Kova amekukuluka awezavyo lakini kaambulia patupu.Kova kanyoosha Mikono?
Kazi ya watumishi wa mungu ni kuonya na kukemea.piga kazi mtumishi.
Katumiwa vipi na wanasiasa? Wanasiasa wepi? Mimi najiuliza anawezaje kutumika na Lowasa, Nape na Slaa kwa wakati mmoja? Mbona hawa wana misimamo tofauti? Fafanua kidogo hapo.Kama anamaanisha anachojkisema na kweli kinatoka rohoni mwake, tunamkaribisha sana. Na historia inaonyesha hivyo kuwa viongozi wa dini walikuwa na msuguano na viongozi wa siasa pale ambapo mambo watawala ( wanasiasa ) walipindisha mambo. Lakini nahisi Askof Gwajima hana muda mrefu katika kujishughulisha na mambo haya zaidi ya kuhubiri enjili tu. Ameibuka ghafla na kufika mbali kama vile
anapewa data na mtu fulani ( remote control ) na kama hivi ndivyo ilivyo namsihi atambue shida na matatizo ya watanzania kwa usahihi wake kuliko kutumiwa na wanasiasa.
Kwanza nashukuru kunipa wakati wa kujibu hoja yako kwa hoja na si vingenevyo., nianze na mipaka ya viongozi wa dini mipaka yao inaanzia kwenye imani zao na kuishia kwenye imani zao hapo hapo na huku tunakuita kuzielekeza imani zao kwa msingi wa kiroho wa waumini wao tofauti na hapo ni kuvuka mipaka na kuanza kutenda jambo ambalo si jema kwenye jamii, ikija kuzungumzia siasa na maisha ya binadamu hapa unazungumzia muono wa wanadamu kuchagua viongozi wa kuaongoza juu ya mambo yao ya kimaisha hapa utakutana na masuala ya viongozi kuomba ridhaa kwa wanainchi ya kuwaongoza na baada ya kushika hatamu hawa wanainchi wanabaki kuiheshimu mamlaka waliyokwisha kuiweka soma warumi 13;1
KWELI Gwajima anaitawala hii nchi
Ameitwa na MKUU wa wilaya amegoma tena kamwambia ameitupilia mbali barua yake ya wito na wala hapotezi muda wake kumfuata bali atamjibu kwa maombi ya mnyororo.
Amepewa notices zaidi ya mara tatu na national housing cooperation amegoma kuhama na bado anadunda.
Police wamemfungulia mashtaka ya ajabu ajabu ambayo ni rahisi sana kuona mwisho wa kesi hizo zilivyonyepesi na bado anadunda.
Lazima Gwajima ana kitu cha tofauti.
Tafakari.
Yeye mwenyewe hajanyooka, kuwalamba waumini wake tena wake za watu kanyooka vip
Weweee, usimdanganye Gwajima, Mabwepande siyo mchezo. Una hakika malaika wa Gwajima wana uwezo wa kuwashinda wale jamaa? Msimtakie balaa Mtumishi wetu.Hakika umenena mtu wa Mungu. Na mimi kwa kuongezea kwenye thread yako iliyojaa ukweli; hapo kwenye namba 2, nabii aliyemwonya Ahabu anaitwa MIKAYA (1Wafalme 22:1 - 40).
Na hapo kwenye namba 5, tuseme waziwazi kwamba hao vijana Daniel,Shedrack,Abedinego na Meshaki walitakiwa kuuwawa na watawala kwa sababu walikataa kumsujudia
mfalme na lisanamu lake. Lakini Mungu aliwaokoa na kuwatoa kwenye viwanja vya vifo. (Daniel 3:8 - 27) na (Daniel 6:4 - 24)
Gwajima usiogope kuwakemea watawala watawalao vibaya
kondoo wa Mungu. Hata wakikutupa kwenye msitu wa Mwabwepande, Mungu atatuma malaika wake kuja kukuokoa maana Mungu habadiliki. Usihofu mtumishi wa Mungu. Simama katika haki na hakika katiba pendekezwa ni
janga la kitaifa. imeandikwa na mwenyekiti wa mafisadi nchini,yaani mzee wa vijisenti na joka la...
Napingana na wewe kwa hili, kama kukemea maovu ni kazi ya watu wa Mungu basi Mungu hatamuacha nabii wake aanguke kwa wakati asioutaka yeye. Atakae taka kumuangusha atangamia yeye. We tulia angalia movie iendelee ili TUJUE ALIEKEMEA NA ANAYEDAI katukanwa nani kafanya kazi ya Mungu kwa kete iliyoko uwanjani.Ni heri kukaa kimya na kufanya kile kinachokuhusu kuliko kuendelea kupayuka yasiyobeba uhalisia na yenye makengeza mengi....!!
Kuna mkakati unaandaliwa wa kufutia usajili taasisi za kidini na vyama vya kijamii vinavyojihusisha na siasa, Gwajima anaweza kuwa mhanga namba moja
Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima,amesema haogopi mtu yeyote wala kufa bali ataendelea kuinyoosha nchi anapoona haiendi sawa.
Alitoa kauli hiyo Dar es Salaam juzi,wakati wa mahubiri yaliyofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe.
Alisema uhusiano wake na watu mbalimbali wakiwamo wanasiasa utaendelea kubaki palepele.
Kwa mujibu Askofu Gwajima, baadhi ya watu wamekuwa wakimhusisha kuwa na urafiki na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa jambo ambalo alikiri ni la ukweli kwa sababu walifahamiana tangu mwaka 1996.
"Niliwahi kumuita Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara nne hapa ili aje azindue moja ya kazi zangu,hakuja badala yake nilimuita Lowassa na aliitikia wito wangu na kuja kuifanya kazi hiyo hivyo siwezi kumuacha.
"Wapo viongozi wengi ambao wanakuja kusali katika kanisa langu, kwa mfano Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye, kwa nini wasimseme yeye badala yake wanamsema Lowassa tu?.
"Nashangaa mnatoka mlipotoka mnaongea kwa kubana pua, ukimuogopa mtu nchi itakuwa haiendi vizuri na mimi sitaogopa kukemea mambo ambayo hayafai katika jamii, mfano suala la Escrow.
"Nitaendelea kuinyoosha nchi ninapoona haiendi sawa.
"Siwezi kwenda mbali na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbrod Slaa hata kama atakuwa Rais… na yeye pia ni rafiki yangu," alisema Askofu Gwajima.
Wiki iliyopita, Askofu Gwajima alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mashitaka mawili ambayo ni kumtolea lugha ya matusi ambayo imemfedhehesha Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, na kuweka vibaya silaha anayomiliki.[/QUOT
ndio uzuri wa jf, unabadili ID unakuwa mpya, unashusha vitu..
pinda yupo nyuma ya hili ,lengo ni kumdhoofisha gwaijima kwakuwa anamuunga mkono Mzee wetu Lowasa .
atashindana lakini hatashinda.
hebu fafanua hapo kwenye maandishi meusiKova mwenyewe anamhahaha! Sembuse Makonda. Gwajima ni kiboko ya wapuuzi kama kova.
askofu ahubiri dini sio siasa, maovu tutaamua kwenye uchaguzi nani tumpe uongoziKila la heri Askofu. Endelea kukemea maovu yaliyokithiri ktk nchi hii.
Weweee, usimdanganye Gwajima, Mabwepande siyo mchezo. Una hakika malaika wa Gwajima wana uwezo wa kuwashinda wale jamaa? Msimtakie balaa Mtumishi wetu.