PreGE2025 Habari Leo waondoa taarifa ya Makalla kuwatuhumu CHADEMA kutaka kusambaza Ebola, wasema haikuwasilishwa kwa usahihi

PreGE2025 Habari Leo waondoa taarifa ya Makalla kuwatuhumu CHADEMA kutaka kusambaza Ebola, wasema haikuwasilishwa kwa usahihi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Oh, walitaka reaction!! Kimya ni jibu zuri sana kwa mjinga. Unamwacha na maswali mengi yanayomkosesha amani!

Tanzania nchi yangu, waliokupigania uwe huru wangeamka leo wakuone..... 😭😭😭.
 
Kila nikitafakari uwezo wa huyo mwenezi nashindwa kuielewa sisiem, eti wanataka kuingiza virus vya ebola, ni kichaa peke yake ndio anaweza kumwelewa huyu zumbukuku. Hayo madaraka mnayopewa yatumieni kwa akili. Madaraka hayo yasiwalevye. Tumieni hekima na busara mnapotoa kauli zenu. Zaidi naona mnajivua nguo tu na kuonyesha jinsi gani hamjakomaa kisiasa
Hali suala nikifikiria namna walivyodeal na COVID-19, Mpox na Marburg, unaona kabisa kuna trend fulani ya denial, na conspiracy theories zinaongoza maamuzi ya wanasiasa kudeal na majanga ya kiafya, kitu ambacho ni hatari sana. Mfano COVID-19 ingekuwa virulent kama strains wa mwanzo kabisa nchi hii ingepukutisha wanacho wengi hata zaidi. Hata Marburg inaonekana ililazimika kuweka jitihada kubwa sana kufukia gap ku-catch-up na rate ya ugonjwa kusambaa kwenye jamii.

Sinaga mashaka kabisa na watalam wa afya wa nchi hii, wanaweza ila wako kimya mno, sidhani hawa wanasiasa wanaambiwa ukweli kuhusu ugonjwa, nahisi kuna hali ya kudownplay hatari wasiumize hisia za wakuu wao. Hii inapelekea response kuwa late sana, na slow. Huwezi kudeal hivi na hatari inayogusa nchi nzima. Ukifeli unaweza kufeli mazima! Watu wengi walikufa kwa COVID-19 kwa kuwa walikuwa misinformed.
 
Back
Top Bottom