Habari njema kwa Vibonge!

Habari njema kwa Vibonge!

ukitaka matokeo haraka ni bora iwe mchemsho, mimi ndivyo nilivyofanya

Kwa matokeo makubwa zaidi iwe ya kuchoma, kwani hata nyama ya kuchoma na maji inapunguza uzito sana.
 
Acha hizo Maty utaukosesha raha sisi tunaopenda hao vibonge wenye nyama nyama kama sponji.

Wanene wataendelea kuwepo Tata ili uwe mwembamba inahitajika discipline yali ya juu. Wengi wanashindwa
 
Last edited by a moderator:
Yaani bidada ubarikiwe kwa hii makitu uliyotumegea!! Swali langu je unaweza kutumia ukiwa mjamzito? maana shostito wangu anaujauzito wa miezi mitatu ila uzito wake umeongezeka kwa kasi sana mpk presha imeanza kumsumbua na safari bado! Msaada plz sho
Kwa wale wenzangu na mimi vibonge suluhisho hili hapa. Hapa kati niliongezeka uzito kwa kiwango kikubwa sana, kasheshe ikawa ni jinsi gani nitapungua kufanya mazoezi kidogo ni mvivu na pia hata muda wa kufanya mazoezi sina. Nimekunywa juice ya ukwaju wapi? maji moto na limao wapiiiiiiiiiiiiiiiii dah kidogo nikate tamaa nikasema labda uzee huu unaonijia inawezekana ndio imetoka hiyo kwa nini kila ninachojaribu kinashindikana

Atafutae hachoki katika kuperuzi peruzi nikakutana na hii soup ya kupunguza mafuta mwilini nikasema ngoja niijaribu ni ngumu kidogo mwanzoni, wiki ya kwanza nikajaribu nikashindwa nikapiga moyo konde wiki inayofuata nikajitahidi mpaka nikamaliza.

Wapendwa nimepungua kilo tano na nusu ndani ya wiki moja mpaka naandika hapa hata siamini kwa kweli ila ndio hivyo imetokea. Nikaona bora nishee na nyinyi maana hili janga la unene ni janga la kitaifa hasa kina mama wanaotoka kujifungua. Jaribu na wewe mimi imenitendea muujiza asee

Soup yenyewe hii

SOUP YA KUPUNGUZA MAFUTA MWILINI

Mahitaji:
Vitunguu vikubwa 6, Pilipili hoho 2, Nyanya 4 kubwa, Cabbage 1 kubwa, Leeks kubwa 4, Cube 2 za Knorr au Roiko (kwa ladha na si lazima). Hii inaweza kutosha kwa nusu siku mpaka siku nzima kutegemea uwezo wako wa kuila.
Boresha ladha kwa kuongeza chumvi, pilipili kawaida au manga, hot sauce au malimao/ndimu.

Namna ya kutengeneza:
Katakata mboga viwe vipande vidogodogo. Weka maji yajae kufunika mboga. Chemsha haraka kwa muda wa dakika kumi halafu punguza moto zitokote taratibu mpaka zilainike kabisa.
Baada ya hapo saga kwenye blender au utakavyoweza ili upate supu yenye rojorojo.
Kula hii supu kwa kadiri uwezavyo kwa kuwa haita ongeza calories kwenye mwili. Jinsi utakavyo kula hii supu ndivyo utakavyo pungua uzito.
Ni vema kuweka supu kwenye thermos asubuhi kama hautakuwepo nyumbani ili uendelee kula mahali popote utakapo kuwa.

TAFADHALI KUMBUKA: Mahali popote panapoandikwa supu, ni hii Basic Fat Burning soup hapo juu na siyo supu nyingine.
UKILA HII SUPU PEKE YAKE KWA MUDA MREFU SANA UNAWEZA KUPATA UTAPIAMLO (MALNUTRITION).
SIKU YA KWANZA
· Kula matunda aina yeyote isipokuwa ndizi.
· Matikiti maji yana calories chache kuliko matunda mengine kwa hiyo ni bora kula hayo.
· Siku hii kula supu peke yake na matunda.
· Kunywa chai isiyo na sukari pamoja na maji.
SIKU YA PILI

· Kula mboga aina yeyote ile.
· Kula mpaka ushibe mboga ambazo ni fresh kama vile saladi au mboga za majani zilizosindikwa kwenye kopo.
· Usile maharage yaliokaushwa, njegere au mahindi makavu.
· Kula hizo mboga pamoja na supu.
· Kwa chakula cha jioni siku hii unaweza kula kiazi kimoja kikubwa kilicho okwa na unaweza kupakaa siagi.
· Usile matunda ya aina yeyote nyingine.
SIKU YA TATU

· Kula supu, matunda na mboga za majani aina yeyote.
· Usile kiazi kilicho okwa.

Kama utakuwa umekula kama ilivyo onyeshwa hapo juu, na huja danganya, basi utakuwa umepoteza uzito wa mwili kwa wastani wa kilo 2 mpaka 3 baada ya siku hii ya tatu.
SIKU YA NNE

·
Kula ndizi mbivu na maziwa yaliyopunguzwa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula ndizi mbivu tatu, maziwa glasi nyingi uwezavyo pamoja na supu.

SIKU YA TANO

· Kula nyama ya Ng’ombe na nyanya fresh.
· Kula nyama kiasi cha robo mpaka nusu kilo pamoja na nyanya fresh kadiri uwezavyo.
· Jaribu kunywa glasi 6 mpaka 8 za maji ili kupunguza uric acid kwenye mwili.
· Kula supu angalau mara moja siku hii.
SIKU YA SITA

· Kula kiasi chochote cha nyama ya Ng’ombe na mboga za majani. Ni bora kula saladi kwa wingi pamoja na nyama, lakini usile kabisa Viazi siku hii.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.
SIKU YA SABA

· Kula wali, juice isiyo na sukari na mboga za majani. Kula kadiri utakavyoweza.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.

Inategemewa kuwa baada ya siku ya saba utakuwa umepoteza kati ya kilo 4.5 mpaka 7.7 ya uzito wa mwili.
Kama umepoteza zaidi ya kilo 6.8 simama kwanza kwa siku mbili kabla hujaendelea na huu utaratibu wa mlo tena.
Utakapo anza tena, anzia siku ya kwanza na kuendelea mpaka siku ya saba tena.
Kwa kuwa miili ya binaadamu inatofautiana, diet hii italeta mabadiliko tofauti tofauti kutegemea mwili unavyo ipokea. Kawaida baada ya siku tatu mwili wako utajisikia nguvu zaidi kama hujadanganya.
VITU VISIVYO RUHUSIWA KABISA WAKATI WA DIET HII.

· Hairuhusiwi kutumia Mkate, Pombe aina yeyote, vinywaji vyenye gesi kama vile soda na vyakula vilivyo kaangwa na mafuta.
· Tumia maji, chai isiyo na sukari, kahawa isiyo na maziwa wala sukari, juice za matunda zisizo na sukari na maziwa yalio ondolewa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula Kuku aliochemshwa au kuokwa badala ya Nyama, lakini uondoe ngozi yake. Unaweza vilevile kutumia Samaki aliyechemshwa katika siku moja inayohitaji Nyama badala ya Nyama lakini sio zaidi ya siku moja.
· Supu hii inaweza kutumika saa yeyote unapo hisi njaa. Kunywa uwezavyo. Kumbuka jinsi unavyo inywa kwa wingi ndivyo unavyo punguza uzito.
Supu hii haingiliani na dawa zozote utakazo andikiwa.
Endelea na utaratibu huu mpaka utakaporidhika kuona mabadiliko katika mtazamo na mwili wako.

ANGALIZO
Hii soup inapunguza mwili kwa haraka sana ila ukishapungua inabidi uangalie mlo wako inabidi upunguze vyakula vya mafuta mawali maugali badala yake ule mboga nyingi kuliko chakula, sio baada ya wiki unaanza kufakamia misosi mfululizo utanenepa zaidi ya mwanzo.
 
Tenda ya skin jeans, hahahahaaha! naona unataka kuja kushuhudia kama ni kweli. ngoja nitakutumia pic yangu kuanzia kiunoni mpk miguu ili uhakikishe kama nikwambiayo ni kweli.

Hiyo mail naomba..
Cc: Mentor
Bcc: Asprin:cheer2:
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe mkuu EMT nilikua nataka kupungua kwanza kwa haraka halafu ndio nianze kurekebisha ulaji wangu, nilikua nanyonyesha bana so kipindi hiyo kucontrol msosi sio rahisi

Maty,

Ukiangalia kwa undani na kuwa mkweli na wewe kilichosaidia kupungua wala siyo hiyo supu. Kilichokusaidia ni wewe kutokunywa pombe, fizzy drinks na vyakula kwa kukaangwa na mafuta kama ulivyokuwa unakunywa au kula kabla ya kuacha.

Kilichokusaidia ni wewe kunywa maji mengi, na pia kupunguza sukari kweye chai, kahawa na kutokunywa juice zenye sukari nyingi na maziwa (whole milk).

Kilikuchosaidia ni kutokula ngozi za kuku ambazo zinahifadhi mafuta mengi na kujikita zaidi kwenye kuchemsha badala ya kukaanga. Najua kuna watu wanapenda sana kula ngozi za kuku, but I hate them.

Kwa hiyo, kwa kifupi ulichofanya ni kuwa makini na ulichokuwa unakula. That's all.

Kwa hiyo, unaposema kuwa ulitaka kwanza kupungua kwa haraka halafu ndio uanze kurekebisha ulaji wangu, siyo sahihi kwa sababu ulikuwa tayari umeshaanza kurekebisha unywaji na ulaji wako.

Unless labda uniambie ukianza kurekebisha ulaji wako, ni vitu gani utarekebisha zaidi ya hivyo ambavyo tayari umesharekebisha hapo juu?

I am sure you don't want to be disappointed wakati utakapoanza kurekebisha ulaji wako halafu usione mabadiliko.
 
Yaani bidada ubarikiwe kwa hii makitu uliyotumegea!! Swali langu je unaweza kutumia ukiwa mjamzito? maana shostito wangu anaujauzito wa miezi mitatu ila uzito wake umeongezeka kwa kasi sana mpk presha imeanza kumsumbua na safari bado! Msaada plz sho

Mama mjamzito anatakiwa ale vizuri, mambo ya madiet hayamfai kabisa. Mwambie akaonane na daktari wa kina mama ASAP ili aweze kujua tatizo ni nini asipuuzie kabisa. Mimba si kitu cha kukifanyia masihara watu wanakufa sana siku hizi mwambie akachunguzwe
 
Love you for such a detailed and useful piece of information!!!

Mimi ya kwangu nilikua nakatakata kila kitu vipande vidogo vidogo nachanganya vyote kwa pamoja nachemsha siweki mafuta hata kidogo, ikiiva naacha ipoe mara nyingi nachemsha usiku asubuhi nasaga kwenye blender, kisha naipasha tena nakunywa kidogo kama nina muda na nyingine nabeba kwenda nayo kazini. Nikisikia njaa nakunywa

Nakunywa sana hii supu majia na matunda. Mboga mboga zimenishinda kidogo labda kama ningekua nazisaga na zenyewe
 
Maty,

Ukiangalia kwa undani na kuwa mkweli na wewe kilichosaidia kupungua wala siyo hiyo supu. Kilichokusaidia ni wewe kutokunywa pombe, fizzy drinks na vyakula kwa kukaangwa na mafuta kama ulivyokuwa unakunywa au kula kabla ya kuacha.

Kilichokusaidia ni wewe kunywa maji mengi, na pia kupunguza sukari kweye chai, kahawa na kutokunywa juice zenye sukari nyingi na maziwa (whole milk).

Kilikuchosaidia ni kutokula ngozi za kuku ambazo zinahifadhi mafuta mengi na kujikita zaidi kwenye kuchemsha badala ya kukaanga. Najua kuna watu wanapenda sana kula ngozi za kuku, but I hate them.

Kwa hiyo, kwa kifupi ulichofanya ni kuwa makini na ulichokuwa unakula. That's all.

Kwa hiyo, unaposema kuwa ulitaka kwanza kupungua kwa haraka halafu ndio uanze kurekebisha ulaji wangu, siyo sahihi kwa sababu ulikuwa tayari umeshaanza kurekebisha unywaji na ulaji wako.

Unless labda uniambie ukianza kurekebisha ulaji wako, ni vitu gani utarekebisha zaidi ya hivyo ambavyo tayari umesharekebisha hapo juu?

I am sure you don't want to be disappointed wakati utakapoanza kurekebisha ulaji wako halafu usione mabadiliko.
EMT kabla sijanywa hii soup nilishaanza kurekebisha ulaji, lakini kiukweli sikuona matokeo yoyote yale sana sana nilikua napigwa tu madongo nanenepeana hovyo kama nilikua napungua basi kilo moja kwa mwezi.

Ila kikweli kabisa hii soup imeleta mabadiliko makubwa, kabla sijaanza kunywa nikapima kilo na baada ya wiki moja ya kula hii soup kwanza nilijiona kabisa nimepungua nikapima kilo na kukuta nimepungua kilo tano na nusu (5.5 ndani ya wiki moja) mimi mwenyewe sikuamini hii soup ni kiboko mkuu kama ukijitoa kweli na una nia
 
Last edited by a moderator:
Tamatheo asante kwa kuboresha, next time nitakula ya kuchoma

Utanikubali ila usinganye na aina yeyote ya sukari unaharibu matokeo kwani zikiungana zinaongeza uzito, hongera kwa kupunguza uziko kwani unakera sana.
 
Maty,

Ukiangalia kwa undani na kuwa mkweli na wewe kilichosaidia kupungua wala siyo hiyo supu. Kilichokusaidia ni wewe kutokunywa pombe, fizzy drinks na vyakula kwa kukaangwa na mafuta kama ulivyokuwa unakunywa au kula kabla ya kuacha.

Kilichokusaidia ni wewe kunywa maji mengi, na pia kupunguza sukari kweye chai, kahawa na kutokunywa juice zenye sukari nyingi na maziwa (whole milk).

Kilikuchosaidia ni kutokula ngozi za kuku ambazo zinahifadhi mafuta mengi na kujikita zaidi kwenye kuchemsha badala ya kukaanga. Najua kuna watu wanapenda sana kula ngozi za kuku, but I hate them.

Kwa hiyo, kwa kifupi ulichofanya ni kuwa makini na ulichokuwa unakula. That's all.

Kwa hiyo, unaposema kuwa ulitaka kwanza kupungua kwa haraka halafu ndio uanze kurekebisha ulaji wangu, siyo sahihi kwa sababu ulikuwa tayari umeshaanza kurekebisha unywaji na ulaji wako.

Unless labda uniambie ukianza kurekebisha ulaji wako, ni vitu gani utarekebisha zaidi ya hivyo ambavyo tayari umesharekebisha hapo juu?

I am sure you don't want to be disappointed wakati utakapoanza kurekebisha ulaji wako halafu usione mabadiliko.

mkuu uko sahihi maana vilivyokatazwa ndio source ya mafuta na digestion yake huwa ni ngumu sana ndani ya tumbo kwa hiyo hupeleka kuzalisha mafuta mengi sana na kuufanya mwili unenepeane haswa kwa wale ambao hawafanyi mazoezi wao ni kula na kulala au kukaa bila kufanya kazi nzito
 
EMT kabla sijanywa hii soup nilishaanza kurekebisha ulaji, lakini kiukweli sikuona matokeo yoyote yale sana sana nilikua napigwa tu madongo nanenepeana hovyo kama nilikua napungua basi kilo moja kwa mwezi.

Right. Hapo kwenye red, ni ulaji gani ulirekebisha? Unaweza kuothoresha vitu ambavyo ulikuwa unakula na kunywa ukarekebisha lakini hukuona matokeo? Be honest katika list yako.

Ila kikweli kabisa hii soup imeleta mabadiliko makubwa, kabla sijaanza kunywa nikapima kilo na baada ya wiki moja ya kula hii soup kwanza nilijiona kabisa nimepungua nikapima kilo na kukuta nimepungua kilo tano na nusu (5.5 ndani ya wiki moja) mimi mwenyewe sikuamini hii soup ni kiboko mkuu kama ukijitoa kweli na una nia
Maty naomba nikuulize swali. Dhumuni lako hasa ni nini kati ya haya mawili: Kupunguza uzito (weight) au kupunguza unene (fat)?
 
neggirl ni kweli nilikua mwembamba kama unionavyo kwenye avatar balaa la unene lilianza baada ya kujifungua nikafumka balaa kama ujuavyo ukiwa unanyonyesha lazima ule hasa ili chakula ya mtoto inone. Sasa nishamaliza nilikua nataka nipungue haraka kwanza halafu ndio nianze kuishi kama zamani kabla ya kujifungua
Unataka upungue ili wakutamani fastafasta??
weee mtoto wewe una balaa....!! shaurilo.
 
Lol, asante mdada uloshare hii habari, i had one diet, hii soup walikuwa wanaita "wounder soup" kama ulivyosema kiukweli hii supu mimi ilinishinda, mmmh, may be nijaribu tena, ila mimi nimefanya diet, so far nimeshaloose 20 kgs, na ninaendelea nayo, ninakata kilo 3 kwa week kama sikucheat, nikicheat 1 - 2 kgs!

Weka diet yako hapa!
 
Hii inawahusu walio nenepa bila mpangilio
 
mkuu uko sahihi maana vilivyokatazwa ndio source ya mafuta na digestion yake huwa ni ngumu sana ndani ya tumbo kwa hiyo hupeleka kuzalisha mafuta mengi sana na kuufanya mwili unenepeane haswa kwa wale ambao hawafanyi mazoezi wao ni kula na kulala au kukaa bila kufanya kazi nzito

Thanks for noting that.

Suala ni kama hiyo supu ndiyo iliyosaidia au kuacha kula na kunywa vyakula/vinywaji tajwa.

The answer is very clear.
 
@Maty

Unene aka Ubonge unaletwa na kula vyakula vya mafuta mengi au inatokana na mtu "kutotumia sehemu kubwa ya ubongo wake"? Nauliza tu!!!
 
Hahahaha huyu naona amenenepa vizuri tu haitaji kupungua
Mhh,akipunguza nguo ngozi yake haipendezi kwa unene bana!kama ganda la limao ,apunguze bana nyie mkiangalia kwa barabarani ndani ya vifungashio mnao poa hamjui wamiliki wa binadamu nene wanavyotamani ngozi mafundofundo free!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom