Habari katika picha: Kilichojiri Arusha Jan 5, 2011

Habari katika picha: Kilichojiri Arusha Jan 5, 2011

Kwa yale yaliyotokea Arusha na hali ya kutotii mamlaka za sheria zilizowekwa. Hii yaonyesha kabisa kuwa haki hivi sasa mahala pake pa kupatikana si mahakamani tena bali ni kwa njia ya maandamano na kufanya fujo. Kama sababu ya maandamano yale kama ilivyoelezwa na F. Mbowe kuwa ni kuhusu uchaguzi wa meya wa arusha, haina msingi, kwani wangeenda mahakamani ndipo haki ingepatikana sio kupoteza roho za watu ambao hawana hatia bure.

CHADEMA wamedharau umma wa watanzania na kukaidi kuiamini mahakama ndio yenye kutoa haki.

Aliyekwambia CHADEMA waliandamana ni nani?
 
CrapBrain ndio maana wewe ni mshauri wa Makamba aka mzee wa pumba!!

Nimemuona Mzee makamba leo kwenye foleni, analala lala tu kwenye lile li-mV8 lake; namba.........BKW!!!

Mzee anapaswa lumpumzika yule.
 
Jina lako (Jeykey=JK) linafanana na mawazo yako. Usitutishia kuona damu, ni vitu vya kawaida kwa mtaka haki.
 
Vurugu za arusha zimeleta mafanikio sana hata ulimwengu umefahamu kuwa ccm hawapendi kuleta mabadiliko kwa amani. Lowasa aliwashauri makamba akachonga oh! Pelekeni mahakamani. Anajua mahakamani watachakachua kesi lakini wenye akili wakagundua ndiyo maana waliamua kuandamana ili kutafuta haki kwa kutumia majukwaa. Mahakama ni kama choo cha ccm
 
Hapa naona kuna shida katika kufikiri, inaonyesha kuna watu wanatumia midomo kutizama, kinadharia jimbo la Arusha unapozungumza habari ya idadi ya wajumbe utagundua kuwa CCM wao ni wachache, na hakuna namna yoyote ambavyo wangeweza kushionda kiti kile kama siyo kufanya hujuma/rafu na kujitwalia mamlaka hayo. Kama CCM Wanajiamini kabisa na ni wapenda amani watangaze rasmi leo kuwa uchaguzi utafanyika na wajumbe wapewe taarifa kwa Barua ya muda na wapi mkutano wa uchaguzi utafanyika na tuone kama kutakuwa na vurugu.

Pia nataka kukuambia ndugu yangu Genius kuwa matusi si hoja na kama wewe una benefits unazo pata huko tafadhali sana tumia akili sana namna ya kuwasilisha hoja zako.

CCM - (ChakaChua Matokeo) mnapaswa kujua msemo huu
Ukila na Kipofu usimshike Mkono
Ninawapongeza CCM kwa kipindi chote ambacho mliwezakuvumilia kula bila kumshika kipofu mkono ila bahati mbaya sasa mmemgusa pabaya! Anataka kujua huyu naye kula naye ni nani?
 
safi sana hii ndo namna ya kuwatia discipline wapuuzi kama hawa wanaotumiwa na wanasiasa kama chambo..tena nina uhakika katika maandamano yote hawakuwepo vijana wasomi..wenye uwezo wa kupinga ama kuunga mkono jambo fulani kwa hoja sio nguvu....
Hata kama watu wamevunja sheria hawapaswi kutendewa namna hii,
Watu wanaoshabikia kama wewe hawafai kwenye jamii, wanatakiwa kuondolewa kwenye watu wema ili wasiambukize wengine. Jirekebishe haraka.
Lazima tujenge jamii ya watu wenye akili ya kujua jema na baya kwa kutumia reasonable means/force!
 
hawa polisi nnawachukia kinoma na hawa bungeni hakuna kuwasaidia kuwekea mazingira mazuri, bajeti yao lazima tukwamishe wahuni hawa
 
Kwa yale yaliyotokea Arusha na hali ya kutotii mamlaka za sheria zilizowekwa. Hii yaonyesha kabisa kuwa haki hivi sasa mahala pake pa kupatikana si mahakamani tena bali ni kwa njia ya maandamano na kufanya fujo. Kama sababu ya maandamano yale kama ilivyoelezwa na F. Mbowe kuwa ni kuhusu uchaguzi wa meya wa arusha, haina msingi, kwani wangeenda mahakamani ndipo haki ingepatikana sio kupoteza roho za watu ambao hawana hatia bure.

CHADEMA wamedharau umma wa watanzania na kukaidi kuiamini mahakama ndio yenye kutoa haki.
Mlalamikiwa mkuu ni JK, huyu huyu JK ndiye kamteua na kumwapisha Jaji mkuu ambaye ndiye mkuu wa mahakama. Je unategemea huyu anayemlalamikia JK apate haki kwa huyu mteule wake?
 
kwa yale yaliyotokea arusha na hali ya kutotii mamlaka za sheria zilizowekwa. Hii yaonyesha kabisa kuwa haki hivi sasa mahala pake pa kupatikana si mahakamani tena bali ni kwa njia ya maandamano na kufanya fujo. Kama sababu ya maandamano yale kama ilivyoelezwa na f. Mbowe kuwa ni kuhusu uchaguzi wa meya wa arusha, haina msingi, kwani wangeenda mahakamani ndipo haki ingepatikana sio kupoteza roho za watu ambao hawana hatia bure.

chadema wamedharau umma wa watanzania na kukaidi kuiamini mahakama ndio yenye kutoa haki.

haki inapiganiwa, hakuna atakayekuletea haki kwenye sahani
 
Do not tell us where right can be obtained! We know more than you LAYMAN. nikikuuliza haki ni nini unaweza kunijibu? Au unadandia mada usizo na ujuzi nazo?? Acha tutumie nguvu za umma kwani tumechoka kuchezewa mchezo wa kuigiza. Kama mnadhani mna haki miliki ya kuongoza nchi hii mtakavyo SORRY YOU ARE MISTAKEN. mwisho wenu unakuja tena kwa kasi kubwa kuliko ilivyotarajiwa! Tunaikomboa nchi yetu na tukwenda mahakamani kuwapeleka hao mafisadi kwa maovu yao. Kumbuka hawa: Nicholae Chausescu (Romania), Agustino Pinocet (Chile), Iddi Amini (Uganda), Mobutu SeseSeko (Congo), then JK na mafisadi wake (Tanzania) tutawashtaki just wait
icon8.png

Kama hujui na tena ndio LAYMAN , tutafanyaje sasa kama hujui ? inabidi tukueleweshe sasa. Nakushangaa wewe unayejifanya kujua haki hujui kama mahakamani ndiko haki inapatikana na tena ni muhimili mwingine wa nchi, pole sana kijana mbona unalia machozi kiasi hicho
 
Mlalamikiwa mkuu ni JK, huyu huyu JK ndiye kamteua na kumwapisha Jaji mkuu ambaye ndiye mkuu wa mahakama. Je unategemea huyu anayemlalamikia JK apate haki kwa huyu mteule wake?

Kwa hiyo ulitaka jaji mkuu achaguliwe na Slaa ? soma katiba. Ndio maana nasema wanachama wa CDM ni watu wasio jua kitu mnabisha
 
Hapa naona kuna shida katika kufikiri, inaonyesha kuna watu wanatumia midomo kutizama, kinadharia jimbo la Arusha unapozungumza habari ya idadi ya wajumbe utagundua kuwa CCM wao ni wachache, na hakuna namna yoyote ambavyo wangeweza kushionda kiti kile kama siyo kufanya hujuma/rafu na kujitwalia mamlaka hayo. Kama CCM Wanajiamini kabisa na ni wapenda amani watangaze rasmi leo kuwa uchaguzi utafanyika na wajumbe wapewe taarifa kwa Barua ya muda na wapi mkutano wa uchaguzi utafanyika na tuone kama kutakuwa na vurugu.

Pia nataka kukuambia ndugu yangu Genius kuwa matusi si hoja na kama wewe una benefits unazo pata huko tafadhali sana tumia akili sana namna ya kuwasilisha hoja zako.

CCM - (ChakaChua Matokeo) mnapaswa kujua msemo huu
Ukila na Kipofu usimshike Mkono
Ninawapongeza CCM kwa kipindi chote ambacho mliwezakuvumilia kula bila kumshika kipofu mkono ila bahati mbaya sasa mmemgusa pabaya! Anataka kujua huyu naye kula naye ni nani?

Hakuna mtu aliyewasilisha hoja kwa matusi , ni nyie mnao jibu ndio mwajibu kwa matusi. Hapo ndipo ninapo pata walakini na uelewa wa wanachama/mashabiki/wapenzi wa CHADEMA
 
mjue yakuwa wa tanzania wa leo sio wale!!!!!!!!! We know our rights na hiyo haki soon itatuweka huru na ccm yenu!!!!!!!! Mbona mwanza hamjafanya fyoko? Tena tulikuwa tumejipanga kuangamiza, oleeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!

CHADEMA inaongoza Halmashauri 6 tu kati ya Halmashauri 133, ni sawa na asilimia 4.5, zinazobakia ni za CCM wanaongoza ambazo ni sawa na asilimia 95.5. Hebu chambua hapo !
 
Aliyekwambia CHADEMA waliandamana ni nani?

Mliandamana na mie mwenyewe niko hapa Arusha niliona. Acheni kuruka kivuli chenu , mmewashawishi watu wasio kuwa na hatia kuwafanya kafara kama mtaji wenu wa kisiasa. Kweli chadema si chama ni genge la watu wenye maslahi yao binafsi kama alivyosema SHIBUDA
 
CHADEMA sio Chama makini hata siku moja na wafuasi wake nina wasiwasi ni MA*****RA kwani hawajui watendalo wala wafanyalo , mambo ya bendera kufuata upepo hayo, pole sana kwa kuwa mbuzi wa kafara bana ! mtauliwa sana safari hii .

Halafu unajiita genius brain?Kwa mawazo hayo yasiso na maana,hivi unajua kweli hata maana ya genius au umejiita tu?
 
Samahani kwa kukuita stupidbrain (showing a lack of intelligence, perception, or common sense). To me you will never sound genius with such kind of thinking. Unapaswa kujua kuwa CHADEMA wamepokwa ushindi, sio tu wa Arusha, bali pia Ubunge na udiwani maeneo mengi (sina sababu ya kuyataja kwa sasa kwakuwa najua wajua). Trend inaendelea, kila CCM wanapotumia hila kupora ushindi ndivyo wanavyojipanga kutumia mbinu zaidi kwa maeneo mengine. Kimsingi wanapora ushindi na utawala bora wa wananchi. Wanataka CHADEMA waende mahakamani (unakotaka wewe pia) ili kesi ichukue miaka mitano ilihali meya feki akiendelea na kumaliza muda wa kuwakandamiza wananchi. Mahakama kama walivyoonyesha polisi wanafuata amri ya CCM, wao ndio wanaojiita chama tawala. Wanatawala nchi katika kila nyanja. Hakuna haki huko wewe unakoita mahakamani. Haki (walau kwa sehemu) inatafutwa, hailetwi. Katiba ya nchi, pamoja na mapungufu tunayoyapigia kelele inatoa haki ya kutoa maoni. Katika maandamano kinachotakiwa ni kutoa taarifa. Sio kutafuta ruhusa. Polisi hawana haki ya kutoa ruhusa ya maandamano. Uzuiaji wa maandamano kwa polisi unakubalika kikatiba tu pale ambapo imethibitka kutakuwa na uvunjifu wa amani. Narudi inapothibitika kutakuwa na uvunjifu wa amani. Mwema hakutupa uthibitisho wa uvunjifu wa amani. Taarifa alizoziita za kiinteligensia ni amri kutoka kwa wakubwa wake (CCM). Chadema wameandamana kwa amani (kama kukutanika kwao ni kuandamana). Polisi wamewaletea fujo ili litimie walilosema siku moja kabla. Najua ya kwamba haya yote huwezi kuyafikiri hata kama yanahitaji common sense tu. Ndio maana kamwe sitakuhisi kuwa u genius. To me you a gread STUPID (refer my definition of stupid provided early)
 
Mliandamana na mie mwenyewe niko hapa Arusha niliona. Acheni kuruka kivuli chenu , mmewashawishi watu wasio kuwa na hatia kuwafanya kafara kama mtaji wenu wa kisiasa. Kweli chadema si chama ni genge la watu wenye maslahi yao binafsi kama alivyosema SHIBUDA

Una ushaidi kwamba watu walishawishiwa waje?Kwani walifuatwa majumbani mwao?
 
Genius brain vp? Ugenious umezd hadi unachizika au imekuwaje? Kumbuka chadema walikuwa na kibali from nowhere polisi akabadilika gafla na kusema hakuna maandamano. Sasa najiuliza alipokuwa anatoa kibali alikuwa kalewa or ana hangover! Nafkr baada ya kuzinduka ndo kaöna ndivyo sivyo.
Hata Makamba haipatikani.
 
Back
Top Bottom