Hadithi hadithi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hadithi hadithi

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Viol, Oct 7, 2012.

 1. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Hapo zamani za kale fisi walikuwa wanakaanga karanga zao,walipomaliza kukaanga sungura akaiba karanga zote,walipogundua sungura ameiba wakamfungia ndani ya nyumba,wakamkamata,wakamfungia ndani ya gunia,halafu wakamwacha fisi mmoja wengine wakaenda kutafuta fimbo zao ili wakirudi wamtandike sugura akiwa ndani ya gunia,walipondoka sungura akaanza kumdanganya yule aliyeachwa amlinde....akamwambia huku ndani ya gunia nakula nyama,njoo chukua nyama fungua gunia,akafungua gunia na kuingia ndani halafu sungura akaponyoka na kumfungia fisi ndani ya gunia,wale walioenda kuchukua fimbo waliporudi wakaanza kumpiga mwenzao wakidhani ndo sungura yupo ndani ya gunia,yule wa ndani ya gunia akaanza kulia....""jamani mi mwenzenu,jamani mi mwenzenu"...wao wakawa wanaambizana "we umekuwa mwenzetu tangu lini?acha ujanja wako".Walipofungua gunia wakakuta kweli ni fisi mwenzao halafu wamemwua,hasira zikawapanda...
  halafu kumbe sungura alikuwa juu ya mti akawacheka,..""hahahahahaha hahaha,wajinga waliomwua mwenzao,fisi wote wakauzunguka mti kwa hasira,ili wamkamate sungura akishuka...Wakamwambia shuka chini.
  Sungura akawaambia kama mnataka kushuka basi kusanyeni mchanga chini ya mti,,wakakusanya mchanga.
  Akawaambia nashuka sasa,fungueni macho yenu vizuri nisiwatoroke,wakaangalia vizuri,sungura akaruka juu ya
  Mchanga na kuwatupia mchanga machoni halafu akatoroka.
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Hadithi yako imetufundisha nini?
   
 3. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,182
  Likes Received: 10,534
  Trophy Points: 280
  Singura akaishi kwa raha mustarehe...
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  tuwe wajanja kama sungura
   
 5. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Hao fisi watakuwa wana Magamba bila shaka.
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mbona hii hadithi inafanana na Watanzania na viongozi wa ccm?
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ccm wanatuibia tukiwashukia wanatutandika risasi tunafyata mikia.mafisi ni Watanzania na Sungura ni magamba,
   
 8. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Nimejikuta nacheka mwanzo mpaka mwisho wa hadithi..
   
 9. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2013
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Dalili ya ambaye hakupendi utajua tu
   
 10. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2013
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  tangu post ya mwaka jana nimeona leo comment yako nimekuta nacheka,teh teh,hujakosea kabisa
   
 11. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #11
  Oct 22, 2013
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  Wapenda hadithi eeeeh za sungura na fisi
   
 12. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2013
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  santeeee kwa hadithi yako
  Nalog off
   
 13. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2013
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  napenda sana aisee,kama unayo nihadithie basi
   
 14. Bufa

  Bufa JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2013
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 4,182
  Likes Received: 3,406
  Trophy Points: 280
  Hahahah
   
Loading...