Habari njema kwa Vibonge!

Habari njema kwa Vibonge!

Habari senyu kwa mpigo.

Kwa wale wenzangu na mimi vibonge suluhisho hili hapa. Hapa kati niliongezeka uzito kwa kiwango kikubwa sana, kasheshe ikawa ni jinsi gani nitapungua kufanya mazoezi kidogo ni mvivu na pia hata muda wa kufanya mazoezi sina. Nimekunywa juice ya ukwaju wapi? maji moto na limao wapiiiiiiiiiiiiiiiii dah kidogo nikate tamaa nikasema labda uzee huu unaonijia inawezekana ndio imetoka hiyo kwa nini kila ninachojaribu kinashindikana

Atafutae hachoki katika kuperuzi peruzi nikakutana na hii soup ya kupunguza mafuta mwilini nikasema ngoja niijaribu ni ngumu kidogo mwanzoni, wiki ya kwanza nikajaribu nikashindwa nikapiga moyo konde wiki inayofuata nikajitahidi mpaka nikamaliza.

Wapendwa nimepungua kilo tano na nusu ndani ya wiki moja mpaka naandika hapa hata siamini kwa kweli ila ndio hivyo imetokea. Nikaona bora nishee na nyinyi maana hili janga la unene ni janga la kitaifa hasa kina mama wanaotoka kujifungua. Jaribu na wewe mimi imenitendea muujiza asee

Soup yenyewe hii

SOUP YA KUPUNGUZA MAFUTA MWILINI

Mahitaji:
Vitunguu vikubwa 6, Pilipili hoho 2, Nyanya 4 kubwa, Cabbage 1 kubwa, Leeks kubwa 4, Cube 2 za Knorr au Roiko (kwa ladha na si lazima). Hii inaweza kutosha kwa nusu siku mpaka siku nzima kutegemea uwezo wako wa kuila.
Boresha ladha kwa kuongeza chumvi, pilipili kawaida au manga, hot sauce au malimao/ndimu.

Namna ya kutengeneza:
Katakata mboga viwe vipande vidogodogo. Weka maji yajae kufunika mboga. Chemsha haraka kwa muda wa dakika kumi halafu punguza moto zitokote taratibu mpaka zilainike kabisa.
Baada ya hapo saga kwenye blender au utakavyoweza ili upate supu yenye rojorojo.
Kula hii supu kwa kadiri uwezavyo kwa kuwa haita ongeza calories kwenye mwili. Jinsi utakavyo kula hii supu ndivyo utakavyo pungua uzito.
Ni vema kuweka supu kwenye thermos asubuhi kama hautakuwepo nyumbani ili uendelee kula mahali popote utakapo kuwa.

TAFADHALI KUMBUKA: Mahali popote panapoandikwa supu, ni hii Basic Fat Burning soup hapo juu na siyo supu nyingine.
UKILA HII SUPU PEKE YAKE KWA MUDA MREFU SANA UNAWEZA KUPATA UTAPIAMLO (MALNUTRITION).
SIKU YA KWANZA
· Kula matunda aina yeyote isipokuwa ndizi.
· Matikiti maji yana calories chache kuliko matunda mengine kwa hiyo ni bora kula hayo.
· Siku hii kula supu peke yake na matunda.
· Kunywa chai isiyo na sukari pamoja na maji.
SIKU YA PILI

· Kula mboga aina yeyote ile.
· Kula mpaka ushibe mboga ambazo ni fresh kama vile saladi au mboga za majani zilizosindikwa kwenye kopo.
· Usile maharage yaliokaushwa, njegere au mahindi makavu.
· Kula hizo mboga pamoja na supu.
· Kwa chakula cha jioni siku hii unaweza kula kiazi kimoja kikubwa kilicho okwa na unaweza kupakaa siagi.
· Usile matunda ya aina yeyote nyingine.
SIKU YA TATU

· Kula supu, matunda na mboga za majani aina yeyote.
· Usile kiazi kilicho okwa.

Kama utakuwa umekula kama ilivyo onyeshwa hapo juu, na huja danganya, basi utakuwa umepoteza uzito wa mwili kwa wastani wa kilo 2 mpaka 3 baada ya siku hii ya tatu.
SIKU YA NNE

·
Kula ndizi mbivu na maziwa yaliyopunguzwa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula ndizi mbivu tatu, maziwa glasi nyingi uwezavyo pamoja na supu.

SIKU YA TANO

· Kula nyama ya Ng’ombe na nyanya fresh.
· Kula nyama kiasi cha robo mpaka nusu kilo pamoja na nyanya fresh kadiri uwezavyo.
· Jaribu kunywa glasi 6 mpaka 8 za maji ili kupunguza uric acid kwenye mwili.
· Kula supu angalau mara moja siku hii.
SIKU YA SITA

· Kula kiasi chochote cha nyama ya Ng’ombe na mboga za majani. Ni bora kula saladi kwa wingi pamoja na nyama, lakini usile kabisa Viazi siku hii.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.
SIKU YA SABA

· Kula wali, juice isiyo na sukari na mboga za majani. Kula kadiri utakavyoweza.

Inategemewa kuwa baada ya siku ya saba utakuwa umepoteza kati ya kilo 4.5 mpaka 7.7 ya uzito wa mwili.
Kama umepoteza zaidi ya kilo 6.8 simama kwanza kwa siku mbili kabla hujaendelea na huu utaratibu wa mlo tena.
Utakapo anza tena, anzia siku ya kwanza na kuendelea mpaka siku ya saba tena.
Kwa kuwa miili ya binaadamu inatofautiana, diet hii italeta mabadiliko tofauti tofauti kutegemea mwili unavyo ipokea. Kawaida baada ya siku tatu mwili wako utajisikia nguvu zaidi kama hujadanganya.
VITU VISIVYO RUHUSIWA KABISA WAKATI WA DIET HII.

· Hairuhusiwi kutumia Mkate, Pombe aina yeyote, vinywaji vyenye gesi kama vile soda na vyakula vilivyo kaangwa na mafuta.
· Tumia maji, chai isiyo na sukari, kahawa isiyo na maziwa wala sukari, juice za matunda zisizo na sukari na maziwa yalio ondolewa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula Kuku aliochemshwa au kuokwa badala ya Nyama, lakini uondoe ngozi yake. Unaweza vilevile kutumia Samaki aliyechemshwa katika siku moja inayohitaji Nyama badala ya Nyama lakini sio zaidi ya siku moja.
· Supu hii inaweza kutumika saa yeyote unapo hisi njaa. Kunywa uwezavyo. Kumbuka jinsi unavyo inywa kwa wingi ndivyo unavyo punguza uzito.
Supu hii haingiliani na dawa zozote utakazo andikiwa.
Endelea na utaratibu huu mpaka utakaporidhika kuona mabadiliko katika mtazamo na mwili wako.

ANGALIZO
Hii soup inapunguza mwili kwa haraka sana ila ukishapungua inabidi uangalie mlo wako inabidi upunguze vyakula vya mafuta mawali maugali badala yake ule mboga nyingi kuliko chakula, sio baada ya wiki unaanza kufakamia misosi mfululizo utanenepa zaidi ya mwanzo.
Red: ngumu kumesa..
 
Madame B watu wenye shepu za hivyo ni wachache sana. We ukipita barabarani unakutana na wangapi wenye pododo kama lako? wengi wamenenepa hovyo hovyo tu matumbo yametangulia

Hata mm ninalo kama la Maddame b, ila mm nataka lipungue maana linaniletea tabu sana kwenye maisha yangu, mpk najuta kuwa nayo, ingekuwa unaweza kuyafungia kwenye kabati , unakuja ofisini bila hayo, naona maisha yangu yangekuwa burudaniiiii hapa ofisini. Halafu unayavaa ukirudi au ukienda kwenye part tu. KWA KWELI MM ITABIDI NIKAANZE MARA MOJA.
 
Habari senyu kwa mpigo.

Kwa wale wenzangu na mimi vibonge suluhisho hili hapa. Hapa kati niliongezeka uzito kwa kiwango kikubwa sana, kasheshe ikawa ni jinsi gani nitapungua kufanya mazoezi kidogo ni mvivu na pia hata muda wa kufanya mazoezi sina. Nimekunywa juice ya ukwaju wapi? maji moto na limao wapiiiiiiiiiiiiiiiii dah kidogo nikate tamaa nikasema labda uzee huu unaonijia inawezekana ndio imetoka hiyo kwa nini kila ninachojaribu kinashindikana

Atafutae hachoki katika kuperuzi peruzi nikakutana na hii soup ya kupunguza mafuta mwilini nikasema ngoja niijaribu ni ngumu kidogo mwanzoni, wiki ya kwanza nikajaribu nikashindwa nikapiga moyo konde wiki inayofuata nikajitahidi mpaka nikamaliza.

Wapendwa nimepungua kilo tano na nusu ndani ya wiki moja mpaka naandika hapa hata siamini kwa kweli ila ndio hivyo imetokea. Nikaona bora nishee na nyinyi maana hili janga la unene ni janga la kitaifa hasa kina mama wanaotoka kujifungua. Jaribu na wewe mimi imenitendea muujiza asee

Soup yenyewe hii

SOUP YA KUPUNGUZA MAFUTA MWILINI

Mahitaji:
Vitunguu vikubwa 6, Pilipili hoho 2, Nyanya 4 kubwa, Cabbage 1 kubwa, Leeks kubwa 4, Cube 2 za Knorr au Roiko (kwa ladha na si lazima). Hii inaweza kutosha kwa nusu siku mpaka siku nzima kutegemea uwezo wako wa kuila.
Boresha ladha kwa kuongeza chumvi, pilipili kawaida au manga, hot sauce au malimao/ndimu.

Namna ya kutengeneza:
Katakata mboga viwe vipande vidogodogo. Weka maji yajae kufunika mboga. Chemsha haraka kwa muda wa dakika kumi halafu punguza moto zitokote taratibu mpaka zilainike kabisa.
Baada ya hapo saga kwenye blender au utakavyoweza ili upate supu yenye rojorojo.
Kula hii supu kwa kadiri uwezavyo kwa kuwa haita ongeza calories kwenye mwili. Jinsi utakavyo kula hii supu ndivyo utakavyo pungua uzito.
Ni vema kuweka supu kwenye thermos asubuhi kama hautakuwepo nyumbani ili uendelee kula mahali popote utakapo kuwa.

TAFADHALI KUMBUKA: Mahali popote panapoandikwa supu, ni hii Basic Fat Burning soup hapo juu na siyo supu nyingine.
UKILA HII SUPU PEKE YAKE KWA MUDA MREFU SANA UNAWEZA KUPATA UTAPIAMLO (MALNUTRITION).
SIKU YA KWANZA
· Kula matunda aina yeyote isipokuwa ndizi.
· Matikiti maji yana calories chache kuliko matunda mengine kwa hiyo ni bora kula hayo.
· Siku hii kula supu peke yake na matunda.
· Kunywa chai isiyo na sukari pamoja na maji.
SIKU YA PILI

· Kula mboga aina yeyote ile.
· Kula mpaka ushibe mboga ambazo ni fresh kama vile saladi au mboga za majani zilizosindikwa kwenye kopo.
· Usile maharage yaliokaushwa, njegere au mahindi makavu.
· Kula hizo mboga pamoja na supu.
· Kwa chakula cha jioni siku hii unaweza kula kiazi kimoja kikubwa kilicho okwa na unaweza kupakaa siagi.
· Usile matunda ya aina yeyote nyingine.
SIKU YA TATU

· Kula supu, matunda na mboga za majani aina yeyote.
· Usile kiazi kilicho okwa.

Kama utakuwa umekula kama ilivyo onyeshwa hapo juu, na huja danganya, basi utakuwa umepoteza uzito wa mwili kwa wastani wa kilo 2 mpaka 3 baada ya siku hii ya tatu.
SIKU YA NNE

·
Kula ndizi mbivu na maziwa yaliyopunguzwa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula ndizi mbivu tatu, maziwa glasi nyingi uwezavyo pamoja na supu.

SIKU YA TANO

· Kula nyama ya Ng'ombe na nyanya fresh.
· Kula nyama kiasi cha robo mpaka nusu kilo pamoja na nyanya fresh kadiri uwezavyo.
· Jaribu kunywa glasi 6 mpaka 8 za maji ili kupunguza uric acid kwenye mwili.
· Kula supu angalau mara moja siku hii.
SIKU YA SITA

· Kula kiasi chochote cha nyama ya Ng'ombe na mboga za majani. Ni bora kula saladi kwa wingi pamoja na nyama, lakini usile kabisa Viazi siku hii.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.
SIKU YA SABA

· Kula wali, juice isiyo na sukari na mboga za majani. Kula kadiri utakavyoweza.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.

Inategemewa kuwa baada ya siku ya saba utakuwa umepoteza kati ya kilo 4.5 mpaka 7.7 ya uzito wa mwili.
Kama umepoteza zaidi ya kilo 6.8 simama kwanza kwa siku mbili kabla hujaendelea na huu utaratibu wa mlo tena.
Utakapo anza tena, anzia siku ya kwanza na kuendelea mpaka siku ya saba tena.
Kwa kuwa miili ya binaadamu inatofautiana, diet hii italeta mabadiliko tofauti tofauti kutegemea mwili unavyo ipokea. Kawaida baada ya siku tatu mwili wako utajisikia nguvu zaidi kama hujadanganya.
VITU VISIVYO RUHUSIWA KABISA WAKATI WA DIET HII.

· Hairuhusiwi kutumia Mkate, Pombe aina yeyote, vinywaji vyenye gesi kama vile soda na vyakula vilivyo kaangwa na mafuta.
· Tumia maji, chai isiyo na sukari, kahawa isiyo na maziwa wala sukari, juice za matunda zisizo na sukari na maziwa yalio ondolewa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula Kuku aliochemshwa au kuokwa badala ya Nyama, lakini uondoe ngozi yake. Unaweza vilevile kutumia Samaki aliyechemshwa katika siku moja inayohitaji Nyama badala ya Nyama lakini sio zaidi ya siku moja.
· Supu hii inaweza kutumika saa yeyote unapo hisi njaa. Kunywa uwezavyo. Kumbuka jinsi unavyo inywa kwa wingi ndivyo unavyo punguza uzito.
Supu hii haingiliani na dawa zozote utakazo andikiwa.
Endelea na utaratibu huu mpaka utakaporidhika kuona mabadiliko katika mtazamo na mwili wako.

ANGALIZO
Hii soup inapunguza mwili kwa haraka sana ila ukishapungua inabidi uangalie mlo wako inabidi upunguze vyakula vya mafuta mawali maugali badala yake ule mboga nyingi kuliko chakula, sio baada ya wiki unaanza kufakamia misosi mfululizo utanenepa zaidi ya mwanzo.
MMMhhh nimeipenda hiyo Leeks na cube ndo nini? vingine vyote navijua,
 
Hata mm ninalo kama la Maddame b, ila mm nataka lipungue maana linaniletea tabu sana kwenye maisha yangu, mpk najuta kuwa nayo, ingekuwa unaweza kuyafungia kwenye kabati , unakuja ofisini bila hayo, naona maisha yangu yangekuwa burudaniiiii hapa ofisini. Halafu unayavaa ukirudi au ukienda kwenye part tu. KWA KWELI MM ITABIDI NIKAANZE MARA MOJA.

Tufanye diet hyo.
 
Jamani Lisa unajua kufanya hivyo unakuwa hututendei haki si wanaume? Mungu kakuumba na mpododo nyama laini kakupa alafu wewe unataka kulipunguza kwa nini jamani? kwani limekuwa zito unapo tembea?:madgrin:
 
Last edited by a moderator:

Hapana halijawa zito, ila na mm nataka nivae skin jeans,na niwe na uhuru ,maana akina Fidel80 mnanisumbua sana, na kufanya maisha yangu kutokuwa mazuri kwa sababu ya kuwakatalia kuwa na access nayo, kwa hiyo na nyinyi mnaninyima vyeo, safari nakuwa ni mtu wa hapa hapa ofisini. kwa hiyo yananihukumu. na ndiyo mana nikasema yangekuwa yanaweza kukaa kwenye kabati home, halafu nikaja hivyo hivyo ingekuwa bora sana.
 
:becky::becky: sasa Mungu amesha kupa huo mpododo ili utunyanyase sisi huoni kama kuna ufahari kujaaliwa hilo furushi? hata hivyo mbona skin jeans unaweza ukavaa tu au umekosa size yako unipe tender ya kukuletea size ya kukutosha wewe?
 
Tenda ya skin jeans, hahahahaaha! naona unataka kuja kushuhudia kama ni kweli. ngoja nitakutumia pic yangu kuanzia kiunoni mpk miguu ili uhakikishe kama nikwambiayo ni kweli.
 
Mpwa kwa kubadilika badilika......kama kinyonga!!

Umeonaeee kumbe na wewe umeshastuka lol

ni kweli,unakuta mdada kanenepa tumbo mbele,---- kule vurugu tupu, shepu inakua hovyo kabisa,anakosa mvuto zaidi ni kituko!
Na hawa ndio wanatakiwa kuwa wembamba tu ndio watavutia, mi kuna rafiki yangu mmoja alivyokua mwembamba alikua anapendeza sana baada ya kujiachia amekuwa na shepu ambayo huwa siielewagi kabisa simba si simba, kabati si kabati mradi vurugu tupu

Maty njia bora ya kupunguza unene ni kufanya mazoezi na kurekebisha unachokula na unakula wakati gani.

Pili sielewi ni kwa nini mtu upunguze unene lakini still ukubali kuwa mwili flabby. Tuache visingizio. Mazoezi ni muhimu sana kwa afya zetu.

These short cuts won't lead us anywhere.
Nakubaliana na wewe mkuu EMT nilikua nataka kupungua kwanza kwa haraka halafu ndio nianze kurekebisha ulaji wangu, nilikua nanyonyesha bana so kipindi hiyo kucontrol msosi sio rahisi
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Mazoezi yanafanya mtu unakua na mwili na figure nzuri kiukweli,ila kuna mwingine akifanya mazoezi anakula huyooo badala ya kupungua anazidi kua bonge kwa sababu akifanya mazoezi njaa inakua ya hatari, ila akijua kujicontrol kwny msosi tu atafrai maana huo mvuto wake ni balaa
 
Maty asante mwayaa... mbona lakini hapo kwa avatar wewe ni mwembamba? au huyo ni mdogo wako (joke), BUT nafikiri mtu kabla huja ji commit katika diet au mazoezi kwa ajili ya kupunguza mwili ni bora kujifunza kwanza maisha utakayoishi baada ya diet... as inabidi uchange life style ili umaintain.

Na ni muhimu tutambue kwamba kupunguza na kuongezeka uzito mara kwa mara (kwa njia za short curt) si nzuri kiafya.
neggirl ni kweli nilikua mwembamba kama unionavyo kwenye avatar balaa la unene lilianza baada ya kujifungua nikafumka balaa kama ujuavyo ukiwa unanyonyesha lazima ule hasa ili chakula ya mtoto inone. Sasa nishamaliza nilikua nataka nipungue haraka kwanza halafu ndio nianze kuishi kama zamani kabla ya kujifungua
 
Last edited by a moderator:
Umeonaeee kumbe na wewe umeshastuka lol

Na hawa ndio wanatakiwa kuwa wembamba tu ndio watavutia, mi kuna rafiki yangu mmoja alivyokua mwembamba alikua anapendeza sana baada ya kujiachia amekuwa na shepu ambayo huwa siielewagi kabisa simba si simba, kabati si kabati mradi vurugu tupu

Nakubaliana na wewe mkuu EMT nilikua nataka kupungua kwanza kwa haraka halafu ndio nianze kurekebisha ulaji wangu, nilikua nanyonyesha bana so kipindi hiyo kucontrol msosi sio rahisi
Maty, hii inawahusu 'wababa'?
 
Last edited by a moderator:
MMMhhh nimeipenda hiyo Leeks na cube ndo nini? vingine vyote navijua,

leeks ni jamii ya vitunguu ila sijui tutaviitaje ila ukienda sokoni utaviona nivitunguu chini ni vyeupe na havikatwi majani yake hivyo viko na majani yake. nadhani utakuwa unavijua ila nikutokana na lugha iliyotumika. ukienda kwenye google ukasearch maana ya leeks unapata wanakutolea na picha yake utaona ni kitu ambacho kinapatikana kwa urahisi. Cube hata mimi sikuelewa nikaacha kama ilivyo
 
Maty, hii inawahusu 'wababa'?

kwa mujibu wa alietupa hii diet alimalizia

[Diet hii imetumiwa na The Sacred Heart Memorial Hospital, Rochester, Mayo Clinic, Marekani. Inatumika kwa wagonjwa wa moyo, wenye uzito mkubwa ambao wanahijati kupunguza uzito wa mwili haraka kabla ya upasuaji wa moyo.Hata watu wengine wanaohitaji kupungua wanaweza kuitumia Imebadilishwa kidogo kutokana na vitu vinavyopatikana hapa kwetu bongo kirahisi.]

Nafikiri na wababa inawafaa
 
Acha hizo Maty utaukosesha raha sisi tunaopenda hao vibonge wenye nyama nyama kama sponji.
 
Dear baadhi ya viungo hujaelezea namna na wakati wa kuviweka, ila kwa kuwa nafahamu upishi kwangu haijawa shida kuelewa...

Mimi ya kwangu nilikua nakatakata kila kitu vipande vidogo vidogo nachanganya vyote kwa pamoja nachemsha siweki mafuta hata kidogo, ikiiva naacha ipoe mara nyingi nachemsha usiku asubuhi nasaga kwenye blender, kisha naipasha tena nakunywa kidogo kama nina muda na nyingine nabeba kwenda nayo kazini. Nikisikia njaa nakunywa

Nakunywa sana hii supu majia na matunda. Mboga mboga zimenishinda kidogo labda kama ningekua nazisaga na zenyewe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom