Aibu iliyoje na si kawaida kwa injinia kuwa mzushi.Kwa vile maandiko yako hayana ushahidi wowote isipokuwa kutoelewana kwako na Mwakyembe , basi hayo maneno yanalingana na haiba yako.MZUSHI
Lole,
Wenzako walisema hivyo hivyo huko nyuma nilipoandika mambo ya CCM kupigana ngumi, Mwakyembe kubanwa na CCM- Kyela. Sasa na wewe leo unaniita Mzushi, ni sawa.
Kwa kukushauri tu tafuta simu za viongozi wa wilaya ya Kyela waulizie kuhusu hiyo KDF. Au mwulize Mwakyembe mwenyewe kuhusu hiyo KDF yake.
Pia uliza mtu yeyote Kyela, wakati Mwakyembe anafungua tawi la CCM wiki mbili zilizopita alisema nini?
Mimi nimemaliza kazi yangu ya kutoa habari, kama ni uzushi basi utupe nje.
Nakerwa sana na hoja hizi za kipuuzi za kuwashambulia wapiganaji hodari. Natambua kwamba mafisadi wanataka kutumia hili suala la ajali ya Mwakyembe kumtia doa mpiganaji huyu. Hawa ni wale wale ambao wamekuwa wakimuandama Mengi kwa kutumia mamluki wao kwenye vyombo vya dola na vijigazeti vingi walivyovianzisha kwa lengo hilo hilo.
Ili tufikie ukombozi wa kweli wa taifa letu lazima wote tuwaunge mkono walio frontline katika mapambano dhidi ya ufisadi na tusiwakatishe tamaa kwa kuwatungia mambo ya ajabu ajabu kwa lengo la ku-lower credibility yao. Hoja hizo hapo juu ni za kupikwa kwani hazina usahihi wowote. Mambo yaliyo wazi yanapotoshwa makusudi. Kuweni macho, hiyo ndiyo sura halisi ya ufisadi nchini iliyopelekea kwenye 'state capture' kama zilivyoonya zile asasi 50 zisizo za kiserikali.
Kwa wapiganaji walio ndani ya CCM ushauri wangu ni kwamba wajitoe haraka, kama kweli wana uchungu na nchi yao, wakae pamoja na kuanzisha upinzani wa nguvu dhidi ya CCM. Nina uhakika asilimia zaidi ya 60 ya wananchi watawaunga mkono baada ya kufanya kampeni nchi nzima. Hiyo ndio njia pekee ya kuking'oa chama cha mafisadi. Na kama alivyotabiri Nyerere, "Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM yenyewe". Andiko lakaribia kutimia! Sioni sababu kwa nini watu kama Mwakyembe, Zambi, Mpendazoe, na wengine waendelee kubaki CCM.
Engineer
Asante kwa analaysis yako, ila ninaomba ushauri , kwa uzoefu wako wa siasa za Kyela una dhani ni nani atafaa zaidi ya Mwakyembe, Kuiwakilisha Kyela. Because is good to start thinking of someone who will have credibility than Mwakyembe and I believe you can help us on that, naomba uje na few names tuwajadili na tuwafanyie vetting .
Leokweli
Pia (Mwakyembe)aache kuwa na wapambe wale wa Dar ambao kila mtu anajua ni mafisadi. Wewe unapigana na ufisadi huku unashinda na akina Kifukwe ambaye hata wananchi wa kawaida vijijini wanajua ni fisadi.
Engineer ninachopinga juu ya mawazo yako ni hizi sweeping statements ambozo mtu ambaye hayuko informed anatafikiri kuwa kuna ukweli ndani yake.Hivi unaweza kutueleza ufisadi wa Kifukwe?
Mkuu Lole,Engineer ninachopinga juu ya mawazo yako ni hizi sweeping statements ambozo mtu ambaye hayuko informed anatafikiri kuwa kuna ukweli ndani yake.Hivi unaweza kutueleza ufisadi wa Kifukwe?
Engineer,Lole,
Inaelekea hujui lolote na afadhali ukae kimya tu. Kama unataka ufisadi wa Kifukwe wala hutakiwi kwenda mbali, hapa JF kwa juu kuna search button, weka jina la Kifukwe na utajionea mwenyewe. Unajua ameondokaje Norconsult?
Ukishindwa tuambie na tutakutafunia kabisa, JF tuko mbele, ukipata jibu usisahau kuja kutuambia.
Next Level uko makini, maana inaonekana kuna nguvu moja kubwa sana inahangaika kumwangusha Dk Mwakyembe nina mashaka hata JK huenda nae yumo! Lakini wanakosea wanafanya haraka mno kumuandama ilitakiwa wasubiri tena wawe kimyaa kabisa labda hata baada ya miaka 5 hivi ndiyo wafanye huo uovu wao.
Lakini sasa hivi tunashtuka,....bado hakuna kosa lolote alilonalo Mwakyembe ukilinganisha na makosa ya mafisadi kama Rostam linaloweza kumfanya apungue credibility yake.
Ni kweli mafisadi wako smart kwenye kushughulikia maadui zao kwani pia huwa shirikisha UWT, lakini wanafanya makosa ya wazi kwenye plan zao ovu, wenye uwezo wa kufikiri tunawashtukia mapema tu.
Engineer,
Kifukwe ninayemfahamu mie ni mtu aliyesaidia sana wananchi wenziwe kwa hali na mali tofauti na mafisadi wanaojilimbikizia mali kwa kuwanyonya wananchi na kiukamua nchi kwa faida yao bila kujali wananchi wenzao.
Engineer,
Kama Kifukwe ni fisadi, jambo ambalo wala si kweli, unataka hata ndugu zake wamkimbie wasiongee wala kuwa karibu naye kwa kuwa wewe na wengine mnaamini kuwa ni fisadi? Unaweza kuulinganisha huo unaoitwa 'ufisadi' wa Kifukwe na ufisadi wa EPA?
Kifukwe ninayemfahamu mie ni mtu aliyesaidia sana wananchi wenziwe kwa hali na mali tofauti na mafisadi wanaojilimbikizia mali kwa kuwanyonya wananchi na kiukamua nchi kwa faida yao bila kujali wananchi wenzao.
Mtake msitake, Mwakyembe ni mpiganaji anayestahili pongezi za wananchi wote wapenda haki. Watanzania tuache 'wivu' wa kuwashupalia wenzetu wanaojitolea na kuhatarisha maisha yao kwa kujaribu kutetea maslahi ya wananchi na taifa letu kwa ujumla.
Mzzi (Boramaisha),
Naona wewe ni mgeni. Ukienda kurasa za nyuma, huko tumeandika vya kutosha. Na kwa taarifa yako, Mafisadi bado hawajaanza kumshambulia Mkwanyembe. Jamaa siku wataanza, basi utasikia Mwakyembe akianza kumumunya maneno.
Humu wengi tunaoandika ni wale tunamtakia mema kwa kujua uwezo wake na kwamba kama akijirekebisha, anauwezo wa kufanya maajabu na hata kuwa mfano wa kuigwa. Tulisema hapa zamani sana (soma nyuma) kuwa anagawa watu, na watu kibao wakasema tunamajungu. Juzujuzi kaambiwa live na akaambiwa aache kugawa watu. Kwa nini hakusikiliza maelezo yetu na kubadili hiyo tabia hadi anakuja kuumbulika? Kasababisha hadi mwenzake katandikwa masumbwi.
Karibu sana ukumbini na jitahidi usome hii makala kuanzia mwanzo hadi hapa ndipo uanze utowe maoni yako maana vinginevyo, unaongea/kuuliza kile ambacho huko nyuma tumekieleza.
Dilunga,
Achana na Lowassa. He conveniently disappeared alipopewa taarifa ya kuhojiwa na leo anajidai kuwa victim. Hapana. Kama ni victim, mbona alijiuzulu? Angetumia muda wake bungeni kujibu shutuma lakini alikacha? Achana naye!
Mkuu Shalom,
"Mtu wa watu" kwi kwi kwi!! nimeipenda hii na nitaiweka kwenye manifesto yangu ya kugombea ubalozi wa mtaa hapa kijijini kwangu.
Mwenye wivu si ni yule anayekwamisha vijana wa Kyela wasiendelee? Mtu akiona vijana wanafanya kweli kiroho kinaanza kumpanda? Utamwonea wivu mtu anayeshindwa ku deliver ili iweje?
Mkuu nimekwambia tafuta sababu nyingine lakini huko kwenye majivuno au wivu hutanikuta. Kama Wanyika mmejaaa majivuno huku mnashindwa kufanya la maana kule kwenu mtakuwa wajinga kweli kweli.
Elimu ya kweli ni ile inayokusaidia kutatua matatizo yanayokuzunguka, sio ile ya kutamba mitaani na kutundika vyeti ofisini.
Elimu nzuri ni kama Dr. aliyoitumia kule kwenye Richmond, wala hakuhitaji kutamba, ile report ilikuwa inajiuza yenyewe.
Shalom,Hujanijibu wewe mwenye wivu na yeye mwenye majivuno yupi afadhari jibu hilo mzee. Na nani aliyekwambia maendeleo yanaletwa kwa kugawa misaada fulani. Ni lazima awachukie nyie mlioikimbia kyela halafu mnakuja na vijizawadi eti mnaita ni kuendeleza kyela nani amesema anataka dezo?. Watu wengi kwa kweli tuanwachukia sana nyie mnaotaka kuonekana eti mna huruma kwa kugawa vijizawadi hii hata mimi ningekuwa Dr ningechukia tu!
Kuna jamaa mmoja nilikutana naye jina lake linaanzia na G yuko UK anamalizia Phd yake akaniambia kuwa akimaliza tu shule anakwenda kyela kufanya kazi hataki ulaya (mama yake ni mzungu) wala DSM anakwenda kyela. Huyu jamaa ni zawadi tosha kwa wana kyela sio watu wanaotoa vijizawadi vya muda mfupi na kujiona ndiyo kuleta maendeleo. kwa sisi tunaojua kuwa hakuna bure tunajua tu kuna siku ya kuvilipa. ikiwemo kugombea ubunge yes! kugombea ubunge.
samahani kwa language kama imekuwa kali ila mawazo yako, siyo wewe yananikwaza sana port!
Ogah,
Ndio maana nchi inaenda hovyo; kazi za maana zimeshikwa na wababaishaji wengi. Ukiwa mchapa kazi au kama unauliza maswali magumu magumu, huwezi kupanda vyeo.
Wana JF nendeni mkaokoe jahazi, wabaishaji wengi mno kwenye system. Tatizo ni chini mpaka juu.
Asante kwa kugundua kuwa kumbe kugawa vizawadi siyo deal bali kuenda front ndiyo suluhisho karibu! Mwenzio kesho tunaenda kyela kuangalia jinsi ya kuivest huko ikiwamo Mbeya mjini.
Nakuhakikishia sitatoa msaada wa bure kwa yoyote hasa kwa vijana wa kyela ambao ni wavivu sana kufanya kazi kazi kupenda kuwa smart tu. Mungu anasema asiyefanya kazi na kula asile halafu watu wanataka kupinda kanunu ya mungu.
kama baba yake aliiba sawa tu lakini hatuwezi kumbebesha huyu kijana haya mambo kama ambavyo hatuwezi kukupa wewe mambo ya baba yako. Au mzee niyaweke hewani?