Habari Zenu Waungwana

matembele

JF-Expert Member
Nov 4, 2009
322
188
Na mie nimejitutumua kujumuika nanyi kimawazo, kujifunza na kufundisha mtandaoni. Natumai kuna mengi na wengi tutakao afikiana na kutoafikiana, ila kadri ya itavyokua tuweke mbele uungwana.

Matembele
 
Karibu sana Matembele jisikie upo nyumbani, mawazo yako ni muhimu sana hapa JF.

NB. Hilo jina lako kama ni mboga fulani hivi ya majani.
 
Karibu mkubwa,unajua nini hilo jina lako limenikumbusha nyumbani,sie kwetu tunaita ntolilo.Kwa ninavyoyafahamu matembele ujio wako naamini utakuwa na manufaa makubwa sana kwetu.Karibu tuelimishane.
 
Karibu mkubwa,unajua nini hilo jina lako limenikumbusha nyumbani,sie kwetu tunaita ntolilo.Kwa ninavyoyafahamu matembele ujio wako naamini utakuwa na manufaa makubwa sana kwetu.Karibu tuelimishane.

duh jamani watu wanavisa...jina linakukumbusha home, nadhani we ulikuwa na njaa!!!!
 
Dah! Ili jina la matembele, nasikia wajawazito wengi wanaipenda sana mboga hii, kwa kukolea ugwadu na chumvi!

Karibu Matembele.
 
duh jamani watu wanavisa...jina linakukumbusha home, nadhani we ulikuwa na njaa!!!!

No sio njaa mkuu,unajua huku niliko tangu nimefika sijala ugali.Sasa si unajua ugali kwa matembele mkubwa,acha hiyo habari.Sasa nilipoona hili jina la huyu mkurugenzi,kwa kweli kahamu ka ugali kakaongezeka.
 
Back
Top Bottom