#COVID19 Askofu Gwajima amshukia Waziri Doroth Gwajima. Awataka Mawaziri wa Wizara ya Afya wajiuzulu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,868
Bwana Yesu aliye mponya na apewe sifa.

Askofu Gwajima leo ataongoza ibada katika kanisa la ufufuo na uzima kabla hajaelekea bungeni Dodoma ambako kesho atahojiwa na kamati ya maadili ya bunge.

Updates;

Familia ya mzee Gwajima imemtaka waziri wa afya Dr Dorothy Gwajima ambaye ni mke wa mtoto wake aache kutumia jina la Gwajima na arudie jina lake la kinyiramba la Mkumbo!
===

1629631176808.png

Akofu Gwajima leo akiongoza ibada katika kanisa lake la ufufuo na uzima ameeleza masuala mbalimbali ya kiserikali ikiwamo kumjibu waziri wa Afya Dkt. Doroth Gwajima katika masuala mbalimbali.

Akiongea katika ibada hiyo Askofu Gwajima alisema mambo yafuatayo:

Askofu Gwajima: Unatakiwa ufanye uchunguzi kidogo, kwamba Gwajima ukimchokoza anakuaje, mimi ukimtoa Yesu aliye mwana wa Mungu, ambaye nimeweka maisha yangu kwake, kingine hakinitishi. Na hiyo ndiyo imani yetu sisi, hatugeuki, hatubadiliki, hatujadili.

Askofu Gwajima: Mimi huwa nafanya vizuri zaidi wakati wa mawimbi, tufani, upepo na kimbunga. it’s the time I fly higher and higher, ndivyo nilivyotengenezwa. Mimi kumkabili mtu nimeumbiwa hivyo, hasa anayemchezea Mungu na nguvu zake

Askofu Gwajima: Sisi imani yetu ni kwamba kwa kupigwa kwake Yesu sisi tumepona na kwa imani yetu sisi hatuchanjwi, sasa tisha tisha ya nini? Mbona tumeweka bayana! wiki iliyopita nilisema nafunga mjadala sisi hatujaona tafiti ya kutosha kufanya miili yetu ichanjwe.

Askofu Gwajima: Nataka nimtetee mheshimiwa rais na nimwambie kinachomkwamisha. Mimi ni nabii wa Mungu, nabii wa Mungu wako namna hiyo. Waziri akikaribishwa kanisani haongei? Mimi mbunge niko naongea kanisani tatizo liko wapi?- Askofu Josephat Gwajima.

Askofu Gwajima: Nini kinachokwamisha? Kinachokwamisha ni waziri yule yule mkwe wetu, tuna bahati mbaya sana ndani ya ukoo wa Gwajima. Mzee Gwajima pole sana, tumepata matatizo ya mkwe wako, huyu sasa tutafanyaje, hii oa oa ya wadogo zetu imetuletea tabu kwenye familia.

Askofu Gwajima: Waziri wa Afya na Naibu wako Molel, mjiuzulu tena haraka… ili mumtengenezee Rais mazingira rahisi ya kufanya kazi yake. Wanatakiwa kusema kwa sasa hivi sisi mama tutaharibu kwa sababu tulisema hivi na video zipo wakijifukiza wenyewe.”

Askofu Gwajima: Mimi huyu waziri wa afya siwezi kumpasua vipande vipande kwa sababu ni mteule wa rais, bado ninamheshimu rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM, nilitamani nimkate vipande vipande lakini ninamheshimu sana na Rais Samia Suluhu Hassan.

Askofu Gwajima: Rais Samia Suluhu ni mtu mzuri, alisema acheni watu waseme, ndio tunasema sasa hatutaki kuchanjwa na hatutachanjwa, Dorothy na Mollel wakiendelea kuwa kwenye hizo ofisi nitawatwanga mpaka wakome.

Mkwe wa Waziri Gwajima amtaka aache kutumia jina
Mathias Gwajima:
Mimi kwa kweli usemi sina isipokuwa sasa huyu mama yetu huyu anajiita Gwajima, nasikitika sana na mimi ningekuomba hata jina la Gwajima asingelitumia, anataka kuniharibia familia yangu (Mkwe wa Waziri wa Afya).

Anaendelea Askofu Gwajima

Askofu Gwajima: Yule waziri aliyekataliwa na mzee wetu nafikiri ni vizuri atumie jina la kwao, atupishe. Tangu aingie familia hatuelewani yaani yuko waluwalu tu hatulii, juzi alisema mume wangu baada ya kuchanjwa ame-test mitambo yangu iko fiti, kiongozi unasema hivyo?
 
Mbele ya kamati ya maadili ya bunge.

#NchiKwanzaKablaYaYeyoteNaChochote
#SiempreJMT
 
Chanjo anayoipinga ni ya wazungu,makanisa yameletwa na wazungu,

Kwanini asiachane na kanisa aende kwenye matunguli ambayo ndiyo asili ya mtanzania na waafrika,alafu unajuta watul wazima na akili zai ambao yeye Gwajima anaowaita kondoo wamekusanyika kumsikiliza.
 
Askofu alieamua kuwa mwanasiasa ni tapeli tu, ameshindwa kuishi kwa kufuata kauli zake, kazi za Mungu na za mwanadamu hazifanani, na haziwezi kuingiliana kwa namna yoyote.

Udhaifu wa kiongozi wa nchi ambaye ndie kiongozi wa chama chao ndio sababu ya hizi kelele, huyu Gwajima leo anajidai kumuogopa Mungu wakati ubunge aliupata kwa wizi ni jambo la kushangaza.
 
Back
Top Bottom