Jumuiya ya kimataifa yashtushwa na tamko la Makonda kuhusu ushoga

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Balozi wa Umoja wa Mataifa anaye simamia Haki za Binadamu Michelle Bachelet Ijumaa amesema ameshtushwa na tamko la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwamba kuna kamati itakayo undwa kufuatilia na kuwakamata mashoga, na kuwahamasisha watu kuripoti wale wanaoshukiwa kuwa mashoga.

“Watu wajinsia moja wanaofanya mapenzi nchini Tanzania tayari wamekuwa wanakabiliwa na ongezeko la uvunjifu wa amani, kubughudhiwa na kubaguliwa kwa kipindi cha miaka 2,” Balozi Bachelet amesema. “Na wale wanaojitetea haki zao kupata huduma za afya, kuishi maisha huru yasiyo kuwa na ubaguzi, uvunjifu wa amani na kukamatwa bila hatiya wameendelea kulengwa na hata kukamatwa.”

“Hili limegeuka kuwa ni kumtafuta mchawi na inaweza kutafsiriwa kama ni leseni ya kuendesha vitendo vya uvunjifu wa amani, kunyanyasa, kubughudhi na kuwabagua wale wote wanaohisiwa kuwa ni mashoga.”

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amewatoa hofu jumuiya ya kimataifa pamoja na Watanzania na wanadunia kwa ujumla na kuwashauri kuwa ingekuwa vyema kupata taarifa kutoka kwenye chanzo chenyewe, kuhusiana na kusakwa na kukamatwa mashoga.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Sauti ya Amerika amelaumu kuwa jumuiya ya kimataifa imekuwa ikichukua taarifa kutoka kwa watu yumkini ni washirika au wana maslahi binafsi na jambo hili husika, na hivyo wanatengeneza mazingira ambayo siyo juu ya zoezi hili.

Serikali ya Tanzania iwajibike

Bachelet amesisitiza kuwa serikali ya Tanzania itekeleze wajibu wake wa kulinda haki za binadamu za wananchi wote katika ardhi yake, ikiwemo kuwawajibisha watu ambao wanahamasisha chuki na ubaguzi na wale wanafanya vitendo vya kuvunja sheria. Serikali inawajibika kuhakikisha kuwa wanaotetea haki za binadamu, waandishi wa habari na wanaotoa huduma ya afya wanaweza kufanya kazi zao muhimu, bila ya kudhuriwa au kubughudhiwa.

Mpango uliotangazwa na serikali unahusisha jaribio la kile kinachosemwa kuwa ni “kuwatibu” mashoga - kitendo kinacho laaniwa kama ni chenye madhara, kinyume cha maadili na hakina hoja ya kisayansi kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

“Naitaka serikali na wananchi wa Tanzania kusimamia haki za binadamu ya kila mtu nchini, bila ya kujali ni kina nani au wanawapenda,” Bachelet amesema. Viongozi wa kisiasa, kidini na wengine wanawajibu wakupambana na vitendo vya ukandamizaji venye misingi ya utambulishi na mwenendo wa kijinsia.

Balozi huyo pia ametaka kupitiwa tena sheria zinazo toa adhabu kwa watu wa jinsia moja walioridhia kuwa na mahusiano yakimapenzi.

Sheria ya Tanzania

Mkuu wa Mkoa huyo amesisitiza kuwa anafuata sheria ya nchi inayokataza tendo la kutembea na mtu kinyume cha maumbile.

“Sheria hiyo imeweka wazi kabisa kwamba mtu anayefanya hivyo akibainika na akithibitika ni kifungo cha maisha au jela miaka 30,” amesema.

Ameongeza kusema kuwa: “ nchi ya Tanzania haijakubali kwamba ni nchi inayokubali mashoga, na hata katika tamko la haki za binadamu, sisi hatujachukuwa ushoga ni sehemu ya haki za binadamu, vinginevyo sheria hii isingeweza kuwepo iwapo ushoga ni sehemu ya haki za binadamu.”

“Tuwaulize hao wanao tutangazia haki za binadamu, ni haki kutusambazia mambo yenu ya faragha. Kwa sababu sasa hivi kama ninavyo ongea tayari kuna watu wamekwenda mahakamani, ambao wao wamefanyiwa kinyume cha maumbile, hawakuridhika wakaamua kujiripoti....”

Amekemea wale wanaotetea watu wanaoharibu kizazi, akisema ingekuwa ni vyema jambo lako la faragha libaki kuwa la faragha.

“Na ndiyo vita iliyoko kati yetu na hawa watu, kwa nini msifanye mambo yenu faragha mnayofanya na mnayatangaza mpaka kwenye dunia kwa watu ambao hawahusiki,” “Kwa nini mnataka watoto wetu waone mambo yenu ambao hawako hata katika umri wa kujua mambo hayo, amehoji Makonda.

Watu 47,000 watuma taarifa za mashoga

Makonda amesema mpaka Ijumaa wananchi wasiopunguwa 47,000 wametuma taarifa juu ya matokeo mbalimbali.

“Zoezi hili haliko kwa ajili ya kumwinda mtu au kumharibia mtu heshima yake, na ndio maana taarifa zote tulizopewa kama serikali bado zinafanyiwa kazi, na wale wanaotaja majina wataitwa kwenye vituo vya polisi, kuja kufafanua.”

Mkuu wa Mkoa amesema kuhusu zoezi la kupimwa: “Watu wanataka kwenda kupimwa kwa sababu mpaka hivi sasa tunavyo ongea kuna takriban mashoga wasiopungua 200 wanaotaka kuacha biashara hiyo ya ushoga na wanaomba msaada."

Ameeleza kuwa tayari mkoa umeandaa timu ya madaktari pamoja na wanasaikolojia wakiwasaidia kuwapa ushauri nasaha ili watoke kwenye kundi hilo la ushoga.

Chanzo: VOA-Swahili
 
Mbona kama ni haki za binadam yeye hajaolewa na mwanamke mwenzie. Au yeye sio binadam kamili. Hata kama hio sheria ya kuyakataza hayo isingekuwepo bado tuna imani za dini, dini ambazo wametuletea hao hao zinakataza huo ufedhuli. Je tufuate imani za dini au sheria zao?
 
CDM lazima waungane Na hiyo mzungu! The so called ugandamizaji wa democracy/Liberty
 
Mbona kama ni haki za binadam yeye hajaolewa na mwanamke mwenzie. Au yeye sio binadam kamili. Hata kama hio sheria ya kuyakataza hayo isingekuwepo bado tuna imani za dini, dini ambazo wametuletea hao hao zinakataza huo ufedhuli. Je tufuate imani za dini au sheria zao?

Verónica Michelle Bachelet Jeria
She is Surgeon and former president of Chile

1541206763197.png

1541206827596.png
 
Hapa nipo upande wa Makonda,
Kama jamaa hawawezi kutupa misaada mpaka tuwaache mashoga ngoja tufe njaa.
Na lau ingekuwa rai yangu mimi,basi ningeshauri wote wauawe
 
Mimi naona tuwe SERIOUS KABISA, tufute kabisa na UNAFIKI koko.

"Tukatae MISAADA YOTE na MIKOPO tunayopewa na hawa WAZUNGU kwasababu PESA wanazotupa NI KODI ZA WATU WAO wakiwemo MASHOGA, WASAGAJI na WACHEZA PORN"

Tufukuze hata mabalozi wao.
 
There is only one Lawgiver and Judge, the one who is able to save and destroy. But you—who are you to judge your neighbor?
 
Mkuu wa Mkoa amesema kuhusu zoezi la kupimwa: “Watu wanataka kwenda kupimwa kwa sababu mpaka hivi sasa tunavyo ongea kuna takriban mashoga wasiopungua 200 wanaotaka kuacha biashara hiyo ya ushoga na wanaomba msaada


Kwahiyo kama wanataka kuacha watakuwa hawajatenda kosa na wala hawatatakiwa kwenda mahakamani kama sheria inavyotaka
 
Mbona Bashite kajieleza fresh tu, hao mashoga wanaojitangaza mitandaoni na hawa kina Amber Ruty wanaosambaza video ndo wanaponza wenzao. Japo Ushoga ni tabia iliyolaaniwa na haipaswi kuungwa mkono, ila sheria zake ziangaliwe ukimfunga shoga miaka 30 ujue hyo ni ndoa yake ya mkataba na manyapara kwa miaka hyo
 
Ninachokiona mimi hapa...
Kuna uwezekano hizi harakati za kuwasaka hao wapenzi wa jinsia moja... Ndio ukawa mwanzo wa kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja...

Ngoja tuone mwisho wake...
 
Fatuma Karume (Aunt) huku ndiko anatoa Ruzuku ndiyo maana wanapambania hili. Yani niwe na mtoto wa kiume eti analiwa kiboga? Walaaah bora nimchinje. maana ata kumtoa sadaka Mungu hawezi kuikubali sadaka ila nitamkashoggi.
SHUBABIITIII.....
 
Back
Top Bottom