Gwajima azungumzia sakata la madini,Mwenge na kuwatahadharisha wanaomchokoza

Angetuambia pia na ile lugha anayozungumzaga kama kweli huwa ni roho mtakatifu au mbwembwe tu !! Maana angeshampa jibu sahihi.
 
Huyo awahubirie waumini wake namba gani ya kwenda Mbinguni na kurithi ufalme wa Mbinguni sio vijembe na udaku wa Tandale na Manzese uwanja wa fisi.

Kama ana hamu na siasa aachane na Dini aingie kwenye kuvuana mataulo na chupi kwenye siasa maana huko utachambuliwa mpaka unakolala!!
 
Leo katika mahubiri yake alikuwa akizungumzia swala la uchawi wa kufungwa kutooana (kuinamishwa) kazungumzia mengi hasa mali tulizonazo kuanzia maziwa, mito, mbuga lakini tunalia pia migodi ya dhahabu kuwa tumefungwa hatuoni.

Ana sema anauliza kwanini mwenge unakimbizwa nchi nzima mtaa kwa mtaa unamaana gani? Je unazunguka kutulaza? (Kutuloga)

Anataka aupige ila akijibiwa ndo ataupiga vizuri.

Sasa lengo la kuanzishwa mpka leo unakimbizwa kufanya nini na kwa gharama kubwa? Kwanini wasiukimbize toka mwenge hadi posta tena live kwenye tv na radio si inatosha?

Huu mwenge sio unatuinamisha watanzania tusione?

Kunanini kwenye mwenge?

Kama Magufuli kaanza na madini na hili litamshindaje? Maana usiku huwa watu hukutana kwa maovu tupu na hasara kwa taifa.

Huo ndio mwelekeo wa dini Tanzania kwa sasa. Hadi Gwajima amalize watu kama alivyofanya Kibwetere ndio watu watashtuka.
 
Kama ni nembo ya taifa, ni bora kuuwasha huo mwenge siku moja yaani siku ya kuanza ujenzi wa miradi mbalimbali nchini au mipango ya maendeleo nchi nzima na kuuzima siku hiyo. Ukasubiri siku ambayo tukifanikiwa kusherehekea kipindi cha kuzindua miradi husika huku report ya nchi nzima ikisomwa siku hiyo.
 
Gwajima una haki ya kuwaonya wanaokufuata fuata, ni haki yako kikatiba na hata kidini. Yesu kristo aliwaonya waliokua wanamfuata fuata, mtume mohamad yeye aliwaua kabisa wabaya wake waliokua wanamfuata fuata.

Hakuna mahala ambapo unakatazwa kukomaa na wanaokufuata fuata/wabaya wako.

Muda mwingine ukiona watu wapumbavu wanakufuata fuata lazima ukomae nao, yesu kristo alihubiri kua mtu akichukua shati yako muachie na koti na suruali lakini alipowakuta watu wamegeuza sinagogi sehemu ya kuchezea kamari hakuwaachia hilo sinagogi, aliwapa kipigo kizito na kuwafukuza, kwa nini hakuwaaachia???
 
Huyo awahubirie waumini wake namba gani ya kwenda Mbinguni na kurithi ufalme wa Mbinguni sio vijembe na udaku wa Tandale na Manzese uwanja wa fisi.

Kama ana hamu na siasa aachane na Dini aingie kwenye kuvuana mataulo na chupi kwenye siasa maana huko utachambuliwa mpaka unakolala!!
Hahahaha
 
Wasiwasi wangu ni kama ukishawavua hutowatamani na kuvunja amri ya Mungu Mtumishi Gwajima
 
Gwajima kuwavua mataulo wanaomchokoza
Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewatahadharisha wanaomchokoza akisema ni sawa na mtu anayeanzisha ugomvi huku akiwa amevaa taulo.

Akihubiri leo, Gwajima amesema wakiendelea atawavua mataulo ili jamii iwaone.

Bila kufafanua kuhusu kauli hiyo, Gwajima amesema hawezi kunyamaza wakati watu wanaendelea kumfuata fuata.

"Leo nitakwapua mataulo ya watu,"amesema huku akishangiliwa na waumini wake.

Madini
Dar es Salaa,. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema ni muhimu madini yasichimbwe hadi itakapowekwa mashine za kuchenjua makinikia.

Akizungumza kwenye ibaada kanisani kwake leo Askofu Gwajima amesema, "Tusiogope kushtakiwa Magufuli(Rais John) piga marufuku makinikia kusafirishwa nje."

"Madini yaliyopo Tanzania ni zaidi ya 300 lakini bado tuna umaskini tumelogwa na nani."
Sikuhizi naona kuna raisi mkuu na rais msaidizi
 
Gwanjima yupo sawa lkn gwanjima dini na siasa ni tofauti acha din fanya siasa au acha siasa komaa na din
 
Askofu Gwajima azungumzia sakata la madini
Screenshot_2017-05-28-19-33-34.jpg
 
Leo katika mahubiri yake alikuwa akizungumzia swala la uchawi wa kufungwa kutooana (kuinamishwa) kazungumzia mengi hasa mali tulizonazo kuanzia maziwa, mito, mbuga lakini tunalia pia migodi ya dhahabu kuwa tumefungwa hatuoni.

Ana sema anauliza kwanini mwenge unakimbizwa nchi nzima mtaa kwa mtaa unamaana gani? Je unazunguka kutulaza? (Kutuloga)

Anataka aupige ila akijibiwa ndo ataupiga vizuri.

Sasa lengo la kuanzishwa mpka leo unakimbizwa kufanya nini na kwa gharama kubwa? Kwanini wasiukimbize toka mwenge hadi posta tena live kwenye tv na radio si inatosha?

Huu mwenge sio unatuinamisha watanzania tusione?

Kunanini kwenye mwenge?

Kama Magufuli kaanza na madini na hili litamshindaje? Maana usiku huwa watu hukutana kwa maovu tupu na hasara kwa taifa.
Vipi yale mapepo aliyotuma kwenda kwa Rc Makondo alifikia wapi? Je hayo mapepo anayahifadhi kanisani mwake au anatembea nayo?
 
Back
Top Bottom