Gwajima azungumzia sakata la madini,Mwenge na kuwatahadharisha wanaomchokoza

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
18,716
28,622
Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewatahadharisha wanaomchokoza akisema ni sawa na mtu anayeanzisha ugomvi huku akiwa amevaa taulo.

Akihubiri leo, Gwajima amesema wakiendelea atawavua mataulo ili jamii iwaone.

Bila kufafanua kuhusu kauli hiyo, Gwajima amesema hawezi kunyamaza wakati watu wanaendelea kumfuata fuata.

"Leo nitakwapua mataulo ya watu,"amesema huku akishangiliwa na waumini wake.

Madini
Dar es Salaa,. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema ni muhimu madini yasichimbwe hadi itakapowekwa mashine za kuchenjua makinikia.

Akizungumza kwenye ibaada kanisani kwake leo Askofu Gwajima amesema, "Tusiogope kushtakiwa Magufuli(Rais John) piga marufuku makinikia kusafirishwa nje."

"Madini yaliyopo Tanzania ni zaidi ya 300 lakini bado tuna umaskini tumelogwa na nani."

Mwenge
katika mahubiri yake alikuwa akizungumzia swala la uchawi wa kufungwa kutooana (kuinamishwa) kazungumzia mengi hasa mali tulizonazo kuanzia maziwa, mito, mbuga lakini tunalia pia migodi ya dhahabu kuwa tumefungwa hatuoni.

Ana sema anauliza kwanini mwenge unakimbizwa nchi nzima mtaa kwa mtaa unamaana gani? Je unazunguka kutulaza? (Kutuloga)

Anataka aupige ila akijibiwa ndo ataupiga vizuri.

Sasa lengo la kuanzishwa mpka leo unakimbizwa kufanya nini na kwa gharama kubwa? Kwanini wasiukimbize toka mwenge hadi posta tena live kwenye tv na radio si inatosha?

Huu mwenge sio unatuinamisha watanzania tusione?

Kunanini kwenye mwenge?

Kama Magufuli kaanza na madini na hili litamshindaje? Maana usiku huwa watu hukutana kwa maovu tupu na hasara kwa taifa.


 
ingia playstore na download hii application yupo live in audio form katika radio inayoitwa rudisha radio!
 

Attachments

  • IMG_20170528_111345_370.JPG
    IMG_20170528_111345_370.JPG
    6.2 KB · Views: 41
Back
Top Bottom