Habari leo: Mbowe, Makonda waongea, na mifugo ikatwe kodi!

OGTV

JF-Expert Member
May 22, 2016
353
167
1. Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda amesema tayari wametenga bajeti ya kuwarudisha ombaomba wa mtaani makwao na wataoendelea kupatikana mtaani watafungwa jela.

2. Mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni amepinga vikali kitendo cha Magufuli kuzuia watu kusema amesema unapozuia watu kusema unasababisha watu kusema kwa vitendo na wakisema kwa vitendo vitendo hivyo vinakuwa vya uvunjiiu wa Amani.


3. Mbunge Ally Kessy ametaka mifugo kama mbwa, kuku,mbuzi na vitu kama baiseli vilipiwe kodi.
 
Hahaha,aisee Kessy ni kituko
Sasa mbwa hawa wa mitaani lishe yenyewe tata,si ndio watachekelea kukamatwa ili wakale bure.
Ila amesahau na Njiwa pia walipiwe kodi,sasa kwenye kukamata inabidi iwe usiku aisee
Ila watuambie hawa kunguru waiba chupi nao walipe kodi,sasa sijui nani atalipa,maana wanakera kinoma
 
Nchi za wenzetu vipi, wanakusanya kodi ktk kila kitu km mbunge huyu anavo dai iwe Tz, wenye data mnijuze, maana nafikiria km n ivo, tungekusanya fedha nyingi za kuendesha nchi yetu bila hata misaada ya nje km tutakusanya kodi kwa kila kitu
 
Nchi za wenzetu vipi, wanakusanya kodi ktk kila kitu km mbunge huyu anavo dai iwe Tz, wenye data mnijuze, maana nafikiria km n ivo, tungekusanya fedha nyingi za kuendesha nchi yetu bila hata misaada ya nje km tutakusanya kodi kwa kila kitu
Kama milo mitatu kwa siku inatushinda tutaweza kulipa kodi zote hizo?
 
Ni rahisi kutamka kwa kessy lakn tujiulze vyanzo vya mapato vmeisha kweli mpaka hivyo
 
Milo mitatu, chini ya dola moja ina maana gani? Hizi kauli tata zinamsaidia nini mwananchi wa Mwakaleli Mbeya au Matai Sumbawanga
 
Heading imekaa kisiasa...irekebishwe.

Walau isomeke hivi....

Habari leo: Mbowe, Makanda waongea. Mbunge adai na mifugo ikatwe kodi.
 
Waanze kufuatilia mikataba ya gas na madini na utalii waache usanii ndiyo kuna hela
 
YAANI PESA NINAPATA MOJA ILA INAANGALIWA NA WENGI

1.kodi ya pango ninapoishi
2.umeme
3.maji
4.kuchangia usafi
5.usafiri kwenda kazini
6.kodi ya kazini kwangu
7.umeme
8.maji
9.mlinzi
10.tra
11.leseni
12.omba omba
13.chakula kazini
14.chakula nyumbani
15.mavazi
16.mbwa kuku paka
17.king'amuzi
18.transaction Mpesa
19.hospitality
20.vibaka
21...
22...
23..
24.
 
Sio kosa la uyo mbunge ndio uwezo wake umefikia hapo! Wkt wana kuna mabilion yanaporwa kwy madini,gesi,mahotel ya kitalii,watu wanadecleare loss kila mwaka ili wasilipe kodi,yeye anawaza kodi ya mbuzi,kuku,bata,paka,mbwa Huuu ni udhaifu wa kufikiria uliotukuka.
 
Ni baada ya wandishi uchwara wa NIPASHE kumdhihaki RC huyo Mchapakazi katika serikali ya awamu ya tano.
IMG-20160627-WA0012.jpg.jpeg
 
Back
Top Bottom