PreGE2025 Habari Leo waondoa taarifa ya Makalla kuwatuhumu CHADEMA kutaka kusambaza Ebola, wasema haikuwasilishwa kwa usahihi

PreGE2025 Habari Leo waondoa taarifa ya Makalla kuwatuhumu CHADEMA kutaka kusambaza Ebola, wasema haikuwasilishwa kwa usahihi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
2,786
Reaction score
7,567
Wakuu,

Hawa walitaka usahihi gani wakati Makalla ametamka hayo loud and clear? Walitaka aelezee nini tena ndio waiweke?

Wameiondoa sababu CHADEMA hawajajibu? Kwahiyo CHADEMA wakikaa kimya inaondoa the fact kwamba Makalla ametamka upuuzi huo?

Pia soma: Pre GE2025 - Makalla: CHADEMA wanataka kuingiza Ebola Tanzania ili wazuie uchaguzi!

Halafu CHADEMA na nyinyi mnafeli, yaani mnataka kufungulia kesi gazeti huku mnamuacha Makalla aliyewapa tuhuma hiyo? Hii inaingia akilini kweli?

Sawa ni gazeti la serikali, mnataka kuona action huko, vipi huyu Makalla? Yeye aende off the hook kwakuwa mmeamua kutarget gazeti?

Mnatukoroga tu!

Baada ya haya yote tunakuja kusema kuna uhuru wa vyombo vya habari nchini? Yaani bado sijaelewa huo ufafanuzi wametoa mpaka sasa!

IMG_20250323_230345_277.jpg




Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Back
Top Bottom