- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- Josephat Gwajima ni Askofu na mwanzilishi wa kanisa la 'Glory of Christ Tanzania Church' GCTC (Ufufuo na Uzima Ministries), kadhalika ni mwanasiasa ambaye mwaka 2020 alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa (MNEC).
Tarehe 15 Agosti, 2025 Askofu Gwajima alizungumza mbashara kupitia Mtandao wa YouTube ambapo alitumia nafasi hiyo kutoa ushauri wake kwa Taifa la Tanzania pamoja na viongozi wake hususani kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
Ipo video inayosambazwa mtandaoni ikimuonesha Askofu Gwajima akisema makanisa yake na watu wake wataipigia kura CCM
Uhalisia wa video hiyo
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image Search pamoja na marejeo ya video, Umejiridhisha kuwa video hiyo imepotoshwa uhalisia wake.
Video imepotoshwa kwa kukata vipande vidogo vidogo kutoka kwenye hotuba hiyo na kuviunganisha katika mpangilio ulioharibu ujumbe halisi uliokusudiwa na Askofu Gwajima.
Aidha akizungumza kwa njia ya mtandao pamoja na mambo mengine Askofu Gwajima alishauri viongozi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoingia kwenye Uchaguzi mkuu bila kushughulikia malalamiko yaliyopo miongoni mwa makundi mbalimbali ya wananchi.
Rejea kiungo hiki kilichohifadhiwa hapa.
"Kanisa tu la ufufuo na uzima ambalo mimi naliongoza lina makanisa 2006, makanisa ya mikoani, wilayani, kwenye kata, tarafa na vijiji ambalo lina maaskofu 33, watu wake sasa hivi hawaabudu kabisa, hawawezi kuabudu kwa sababu kanisa lao litafungwa.
Je, makanisa haya elfu mbili na waumini wao, na wachungaji wao na maaskofu wao sisi CCM watatupigia kura wakati wa uchaguzi? .... hawa watu watakupenda kiasi cha kukupigia kura? nataka tujiulize sisi kwa sababau mimi bado ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi. Nina concern sana kama Chama kinaingia kwenye uchaguzi na hali hii"
View: https://youtu.be/twy9ahsTVXc?si=jWb5yCiASWtXGFQi&t=220