Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
- Thread starter
- #21
Sasa hapa unazungumzia kumuuzia Osama. Sisi kama nchi hatuwezi ku-base projections zetu kwenye bei ya kumuuzia Osama kwenye black market! Badala ya kudai mgao, tukigundua kuwa kuna watu wanafanya hivyo inabidi tuwapeleke mbele ya sheria. Kama vile ambavyo tukimkuta mtu anauza viungo vya Albino. Vyote ni criminal activities.
Kwa kugida kidogo kidogo kwenye hizo sample zinazochukuliwa kila siku huwezi kujua anakwenda kuuziwa nani ,hicho ambacho nisafi. Ndio kusema mambo haya yataisha lini ? Project zipo matunda tayari yameshaonekana na watu weshapanga mahesabu ,yaani ukichunguza mambo ya migodi ya dhahabu utaona ni jinsi gani pasi zinavyokwenda na local businessman ambao ni wakubwa huwa wanaweka saini kiulaini,sasa kila miaka inapokwenda hakuna kinachofikia mwisho na kujulikana palipofikiwa na mwisho wa kuchukua sampuli utakuwa lini kwani kila anepasiwa hutaka kuondoka na sampuli ili akakaguwe zaidi au kwa nini baada ya uchunguzi wa mwanzo Serikali haiweki kumbukumbu na badala yake anaekuja aambiwe uchunguzi ni huu hapa ,hakuna haja ya kufanya uchunguzi mwengine au hizi chunguzi zinazofanywa baada ya kukamilika serikali huwa haipewi na hubakia mikononi mwa waliochungua na kuwa ni mali yao ,na kama ndio hivyo kwa nini haiwekwi sheria kwa kila anaechunguza uchunguzi utakuwa ni mali ya nchi na riporti yake kuwepo katika wizara husika ? Uranium ilianza kuchunguzwa na wajerumani katika miaka ya 70 na sehemu ni hizo hizo zinazochunguzwa leo.
Au hizi leseni zikishatolewa ndio serikali haitakiwi tena kuingilia au kuhoji kinachoendelea na wenye leseni huwa huru kuuza au kuikodisha sehemu wenye leseni nayo kwa mwengine bila ya shaka yeyote atalipwa dau kubwa kuliko gharama za leseni na serikali huwa inakodoa macho tu. wateja wanauziana rasilimali za nchi kama yao na hakuna wa kuwahoji sijui kama hawana viwanja vya ndege ndani ya maeneo yao ambayo wataruka kuelekea nchi jirani bila ya kupingwa.