Haaaa!! Baada ya kuoa na kupata kazi brazza kimyaa

Haaaa!! Baada ya kuoa na kupata kazi brazza kimyaa

Huyu brazza tunasikia tayari kashajenga nyumba ila mimi binafsi sijui hata anakaa wapi kiukweli mjomba ndiye anayetuambia/anayetupa taarifa zake

Mtumie huyo huyo mjomba kujua what is wrong with him kwani mjomba yuko well informed na yupo naye karibu kiasi cha kutosha.
 
naomba nikuulize kuna kitu gani ambacho mama yako anaweza kukufanyia ....nikakufanya umsahau hvyo...hata kumtumia hela ya chumvi....hata kumtaarifu kama unaoa mpaka asikie kwa mtu.......

Mimi mwenyewe nimeshangaa sana, hata kama mama amefanya makubwa vipi, husamehewa,mimi nimeona kijana mmoja mama yeke ni kigwagula , na huyo kijana alikuwa anaishi ujerumani na ameoa mzungu akija hapa Dar anafikia kwa mjomba wake, anaacha watoto na mkewe, yeye peke yake ndiyo anakwenda kumsalimu mama yake, ukimuuliza anasema heri aniuwe mm kuliko wanangu. na licha ya hivyo kamjengea nyumba kubwaaa na kila kitu ndani , ila hapeleki watoto wake pale home.Sasa huyo hata hela ya chumvi hapeleki wala mawasiliano, Mhhhhhhh!!! Inanishangaza.
 
hyo sababu ya 1&3 sikubaliani nayo kabisa....mwanaume jua waZi kabisa hata ukija kuoa mama yako bado ni jukumu lako....kuna watu unaweza usiwasaidie labda kuwe na shida ya muhimu kabisa.....lakini wazazi wako bado ni jukumu lako unapaswa kuwatunza mpaka pale Mungu atakapowaita mbele ya haki.........
na hyo sababu ya 2 may be lakini pia haina uzito........mwombe Mungu akupe mwananke ambaye atakusaidia kukukumbusha kuhusu wazazi wako mana wanaume wengi wanajisahau.....wakati sis wanawake piga ua lazima mwisho wa mwezi mama apate hata 200 ya kunununulia chumvi....
 
kazi kweli kweli
kaka yenu ni wa kwanza? au ni mwanaume wa kwanza? kama jibu ni ndiyo basi huyo ni lango hakuna linaloweza kufanyika vizuri bila ya yeye kutolewa kwa Bwana inahitajika sadaka ya kukombolewa hivyo mwambie mama akaonane na padre au mchungaji atamwambia cha kufanya ila huwa hakuna cha kutisha ni ibada ya kawaida unatakiwa uwe na sadaka inayouma. baada ya hapo mengine yanaweza kuendelea.
inawezekana kwa kiasi kikubwa amekamatwa na mizimu tena ya kwenu wala hajalongwa.
 
^^
sister japo mtoa mada hajaeleza kwa kina,,ila nadhani kuna mambo matatu
1.MABADILIKO YA MAJUKUMUF
Inatokea sana kabla ya mwanaume kuoa hujali sana watu wa kwao.Ila anapooa basi majukumu yote ni kuhakikisha familia yake anaitimizia mahitaji.Hapa kuna jambo kuwa inawezekana ni kwa muda mfupi tu hapigi simu,hajali au vingnevyo tayari ukoo umeona pengine mke ni mbaya.Kuhusu kutotoa taarifa ukumbuke kuna wanaume wachache hufanya usiri unaopindukia ktk mambo yao.
2.KUKAMATWA KINAMNA
Inawezekana mke kaja amejipanga vilivyo kwa kutumia sayansi isiyoonekana.
Na ndio maana yote yanatokea na badae hata ndugu watafukuzwa wakienda kumtembelea..yeye ndiye anajua ampende nani amwache nani.
3.NANI MTAWALA?
Hutokea wakati mwingine bila dawa,,ukampata mwenza akawa na strong affection (huba zito) kiasi cha yule wa pili kuishi maisha yake yote kwa kutii amri.Hili huanza kati ya siku 1 hadi 21 ya mwanzo wa ndoa.
sister yote haya yanahitaji kuangaliwa
^^
mwe nimekujibu ila nimesahau kuku quote hapa..
 
Last edited by a moderator:
Mimi mwenyewe nimeshangaa sana, hata kama mama amefanya makubwa vipi, husamehewa,mimi nimeona kijana mmoja mama yeke ni kigwagula , na huyo kijana alikuwa anaishi ujerumani na ameoa mzungu akija hapa Dar anafikia kFwa mjomba wake, anaacha watoto na mkewe, yeye peke yake ndiyo anakwenda kumsalimu mama yake, ukimuuliza anasema heri aniuwe mm kuliko wanangu. na licha ya hivyo kamjengea nyumba kubwaaa na kila kitu ndani , ila hapeleki watoto wake pale home.Sasa huyo hata hela ya chumvi hapeleki wala mawasiliano, Mhhhhhhh!!! Inanishangaza.
bora huyo mama kidogo ameonja matunda ya huyo mtoto...ila huyu ni janga.....unawezaje kumsahau mama kiasi hicho.........akuna ambacho mama anaweza kukufanyia usimsamehe na kuamua kumlipizia........
 
kazi kweli kweli
kaka yenu ni wa kwanza? au ni mwanaume wa kwanza? kama jibu ni ndiyo basi huyo ni lango hakuna linaloweza kufanyika vizuri bila ya yeye kutolewa kwa Bwana inahitajika sadaka ya kukombolewa hivyo mwambie mama akaonane na padre au mchungaji atamwambia cha kufanya ila huwa hakuna cha kutisha ni ibada ya kawaida unatakiwa uwe na sadaka inayouma. baada ya hapo mengine yanaweza kuendelea.
inawezekana kwa kiasi kikubwa amekamatwa na mizimu tena ya kwenu wala hajalongwa.

Yeye ndio wa kwanza 1974 ,dada yangu 1978 ,kaka mwingine ,na mimi ndio wa mwisho
 
hyo sababu ya 1&3 sikubaliani nayo kabisa....mwanaume jua waZi kabisa hata ukija kuoa mama yako bado ni jukumu lako....kuna watu unaweza usiwasaidie labda kuwe na shida ya muhimu kabisa.....lakini wazazi wako bado ni jukumu lako unapaswa kuwatunza mpaka pale Mungu atakapowaita mbele ya haki.........
na hyo sababu ya 2 may be lakini pia haina uzito........mwombe Mungu akupe mwananke ambaye atakusaidia kukukumbusha kuhusu wazazi wako mana wanaume wengi wanajisahau.....wakati sis wanawake piga ua lazima mwisho wa mwezi mama apate hata 200 ya kunununulia chumvi....

^^
Unachosema ni sahihi 100% ila ukumbuke pia tukilinganisha mwanaume na mwanamke baada ya ndoa..MWANAMKE hukumbuka nyumbani zaidi kuliko mwanaume.
Pia kila mmoja huomba Mungu apate mke au mume mwema,,hakuna anaependa matatizo ila ndo ivyo wakati mwingine unapewa aliyekadri ya uwezo wako.
^^
 
^^
Unachosema ni sahihi 100% ila ukumbuke pia tukilinganisha mwanaume na mwanamke baada ya ndoa..MWANAMKE hukumbuka nyumbani zaidi kuliko mwanaume.
Pia kila mmoja huomba Mungu apaFte mke au mume mwema,,hakuna anaependa matatizo ila ndo ivyo wakati mwingine unapewa aliyekadri ya uwezo wako.
^^
okay....ni kitu gani ambacho nyie wanaume kinawafanya msikumbuke nyumbani baada ya kuoa....natamani kujua hilo ili niache kuwashangaa....
 
...akivunjika mguuu atarudi zizini (home) akichechemea...
 
mizimu itakuwa inamshikilia unajua walifanya nini wakati wa kuzaliwa kwake? kama walifanya tambiko lolote ujue ni lango la mizimu sasa kinachotokea yeye mila hafanyi na kujitenga nazo hajafanya hivyo lazima itasumbua.
 
Atakuwa siyo kakako wa damu wala siyo mtoto wa mamako!! Chunguza kisha tupe updates!!!
Munkari, ningekubaliana na wewe hapo kwenye Bold tu kama hata mjomba asingeshirikishwa, kumbuka huyu mjomba tumeisha ambiwa ni kaka wa mama yao.
 
Lol..pole sana mkuu ila omba Mungu sana amfungue kakaako amefungwa huyo. Haiwezekani mtu umsahau mama yako kiasi hicho, Mama ni mama huwezipata mwingine kama yeye.
 
Huyu brazza tunasikia tayari kashajenga nyumba ila mimi binafsi sijui hata anakaa wapi kiukweli mjomba ndiye anayetuambia/anayetupa taarifa zake

Nikuulize maswali haya, baba yenu ni mmoja??
Kujenga kwake nyumba ya kuishi yeye na familia yake ni tatizo kwako wewe binafsi??
Kwa kipindi hicho anasoma alikuwa anasomeshwa na nani na alikuwa anaishi wapi?
Akiwa sekondari na chuo alikuwa anaenda wapi likizo?
Nakushauri wakati fulani ujaribu kuingia ndani ya viatu vyake na ufikiri kwa umakini ni nini kinaweza kuwa sababu ya yeye kufanya hivo!

Kisaikolojia zaidi; Inawezekana kuna maisha fulani amekuwa akiyaishi kwa kipindi kirefu cha kutafuta maisha ambayo nyinyi kama wanafamilia hamkuwa mkifahamu kabisa na hamkuonekana kuhitaji kujua au mama na ndugu zake wa karibu hawakuwa karibu naye, hiyo ilimfanya ajione kuwa yuko peke yake, no one around. Kama alikuwa katika hali hiyo then ndani ya moyo wake kuna kitu kama , "I've been alone during my struggle, i'll be alone during my success!"

Kwako wewe binafsi, usifikirie sana kuwa he is responsible for your life, u'r responsible for ur life dude! Leo amejenga nyumba unalalamika, kesho akinunua gari utalalamika, akipeleka wanae shule nzuri utalalamika. Take it easy, kama mjomba wenu anajua kila kitu kuhusu maisha ya kaka yako then fikiria why uncle not you and your family?
Kuhusu mke wa kaka yako naona sio sahihi kumuingiza katika mahusiano mabovu ya kaka yako na familia yenu, as kaolewa na kaka yako hajaolewa na ndugu wa mume wake, she is innocent on this!
 
Huyo itakuwa Mkewe kamacomvise Maza wako kigagula, anataka kutoa kafara au kumchukua msukule! Haji hata mmfanyaje! Kwa akili zake anaona aje mumle nyama!!!!!!! Thubutuuuuuuuuuu!

Wanume mkeo akikwambia twende kwenye maombi gani sijui muwe macho sanaaa! Inaishiaga kuambiwa mama yako na ndugu zako ndo wachawi wakubwaa, wangekuua ungechelewa kwenda huko, blah blah blah! Ndugu zako wewe tu ndo washirikina wa mkeo watakatifu je na uwasaidie sanaa! Hio ni trick tu ya wanawake kuwatengeni na ndugu zenu! We wasikuue ukiwa kachanga help less, unawatia shoti tu za maziwa, nguo na chakula waje wakuloge umeisha Bingo si watakuwa punguwani!!!!!!!!!!
Leo umekuja tofauti na nilivyokuzoea ila umegusa IKULU kabisa tena nimefurahi zaidi kwa kuwa umeusema ukweli japo unawananga wanawake wenzako.... Ni hatari sie pia tuna ndugu yetu kapotezwa kabisa ila tunamwomba mungu kuna siku atamwashia taa auone ukweli ili awe huru.
 
okay....ni kitu gani ambacho nyie wanaume kinawafanya msikumbuke nyumbani baada ya kuoa....natamani kujua hilo ili niache kuwashangaa....

Ushawishi wa baadhi ya wanawake wasio na malezi ambao wanaamini baada ya kuolewa wamemchukua mwanamme na hana familia tena ila wao wana ndg na familia inayohitaji msaada ktk ndoa yao. Huu ni ubinafsi na uhuni ambao unatoka hata kwa ushauri wa wazazi wa wanawake. Nina shuhuda chache za hali hii ila tuache mada iendelee kwani nyingine inahusu familia yangu kabisa.
 
Back
Top Bottom