Haaaa!! Baada ya kuoa na kupata kazi brazza kimyaa

Haaaa!! Baada ya kuoa na kupata kazi brazza kimyaa

Mpigamsuli

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2012
Posts
3,885
Reaction score
584
Wakuu nina kakayangu mmoja ana miaka39 ,kasomea ARUSHA Msingi mpaka sekondari kipindi anasoma sekondari alisomeshwa kwa gharama kubwa sanaaa , advance(a-level)kasome dsm kamaliza form6 mwaka 1996, akaingia chuokikuu mwaka 1998 mwaka 2001 kamaliza degree yake ya kwanza , mnamo mwaka 2003 alipata kazi nzuri sanaa ,akapata mke akaoa hakumjulisha mamayangu kwamba anaoa , akapata watoto hakumwambia mama bali ni mjomba wangu(kaka wa mama yangu) ,ndiye aliyemwambia kwamba kaka yangu ameoa na anawatoto watatu ,sasa basi huyu kakayangu hana mawasiliano kabisa na mama yangu ,sasa hapa tatizo lipo wapi ni huyu mwanamke aliyemuoa au tatizo ni kuwa na kazi nzuri na kutusahau kabisa mama yangu ,maana hata nyumbani hataki kuja ,mimi mdogo wake wa mwisho sina namba namba yake na hana habari na mimi ,tunatamani sana kaka yetu kumuona akija nyumbani kwetu lakini hataki wakuu , tatizo linaweza kuwa nini wakuu au tayari kashawekewa limbwata(kizizi) na huyo mkewake ?
 
Kuna kitu mama yako aliwaikumfanyia kibaya we chunguza usitoe lawama kesi hizo huku uchagani nyingi mno inafika wakati hata ndugu yake anakufa yeye anaweza asije
 
Mkakamate mpelekeni kwa kakobe,mtkila au masanja mkandamizaji akaombewe! Huwezi kutomjali bi mkubwa wako kama una akili timamu! Halaf kaka yako ni member humu jf
 
Mkakamate mpelekeni kwa kakobe,mtkila au masanja mkandamizaji akaombewe! Huwezi kutomjali bi mkubwa wako kama una akili timamu! Halaf kaka yako ni member humu jf

ni member wa jf?? anaitwa nani mkuu
 
^^
Kuna sababu usiwe mwepesi wa kufikiri unavyofikiri..chunguza
^^
 
Huyo itakuwa Mkewe kamacomvise Maza wako kigagula, anataka kutoa kafara au kumchukua msukule! Haji hata mmfanyaje! Kwa akili zake anaona aje mumle nyama!!!!!!! Thubutuuuuuuuuuu!

Wanume mkeo akikwambia twende kwenye maombi gani sijui muwe macho sanaaa! Inaishiaga kuambiwa mama yako na ndugu zako ndo wachawi wakubwaa, wangekuua ungechelewa kwenda huko, blah blah blah! Ndugu zako wewe tu ndo washirikina wa mkeo watakatifu je na uwasaidie sanaa! Hio ni trick tu ya wanawake kuwatengeni na ndugu zenu! We wasikuue ukiwa kachanga help less, unawatia shoti tu za maziwa, nguo na chakula waje wakuloge umeisha Bingo si watakuwa punguwani!!!!!!!!!!
 
Kuna kitu mama yako aliwaikumfanyia kibaya we chunguza usitoe lawama kesi hizo huku uchagani nyingi mno inafika wakati hata ndugu yake anakufa yeye anaweza asije
akuna kitu kibaya ambacho mama anaweza kukufanyia nawe ukamsahau hvyo....katika ukuaji wake hata yey kuna kitu kibaya alishawah mfanyia mama yake lakini mama yake hakumuacha bali alizidi kumpenda kama mtoto.....kwangu mim hyo siyo sababu ya kumfanya hamsahau mama yake kiasi hicho...
 
hapa majibu tunayotoa ni ya kubahatisha kulingana na maelezo lakini ulipaswa kujua zaidi hata upande mmoja wa mama angalau hata picha kidogo unaweza kupata.
BACK TO TOPIC.
huyo kaka yako ni JEURI sana,haiwezekani akaoa na mama asimwambie,kwani wazazi wangapi hawapatani na watoto wao lakini sherehe ikifika tofauti zinawekwa pembeni,kwa picha ya maelezo kaka yako ni adui kwa mama yako,mana muda wote aliweza kutuma taarifa kwa mjomba wenu katika muda muafaka na kila tukio muhimu lakini hakuona maana yoyote ya kutuma taarifa kwa mama,why????????Majibu ni siri ya kaka yako kwa nini alifanya hayo.
Kuhusu limbatwa sikubaliani na hiyo hoja kwa sababu
hakuna mwanamke anaekupa limbwata hata hujamuoa ili azuie hadi wazazi wako kupata taarifa kuwa mwanao anaoa ama kaoa,mambo na matukio ya limbwata huja baadae inapopita ndoa ndio mtu anabadilika.
Mimi nimejaribu hivi.
 
^^
Kuna sababu usiwe mwepesi wa kufikiri unavyofikiri..chunguza
^^
naomba nikuulize kuna kitu gani ambacho mama yako anaweza kukufanyia ....nikakufanya umsahau hvyo...hata kumtumia hela ya chumvi....hata kumtaarifu kama unaoa mpaka asikie kwa mtu.......
 
Poleni sana. Kama familia inaumiza kumkosa ndugu yenu.

Haijalishi na sidhani kama kashawishiwa na mke. Ila sasa cha kufanya, wewe soma. Mungu yupo na utatoka tu. Msaidie mama na kumfariji. Wakati wa Mungu ukifika atakuja mwenyewe kuwatafuta. Kama mkiweza kumpata kwa simu ama hata barua mumpigie na kumuambia mnampenda. Katu msimuombe hela kwa sababu undugu ndio muhimu hapo.
 
mh,samahanai lkn,huyo mke wake kabila gani!?......haiwezekani kumsahau mama yako! na hyo mwanamke ana akili kweli?anaona sawa tu?. haiwezekani,there must b something wrong kwa hyo mwanamke
 
Atakuwa siyo kakako wa damu wala siyo mtoto wa mamako!! Chunguza kisha tupe updates!!!
 
hata mama awe mbaya kiasi gani haitofikia hatua ya kumsahau,,hebu fikiria miezi 9 aliyokuweka tumboni,amekuzaa kwa uchungu,amekesha usiku mara ngapi ukiwa unadeka mikononi mwake,amekosa amani kila ukipoumwa,amekusaidia hadi ulipofikia utu uzima ndo uone mama mbaya,what a pity!!?? KAKA MDOGO WAKO AMEANDIKA KWA UCHUNGU HADI NA MI NIMEHUDHUNIKA,,pliz hakuna kama mama hapa duniani,hope utasoma ujumbe na kumuomba mama msamaha!
 
naomba nikuulize kuna kitu gani ambacho mama yako anaweza kukufanyia ....nikakufanya umsahau hvyo...hata kumtumia hela ya chumvi....hata kumtaarifu kama unaoa mpaka asikie kwa mtu.......

^^
sister japo mtoa mada hajaeleza kwa kina,,ila nadhani kuna mambo matatu
1.MABADILIKO YA MAJUKUMU
Inatokea sana kabla ya mwanaume kuoa hujali sana watu wa kwao.Ila anapooa basi majukumu yote ni kuhakikisha familia yake anaitimizia mahitaji.Hapa kuna jambo kuwa inawezekana ni kwa muda mfupi tu hapigi simu,hajali au vingnevyo tayari ukoo umeona pengine mke ni mbaya.Kuhusu kutotoa taarifa ukumbuke kuna wanaume wachache hufanya usiri unaopindukia ktk mambo yao.
2.KUKAMATWA KINAMNA
Inawezekana mke kaja amejipanga vilivyo kwa kutumia sayansi isiyoonekana.
Na ndio maana yote yanatokea na badae hata ndugu watafukuzwa wakienda kumtembelea..yeye ndiye anajua ampende nani amwache nani.
3.NANI MTAWALA?
Hutokea wakati mwingine bila dawa,,ukampata mwenza akawa na strong affection (huba zito) kiasi cha yule wa pili kuishi maisha yake yote kwa kutii amri.Hili huanza kati ya siku 1 hadi 21 ya mwanzo wa ndoa.
sister yote haya yanahitaji kuangaliwa
^^
 
Last edited by a moderator:
mh,samahanai lkn,huyo mke wake kabila gani!?......haiwezekani kumsahau mama yako! na hyo mwanamke ana akili kweli?anaona sawa tu?. haiwezekani,there must b something wrong kwa hyo mwanamke

Ni mtu wa iringa
 
Huyu brazza tunasikia tayari kashajenga nyumba ila mimi binafsi sijui hata anakaa wapi kiukweli mjomba ndiye anayetuambia/anayetupa taarifa zake
 
Back
Top Bottom