Habari njema kwa Vibonge!

Habari njema kwa Vibonge!

naomben kita mbadala nachoweza kutumia badala ya leeks. Nataka kuanza diet kesho.

Nakushauri utafute na leeks, zinauzwa nafuu sana Tshs. 500 fungu. Uzuri hii diet haina gharama makabichi bei nafuu, leeks bei nafuu nyanya na vitunguu ndio kabisaaaaaaaaa. Kama unakaa mbali na soko chagua siku moja nenda sokoni sio gengeni (gengeni huwezi pata leeks) nunua mahitaji yako ya wiki nzima halafu anza diet yako bila wasiwasi
 
Maty hii kitu inashauriwa kutumiwa na mwanaume? na kama akitumia wakati yuko kwenye hii program anaruhusiwa kupiga "GAME"
 
mkuu nisaidie hiyo diet unayotumia manake na mimi nazidi kuwa chibonge
 
Uzoefu wangu kwa ndugu jamaa na marafiki kupungua si kazi; kazi kubaki ulivyo;

Hili ni suala la kisaikolojia zaidi...will power....unakuta mtu anajisifu ame loose 20 Kg baada ya muda ameongezeka kilo 30...work done sawa na negative maana si zero

mfano mimi nimeacha kula usiku muda mrefu sana...hiyo ni njia rahisi sana ya kulinda mwili usiongezeke na ni nzuri kwa kupumzisha tumbo sio kila saa linafanya kazi ya kumeng'enya(unakuwa na tumbo flat kabisa)

Usile usiku, mchana na asubuhi kula kawaida ila watch what you eat...(mfano tumia mafuta ya mimea) hizi formular za leo kula hiki; kesho kula hiki ni ngumu na ni za mpito sana. Hata gym ni ngumu kupunguza mwili wa mtu; zaidi inasaidia ku shape mwili si kupunguza
 
mbona mie nafanya diet napungua juu tu maty? kuna diet ya kupunguza mwili wote?
 
em nijibiwe kwanza hili swali!
ivi inamaana juice ya ukwaju huondoa unene??
manake me hua nainywa sana, naipendagatu ladha yake na poia nafaham kua husaidia kuondoa sumu mwilini.
sasa hili la unene nisaidieni tafadhali.
 
Daah mi mbona bonge sana na wanaume wakware wananitaka sana kwa unene wangu? unene ndo mwake mwake
 
CC: Kongosho...Kila la heri katika jitihada zako.

Habari senyu kwa mpigo.

Kwa wale wenzangu na mimi vibonge suluhisho hili hapa. Hapa kati niliongezeka uzito kwa kiwango kikubwa sana, kasheshe ikawa ni jinsi gani nitapungua kufanya mazoezi kidogo ni mvivu na pia hata muda wa kufanya mazoezi sina. Nimekunywa juice ya ukwaju wapi? maji moto na limao wapiiiiiiiiiiiiiiiii dah kidogo nikate tamaa nikasema labda uzee huu unaonijia inawezekana ndio imetoka hiyo kwa nini kila ninachojaribu kinashindikana

Atafutae hachoki katika kuperuzi peruzi nikakutana na hii soup ya kupunguza mafuta mwilini nikasema ngoja niijaribu ni ngumu kidogo mwanzoni, wiki ya kwanza nikajaribu nikashindwa nikapiga moyo konde wiki inayofuata nikajitahidi mpaka nikamaliza.

Wapendwa nimepungua kilo tano na nusu ndani ya wiki moja mpaka naandika hapa hata siamini kwa kweli ila ndio hivyo imetokea. Nikaona bora nishee na nyinyi maana hili janga la unene ni janga la kitaifa hasa kina mama wanaotoka kujifungua. Jaribu na wewe mimi imenitendea muujiza asee


Soup yenyewe hii

SOUP YA KUPUNGUZA MAFUTA MWILINI

Mahitaji:
Vitunguu vikubwa 6, Pilipili hoho 2, Nyanya 4 kubwa, Cabbage 1 kubwa, Leeks kubwa 4, Cube 2 za Knorr au Roiko (kwa ladha na si lazima). Hii inaweza kutosha kwa nusu siku mpaka siku nzima kutegemea uwezo wako wa kuila.
Boresha ladha kwa kuongeza chumvi, pilipili kawaida au manga, hot sauce au malimao/ndimu.

Namna ya kutengeneza:
Katakata mboga viwe vipande vidogodogo. Weka maji yajae kufunika mboga. Chemsha haraka kwa muda wa dakika kumi halafu punguza moto zitokote taratibu mpaka zilainike kabisa.
Baada ya hapo saga kwenye blender au utakavyoweza ili upate supu yenye rojorojo.
Kula hii supu kwa kadiri uwezavyo kwa kuwa haita ongeza calories kwenye mwili. Jinsi utakavyo kula hii supu ndivyo utakavyo pungua uzito.
Ni vema kuweka supu kwenye thermos asubuhi kama hautakuwepo nyumbani ili uendelee kula mahali popote utakapo kuwa.

TAFADHALI KUMBUKA: Mahali popote panapoandikwa supu, ni hii Basic Fat Burning soup hapo juu na siyo supu nyingine.
UKILA HII SUPU PEKE YAKE KWA MUDA MREFU SANA UNAWEZA KUPATA UTAPIAMLO (MALNUTRITION).
SIKU YA KWANZA
· Kula matunda aina yeyote isipokuwa ndizi.
· Matikiti maji yana calories chache kuliko matunda mengine kwa hiyo ni bora kula hayo.
· Siku hii kula supu peke yake na matunda.
· Kunywa chai isiyo na sukari pamoja na maji.
SIKU YA PILI

· Kula mboga aina yeyote ile.
· Kula mpaka ushibe mboga ambazo ni fresh kama vile saladi au mboga za majani zilizosindikwa kwenye kopo.
· Usile maharage yaliokaushwa, njegere au mahindi makavu.
· Kula hizo mboga pamoja na supu.
· Kwa chakula cha jioni siku hii unaweza kula kiazi kimoja kikubwa kilicho okwa na unaweza kupakaa siagi.
· Usile matunda ya aina yeyote nyingine.
SIKU YA TATU

· Kula supu, matunda na mboga za majani aina yeyote.
· Usile kiazi kilicho okwa.

Kama utakuwa umekula kama ilivyo onyeshwa hapo juu, na huja danganya, basi utakuwa umepoteza uzito wa mwili kwa wastani wa kilo 2 mpaka 3 baada ya siku hii ya tatu.
SIKU YA NNE

·
Kula ndizi mbivu na maziwa yaliyopunguzwa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula ndizi mbivu tatu, maziwa glasi nyingi uwezavyo pamoja na supu.

SIKU YA TANO


· Kula nyama ya Ng’ombe na nyanya fresh.
· Kula nyama kiasi cha robo mpaka nusu kilo pamoja na nyanya fresh kadiri uwezavyo.
· Jaribu kunywa glasi 6 mpaka 8 za maji ili kupunguza uric acid kwenye mwili.
· Kula supu angalau mara moja siku hii.
SIKU YA SITA

· Kula kiasi chochote cha nyama ya Ng’ombe na mboga za majani. Ni bora kula saladi kwa wingi pamoja na nyama, lakini usile kabisa Viazi siku hii.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.
SIKU YA SABA

· Kula wali, juice isiyo na sukari na mboga za majani. Kula kadiri utakavyoweza.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.

Inategemewa kuwa baada ya siku ya saba utakuwa umepoteza kati ya kilo 4.5 mpaka 7.7 ya uzito wa mwili.
Kama umepoteza zaidi ya kilo 6.8 simama kwanza kwa siku mbili kabla hujaendelea na huu utaratibu wa mlo tena.
Utakapo anza tena, anzia siku ya kwanza na kuendelea mpaka siku ya saba tena.
Kwa kuwa miili ya binaadamu inatofautiana, diet hii italeta mabadiliko tofauti tofauti kutegemea mwili unavyo ipokea. Kawaida baada ya siku tatu mwili wako utajisikia nguvu zaidi kama hujadanganya.
VITU VISIVYO RUHUSIWA KABISA WAKATI WA DIET HII.

· Hairuhusiwi kutumia Mkate, Pombe aina yeyote, vinywaji vyenye gesi kama vile soda na vyakula vilivyo kaangwa na mafuta.
· Tumia maji, chai isiyo na sukari, kahawa isiyo na maziwa wala sukari, juice za matunda zisizo na sukari na maziwa yalio ondolewa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula Kuku aliochemshwa au kuokwa badala ya Nyama, lakini uondoe ngozi yake. Unaweza vilevile kutumia Samaki aliyechemshwa katika siku moja inayohitaji Nyama badala ya Nyama lakini sio zaidi ya siku moja.
· Supu hii inaweza kutumika saa yeyote unapo hisi njaa. Kunywa uwezavyo. Kumbuka jinsi unavyo inywa kwa wingi ndivyo unavyo punguza uzito.
Supu hii haingiliani na dawa zozote utakazo andikiwa.
Endelea na utaratibu huu mpaka utakaporidhika kuona mabadiliko katika mtazamo na mwili wako.

ANGALIZO
Hii soup inapunguza mwili kwa haraka sana ila ukishapungua inabidi uangalie mlo wako inabidi upunguze vyakula vya mafuta mawali maugali badala yake ule mboga nyingi kuliko chakula, sio baada ya wiki unaanza kufakamia misosi mfululizo utanenepa zaidi ya mwanzo.
 
Last edited by a moderator:
Lol, asante mdada uloshare hii habari, i had one diet, hii soup walikuwa wanaita "wounder soup" kama ulivyosema kiukweli hii supu mimi ilinishinda, mmmh, may be nijaribu tena, ila mimi nimefanya diet, so far nimeshaloose 20 kgs, na ninaendelea nayo, ninakata kilo 3 kwa week kama sikucheat, nikicheat 1 - 2 kgs!
share basi diet yako nasi tufaidike nayo
 
hii diet nilishawahi jaribu, inaitwa cabbage soup diet ukigoogle utakutana nayo. ila sikufanikiwa. ilipofika siku ya kula ndizi na maziwa nafikri niliover-eat kwa njaa niliyokuwa nayo, tumbo lilinichafuka si mchezo. sasa ukichanganya na ile kushindia supu kwa siku 3 niliishiwa nguvu kabisa. nikashindwa kuendela na sikurudia tena.
nitarudia next week nione, then nitaleta feedback
 
naomba unisaidie leeks kwa lugha yetu ya taifa.
lEEKS NI VITUNGUU VICHANGA VYENYE MAJANI YAKE (YA KIJANI) KWA JUU. VINAKUWA BADO VIBICHI (MARA NYINGI VINA RANGI NYEUPE).

300px-Leeks.jpg
 
Bila hata ya kunywa supu hyo cha muhimu ni kukontrol kiasi cha ulaji wako,mambo mengine ni mbwembwe tu
 
Sidhani kama ni vitunguu na kama ni vitunguu basi ni vya aina yake (haviweki kitunguu kwenye mzizi) maana majani yake magumu kama mua...ingawa yana harufu kama kitunguu

yanapatikan super markets nyingi au soko la Kisutu

lEEKS NI VITUNGUU VICHANGA VYENYE MAJANI YAKE (YA KIJANI) KWA JUU. VINAKUWA BADO VIBICHI (MARA NYINGI VINA RANGI NYEUPE).

300px-Leeks.jpg
 
Daah mi mbona bonge sana na wanaume wakware wananitaka sana kwa unene wangu? unene ndo mwake mwake

Mwanamke mwembamba HAJAWAHI kuwa chaguo langu!Mm mnyakyusa bana napenda mwanamke mwenye makalio na kwetu mwanamke mwembamba huwa tunawaita "abhalondo":Bujibuji na Watu8 wanajua nina maana gani!
secret kama kweli upo hivyo ume qualify kuanza mazungumzo chemba;ni PM pls tuanze mchakato!

Mwanamke paja bana!
 
Last edited by a moderator:
[h=5]
[/h]


Hawa inawahusu samahani lakini?

Kama huyu apungue ili iweje?Huyu akianza kunywa hayo madudu yenu ya kupungua ni kumkufuru Subhaana Allah wa taalah!Huyo ni pambo la dunia bana na kuiga kama kuwa mwembamba ndiyo sexy ni up u u z i tu!

She is hot akipungua anaharibu!
 
Sidhani kama ni vitunguu na kama ni vitunguu basi ni vya aina yake (haviweki kitunguu kwenye mzizi) maana majani yake magumu kama mua...ingawa yana harufu kama kitunguu

yanapatikan super markets nyingi au soko la Kisutu
yah1 inawezekana zina jina lingine la kiswahili, ila mtaani tunaita hivyo. si leeks zote zina majani magumu, zipo pia zenye majani membamba yapo very soft
 
Sidhani kama ni vitunguu na kama ni vitunguu basi ni vya aina yake (haviweki kitunguu kwenye mzizi) maana majani yake magumu kama mua...ingawa yana harufu kama kitunguu

yanapatikan super markets nyingi au soko la Kisutu
ni jamii ya vitunguu, ni familia moja ya vitunguu vipo vya purple,vyeupe kabisa na hivyo ambavyo havivimbi chini na inawezekana ziko aina nyingine tusizojua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom