Guninita sasa ni 'fomu wani'

nchi haiwezi ikatoka katika janga la ujinga wakati viongozi wao no vihio, mtu kama guninita alipokuwa DC sifikirii kama aliweza hata kufuatilia masuala ya elimu kwenye wilaya yake hii ni aibu sana kwa taifa hili ambalo linapiga vita adui ujinga
 
kweli siasa ni mchezo mchafu......sikuamini huyu mzee alivomkomalia sitta,kumbe ni kihiyo.Kwa tz yetu sdhani kama itafika hata 2012 kabla hajapata degree yake.............

Kwa Bongo si mshangao mwaka 2015 akawa Dr. Guninita!
'Degree' za on-line...
 
Mh. Guninita bora uje humu ukumbini utolee maelezo kashfa hii.

Nakumbuka tuliwa kukuchagua kama mwenyekiti wetu wa Taifa Umoja wa vijana CCM, na ulipokwenda mtaa wa pili kule Chadema walikupatia wadhifa wa juu sana kitaifa.

Tafadhali njoo humu ndani utoe maelezo!
 
jamani cha kushangaza nini! me nadhan amefanya uamuzi sahihi! ila ningependa kujua ilaishia darasa la ngapi kabla ya kuanza form one! na je any other informal education kama anayo! Ntafurahi nikipata kumwanga hako ili niweze kuhisi uwezo wake!
 
jamani cha kushangaza nini! me nadhan amefanya uamuzi sahihi! ila ningependa kujua aliishia darasa la ngapi kabla ya kuanza form one! na je any other informal education kama anayo! Ntafurahi nikipata kumwanga hako ili niweze kuhisi uwezo wake!

Una akili sana mkuu, Unajua inawezekana hata darasa la saba hakufika!
 
No, seriously, wewe unadhani kweli jamaa kichwani zinapanda? I'm willing to put my 7yr old daughter against his big azz and see who's smatter.

Unaweza kumpambanisha na binti yako mwenye umri wa miaka 7, tofauti ni kuwa binti yako hata akimshinda hawezi kupata huo uenyekiti.
 
Nahisi hii habari sio kweli.
Mimi hakuna kinachonishangaza Tanzania miaka hii.
Ila nijuavyo viongozi wengi CCM hasa wilayani na ngazi za chini wana shule mbovu MNOOOO!....!!

May be, ila kwani kosa ni la nani?
Unajua hapa Duniani ni akili kichwani tu, wengine wanaamua kubukua weee, wakishtuka treni ishawaacha...matokeo yake ndo tunakutana hapa kijiweni na kuanza kujadili ma-frustration yetu, ki aina aina.
Halafu wengine wanakuwa wameshtuka mapema na kuanza kusaka hayo maisha mitaani, bila kutafuta formula za mabuku...hawa wengi wao wakaingingia kwenye siasa, bishara halali, na wengine biashara haramu, ila wote wanatengeza pesa na wamenona nona ki fisadi fisadi na mambo mengi kwao ni akili kichwani tu.
 
Unaweza kumpambanisha na binti yako mwenye umri wa miaka 7, tofauti ni kuwa binti yako hata akimshinda hawezi kupata huo uenyekiti.

Princess hataki uenyekiti na wala hapendi siasa. Ni kwamba tu huyo Guninita darasa halipandi ndio maana kasubiri hadu uzeeni kuanza form one. Shameful even though you are never too old to learn.

Sasa zee zima likitolewa nishai (intellectually) na mtoto wa miaka saba si bonge la aibu hilo.
 
Tanzania being led by semi-literate cadres of CCM, the likes of Guninita, has brought us to this stage where top echelons do not recognize the separation of powers between the Executive, Parliament and Judiciary. It was pathetic and shame for us to display that muddle-headedness in the confrontation between the ruling party and Speaker Sitta.

Tanzanians must decide soon whether CCM can really carry us far into the 21st century. It needs to be restructured to survive as a political party; but most important of all, for Tanzania, it must be defeated in 2010.

This is a challenge and an opportunity for dynamic, innovative parties like Chadema.
 
Last edited:
kwa sasa huyu jamaa inabidi afukuzwe kazi ya ukuu wa wilaya nijuavyo mimi kwa utaratibu mpay wa serikali bila kidato cha nne ajira hupati na kwa wale wafanyakazi ambao walikuwa na elimu yadarasa la saba waliambiwa wakajiendleze la sivyo nafasizao itafika wakati zitachuliwa na vijana wasomi hastahili kuendlea kuwa mkuu wa wilaya aachie ngazi mpaka atakapohitimu elimu yasekondarii
Inaonyesha unasoma vipande vipande. Ukuu wa wilaya ilikuwa miaka ileeee. Sasa hivi ni mwenyekiti wa chama cha mafisadi Dar es salaam.

Nyie wasomi kwanini hamtaki kujiunga na siasa? Huwezi ku-win bahati nasibu bila kucheza mchezo wenyewe.

Kama una bachelor, masters, Phd or THD, good for you. Lakini kama haupo kwenye siasa, vyeo vya kisiasa waachieni wanasiasa.
Kuazima maneno ya fisadi mtoto, "mawazo yako ni yaovyo ovyo". watu wote hawawezi kuwa wanasiasa. Na kuwa usipokuwa mwanasiasa huna haki ya kusema chochote. Kama mwili wote ni sikio kuwapi basi kusikia?
 
DU! Ama kweli hii nchi haina mwelekeo, kama kweli huyo jamaa ni std 7 alafu alishakuwa DC? Maumivu ya kichwa huanza pole pole!!! Kwanini wasiige mfano wa Chadema?
 
Sijawahi kucheka kama leo;ndiyo naelewa sasa kuwa Guninita kumbe alimshambulia sana Spika wa Jamhuri ya Muungano kwa sababu ya uwezo wake haba wa kufikiri!

Guninita naweza kukupa bure vitabu vya English kama vile "Think Fall Apart"na vinginevyo ambavyo alikuwa anatumia mwanangu kwani yeye sasa kaisha vuka O level na kuingia mchepuo wa sayansi A level,na kwa hiyo vitabu hivyo havitumii!Naomba tuwasiliane.

Bytheway for this kind of credibility,Guninita hafai hata kuwa Mwenyekiti wa Vijana wa CCM wa ngazi ya kijiji,na sijui ilikuwaje hadi akashinda Uenyekiti wa CCM-Taifa!Mhitimu wa darasa la saba tena aliye feli anakuwa Mwenyekiti wa Jumuia yenye nguvu ya vijana ya CCM-Taifa?Haya ni maajabu na lzm yaingizwe kwenye "guiness book" na Masatu tueleze kama una lolote ilikuwaje Guninita akashinda!

Mkuu Guninita,nakutakia masomo mema hasa ya kukokotoa "Length and width" na baadae kufundishwa"vowels".
teh teh,eeeh mnyezi mungu asante sana kunionyesha jamii forum (the great thinker)bro you make my day goin to sleep now
 
Hili desa maaalum kwa Guninita, a, e, i, o, u.akimaliza hapo ajifunze kuandika 1 hadi 10, baada ya hapo anaingia form two!
 
Guninita amepiga shule nyinyi. Ana ThD.

CCM Chairman (Wizard of Oz): They have one thing you haven’t got: a diploma. Therefore, by virtue of the authority vested in me by the Universitartus Committiartum E Pluribus Unum, I hereby confer upon you the honorary degree of ThD.

Guninita (Scarecrow): ThD?

CCM Chairman (Wizard of Oz): That’s… Doctor of Thinkology.
 
Ukiachana na Guninita, kuna wengi sana ndani ya CCM ambao wana digrii au vyeti vya kuokota. Watu wa aina hii wanachojua maishani mwao ni CCM politics tu kwa vile ndizo zimewafikisha huko waliko; watu hawa hawasadii lolote kujenga taifa hili zaidi ya kulinda msalahi yao. Itatuchukua muda mrefu sana kung'oa mizizi ya aina hii na sumu yake kabla ardhi ya taifa la Tanzania haijaanza kuwa na rutuba tena.
 
jamani tunakwenda wapi kama huyu mkubwa ndio kiongozi wa siasa za chama tena town alafu elimu yake famfa namna hii inatisha sana dah sasa hata yule mkubwa atakuwa alidanganywa mpaka akampa madaraka kipindi kile ukuu wa wilaya dah kweli bongo inawezekana kila kitu ila kweli ndugu zangu kazi ipo
 
Hili desa maaalum kwa Guninita, a, e, i, o, u.akimaliza hapo ajifunze kuandika 1 hadi 10, baada ya hapo anaingia form two!

Baada ya hapo anaingia form 3, kwasababu ameunganisha form one na two. Kuna kitabu kimoja ninacho itabidi niwasiliane nae ili nipatie ni kizuri sana kwa kujibia maswali ya Literature kinaitwa "The River between".
 
Sidhani kama Guninita ana akili ya kutosha kuelewa Trigonometry, Algebra, na Calculus.


Huko mbali sana simultaneous equations tu ataona nyota.....................aaah kumbe pia quadratic equations zipo around pia...! Kikubwa mswaki (F) wa mathematics utakuwepo hauna ubishi. Lakini as usual yale masomo yao ya kuwatoa na D mbili apate cheti yapo ie Kiswahili na Civics/history/english........!
 
Tusiishie hapo.

Ni lipi ambalo yeye alishindwa na ambalo wenye 'kisomo rasmi' waliweza?

Je, waliomteua hawakutambua hilo?

Nampongeza kwa kuitikia wito wa kwamba elimu haina mwisho wala utu uzima.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom