina, hivyo naye alitaka kwenda huko.

“Ninataka kwenda Dar,” alisema Pamela.

“Kufanya nini?” aliuliza rafiki yake.

“Kufanya hiki ninachokifanya hapa,” alijibu Pamela.

“Mmmh! Shosti, yaani pamoja na kupata fedha hapa bado unataka kwenda Dar?” aliuliza rafiki yake huku akishangaa.

“Ndiyo! Sifuati fedha, ninataka kwenda kupaona, natamani niishi sehemu Ikulu ilipo,” alisema Pamela huku akiachia tabasamu pana.

“Sawa! Utafikia wapi?”

“Hilo nalo ni swali jamani?”

“Ndiyo! Una ndugu?”

“Sina ndugu ila nina pesa,” alijibu Pamela.

Hakutaka kubadilisha mawazo yake, alichokuwa amekifikiria mahali hapo ilikuwa ni lazima kwenda jijini Dar es Salaam, alitaka kufanya matanuzi, alitaka kuwa katika jiji lililosifika kwa starehe na kuwa na wanaume wengi waliojua kuhonga.

Katika wiki ya mwisho kukaa Mererani, aliamua kukusanya fedha nyingi mno, kila mwanaume aliyelala naye katika siku hizo, alimlipa kiasi kikubwa cha fedha na baada ya siku kadhaa, alikuwa ndani ya ndege akielekea jijini Dar.

Hakuwahi kufika huko, hakuijua mitaa ya huko zaidi ya kuisikia tu. Hakuwa na presha, aliamini katika pesa kwamba unapokuwa nazo kila kitu kitakwenda sawa. Baada ya saa kadhaa, ndege hiyo ikaanza kushuka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akateremka, hakuamini kama mwisho wa siku miguu yake ingekanyaga ardhi ya Jiji la Dar, akaanza kupiga hatua na abiria wengine kuelekea katika jengo la uwanja huo kwa ajili ya kuchukua mabegi yake, kila alipokuwa akitembea, hakuamini kama alikuwa jijini Dar.

*****

Kama kawaida yake, Dickson alikuwa amesimamisha gari lake pembezoni mwa baa maarufu ya Caspinho iliyokuwa Sinza Mori jijini Dar. Macho yake hayakutulia, alikuwa akiangalia huku na kule, alionekana kuwa bize kumtafuta msichana fulani.

Wanawake wengi walijipanga barabarani, kila mwanaume aliyekuwa akipita karibu na eneo walilosimama, walimfuata na kumwambia kiasi walichokuwa wakijiuza, ili kama mnunuzi asimame na kununua na kama si mnunuzi basi aendelee na safari yake.

Machangudoa wengi walioliona gari la Dickson, hawakutaka kulisogelea, walizoea kuliona mahali hapo, mara kwa mara alikuwa akifika na kumchukua changudoa mmoja ambaye kwa siku mbili tatu hakuwepo, changudoa huyo alikuwa Magreth.

Aliendelea kuangalia huku na kule, mara kwa mbali akamuona msichana mmoja akimfuata, akamwangalia vizuri, hakuwa mgeni, alikuwa Magreth ambaye alikuwa akitembea kwa kasi kumfuata kule aliposimamisha gari lake, alipofika, akaufungua mlango na kuingia ndani.

“Nimekumisi mpenzi,” alisema Magreth kwa sauti ndogo, garini kulikuwa na mwanga hafifu mno, hakuweza kumuona vizuri Dickson.

“Nimekumisi pia, upo tayari?” aliuliza Dickson.

“Ndiyo! Ushindwe wewe tu,” alisema Magreth, hapohapo akawasha gari na kuondoka.

Njiani walizungumza mengi, walizoeana na kuwa marafiki wa damu, Dickson alikuwa na maswali mengi mno, yote hayo alitaka kufahamu mahali alipokuwa Magreth kipindi cha nyuma kwani alifika mahali hapo mara ka mara lakini hakuwa akimkuta.

“Niliumwa sana, ila kwa sasa nipo fiti,” alisema Magreth.

“Hahaha! Usije ukanifia kitandani.”

“Usijali kipenzi,” alisema Magreth, muda wote huo alikuwa akiongea kwa sauti ya kimahaba.

Walipofika katika gesti ya Chenchebe iliyokuwa Mwananyamala A, wakateremka na kuanza kuelekea ndani. Dickson akalipia na kuingia ndani huku akiwa amemshikilia kiuno Magreth, tena kofia ikiwa kichwani mwake.

Walipoingia chumbani, hata kabla ya kufanya kitu chochote, Dickson akachukua taulo na kuelekea bafuni kuoga. Alitaka kujiandaa hata kabla ya kufanya kile kilichompeleka ndani ya gesti ile.

Wakati anatoka, huku akiwa amejisahau, tena taa ikiwaka, macho yake yakatua usoni mwa mhudumu wa kike wa gesti ile aliyekuwa akielekea chooni. Macho ya mhudumu yule yalipotua usoni mwa Dickson, akaonesha mshtuko mkubwa, akakumbuka kwamba hata kofia yake aliisahau bafuni.

“Mungu wangu! Kamanda Dickson..!!” alisema mhudumu yule huku akionesha mshtuko wa waziwazi. Dickson akachanganyikiwa, akajikuta akirudi bafuni haraka kuchukua kofia yake na kuanza kumtafuta yule mhudumu.

Licha ya kumtafuta mapokezi na nje ya gesti hiyo, hakuweza kumuona yule mhudumu, akaanza kuiona aibu ikianza kumsogelea. Akapagawa!!

Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 39

Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.

Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anaendelea na tabia yake ya kununua machangudoa na kwenda nao gesti. Siku moja akiwa huko na changudoa aliyeitwa Magreth, ghafla mhudumu wa gesti hiyo anamuona na kugundua kwamba alikuwa DCP Dickson, anashtuka mno na kuanza kukimbia.

Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

“Samahani kaka!”

“Bila samahani!”

“Nataka nifike kwenye hoteli moja ya kawaida.”

“Poa! Panda twende! Unataka ya chumba kiasi gani kwa siku?”

“Hata elfu thelathini!”

“Umefika! Ingia!”

“Ipo wapi?”

“Kinondoni, kuna hoteli nzuri tu, usijali.”

Pamela alikuwa akizungumza na dereva ambaye alikuwa nje ya teksi yake iliyokuwa imepaki nje ya jengo la Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Macho yake yaliangalia huku na kule, hakuamini kama pale alipokuwa kwa kipindi hicho alikuwa jijini Dar es Salaam.

Alilisikia tu jiji hilo alipokuwa Arusha, aliambiwa kwamba lilikuwa jiji la raha lenye wanaume wengi waliojua kuhonga huku kukiwa na starehe za kila aina na ndiyo maana katika kipindi hicho aliamua kufika jijini humo ili kushuhudia kile alichokuwa amekisikia.

Gari likaanza safari, katika njia nzima, Pamela alikuwa akiangalia huku na kule, kulikuwa na idadi kubwa ya watu. Alihitaji kulizoea jiji kwani aliamini kwamba humo ndimo yangekuwa maisha yake yote katika miaka yote.

Walichukua dakika arobaini na tano ndipo wakaingia katika Hoteli ya Swing iliyokuwa Kinondoni B. Mlango ukafunguliwa na Pamela kuteremka, akamlipa dereva kiasi cha fedha alichokuwa akikihitaji kisha kuelekea mapokezi.

Hakuwa mshamba wa hoteli, aliwahi kukaa katika hoteli nyingi, zenye gharama kubwa na kulala chumba chochote alichokihitaji, kuwa ndani ya hoteli hiyo kwake lilionekana kuwa suala la kawaida. Macho yake hayakutulia, bado alikuwa akiangalia huku na kule, alitamani kuyazoea mazingira kwa haraka sana ili pale atakapoanza kufanya kazi basi asiweze kupata shida yoyote ile.

Alipopewa chumba na kuelekea chumbani, akalala kitandani, mawazo yakamsonga, akili ikachemka. Alikuwa ndani ya jiji jingine, alikuwa mgeni, hakumfahamu mtu yeyote yule, kwake, kila kitu kilikuwa kigeni. Hakujua ni wapi angeanzia kufanya biashara yake ya kuuza mwili, hakujua viwanja, kiwanja pekee alichokuwa amekisikia ni kile kilichoitwa Kinondoni Makaburini ambacho hakujua kilikuwa mahali gani.

Usiku hakutaka kukaa ndani, akatoka nje ili kuona ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea. Nje ya hoteli ile aliwaona wasichana wengi wakiwa wamesimama pembezoni, walivalia nguo fupi na kuyaacha mapaja yao wazi kabisa huku wengine wakiwa wameshika sigara.

Hakutaka kujiuliza hao walikuwa akina nani, kitu kilichomjia kichwani ni kwamba wanawake wale aliokuwa amewaona walikuwa machangudoa kama alivyokuwa.

“Kumbe hapa napo kuna biashara, nitaanza kufanya,” alisema Pamela.

Kitu alichokifanya hata kabla ya kuanza kufanya biashara hiyo ni kumtafuta msichana ambaye aliamini kwamba kupitia yeye angeweza kumwambia mambo mengi ili hata siku atakapoanza kufanya biashara hiyo asiweze kupata usumbufu wowote.

“Wapi kupo poa tu, kodi yako ndiyo inahitajika,” alisema msichana huyo.

“Hiyo kodi inalipwa wapi?”

“Paleee…kwenye ile kaunta. Kama mnunuaji atakuwa bahili, utawaambia wenye Bajaj, wote watu wetu, unaweza kumalizia shida zako humo,” alisema changudoa huyo, maneno hayo yakamwingia akilini Pamela.

*****

Hakukuwa na siku ambayo Dickson alichanganyikiwa kama siku hiyo, msichana wa mapokezi ambaye alimuona uso wake na kumgundua hakuwepo, alikimbia na kwenda kusipojulikana. Dickson akarudi chumbani kwake, alionekana kuwa na haraka mno, kijasho chembamba kikaanza kumtoka japokuwa alitoka kuoga.

“Vipi tena?”

“Unasemaje?” aliuliza, hata hakumsikia vizuri Magreth, tayari alianza kuvaa nguo zake haraka.

“Mbona unavaa nguo?”

“Nimepigiwa simu nimefiwa!”

“Umefiwa? Hiyo simu umepigiwa wapi na wakati ilikuwa kwenye nguo yako?” aliuliza Magreth.

“Subiri kwanza. Ni lazima niondoke.”

Uondoke tena?”

“Ndiyo!”

Hakutaka kuzungumza sana, kichwa chake kilichanganyikiwa, kitendo cha msichana yule wa mapokezi kuondoka na kuelekea asipopafahamu kilionekana kuwa tatizo kubwa kwa upande wake, hakutaka kubaki ndani ya chumba kile.

Alichokifanya ni kumpatia Magreth kiasi cha shili laki moja kisha kutoka mle chumbani kwa kasi.

Alipofika mapokezi, msichana yule hakuwepo, alichanganyikiwa zaidi, hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka kuelekea nje. Alijua kwamba msichana yule hakuwa mtu wa kukaa mbali na gesti ile, alikuwa na uhakika alikuwa akiishi karibu na maeneo hayo.

Huku akiwa na kofia yake kichwani, akaanza kutembea kwa mwendo wa haraka kuelekea katika upande waliokuwepo wanaume fulani waliokuwa wamekaa wakipiga stori kwenye banda la muuza chipsi. Alipowafikia, akawasalimia na kuanza kuzungumza nao.

“Kuna dada namuulizia,” alisema Dickson huku akiwaangalia wanaume hao, hawakuwa wakimtambua kutokana na giza pamoja na ile kofia kubwa aliyokuwa ameivaa.

“Dada yupi?”

“Yule anayehudumia kwenye ile gesti! Mnamfahamu?”

“Nani? Fatuma?”

“Sijui, ni mweupe, mrefu kidogo ana kidoti hapa karibu na pua.”

“Ni Fatuma huyo! Anaishi nyumba ile pale.”

“Ipi?”

“Ile inayowaka taa nyekundu yenye bustani ya maua kwa nje,” alisema kijana mmoja.

“Asante sana.”

“Kwani kuna nini braza? Tumemuona ametoka huku akikimbia!”

“Hakuna kitu, asanteni,” alisema Dickson na kuanza kupiga hatua kuelekea kule ilipokuwa nyumba ile. Hakuonekana kuwa na masihara, alichokuwa amekipanga, ilikuwa ni lazima Fatuma afe.

Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 40

Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.

Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.

Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.

Mara baada ya kufanikiwa na kuwa DCP Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Dickson anaendelea na utaratibu wake wa kununua machangudoa mitaani. Akiwa kwenye harakati hizo anakutana na changudoa mmoja aitwaye Magreth, wanakuwa marafiki na kila anapofika pa kununulia machangudoa, anamtafuta Magreth kwani ndiye aliyemzoea.

Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

Dickson aliendelea kuisogelea nyumba ile, alichokuwa akikitaka ni kumuona Fatuma tu, yule msichana wa mapokezi kwani alihisi kama angemuacha ilikuwa ni lazima kutoa siri kwamba alikwenda katika gesti ile usiku akiwa na mwanamke kitu ambacho kwake alikiona kuwa aibu kubwa.

Mishipa ya shingo ilimsimama, mzunguko wake wa damu ukazidi kuongezeka mwilini mwake, alikuwa na hasira iliyochanganyikana na hofu kubwa kwa kuhisi kwamba ilikuwa ni lazima kwa mtu kama Fatuma kuwaambia watu kile alichokiona mle ndani.

Alipoifikia nyumba ile, hakutaka kupiga hodi, kwanza akatulia na kusikiliza ndani kama kulikuwa na sauti za watu waliokuwa wakiongea, aliposikiliza kwa kutegesha sikio lake, ukimya mkubwa ulitawala.Alichokifanya ni kuanza kuusogelea mlango wa kuingilia ndani, alitaka kuufungua na kuingia katika nyumba hiyo iliyokuwa na vyumba vingi vya kupanga. Alijaribu kuusukuma mlango, haukufunguka.

“Ngoja...” alijisemea, alichokifanya baada ya hapo ni kuanza kupiga hodi. Alitaka kufunguliwa mlango, aingie ndani kisha kutekeleza kile alichotaka kukifanya mahali hapo. Haukuchukua muda mrefu, mlango ukafunguliwa, mwanaume mwenye kipensi akatoka ndani.

“Karibu,” alisema kijana yule huku macho yake yakiwa mazito kwa usingizi.
“Fatuma yupo?” aliuliza Dickson hata kabla ya salamu.“Fatuma! Sasa hivi? Mmmh! Sidhani! Hebu subiri,” alisema kijana yule, akarudi ndani.

Dickson hakutaka kubaki pale mlangoni, akaanza kumfuata kijana yule kwani alijua dhahiri kwamba endapo msichana huyo angejua kwamba kulikuwa na mtu aliyekuja kumuulizia, ni lazima angesema hayupo, ili kumkamata kirahisi, naye akaanza kumfuata kijana yule ambaye aliishia katika mlango wa chumba kimoja na kuanza kuugonga huku akiliita jina la Fatuma.

“Hayupo kaka! Kwanza huwa harudi muda huu,” alisema kijana yule.
“Huwa anarudi muda gani?”
“Mpaka asubuhi! Analala hukohuko kazini kwake.”

“Ila kuna vijana wameniambia amekuja huku!”
“Mmhh! Sidhani! Au amekwenda kwa bwana wake, kwa sababu huko ndipo huwa anakwenda,” alisema kijana yule.
“Anaishi wapi?”
“Nani? Huyo bwana wake?”
“Ndiyo!”
“Hapo mbele, kuna nyumba fulani hivi kalikali, ila kuwa makini, kuna wavuta bangi wengi wasije wakakutoa roho,” alisema kijana yule kama kumtahadharisha.
“Usijali.”

Kila kitu alikifanya harakaharaka, hakutaka kupoteza muda, kwa kuwa alikwishaambiwa juu ya nyumba ambayo ilisemekana kuwepo kwa Fatuma, akaanza kwenda huko.Hakutaka kusikia kitu chochote kile, kile alichokitaka ni kumuua msichana huyo tu. Aliifikiria nchi ya Tanzania, akawafikiria watu wake, akaifikiria heshima aliyojijengea na kukumbuka siku alizokuwa akiongea kwa msisitizo kwamba machangudoa wote wakamatwe kwani hakupendezwa na uwepo wao, kweli walikamatwa, sasa leo hii, yeye mwenyewe alionwa gesti akiwa na changudoa, alijaribu kuiifikiria aibu yake, ilikuwa kubwa mno.

Nyumba ile haikuwa mbali sana na alipotoka, baada ya dakika mbili, akafika na kulifuata geti. Pua yake ikaanza kunusa harufu kali ya bangi iliyotoka ndani ya nyumba hiyo, hapo akajua kwamba hiyo ndiyo nyumba aliyokuwemo msichana Fatuma hivyo hakutakiwa kugonga, alitaka kuingia moja kwa moja ndani.

Ndivyo alivyofanya, geti lilifungwa ila kwake haikuonekana kuwa tatizo, akauparamia ukuta na kurukia ndani, akaanza kupiga hatua kuelekea kulipokuwa na chumba ambacho kwa nje kilikuwa na viatu vingi. Hata kabla hajaingia, akaanza kusikiliza ndani kulikuwa na watu wangapi, alizisikia sauti ambazo zilimpa uhakika kwamba watu waliokuwamo mle ndani hawakuzidi watatu.

Akakishika kitasa, akajaribu kuufungua mlango, ukafunguka, hapohapo akaanza kuingia ndani kwa mwendo wa kunyata. Taa ilikuwa inawaka, alipoingia tu, macho yake yakatua kwa vijana watatu waliokuwa wamekaa kitandani, walikuwa wakivuta bangi huku pembeni yao kukiwa na karatasi iliyokuwa na madawa ya kulevya.
“Oyaa! Mbona unaingia bila hodi mwana?’ aliuliza jamaa mmoja, kila mmoja alikuwa amelewa kutokana na kubwia madawa yale na kuvuta bangi kwa kiasi kikubwa.

“Fatuma yupo wapi?”
“Nani? Fatuma! Wewe nani mpaka umuulizie demu wangu?” aliuliza kijana mmoja kwa sauti yake ya kilevi.
Hakuwa na muda wa kupoteza mahali hapo, kuulizwa maswali yasiyokuwa na msingi, maswali aliyojua kabisa kwamba yaliulizwa na mtu aliyefahamu fika alizungumzia nini, akajikuta zile hasira alizokuwa nazo zikiongezeka zaidi.
Akakunja ngumi na kuwasogelea vijana wale kitandani pale kisha kuanza kuwapiga ngumi mfululizo. Alikuwa na nguvu, alipitia mafunzo makali hivyo kuwapiga vijana hao watatu halikuwa tatizo kabisa, aliwashushia ngumi mfululizo.
“Fatuma yupo wapi?’ aliuliza huku akiwa amekasirika mno.
“Yupo bafuni anaoga,” alijibu kijana mmoja, uso wake ulikuwa umejaa damu.
Alichokifanya Dickson ni kuchukua ufunguo wa chumba hicho, akatoka ndani kisha kuufunguka mlango kwa nje na kuelekea bafuni. Akaanza kupiga hatua kulifuata bafu ambapo kulisikika sauti ya maji yaliyokuwa yakimwagika,

kaufuata mlango, hakutaka kupiga hodi, akaupiga teke, ukavunjika, naye akaingia ndani. Macho yake yakagongana na macho ya Fatuma aliyekuwa akioga.
“Naomba unisamehe...sitomwambia mtu,” alisema Fatuma mara baada ya kugundua kwamba yule aliyeingia bafuni alikuwa kamanda Dickson.

“Hakuna siri ya watu wawili, ili siri itunzwe, lazima mmoja afe,” alisema Dickson, hapohapo akamsogelea Fatuma na kuanza kumkaba. Japokuwa msichana huyo alianza kukukuruka lakini Dickson hakuitoa mikono yake shingoni mwa Fatuma, alimkaba vilivyo, alitaka kumuua tu.

Je, nini kitafuatia? Usikose
 
SEHEMU YA 41

Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.

Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.

Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.

Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta akinunua machangudoa kwa kuwa tu hakuwa na sura nzuri ya kumpata mwanamke. Kila anapokwenda kuwanunua, kofia kubwa inakuwa kichwani mwake huku akimzuia msichana yeyote kumfahamu alikuwa nani na kila aliyebahatika kumuona na kumgundua, ilikuwa ni lazima auwawe.

Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

Pamela hakuishi sana hotelini akafanikiwa kupata chumba katika nyumba moja ambayo haikuwa mbali na eneo la Makaburini hapohapo Kinondoni. Ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na wanawake wanne ambao wote hao walikuwa na kazi ya kuuza miili yao nyakati za usiku katika eneo la Majaburini.

Wakajikuta wakianza kuwa karibu naye, Pamela alionekana kuwa msichana mrembo, mwenye sura nzuri na umbo matata ambalo hata machangudoa hao walipomwangalia, walibaki wakimsifia tu.

Kuishi ndani ya nyumba moja, wakajikuta wakianza kuwa marafiki, uchangamfu wa Pamela ulimvutia kila mmoja, wakajikuta wakimuuliza maswali mengi mpaka pale walipogundua kwamba mawazo yao yalikuwa sahihi kwamba msichana huyo alitaka kuwa changudoa na kufanya kazi pamoja nao.

“Kwa hiyo umekuja kwa ajili ya kazi hii?” aliuliza msichana mmoja, aliitwa Juliana.
“Ndiyo! Ila kule hotelini wameniambia nilipie,” alijibu Pamela.“Achana nao, wamekaa kitamaa na hakuna wateja wengi, kama vipi njoo kambini kwetu,” alisema Juliana.
“Wapi?”
“Makaburini.”

“Hakuna tatizo, ninashukuru, kesho tutakuwa pamoja.”
Alifika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kazi hiyo tu, alitaka kuwa na fedha nyingi, alitaka kuwa tajiri, ajijengee heshima kubwa nchini Tanzania. Hakukuwa na kitu alichokitegemea kwa wakati huo zaidi ya kujiuza tu.

Siku ya kwanza kufika katika eneo la Makaburini, Pamela alikuwa gumzo, kila changudoa aliyemuona alishtuka, umbo lake liliwaacha midomo wazi, miguu minene, ngozi yake yenye kung’ara na sura ya kitoto iliwafanya machangudoa wote kumkubali na kumuonea wivu.

Kuanzia siku hiyo, hapo ndiyo ilikuwa ofisi yake, kila siku usiku alifika hapo na kujiuza kama walivyofanya wengine. Wale wateja wazoefu waliojiwekea mazoea ya kufika makaburini hapo kununua machangudoa walipomuona Pamela walichanganyikiwa, hawakuamini kama katika eneo hilo kungekuwa na msichana mrembo kama Pamela, umbo na mvuto wake walizoea kuwaona wasichana wa namna hiyo katika klabu kubwa jijini Dar au hata kwenye makasino mbalimbali.

“Mmmh! Wewe ni mgeni?” aliuliza mwanaume mmoja, alikuwa mtu wa miraba minne, kichwani alinyoa upara, pembeni alipaki gari lake la kifahari, kwa kumwangalia, alionekana kuyazoea mazingira ya eneo hilo.
“Siyo sana, wiki yangu ya pili hii.”

“Ooh! Kumbe, basi nilikuwa napitwa sana. Mbona sikuwa nikikuona?”
“Mara nyingi huwa natoka na wateja.”
“Sawa, hakuna tatizo. Gharama yako iko vipi?”
“Showtime au kuamsha popo?”
“Kuamsha popo, mpaka asubuhi.”
“Elfu hamsini.”
“Hakuna tatizo.”

Mara baada ya kukubaliana, wakalifuata gari na kuingia ndani kisha kuondoka. Machangudoa wengine walionekana kumchukia Pamela, tangu kufika kwake ndani ya eneo hilo, biashara ikawa ngumu, wateja wengi waliofika mahali hapo, mtu waliyekuwa wakimtaka alikuwa Pamela tu.

Safari iliendelea mpaka walipofika Upanga ambapo gari hilo likasimama nje ya nyumba moja ya kifahari iliyozungushiwa ukuta. Mzee yule akapiga honi, hapohapo mlinzi akafungua geti na kuanza kuliingiza gari ndani. Pamela akabaki akiishangaa nyumba hiyo, ilikuwa ni ya kifahari sana, ilionesha ni jinsi gani mzee huyo alivyokuwa na fedha.
* * * * *
Hakukuwa na kitu kingine alichokuwa akikitaka zaidi ya kumuua Fatuma. Hakutaka kuamini kama kulikuwa na siri ya watu wawili duniani, alikuwa na uwezo wa kumuacha Fatuma lakini kwa jinsi alivyomuona msichana huyo, hakuwa na moyo wa kutunza siri ile.

Hakutaka kujulikana, hakutaka kupata aibu baada ya kugundulika kwamba hata yeye ambaye kila siku alikuwa mkemeaji mzuri wa uwepo wa machangudoa naye alikuwa mmoja wa wanunuzi waliofika katika viwanja vya machangudoa.

Alimkaba vilivyo, Fatuma alikukuruka huku na kule lakini mkono wa Dickson haukutoka shingoni mwake, aliendelea kumkaba vilivyo. Wala hazikuchukua dakika nyingi, Pamela akaanza kulegea, mapovu yaliyochanganyikana na damu yakaanza kutoka mdomoni mwake, mishipa ikamtoka na hapohapo pumzi ikakata na kufariki dunia.

Alichokifanya Dickson ni kuanza kuufuta mwili ule kwa taulo la Fatuma kwa ajili kuficha alama za vidole vyake, alipomaliza akatoka mle bafuni na kuondoka zake huku akiwa na uhakika kwamba kile kilichokuwa kimetokea kingeendelea kuwa siri milele.
*****
“Mnasemaje?”
“Kuna mwanaume aliingia ndani jana usiku.”
“Mwanaume gani?”
“Mfupi kiasi fulani, alikuwa na mwili uliojazia.”

“Unaweza kumfahamu hata ukimuona?”
“Hapana! Alivalia kofia kubwa ya Marlboro, sikuweza kumuona vizuri.”
“Kweli?”
“Haki ya Mungu tena.”
“Na kwa nini alimuua Pamela?”
“Sijui mkuu.”

“Sawa. Mpelekeni sero, tutamhitaji tena. Mleteni mwingine.”
Vijana wale waliokuwa wakivuta bangi na madawa ya kulevya katika nyumba aliyouawa Fatuma walifikishwa kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa ushahidi juu ya mauaji yaliyokuwa yametokea usiku waliokuwa ndani ya nyumba ile.

Kila aliyeulizwa, majibu yake yalikuwa yaleyale kwamba hawakuweza kumfahamu muuaji kwa sababu kichwani alikuwa na kofia kubwa hivyo uso wake kutokuonekana vizuri. Polisi wakachanganyikiwa, mauaji yale yaliwachanganya mno.

Mwili ulipelekwa katika chumba cha uchunguzi hospitalini kwa ajili ya kumbaini muuaji kwa njia ya kuangalia alama za vidole mwilini mwake lakini majibu yaliyotoka yalionesha mwili ulioshwa na kufutwa, hivyo alama za vidole hazikuonekana kitu kilichowafanya polisi kugundua kwamba mtu aliyefanya mauaji alifahamu mengi, hasa yote walivyokuwa wakifanya wapelelezi. Kukaonekana kuwa na ugumu wa kumpata muuaji huyo. Hawakujua kama kiongozi wao ndiye aliyehusika kwa kila kitu.

Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 42

Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.

Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.

Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.

Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anaendelea kununua machangudoa sehemu mbalimbali na kila changudoa anayegundua kwamba ni yeye, anamuua. Sasa hivi amekutana na changudoa aitwaye Magreth, wametokea kuzoeana mno. Mbali na Dickson, upande wa pili kuna changudoa aliyetoka Arusha, anaitwa Pamela, anasafiri kwenda Dar kwa ajili ya kufanya biashara zake.

Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

“Unasemaje?” aliuliza kamanda Dickson huku akijifanya kushtuka.

“Kuna mwanamke aliuawa jana, taarifa hizo zililetwa saa kumi na mbili asubuhi,” alisema polisi aliyepeleka taarifa.
“Wapi?”
“Mwanayamala.”
“Na muuaji mmemkamata?”

“Hapana. Ila anaonekana kufahamu mambo mengi hasa yanayohusu uchunguzi katika mwili wa marehemu. Tulijaribu kuchunguza ili tupate hata alama za vidole, hatukuambulia kitu,” alisema polisi huyo.
“Kwa hiyo baada ya hapo mkaamua tu mrudi ofisini, mkalie viti, mkunje nne na mgongesheane glasi?” aliuliza Dickson.
“Hapana mkuu.”

“Kumbe?”
“Bado tunalishughulia suala hilo, nakuahidi baada ya wiki moja tutakuwa na majibu,” alisema polisi huyo.
“Sawa. Nenda.”
Polisi yule alipotoka ndani ya ofisi yake, Dickson akashusha pumzi ndefu, akakenua meno kwa furaha. Moyo wake ukafarijika baada ya kuona kwamba alifanya mauaji na mpaka kipindi hicho polisi bado waliendelea kumtafuta muuaji.
Hakuacha kwenda kununua machangudoa usiku, kila baada ya siku tatu ilikuwa ni lazima kwenda huko na mtu ambaye alimchukua alikuwa Magreth. Kwake alikuwa msichana mrembo lakini kitendo cha kumchukua mara kwa mara kikamchosha, akahitaji kuwa na wanawake wengine.

Kumwambia Magreth lilikuwa jambo gumu, alimzoea na hakujua ni kwa namna gani angeweza kumwambia ili amchukue changudoa mwingine. Baada ya kuona ameshindwa kabisa, hapo ndipo alipoamua kufanya maamuzi yaliyoonekana kuwa magumu kwake.

Siku hiyo alipofika katika eneo la kununua machangudoa, kama kawaida yake alilisimamisha gari lake mbali kabisa, akashusha kioo cha dirisha kisha kuchungulia nje. Machangudoa walipoliona gari hilo, wakaanza kujipitisha mbele yake huku wakiinadi miili yao, wengine walivaa suruali za jeans na wengine sketi fupi. Dickson akatoa ishara ya kumuita changudoa mmoja, mwenye umbo namba nane huku akiwa amezibana nywele zake kwa nyuma.
“Niambie baby,” alisema msichana yule mara baada ya kulifikia gari lile.

“Umependeza sana, nahisi nitakuwa mtu mwenye bahati sana kama nitapata huduma yako leo,” alisema Dickson, kama kawaida kofia ya Marlboro ilikuwa kichwani mwake, mwanga hafifu uliokuwa ndani ya gari ulimfanya kutokuonekana vizuri.
“Hakuna tatizo. Laki mbili mpaka asubuhi.”
“Mmmh!”
“Nini tena?”

“Mbona gharama?”
“Wewe unanionaje? Unalionaje hili umbo? Hili ni umbo la kulipia vijisenti hivyo kweli baby wa mie?” aliuliza changudoa yule, ikambidi Dickson amwangalie vizuri, alikuwa msichana mwenye umbo la kuvutia mno.
“Ingia twende,” alisema Dickson, msichana yule akaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea katika nyumba ya wageni ikaanza.

* * *
Gari likaingizwa ndani, Pamela akabaki akiliangalia jumba lile la kifahari, hakuamini kwamba kungekuwa na mtu ambaye alimiliki jumba kubwa kama hilo tena ndani ya nchi kama Tanzania, nchi iliyokuwa na wananchi wengi maskini.

Wakateremka na kuanza kuelekea ndani. Muda wote mzee yule aliyemnunua alionekana na furaha tele, kila alipokuwa akimwangalia Pamela, alijiona kuwa miongoni mwa watu ambao wangefaidi usiku wa siku hiyo.
“Twende tukaoge kwanza,” alisema mzee huyo, hivyo wakavua nguo zao na kuingia bafuni.

Muda wote huo mzee yule alibaki akimwangalia Pamela kwa macho ya matamanio, hakuamini kama kweli amekutana na mwanamke aliyekuwa na umbo zuri kama alivyokuwa Pamela. Wasichana wa aina hiyo hawakuwa wakipatikana kirahisi katika eneo kama Kinondoni Makaburini, wengi wao walipatikana katika makasino makubwa, tena wakilipwa kwa dola kuanzia mia moja kwenda juu.

Walipomaliza, wakatoka bafuni na kuelekea chumbani, huko, mzee yule aliyeonekana kuwa na uchu mkubwa alibaki akimwangalia Pamela, hakutaka kusikia kitu chochote kile, aliituliza akili yake ipasavyo na hata simu yake aliizima, hakutaka kupata usumbufu wowote.

Baada ya kuvua nguo zote, wakapanda kitandani, Pamela aligundua kwamba mzee yule alikuwa tajiri hivyo alipania kufanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha anamteka kimapenzi. Alijiandaa vilivyo mahali hapo lakini hata kabla hajafanya lolote lile, mzee yule akaanza kujishika koo yake na kuanza kukukuruka kitandani pale kama mtu aliyehitaji msaada hali iliyomfanya Pamela kushtuka.

“Nini tena?” aliuliza Pamela, mzee yule alibaki akijikunjakunja huku mikono yake ikiwa mdomoni.
“Give me Fluticasone,” (Nipe Fluticasane)
“What is that?” (Ni nini hicho?)
“I am dying, give me Fluticasone,” (Ninakufa, nipe Fluticasane) alisema mzee yule huku akionesha kidole chake katika droo ndogo iliyokuwa pembeni mwa kitanda.

Mpaka kufikia hatua hiyo Pamela alikuwa amechanganyikiwa, hakujua mzee huyo alikuwa akiumwa ugonjwa gani na hiyo Fluticasane kilikuwa kitu gani. Kwa kuwa yule mzee alionesha kidole katika droo ile ndogo, akaifungua na kuanza kuangalia ndani.

Alikutana na vitu vingi, kulikuwa na dola zaidi ya elfu tano, kamera, bastola, picha na vitu vingine vingi. Hakujua atoe kipi na aache kipi, alibaki akishangaa tu.
“Fluticasone ndiyo nini?” aliuliza Pamela lakini hata kabla hajajua nini cha kuchukua ndani ya droo ile, mzee yule akatulia kitandani, pumzi ikakata, akafariki dunia, Pamela akapata mshtuko.

Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 43

Alijijengea heshima kubwa nchini Tanzania kutokana na utendaji kazi wake mkubwa aliokuwa akiufanya katika jeshi la polisi nchini Tanzania. Kutokana na umahiri wake, akapandishwa vyeo na mwisho wa siku akajikuta akiwa Kamanda Mkuu Kanda ya Dar es Salaam, DCP.

Heshima yake inakuwa kubwa, kila anayemuona anamheshimu kutokana na utendaji wake mkubwa aliokuwa akiufanya. Pamoja na heshima zote hizo, mwanaume huyu aliyeitwa Dickson alikuwa mtu mwenye sura mbaya ambapo huko shuleni kipindi cha nyuma aliitwa kwa jina la Zinjathropus, yaani binadamu wa zamani.

Hakuwa na mchumba, hakuwa na mpenzi, alichokifanya ni kuanza kununua machangudoa. Alifanikiwa sana, alilala na wengi. Alipofika Dar es Salaam, akaendelea kulala nao ila kwa kila ambaye alimuona sura yake na kumgundua, alimuua, alitaka suala la kununua machangudoa liwe siri maisha yake yote.

Upande wa pili kuna mwanamke mrembo aitwaye Pamela, msichana huyu mwenye umbo matata amefika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi ya uchangudoa. Anapofika huko, kutokana na uzuri wake, anawapata wanaume wengi, anamtetemesha kila mtu, si wanaume tu, hata wanawake wenzake.

SONGA NAYO.

Pamela aliogopa, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya mahali pale, dawa ya Fluticasone aliyoambiwa aichukue hakuwa akiiona katika droo ile ya kitanda, alihisi kuchanganyikiwa mno. Kijasho chembamba kikaanza kumtoka, hakujua ni kitu gani cha ziada alichotakiwa kufanya.

Sekunde zilisonga mbele, alibaki akiendelea kupekuapekua ndani ya droo ile mpaka alipofanikiwa kukiona kikopo kimoja kidogo ambacho ndani yake kulikuwa na dawa, kikopo kile kiliandikwa Fluticasone, kutokana na maelezo yaliyoandikwa katika kikopo kile, ndipo alipogundua kwamba hiyo ilikuwa ni dawa ya pumu.

Wakati anamwangalia yule mzee kitandani, ndiyo alikuwa katika hatua ya mwisho kuvuta pumzi, dawa aliipata, hakujua namna ya kufungua kikopo kile, akabaki akihangaika kufanya hili na lile lakini kikopo hakikufunguka.
“Kinafunguliwa vipi kutoa dawa?” alijiuliza lakini hakupata jibu.

Wakati akijiuliza hayo, hali ya yule mzee iliendelea kuwa mbaya zaidi, hakuchukua muda mrefu, akatulia pale kitandani, pumzi ikakata na kufariki dunia. Wakati mzee huyo anakufa, Pamela hakuligundua hilo, aliendelea kuangalia namna ya kufungua kile kikopo, baadaye ndipo kumbukumbu ikamjia kwamba inawezekana zile dawa walizokuwa wakizitumia Wazungu kujipulizia mdomoni ndiyo ilikuwa kama ile.

Alipoangalia pembeni na kubonyeza kwa juu, akaona dawa ikitoka, hakutaka kuchelewa, hapohapo akamsogelea yule mzee kisha kumuweka tundu la lile kopo mdomoni mwake kisha kubonyeza kwa juu, dawa ikatoka lakini alikuwa amekwishachelewa kwani tayari alifariki dunia.

Hakuwa akimfahamu, siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza kumuona lakini kifo chake kilimuhuzunisha mno. Alibaki akimuita pale kitandani lakini yule mzee hakuweza kuamka. Pamela akaogopa, hakutaka kubaki mahali hapo, kitu alichokifikiria muda huo ni kukimbia tu.

“Siwezi kubaki,” alijisemea, hapohapo akavaa nguo zake harakaharaka na kuondoka mle chumbani, tena huku akikimbia, akafungua geti na kutokomea gizani, hata viatu alisahau kuvaa, alivishikilia mkononi.
* * * *
Kichwa cha Dickson kiliwaza mapenzi tu, hakufikiria kitu kingine mahali hapo, kwa kumwangalia msichana yule, alimtamani sana, hakuona kama kulikuwa na sababu ambazo zingemfanya kumuacha hivihivi.

Pepo la ngono alilokuwa nalo lilimuweka kwenye wakati mgumu, hakufikiria kitu kingine chochote kile zaidi ya kulala na mwanamke huyo tu. Njiani, humo ndani ya gari alikuwa akizungumza naye, alitaka kuona akizoeana kabla ya kuingia ndani.

Walichukua muda wa dakika ishirini ndipo walipofika nje ya nyumba moja ya wageni, wote wakateremka na kuanza kuelekea ndani. Muda wote huo Dickson alikuwa na kofia yake kichwani mwake, hakutaka kugundulika, hakukuwa na kitu alichokuwa akikihofia kama kugundulika kwani aliona kama hilo lingetokea ilikuwa ni lazima ashtakiwe hata kama alikuwa kiongozi mkubwa wa jeshi la polisi.

Wakaingia ndani, akalipia kisha kuelekea chumbani. Walipofika humo, akamlaza kitandani msichana yule na kuanza kumwangalia kwa matamanio. Hakutaka taa iwake, aliogopa kugundulika, alichokifanya ni kuifuata swichi na kuizima.
“Mbona unazima taa?” aliuliza mwanamke yule huku akionekana kuhamaki.
“Sasa si ninataka tuanze kufanya kilichotuleta humu ndani,” alijibu Dickson.

“Yaani tufanyie gizani?”
“Ndiyo! Kwani kuna ubaya?”
“Hapana! Kufanyia gizani siwezi,” alisema mwanamke yule huku akiinuka kitandani.
“Kwani kuna tatizo gani kufanyia gizani?”
“Raha ya chumbani tuonane, sasa giza la nini?” alisema mwanamke yule.
“Sasa kama mimi mteja nahitaji giza!”
“Hapana! Kwa giza siwezi kabisa.”

Wakati akiyasema maneno hayo, tayari yule mwanamke alikwishaifikia swichi iliyokuwa mle chumbani na kuiwasha. Dickson akashtuka, mwanga mkali ukampiga usoni mwake, kofia haikuwepo kichwani mwake, alikuwa amekwishaiweka pembeni tayari kwa kulala na mwanamke yule.

Alipoiwasha taa ile akarudi kitandani pasipo kumwangalia mteja wake, alipolala tu kitandani na kumwangalia mteja wake usoni, mwanamke yule akashtuka sana, mtu aliyesimama mbele yake alimfahamu vilivyo, alikuwa yuleyule mwanaume ambaye mara kwa mara alizungumza mbele ya waandishi wa habari akipinga sana wanawake kujiuza, yuleyule ambaye aliagiza machangudoa wote wakamatwe na wapigwe faini, alikuwa kamanda Dickson.
“Aaah! Kamanda Dick,” alisema mwanamke yule kwa kuhamaki.

Dickson akashtuka, hakuamini kama mwanamke yule alikuwa akimwangalia usoni, hakuwa na kofia wala miwani, alionekana kuchanganyikiwa mno.
Yule mwanamke akasimama kitandani kwa lengo la kuondoka, alipoanza kupiga hatua, Dickson akamshika mkono.
“Niachie niondoke,” alisema yule mwanamke.

“Kwenda wapi?”
Kumuacha hivihivi halikuwa jambo rahisi, hata kabla yule mwanamke hajafanya chochote akashtukia akipigwa kofi moja usoni, kofi lililompepesua na kujikuta akiangukia kitandani. Alichokifanya Dickson ni kumfumba mdomo wake kwa kutumia taulo lililokuwa kitandani na kuiziba pua yake.

Yule changudoa alibaki akikukuruka lakini Dickson hakumuacha, aliendelea kumziba mdomo na pua yake kwa lengo la kumuua tu. Hakukuwa na kingine alichotakiwa kufanya, kugundulika na yule mwanamke aliamini kwamba kungemletea matatizo makubwa hivyo ili kuficha kila kitu kilichokuwa kimetokea ilikuwa ni lazima amuue.
“Siku zote hakuna siri ya watu wawili, ni lazima ufe kama wenzako,” alisema Dickson.

Mwanamke yule akatulia kitandani, shuka lilikunjikakunjika, mwili wake ulivimba, Dickson akaelekea bafuni, akalilowesha maji lile taulo kisha kuurudia mwili wa yule mwanamke na kuanza kufuta sehemu zote ambazo vidole vyake vilitumika kumgusa. Alipomaliza, akatoka nje.
“Hapo nje si kuna chipsi?” alimuuliza dada wa mapokezi.

“Ndiyo!”
“Oke! Ngoja nikanunue kwanza, nakuja,” alisema Dickson, dada yule akakubaliana naye, akatoka nje na kulifuata gari lake, kilichosikika baada ya hapo ni muungurumo wa gari lililoanza kuondoka mahali hapo.

Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 44

Alijijengea heshima kubwa nchini Tanzania kutokana na utendaji kazi wake mkubwa aliokuwa akiufanya katika jeshi la polisi nchini Tanzania. Kutokana na umahiri wake, akajikuta akipandishwa vyeo na mwisho wa siku akijikuta akiwa Kamanda Mkuu Kanda ya Dar es Salaam, DCP.

Heshima yake inakuwa kubwa, kila anayemuona anamheshimu kutokana na utendaji wake mkubwa aliokuwa akiufanya. Pamoja na heshima zote hizo, mwanaume huyu aliyeitwa Dickson alikuwa mtu mwenye sura mbaya ambapo huko shuleni kipindi cha nyuma aliitwa kwa jina la Zinjathropus, yaani binadamu wa zamani.

Hakuwa na mchumba, hakuwa na mpenzi, alichokifanya ni kuanza kununua machangudoa. Alifanikiwa sana, alilala na wengi. Alipofika Dar es Salaam, akaendelea kulala nao ila kwa kila ambaye alimuona sura yake na kumgundua, alimuua, alitaka suala la kununua machangudoa liwe siri maisha yake yote.

Upande wa pili kuna mwanamke mrembo aitwaye Pamela, msichana huyu mwenye umbo matata amefika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi ya uchangudoa. Anapofika huko, kutokana na uzuri wake, anawapata wanaume wengi, anamtetemesha kila mtu, si wanaume tu, hata wanawake wenzake.

SONGA NAYO...

Taarifa zikaanza kusambaa Upanga kwamba kulikuwa na mwanaume aliyekuwa amekufa chumbani kwake. Kila mtu aliyezisikia taarifa hizo alishtuka, walimfahamu mzee huyo, alikuwa mzee mpole, aliyeheshimika ambaye alisumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu.

Watu walihuzunika mno, wengi walisema kwamba pumu ndiyo iliyokuwa imemuua mzee huyo lakini baadhi ya watu wakaibuka na kusema kwamba mzee huyo alikuwa ameuawa. Hakukuwa na aliyejua ukweli halisi wa kifo chake.

Polisi walipoingia ndani ya chumba chake waliukuta mwili wake ukiwa kitandani, alikuwa ameishika shingo yake na pembeni kulikuwa na dawa yake iliyokuwa kwenye kichupa, dawa iitwayo Fluticasone ambayo ilikuwa maalum kwa wagonjwa wa pumu.

Pamoja na kukuta hali halisi ndani ya chumba hicho, hali iliyoonesha kwamba mzee huyo alikuwa amekufa lakini bado baadhi ya watu waliendelea kung’ang’ania kwamba mzee huyo alikuwa ameuawa jambo lililowafanya polisi kuanza kuhoji.

“Mnasema ameuawa?” aliuliza polisi mmoja, alikuwa mbele ya vijana wanne.

“Siyo sisi, ni walinzi wa maeneo haya,” alijibu kijana mmoja huku akionekana kuwa na wasiwasi.

“Walinzi gani?”

“Wa nyumba zile kule,” alijibu kijana mwingine huku akizinyooshea kidole nyumba mbili.

Polisi huyo hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuelekea kule kijana yule aliponyoosha kidole, alipoifikia nyumba moja miongoni mwa nyumba zile mbili, akapiga hodi ambapo mlinzi akaufungua mlango na macho yake kukutana na macho ya polisi.

“Kwa nini unasema kwamba mzee Ibrahim ameuawa?” aliuliza polisi yule mara baada ya salamu.

“Jana alikuja usiku kama saa nane hivi mzee Ibrahim alifika nyumbani kwake hapa na kuliingiza gari lake ndani ya ngome ya nyumba yake. Sikujua alikuwa na nani kwa sababu gari lake lilikuwa na vioo vyeusi,” alijibu mlinzi huyo kwa kirefu.

“Ikawaje?”

“Baada kama ya saa moja hivi, nikamuona msichana mmoja akitoka huku akikimbia, kilichotokea ndani, sikukijua na hata wenzangu hawakujua pia,” alisema mlinzi yule.

Maelezo ya mlinzi yalikuwa muhimu kwani yule polisi aliamini kwamba yangeweza kufanikisha kukamatwa kwa muuaji huyo, alichokifanya ni kumchukua na kutangulizana naye kituoni kwa sababu ya kutoa maelezo zaidi.

* * *

Ukiachana na taarifa za kufariki kwa tajiri aliyekuwa akiishi Upaga, pia kukawa na taarifa zingine za mwanamke aliyeuawa ndani ya nyumba moja ya wageni iliyokuwa Mwananyamala. Polisi waliosikia tetesi hizo hawakubaki kituoni, wakaelekea mpaka katika nyumba hiyo ya wageni kwa ajili ya kushuhudia kilichokuwa kimetokea.

Umati wa watu uliokuwa nje ya nyumba hiyo ya wageni uliwapa uhakika kwamba kile walichokuwa wamekisikia kilikuwa kweli kabisa, wakateremka kutoka garini na kuelekea ndani huku wakiwa na bunduki zao mikononi.

Msichana mrembo wa sura, aliyekuwa na umbo la kuvutia alikuwa kimya kitandani. Mapovu yalikuwa yamemtoka mdomoni, shuka lilikuwa limechafuliwa kwa haja kubwa iliyokuwa imemtoka mara baada ya kunyongwa na muuaji.

Kila polisi aliyemwangalia msichana yule, alimkumbuka yule msichana Fatuma aliyenyongwa bafuni alipokuwa akioga. Watu wa kwanza waliotiwa hatihani walikuwa vijana waliokuwa chumbani wakivuta bangi, walichokisema ni kwamba aliyemuua Fatuma alikuwa mwanaume aliyevalia kofia kubwa kichwani.

Haikuwa hiyo tu, hata alipouawa msichana mmoja porini na mzee aliyeshuhudia tukio lile kusema kwamba mtu aliyefanya mauaji alikuwa amevalia kofia kubwa kichwani, iliwapa uhakika kwamba mtu huyo ndiye aliyehusika katika mauaji ya watu hao wawili.

Leo hii kulikuwa na mtu mwingine aliyeuawa, alikuwa msichana mrembo ambapo kwa maelezo ya dada wa mapokezi alisema kwamba msichana huyo alikuwa akijiuza na alikuja katika nyumba hiyo ya wageni na mteja wake, kilichotokea, baadaye yule mwanaume akatoweka, hata sura hakuwa ameiona.

“Kwa nini? Kwa sababu ya giza?”

“Hapana! Alikuwa amevaa kofia,” alijibu msichana huyo.

Polisi wakachanganyikiwa, mtu mmoja mwenye utambulisho wa kuvaa kofia alikuwa amefanya mauaji ya watu watatu kwa nyakati tofauti, polisi wakaanza kujiuliza juu ya mtu huyo kufanya mauaji hayo lakini hakukuwa na yeyote aliyefahamu.

Wapo waliohisi kwamba muuaji alitumwa na mganga kuua ili kupata utajiri lakini kitu kilichowafanya kuyapuuzia mawazo hayo ni kwamba miili ya watu hao ilikutwa na viungo vyote, hakukuwa na kiungo kilichonyofolewa.

Taarifa zikapelekwa kwa DCP Dickson, alichokifanya ni kuwaita polisi wawili waliokuwa katika kitengo cha upelelezi na kuanza kuwauliza juu ya kile kilichotokea katika upelelezi wao.

“Kuna mtu anavaa kofia, huyo ndiye anayeua,” alisema polisi mmoja.

“Yaani ishu ya kuvaa kofia mmeiona kuwa sababu kubwa? Wangapi wanavaa kofia? Yaani badala ya kuja na kuniambia kwamba muuaji ni fulani, mnakuja hapa na kuniambia muuaji anavaa kofia, kweli mnaweza kuniletea taarifa ya kijinga namna hii?” aliuliza Dickson huku akijifanya kuwa na hasira.

“Tutafanya kazi kwa juhudi mkuu! Mpaka atakapopatikana,” alisema polisi mmoja.

“Acheni uvivu, fanyeni kazi kama watu wanaotaka kufanya kazi, siyo mnakuja hapa na kuniambia mambo ya kofia,” alisema Dickson.

“Sawa mkuu! Tutafanya hivyo,” alisema polisi mmoja kisha wote kwa pamoja kupiga saluti kama heshima, baada ya hapo wakaondoka.

Dickson akarudi ofisini na kutulia kitini, uso wake ulijawa na tabasamu pana lakini kwa mbali alionekana kuwa na hofu mno. Alihisi kama angeweza kukamatwa kwani staili ya kofia aliyokuwa akiivaa ingemponza.

“Ni lazima nitoke kivingine, siwezi kukamatwa kirahisi,” alisema Dickson huku akijipanga usiku wa siku hiyo atoke na kwenda kuonana na msichana mwingine maeneo ya Kinondoni Makaburini. Alitaka soko lake lihamie huko, hivyo akajipanga.

Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 45

Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.

Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta kwenye wakati mgumu mara baada ya kumnunua changudoa, walipokuwa hotelini na kugundulika na changudoa yule kwamba ni yeye, anaamua kumuua na mwili kwenda kuuzika porini. Wakati anauzika, kulikuwa na mzee ambaye aliona kila kinachoendelea.

Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

Uzuri wake uliendelea kuwa gumzo, machangudoa wengine waliogopa kwa kuwa kila alipokuwa, hakukuwa na biashara nzuri kwa upande wao. Kila mteja ambaye alifika mahali hapo na kumuona Pamela, hakutaka kumuacha, alimfuata na kumnunua kisha kuondoka naye au wakati mwingine kumaliza shida zake katikati ya makaburi.

Machangudoa wengi walimuonea wivu na wengine kumkasirikia, ili biashara zao ziende kama inavyotakiwa ilikuwa ni lazima Pamela aondoke mahali hapo kwani uwepo wake uliwaletea shida sana.

Baadhi ya machangudoa wakakutana na kuanza kumjadili kwamba ilikuwa ni vizuri kumfukuza au wamuache. Katika kushauriana huko, wengine wakaona ilikuwa ni lazima aendelee kubaki kwani kwa wakati huo Pamela alikuwa kivutio, wanaume wengi walifika na walipomkosa, waliwachukua machangudoa wengine.

Maisha yaliendelea kila siku, thamani yake ikaanza kupanda, akawa msichana mwenye bahati, alitengeneza kiasi kikubwa cha fedha mpaka pale alipokuja kukutana na mwanaume aliyemfuata huku akiwa na kofia kubwa kichwani, mteja aliyekuwa na muonekano wenye fedha ambaye kwake alijitambulisha kama muuzaji wa nafaka kutoka vijijini aliyejiita kwa jina la Mandingo.

“Mandingo!” alisema kwa mshangao.

“Ndiyo! Mimi ni Mkurya, huwa nasafirisha nafaka kutoka huko vijijini kuja huku mjini,” alisema mwanaume huyo.

“Aisee! Kumbe nipo na bosi!”

“Yeah! Nipo hapa kwa ajili ya kutumbua hela, zinaniwasha sana. Kwanza gharama yako inakwendaje?” aliuliza mwanaume huyo.

“Kwa sababu wewe ni mfanyabiashara mkubwa, mwenye fedha, nitakufanyia laki mbili kwa usiku mmoja,” alisema Pamela.

“Mmmh! Hakuna tatizo, kwa ajili yako, kwa jinsi ulivyo, nipo tayari,” alisema mwanaume huyo.

Huyo hakuwa mfanyabiashara kama alivyojitambulisha, alikuwa Dickson ambaye aliamua kubadilisha kiwanja cha kuchukua machangudoa na kuhamia Kinondoni Makaburini. Alipomuona Pamela kwa mara ya kwanza, moyo wake ukafarijika, alifurahia moyoni mwake kwani kwa kipindi kirefu alichokitumia kununua machangudoa, hakuwahi kukutana na changudoa aliyekuwa na umbo zuri, sura nzuri kama alivyokuwa Pamela.

Staili yake ilikuwa ileile, hakutaka kujulikana, kichwani alikuwa na kofia kubwa ya Marlboro huku kukiwa na mwanga hafifu ambao hata ulipompiga usoni, hakuonekana vizuri.

“Unaishi wapi?’ aliuliza Pamela.

“Naishi Msasani, ila hatutoweza kwenda nyumbani,” alijibu Dickson.

“Kwa hiyo tutafanyia wapi? Garini?”

“Hapana. Tutakwenda kuchukua chumba katika gesti moja uswahilini.”

“Mmmh!”

“Nini sasa?”

“Umejisifia mfanyabiashara mkubwa, halafu tuchukue gesti! Kweli jamani baby? Kwa nini tusichukue hoteli kabisa?” aliuliza Pamela huku akionekana kushtuka kwa mbali.

“Hahaha! Si unajua sisi wengine watu maarufu Tanzania, tukionekana, siyo poa kabisa,” alijitetea Dickson.

“Basi sawa. Cha msingi hela tu,” alisema Pamela.

Hakukuwa na muda wa kupoteza tena mahali hapo, alichokifanya Dickson ni kuliondoa gari mahali hapo na kuelekea katika gesti moja iliyokuwa Manzese Midizini. Hakutaka kwenda katika hoteli kubwa kwa kuwa alijua fika kwamba kugundulika ilikuwa rahisi sana tofauti na gesti bubu za mitaani.

Huko, aliamini kwamba hakukuwa na ulinzi wa kutosha, wahudumu hawakuwa na umakini wowote ule kwa wageni waliokuwa wakiingia, zaidi, wao waliangalia fedha tu. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kutokugundulika katika kila gesti aliyokwenda kule Mwananyamala.

Garini alikuwa mzungumzaji mkubwa, alitaka kuzoeleka kwa msichana huyo ili hata watakapofika chumbani kusiwe na maswali mengi. Hapohapo garini ndipo Dickson alipomwambia Pamela kwamba hakukuwa na kitu alichokichukia kama kufanya mapenzi katika chumba kilichokuwa na mwanga mkali wa taa.

“Kwa nini?”

“Basi tu, unajua sisi wengine tunakuwa na aibu kubwa sana.”

“MmmH! Kweli makubwa, halafu si kwako tu, mpo wengi wa namna hiyo, sijui huwa mnaogopa nini,” alisema Pamela.

Maneno hayo yakawa ahueni kwa Dickson, alijiona kuwa mshindi, kitendo cha Pamela kumwambia kwamba yeye hakuwa mmoja wake akawa na uhakika kwamba iwe isiwe ilikuwa ni lazima kuzima taa ya chumbani na hatimaye kufanya mapenzi kama alivyokuwa amepanga.

Hakuwa na hofu tena, alijua jinsi ya kucheza na wanawake hao, kuua, wala hakuogopa, alitaka kuona mambo yake yote yanakwenda sawa kama inavyotakiwa hivyo kunapotokea kizuizi chochote cha kuitunza siri ile, hakuhofia kuua hata kidogo.

Waliendelea na safari mpaka walipofika katika gesti hiyo iliyokuwa Manzese Midizini, tena kwa kuingia ndani kabisa. Walipofika, akasimamisha gari na kisha kuteremka. Katika kipindi chote hicho alihakikisha kofia yake haitoki kichwani mwake.

Vijana waliokuwa wamekaa pembeni mwa gesti hiyo walibaki wakimwangalia Pamela ambaye alikuwa akipiga hatua kuelekea ndani ya jengo hilo na Dickson ambaye hawakuwa wamemtambua kabisa.

Umbo lake liliwaacha midomo wazi, hawakuamini kama kulikuwa na mwanamke aliyekamilika kama alivyokuwa Pamela. Sura nzuri na yenye mvuto, umbo namba nane, hipsi kubwa ambazo vijana wa mitaani walipenda kuziita kwa jina la pisto.

“Nahitaji chumba.”

“Vipo. Show time au mpaka asubuhi?” aliuliza dada wa mapokezi.

“Mpaka asubuhi.”

“Elfu sita.”

“Hakuna tatizo,” aliitikia Dickson, akalipia, wakapewa ufunguo na kuelekea huko chumbani. Wakati Pamela akifikiria fedha, hakujua kama alikuwa katika mikono ya mtu muuaji. Endapo angejua, asingekubali kuelekea gesti na mwanaume huyo.

Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 46

Hali ya sintofahamu inazuka jijiniDar es Salaam kufuatia kupoteamfululizo kwa machangudoa katikamazingira ya kutatanisha.Taharuki kubwa inazuka kwanindani ya kipindi kifupi tu, zaidi yamachangudoa kumi na mojawanapotea na hakuna anayejuawalikopotelea.Jambo hilo linasababisha jeshi lapolisi kuingilia kati. Kinachozidikuzua utata, wote wanapoteakatika mazingira yanayofanana.Mwanaume mmoja asiyejulikana,aliyekuwa anatembelea gari lakifahari aina ya Volkswagen,aliyekuwa akienda eneo hilo usikuwa manane ndiye anayehusishwana wote wanaopotea. Upande wa pili, kijana aliyekuwana mwonekano tofauti nabinadamu wa kawaida, DicksonMaduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania,amejiunga na Chuo Kikuu cha Dares Salaam.

Hisia kali za mapenzizinasababisha kijana huyo aanzekutoka usiku na kwenda kutafutamachangudoa. Hivyo baadayeanahamishiwa Dar es Salaam.Mara baada ya kufanikiwa kuwaDCP, Dickson anajikuta akinogewana penzi la changudoa mmojaaitwaye Pamela, umbo lake, ngozivinamchanganya na kujikutaakianza kumganda pasipo kujuakwamba ukaribu wake namsichana huyo ungewezakubadilisha kila kitu.Je, ninikitafuatia? SONGA NAYO…Huo ulikuwa mwanzo wa ukaribubaina ya Dickson na changudoaPamela. Msichana huyo mremboambaye alivutia kilaalipomwangalia aliliteka penzi laDickson kiasi kwamba hataalipokuwa ofisini, hakuwa akifikiriakitu chochote kile zaidi ya penzi lamsichana huyo mwenye umbolenye mvuto.

Siku zikaendelea kukatika,hakukuwa na muda wa kutulia, saambili ofisini pasipo Pamelazilionekana kuwa nyingi, wakatimwingine alihakikisha anafanyakazi zake haraka iwezekanavyokisha kurudi nyumbani ambapoalimpigia simu Pamela na kujanyumbani kwake. Wivu ukamjaa moyoni, wakatimwingine alimlazimisha msichanahuyo alale nyumbani kwake kwanikila alipokuwa naye mbali, alihisimsichana huyo kulala nawanaume wengine kitukilichouumiza mno moyo wake,kwa jinsi alivyokuwa na mapenzimazito kwa Pamela, kuna kipindialisahau kabisa kwamba msichanahuyo alikuwa changudoa tuambaye alilala na mwanaumeyeyote aliyekuwa na pesa.“Vipi tena?” aliuliza Pamela, ilikuwa mchana wa saa saba, alipigiwa simu na Dickson, haikuwa kawaida kitu hichokutokea.“Upo wapi?”“Nipo nyumbani, kuna ninimpenzi?” aliuliza Pamela.“Unaweza kuja mara moja?”“Wapi?”“Nyumbani kwangu.”“Kwani haupo kazini?”“Haujanijibu swali langu, unawezakuja?”“Naweza. Ila kuna nini?”“Wewe njoo, wala usiogope,”alisema Dickson na simu kukatwa.Kichwa chake kilichanganyikiwamno, alichokitaka mahali hapo nikumuona msichana huyo tu kwanihakukuwa na kitu alichokuwaakipenda kama kuwa karibu naPamela.

Hakutaka kuendelea kukaa ofisini, alichokifanya ni kuondoka nakurudi nyumbani haraka ambapowala hazikupita dakika nyingi,Pamela akafika, moja kwa mojaakampeleka chumbani na kulalanaye, hata kazi aliamua kuachananayo kwa siku hiyo kwani penzi laPamela lilimchanganya.****Magreth alibadilisha ratiba yake,kila siku akawa mtu wa kutembeakatika viwanja mbalimbali vyamachangudoa huku lengo lakelikiwa ni kuona kama angefanikiwakumpata mteja wake aliyemkimbiakatika kipindi alichomhitaji sana.Alizunguka na kuzunguka, tenawiki nzima mpaka alipofanikiwakupata taarifa ambazo aliaminikwamba mtu aliyekuwaakizungumziwa alikuwa huyohuyoaliyekuwa akimhitaji.“Umesema ana BMW nyeusi?”aliuliza changudoa mmoja.“Ndiyo! Unamfahamu?”“Kwa kweli sijawahi kumuona, ilahuyo mteja anafika sana hapakiwanjani,” alijibu changudoahuyo.“Nitampata vipi?”“Kwani ni nani kwako? Mumeo?”“Hapana! Ila ninataka kuonananaye,” alisema changudoa huyo.

Jibu pekee alilopewa ni kwambaisingewezekana kuonana na mtejahuyo kwani siku hizo hakuwaakifika sana kutokana na kulipatapenzi la kudumu kutoka kwamsichana mrembo aliyetokeaArusha, Pamela.Kitu alichokitaka Magreth nikuonana na huyo Pamela kwakuamini kwamba angepata taarifanyingi juu ya mwanaume huyo nahata ikiwezekana kupafahamukwake kwani hakukuwa na mtejaambaye alimpa fedha nyingi kamamwanaume huyo ambaye mpakakatika kipindi hicho hakujuaalikuwa na sura gani.

Alipofanikiwa kuonana na Pamela,akajaribu kutengeneza urafiki naye,akaanza kumzoea, kila sikumchana akawa mtu wa kwendakumtembelea, kwa kuwa Pamelahakuwa na marafiki wengi na piahakuwa amelizoea sana jiji,akaupokea urafiki wa Magrethpasipo kujua msichana huyoalihitaji nini.Mpaka siku ambayo Dicksonalimpigia Pamela simu na kumuitanyumbani, Magreth alikuwapamoja naye chumbani,alichokifanya ni kumuaga kwalengo la kwenda huko.“Ndiyo unakwenda kuonana naye?”aliuliza Magreth.“Ndiyo! Unataka twende wote?”aliuliza Pamela huku akionekanadhahiri kwamba alikuwa akitania.“Hahah! Kama inawezekana!Kwani hawezi kulala na wanawakewawili?” aliuliza Magreth, nayemwenyewe alionesha kutania.

Pamela hakujibu swali hilo zaidiya kucheka kisha kuondokanyumbani hapo. Kwa Magrethalionekana kuwa na uhakikakwamba mwanaume huyo ambayePamela alikwenda kuonana nayendiye yule ambaye alifika sanakatika kiwanja chake, Sinza Morina kumnunua, lakini ghaflaakapotea na hakurudi tena.“Atakuwa ndiye yeye tu, ni lazimanimtafute, nipajue kwake nakumrudisha mikononi mwangu,”alisema Magreth pasipo kujua mtuhuyo alikuwa nani.

Je, nini kitafuatia?
 
Back
Top Bottom