Habari Njema - Je Mnayajua haya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari Njema - Je Mnayajua haya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Nov 21, 2008.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wabunge mliomo JF ,jamii inahitaji maelezo juu ya miradi hii iliyoambatanishwa hapa chini ,ilianzishwa lini ,imefikia wapi na nani mhusika Mkuu Serikali au mafisadi.

  1) Lake Rukwa Uranium project.
  2) North Bahi Uranium Project.
  3) Bahi Uranium Project.
  4) Kiwira Uranium Project.
  5) Njombe Uranium Project.
  6) Ruhuhu Uranium Project.
  7) Morogoro Uranium Project.
  8) Rufiji Uranium Project.
  9) Mbinga Uranium Project.
  10) Tunduru Uranium Project.
  11) Mkuju Uranium Project.
  Miradi hiyo kumi namoja hapo kuna lisence zaidi ya mia moja na ukienda kwenye miradi 13 ya dhahabu kuna license kama hamsini ,WaTz wanafaidika vipi na leseni hizi mikataba gani ilitumika kutowa lisence hizi na je leseni zote zina faida kwa Taifa hili masikini japo ni tajiri.

  Hivi hayo hapo juu ni utajiri unaochimbuliwa kwa kuambiwa ni project lakini kuna tetesi kuwa uchimbwaji wa Uranium upo na unafanyika ndani ya Tanzania ,wasiwasi nilionao ni moja ya hizo Project hapo juu ambayo imekuwa ikitajwa Kiwira kama mradi wa Dhahabu lakini hapa inaonekana ni mradi wa kubukua Uranium.
  Mwenyezi Mungu ametupa utajiri wa Uranium sielewi kwa nini bado Mtz analala gizani.Hata wanyama wetu wangefaidi barabara zote mikoani vijijini na mwituni zingejaa nuru,wacheni kusingizia mvua,mvua imetubeba mpaka inaonekana sasa kuchoka

  Hiyo ni miradi kumi na moja iliyochawanyika Tanzania nzima."UK companies have invested about £230 million in Tanzania over the last 11 years..." Katika miaka hii kuminamoja wazungu wanatupa sentensi isemayo Uranium not proven hivyo uhakika wa uchimbaji bado ,Je wabunge wetu mnaosimamia wananchi kuwepo uhakika kuna hitaji muda gani miaka mingapi ,mkizingatia siku hizi hatua za uchunguzi ziko mbele na za kisasa zaidi ,au uhakika wa kuwepo kwa Uranium unahitaji miaka mingapi ? Hizi longolongo za Wazungu wakati wanatuibia kwa kutuimbia mahesabu za uhakika
  ,natumai wapo WaTz wanaoelewa kabisa ukweli na huenda wamo katika machimbo husika ndani ya mikoa au miji iliyotajwa ,watu hawa watavumilia mpaka lini wakati ukweli kuwa Uranium ipo na inachimbwa na kuchukuliwa.
  Nikiwarudia Wabunge wetu ,nawauliza hawa wazalendo wanaoonekana kufuatana na wazungu ndani ya machimbo ni WaTz au ni wa kutoka nchi jirani ila tumefanana kwa rangi.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Very interesting to know the status /progress of those ''projects''! Sikujua before kama kuna list ndefu hivyo ya uranium projects, including Wilayani kwangu!
   
 3. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135

  Duh... this is eye opening kwa kweli maana hata mimi nilikuwa kizani kabisa....
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ukienda wizara ya madini unapata full data kwa kuanzia tembelea stamico iko upanga hiyo
   
 5. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #5
  Nov 21, 2008
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160

  Tutafuatilia kujua maendeleo ya miradi hii. Kitu kimoja tu muhimu ni kwamba Leseni hotelewwa kabla ya mikataba. Leseni za kutafuta madini na baada ya madini kugundulika na vigezo kutumia ndipo mkataba hufuata. Kwa miradi yote hiyo bado ni utafutaji. Sasa kujua utafuutaji umefikia wapi ngoja tufuatilie, may be a parliamentary question!
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Na sio ulifikia wapi ,bali ulianza lini ,na kukamilika kwake ni muda gani ,je kipimo chake kwa maendeleo ya kidunia yalipofikia ni jambo nadhani lisilohitaji muda mrefu kujua.

  Kuna msemo unaosema chelewa chelewa utamkuta mtoto si wako ,ni msemo wetu,miradi hiyo pengine haipungui chini ya miaka kumi na moja,watu wanachunguza tu !!

  Vievile kuna kihio cha kudili na kampuni moja tu, nilichokiona kuwa behind kampuni ambazo zinaonekana ni za wazalendo ,hao wapo kama tawi tu ili kurahisisha mambo kwa wazungu ,catalyst wakati wahusika wakuu wapo nje huuza hupanga na kugaiana mapande.wakipangiana %.
  Je ndugu zetu wabunge kwa uchache Tz inahitaji au Serikali yetu itahitajika asilimia ngapi katika kugawana na muwekezaji.
  Nimeona katika kampuni ya Wiliamson au Mwadui Mines serikali inapata asilimia 25% na wazungu wanaondoka na 75%
  Inasemekana kampuni hii ilianzishwa 1940 au 1925 na hadi leo imeshachimba kilo 3800 za almasi (19 million carats).
  Huu mradi umekuwa wakupokezana na sasa wanao Petra ambapo wanachukua 75% na Serikali kuambulia 25% ,jamani makampuni yapo mengi tu ,natumai kama itawekwa tenda na kugawana angalau serikali iwe inapokea 50% basi lazima wateja watakuja tena kwa makundi na wengine wakiahidi kuipatia serikali zaidi 50%.
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Tusiwe walafi. Neno lilotumiwa ni project bila kuainisha ni project ya aina gani. Wengi wa hawa bila shaka ni speculators na hamna la maana linaloendelea. Mtu kuchukua leseni hakumlazimishi kuendeleza anachodai kukusudia. Unaweza kukuta wengi wa hawa jamaa wamechukua hizo leseni kwa nia ya kuja kumuuzia mwenye uwezo hapo baadae. Kusema kuwa uranium inachimbwa lakini sisi hatujui ni kuwa disingenuous. Haya madini soko lake ni limited na si kama rubies au Tanzanite. Hauwezi kuchukua uranium katika mkoba na kwenda nayo Dubai kutafuta soko! Kama inachimbwa, ni lazima inafanywa hivyo kwa ridhaa ya serikali. Kama nilivyosema mwanzo, tusiwe walafi wa kupenda kuvuna tusichopanda.

  Amandla....
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  ? may start operating a mine in Tanzania's central Bahi region within two years, Chief Executive Officer said. Studies conducted at Manyoni, about 80 kilometers west of the capital, Dodoma, in the Bahi region show an inferred resource estimate of 6,900 metric tons of uranium oxide, said in an interview today in the commercial capital, Dar es Salaam. "These are very shallow deposits so we expect it to be low-cost and relatively simple to process," "We would like to start producing in that region in 2010."

  Sasa ujanja hapa ni wa kuondoka na mifuko ya rambo wakidai ni sample wakati wakifanikiwa kuondoka na gramu 500 tu basi wako mbali pengine warudi na madai ya uchunguzi unahitajika kwa miaka mingine zaidi. Huku tunaisabu miaka. Kwa nini zisitumike states kampuni za uchina ambao uchunguzi na kila kitu kitafanyika ndani ya nchi badala ya kuondoka na sampuli kwenye vigunia ,tuamkeni mambo ya kuchukuliwa mali ya asili na kwenda kufanyiwa uchunguzi na ukarabati nchi za nje ni wizi wa kimachomacho ,yaani wataalamu wetu wanaona jamaa wakiondoka na vigunia eti vya mchanga.

  http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/2477367.stm Imesemwa inatoka nchi jirani lakini Tz drilling zinafanya kazi hivyo kama waTz walikuwa wanne na Mkongo mmoja ,huoni unga huo wa manjano unaweza kuwepo na kupatikana ndani ya Tz ikiwa kuna miradi 11 , Mkuu Dadi hatujui aliishia vipi na watuhumiwa hao ,kama kuna mtu alijua kesi ile iliishia wapi atujuvye .
   
 9. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama itakuwa ni ulafi mtu anapotaka kujua status ya mradi fulani ambao upo Tanzania, nafikiri ni haki ya watz kujua nini kinaendelea kwenye miradi hiyo! Halafu hizo leseni wanazo pewa zinakuwa na exclusive rights kwenye eneo fulani au sio, kama ni ndiyo...hawa wanaohodhi hizo leseni bila ya kuendeleza hiyo miradi husika ndio walafi wanazuia other upcoming & potential investors kwenye miradi hiyo, ambao wanaweza kuwa na uwezo wa kuifanya miradi husika itake off mara moja!

  Hao wenye leseni halafu hawaiendelezi eti wanasubiri kuja kuiuza kwa potential investors, nawafananisha na mafisadi waliochukua viwanja vingi kwenye miji mikubwa like DSM, halafu hawaviendelezi na kuzuia wananchi wenye hitaji hasa la hivyo viwanja, lakini hawawezi kuvipata kwa sababu tu vimehodhiwa na walafi wachache!
   
 10. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hapa, Mkuu unataka kusema nini? Huyo C.E.O ni nani? Huyo Cottle ni nani? Hawa wanasema they MAY start operating a mine within two years, leo ushaanza kuulizia tunafaidika vipi? Hawa kama kweli walikuwa na nia ya kuibia serikali wangefanya hizo interviews ambazo unanukuu? Kwani uranium inathamani kuliko dhahabu kiasi cha mwekezaji achimbe uranium akidai kuwa ni dhahabu?

  Hapana, Mkuu. Kwangu mimi bado taarifa yako inanitatiza.
   
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Tunakawaida moja ya kuona kila mtu anataka kutudhulumu. Kuulizie status ya mradi si kosa bali ni wajibu. Lakini hii habari imeletwa kana kwamba kwenye hizi projects zote uchimbaji ushaanza na watu wanakwapua hiyo uranium. Inabidi tuwe realistic na tusi-overreach. Tunatakiwa kuwa makini kuliko tulivyo hivi sasa.

  Speculation, ingawa inatia kinyaa, ni sehemu ya biashara. Ni sisi ndio tunaotakiwa kuweka sheria na mipango ya kufanya gharama ya ku-speculate inakuwa kubwa kiasi kuwa haiwi worth it.
   
 12. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Bado tuko kule kule. Hauwezi kuondoka na sample ya uranium katika kifuko cha rambo. Hauwezi kutegemea mwekezaji akubaliane mgawane 50/50 kwa sababu tu madini yanapatikana kwako! Ukitaka mgawane kiasi hicho wekeza fedha zako katika utafutaji na uendelezaji wa madini hayo. Ndivyo ilivyo.
   
 13. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hapo Fundi tuna kwenda sawaaaaaaaaaaaa!!!
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  The Right Projects, the Right Area, the Right Time & the right people (Mafisadi).Wateja.
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  Nov 21, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Naona unazusha mabishano mifuko ya rambo haimaniishi asili ya kitu hicho,ni lugha ya uandishi tu nikimaanisha usafirishaji,na ukiangalia usafirisha ni katika hali ambayo hapajakuwa na usafishaji au utenganisho ni kitu raw kama Kamanda Dadi alipowakamata watu ni mchanga tu wa manjano katika vipolo.
  Hebu nipe maana ya haya maandishi yanayofuata:-

  The projects are held in two partnership arrangements:

  Has signed a farm in agreement for five of the licences whereby their partner can earn 40% by spending A$2 million (US$1.6 million) in 2 years, and a further 20% by spending another A$2 million. ? has a free carry.

  The remaining 3 licences and 2 pending applications are held in a 42.5% ? with ? (also 42.5%) and a local businessman(Mafisadi) (15%).
  Recent exploration results have been favourable. At Mtonya several anomalies have been identified along a 7km strike and assay results from grab samples have yielded high grade uranium; in the best case it was 55,600 parts per million (5.56%). More representative are the results from the channel samples which in the majority of cases ranged from 0.1%-2.2% uranium.

  Sasa hawa watu ambalo kwangu naona ni tatizo ni kuondoka na hizi sampuli kila kukicha na kurudi na data,ni muda gani wanaochukua hadi tufaidike na matunda haya. Hili ndilo hasa ninalotaka kulijua weka kando utitiri wa makampuni na leseni wanazopata na dili zao ,sisi wahusika tunafaidika vipi au tutafaidika lini ,tusikae na kuwatazama wao wakija na kuondoka na viroba vya sampuli maana urahisi wa kuona unavyoibiwa huwepo kwenye mafuta lakini kwenye madini ni rahisi sana. Hivi ni miaka mingapi wanahitaji hadi kuanza kufukua na kupata product yenyewe ?
   
 16. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #16
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Uranium inapatikana kwa wingi kuliko tunavyodhani na kwa vile matumizi yake ni specialised, haina bei kubwa sana. Kilo moja ya uranium oxide ni US dola 163.1 na uranium inauzwa kwa US dola 192.4 kwa kilo. Wakati huo dhahabu inauzwa kwa dola 24,360.62 kwa kilo. Sasa mtu kweli achimbe uranium halafu aseme kuwa ni dhahabu!

  Hatari iliyokuwepo, nionavyo mimi, si sisi kudhulumiwa bali ni kwa hiyo uranium kuishia mikononi kwa watu waovu. Hawa hawana interest na source iliyokuwa sustainable bali ni kupata kiasi cha kutosha kutengeneza kabomu cha kuweza kukatengua Time Square. Hao ndio wa kuwahofia.
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Lakini unaiona hiyo bei ni ndogo ila kwenye black market ina bei mbaya sana sana kuliko dhahabu ,na ndio ukaiona ipo well controlled kuliko dhahabu.na kuisafisha kwake inakubidi upate waraka kutoka UN kwenye kamati ya nguvu za nyuklia,hivyo bado naona inathamani kuliko dhahabu.
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Siwezi kutafsiri maana kuna ? nyingi mno. Nionavyo mimi hata hayo makampuni yanayodai kuwa ni ya wawekezaji nazo ni za speculators. Hawa wanaingia ubia na hawa wazao kwa matumaini kuwa wataweza kuya-convince makampuni makubwa kuwanunua. Tatizo letu ni kuwa kwa sababu ya kupenda majibu marahisi tunakaribisha vijikampuni uchwara kutoka nje ambavyo vinatuahidi tunachokitaka na mwishoni kujikuta tumeliwa. Speculators si wazawa tu hata huko nje wako. Kama nilivyokuweka bei ya uranium, hautaweza kupata utajiri kwa kubeba kwenye rambo, viroba au ndoo za plastiki. Mwekezaji gani wa maana anazungumzia kuwekeza Australian dola milioni mbili kwa miaka miwili ili apate dola 800,000? Kupenda kwetu vya haraka haraka ndiko kunakochangia kwa kiasi kikubwa kuumizwa kwetu.
   
 19. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #19
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Sasa hapa unazungumzia kumuuzia Osama. Sisi kama nchi hatuwezi ku-base projections zetu kwenye bei ya kumuuzia Osama kwenye black market! Badala ya kudai mgao, tukigundua kuwa kuna watu wanafanya hivyo inabidi tuwapeleke mbele ya sheria. Kama vile ambavyo tukimkuta mtu anauza viungo vya Albino. Vyote ni criminal activities.
   
 20. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #20
  Nov 21, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Explaration inachukua muda mrefu sana. Ni wajibu wa serikali kupitia Wizara ya Madini na Nishati kutoa elimu kwa umma kuhusu hili.

  Ni mambo ya kitalaamu ambayo yanahitaji ufafanuzi wa kina. Watu wakiona mwekezaji anasafirisha sample za mchanga kupeleka Australia au Canada kwenye maabara wanasema kwamba anaiba madini!
   
Loading...