Gwajima: Nitaendelea Kuinyoosha Nchi Ninapoona Haiendi Sawa!

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,830
Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima,amesema haogopi mtu yeyote wala kufa bali ataendelea kuinyoosha nchi anapoona haiendi sawa.

Alitoa kauli hiyo Dar es Salaam juzi,wakati wa mahubiri yaliyofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe.

Alisema uhusiano wake na watu mbalimbali wakiwamo wanasiasa utaendelea kubaki palepele.

Kwa mujibu Askofu Gwajima, baadhi ya watu wamekuwa wakimhusisha kuwa na urafiki na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa jambo ambalo alikiri ni la ukweli kwa sababu walifahamiana tangu mwaka 1996.

“Niliwahi kumuita Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara nne hapa ili aje azindue moja ya kazi zangu,hakuja badala yake nilimuita Lowassa na aliitikia wito wangu na kuja kuifanya kazi hiyo hivyo siwezi kumuacha.

“Wapo viongozi wengi ambao wanakuja kusali katika kanisa langu, kwa mfano Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye, kwa nini wasimseme yeye badala yake wanamsema Lowassa tu?.

“Nashangaa mnatoka mlipotoka mnaongea kwa kubana pua, ukimuogopa mtu nchi itakuwa haiendi vizuri na mimi sitaogopa kukemea mambo ambayo hayafai katika jamii, mfano suala la Escrow.

“Nitaendelea kuinyoosha nchi ninapoona haiendi sawa.

“Siwezi kwenda mbali na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbrod Slaa hata kama atakuwa Rais… na yeye pia ni rafiki yangu,” alisema Askofu Gwajima.

Wiki iliyopita, Askofu Gwajima alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mashitaka mawili ambayo ni kumtolea lugha ya matusi ambayo imemfedhehesha Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, na kuweka vibaya silaha anayomiliki.
 
Tunahitaji watu wanaokemea maovu katika taifa. Tangu zamani waonyaji walikuwepo na siku zote hawakuwa watu wa kupendwa sana. Wote waliokemewa walisaga meno na kutafuta namna ya kuwaua kwa sababu ya viburi na kujiona wao ni miungu wasiopaswa kuonywa hata wakikosea. Walisahau kwamba yuko Mungu mmoja aliyezifanya mbingu na nchi. Lakini katika halakati zote zile, wako waliopoteza maisha na wapo walioishi ila mwisho wa yote Mungu alijitwalia utukufu. Mifano michache sana.

1. Yohana Mbatizaji aliyekatwa kichwa kwenye birthday ya mtoto wa mfalme kwa sababu tu mke wa mfalme alimchukia kwa kuonywa, na hivyo kumwagiza binti yake aombe kichwa cha Yohana Mbatizaji kama birthday gift!.

2. Mfalme Ahabu aliyekufa vitani kwa sababu ya kukataa sauti ya Nabii mmoja wa Mungu aliyemwambia ukweli lakini yeye Ahabu, akaamuru akamatwe na kuwekwa jela kwa sababu hamtabilii mazuri. Badala yake akaenda vitani kwa ushawishi wa majitu manafiki yaliyokuwa yamemezunguka naye kwa ujinga akaamini kwamba 'sauti ya wengi ndiyo sauti ya Mungu". Lakini ahabu alikufa sawa na Nabii mmoja wa Mungu alivyonena wala yale manafiki hayakumwokoa badala yake yalibakia yameduwaa kama mehu!.

3. Ninaona Nabii Eliah pia, aliwindwa kuaawa kwa sababu alikuwa tofauti na watawala. Muda wa Mungu ulipokuwa umewadia, ilijulikana ni nani Mungu wa Kweli kati ya Yahweh na Baal!. Mungu Yahweh, hajawahi kushindwa.

4. Bwana Yesu Christ, pamoja na kwamba ilikuwa lazime afe kifo cha aibu ili alipe fedheha na adhabu ya dhambi za ulimwengu, lakini katika shauri lake, walitafutiza mashitaka ya uwongo kwa sababu "aliwaambia maneno ya kwei yaliyochoma mioyo yao". Mob iliitikia "asuribiwe, asurubiwe" na hata wakadirki kutamkoa maajabu kwamba damu yake na iwe juu yao na juu ya watoto wao kwa sababu walimchukia juu ya kweli wala hakuwa na hatia!. Yesu hakuwa na umati mkubwa wa binadamu upande wake, lakini matokeo yake ni Utukufu Mkuu wa Mungu ambao hauelezeki.

5. Daniel. Shadrack na Abednego. Kumbuka walikuwa vijana wachache mateka wa vita na walikuwa niwatu wa kudhihakiwa na kudharauliwa na watu waliojiona kuwa ni bora. Wakajenga mazingira ya fitina kwa sababu walisimama katika kweli. Lakini hata katika vitisho, jamii kuwa kinyume nao na kuwekewa mtego wa kuuawa, hawakuacha kusimama katika kweli ya Mungu. Hata walipohukumiwa kifo hawakuacha kusimama na Mungu. Lakini Mwisho wake, nai asiyeujua? Ile amri ya kuabudu miungu ikafutwa na badala yake ikaandikwa Amri ya kila mtu amwabudu Mungu wa Daniel maana ilithibitika kuwa hakika ndiye Mungu wa Kweli.

Watumishi wa Mungu songeni mbele na kila mtu asimame katika nafasi yake kwa ajili ya Bwana. Msiyumbishwe na matusi wala dhihaka za watu wasiomjua Mungu ambao wapo hapa mtandaoni na kwingine kote. Hawajaanza leo wapo siku zote na mara zote ni Wapinzani wa neno la kwlei kwa sababu hawaijui kweli na kweli haimo ndani mwao. Songeni mbele kuweka vyema misingi ya nchi na taifa. Mungu hatawaacha.
 
Kwa jinsi nchi ilivyipinda hii,sidhani kama anaweza kuinyoosha!!

Aanze kutunyooshea kwanza kipengele cha soka!!
 
Of course kuinyosha inahitaji maamuzi magumu mi nko naye bega kwa bega na yeye
 
Ni heri kukaa kimya na kufanya kile kinachokuhusu kuliko kuendelea kupayuka yasiyobeba uhalisia na yenye makengeza mengi....!!
Kuna mkakati unaandaliwa wa kufutia usajili taasisi za kidini na vyama vya kijamii vinavyojihusisha na siasa, Gwajima anaweza kuwa mhanga namba moja
 
Hongera Sana Gwajima. Usiogope songa mbele watakuelewa tu!
 
Gwajima sio msafi....watu wa kwenye system wanakujua wanataka kukuumbua hadharani ,ili watumishi wako unawaaminisha wewe ni mtakatifu wazijue rangi zako,nakushauri ukae kimya kipindi hiki ,unao mess nao wameshazoea kuloa damu na pesa chafu mikono yao
 
Waumini wake wote wameshanyooka?
Kama vp atangaze nia tujue moja!!
 
Katika ile list ya ma drug lords aliyokakabidhiwa JK nilisikia jamaa yumo halafu wakammezea sasa wanashangaa kawasaliti ndo kisa cha kum victimise wanajua sio mtu safi

Kumbe ulisikia?
 
Namuunga mkono Gwajima. Anyooshe nchi maana CCM wanalewalewa tu na madaraka
 
Tunahitaji watu wanaokemea maovu katika taifa. Tangu zamani waonyaji walikuwepo na siku zote hawakuwa watu wa kupendwa sana. Wote waliokemewa walisaga meno na kutafuta namna ya kuwaua kwa sababu ya viburi na kujiona wao ni miungu wasiopaswa kuonywa hata wakikosea. Walisahau kwamba yuko Mungu mmoja aliyezifanya mbingu na nchi. Lakini katika halakati zote zile, wako waliopoteza maisha na wapo walioishi ila mwisho wa yote Mungu alijitwalia utukufu. Mifano michache sana.

1. Yohana Mbatizaji aliyekatwa kichwa kwenye birthday ya mtoto wa mfalme kwa sababu tu mke wa mfalme alimchukia kwa kuonywa, na hivyo kumwagiza binti yake aombe kichwa cha Yohana Mbatizaji kama birthday gift!.

2. Mfalme Ahabu aliyekufa vitani kwa sababu ya kukataa sauti ya Nabii mmoja wa Mungu aliyemwambia ukweli lakini yeye Ahabu, akaamuru akamatwe na kuwekwa jela kwa sababu hamtabilii mazuri. Badala yake akaenda vitani kwa ushawishi wa majitu manafiki yaliyokuwa yamemezunguka naye kwa ujinga akaamini kwamba 'sauti ya wengi ndiyo sauti ya Mungu". Lakini ahabu alikufa sawa na Nabii mmoja wa Mungu alivyonena wala yale manafiki hayakumwokoa badala yake yalibakia yameduwaa kama mehu!.

3. Ninaona Nabii Eliah pia, aliwindwa kuaawa kwa sababu alikuwa tofauti na watawala. Muda wa Mungu ulipokuwa umewadia, ilijulikana ni nani Mungu wa Kweli kati ya Yahweh na Baal!. Mungu Yahweh, hajawahi kushindwa.

4. Bwana Yesu Christ, pamoja na kwamba ilikuwa lazime afe kifo cha aibu ili alipe fedheha na adhabu ya dhambi za ulimwengu, lakini katika shauri lake, walitafutiza mashitaka ya uwongo kwa sababu "aliwaambia maneno ya kwei yaliyochoma mioyo yao". Mob iliitikia "asuribiwe, asurubiwe" na hata wakadirki kutamkoa maajabu kwamba damu yake na iwe juu yao na juu ya watoto wao kwa sababu walimchukia juu ya kweli wala hakuwa na hatia!. Yesu hakuwa na umati mkubwa wa binadamu upande wake, lakini matokeo yake ni Utukufu Mkuu wa Mungu ambao hauelezeki.

5. Daniel. Shadrack na Abednego. Kumbuka walikuwa vijana wachache mateka wa vita na walikuwa niwatu wa kudhihakiwa na kudharauliwa na watu waliojiona kuwa ni bora. Wakajenga mazingira ya fitina kwa sababu walisimama katika kweli. Lakini hata katika vitisho, jamii kuwa kinyume nao na kuwekewa mtego wa kuuawa, hawakuacha kusimama katika kweli ya Mungu. Hata walipohukumiwa kifo hawakuacha kusimama na Mungu. Lakini Mwisho wake, nai asiyeujua? Ile amri ya kuabudu miungu ikafutwa na badala yake ikaandikwa Amri ya kila mtu amwabudu Mungu wa Daniel maana ilithibitika kuwa hakika ndiye Mungu wa Kweli.

Watumishi wa Mungu songeni mbele na kila mtu asimame katika nafasi yake kwa ajili ya Bwana. Msiyumbishwe na matusi wala dhihaka za watu wasiomjua Mungu ambao wapo hapa mtandaoni na kwingine kote. Hawajaanza leo wapo siku zote na mara zote ni Wapinzani wa neno la kwlei kwa sababu hawaijui kweli na kweli haimo ndani mwao. Songeni mbele kuweka vyema misingi ya nchi na taifa. Mungu hatawaacha.[/

asante kwa ufuafanuzi mzuri
 
Katika ile list ya ma drug lords aliyokakabidhiwa JK nilisikia jamaa yumo halafu wakammezea sasa wanashangaa kawasaliti ndo kisa cha kum victimise wanajua sio mtu safi

Kuna mengi yaliyo chini ya zulia ambayo ikitokea yakawekwa yote hadharani nchi itakumbwa na kiwewe kikubwa, si kwa gwajima tu bali kwa hata wanasiasa, viongozi mbalimbali wa kada tofauti na wafanyabiashara wakubwa
 
Gwajima sio msafi....watu wa kwenye system wanakujua wanataka kukuumbua hadharani ,ili watumishi wako unawaaminisha wewe ni mtakatifu wazijue rangi zako,nakushauri ukae kimya kipindi hiki ,unao mess nao wameshazoea kuloa damu na pesa chafu mikono yao

Asubiri kidogo moto ukolezwe atapelekewa chai yake ainywe
 
Hekima na Busara kwa gwajima ni kidogo sana mda huu alipaswa kuwa kwenye chumba cha kufikiri. Dini na siasa wapi na wapi anapotosha umma kwa visingizio vingi vingi tu.
 
Back
Top Bottom