Habari! Kwanamna gani unaweza kuomba ufadhili wa kusomeshwa au kufadhiliwa masomo kwenye NGO Kama help to help

Kama uko huko Arusha fuata maelekezo yafuatayo;

UFADHILI - NAFASI ZA MASOMO - BURE Chuo cha Ufundi cha Help to Self Help kilichopo SAKINA - JIJINI ARUSHA kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu tunatekeleza programu ya kukuza UJUZI kwa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa miezi 6 kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 - 35. Mafunzo haya YANAFADHILIWA na SERIKALI kwa ADA yote kulipwa na SERIKALI KWA ASLIMIA 100. Fomu zitaanza kutolewa na zitapatikana chuoni HELP TO SELF HELP kuanzia tarehe 19 Aprili hadi 30 Aprili 2021. Masomo yataanza tarehe 17 Mei 2021. KOZI ZITAKAZOTOLEWA NA SIFA ZAKUJIUNGA 1. Umeme wa Majumbani Sifa: kidato cha nne au zaidi 2. Upishi Sifa: kidato cha nne au zaidi 3. Ushonaji Nguo Sifa; darasa la saba au zaidi Fika chuoni SAKINA - ARUSHA kwa maelezo zaidi KWA MAWASILIANO YA KUCHUKUA FOMU - HELP TO SELF HELP VTC Piga simu zifuatazo; 0744 666 685 au 0744 666 680 Kwa maelezo zaidi tembelea katika tovuti zifuatazo; www.kazi.go.tz www.hsh.or.tz

KAMA UKO NJE YA ARUSHA, WAPIGIE KWA HIZO NAMBA UPATE MSAADA ZAIDI.

Kila la heri mdogo wangu.
 
Back
Top Bottom