Guninita sasa ni 'fomu wani'

Kieleweke

Member
Jun 23, 2009
79
8
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -Chanzo: Gazeti TAIFA LETU
Toleo: 517
Tarehe: Septemba 11, 2009: {Leo}, Front Page, Bolded article

- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
1: Ajiunga na sekondari ya Perfect Vision
2: Aamua kufuta 'ukihio' wa muda mrefu
3: Aunganisha kidato cha 1 na 2 kwa mpigo
4: Atapimwa kwa mitihani ya majaribio "QT"
5: CCM Dar, Wabunge, Vijana wampongeza



- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -

Yule kada maarufu wa CCM aliyetamba katika Umoja wa Vijana na ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa D'Salaam amejisalimisha darasani na sasa anasoma kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Perfect Vision iliyoko Ubungo jijini D'Salaam.

Mwenyekiti huyo wa CCM mkoani Dar ambaye alifanikiwa kuwa DC huku akiwa hana kisomo, ameamua kukata mzizi wa fitina wa wale wanaomuita ”kihiyo” kwa kukimbilia darasani huku akiwa ni mwanafunzi mzee kupita wanafunzi wote nchini Tanzania.

Gazeti la TAIFA LETU lililazimika kumchimba kwa undani mwanasiaia huyo ili kujua uwezo wake wa kufikiri, baada ya kumsakama Spika wa Bunge Samwel Sitta, huku akivishauri vikao vya chama vimfute uanachama.

Mhariri wa TAIFA LETU aliamuru kwamba kabla ya kumhukumu Guninita na kumlaumu kwa hoja yake ya kutaka Spika Sitta afukuzwe ufanyike uchuguzi wa kina ili kujau mtu mwenye wazo jepesi kiasi hicho ni nani, ametokea wapi, yuko wapi na ana elimu gani.

Mhariri alitoa agizo hilo kwa vile katika nchi ya kidemokrasia kama Tanzania kiongozi wa chama kinachotawala, tena katika jiji la Dar kutoa wazo la kushangaza kama hilo, bila yeye mwenyewe kuwa mtu wa kushangaza.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti dada la hili la SEMA USIKIKE umebaini kwamba Guninita na uzee wake amejiunga katika shshule ya sekondari ya Perfect Vision iliyoko Ubungo jijini D'Salaam.

Baadhi ya maafisa wa juu wa shule hiyo ambao hawakutaka majina yao yachapishwe, walithibitishia gazeti hili kwamba ni kweli kada huyo wa CCM anasoma hapo shuleni.

“Ni kweli Guninita ni mwanafunzi wetu, anasoma hapa na hazi tunavyozungumza yupo kidato cha kwanza ingawa anaunganisha na kidato cha pili”, walisema maafisa hao.

Mwandishi wa habari hizi alikwenda kwenye shule hiyo na kukutana na Guninita ambaye alipata nafasi ya kuongea naye kama mwanafunzi mwenzake bila kujua ni ripota wa wa TAIFA LETU.

Guninita bila kujua katika mazungumzo na “mwanafunzi mwenzake” alitamba kuwa elimuhaina mwisho na ndiyo maana ameamua kusoma na uzee alio nao. Hata hivyo mwandishi TAIFA LETU alipotaka ufafanuzi kuhusu mtindo wa Guninita kusoma vidato viwili kwa mpigo, afisa mmoja wa shule alisema utaratibu wa aina hiyo upon a kuongeza kuwa chini ya utaratibu huo kabla ya kusonga mbele Guninita atalazimika kufanya mtihani wa kupima Kiwango chake yaani Qualifying Test (QT).

Alisema kutoaka na mtihani huo kuwa “tafu” Guninita atatakiwa kuwa makini na kutuliza kichwa chake, vinginevyo anawez kupiga mweleka.

Alipoulizwa kwamba ikitokea akafeli itakuwaje, afisa huyo alisema atalazimika kurudia.

“Ameamua kuuganisha, sisi hatukatai maana walimu wapo, ila atatakiwa kufanya mtihani ili afaulu, na kwa vile shule yetu ina Perfect Vision ina walimu waliobobea nchini, lazima atafundishwa hadi aelewe”, alisema.

Habari zilizopatika shuleni hapo zinasema tangu Guninita afichuliwe upeo wake {kwenye toleo lililopita} amekuwa mpole na anatembea kama kondoo aliyelowa maji.

Hatua hiyo ya Guninita imepongezwa na wananchi huku wengine wakisema “Kila baya lina uzuri wake na kila zuri lina ubaya wake”.

Akifafanua mmoja wa wananchi waliohojiwa alisema hatua ya Guninita kujaribu kumrarua Spika wa Bunge Samwel Sitta, ilikuwa mbaya lakini kwa upande mwingine ilikuwa nzuri, kwani kufanya hivyo gazeti hili lilimchimba na kuwaeleza watu udhaifu wake kielimu hadi akaamua kwenda shule.

“Kwa sakata hili la Sitta na Guninita mtu anaweza kusema kwamba mchimba kisima kaingia mwenyewe kwa jinsi ambavyo alishugulikiwa. Binafsi sikujua kiundani mambo ya mwenyekiti huyu lakini sasa naelewa” alisema.

Miongoni wa watu waliompongeza Guninita ni wafanyakazi wa Wilaya aliyofanya kazi zamani, baadhi ya viongozi wa Vijana wa CCM, baadhi ya wabunge, mwandishi wa habari hizi pamoja na mhariri wakeambao wamesema kwa furaha waliyo nayo watamzawadia Guninita madaftari na mkebe wa “kompasi” kama atahitaji.

Aidha wamesema kwa vile mwanafunzi huyo ni “Mheshimiwa Mwenyekiti wa Mkoa”, hatatakiwa kufuata zawadi zake ila atapelekewa mahala popote atakapotaka.

Hatua ya Guninita kuanza “fomu wani” ni changamoto kubwa kwake na kwa chama chake na uthibitisho kwamba elimu haina mwisho.

Hata hivo habari toka baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa D’Salaam zimesema kwamba huenda lengo la Guninita kuanza masomo ya sekondari, sio kujielimisha tu, bali anataka kutumia elimu yake ndogo angalau wakubwa wamfikirie kumpa nyadhifa za juu.

“Sijui ni iutu gani kimemfanya ashtuke na kuanza masomo wakati huu, lakini nafikiriamesukumwa na hali ya kisiasa na maendeleo nchini, kwamba kwa elimu aliyo nayo asingeweza kupata wadhifa wa juu kwa sasa” alisema afisa mmoja ndani ya CCM.

Afisa huyo aliyetakiwa kutoa maoni yake kuhusu “Guninita” alisema kutoka ‘ukihio’ hadi kidato cha kwanza” alisema elimu ya mwanasiasa huyo ingekuwa inajulikana tangu awali huenda hata hicho cheo cha uenyekiti wa Mkoa asingekipata.

Hata hivyo alisema haelewi ni kwanini mtu ambaye alikuwa darasa la saba aliweza kupewa cheo cha Ukuu wa Wilaya ya Rufiji.

“Lakini yaliyopita si ndwele sasa tugange yajayo, mimi binafsi nasubiri digrii yake kwa hamu” alisema.

Hata hivyo kwa mahesabu yetu ya harakaharaka ni kwamba mheshimiwa huyo atamaliza kidato cha sita mwaka 2015 kama atafaulu mitihani na wakati huo atakuwa anakaribia miaka 66 hivi.

- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
 
Hii ndo TZ kila kitu kinawezekana......wenye elimu zao wanasaga lami, wasio nazo ndio kwanza wameshika hadi vyeo kama ukuu wa wilaya. na sasa Dar nzima hakuna aliyeweza kufanya vetting kujua mgombea uwenyekiti wa chama ana elimu darasa la saba.
 
Billions of bilious blue blistering barnacles and trillions of true thundering typhoons !!!!

The good Captain is voicing my outrage towards Guninita and the odd-toed ungulates who let him ride all along.

captainhaddock.jpg
 
Soma babu tena kazana waweza hata pata madigrii kibao oooooh elimu ni bahari
 
Sijaamni hii habari naomba nieleweshwe jamani...Guninita yule aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuia ya vijana CCM baadaye akadefect kwenda upinzani na kurudi CCM? Ama kweli Tanzania kiboko.. baada ya miaka 4 sintoshangaa nikishikia ana PhD kama ya Nchimbi!
 
Sijaamni hii habari naomba nieleweshwe jamani...Guninita yule aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa vijana CCM baadaye akadefect kwenda upinzani na kurudi CCM? Ama kweli Tanzania kiboko.. baada ya miaka 4 sintoshangaa nikishikia ana PhD kama ya Nchimbi!


Mambo ya Pacific west sijui huko. wanacombine na work experience mkuu!
 
Tukiwaambia CCM inaongozwa na vihiyo mnabisha!! Sasa bado babu Makamba nae aende shule akapate digrii kabla ya uchaguzi mwaka kesho. Salum Londa nae aliyeshitakiwa pamoja na Makamba kwa Ufisadi wilaya ya Kinandoni ana Elimu gani?? Maanake yeye meya wa Kinondoni kiliko Chuo Kikuu cha DSM!
 
kweli siasa ni mchezo mchafu......sikuamini huyu mzee alivomkomalia sitta,kumbe ni kihiyo.Kwa tz yetu sdhani kama itafika hata 2012 kabla hajapata degree yake.............
 
Hii kali kuliko,darasa la saba mkuu wa wilaya na sasa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar..?!Hivi ni John Guninita ama mtu mwingine?!
Kama ni yeye nimewahi kushirikiana nae katika mambo fulani ya kifamilia lakini hii habari ya kiwango chake cha elimu nilikuwa siijui!
Anyway,naweze sema jamaa zali lilimdondokea;au ndiyo yale mambo ya kujuana mpaka mnavuka mipaka!!Good move ndugu yangu,nitaenda kumcheki home kwake week-end hii nikishindwa nitachonga na mkewe.
 
Majitu kama uninita yako mengi CCM, kumbuka bwana Choya alikuwa ameteuliwa na rais kua DC mahali fulani lakini ni form 4, lakini angalau form 4 ila kinachouma tuna watu wenye degree hawana cha kufanya lakini form 4 au std 7 anankuw DC. Kikwete nadhani ana matatizo ya akili pia au naye alighushi vyeti kwa sababu hata mkapa anamzidi ktk uteuzi.
 
Hivi website ya bunge imefungwa? nilikuwa nataka kutafuta CV ya .... sasa haifunguki.
 
Kama sikosehi Guninita alikuwa kamanda wa chipukizi. Na kuna miaka walifikiria kuwa chipukizi wanaofanya vizuri itabidi wachaguliwe kwenda sekondari. Alichaguliwa kwenda sekondari lakini alivulunda big time.

Sina memory nzuri kama ni huyu.
 
Sidhani kama Guninita ana akili ya kutosha kuelewa Trigonometry, Algebra, na Calculus.
 
Kamati kuu ya CCm si ndio wanaotoa dira ya maendeleo ya taifa? Halafu mnajiuliza ni kwa nini watanzania ni maskini hivi hata baada ya miaka 50 ya uhuru?

Uongozi... uongozi...uongozi.....
 
Sidhani kama Guninita ana akili ya kutosha kuelewa Trigonometry, Algebra, na Calculus.

ha ha ha ha .....
Ila 0-level haina calculus (integration na differentiation) kwa syllabus ya Tanzania. Hizo ni mpka A-level
 
Back
Top Bottom