Gwajima: Nitaendelea Kuinyoosha Nchi Ninapoona Haiendi Sawa!

Gwajima: Nitaendelea Kuinyoosha Nchi Ninapoona Haiendi Sawa!

Je, Wakristo wa Karne ya
Kwanza Walijihusisha na
Siasa?
▪ Kabla ya kupaa mbinguni, Yesu aliwapa wanafunzi wake maagizo yaliyo wazi kuhusu jinsi ambavyo wangetimiza huduma yao, lakini hakuwapa mashauri yoyote ya kisiasa. (Mathayo 28:18-20) Hivyo, wanafunzi wake waliendelea kutii kanuni ambayo Yesu alikuwa amewapa mapema: “Mlipeni Kaisari vitu vya Kaisari, lakini Mungu vitu vya Mungu.”—
Marko 12:17.
Kanuni hiyo iliwasaidiaje wafuasi wa Yesu waishi katika ulimwengu lakini wasiwe sehemu yake? Walitenganishaje kati ya mambo ya Serikali, au ya Kaisari, na mambo ya Mungu?
Mtume Paulo aliona kwamba mtu angekosa kutii kanuni ya Yesu ikiwa angeshiriki katika siasa. Kitabu Beyond
Good Intentions—A Biblical View of
Politics kinasema: “Paulo alikuwa tayari kutumia haki yake akiwa raia Mroma kupata ulinzi kupitia mfumo wa kisheria, lakini hakuunga mkono mabishano yaliyohusu sera za serikali.”
Paulo aliwapa Wakristo wenzake mwongozo gani? Kitabu hichohicho kinaongezea hivi: “Barua zake kwa waamini katika majiji muhimu kama vile Korintho, Efeso, na hata Roma hazikutaja mizozano yoyote ya kisiasa.” Pia, kitabu hicho kinasema kwamba Paulo “aliwaamuru wazitii serikali, lakini hakuandika kamwe katika barua zake nyingi kuhusu sera yoyote ambayo kanisa lilipaswa kupendekeza kwa serikali.”—Waroma 12:18; 13:1, 5-7 .
Wakristo walioishi miaka mingi baada ya kifo cha Paulo walidumisha mpaka huo kati ya wajibu wao kumwelekea Mungu na wajibu wao kuelekea Serikali. Waliendelea kuheshimu mamlaka za kisiasa lakini hawakujihusisha na shughuli za kisiasa. Kitabu Beyond Good
Intentions kinasema hivi kuhusu waamini hao: “Ingawa waliamini kwamba walikuwa na wajibu wa kuheshimu mamlaka za kiserikali, Wakristo wa mapema hawakuamini kwamba walipaswa kushiriki katika mambo ya kisiasa.”
Hata hivyo, mambo yalibadilika miaka 300 hivi baada ya kifo cha Kristo. Mwanatheolojia Charles Villa-Vicencio anasema hivi: “Mifumo ya kisiasa ilipobadilishwa chini ya utawala wa Konstantino, inaonekana Wakristo wengi walianza kufanya kazi katika serikali na jeshi na wakakubali vyeo vya kisiasa.” (Between Christ and Caesar) Matokeo yalikuwa nini? Mwishoni mwa karne ya nne W.K., muungano huo wa dini na siasa ulibadilika na kuwa Serikali ya kidini ya Milki ya Roma.
Leo, dini nyingi zinazodai kumfuata Kristo zinaendelea kuwatia moyo wafuasi wake wajihusishe na siasa. Hata hivyo dini hizo hazifuati mfano wa Kristo, wala hazifuati mfano wa Wakristo wa karne ya kwanza.
Copyright © 2015
 
Hivi Jesus si ndiye alisema ya kaisar aachiwe kaisari?

Sasa hawa viongozi wetu wa kidini mbona wanaenda kinyume na imani yao? Inamaana hawajui mipaka yao au ndio kujitoa ufahamu?

It's time wapigwe marufuku kupewa political platform. Wachague moja, kuwa wanasiasa au viongozi wa dini.

Huu ushamba wa wachungaji na mashehe kujigeuza political analysts unakera na kufadhaisha sana.
mkuu naomba nirudie hapa chini, hii ni busara...
It's time wapigwe marufuku kupewa political platform. Wachague moja, kuwa wanasiasa au viongozi wa dini.

Huu ushamba wa wachungaji na mashehe kujigeuza political analysts unakera na kufadhaisha sana
 
Kazi ya watumishi wa mungu ni kuonya na kukemea.piga kazi mtumishi.
Ni sawa ila atumie tafsida
zio mtu mzima unapayuka ''maharage ya wapi yuleeeee
-ishia zako mzeee
-tumekuchoka mzee
hufaaaiii mzeee
na
pampers
na mpuuzi
 
Kova amekukuluka awezavyo lakini kaambulia patupu.

Kama Alinyosha Mikono Kwa Makahaba, Alifika Kwa Mbwembwe, Kwamba Lazima Waondoke Jijini, Walimjibu Kwa Jeuli Kuwa Hautuwezi, Kwanza Wewe Ni Shemeji. Atamuwezea Wapi Mtu,anaesimamia Watu Zaid Ya Elfu 70?
 
Kwa jinsi nchi ilivyipinda hii,sidhani kama anaweza kuinyoosha!!

Aanze kutunyooshea kwanza kipengele cha soka!!

Mkuu umeonaeee, akimaliza kutunyooshea soka atusaidie kutatua tatizo sugu la sembe. Baada ya hilo atusaidie kudhibiti biashara haramu ya pembe za ndovu maana kwa mfumo huu tumeshindwa.
 
Mashaka yanaanzia pale mtumishi wa MUNGU au mchunga kondoo wa bwana anapomiliki silaha kwa ajili ya kujilinda huku akiwahubiria waumini wake wanaokabwa na vibaka kila siku uswahilini kuwa watalindwa na damu ya yesu....swali la kujiuliza ni je ina maana mchunga kondoo haamini kile anachowalisha kondoo wake....je anajilinda dhidi ya nani au watu gani ikiwa yeye ni msafi na ni mtumishi wa bwana.....Kama ni msafi kwa maana ya usafi hofu ya nini katika vyombo vya dola....mimi nadhani mtumishi wa MUNGU kwa usafi wake angetakiwa aonyeshe usafi wake kwa matendo kuliko maneno ili mwishowe jamii iamue kuwa kumbe mtumishi wa MUNGU alikuwa anasingiziwa na sio kubwabwaja kila siku kuhusiana na suala hilo ambalo yeye analiona la kipuuzi hali ya kuwa linamnyima usingizi....kuendelea kutapa tapa kuna maanisha kuwa bado ana hofu kubwa ndani yake...kunaonyesha kuwa kuna mambo anayotaka jamii isiyafahamu kumhusu na ndio maana anakuwa mtu wa kupanic kila anapoguswa....Kuna kila dalili kuwa wanakondoo wa mtumishi wa MUNGU wamepoteza uwezo wao kufikiri kabisa au labda huwa wanaviacha vichwa vya nyumbani kila waingiapo ibadani.....Mwanakondoo uliyepewa kichwa chenye ubongo unawezaje kuongozwa na mchungaji ambaye hata yeye mwenyewe haamini kile ambacho anakihubiri....Unawezaje kuwa na mchungaji asiyejua hata kuuchunga ulimi wake yeye mwenyewe na kuuacha utoe maneno machafu kama mtaro wa maji taka....Watumishi wa MUNGU ni kimbilio letu kwa sababu tunaamini kuwa ni watu waliojaa hekima huku wakiongozwa na nguvu ya roho mtakatifu wa MUNGU na daima tunategemea maneno yenye hekima na yaliyoshiba busara kutoka kwao kwa kuwa wao ni zaidi ya kioo cha jamii na tunawategemea kuzalisha jamii iliyobora....sasa jamii itakimbilia wapi ikiwa watu tunaowategemea katika kutuweka sawa na kutuunganisha ndio hao wanaotugawa na kuleta machafuko miongoni mwa wanajamii.....Sasa umefika wakati kwa wanakondoo kutoa vichwa vyao nje ya box na kuutazama ulimwengu mwengine kwa kufungua akili zao na sio kuenendea mithili ya watu wasio vichwa...maana kwenye vichwa vyao wao wanadhani kuwa kila lifanywalo na mtumishi wa MUNGU ni sahihi hata kama halikubaliani akili zao......
 
Tunahitaji watumishi wa Mungu wenye ujasili kama wako,mwana wa Adamu alikuja ili wanyonge wasiwe wanyonge,wenye kudhulumiwa wasidhulumiwe tena.Angalia Mtoza ushuru baada ya kukutana na Yesu aliacha UFISADI naakawarudishia watu aliowadhulumu.Hayo hayawezi kufanyika hadi tuwe na viongozi wa Mungu wa neno nasi viongozi wa mishahara.Askofu vita yako hauko pekee yako Kristo yu upande wako.Kosa la kumpinga Askofu PENGO analetewa kikosi kizima cha polisi kuanzia usiku wa manane tulijiuliza sana,Askofu ni gaidi au jambazi? Jibu tumeshaanza kulijua sasa kuanzia ISSUE ya Dr ULIMBOKA na msimamo wako wa katiba PANDIKIZI.Hata hivyo nakupa moyo hawanzii kwako,hata Yesu walimfata usiku wa manane na mikuki na marungu,UTASHIDA USIPOZIMIA ROHOwanyonge wote wa Tanzania tuko upande wako hatuungi mkono katiba hiyo.
 
hebu fafanua hapo kwenye maandishi meusi

Mkuu pale central Gwajima alimuuliza kova, unataka nilete document za mali zangu kwa kipengele kipi cha sheria? Kova si akaanza kurembua makengeza yake, mpaka ofisa mmoja ikabidi apige simu kwa MizengweP awape mwongozo. Sasa mtu kama kova anafanya kazi kwa maelekezo huyo si mpuuzi kabisa.
 
Mimi nadhani kuendelea kuzifungia taasisi kwa sababu zinaenda kinyume na matakwa ya watawala haisadii sana. Mbinu nzuri ni kuacha kutenda na maovu na kuyatenda yaliyo mema ili hata yakiwekwa hadharani iwe sifa nzuri kwao kuliko kuwa aibu. Ukitaka usisemwe fisadi acha ufisadi, kama watu wanasema serikali inayumba njia nzuri ya kukanusha ni kutoyumba, kama kunatuhuma za kutokuwa mwadilifu jibu zuri ni kuwa kinyume chake sio kuwafunga midomo wanaosema ili hata ukifuatiliwa usipatikane na hatia hiyo
Ni heri kukaa kimya na kufanya kile kinachokuhusu kuliko kuendelea kupayuka yasiyobeba uhalisia na yenye makengeza mengi....!!
Kuna mkakati unaandaliwa wa kufutia usajili taasisi za kidini na vyama vya kijamii vinavyojihusisha na siasa, Gwajima anaweza kuwa mhanga namba moja
 
Mashaka yanaanzia pale mtumishi wa MUNGU au mchunga kondoo wa bwana anapomiliki silaha kwa ajili ya kujilinda huku akiwahubiria waumini wake wanaokabwa na vibaka kila siku uswahilini kuwa watalindwa na damu ya yesu....swali la kujiuliza ni je ina maana mchunga kondoo haamini kile anachowalisha kondoo wake....je anajilinda dhidi ya nani au watu gani ikiwa yeye ni msafi na ni mtumishi wa bwana.....Kama ni msafi kwa maana ya usafi hofu ya nini katika vyombo vya dola....mimi nadhani mtumishi wa MUNGU kwa usafi wake angetakiwa aonyeshe usafi wake kwa matendo kuliko maneno ili mwishowe jamii iamue kuwa kumbe mtumishi wa MUNGU alikuwa anasingiziwa na sio kubwabwaja kila siku kuhusiana na suala hilo ambalo yeye analiona la kipuuzi hali ya kuwa linamnyima usingizi....kuendelea kutapa tapa kuna maanisha kuwa bado ana hofu kubwa ndani yake...kunaonyesha kuwa kuna mambo anayotaka jamii isiyafahamu kumhusu na ndio maana anakuwa mtu wa kupanic kila anapoguswa....Kuna kila dalili kuwa wanakondoo wa mtumishi wa MUNGU wamepoteza uwezo wao kufikiri kabisa au labda huwa wanaviacha vichwa vya nyumbani kila waingiapo ibadani.....Mwanakondoo uliyepewa kichwa chenye ubongo unawezaje kuongozwa na mchungaji ambaye hata yeye mwenyewe haamini kile ambacho anakihubiri....Unawezaje kuwa na mchungaji asiyejua hata kuuchunga ulimi wake yeye mwenyewe na kuuacha utoe maneno machafu kama mtaro wa maji taka....Watumishi wa MUNGU ni kimbilio letu kwa sababu tunaamini kuwa ni watu waliojaa hekima huku wakiongozwa na nguvu ya roho mtakatifu wa MUNGU na daima tunategemea maneno yenye hekima na yaliyoshiba busara kutoka kwao kwa kuwa wao ni zaidi ya kioo cha jamii na tunawategemea kuzalisha jamii iliyobora....sasa jamii itakimbilia wapi ikiwa watu tunaowategemea katika kutuweka sawa na kutuunganisha ndio hao wanaotugawa na kuleta machafuko miongoni mwa wanajamii.....Sasa umefika wakati kwa wanakondoo kutoa vichwa vyao nje ya box na kuutazama ulimwengu mwengine kwa kufungua akili zao na sio kuenendea mithili ya watu wasio vichwa...maana kwenye vichwa vyao wao wanadhani kuwa kila lifanywalo na mtumishi wa MUNGU ni sahihi hata kama halikubaliani akili zao......

Huu ukweli mtu kama Fandre ni ngumu kuuelewa...
 
Last edited by a moderator:
Hekima na Busara kwa gwajima ni kidogo sana mda huu alipaswa kuwa kwenye chumba cha kufikiri. Dini na siasa wapi na wapi anapotosha umma kwa visingizio vingi vingi tu.

Mbona wakati wa kuwapa madaraka mnawaita hao hao viongozi wa dini kuja kutoa kiapo cha kushika madaraka kwa nini msifanye tu kwa kuwa ni siasa ?
Watu wa Mungu wanao umizwa kwa kukoseshwa haki zao ambazo Siasa ba hasa CCM hawawezi kutoa wataka aendelee kukaa kimya tu ? Kama ni drug deal wasema na wa deal naye na wasema tangia lini kaanza hiyo kazi na walikuwa wapi muda wote ? Unataka awe kama yule mama ana kanisa kubwa lakini ahakwepa kulipa bill ya Umeme na kazi yake ni kulala Bungeni? Ni kweli siasa na dini si ndugu ? Yue mama Mchungaji imekuwaje kaamuwa watumikia mabwana 2 na sio shida kwa CCM ?
 
Roho ni nini na misingi ya kiroho ninini?

Kwa hiyo kwako wewe, siasa ni uchaguzi wa viongozi basi?

Kwa hiyo wewe unasema kwamba watu wenye dini hawatakiwi kuhusika na masuala yoyote yanayohusu mazingira yao wanayoishi na maisha yote kwa ujumla. Ila kazi yao ni kuchagua viongozi na kutii, (sijui wanatii nini ikiwa maisha yote hayawahusu). Kwa nini unawapa haki ya kuchagua ikiwa uchaguzi ni siasa na unasema hawatakiwi kuhusika na siasa?

Kwa kukusaidia, ukipewa madaraka yoyote katika ngazi yoyote iwe ya familia ama vipi, unatakiwa kuitumia kwa uelekevu na uadilifu kama inavyokupasa. Kinyume cha pale hutakuwa na uwezo wowote wa kukataa kukosolewa ama kuonywa na jamii pale unapokosea kwa kisingizio eti wengine hawahusiki na makosa yako. Wewe unaongoza vibaya, unaowangoza unaanza kuwazuia wasiseme kwa kuwa eti wewe ni mwanasiasa wakati makosa unayoyafanya yako dhahiri kwamba wewe si mwana siasa safi bali mharibifu!.

Ni aibu kwa taifa kutaka viongozi wa dini wasiongelee masuala ya siasa wakti yanagusa maisha ya kila mtu na pia wanahaki kama watanzania wengine. Ni vizuri kiongozi bomu, abebe mzigo wake mwenyewe badala ya kuanza kufunga vinywa vya wakosoaji.
Asante kunipa wakati ama nafasi nyingine ya kueleza juu ya jambo lililo mbele yetu kwanza nianze na nini maana ya Roho, ROHO ni sehemu katika moyo wa mwanadamu amabyo kazi yake kubwa ni kuunganisha nguvu ya Mungu katika maisha ya kila siku ya mwanadamu hata wewe unayo roho ambayo hukukumbusha juu ya KUTENDA WEMA, KUEPUKA DHAMBI NA K.N na hii kwa imani ya kikiristo huiita msaidizi soma wagalatia 4:6 pia kumbuka kusoma yohana 14:16na 17 juu ya roho kutonekana.Hapo nafikiri utakuwa umenielewa sasa nije kwenye misingi ya kiroho ambayo umeiuliza 1. kuzaa na kuingiza katika ufalme wa Mungu soma yohana 3:1-8 2. Kuwasaidia waumini katika kumjua Mungu. 3.Kuwashawishi wasioamini na kuwa waumini 4. Kuwaombea waumini mahitaji yao. Ngoja niishie hapo kwenye misingi ya kiroho na misingi hii ndio wajibu wa MASKOFU NA WACHUNGAJI. kwa maana nyingine wanafanya shughuli alizo zifanya YESU KRISTO mwanzilishi wa imani hii ona yeye alichokifanya soma kitabu cha mathayo 28:18-20 neno linasema yesu akaja kwao akasema nao,akawaambia nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani 19 Basi endeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkibatiza kwa jina la Baba, na Mwana,na Roho mtakatifu 20, Nakuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. kwa msingi huo tunapata kazi kuu tatu kwenye maandiko matakatifu i/ KUWAFANYA WANAFUNZI WA MUNGU, ii/ KUFUNDISHA NENO LA MUNGU iii/ KUWABATIZA KUWA WANA WA MUNGU. MWISHO JITAHIDI KUSOMA MAELEZO YOTE NILIYOAANDIKA .
 
Mbona wakati wa kuwapa madaraka mnawaita hao hao viongozi wa dini kuja kutoa kiapo cha kushika madaraka kwa nini msifanye tu kwa kuwa ni siasa ?
Watu wa Mungu wanao umizwa kwa kukoseshwa haki zao ambazo Siasa ba hasa CCM hawawezi kutoa wataka aendelee kukaa kimya tu ? Kama ni drug deal wasema na wa deal naye na wasema tangia lini kaanza hiyo kazi na walikuwa wapi muda wote ? Unataka awe kama yule mama ana kanisa kubwa lakini ahakwepa kulipa bill ya Umeme na kazi yake ni kulala Bungeni? Ni kweli siasa na dini si ndugu ? Yue mama Mchungaji imekuwaje kaamuwa watumikia mabwana 2 na sio shida kwa CCM ?
hakuna anayeitwa kama kumbukumbu zako ziko sawa Rais huapishwa na Jaji mkuu na si kiongozi wa dini ila wao wenye dini huwaita viongozi wa kisiasa kushuhudia kuapishwa kwa askofu
 
mkuu naomba nirudie hapa chini, hii ni busara...
It's time wapigwe marufuku kupewa political platform. Wachague moja, kuwa wanasiasa au viongozi wa dini.

Huu ushamba wa wachungaji na mashehe kujigeuza political analysts unakera na kufadhaisha sana

Very true, mie nawshangaa sana watanzania, mnasomesha wanasheria wa kila aina, halafu ukifika wakati wa kuwaandikia katiba, mnachagua mashehe na wachungaji wafanye maamuzi na kuhamasisha upigaji wa kura. EBO.

Halafu mambo yakiwa ya hovyo lawama zinarudi kwa wanasheria na wasomi waliojipinda kutengeneza sheria nzuri (warioba and team).

wakishapokea maoni na busara za ngumbaro wao wa sheria, wanaita wanasheria wezi wao kina chenge waje ku-rubber stamp utapeli wao.

HIVI kuna Kiongozi wa CCM au CHADEMA anapeleka gari yake Kanisani au Msikitini kufanyiwa service? Kama tunaheshimu mafundi magari kuwa ni wajibu wao kutatua matatizo ya magari, kwa nini matatizo ya katiba yenye kuhitaji utaalamu wa hali ya juu wa sheria tuwape turufu hawa wasanii wetu tunaowaita viongozi wa dini? (disclimer: kiongozi yoyote wa dini asiyekwisha kutoa matamko ya kisiasa kwangu ni msanii, hana tofauti na mishen tauni wa posta.)

nchi imejaa vituko kweli kweli.
 
Back
Top Bottom